Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Iran yaionya Marekani kuhusiana na njama zake za kutaka kuishambulia kijeshi nchi hio

$
0
0
Msemaji wa makao makuu ya jeshi la Iran, Meja Jenerali Ebulfazl Shikarchi amesema shambulizi lolote la kijeshi kutoka kwa Marekani litajibiwa vikali kwa wao kushambulia maslahi ya Marekani katika eneo hilo pamoja na kushambulia washirika wa Marekani.

Shikarchi akiongea na shirika la habari la Tesnim alitoa onyo kuhusiana na matokeo ya kuishambulia Iran kijeshi.

Shikarchi alisema hawatakuwa waanzilishi wa vita dhidi ya nchi yeyote lakini watakaposhambuliwa watajibu mapigo vikali mno.

Asubuhi ya Alhamisi iliyopita, Ofisi ya Mahusiano ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ilitangaza habari ya kusambaratishwa ndege ya ujasusi ya Kimarekani, baada ya ndege hiyo kukiuka anga na ardhi ya Iran katika eneo la Kouh-e-Mobarak katika mkoa wa Hormozgan.

Komandi ya jeshi la  Marekani katika eneo la Asia Magharibi (CENTCOM) sambamba na kukiri habari hiyo ilidai kwamba ndege hiyo isiyo na rubani ya Marekani ilikuwa bado haijaingia katika anga ya Iran na kwamba  ilikuwa katika maji ya kimataifa. 

Taifa Stars kushuka dimbani leo dhidi ya Senegal .....Mchezo Utapigwa Saa Mbili Usiku

$
0
0
Timu yetu ya Tanzania, Stars  leo Jumapili June 23  itachuana na Senegal katika mchezo wa Fainali za Afcon, mechi itakayopigwa saa 2 usiku kwa saa za nyumbani (Tanzania).

Nahodha wa Taifa Satars, Mbwana Samatta amesema kamwe  hawatokubali kufungwa kirahisi katika mchezo huo.
 
Samatta amesema anajua wanaenda kucheza na timu kubwa yenye wachezaji wanaotazamwa kila wikiendi katika ligi bora lakini hilo haliwatishi wao kupambana katika mchezo huo.
 
"Tunajua kwamba wapinzani wetu ni wazuri na tunawaheshimu, hatuendi kuwashangaa zaidi na sisi tunaenda kupambana nao na ndio maana tumejiandaa kwa muda mrefu kuweza kupambana," amesema.
 
Ameongeza anaamini mchezo huo mpaka dakika ya mwisho kila timu ina uwezo wa kupata matokeo uwanjani.

Katibu Mkuu CCM Dr. Bashiru ahoji maswali Haya kwa wanaosema uchumi wa Tanzania haukui

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Bashiru Ally amezindua ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano wa CCM mkoani Pwani,ambapo amechangisha zaidi ya milioni 25 na vifaa mbalimbali.

Katika uzinduzi huo, jumla ya mifuko ya saruji 2,861 imechangiwa ,nondo tani tano thamani ya milioni 9 ,malori ya mchanga, fedha taslimu ni sh.milioni 22.562 na ahadi ni sh.milioni 2.5 .

Alisema kati ya fedha hizo milioni tano imechangiwa na mwenyekiti wa CCM Taifa dk.John Magufuli.

Bashiru alisema, kwasasa hakuna mtindo wa kuchangia shughuli za kichama kwa fedha za mikononi ili kuweka mifumo mizuri ya kuaminiana.

Aidha alisisitiza ujenzi wa ofisi za chama ili kukijenga chama kwa maslahi ya wanaCCM.

“Uhai wetu unatokana na vikao na vikao haviwezi kufanyika chini ya miti,au kukutana gesti ,hivyo jengeni ofisi za chama kuanzia matawi na kata ili kuimarisha chama chetu”

Hata hivyo aliwasihi wananchi wasiwasikilize wale wanaokebehi Chama kilichopo madarakani na wale wanaopotosha kuhusu hali ya uchumi wa nchi.“Upotoshaji ni dhambi hasa kwa mtu aliyesoma chuo cha Dar es salaam na kusisitiza kwamba ,hali ya uchumi wetu ni imara” .

“Huwezi kudanganya watu na kuwaona ni wa pumbavu ,hakuna uchumi uliokufa ,hatuna deni la ndege,tunajenga vituo vya afya ,tunatundika nishati ya umeme hadi vijijini,watoto wanasoma bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne leo mtu unaibuka anasema uchumi umekufa”alikemea Bashiru.

Hakusita ,kuupongeza mkoa kwa kushirikiana ,kushikamana na kuwa na mahusiano mema baina ya serikali na chama. Aliweka wazi wilaya ambazo bado hazina mahusiano mazuri kati ya serikali na chama ikiwemo Bagamoyo ,Rufiji na Kibaha Vijiji ambako pale tatizo lipo kwa mkurugenzi mtendaji wa Kibaha Vijijini.

Alimjia juu mkurugenzi huyo wa wilaya ya Kibaha kwa kufanya kazi zake kwa mazoea na kushindwa kujenga mahusiano na ushirikiano na chama na kwenye majukumu yake ya kazi. Katika hatua nyingine akielekeza juu ya muelekeo wa chaguzi zijazo ,Bashiru aliwataka viongozi wanaokaa kwenye vikao vya maamuzi waache kutembea na wagombea mifukoni na badala yake waache wabunge,madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa waliopo wafanye kazi.

Pia aliwaasa baadhi ya wabunge kuacha kutumwa na kuwa wapiga debe kwa wawekezaji uchwara bali waelekezeni wawekezaji masharti na taratibu za nchi kwa maslahi mapana ya nchi.

PICHA: Rais Magufuli Ashiriki Misa Takatifu Ya Maadhimisho Ya Sherehe Ekaristi Takatifu Kanisa La Mtakatifu Petro Jijini Dar Es Salaam Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Padre Dkt. Alister Makubi, Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam baada ya kushiriki Misa ya Maadhimisho ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu kanisani hapo katika leo Jumapili Juni 23, 2019. Katikati ni Paroko Msaidizi wa kanisa hilo Padre Paul Haule na Mzee wa Kanisa Dkt. Aldehem Meru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki katika Misa ya Maadhimisho ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Juni 23, 2019

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

$
0
0
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. 

Simu:  +255745495181 au 0682644040  

www.tumainitibaasili.co.tz

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Waziri Kangi Lugola Ashangaa Kukuta Mahabusu Waliokaa Rumande Kwa Miezi 6 Kituo Cha Polisi Gogoni

$
0
0
WAZIRI wa mambo ya ndani nchini Kangi Lugola maarufu kama Ninja amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha polisi Gogoni kilichopo wilaya ya kipolisi Kimara ikiwa ni katika kuangalia utendaji kazi vituoni humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi kituoni hapo Waziri Kangi amesema kuwa wamekagua na kuona ufanisi wa namna jeshi la polisi linavyotoa huduma kwa wananchi na kuwasikiliza maoni ya wananchi juu ya huduma wanazozipokea kutoka kwa jeshi la polisi.

Waziri Kangi amesema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli kupitia ya ilani ya Chama cha mapinduzi iliyodhamiria kupambana na umaskini na changamoto ya ajira serikali ipo makini na wanahakikisha wananchi wanapambana na umaskini na tatizo la ajira.

Amesema kuwa vijana wengi wameamua kupambana na umaskini kwa kujiajiri kupitia pikipiki maarufu kama bodaboda lakini kumekuwa na malalamiko mengi ambayo yalifika hadi bungeni kwa vijana hao kuonewa, kupigwa na kunyang'anywa pikipiki zao.

Amesema kuwa kutokana na malalamiko hayo alitoa maagizo kwa vyombo husika juu ya bodaboda ambazo zinawezwa kukamatwa na kuwekwa katika vituo vya polisi; ambapo amesema kuwa bodaboda  zinazostahili kukamatwa ni zile zilizohusika na uharifu, zilizohusika na ajali, zilizopotea na kuonekana na zile zilizookotwa na kueleza kuwa bodaboda nyingine zitakamatwa na makosa mengine ya usalama barabani kama vile kupakia abiria zaidi ya mmoja maarufu kama mshikaki na kutovaa kofia ngumu na mshtakiwa anaweza kutozwa faini ambayo italipwa ndani ya siku saba.

Kangi amesema kuwa baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha polisi Gogoni Wilaya ya Kimara na baada ya kuzikagua amejiridhisha kwa kukuta bodaboda  zote zipo kwenye makundi aliyoyaainisha na amelipongeza jeshi la polisi.

Vilevile amesema kuwa kuna malalamiko ya vituo kukaa na watuhumiwa bila kupelekwa mahakama na kituo hicho  kilikuwa kinaongoza kwa kukaa na mahabusu kwa muda mrefu na leo amekuta mahabusu 32, na amekutana na mahabusu 11 wanaohusika na kesi za mauaji na wamekaa magereza kwa miaka 7 na baadaye kurudishwa kituoni hapo ili kuweza kufutiwa kesi zao ila hadi sasa wapo kituoni hapo kwa  miezi 6 jambo ambalo sio sahihi na ameongea na viongozi wa vituo hivyo na tatizo hilo litatatuliwa.

Kuhusiana na suala la mawasiliano hasa katika suala hilo la mahabusu kukaa vituoni muda mrefu amelichukua kama changamoto na watalifanyia kazi na kueleza kuwa kuhusiana na changamoto ya dhamana amempa maelekezo mkuu wa kituo cha polisi na kupinga kauli ya utakaa ndani hadi jumatatu ili hali kuna wadhamini.

Mwisho amesema kuwa kufuatia  taarifa ya uwepo kwa ugaidi nchini, Waziri Kangi amehakikisha usalama wa wananchi na mali zao na kusema kuwa serikali ya Magufuli ipo macho na kwa wale wanaotumia mitandao ya kijamii kutisha wengine watapambana na sheria.

Waziri Mkuu Atoa Pole Kwa Naibu Katibu Mkuu Wa CCM Zanzibar Kufuatia Kifo Cha Mke Wa Katibu Mkuu Huyo

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole, Naibu Katibu Mkuu wa CCM – Zanzibar, Abdallah Juma Mabodi ambaye amefiwa na Mkewe, Dkt. Badriya Abubakar Gurnah wakati alipokwenda nyumbani kwa wazazi wa marehemu, Mikocheni jijini Dar es salaam Juni 23, 2019 kutoa pole kwa familia. Katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Marekani yashambulia mifumo ya kompyuta ya silaha za Makombora za Iran

$
0
0
Marekani imefanya mashambulizi ya mtandao kwenye mifumo ya silaha za Iran na kuiharibu kabisa.

Tukio hilo limefanywa siku chache baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kutangaza kuachana na mashambulizi ya anga katika nchi hiyo yenye lengo la kulipiza kisasi.

Jumanne iliyopita Iran iliitungua ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani kwa madai kuwa ilipita katika anga lake jambo ambalo lilipingwa na Rais Trump na kudai kuwa ilikuwa katika anga la kimataifa.

Gazeti la Washinton Post limeripoti leo June 23, kwamba nchi hiyo imeharibu mifumo ya kompyuta inayodhibiti roketi na mitambo ya kurushia makombora ya Iran.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, tukio hilo ni kulipiza kisasi kufuatia mashambulizi mawili yaliyofanywa na Iran ikiwamo lile la kuteketezwa kwa meli ya mafuta kwenye Ghuba ya Oman.

Trump ameahidi kuiwekea Iran vikwazo vipya zaidi kuanzia kesho Jumatatu.


 Lakini Iran nayo imeionya Marekani kuwa shambulizi lolote dhidi yake litawafanya washirika wa Marekani walioko Mashariki ya Kati kuona moto.

Ulevi Wa Kupindukia Wasababisha Kifo Cha Mwanamke Shinyanga

$
0
0
MKAZI wa kata ya kambarare Mjini Shinyanga Nadia Rajab (18)mhaya amefariki dunia baada ya pikipiki aliyokuwa amepanda ikiendeshwa na askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) Othuman Hassan (30) mkazi wa Old Shinyanga kuacha njia na kugonga ukingo wa barabara.

Kamanda wa  Polisi mkoa Shinyanga Richard Abwao amesema kuwa, tukio hilo lilitokea jana  alfajiri katika barabara ya Uhuru na chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa mwanajeshi huyo aliyekuwa anaendesha pikipiki yenye MC.402 BYN aina ya SANLG akiwa amelewa.

 Amesema Othumani  amekamatwa huku pikipiki yake imepelekwa kituo cha polisi na kufafanua kuwa alikuwa ametoka kwenye starehe na alikuwa akiendesha pikipiki akiwa amembeba Nadia Rajab(18) huku akiwa amelewa hali ambayo alishindwa kuimudu pikipiki na kwenda kugonga ukingo wa barabara na kusababisha kifo cha Nadia papo hapo.

Hata hivyo Abwao amesema kuwa,mwanajeshi huyo atachukualiwa hatua za kisheria kama ambavyo wamekuwa wakichuliwa watu wengine nakuongeza ni marufuku mtu yoyote bila kujali cheo cheke kuendesha chombo cha moto huku akiwa umelewa kwani hatari na inaweza kusababisha ajali wakati wowote.

Mbali na hilo Kamanda Abwao amesema jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wameanzisha program ya kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki na baskeli walioko pembezoni mwa mji ili kujikinga na ajali ambazo zinaweza kujitokeza wakati akiendesha vyombo hivyo.

Serikali Yapiga Marufuku Wanaoshitakiana Kugharimia Usafiri Mabaraza Ya Ardhi

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amepiga marufuku wananchi wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi kutoa pesa kwa ajili ya kugharimia usafiri wa kwenda eneo lenye mgogoro.

Akizungumza wakati wa kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki Dkt Mabula alisema, kutoa pesa ya kugharamia usafiri kwa mmoja wa wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi kwenda eneo la tukio kunaweza kuleta ushawishi kwa wajumbe wake hasa kwa yule aliyetoa kiasi kikubwa cha pesa.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, ni lazima wakati wa zoezi la kwenda eneo lenye mgogoro kwa wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi Mkurugenzi wa Halmashauri husika aratibu zoezi hilo huku ratiba nzima ikiwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya katika kipindi cha mwezi mmoja.

‘’ Jamaa anatoa laki mbili anayelalamika hana kitu unategemea hapo haki itatendekaje, ni marufuku kabisa na taratibu zote za kwenda uwandani zipitie kwa DC na ratiba ijulikane mapema’’ alisema Dkt Mabula.

Akigeukia uzinduzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba katika wilaya ya Ulanga, Dkt Mabula alisema Serikali imezindua Baraza hilo ili kupeleka huduma karibu na kurahisisha usikilizaji  kesi za ardhi kwa wananchi ambao baadhi ya maeneo wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kupata huduma hiyo na kubainisha kuwa sasa wananchi wa Ulanga watapata  haki kwa wakati na kwa umbali mdogo.

Aliwaasa wananchi wa wilaya ya Ulanga kulitumia vyema Baraza Ardhi na Nyumba lililozinduliwa na kuwataka kuhakikisha wanafuata taratibu zote za utatuzi wa migogoro ya ardhi pamoja na kuachana na ile migogoro ya kifamilia kwa kutumia Mabaraza ya Vijiji na Kata kushughulikia migogoro hiyo.

Dkt Mabula aliusifu mkoa wa Morogoro kwa kutoa mafunzo kwa wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi na kubainisha kuwa mafunzo hayo yawe chachu kwa wajumbe wake kutenda haki wakati wa kufanya maamuzi kwa kuwa tayari wana weledi katika eneo hilo.

Kwa upande wake Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini Stela Tulo alisema, uzinduzi wa Barazala la Ardhi katika wilaya ya Ulanga limejibu kiu ya muda mrefu ya wananchi wa wilaya hiyo kupata huduma kwa ukaribu ambapo awali iliwalazimu kusafiri umbali mrefu hadi Kilombero kupata huduma.

Kwa mujibu wa Stela, kuzinduliwa kwa Baraza la Ulanga sasa kunaufanya mkoa mzima wa Morogoro kuwa na Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Manne (4) na kubainisha kuwa Baraza hilo sasa linaongeza idadi ya Mabaraza yanayofanya kazi nchini kufikia 54 kati ya 97 yaliyoidhinishwa.

Msajili huyo wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini alisema, mkoa wa Morogoro pekee kwa sasa una Mashauri 2,500 ya ardhi kati ya 29,000 nchi nzima na kubainisha kuwa, kuzinduliwa kwa Baraza la Ulanga ni moja ya jitihada kuhakikisha Mashauri katika mkoa huo yanapungua kama siyo kuisha kabisa.

Dr. Ndugulile Atoa Rai Kwa Jamii Zenye Ndoa Za Asili Kusajili Serikalini Ili Kuondoa Migogoro Inayotokana Na Wajane Kudhurumiwa Haki Za Mirathi.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Ikiwa leo Juni 23,2019  ambapo Tanzania imeungana na mataifa mengine Ulimwenguni kuadhimisha siku ya Wajane Duniani,Naibu  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii jinsia ,Wazee  na Watoto Dokta.Faustine Ndugulile  ametoa rai kwa jamii zenye ndoa za Asili kusajili  Serikalini ili kuondoa usumbufu baadaye pindi wanapohitaji kutafuta haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na mirathi. 

Dokta.Ndugulile ametoa rai hiyo leo Juni  23,2019 katika kilele cha siku ya Wajane Duniani ambapo kwa Tanzania yamefanyika katika viwanja vya Nyerere Square  jijini Dodoma. 

Dokta Ndugulile amesema hapa nchini Tanzania hususan vijijini watu wengi hawajui  haki zao   hivyo ni muhimu kusajili ndoa zao za asili katika mamlaka husika za  serikali huku akizitaka Taasisi za serikali zinazohusika na masuala ya mirathi kutoa elimu kwa jamii kuhusu taratibu za Mirathi kwani pamekuwepo kwa baadhi ya ndugu wasio wahusika wamekuwa wakiwageuka walengwa wa mirathi na kujifanya wasimamizi wa miradhi kwa nia mbaya ya kujipatia mali huku walengwa wa Mirathi hiyo wakiachwa wakihangaika. 

Katika hatua nyingine Dokta Ndugulile amesema maandalizi ya Wosia  yanatakiwa kuanza mapema ili kuondoa na kupunguza  migogoro ya mirathi inayojitokeza pindi mwenza mmoja anapofariki. 

Hata hivyo,Dokta Ndugulile amewatia moyo Wajane na kusema kuwa Ujane sio Mwisho wa Maisha na kinachotakiwa ni kutokata tamaa bali ni kufanya kazi za maendeleo na kuinua uchumi kwao.

Siku   Ya   Wajane  Duniani imekuja kutokana na kampeni za mwanasiasa mmoja Muingereza ambae, alifiwa na baba yake akiwa mtoto  nchini India  ambapo   Serikali ya Gabon ilidhamini azimio hilo la Umoja wa Mataifa    na  Inakisiwa kuna takriban wajane millioni 245 duniani na 115millioni wanadhulumiwa wakikabiliwa na ukatili,umasikini na kutengwa na jamii.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu June 24

Wema Sepetu amaliza siku saba za kukaa gerezani....Mahakama Yampa Onyo la Mwisho

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania imemuonya msanii wa Filamu nchini humo, Wema Sepetu(30), kutokukiuka masharti ya dhamana, vinginevyo haitasita kufutia dhamana yake.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatayu, Juni 24, 2019 na Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde wakati akitoa uamuzi kuhusiana na mshtakiwa kukiuka masharti ya dhamana.

"Mahakama inatoa onyo  la mwisho kwa mshtakiwa, ikitokea mshtakiwa huyu amevuja sheria kwa kutokufika mahakamani bila taarifa, Mahakama hii haitasita kumfutia dhamana.”

“Hivyo Mahakama imekurudishia dhamana yako na utakuwa nje kwa dhamana,"  amesema Hakimu Kasonde wakati akisoma uamuzi wake dhidi ya mshtakiwa huyo.

Wema ambaye alishawahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006, anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandaoni  wa Istagramu kinyume cha sheria.

Uamuzi wa kumpeleke Wema mahabusu ulifikiwa baada ya mshtakiwa huyo aliyekuwa anadaiwa kuruka dhamana kufikishwa mbele ya mahakama.

Akiiwakilisha Jamhuri Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani baada ya kuruka dhamana na mahakama kutoa hati ya kumkamata Juni 11 mwaka huu.

Hakimu Maira alisema mshtakiwa hakufika mahakamani Mei 14 mwaka huu bila taarifa na Juni 11 pia hakufika hivyo alimtaka kujieleza kwanini hakuhudhuria mahakamani na kwanini asifutiwe dhamana.

Akijieleza Wema alidai Mei 14 alisafiri kikazi kuelekea Morogoro akamjulisha Wakili wake, Ruben Simwanza na Juni 11 mwaka huu alifika mahakamani lakini aliumwa.

“Nilishindwa kupanda mahakamani, ninapofika kwenye siku zangu huwa napata maumivu makali, nilienda kuchoma sindano ya maumivu, nikapumzika kisha nikarudi nyumbani.

“Nilienda kuchoma sindano Hospitali ya Mbuyuni karibu na makaburi ya Kinondoni, nilifanyiwa upasuaji wa kizazi India hivyo maumivu yanatokea kila mwezi, naomba msamaha Mheshimiwa,”aliomba Wema.

Akijibu Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai ni kweli mshtakiwa hakufika mahakamani kwa siku hizo lakini siku zote za kesi amekuwa akitoa taarifa hivyo aliiomba mahakama impe onyo kwa kutohudhuria sababu imeleta usumbufu.
 
Glory alidai siku nyingine asipofika wadhamini wake wafike kumwakilisha.

Wakili wake, Ruben aliomba Mahakama imsamehe mteja wake kwa usumbufu uliojitokeza na kuahidi kwamba hautajirudia.

“Tunaomba busara ya mahakama mshtakiwa abaki na dhamana yake,”alidai Ruben.

Hakimu Kasonde baada ya kusikiliza hoja za pande zote alisema atazizingatia pamoja na kiapo cha Wema kilichowasilishwa mahakamani hapo.

Alisema hawezi kutoa uamuzi siku hiyo kwani alikuwa na kazi nyingine, akaahidi kutoa uamuzi leo kisha aliamuru mshtakiwa akae mahabusu hadi leo atakapotoa uamuzi wa ama aendelee kuwa nje kwa dhamana ama amfutie dhamana.

Hakimu Maira ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 4, 2019 itakapoanza kusikilizwa ushahidi.

Viongozi Wa Serikali Watakiwa Kuilea Na Kuisadia Sekta Binafsi

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewataka viongozi wa Serikali mkoani Simiyu kuisaidia na kuilea Sekta Binafsi ili iendelee kukua na wahakikishe kuwa maamuzi wanayofanya hayawi vikwazo  katika mazingira ya biashara na uwekezaji.

Mtaka ameyasema hayo wakati akifungua Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu ambayo imefanyika mjini Bariadi.

Amesema viongozi wa Serikali mkoani humo wanapofanya maamuzi katika biashara za watu ni lazima wawe na nia ya dhati ya kuona sekta binafsi inakuwa, ili maamuzi ya viongozi hao yasiwe vikwazo kwa ukuaji wa Sekta binafsi na mazingira ya biashara na uwekezaji.

“Sekta binafsi ni lazima ilelewe anaeilea ni Serikali, Sekta binafsi ni lazima ilindwe anayeilinda ni Serikali,Sekta binafsi ni lazima isimamiwe anayeisimamia ni Serikali na Serikali inaisimamia kwa maana ya kuilea ili ifanye vizuri” alisema Mtaka.

Aidha, ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya mkoani Simiyu kuendeleza utaratibu wa kukutana na wafanyabishara ili kupata nafasi ya kujadiliana juu ya fursa mbalimbali za uwekezaji na namna ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, huku akisisitiza pia kuendelea kufanyika kwa mabaraza ya biashara ya wilaya.

Katibu wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA) Mkoa wa Simiyu, Bi. Christina Matulanya amesema ili kuboresha mazingira ya biashara Serikali inapaswa kuendelea kuvutia wawekezaji  na kusimamia sheria, sera na kanuni zisipindishwe, huku akiupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuandaa mwongozo wa uwekezaji.

Katika hatua nyingine Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Charles Mkumbwa  ametoa wito kwa wafanyabiashara kuwa wazalendo, kutoa risiti ipasavyo, kufuata sheria za kodi na akaahidi kuwapa ushirikiano wafanyabiashara kila wanapohitaji.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule ya biashara,  Khalidi Swabiri ambaye alikuwa mwezeshaji wa warsha hii amesema ni vema mabaraza ya biashara ya wilaya yakafanyika ili wafanyabiashara wapate muda wa kukutana na viongozi wa Serikali, sekta binafsi kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika mazingira ya biashara na uwekezaji na ufumbuzi wake.

Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA), Dkt. Meshack Kulwa  amesema pamoja na kuomba mabaraza ya biashara ya wilaya yafanye kazi, ameomba  TCCIA mkoani Simiyu itafute viongozi watakaofanya kazi kwa kujituma ili TCCIA Simiyu iweze kuwa imara.

MWISHO

Rais Mstaafu Mkapa akumbuka alikosoma

$
0
0
Katika kuonesha anathamini alikotoka kielimu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa anatarajiwa kuungana na wahitimu wengine wa shule kongwe ya Sekondari Ndanda ya Masasi, Mtwara kuitembelea shule yao Septemba 27, mwaka huu kwa ajili ya Siku ya Wahitimu wa shule hiyo iliyoanzishwa miaka 91 iliyopita.

Mkapa aliyesoma Ndanda katika miaka ya 1950, alithibitisha kuungana na wahitimu wengine wa shule hiyo alipokutana na kuzungumza na viongozi wa Umoja wa Wahitimu wa Shule ya Sekondari Ndanda (UWAHISSENDA) waliokwenda kuutambulisha umoja wao ofisini  kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Alisema, kama mmoja wa waliobahatika kusoma Ndanda, anajiona ana wajibu wa kuungana na wana umoja wengine walioanzisha wazo la kuitembelea shule yao ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa shule katika maisha yao.

“Hili ni wazo la kupongezwa sana. Hongereni kwa ubunifu na uthubutu wa kutambua umuhimu wa kule mlikopata elimu. Ni wachache sana wanaokumbuka mambo kama haya,” alisema Mkapa huku akiahidi mwaka huu ataungana nao.

Kwa wahitimu hao, hii Hii itakuwa mara ya pili kurejea Ndanda, kwani mwaka jana walikwenda kwa mara ya kwanza na kuzindua umoja wao wakiwa shuleni hapo na kukabidhi vitabu vyenye thamani ya takribani Sh milioni 5, kupanda miti, kuzungumza na wanafunzi wa sasa na pia kushiriki katika shughuli mbalimbali shuleni hapo, ikiwa ni pamoja na kufyatua matofali.

Mwenyekiti wa umoja huo, Yohana Kasawala alimshukuru Rais Mstaafu kwa kuridhia kuwa mwanachama mpya, lakini kipekee kwa kukubali kuungana na wanafunzi wengine wa zamani kwa safari ya shuleni Ndanda. Aliwataka wahitimu wengine kuona fahari ya kusoma Ndanda na hivyo wajitokeze kufanikisha Siku ya Wahitimu Ndanda.

Umoja huo uliasisiwa mwaka 2015 kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp na tayari una wanachama hao zaidi ya 150, wakiwa na malengo ya kutanua wigo wa ukaribu hata baada ya kuhitimu masomo yao, kuinuana kiuchumi na pia kushiriki katika kuijengea uwezo shule yao.

 “Daima umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu, nasi tumeona ni vyema tukatumia mshikamano huu kama fursa ya kujiimarisha kiuchumi.

Bajeti Kuuu ya Serikali Kupigiwa Kura ya Ndio au Hapana Kesho

$
0
0
Wabunge kesho wanatarajiwa kupiga kura kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya 2019/20 ya Sh trilioni 33.11 kwa kuitwa majina na kupiga kura ya Ndiyo au Hapana.


Bajeti hiyo Kuu ya Serikali itapitishwa kama kura za Ndiyo zitakuwa nyingi zaidi ya kura za Hapana.

Ikiwa kura za Hapana zitakuwa nyingi zaidi, Bajeti Kuu ya Serikali haitapita na moja ya athari ya tukio hilo ni Rais kuwa na mamlaka ya kulivunja Bunge endapo litakwamisha Bajeti Kuu ya Serikali kupita.

Kwa kawaida upigaji wa kura, huongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, lakini kuna kila dalili upigaji kura huo kesho kuongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson ambaye ndiye aliyeongoza mjadala wa bajeti kwa wiki nzima kutokana na Spika Ndugai kuwa nje ya nchi.

Matokeo ya kura zilizopigwa, yatatangazwa na Katibu wa Bunge, Steven Kigaigai jioni baada ya wabunge wote waliopo bungeni kupiga kura. Idadi ya wabunge waliopo bungeni, wa CCM ni 288, Chadema 62, CUF 39, NCCR Mageuzi 1 na ACT Wazalendo 1.

Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari 2016 Kifungu cha 107 (1) kinaeleza kuwa Mjadala kuhusu Bajeti ya Serikali utakapomalizika, Spika atalihoji Bunge litoe uamuzi wake wa kupitisha au kutokupitisha bajeti ya serikali ili kukidhi matakwa ya Ibara ya 90 (2) (b) ya Katiba.

Nacho Kifungu cha 107 (2) cha Kanuni hizo, kinasema Uamuzi wa Bunge wa kupitisha au kutokupitisha Bajeti ya Serikali, utafanywa kwa kupiga kura ya wazi kwa kuita jina la mbunge mmoja mmoja 

Bajeti hiyo ya serikali iliwasilishwa bungeni Juni 13, mwaka huu na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, na imejadiliwa na wabunge kwa wiki nzima tangu Jumatatu, Juni 17 hadi leo.

Akiwasilisha bajeti hiyo, Waziri Mpango alisema mapendekezo ya serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2019/20 ni ya Sh trilioni 33.11, kati yake Sh trilioni 20.86 sawa na asilimia 63.0 ya bajeti, ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, zikijumuishwa Sh trilioni 9.72 kwa ajili ya ulipaji deni la serikali na Sh trilioni 7.56 kwa ajili ya mishahara.

Dk Mpango alisema Sh trilioni 3.58 zimetengwa kwa ajili ya matumizi mengineyo, zikijumuisha Sh bilioni 460.5 kwa ajili ya matumizi yatokanayo na vyanzo vya ndani vya halmashauri.

Mama adaiwa kumchinja mtoto wake na kumpika kama Supu

$
0
0
Mama Happiness Shadrack(36) Mkazi wa kijiji cha Buligi Kata ya Senga Wilayani na Mkoani  Geita anayedaiwa ni mwenye tatizo la akili, amemchinja mtoto wake  Martha Yakobo (1) mwaka mmoja  na kisha kumuweka ndani ya sufuria kumkata vipande vipande na baadaye kumchemsha  kwenye maji ya moto kama supu.
 

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Dismas Kissusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Juni 21 mwaka huu.

Kamanda Kissusi ameeleza kuwa historia ya mwanamke huyo Happyness Shedrack (36) inaonesha kuwa ana matatizo ya akili.

Ameongeza kuwa upelelezi unaendelea na ukikamilika mama huyo atapelekwa mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji.

Lugola: Mwanamke anayefikishwa Polisi hapaswi kukaguliwa na Askari wa kiume

$
0
0
Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Kangi Lugola imesema mtuhumiwa mwanamke anayefikishwa kituo cha polisi hapaswi kukaguliwa na askari wa kiume, kwamba kazi hiyo inapaswa kufanywa na askari wa kike, mgambo wa kike au mke wa askari aliyepo karibu na eneo husika.

Lugola ametoa kauli hiyo  leo Jumatatu Juni 24, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku ‘Musukuma’ aliyetaka kujua ni lini askari wa kike watapelekwa katika kituo cha polisi Nkome kwa maelezo kuwa kituoni hapo upekuzi kwa akina mama hufanywa na askari wa kiume.

“Nimeshamuagiza RPC (Kamanda wa polisi Geita) kupeleka askari wa kike katika kituo hicho. Taratibu zinaruhusu upekuzi kwa wanawake kufanywa na askari wa kike na kama hayupo basi kazi hiyo ifanywe na mgambo wa kike au mke wa askari,” amesema Lugola.

Katika swali la msingi, Musukuma alihoji sababu za kituo hicho kutokuwa na askari wa kike na kujibiwa na naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masuani kuwa vituo vya polisi Nkome, Nyamboge, Kakubilo na Nzela havina askari wa kike kutokana na ukosefu wa miundombinu.

Wazazi wapigwa marufuku kufanya biashara na watoto Wadogo sokoni

$
0
0
Uongozi wa soko kuu la mitumba la Memorial, Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, umeahidi kushirikiana na jeshi la Polisi kupiga marufuku wafanyabiashara wa soko hilo kwenda sokoni hapo na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa soko hilo, Godfrey Shayo, leo Juni 24, wakati wa utafiti wa kuongeza uelewa, uwajibikaji wa huduma bora za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto (ECD),  zoezi linalo tekelezwa na muungano wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) kwa kushirikiana na taasisi ya CIC ya Ireland

“Ukija sokoni hapa majira ya saa 11 Alfajiri utaona wazazi na walezi wakiwa na watoto wachanga huu ni ukatili na unaathiri afya ya mtoto na malezi yake ya baadaye, tumeliona hili na tunaandaa mpango wa kutoa elimu kabla ya kuchukua hatua” amesema.

Kwa upande wake mwenyekiti wa masoko la Mbuyuni, Lameck Mziray na mwenyekiti mtaa wa soko la Pasua, Rahibu Juma walikiri kuwapo kwa changamoto inayoathiri afya za watoto hao lakini wameahidi kuandaa mpango wa ushirikishwaji na wafanyabiashara ili kujadili suala hilo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images