Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Pinda: Mnapaswa Kudumisha Nidhamu Ya Matumizi Ya Fedha Baada Ya Kustaafu

$
0
0
NA. MWANDISHI  WETU
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda amewaasa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni kudumisha nidhamu katika matumizi ya fedha baada ya kustaafu utumishi wa umma na kujikita katika shughuli za uzalishaji.

Akizungumza katika makazi yake yaliyopo Zuzu Jijini Dodoma  wakati watumishi hao walipomtembelea Juni 20, 2019 kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji katika sekta ya kilimo na mifugo ikiwa ni sehemu ya  maandalizi ya kustaafu pamoja na kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma , Mhe Pinda amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa watumishi wote wanaotarajia kustaafu kujenga utamaduni wa nidhamu katika matumizi ya rasilimali ikiwemo fedha watakazopata kama kiinua mgongo.

" Nidhamu ya maisha baada ya kustaafu ni muhimu sana hivyo niwaase mjitahidi kuacha baadhi ya masuala ambayo mnafanya  kwa sasa kama starehe na mambo yote yanayoendana na kupoteza muda wenu badala yake mjikite katika uzalishaji" Alisisitiza Mhe. Pinda

Aliongezea kuwa  ni vyema watumishi  hao wakajenga utamaduni wa kufanya kazi za uzalishaji na kujikita katika usimamizi wa  miradi ya uzalishaji watakayoanzisha kwa lengo la  kujiongezea kipato na kukuza uchumi .

Pia aliwaasa watumishi hao kuzingatia mawazo kutoka kwa watumishi ambao wameshastaafu na wamefanikiwa  kimaisha baada ya kustaafu.

"Kila mmoja wenu akatekeleze miradi ya kujikwamua kiuchumi kwa kuzingatia mafao atakayopata badala ya kutaka kufanya mambo kwa mashindano bali kila mtu ajikune kulingana na mkono wake unapoweza"

Kwa upande wake Katibu mkuu wa  Ofisi ya Waziri Mkuu  (Bunge na Waziri Mkuu) Bi Maimuna Tarishi amesema kuwa mafunzo yakuwajengea uwezo wa kujiandaa  kustaafu,  yameandaliwa ikiwa ni sehemu ya  maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma.

Aliongeza kuwa watumishi hao wamefarijika kuona shughuli za uzalishaji anazofanya Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Pinda na kuwa ni mfano kwa watumishi wa umma wanaostaafu  na kuanza kujikita katika uzalishaji mali .

Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa mafunzo ya siku 5 kwa watumishi wake wanaotarajia kustaafu ili kuwapa mbinu za kisasa zinazolenga kuwawezesha kuendelea na maisha yao baada ya kustaafu huku wakiendeleza shughuli za uzalishaji  zitakazowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku na kuweza kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu.

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Yaimarisha Utendaji wake Kwa Kutumia TEHAMA

$
0
0
Na Frank Mvungi- MAELEZO
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imetajwa kuongeza tija katika utendaji wake kutokana na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)katika huduma zake kwa wadau.

Akizungumza katika kipindi cha “TUNATEKELEZA”   Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Prof. Lazaro Busagali amesema kuwa Tume hiyo imeimarisha utoaji wa huduma zake kwa wadau kuanzia katika utoaji wa vibali na huduma zote ikiwemo za maabara.

“ Tunaipongeza na kuishukuru Serikali kwa kuiwezesha Tume kuwa na  Ofisi za Kanda 21 na asilimia 90 ya vibali vinatolewa ndani ya siku moja kutokana na kuimarishwa kwa miundombinu yetu ya kutolea huduma “ Alisisitiza Prof. Busagali

Akifafanua Prof. Busagali amesema kuwa Teknolojia ya nyuklia ikitumika vizuri inaleta matokeo chanya katika jamii kwa kuwa ni muhimu katika kuchangia maendeleo kutokana na umuhimu wake katika kuchochea maendeleo.

Akizungumzia utendaji wa Tume hiyo Prof. Busagali amesema kuwa moja ya majukumu ya Tume ni kuhakikisha kuwa Taasisi zote zinazotumia mionzi katika kutoa huduma zake zikiwemo Hospitali zinazingatia matumizi bora ya mionzi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia  sekta hiyo.

Aliongeza kuwa Tume hiyo imekuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara katika Taasisi zote zinazotumia mionzi   hapa nchini ili kuhakikisha kuwa watumiaji wa huduma za Taasisi husika wako salama dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi.

Aidha alifafanua kuwa, Tume imejiwekea utaratibu wa kutoa  elimu kwa wananchi na wadau ili kuepuka matumizi ya mionzi yasiyozingatia sheria, kanuni na taratibu ili kuepusha madhara ya mionzi hiyo pale inapotumika vibaya.

“Serikali ya Awamu ya Tano imetuwezesha kuwa na maabara ya kisasa na pia wadau wetu ambao ni  Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani kwa kutuwezesha kupata vifaa vya kisasa vya maabara yetu” Alisisitiza Prof. Busagali.

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ni Taasisi ya Serikali inayosomamia na kuratibu masuala yote yanayohusu mionzi hapa nchini ikiwa na maabara ya kisasa ambayo ni mwanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Trump Kasema Kilichomfanya Asiishambulie Kijeshi Irani Ni Kuhofia Vifo vya Watu 150.....Jana Iran Iliitungua Ndege Moja ya Marekani

$
0
0
Rais wa Marekani Donald Trump amesema leo kuwa alisitisha shambulizi la kijeshi dhidi ya Iran kwa sababu jibu kama hilo kwa hatua ya Iran kutungua ndege ya Marekani isiyoruka na rubani lingesababisha idadi kubwa kabisa ya vifo. 

Katika mfululizo wa ujumbe aliondika kwenye mtandao wa Twitter, Trump amesema vikwazo vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Iran vinafanya kazi na vingine vimetangazwa jana usiku kufuatia kuharibiwa kwa ndege ya Marekani isiyoruka na rubani iliyotunguliwa na kombora la Iran.

Trump amesema mpango ulikuwa ni kulipua maeneo matatu tofauti ya Iran kama jibu la kitendo cha Iran, na kuwa aliambiwa watu 150 wangeuawa na ndio maana akasitisha shambulzii hilo zikiwa zimesalia dakika 10 tu kwa ndege za Marekani kufyatua makombora.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya June 22

Bodi ya TCRA watembelea maktaba mpya ya kisasa UDSM

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
BODI ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), pamoja na Menejimenti ya Mamlaka hiyo, zimemefanya ziara kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere ili kujionea jengo jipya la kiwanja hicho, Terminal III (TBIII), pamoja na Maktaba mpya na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.

Ziara hiyo iliyofanyika Ijumaa Juni 21, 2019 pia iliwahusisha wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA.

Akizungumzia  nia ya ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba alisema, Mamlaka kama Mdhibiti na Msimamizi wa Mawasiliano nchini, imeona ni vema kutembelea taasisi hizo mbili kwani kuna mambo ya msingi yanayofanywa na taassi hizo yanahusiana moja kwa moja na huduma zinazotolewa na TCRA.

“Lengo la ujio wetu hapa Terminal III nikuangalia katika hatua hizi ambazo ujenzi umekamilika ni mahitaji yapi ambayo bado ili sisi tuongeze ushiriki wetu ili kuyakamilisha hususan katika mifumo ya mawasiliano.” Alsiema Mhandisi Kilaba.

Alisema wakiwa hapo TBIII wamepata fursa ya kuulizia hali ya mawasiliano kama imekamilika ambapo watoa huduma, TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo, Zantel, Halotel na hata Internet kama wako tayari.

“Huduma hizi ni muhimu sana na zinatakiwa ziwe kwenye maeneo kama haya kwa sababu zinawezesha hata kufanya utalii kuwa rahisi, mgei anapoingia hapa na anataka kwenda eneo Fulani la utalii lazima awasiliane, lakini pia TCRA inatoa masafa kwa ajili ya kuongozea ndege zinapotua na kuruka na lengo hasa ni kuhakikisha hakuna muingiliano katika huduma hizo." Alibainisha Mkurugenzi huyo Mkuu wa TCRA.

"Kuja kwetu kumetupa fursa ya kujifunza mengi kama ambavyo watanzania wanaweza kushuhudia kuwa kiwanja hiki ni kizuri, kinapendeza na mawasiliano yapo yanaendelea kukamilishwa na tumejionea hata Wifi point ipo.” Alifafanua Mhandisi Kilaba.

Aidha kuhusu Maktaba mya ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhandisi Kilaba alisema, Maktaba hiyo inatumia huduma za TCRA kwani moja ya huduma zitolewazo ni pamoja na Maktaba mtandao (e-library) na hili ni jambo jema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt.Jones Killimbe alisema, ziara hiyo imekuwa ni ya mafanikio makubwa kwani imewezesha timu nzima ya TCRA, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti, Wajumbe wa Kamati zinazosaidia kutekeleza majukumu kwenye mamlaka  kwa pamoja wameelimika sana.

“Kiwanja hiki  katika lugha ambayo ningeiazima ni flagship project….ni mradi wa kimkakati wa taifa hili... nikisema kimkakati ni kwasababu mojawapo ya masuala ya kiuchumi ya nchi yetu ni utalii, na nadhani huu utakuwa mlango mkubwa sio dirisha…utakuwa mlango mkubwa wa utalii na mchango wa utalii kwenye uchumi wetu utaongezeka sana.” Alisema Dkt. Killimbe.

Ziara hiyo imewezesha wajumbe kupata maelezo ya kina ya kukamilika kwa huduma mbalimbali kwenye jengo la TBIII hali kadhalika kwenye maktaba ya ksiasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaa,

 

Misri Yaanza Vizuri Michuano ya AFCON Kwa Ushindi wa Bao 1:0 Dhidi ya Zimbabwe

$
0
0
Michuano ya 32 ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika imefungua pazia lake nchini Misri jana Ijumaa kwa mchezo kati ya wenyeji Mafarao wa Misri  dhidi ya timu ya taifa ya Zimbabwe.

Katika mchezo huo wa kundi A wenyeji Misri wameichapa Zimbabwe bao moja kwa bila mbele ya zaidi ya mashabiki 70,000 waliofurika katika uwanja wa kimataifa wa michezo mjini Cairo.

Kiungo wa timu ya taifa ya Misri, Mahmoud Trezeguet ndiye aliyewatoa kimasomaso wenyeji hao wa michuano ya 32 ya kombe la mataifa ya Africa wakati wa mechi hiyo ya ufunguzi iliyokuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki wa kandanda nchini Misri.

Bao lake la mnamo dakika ya 41 lilisadifu kuwa muhimu kuiwezesha timu yake kijinyakulia alama tatu za mapema katika fainali hizo zitakazoendelea karibu mwezi mzima.

Bao la Trezeguet liliibua shangwe na kuizima kwa muda nyota ya mshambuliaji mashuhuri anayeichezea ligi ya Premier Mohamed Salah ambaye alishangiliwa kwa nguvu mara zote alipougusa mpira.

Salah alipata nafasi mbili muhimu katika dakika za awali za mchezo na baadaye wakati wa kipindi cha pili lakini hakufanikiwa kutikisa nyavu za wazimbabwe.

Wivu Wa Mapenzi Wasababisha Mauaji Shinyanga

$
0
0
SALVATORY NTANDU
Mkazi wa Mhunze wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Rafael Martine (34) anashikililiwa na Jeshi la polisi kwa Tuhuma ya kumuua Shija Mahoiga (45) mkazi wa kijiji cha Igaga kwa kutumia kipande cha chuma baada ya kumfumania akiwa amelala na mkewe.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Richard Awabwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea june 21 majira saa tatu usiku nyumbani kwa Marehemu ambapo Rafael anatuhumumiwa kumshabulia kwa kumpika katika sehemu mbalimbali na kusababisha kifo.

Amefafanua kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi ambapo Rafaeli alivunja Mlango nyumba ya marehemu na kuanza kuwashambulia wawili hao hadi kusababisha kifo cha Marehemu huku mkewe aliyefahamika kwa jina la Maria Shija akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya kishapu kwa matibabu.

Kamanda Abwao ametoa wito kwa watu mkoani humo kutojichukulia sheria mkononi kwa kuheshimu sheria za nchi na na baada ya upelelezi mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira Ahimiza Ushirikiano kwa Watumishi

$
0
0
Na; Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe amewaasa watumishi wa ofisi hiyo kufanyakazi kwa ushirikiano ili waweze kutumiza malengo waliyojiwekea.

Hayo ameyasema wakati alipokutana na watumishi wa ofisi yake Dodoma kwa lengo la kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika kila mwaka kuanzia Juni 16 hadi 23 kwa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la kuonesha mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya nchi zao na Bara la Afrika kwa ujumla ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni;

“Uhusiano kati ya uwekezaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Jenga utamaduni wa Utawala bora, matumizi ya TEHAMA na Ubunifu katika utoaji wa huduma jumuishi.”

Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo ipo kisheria Katibu Mkuu huyo alisema kuwa Ofisi hiyo ina majukumu makubwa ya kiutendaji hivyo watumishi wanawajibu wa kufanyakazi kwa kushirikiana na kujenga umoja.

“Ushirikiano katika kazi ni muhimu na husaidia kuboresha mifumo ya kiutendaji ikiwemo kuwa na mikakati endelevu ya ofisi, mawasiliano mazuri, kujenga mahusiano mazuri na wadau na kutoa huduma bora kwa wananchi,” alisema Massawe.

Sambamba na hilo aliwasihi watumishi wa ofisi hiyo kufanyakazi kwa bidii, weledi, uzalendo na kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao na utoaji wa huduma kwa wadau na wananchi.

Pia amewashauri watumishi hao kuepukana na vitendo vya rushwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na maadili ya Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia haki na usawa.

Aidha, Katibu Mkuu alikutana na kufanya kikao na wadau mbalimbali wa nje na alipokea maoni na mrejesho wa huduma zinazotolewa na Ofisi ya Waziri kuhusu sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira, Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii na masuala ya Vyama vya Wafanyakazi.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Peter Kalonga aliafiki yaliyosemwa na kuahidi kuahidi kufanyia kazi maagizo hayo ikiwemo suala la ushirikiano na mawasiliano katika utendaji kazi baina ya watumishi ili kuimarisha mshikamano baina ya watumishi.

Kwa upande wake alisema kuwa kikao hiko kimewezesha watumishi wa ofisi hiyo kubadilishana taarifa zaidi za kiutendaji na kitasaidia kuimarisha ushirikiano baina yao.

Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) chatoa Onyo Kali Kwa Viongozi Wa Vyama Vya Msingi Ambao Vyama Vyao Vitabainika Kufanya Udanganyifu.

$
0
0
SALVATORY NTANDU
Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Katika mkoa wa kitumbaku Kahama, kimekitoza faini ya shilingi laki 300,000  viongozi wa chama cha Msingi Mweli baada ya kubainika kwa mwanachama wake  kubainika  kuchanganya tumbaku safi na Chafu kwenye mabelo yake sokoni kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hayo yamebainishwa leo na Mwenyekiti wa (KACU) Emanuel Charahani baada ya kubaini tumbaku ya Majaliwa Joseph Masaluta Mkulima na mkazi wa bulungwa katika halmashauri ya Ushetu kufayanya udanganiyifu huo huku viongozi wake wakishindwa kuchukua hatua za haraka kabla ya kuingizwa sokoni.

Amefafanua kuwa Majaliwa  alikuwa na Mabelo  50 yenye zaidi ya kilo 500 ambayo yamebainika kuwa na mchanganyiko wa tumbaku safi na chafu na kwa hatua ya awali ambazo zimekwisha chukuliwa ni pamoja na kuziondoa sokoni tumbaku hizo ili  ukaguzi wakina uweze kufanyika.

Katika hatua nyingine Charahani amesema wakulima waliosajiliwa kulima  zao la tumbaku katika mkoa huo wamelima walikuwa 4,670 na wamelima hekta 5,888 na kuzalisha tumbaku zaidi ya kilo Milioni 8.1 kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na matarajio ya Kampuni zinazonunua zao hilo kwa mkataba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha ushirika KACU Wilayani hapa Emmanuel Charahani alikili kuwepo kwa vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikijitokeza kila msimu wa uzaji wa tumbaku nakuongeza mwaka huu wamemkamata mkulima mmoja kutoka chama cha msingi Mweli Majaliwa Joseph Masaluta.

Alisema kuwa,alikuwa na tumbaku mabero 50 yenye zaidi ya kilo 500 ambayo yalibainika kuwa na mchanganyiko wa tumbaku safi na chafu na kwa hatua ya awali tumbaku hizo zimeondolewa kwenye soko kwa ajili ya ukaguzi wakina na ikibaika ni mabero yote atafutiwa kibali cha uzalishaji wa zao hilo.

 Hivi karibuni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alizitaka mamlaka zinazosimamia zao hilo ikiwemo bodi ya Tumbaku Tanzania kuchukua hatua kali kwa wakulima wote waytakaobainika kufanya udanganyifu huo ambao unaweza ukasababisha nchi ikakosa mapato kutokana na tumbaku chafu.

Amesema endapo hatua za dharura zisipo chukuliwa na mamlaka husika huenda kampuni zinazoendelea kununua zao hilo hapa nchini zikasitisha kufanya biasha na Tanzania kutokana na kupata hasara inayosababishwa na wakulima wasio waaminifu na kuwataka viongozi wote wa vyama vya msingi kuhakikisha wanasimamia kwa makini suala la ufungashaji wa tumbaku.

Bunge Sports Club Kutoana Jasho Na Timu Ya NMB Katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma Leo Juni 22,2019.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Bunge Sports Club leo Juni 22,2019  wanatimuana Vumbi nene  katika Bonanza la Michezo mbalimbali  na timu ya wafanyakazi Benki ya NMB mchezo  unaocharazwa kuanzia Majira ya  saa 12:00 asubuhi. 

Akizungumza na waandishi wa Habari katika  hafla fupi ya makabidhiano ya jezi za mchezo kutoka NMB Benki Kwenye Ukumbi wa Habari,Bunge, jijiniDodoma meneja wa  timu Ya Bunge Sports  Club  ,Mbunge wa Ulyankulu Tabora  Juma Peter Kadutu  amesema amesema wamejiandaa kuwabamiza vyema NMB na kilichobaki ni kutimuliwa Vumbi tu kwani kila mwaka NMB Wamekuwa  wakifungwa. 

Kadutu ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tabora, na mjumbe wa TFF amesema wana uhakika wa kushinda kwa michezo yote ikiwa ni pamoja na mpira  wa pete na watachukua kikombe. 

Aidha,amesema wanajiandaa na michezo ya wabunge Afrika Mashariki ambayo hufanyika kila Mwaka huku mwaka huu ikitarajiwa kufanyika nchini Uganda huku pia akitumia fursa hiyo kuipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kusapoti kila Mwaka. 

Mkaguzi wa ndani Benki ya NMB makao makuu  Bw.Juma  Kimori amesema Benki ipo sambamba na serikali katika kusaidia masuala ya kijamii. 

Meneja wa NMB kanda ya kati ,Nsolo Mlozi amesema Benki hiyo imejikita kutoa huduma katika maeneo makuu manne katika kusaidia jamii ambayo ni sekta ya  afya,Elimu,elimu  Fedha na kuhudumia jamii katika majanga. 

Aidha,amesema asilimia  1%  ya  mapato hurudi kuhudumia jamii ambapo asilimia 1%  ya mwaka jana zilitengwa zaidi ya Tsh.Bilioni 1 na mpaka sasa zaidi ya Tsh.Milioni 450 zimetumika. 

Michezo inayochezwa katika Bonaza hilo ni pamoja na Mpira wa miguu,mpira wa pete,mpira wa kikapu na Jogging.

Waziri wa Viwanda na Biashara Awahakikishia Soko la Uhakika Wakulima wa Tumbaku

$
0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali itatafuta wanunuzi wa zao la Tumbaku endapo Kamapuni iliyokuwa inanunua awali ya TLTC haitaendelea na ununuzi huo.

Amesema kuwa tayari Kampuni ya GTI imekubali kushirikiana na Serikali kununua zao hilo kutoka kwa wakulima msimu ujao.Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo alipokutana na wawakilishi wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) ambapo aliahidi kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo kwa lengo la kujadiliana namna ya kupata kampuni itakayoweza kununua zao la tumbaku kutoka kwa wakulima.

‘’Tutazungumza na kampuni ya awali iliyokuwa ikinunua tumbaku kama watakubali kuendelea kununua zao hilo au kama hawawezi basi serikali itatafuta wanunuzi wengine watakaonunua zao hilo kwa wakulima msimu ujao,’’ alisisitiza.

Aliongeza kuwa wadau wengi wameipongeza serikali kwa kuwa na bajeti rafiki iliyosikiliza wadau wa viwanda na biashara kuhusu masuala ya tozo na kodi mbalimbali.

Bashungwa alisema Serikali itaendelea kuondoa vikwazo vilivyokuwepo kwenye sekta ya biashara kwa lengo la kuleta unafuu na kukuza biashara, ajira na mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wa sekta binafsi.

Naye, Mkurugenzi wa Mahusiano Godson Killiza kutoka TCC alisema kitendo cha serikali kupunguza kodi ya bidhaa mbalimbali ni jambo linaloleta faida kwa wafanyabiashara watanzania kutumia malighafi za ndani kuzalisha bidhaa.

Alisema bajeti ya serikali ya 2019/2020 italeta faida katika ukuaji wa uchumi, kukuza biashara na kupunguza gharama za uzalishaji kwa kampuni nyingi.

Killiza alisema ongezeko la Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa asilimia nane katika biashara yao imesaidia kuongeza ulipaji wa kodi kutoka Sh bilioni 227 mwaka 2017 hadi Sh bilioni 234 mwaka jana.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili June 23

Mkuu wa Majeshi Ethiopia apigwa risasi

$
0
0
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amefahamisha kuwa mkuu wa majeshi Seare Mekonen alipigwa risasi baada ya kuzuka machafuko Jumamosi jioni katika taifa hilo la Pembe ya Afrika. Hata hivyo hali ya mkuu huyo wa jeshi haijulikani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa shirika la habari la AFP,  Abiy alizungumza kupitia kwenye televisheni ya taifa akiwa amevaa mavazi rasmi ya kijeshi baada ya kutokea jaribio la mapinduzi katika jimbo la Amhara lakini maelezo zaidi hayakutolewa kuhusiana na lengo la mashambulio hayo katika jimbo la pili lenye watu wengi zaidi nchini Ethiopia linaloongozwa na Rais wa kikanda Ambachew Mekonen.

Ubalozi wa Marekani ulitoa tahadhari baada ya kusisikia milio ya bunduki katika mji mkuu wa Addis Ababa, na pia vurugu karibu na mji mkuu wa jimbo la Amhara, Bahir Dar.

Serikali ya Ethiopia imesema jaribio hilo la kuipindua serikali ya kikanda kaskazini mwa nchi hiyo lilishindikana. Ofisi ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imelaani jaribio hilo la mapinduzi katika ujumbe wa Twitter uliochapishwa Jumamosi jioni.

Kagame Azungumzia Uwezekano wa Kutokea Vita Kati ya Rwanda na Uganda

$
0
0
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amepuuza uwezekano wa nchi yake kuingia vitani na Uganda, ingawa amesisitiza kuwa nchi hiyo jirani inafadhili waasi wa nchi yake.

Kagame amesema hayo katika mahojiano na Gazeti la Taz la Ujerumani, wakati wa mkutano wa kimataifa jijini Brussels, Ubelgiji na kunukuliwa na The Daily Monitoe la Uganda.

Katika majibu yake kuhusu kuongezeka kwa wasiwasi katika uhusiano wa nchi hizo jirani, Kagame alisema “Watu wanahofia vitana baina yetu (Uganda na Rwanda). Sioni kama kuna vita vinakuja kati yetu, nadhani Uganda inajua gharama zake. Hatutaki kwenda chini katika njia hiyo kwa kuwa kila mmoja atapoteza kitu,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu onyo la vita alilolitoa kwa Uganda Aprili, Rais Kagame alijibu: “Ndiyo, (vita vitatokea) ikiwa utavuka mpaka.

"Unaweza kufanya chochote unachotaka ndani ya himaya yako, kama kukamata watu. Lakini ukivuka mpaka wetu na kutaka kufanya mambo ndani ya himaya yetu – hicho ndicho nilichomaanisha.”

Rwanda imekuwa inaituhumu Uganda kwa kuwakamata watu wake na kuwashikilia wakati mwingine ikiwa kimya na bila kuwafungulia mashtaka, jambo ambalo Kagame alilieleza gazeti la Ujerumani kuwa halikuwa zuri.

Alisema Uganda ingelitumia sheria zake kumshtaki Mnyarwanda yeyote anayekamatwa badala ya kuwashikilia kwa muda mrefu kwa madai ya kuifanyia ujasusi na baadaye kuwaachia.

Taarifa Umma kuhusu Kikao cha Kamati Kuu(CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi.

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kinatarajia kufanya vikao vyake Kamati Kuu (CC) pamoja na Halmashauri kuu (NEC) wiki ijayo Dar es Salaam.

Wakati kikao cha kamati kuu vitafanyika Juni 26, 2019 kikao cha NEC kitafanyika Juni 27,2019 na kitakuwa cha kawaida kwa mujibu wa kalenda ya chama na Katiba ya CCM ibara ya 101(2).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari  Ijumaa Juni 22, 2019 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ilisema kikao cha Kamati kuu kikitanguliwa na vikao vya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachofanyika Juni 24,2019 na kufuatiwa na semina ya makatibu wa mikoa Juni 25, 2019.


Waziri Mkuu: Watumishi Ni Muhimu Kushiriki Michezo

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ni muhimu kwa watumishi kushiriki katika michezo mbalimbali kwa kuwa inaimarisha afya pamoja na kudumisha mshikamano.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Juni 22, 2019) wakati wa bonanza kati ya Wabunge na watumishi wa benki ya NMB lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema mbali na kuimarisha afya kwa watumishi na wabunge, pia michezo inasaidia katika kuimarisha mshikamano baina ya benki hiyo pamoja na wateja.

Akizungumzia kuhusu utendaji wa benki ya NMB, amesema imekuwa ikishirikiana na Serikali kuwaelimisha wakulima umuhimu wa kufungua akaunti na kujiwekea akiba.

“Benki ya NMB ni benki pekee iliyomudu kufungua matawi hadi maeneo ya vijijini, hivyo kurahisha upatikanaji wa huduma kwa watumishi na wananchi waishio maeneo hayo.”

Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu ambapo timu ya Bunge ilishinda baada ya kuifunga timu ya benki ya NMB magoli matano kwa matatu.

Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuifunga timu ya NMB magoli 25 kwa 18, huku katika mchezo wa mpira wa kikapu timu ya NMB ilishinda baada ya kuifunga Bunge vikapu 52 kwa 51.

Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za NMB.
 
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Watafiti Watakiwa Kutumia Mbinu Za Kisayansi Ili Kuleta Tija Katika Jamii

$
0
0
Na. Peter Haule na Farida Ramadhani WFM, Dodoma
Watafiti nchini wametakiwa kuweka mkazo katika mbinu za utafiti zinazokidhi viwango vya kimataifa ili kuwa na majibu ya tafiti zenye tija zilizo na lengo la kutatua changamoto katika jamii ya watanzania na duniani kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe, alipokuwa akifungua warsha ya Watafiti kutoka nchi ya Kenya, Afrika Kusini, Rwanda, Uganda na wenyeji Tanzania, uliofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

Mtahiki Meya Mwamfupe, alisema kuwa ili utafiti uwe na thamani nilazima kutumia mbinu zinazoaminika bila kujali utafiti unaofanyika unahusu kitu gani, kwa lengo la kuondoa mkanganyiko wa matokeo hivyo kuwa na tija kwa jamii.

“Utafiti wa kisayansi ni ule unaotumia njia zinazokubalika kimataifa na kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto zikiwemo za kutokuwa na usawa hasa katika pande mbili za Dunia yani Kasikazini na Kusini lakini pia katika jamii moja na nyingine”, alieleza Meya Prof. Mwamfupe.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda, ambaye alikua mtoa mada katika warsha hiyo alisema kuwa, katika wasilisho lake wadau kutoka nje ya nchi wamefurahishwa na uchambuzi kuhusu hali ya uchumi ambapo ilielezwa namna watu wenye kipato kikubwa kupenda kununua bidhaa nje jambo ambalo limeifanya Serikali ya Tanzania kuweka mikakati ya kutatua tatizo hilo ili kujenga uchumi wa bnchi.

Alisema kuwa tabia ya wenye kipato kikubwa kununua bidhaa nje kuna kosesha ajira, hivyo Serikali imeamua kuweka mikakati ya Ujenzi wa uchumi katika Nyanja ya viwanda, kilimo na miundombinu ikiwemo ya umeme, jambo ambalo ni ajenda ya Afrika

Kwa upande wake Mratibu wa Warsha hiyo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Cha Mipango Vijijini, Dkt. George Kanyasi, alisema kuwa lengo la Warsha hiyo ni kuwakutanisha watafiti wanaochipukia na wanasayansi kutoka nchi tano za Afrika kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kupata watafiti mahiri.

Amesema kuwa kazi ya tafiti sio tu kuongeza maarifa lakini pia kutatua changamoto katika maeneo yaliyokosa usawa katika elimu, uchumi, siasa na masuala ya kijamii

Mkutano huo pamoja na kuwashirikisha watafiti kutoka nje ya nchi, pia umewahusisha baadhi ya wadau kutoka Halmashauri ili kujua changamoto zao na kuweka mikakati ya kuzitatua, aidha warsha zinazofuata zitawakutanisha Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Mipango ili waweze kubaini matatizo ya maeneo yao na waweze kuyatatua.

Mwisho

Watumishi Mambo Ya Ndani ‘waikosha’ Hospitali Ya Mirembe, Wapewa Elimu

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MOHA
UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa ya Wagonjwa wa Akili ya Mirembe, mkoani Dodoma, umefurahishwa na kitendo cha watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenda kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapo.

Pongezi hizo zimetolewa na Kaimu Mganda Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt. Escor Tweve. Watumishi hao wakiwa na baadhi ya viongozi wa Wizara, idara zilizopo chini ya Wizara hiyo, waliadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapo.

“Nawashukuru kwa uamuzi wa kuja kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapa kwa kufyeka, kulima, kuchoma taka, kudeki na kufanya kazi nyingine za kijamii. “Mmeonyesha upendo mkubwa mlionao dhidi yetu, mmejitoa kwa moyo wa dhati, miaka mingi imepita hatujawahi kupata ugeni uliofanya jambo muhimu kama hili,” alisema Dkt. Tweve.

Mbali ya kufanya usafi wa mazingira, watumishi hao walipata fursa ya kupewa elimu juu ya huduma zinazotolewa kwa wagonjwa hospitalini hapo.  Dkt. Tweve alisema changamoto kubwa waliyonayo wagonjwa wa akili huwa hawapendwi katika jamii ila ni watu wanaopaswa kupewa upendo mkubwa na jamii.

“Wagonjwa wa akili hawana tofauti na watu wengine ambao hawana matatizo kama yao kwenye jamii, wanapoletwa hapa hospitali huwa tunawapatia matibabu, kupona, kutoa michango mizuri kwenye jamii na nchi kwa ujumla,” alisema. 

Aliishukuru Wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa wanaowapa kwani kuna wagonjwa wengine wa akili hukamatwa, kuhitajika kufanyiwa matibabu hospitalini hapo.

Pia wapo baadhi ya watumishi wa idara za serikali wakiwemo askari ambao hospitali hiyo huwapatia matibabu ya akili, kupona, kuendelea na majukumu yao ya kazi. 

“Naishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuadhimisha siku hii kwa kuja Mirembe na kufanya usafi wa mazingira, nawaomba muwe na utaratibu wa kuja mara kwa mara,” alisisitiza.

Aliwapongeza watumishi wa Wizara hiyo na viongozi wao akiwemo Waziri Kangi Lugola, Naibu Waziri, Mhandisi Hamad  Masauni, Katibu Mkuu, Meja Jenerali Jacob Kingu, Naibu KaribuMkuu, Ramadhani kailima kwa utendaji mzuri wa kazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha TEHAWA katika Wizara hiyo, Jane Massawe ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu, aliushukuru uongozi wa hospitali hiyo kwa ushirikiano walioutoa kwa watumishi  hao. 

“Tumefurahishwa na mapokezi mliyotupa, tupatapo nafasi kwa siku nyingine tutakuja kuwatembelea na kufanya shughuli za kijamii,” alisema Massawe.

Wiki ya Utumishi wa umma ilianza huadhimishwa kuanzia Juni 17 hadi 22, mwaka huu. Maadhimisho hayo ni kwa mujibu wa Kalenda ya Umoja wa Afrika (AU).  Nchi mbalimbali huadhimisha siku hiyo kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu utumishi wa umma.

Vanessa Mdee atangaza rasmi kuachana na Juma Jux

$
0
0
Msanii wa Bongo Fleva Vanessa Mdee ametangaza rasmi kupitia Instagram story yake kuwa ameachana na aliyekuwa mpenzi wake Juma Jux baada ya shabiki kuuliza kama wameachana   na Jux.

Vanessa Mdee alijibu ‘Ndio, lakini ni marafiki wazuri sana na tutabaki kuwa familia daima’ swali hilo limekua likionekana kutojibiwa mara nyingi endapo wawili hao wakiulizwa kuhusu penzi lao kuvunjika, siku kadhaa zilizopita Mimi Mars ambaye ni mdogo wake Vanessa aliweka wazi kuwa Jma na Vee wameachana na wamebaki kama marafiki.

Juma Jux pamoja na Vanessa walianza mahusiano yao miaka kadhaa iliyopita na August 2017 walitengana lakini ndani ya mwaka huo huo wa 2017 walirudiana rasmi juu ya stage kwenye tamasha la Fiesta lilofanyika Dar Es Salaam.

Wakala wa CIA anyongwa nchini Iran

$
0
0
Taarifa iliyotolewa na mahakama ya kijeshi nchini Iran inasema adhabu ya kunyongwa hadi kufa aliyopewa jasusi wa CIA na Marekani,Jalal Haji Zevar imetekelezwa katika gereza la Recai Shar lililopo kerec kaskazini magharibi mwa Tehran.

Taarifa hio inasema kwamba Zevar aliachishwa kazi mwaka 2010 na kufunguliwa mashitaka ya ujasusi, kutokana na uthibitisho uliotolewa pamoja na kukiri kwake makosa alihukumiwa adhabu ya kifo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images