Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Cyprian Musiba Apewa Siku 7 na Mahakama za Kuwasilisha Utetezi Wake Dhidi ya Benard Membe

$
0
0
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imempa siku 7 mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba na wachapishaji wa gazeti hilo kuwasilisha majibu dhidi ya madai ya Bernard Membe. 

Waziri huyo mstaafu wa Mambo ya Nje anataka kulipwa Sh 10 bilioni kwa kuchafuliwa na gazeti tajwa.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa jana Jumanne Julai 2, mbele ya Jaji Joaquine Demelo baada kupitia maombi ya wajibu maombi ya kutaka waongezewe muda wa kuwasilisha utetezi na majibu kinzani.

Jaji Demelo alisema wajibu maombi walitakiwa kuwasilisha utetezi na majibu kinzani ndani ya siku 21 baada ya shauri kufunguliwa Desemba mwaka jana lakini hawakufanya hivyo ambapo Musiba kupitia Wakili wake Majura Magafu waliomba kuongezewa muda japo wadai walipinga maombi hayo wakitaka yasikubaliwe.

“Mahakama imesikiliza hoja za pande zote mbili imeona kesi ina maslahi kwa umma hivyo ni bora na upande mwingine wakasikilizwa. 


"Hatuwezi kusikiliza shauri upande mmoja, kesi hii  ina maslahi kwa umma kuna haja ya kuusikiliza na upande wa pili, nawapa siku saba muwasilishe utetezi na hati ya kiapo kinzani,” alisema Jaji Demelo.

Jaji Demelo alisema upande wa waleta maombi kama watakuwa na hoja za kujibu utetezi wawasilishe kabla ya Agosti 8, mwaka huu ambapo shauri hilo la madai litaanza kusikilizwa Agosti 6, mwaka huu.

Lugola aagiza magari yaliyokopeshwa kwa watumishi wa NIDA Yarejeshwe Haraka

$
0
0
Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Kangi Lugola ameagiza waliokuwa watumishi watatu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kuyarudisha magari aina ya Toyota Land Cruiser wanayoyamiliki kinyume cha sheria.

Waziri Lugola alitoa kauli hiyo Jumanne hii katika kikao chake na viongozi wa ngazi ya juu wa Nida.

Alisema miongoni mwa watumishi wanaomiliki magari hayo ni pamoja na aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Nida, Dickson Maimu.

Alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk Arnold Kihaule kushughulikia suala hilo hadi ifikapo jana jioni yawe yamerejeshwa katika maegesho ya ofisi za Nida.

Kikao hicho kilifanyika Jijini Dodoma, na kilikuwa kinapokea taarifa ya idadi ya mali za Nida zilizopo na zilizopokelewa na mwenendo wa matumizi yake.

Wafanyabiashara Washauriwa kutumia Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Kutangaza Bidhaa zao

$
0
0
Wafanyabiashara nchini wameshauriwa kutumia Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) kama uwanja wa kutangaza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyao.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan jana Jumanne Julai 2, wakati akizindua maonyesho hayo katika viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam, katika maonyesho hayo yaliyobeba kauli mbiu isemayo ‘usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu’.

Mama Samia alisema maonyesho hayo ambayo yamejizolea umaarufu Afrika Mashariki na Kati hutembelewa na watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi hivyo yakitumika vizuri ni sehemu sahihi ya wafanyabiashara kupanua wigo wao kibiashara.

Katika hatua nyingine Mama Samia amewataka wakulima kulima mazao kwa wingi kwani Serikali inaendelea kujenga viwanda ambavyo malighafi yake itatoka hapa nchini hususani katika sekta ya kilimo.

Isikupite Hii! 👉Naitwa Chief Karim Wa Sultan.....Ni Bingwa Na Mtabiri Wa Nyota

$
0
0
Isikupite hii! 👉Naitwa CHIEF KARIM WA SULTAN Kutoka- TANGA - TANZANIA: Ni Bingwa, Mnajimu na Mtabiri wa Nyota na Matatizo yote ya ndoa/mahusiano.

Natabiri nyota yako, Kung'alisha nyota, Kufungua nyota zako za mafanikio zilizo fungwa  na kusababisha usifanikiwe katika maisha yako, au unajikuta unafanya kazi/biashara unapata hela lakini pesa yako haikai yaani inapita tu katika mikono yako.

Nawezesha  NYOTA, ni UTAJIRI usio na kafara yoyote na ni UTAJIRI unaoendana na nyota yako tu.

Hakika watu wengi wanazidi kufanikiwa na kutimiza ndoto zao , Kulipwa haraka haki zako unazodai, Mvuto wa mapenzi, kumrudisha mpenzi, mme au mke aliyekuacha/kukutelekeza.

 Je unapata wapenzi/wachumba lakini wanakuacha bila kujua sababu? Nitakusaidia!

Kufungua kizazi chako kilichofungwa na kusababisha usipate mimba/mtoto au unashika mimba zinatoka/kuharibika na maumivu makali ya tumbo/chango.

 👉KWA TATIZO LOLOTE  LA KINYOTA WASILIANA NAMI 👉WhatsApp : 0763 103 527
au
👉PIGA SIMU  : 0716 681 318
👉 0688 745 790


NB 👉(KWA MWANAUME YOYOTE MWENYE TATIZO LA KUISHIWA AU KUPUNGUKIWA NGUVU ZA KIUME AU KAMA UMEATHIRIKA NA TATIZO LA KUPIGA PUNYETO TUWASILIANE POPOTE ULIPO)*{لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أيْمَانِكُمْ وَلَٰكِنْ يُؤَاخِذُكُمْ بِمَا عَقَّدْتُمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِمَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ }* ﴿٨٩﴾ ✨WABILLAHHI TAWFIQ ASALLAM  ALAIKUM✨ 

Mawaziri Bara, Zanzibar Wasaini Makubaliano ya Ushirikiano

$
0
0
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo Kale Zanzibar  Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid Karume wamesaini makubaliano ya ushirikiano katika kusimamia na kutekeleza sekta za Habari, Utamaduni,Sanaa na michezo ili kuongeza tija. 
 
Uwekaji wa saini za ushirikiano huo umefanyika jana Jijini Dodoma katika ukumbi wa chuo cha Ufundi Veta, baada ya vikao vya ngazi za wataalam na Makatibu Wakuu wa Wizara husika kuwasilisha taarifa hizo kwa Mawaziri na hatimaye kuridhia tayari kwa ajili ya utekelezaji. 
 
“Hatua hii ni nzuri na muhimu kwetu katika kuhakikisha tunadumisha na kuhifadhi muungano wa kihistoria ambao ulioasisiwa na waasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere na Shehe Amani Abed Karume”  Alisisitiza Dkt.  Mwakyembe. 
 
Aidha, Waziri wa Habari, Utalii na Mambo Kale Zanzibar  Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameeleza kuwa katika sekta ya habari ni muhimu kwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)  kushirikiana na  Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) ili kuandaa vipindi mbalimbali ikiwemo kipindi cha  utalii  Safari chaneli. 
 
 “Kwa kutambua  umuhimu wa sekta ya utalii nchini ,  vyombo hivi vya habari TBC na ZBC vinapaswa kushirikiana kuandaa vipindi vya utalii  ili kuitangaza sekta hii nje na ndani ya nchi” Alisisitiza Mhe. Mahmoud Thabit Kombo . 
 
Kwa upande wake Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid Karume  amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa  lugha ya Kiswahili inatangazwa na kuenezwa kuna umuhimu wa kuandaa kanzi data itakayojumuisha  wataalam  wa Kiswahili ambao watakuwa wakifundisha wageni ndani na nje ya nchi. 
 
“Tanzania imechangia sana katika kukuza  lugha ya Kiswahili na watu wengi wanapenda kuja kujifunza kwetu ,hivyo naamini kwa kuwa na kanzi data hii itasaidia sana katika kuwapata watalaam wazuri wa kufundisha lugha hii”. Balozi Ally Abeid Karume. 
 
Vilevile Mawaziri hao wamekubaliana kuimarisha ushirikano katika sekya ya sanaa kwa kuhakikisha kuwa ifikapo desemba 2019 wanakuwa wamesha andaa kanuni  zitakazowawezesha watayarisha wa filamu kutoka nje ya nchi ili kuruhusu utumiaji wa maudhui hayo kwa vyombo vya habari vya serikali.

Mawaziri hao walimalizia kwa kueleza kuwa sekta ya michezo ni sekta muhimu sana katika kutambulisha taifa kupitia michezo mbalimbali na hivyo walikubaliana   kuandaa kombe la Muungano, namna bora ya kuibua na kukuza vipaji pamoja na kuteua wajumbe wa bodi ya Baraza laTaifa la Michezo   (BMT) na Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar. 
 
Vilevile Mawaziri hao walipata wasaa wa kutembelea shule ya Fountain Gate Academy iliyopo maili mbili Jijini Dodoma, ambayo huibua na kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana wenye vipaji hivyo ili kuwaendeleza na kuweza kufikia ndoto zao ikiwa ni moja ya jitihada za kuendeleza sekta ya michezo nchini. 
 
Mwisho.

Tazama hapa Timu 16 zilizotinga hatua ya 16 bora AFCON 2019 Pamoja na Ratiba

$
0
0
Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kupoeza mechi zake zote kwenye kundi C michuano ya Afcon zilizotinga hatua ya 18 hizi hapa na ratiba yake ipo namna hii:-

1.Egypt v South Africa

2.Madagascar v DR Congo

3.Nigeria v Cameroon

4.Senegal v Uganda

5.Algeria v Guinea

6.Morocco v Benin

7.Mali v Ivory Coast

8.Ghana v Tunisia

Maambukizi ya Fangasi katika Sehemu za Siri

$
0
0
Kati ya maambukizi yanayowasumbua wanawake wengi duniani ni maambukizi ya fangasi. Inakisiwa asilimia 75 ya wanawake wote duniani hupata maambukizi haya katika kipindi cha uhai wao.

Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu kama Candida albicans. 

Maambukizi haya pia hujulikana kama yeast infection au thrush. Fangasi hupatikana kama vimelea vya kawaida katika mdomo, mpira wa kupitisha chakula sehemu inayojulikana kama pharynx, katika kibofu cha mkojo, uume na hata kwenye uke.

Mfumo mzuri wa kinga wa mwili pamoja aina fulani za bakteria wanaoishi pamoja na fangasi hawa husaidia sana katika kuthibiti maambukizi yanayoyosababishwa na aina hi ya fangasi. 
 
Nini hutokea?
Kwa kawaida, Candida albicans huishi kwenye uke na sehemu nyingine (kama zilivyoelezewa hapo juu) bila kusababisha madhara yoyote yale isipokuwa pale mazingira ya eneo husika yanapobadilika kama vile mabadiliko katika hali ya pH ya  eneo husika (ifahamike ya kwamba pH ya kawaida ndani ya  uke ni 4.0 - 4.5) au uwiano wake na vimelea  (microorganisms) wengine unapoharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya madawa aina ya antibiotics, kupungua kwa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali n.k.

Maambukizi haya ya fangasi yanaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili
  1. Maambukizi yasiyo makali yaani uncomplicated thrush: Katika kundi hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi  mara moja hadi nne kwa mwaka na dalili zake huwa si mbaya sana na maambukizi haya husababishwa na fangasi wa jamii hii ya Candida albicans.
  2. Maambukizi makali yaani complicated thrush: Katika kundi hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi zaidi ya mara nne kwa mwaka, dalili zake kuwa mbaya zaidi au kama maambukizi  yatakuwa yametokea kipindi cha ujauzito, ugonjwa wa kisukari, upungufu wa kinga mwilini. Aina hii kusababishwa na vimelea vya aina nyingine tofauti na Candida albicans.
Vihatarishi
Watu walio katika hatari ya kupata maambukizi ya fangasi hawa ni  wale wenye

• Kutumia sana dawa aina ya detergents kwenye sehemu za siri au douches (vifaa vinavyotumiwa kusafishia uke kwa kutumia maji yaliyochanganywa na siki au antiseptic yoyote ile) kwa sababu hali husababisha kuharibika kwa uwiano wa fangasi na aina nyingine ya vinyemelezi kama bakteria aina ya lactobacilli

• Kutumia sana madawa aina ya antibiotics, steroids ambayo yana tabia ya kushusha kinga ya mwili

• Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambayo husababisha mabadiliko katika s ehemu za siri na hivyo kufanya kuwepo kwa ukuaji wa kasi wa fangasi hawa

• Ujauzito (kutokana na kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini na kupungua kwa kinga ya mwili). Hata hivyo ieleweke hapa kuwa si kila mjamzito hupatwa na maambukizi haya.

• Matumizi ya dawa za kupanga uzazi (vidonge vya majira)

• Upungufu wa kinga mwilini kutokana na magonjwa sugu kama kisukari, saratani aina yoyote ile, ugonjwa aina ya mononucleosis na nk.

• Ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS)

• Matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy) kutokana na sababu mbalimbali

• Matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa wale wenye matatizo ya uzazi (infertility treatment)

• Msongo wa mawazo (stress)

• Utapia mlo (malnutrition)

• Kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri kwa muda mrefu kama nguo za kuogelea (swimwear), nguo za ndani (chupi)  zilizotengenezwa kwa kitambaa aina ya nylon, nguo za ndani zinazobana sana nk.

• Kujamiana kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujamiana  kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) au matumizi ya vilainishi venye glycerin wakati wa kujamiana pia yamehusishwa na maambukizi haya.

• Kuvimba kwa tezi la koo (goiter)

• Saratani ya tezi la koo (thyroid cancer)

• Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na thelathini wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi au wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa hawako kwenye hatari kubwa.

Kwa wanaume vihatarishi  vya maambukizi haya ni

• Kujamiana na mwanamke mwenye tatizo hili au maambukizi haya

• Upungufu wa kinga mwilini

• Matumizi ya madawa aina ya antibiotics kwa muda mrefu bila ushauri wa daktari

• Magonjwa sugu kama kisukari, saratani ya aina yoyote ile na nk.

Dalili na viashiria kwa wanawake
• Kuwashwa  sehemu za siri  (kwenye tupu ya mwanamke)

• Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning sensation)

• Kufanya kama vidonda katika sehemu za siri (soreness)

• Maumivu wakati wa kujamiana (superficial dyspareunia)

• Maumivu  au usumbufu wakati wa kujisaidia haja ndogo (wakati mtu anakojoa)

• Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwa  mdomo wa nje wa tupu ya mwanamke (labia minora)

• Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au nyeupe kijivu, unaoweza kuwa mwepesi, majimaji au mzito na ambao umefanana na jibini (cottage cheese like discharge) wenye muonekano unaojulikana pia kama curd-like appearance. Kwa kawaida, uchafu huu haumbatani na harufu yoyote isipokuwa panapokuwa na tatizo la ziada kama ugonjwa wa zinaa aina ya Bacteria vaginosis. Uchafu huu unaotoka hapa unaweza kuenea kwenye maeneo mengine yaliyokaribu na tupu ya mwanamke kama kwenye mitoki (groin area) au perineum na kusababisha kuharibika kwa ngozi katika sehemu hizo.

Dalili na viashiria hivi huwa mbaya zaidi wakati  mwanamke anapokaribia  kupata hedhi.

Dalili na viashiria kwa wanaume ni
• Kuwashwa sehemu za siri 
• Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwenye ncha ya uume
• Kuwepo kwa uchafu wa rangi nyeupe (kama nilivyoeleza hapo juu) kwenye sehemu ya juu ya uume.
• Kuwa na vidonda vidogo kwenye uume (sore on the glans)

Hata hivyo, mara nyingi wanaume hawaoneshi dalili zozote zile, ni vizuri kwa mwanamke kumueleza mwenza wake pale anapopata maambukizi haya ili naye pia apate kutibiwa. 
 

Matibabu
Matibabu ya fangasi huusisha dawa za kutibu fangasi (antifungal drugs) kama vile dawa za kupaka za topical Clotrimazole, topical Nystatin, Fluconazole au topical Ketoconazole. 

Wagonjwa wenye maambukizi yasiyo makali yaani uncomplicated vaginal candidiasis wanaweza kutumia dawa za kupaka (cream) kutoka dawa za fangasi za jamii ya -azole kama vile Butoconozale, Miconazole, Clotricomazole nk. 

Dawa hizi hutumika kwa muda wa siku 3-7 kulingana na aina ya dawa. Mgonjwa anashauriwa kupaka dawa ndani ya uke pamoja na maeneo yote yanayozunguka sehemu hiyo. Jinsi ya kupaka dawa hizi ni kuanzia mbele kuelekea nyuma.

Aidha mgonjwa anaweza kupewa dawa za kutumbukiza ukeni ambayo atatumia kwa muda wa siku 3-14 kulingana na aina ya dawa. Dawa hizo ni pamoja na Miconazole, Tiaconazole, Terconazole, Nystatin nk.

Kidonge cha kumeza aina ya fluconzole pia huweza kutolewa. Dawa hizi nilizotaja hapa juu zina kawaida ya kuharibu ubora wa mipira ya kondomu zilizotengenezwa na mpira aina ya latex (latex condoms) pamoja na vifaa vya upangaji uzazi aina ya diaphragms.

Ni vizuri kwa daktari kabla ya kumpa mgonjwa dawa hizi kumfahamisha kwa ufasaha jinsi ya kuzitumia na tahadhari anayotakiwa mgonjwa kuchukua. Inashauriwa kama baada ya matumizi haya bado mgonjwa ana dalili za maambukizi au mgonjwa akapata tena maambukizi haya ndani ya miezi miwili baada ya matibabu ya awali, basi anashauriwa kwenda kumuona daktari ili apate matibabu zaidi.
 
Kinga ya maambukizi ya fangasi
• Kuosha sehemu ya siri kwa kutumia kitambaa kisafi kila siku na kuosha kuanzia mbele kuelekea nyuma, epuka kurudia ukishafika nyuma.

• Epuka matumizi ya sabuni zenye manukato, bubble baths, vaginal deodorant products, feminine hygiene, na bath powder.

• Vaa chupi ambazo hazibani sana na zilizotengenezwa kwa kutumia pamba au hariri (silk), epuka synthetic underwear.

• Epuka mavazi yoyote ya kubana kama jeans za kubana nk.

• Badilisha nguo za ndani (chupi) kila zinapopata unyevunyevu.

• Fua chupi zako kwa maji yenye nyuzi joto 90 na kuendelea.

• Tumia pad wakati tu unapozihitaji (kama umeingia kwenye mzunguko wako wa hedhi)

• Kula mlo wenye virutubisho vyote kamili (balanced diet)

• Epuka kufanya mapenzi  na mpenzi wako ambaye amepata maambukizi ya fangasi.

• Epuka kuoga  maji moto sana (hot baths) tumia maji ya uvuguvugu, hii kwa wale ambao wanaishi kwenye ukanda wa joto (tropical climate).

• Matumizi ya vifaa vya ngono (sex toys), vifaa vya upangaji uzazi (diaphragms, cervical caps) yanaweza kuleta kujirudia kwa maambukizi ya fangasi kama havitaoshwa  na kukaushwa vizuri baada ya kutumiwa.

• Baadhi ya tafiti zilizofanyika, zimethibitisha ya kwamba unywaji wa maziwa ya mtindi yenye live culture, husaidia kupunguza maambukizi ya fangasi.

IGP Sirro Aongoza Kikao Cha Utendaji Cha Maofisa Wakuu Wa Jeshi La Polisi

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (katikati), akiongoza Kikao cha Utendaji cha Maofisa Wakuu  wa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam, kujadili utendaji wa kazi za Polisi, kufanya tathmini, Mafanikio, Changamoto na kuweka mikakati ya kutekeleza kazi za Polisi hususan kulinda maisha ya raia na mali zao.

Kushoto kwake ni Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Mussa A. Mussa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas na kulia kwake ni Kamishna wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi CP Shabani Hiki na Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba. 

Maofisa Wakuu wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wakifuatilia hotuba inayotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCP Charles Kenyela (aliyesimama), Wakati wa Kikao cha Utendaji cha Maofisa Wakuu kilichofanyika jijini Dar es salaam na kujadili utendaji wa kazi za Polisi, kufanya tathmini, Mafanikio, Changamoto na kuweka mikakati ya kutekeleza kazi za Polisi hususan kulinda maisha ya raia na mali zao ili kuhakikisha jamii inakuwa salama

Fahamu Chanzo Halisi cha Kupungukiwa Nguvu za Kiume

$
0
0
Unafahamu kwa kina tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na  maumbile ya kiume kusinyaa?

Wanaume wengi kwa sasa wanasumbuliwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile  kuwa mafupi na wengi wao huamua kutafuta tiba ili waweze kujilejeshea nguvu zao za asili bila kujua ni nini chazo cha hilo tatizo 

Tambua kuwa hakuna dawa ya kuongeza maumbile ya kiume  kama  ulikuwa mdogo  tangu unazaliwa, labda kama tatizo limeazia ukubwani kwa kujichua ( kupiga punyeto)  au kutokana na magonjwa 

Pia hakuna dawa ya kuongeza nguvu za kiume kama tatizo umezaliwa nalo bali zipo tiba za kutibu na ukapona matatizo hayo kama yameanzia  ukubwani kutokana na sababu zifatazo ;
1,Unene kupita kiasi 
2.Kuvaa nguo za kubana 
3.Magonjwa ya moyo,kisukar,presha,vidonda vya tumbo,ngiri,tumbo kuunguruma na kujaa gesi,kupiga punyeto,Msongo wa mawazo.

Haya ndo mambo makuu yanayosababisha tatizo hilo. kwa ushauri zaidi , piga simu 0683645920

Jinsi ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

$
0
0
Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunakuwa katika uwanja mpana zaidi wa tafakari za kibaiolojia na kisaikolojia walizonazo wanaume.

Lakini kwa kufupisha mlolongo wa mambo sehemu kuu tatu zinaweza kabisa kukidhi mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili linavyowasumbua wanaume wengi duniani.

Sehemu kubwa ya malalamiko ya wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi maeneo matatu ambayo ni kukosa msisimko, kushindwa kurudia tendo na kukosa kabisa nguvu, huku kufika kileleni mapema kukihusishwa pia kama pacha wa janga hili ambalo linawasumbua zaidi wanaume.
 
Sababu zinazosababisha tatizo la nguvu za kiume zinawekwa katika makundi mawili.
*Matatizo ya kiafya ya mwili (organic causes).
*Matatizo ya kisaikolojia ( Psychological cause).
 
Matatizo ya kiafya:
  1. Magonjwa ya kisukari, (diabetes mellitus).
  2. Ugonjwa wa presha (blood pressure).
  3. Matatizo ya tezi dume (kama mtu amewahifanyiwa operation) (prostatectomy surgery),
  4. Upungufu au mvurugiko wa uzalishaji Homoni za uzazi (hormonal insufficiencies /hypogonadism).
  5. Athari za matumizi ya dawa kwa muda mrefu (drug side effect).
Matatizo haya kwa pamoja hupelekea mishipa ya damu kuziba na mwishowe misuli inakosa nguvu za kuweza kusimama na hatimae uume husinyaa.
 
Tatizo la Kisaikolojia(Psychological reasons)
Ukweli wa mambo ulioibuliwa na wanasaikolojia umebaini wale wote wanaolalamikia/lalamikiwa kuwa hawana nguvu iwe ya kufika kileleni mapema, kutokuwa na msisimko na kushindwa kurudia tendo wamekosa maarifa tu ya kufahamu na hawaijui miili yao na wanaishi kwa kusikia zaidi ya kujitambua.

Watu hao kiuhalisia wanakabiliwa  na matatizo ya kimawazo, kama vile migogoro katika mahusiano, matatizo ya kimaisha na mambo mengine
 
Dalili za tatizo hili
  1. Kushindwa kusimamisha uume mara kwa mara,
  2.  Uume kulala(kusinyaa) katikati ya tendo la ndoa.
  3.  kushindwa kusimamisha ipasavyo.
  4. Kufika  haraka mara baada ya kuanza
  5. kujamiiana.
  6.  Maumivu ya misuli ya uume wakati wa tendo la ndoa.

Magonjwa yanayosababisha tatizo hili:
*kisukari (diabetes)
*presha (blood pressure)
*matatizo yafigo (kidney disorders)
*matatizo ya kisaikologia(psychological cause).
* upungufu wa homoni za uzazi (hormonal insufficiencies).
* Matumizi ya dawa kwa muda mrefu (drug side effect).
* Uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi.
* matatizo ya tezi dume.

Matatizo haya yote Yanatibika kwa dawa. Wasiliana Nami kwa msaada zaidi: 0620510598 au 0759208637

 

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
 
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Mke wa Mtawala wa Dubai akimbia mafichoni akiogopa kuuawa

$
0
0
Mke wa mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed Al Maktoum, Binti Mfalme Haya Bint al-Hussein, yuko mafichoni jijini London akidaiwa kuhofia usalama wa maisha yake baada ya kumtoroka Mumewe.

Sheikh Mohammed mwenye miaka 69, ambaye ni Bilionea, aliandika utenzi wenye hisia za hasira kwenye ukurasa wa Instagram akimshutumu mwanamke ambaye hakufahamika kwa vitendo vya ”udanganyifu na usaliti”.

Mke wa kiongozi huyo mzaliwa wa Jordan ana miaka 45, aliolewa na Sheikh Mohammed mwaka 2004 na kuwa mke wa sita, ”mke mdogo”.

Sheikh Mohammed ameripotiwa kuwa na watoto 23 kutoka kwa wake zake.

Binti mfalme Haya awali alitorokea Ujerumani mwaka huu kutafuta hifadhi. Hivi sasa anaelezwa kuishi kwenye nyumba ya thamani ya pauni milioni 85 Kensington Palace Gardens, katikati mwa jiji la London, akijiandaa kufungua mashtaka kwenye mahakama ya juu.

Serikali Yajipanga Kutumia teknolojia sahihi za Kilimo zinazoendana na mahitaji na wakati

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Jitihada za kuongeza uzalishaji zinakuwa na mafanikio hafifu kutokana na kutotumia teknolojia sahihi zinazoendana na mahitaji na wakati; Mathalani, matumizi ya zana za kulimia ama zikiwa za mkono au zinazokokotwa na wanyamakazi au matrekta, zimekuwa zikisababisha mmomonyoko wa udongo hasa katika maeneo yasiyo tambarare na kusababisha upotevu mkubwa wa rutuba na kujengeka kwa jasi (hard pan).

Kwenye maeneo yenye mvua chache njia hizo za kilimo cha kukatua ardhi hazitunzi unyevu na kusababisha uzalishaji kuwa wa chini hasa pale panapokuwa na vipindi virefu vya ukame (dry spells) kama ilivyotokea msimu huu wa kilimo katika baadhi ya maeneo nchini ikiwemo Mkoa wa Dodoma.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 03 julai 2019 kwenye ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma.

Mhe Hasunga anasema kuwa kwa sababu hiyo basi, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni muhimu kubadilisha mifumo inayotumiwa katika kuandaa mashamba ili kupata matokeo mazuri.

Amewashukuru Washirika wa Maendeleo (Development Partners) pamoja na Wadau wote wa Kilimo Hifadhi waliowezesha kufanikisha warsha hiyo muhimu wakiwemo African Conservation Tillage Network (ACTN), Canadian Food GrainBank (CFGB), Diocese of Central Tanganyika (DCT), na Conservation Farming Unit (CFU) –Tanzania.

Alisema juhudi hizo wanazofanya za kuendeleza Kilimo Hifadhi kwa kushirikiana na Serikali kwa maendeleo ya wakulima na Taifa kwa ujumla, ni sehemu ya mwelekeo wa kufikia Uchumi wa Viwanda kwa kukuza uzalishaji wenye tija.

Aliongeza kuwa jitihada hizo zinaendana na Sera ya Kilimo ya mwaka 2013 na Programu ya  Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (Agricultural Sector Development Programme - ASDP II) ambazo zinahimiza usimamizi endelevu wa matumizi bora ya maji na ardhi, kuongeza tija na faida katika uzalishaji, biashara na kuongeza thamani ya mazao na kuiwezesha Sekta katika uratibu, ufuatiliaji na tathmini.

Kadhalika Waziri Hasunga amesema kuwa ili kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo, Serikali imeongeza juhudi za kuwaunganisha wakulima na masoko, huduma za kifedha, usindikaji wa mazao na kuongeza thamani.

Alisema kuwa katika kutimiza azma hiyo, Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Kilimo inaendelea Kuweka mazingira mazuri yanayovutia uzalishaji na uwekezaji, Kuimarisha mafunzo, Utafiti, ubunifu na uenezaji  wa teknolojia za kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na Kilimo Hifadhi na kuboresha Huduma za Ugani, Kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, uongezaji thamani ya mazao, kuimarisha ushirika, kuwaunganisha wakulima na masoko na huduma za fedha; na Kuhamasisha na kusimamia matumizi ya teknolojia za kisasa za kilimo ikiwemo teknolojia za kilimo hifadhi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Mahamoud Mgimwa (Mb) alisema kuwa serikali inapaswa kujipanga vizuri kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini kwa kufanya utafiti wa kina kwa utafiti ndio nguzo ya kilimo.

Alisema kuwa asilimia kubwa ya mbegu zinaagizwa nje ya nchi hivyo aliiomba aserikali kuongeza Bajeti ya Wizara ya Kilimo hususani katika kuendeleza sekta ya mbegu.

Amesema Tanzania bado kuna tatizo kubwa la Masoko kwani wakulima wengi wanazalisha mazao yao lakini hawana mahali pakuyauza kwa bei nzuri huku wengine wakishindwa kusafirisha mzao yao kutokana na miundombinu kutoimarika kwa kiasi kikubwa. Kadhalika ameipongeza wizara ya Kilimo kwa kuanzisha mchakato wa mapitio ya sera ya kilimo ya 56mwaka 2013 itakayopelekea kuwa na sheria mpya ya Kilimo.

Awali akitoa salamu za wizara ya Kilimo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe alisema kuwa Lengo la warsha hiyo ni kuwawezesha washiriki kupata uzoefu na kufahamu juhudi na matokeo ya kazi za kuendeleza kilimo hifadhi zinazofanyika nchini na kuweka mpango utakounganisha, kuratibu na kusimamia shughuli za kuendeleza matumizi bora na endelevu za teknolojia za kilimo hifadhi nchini.

Alisema kuwa matumizi ya kilimo cha kisasa (smart agriculture)  ikiwa ni pamoja na kilimo hifadhi ni nguzo katika kuendeleza kilimo nchini kwa kongeza tija, kuboresha ardhi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hasa katika maeneo yanayopata mvua chache.

Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Katika miaka ya hivi karibuni, matumizi ya teknolojia ya kilimo hifadhi yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka. Tathmini zilizofanywa na Wizara zinaonyesha kuwa karibu hekta 40,000 nchini zinalimwa kwa kutumia  kilimo hifadhi na matokeo yanaonyesha kuwa mavuno (yields) wanayopata wakulima kutoka kwenye mashamba ya kilimo hifadhi ni mazuri hata wakati wa mvua chache.

Aliongeza kuwa Katika kipindi hiki, ambacho Serikali inajitahidi kuongeza miundo mbinu ya umwagiliaji na kuongeza matumizi ya mbolea za viwandani kwa gharama kubwa ili kuongeza tija na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, matumizi ya teknolojia ya kilimo hifadhi ni njia mbadala ya kufikia malengo hayo kwa haraka na kwa gharama nafuu.

MWISHO

Rais Mstaafu Mkapa azindua safari ya SAUT kuelekea Jubilei ya Fedha.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi-SAUT
Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT) kimezindua safari ya miaka mitano kuelekea Jubilei ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1998. 

Uzinduzi huo umefanywa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa uliofanyika chuoni hapo kwa kuweka jiwe la msingi katika jengo la ukumbi wa mikutano unaojengwa kutumika kwa shughuli mbalimbali za kitaaluma na kijamii. 

Akiongea na hadhira ya viongozi mbalimbali, wahadhiri, wanafunzi pamoja na wananchi waliohudhuria  katika tukio hilo liliotanguliwa na ibada ya misa takatifu iliyongozwa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha SAUT na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Askofu Flavian Kassala, Rais Mstaafu Mkapa amesema kuwa vyuo vikuu vya binafsi vinamchango mkubwa nchini katika kutoa elimu kwa Watanzania bila kujali dini zao wala makabila yao hatua ambayo itawaweze kutoa mchango katika kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Taifa ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. 

Kuhusu Sera ya Maendeleo ya Taifa, Rais Mstaafu Mkapa amesema kuwa elimu ya juu ina mchango kwa taifa kwa kuzalisha wataalam wengi wenye ubora, ujuzi na uwezo wa kutatua matatizo ya jamii, kukabiliana na changamoto za maendeleo ili kufikia ushindani katika ngazi za kikanda na za kimataifa. 

“Serikali inatambua na inathamini mchango wa sekta binfsi katika vyuo vikuu kwa kutoa elimu nchini, vyuo vikuu binafsi vina nafasi ya kuzalisha wataalamu mbalimbali kwa manufaa kwa mtu mmoja mmoja, jamii, taifa na hata nje ya mipaka ya Tanzania.” amesema Rais Mstaafu. 

Katika kukuza na kupanua wigo wa kutoa elimu ya juu nchini, Rais Mstaafu Mkapa atakumbukwa kwa mchango wake wa kuwezesha dini mbalimbali nchini kuwa na vyuo vikuu vyake ikiwemo Chuo Kukuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) kinachomilikiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM) kinachomilikiwa na Kinachomilikiwa na Baraza la Waislam Tanzania, Chuo Kikuu Cha Mt. John Dodoma kinachomilikiwa na Kanisa la Waangikana Tanzania, Chuo Kikuu cha Tumaini kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania pamoja na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Sebastian Kolowa. 

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha SAUT na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Askofu Flavian Kassala ameishukuru Serikali ya Tanzania kuwa msaada kwa kwa sekta binafsi ambapo baraza hilo linathamini na linaiunga mkono Serikali kwa kutoa elimu nchini ili wanaoipa waweze kutoa msaada kwa watu wanaohitaji msaada huo kwa wakati. 

“Kanisa linatoa shukrani kwa Serikali, watu binafsi na taasisi zinazoendelea kutoa mchango kwa SAUT, elimu tunayotoa katika ngazi zote imewasaidia watu kutatua matatizo katika mazingira yao” amesema Askofu Kassala. 

Aidha, Askofu Kassala aliendelea kusema “Tunajenga watu ambao wanazingatia maadili na utu wa mtu kwa kusaidia jamii inayohitaji msaada kutoka kwa watu ambao wamepata elimu, SAUT inamchango mkubwa katika kuwajenga na kuwalea watu kiroho na kimwili kupitia elimu” alisisitiza Askofu Kassala. 

Naye Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Balozi Prof. Costa Ricky Mahalu amesema chuo chao kinaendelea kuzalisha wataalam kwa kwa ajili ya nchi hatua ambayo amemshukuru Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kuwa mlezi na msaada mkubwa kwa maendeleo ya SAUT. 

Balozi Prof. Mahalu amesema kuwa wataalamu wanaoandaliwa katika chuo hicho watokana na vitivo vingine vinne (4) ambavyo ni Kitivo cha Sayansi ya Jamii na Mawasiliano ya Umma, Kitivo cha Biashara na Utawala, Kitivo cha Ualimu, Kitivo cha Sheria na Kitivo cha Uhandisi. 

Hatua hiyo imeungwa mkono na Waziri wa Madini Dotto Biteko ambapo alitoa wito kwa Wanzania na wanafunzi wanaosoma na wanaotarajia kujiunga na chuo hicho kuwa katika utoaji wa elimu ya juu SAUT imejipambanua kuwa ni kinu cha kuandaa wanataaluma na viongozi mbalimbali nchini.  

“Tunabahati ya kuzaliwa kwenye nchi yenye usawa na haki, SAUT inatoa haki ya elimu kwa vijana wetu hatua inayowapelekea kuhama kwenye taifa la kulalamika na kuwa taifa la watu wa matokeo, tunathamini kazi inayofanywa na chuo hiki ambacho kimekuwa kuwa chachu ya malezi kwa kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.” Alisisitiza Waziri Biteko. 

Chuo Kikuu cha SAUT kinamilikiwa na kusimamiwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kimeanzishwa kwa mujibu wa sheria za nchi na kinafanya kazi chini ya Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) kwa mujibu wa masharti ya vyuo vikuu sheria namba 7 ya mwaka 2005 ambapo awali kilikuwa kinajulikana kama Chuo cha Maendeleo ya Jamii Nyegezi (NSTI) kilichoanzishwa tangu mwaka 1960 na wamisionari wa kanisa katoliki ambao kwa sasa wanajulikana kama Wamisionari wa Afrika wakiwa chini ya Askofu Joseph Blomjous  wa Jimbo Kuu la Mwanza.

Waziri Mkuu Awakaribisha Wawekezaji Kutoka Vietnam

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Doanh ambapo amewakaribisha wafanyabiashara kutoka Vietnam waje nchini kuwekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.

Amesema Rais Dkt. John Magufuli ameanzisha Wizara ya Uwekezaji iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuifanya Tanzania kuwa ni mahali bora na salama kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Julai 3, 2019), wakati akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Balozi Doanh. Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar Es salaam.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaalika wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Vietnam waje kuwekeza katika sekta ya viwanda hususani vile vinavyotumia malighafi za mazao ya kilimo yanayolimwa hapa nchini. Hatua hiyo itawawezesha wakulima wa Tanzania kuwa na soko la uhakika la mazao yao.

“Serikali imeendelea kuondoa  vikwazo vya  kuanzisha na kuendesha  biashara  kwa kupitia upya   sheria, kanuni na taratibu za biashara  na kuzifuta zile  ambazo zimethibitika  kuwa zinayafanya mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kuwa magumu.”

Waziri Mkuu amesema kwa kuwa nchi ya Vietnam imepiga hatua kubwa katika ujenzi na uendeshaji wa viwanda vya nguo, Tanzania ingefurahi kuona kwamba viwanda vya aina hiyo vinajengwa hapa nchini na wawekezaji kutoka nchi hiyo.

Amesema kuwa ununuzi wa mazao ya kilimo kama vile pamba, koroshao, kahawa na tumbaku ni fursa nyingine ya kibiashara ambayo wafanyabiashara wa Vietnam wanakaribishwa kuichangamkia hapa nchini.

Akizungumzia kuhusu soko la korosho Waziri Mkuu amesema Tanzania ina korosho za kutosha na inawakaribisha wafanyabiashara kutoka Vietnam waje kuzinunua. Kwa wale wenye uwezo wa kujenga viwanda vya kuchakata korosho nao amewakaribisha na kuahidi kuwa Serikali iko tayari wakati wote kuwasaidia.

Kwa upande wake, Balozi Doanh alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu juu wa ujio wa Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Mhe. Trinh Dinh Dung anayetarajiwa kufanya ziara yake ya kikazi nchini kuanzia Julai 9 hadi 11 mwaka huu.

Alisema Naibu Waziri Mkuu huyo anatarajiwa kuambatana na wafanyabiashara wasiopungua 20 kutoka kampuni kubwa za nchini Vietnam.

Nchi za Vietnam na Tanzania zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1965. Mwaka 1984, Vietnam ilifungua ofisi ya Ubalozi  wake hapa nchini kwa muda na kuufungua upya mwaka 2003.

 (mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Mkuchika: Tanzania Inazidi Kupata Heshima Katika Mapambano Dhidi Ya Rushwa

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
WAZIRI wa nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), George Mkuchika amesema Tanzania inaendelea kupata heshima kubwa katika Jumuiya ya Kimataifa katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa kutokana na mshikamano na nguvu ya pamoja iliyopo katika vyombo na taasisi zinazosimamia utawala bora nchini.

Akizungumza katika kongamano la siku maalum dhidi ya rushwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Julai 3, 2019) Waziri Mkuchika alisema utafiti uliofanywa na taasisi hizo zimesifu juhudi za zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano na kuitaja Tanzania kuwa ni nchi ya mfano katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa.

Mkuchika aliasema taasisi hizo zikiwemo MO Ibrahim, Transparency International, APRM na taasisi nyingine kubwa duniani zinazosimamia masuala ya utawala bora zimefanya utafiti na kusifu juhudi kubwa zinazofanywa na  serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo tafiti mbalimbali zimeifanya Tanzania kushika nafasi ya pili nyuma ya nchi ya Rwanda.

Waziri Mkuchika alisema Serikali ya Awamu ya tano imeendelea kuweka mkazo na msukumo  katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo taasisi zote zinazosimamia masuala ya utawala bora zimekuwa zikiunganisha nguvu ya pamoja na kulifanya suala la rushwa sasa kuwa na nguvu na msukumo mpya wa mapambano katika jamii.

“Kwa sasa vyombo vyetu vyote serikalini si TAKUKURU pekee bali pia polisi, tiss (usalama wa taifa), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ICAG) na vingine vyote, vimeendelea kuunga katika kusimamia masuala ya utawala bora na hili limeleta msukumo na hamasa mpya katika vita dhidi ya rushwa hapa nchini” alisema Waziri Mkuchika

Akizungumzia rushwa katika sekta ya viwanda na biashara, Waziri Mkuchika alisema Serikali imeendelea kuweka mikakati mbalimbali katika kupunguza tatizo hilo ambalo limekuwa likiathiri sekta binafsi ambayo imekuwa mshirika wa karibu wa serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika alisema rushwa katika sekta biashara imekuwa ikiathiri sana masuala ya uwekezaji wa kigeni, ambapo eneo lililonyesha kutawala kwa rushwa ni katika eneo la utoaji wa vibali na leseni kutoka katika taasisi na idara muhimu za serikalini na hivyo serikali imeendelea kulifanyia kazi ili kuhakikisha kuwa vikwazo hivyo vinaondolewa kwa wawekezaji na hivyo kuharakisha ukuaji wa uchumi.

Akifafanua zaidi Mkuchika anasema kutokana na serikali kutambua mchango wa sekta ya viwanda na biashara katika kukuza uchumi na uzalishaji wa ajira nchini ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Serikali imekuwa ikifanya marekebisho mbalimbali ya sheria na sera mbalimbali ambazo zimekuwa ni sehemu ya mianya ya rushwa nchini ikiwemo eneo la kodi.

“Kutokana na kudhibiti rushwa kwa sasa kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya mwezi yameweza kuongezeka kutoka Tsh Bilioni 800 kwa mwezi hadi kufikia Tsh trilioni 1.3 hii inaoyesha kuwa kulikuwa na maeneo ambayo kulikuwa na uvujaji wa mapato ya serikali kulikochangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo rushwa”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Diwani Athumani alisema serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa sekta binafsi kupitia Mpango Mkakati dhidi ya mapambano ya rushwa (NASCAP III) ili kuhakikisha kuwa mapambano na vita dhidi ya rushwa yanapata mafanikio nchini.

Anaongeza kuwa kupitia NASCAP III, ofisi yake imeendelea kutekeleza masuala mbalimbaliu ikiwemo kufanya tafiti kubaini ukubwa na kiwango cha rushwa nchini, kupokea maoni, kutoa elimu kwa umma kupitia makongamano, rushwa pamoja na kufanya uchunguzi na kufungua mashtaka kwa watu mbalimbali wanaopatikana na hatia dhidi ya rushwa.

Rais Kenyatta wa Kenya kufanya ziara binafsi ya siku 2 katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita kwa mwaliko wa Mhe. Rais Magufuli.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Muigai Kenyatta keshokutwa Ijumaa July 5, 2019 atafanya ziara binafsi ya siku 2 hapa nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais Kenyatta atatua katika uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita saa 4:00 asubuhi na kisha kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli katika kijiji cha Mlimani Wilayani Chato.

Akiwa Chato, Rais Kenyatta atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi 4 July

Watoto Wamwaga Machozi Mahakamani Wakitoa Ushahidi Baba Alivyomnyonga Mama Yao

$
0
0
Watoto, akiwamo mmoja wa miaka 10, wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, walivyoshuhudia baba yao wa kambo, Godfrey Nkwambi, akimnyonga mama yao Bahati Hussein.

Watoto hao, huku wengine wakibubujikwa machozi, walitoa ushahidi huo jana katika kesi ya mauaji inayomkabili Nkwambi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Msajili Pamela Mazengo.


Mtoto Hassan Hussein (10) alidai kwamba alimwona baba yake wa kambo, Godfrey Nkwambi, akimnyonga mama yake na kumwamuru asipige kelele.

Hassan ambaye alilala chumbani kwa mama yake (wakati huo akiwa na miaka mitano), alidai kuwa siku ya tukio alimwona baba yake wa kambo ni mshtakiwa katika kesi hiyo, alitoa madai hayo wakati akitoa ushahidi dhidi ya mauaji hayo.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Erick Shija, shahidi huyo alidai siku ya tukio akiwa amelala chumbani kwa mama yake chini kwenye godoro pamoja na mdogo wake aliyemtaja kwa jina la Ibrahim, kwa kawaida mama yake na baba yake wa kambo walikuwa wakilala kitandani.

Siku ya tukio, alidai kuwa usiku alishtuka na alimuona mshtakiwa (baba wa kambo) akimnyonga mama yake na alimwambia asipige kelele na mama yake alikuwa akitikisa miguu huku akitoa sauti kwa mbali.

"Nililala lakini niliposhtuka nilimwona mshtakiwa akifanya hivi halafu hivi (alionyesha mahakama mikono ya mshtakiwa ilivyokuwa imeshika kichwa na kidevu na kukizungusha). Mama alikuwa akipiga miguu kitandani na kutoa kelele kwa mbali, God aliniambia nisipige kelele, mimi nikanyamaza, nikamwona akitoka nje sikujua kilichoendelea kwani niliendelea kulala hadi asubuhi," alidai Hussein.

Alidai kuwa asubuhi alimwacha mama yake akiwa bado amelala, yeye akatoka nje kupiga mswaki na baadaye alikwenda kucheza.

"Siku hiyo sikumwona Godfey na sikujua alikokwenda lakini baadaye nilisikia watu wakilia nyumbani kwetu, ndugu zangu wakaniambia mama yetu mzazi amefariki (dunia)," alidai shahidi huyo na kusababisha ndugu wa marehemu waliofika mahakamani kusikiliza kesi hiyo kuanza kutoa machozi.

Shahidi mwingine ni mtoto wa marehemu, Khadija Abibu (15), aliieleza mahakama kuwa mama yake alifariki dunia Juni 21, 2014 na kwamba Juni 20 alipotoka kucheza alikuta baba yake (mshtakiwa), mama yake na watu wengine wakiwa wamekaa katika mkeka nyumbani kwao Ulongoni.

Alidai kuwa dada yake anayeitwa Hadija Shabani, alimwambia kuwa kulikuwa na ugomvi kati ya baba na mama yake ambao ulisuluhishwa na kwisha na baadaye alimshuhudia mshtakiwa akimpa fedha mama yake akanunue mboga kwa ajili ya chakula cha usiku.

Alidai kuwa majira ya saa 5:00 usiku, alikwenda kuwalaza wadogo zake, Hassan na Rahim, chumbani kwa mama yao na kisha akaenda kulala chumbani kwake pamoja na mtoto wa mama yake mdogo.

"Usiku nilishtuka nikasikia mama na Godfrey wanagombana. Mtoto wa mama mdogo alikuwa anaogopa, nikamwambia yataisha sisi tulale, tukabaki macho kitandani. Mtoto wa mama mdogo akabanwa na haja ndogo, hivyo tukatoka nje kujisaidia," alidai Khadija.

Alidai kuwa walipotoka nje walimwona Godfrey akiwa amekaa katika kochi sebuleni akiwa amevaa kipensi, shati begani huku akitokwa na jasho na kuwahoji wanakokwenda.

"Sisi tulimjibu tunaenda kujisaidia, akasema haya. Tuliporudi tukasikia Godfrey akifungua mlango wa sebuleni na kutoka nje, sisi tulijificha nyuma ya mlango wa sebuleni, tulimsikia Godfrey akimgongea mpangaji wa chumba cha nje na kumuuliza kama alisikia kelele, yule mpangaji akamwambia hakusikia kelele," alidai shahidi.

Shahidi huyo alidai, baadaye walienda kulala, asubuhi aliamshwa na mama mwenye nyumba ambaye alimtaka achukuwe beseni la vyombo apeleke chumbani kwa mama yake.

Huku akitokwa na machozi, shahidi huyo alidai aligonga mlango lakini mama yake hakuitikia na alipoingia ndani alimkuta mama yake amelala akiwa amefunikwa shuka jeupe na kanga kichwani, alimtikisa hakuamka na kutoka nje huku akipiga kelele.

"Nilikuta mama kalala, niliendelea kumwamsha bila mafanikio, nikamfunua alikuwa hajavaa nguo, nikamshika kifua kuona kama roho yake inadunda, ilikuwa haidundi, nikatoka nje nikipiga kelele. Mama mwenye nyumba aliniuliza nikamwambia mama yangu hahemi amefunikwa nguo, majirani walikuja na kumwangalia, wakasema atakuwa amezimia, wakamvalisha nguo na kumpeleka hospitalini," alidai.

Khadija alidai kuwa watu waliorudi kutoka hospitalini walimwambia kuwa mama yao amekufa na alinyongwa. Alidai kuwa mama yake alinyongwa na Godfrey kwa sababu alishawahi kumtamkia kuwa atamuua yeye na familia yake kwa kuwa hataki kuiona.

"Mama pia alishawahi kunambia kwamba, 'mwanangu nikifa Godfrey ndiye kaniua," alidai.

Naye shahidi Khadija Shabani, ambaye alikuwa akimwita marehemu shangazi, aliieleza mahakama kwamba wawili hao walikuwa na ugomvi na kwamba Godfrey alikuwa akimtuhumu Bahati kuwa na uhusiano wa kimapenzi na jirani yao.

Taarifa kwa Umma kutoka TCRA kuhusu Mawakala wanaosajili laini za simu

$
0
0
Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzaia (TCRA) inaendela na utekelezaji wa zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya biometria, TCRA imebaini kuwa kuna watu wanaojihusisha na usajili wa SIMU bila kuidhinishwa na watoa huduma za mawasiliano.
 
Kwa mujibu wa kifungu cha 92 na 97 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, 2010 na Kanuni ya 9,10, na 11 ya Kanuni za Usajili wa Laini za Simu (Sim Card Registration Regulations, 2018), TCRA inapenda kuutaarifu na kuukumbusha Umma kuwa:-
  1. Ni marufuku kwa mtu yeyote kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kuwa na uthibitisho kuwa ameidhinishwa na mtoa huduma za mawasiliano kutoa huduma hizo;
  2. Yeyote anayejihususha na uuzaji, usambazaji au usajili wa laini za simu anatakiwa kuwa na ofisi ya kutolea huduma hiyo ya usajili wa laini za simu; na
  3. Ni kosa la jinai kwa mtu yeyoye kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kuwa na ofisi na uthibitisho wa idhini ya mtoa huduma husika.
Umma unakumbushwa na kuonywa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani pamoja na faini, kwa mtu yeyote atakaye bainika kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kufuata taratibu.
 
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu, 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images