Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TID adai kapigwa na majambazi....Mtazame Hapa

$
0
0
Mwimbaji mkongwe wa Bongo Fleva Top In Dar (TID) ameweka picha kwenye ukurasa wake wa instagram akionekana amepigwa na watu ambao amewataja kuwa ni wezi huku akidai kuwa  watu hao wanaweza fanya chochote sababu huwa wana mipango mbadala.


“Washamba Bwana Wakiona tu Unasikika wanaamua kukupiga hivi …. It’s so Sad Jambazi anaeza kukufanyia chochote sababu yeye Jambazi na Yuko na Back Up za Kijambazi #RevengeoftheNinja“ aliandika TID

Milioni 370 zapatikana katika harambee ya kuichangia Taifa Stars

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mpaka sasa zimepatika Milioni 370 katika harambee ya kuichangia Timu ya Taifa Stars.

Makamu wa Rais amewapongeza Watanzania wote waliojitolea kuichangia Timu hiyo kiasi hicho cha Fedha ambapo harambee hiyo imefanyika leo  eneo la serena jijini Dar Es Salaam

Akizungumza mara baada ya Harambee hiyo kukamilika, Mama Samia alisema harambee imeonyesha mafanikio makubwa na anaamini litakuwa chachu kwa timu ya taifa kufanya vizuri kufanya vyema.

"Kazi tuliyoifanya hapa leo imetusogeza hadi Shilingi 370 milioni. Kampeni hii ni endelevu na itaendelea huko mikoani.

“Kampeni hii naamini inawajaza motisha kwa wachezaji wetu na kwa upande mwingine niwashukuru Watanzania wote kwa muitikio chanya na naomba waendelee kuchanga," alisema Mama Samia.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) tayari kiko Misri kwaajili ya mashindano ya Africa, AFCON 2019 ambayo yanatarajiwa kutimua vumbi hapo kesho. 

Tayari Spika wa Bunge, Job Ndugai amewasili nchini humo kwaajili ya kuipa hamasa Timu hiyo.

Apandishwa Kizimbani Kwa Kusafirisha Dhahabu Bila Kibali

$
0
0
Mkazi wa Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam, Mirajdin Tajdin (32), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka ya  kusafirisha dhahabu bila kuwa na kibali.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali Ester Martin amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega, kuwa, Wakili Martin alidai kuwa, April 30, 2019 huko katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, (JNIA) mshtakiwa alikutwa na vipande vya dhahabu vyenye uzito wa gramu 98, vikiwa na thamani ya USD  3636.92, sawa na Sh 8, 364,914 Mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo,  mshtakiwa alikutwa akisafirisha dhahabu hiyo bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka husika.

Mshtakiwa amekiri kutenda makosa hayo lakini amerudishwa rumànde kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka Serikali ya Mtaa, atakayesaini bondi ya Sh 8milioni.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na kesi hiyo itatajwa Julai 4, mwaka huu kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Serikali Kuoitia Wizara ya Mambo ya Nje Yamuita Kaimu Balozi wa Marekani Ajieleze Kuhusu Taarifa yao ya Shambulizi la Kigaidi Nchini

$
0
0
Tarehe 19 June 20, 2019, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania ulitoa taarifa katika mitandao ya kijamii “Twitter” kuhusu angalizo la kiusalama “security alert”. Angalizo hilo la kiusalama lilitokana na uvumi unaodaiwa na ubalozi huo kusambaa kuhusu uwezekano wa kutokea kwa shambulio katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulimwita katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Balozi wa Marekani Bi Ann Marie Warmenhoven – Tilias ili kutoa ufafanuzi wa “twitter” yao.

Ubalozi wa Marekani ulimtuma Mwakilishi wa Kaimu Balozi wa Marekani Bi Ann Marie Warmenhoven – Tilias kuonana na uongozi wa Wizara ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe. 

Bi Ann Marie Warmenhoven – Tilias ameutambua ujumbe huo na kukiri kuwa  umetumwa na ubalozi wa Marekani hapa nchini.

Katika ufafanuzi wake amekiri kuwa Ubalozi umefanya makosa ya kutoa tetesi ambazo hazikuwalenga raia wa Marekani pekee bali raia wote wakitambua kuwa Ubalozi hauna mamlaka ya kufanya hivyo jambo lililosababisha taharuki kwa wananchi na wageni wanaotarajia kuitembelea Tanzania.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeukumbusha Ubalozi wa Marekani umuhimu wa kuzingatia sheria za nchi na taratibu za kidiplomasia zinazokubalika duniani kote katika utoaji wa taarifa za aina hii.

 Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe amewataka wananchi na Jumuiya za Kimataifa pamoja na wageni mbalimbali waliopo  nchini na wanaotarajia kuitembelea Tanzania kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani mpaka sasa hakuna taarifa yeyote iliyothibitishwa ya kuwepo kwa tishio la aina hiyo hapa nchini na kwamba Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimejizatiti kukabiliana na matishio yeyote.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar Es Salaam.
20 Juni, 2019

Serikali Kuajiri Wakaguzi wa Ndani 100

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege (Mb) amesema TAMISEMI imewasilisha maombi ya kupata kibali cha ajira ya Wakaguzi wa Ndani 100 ili kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi wa Kada hii katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mhe. Kandege ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Kazi wa Wakaguzi wa Ndani unaofanyika kwa siku mbili katika chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Kandege amesema Wakaguzi wa Ndani ni watu muhimu, Serikali inawaamini na inatambua mchango wao  katika usimamizi wa fedha na Uwajibikaji hivyo ni vyema rasilimali watu ikawa ya kutosha ili kazi hii iweze kufanyika kwa ufanisi.

“Napenda mfahamu kuwa Wakaguzi wa Ndani ndio Jicho la Kwanza la Serikali bila  ninyi Serikali haiwezi kuona vitu ambavyo vinavyotokea kwenye matumizi ya Fedha; Mmekua mkituonyesha yale yote yanayotendeka kinyume na matumizi stahiki yaliyoelekezwa hivyo ajira hiyo itakwenda kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi wa kada hii” Alisema Kandege.

Akizungumzia changamoto ya Ufinyu wa bajeti kwa vitengo vya ukaguziamesema  Serikali imeongeza bajeti za vitengo vya ukaguzi kutokaa shilingi 5.6 bilioni kwa mwaka wa fedha 2018/2019 hadi kufikia shilingi 6.4 bilioni kwa mwaka wa fedha 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 14.3.

“Ili kuleta tija na matokeo tarajiwa katika vitengo hivi Serikali itaendelea kuongeza bajeti ya rasilimali fedha ili muweze kujitegemea katika kutimiza majukumu yenu badala ya kutegemea fedha kwa wakaguliwa” Alisema Kandege.

Wakati huo huo Mhe. Kandege ameagiza Vitengo vya Ukaguzi wa Ndani kuhakikisha mianya yote ya ubadhilifu inabainishwa na kudhibitiwa kwenye mifumo ya kukusanyia mapato na usimamizi wa fedha.

Pia aliziagiza Halmashauri zote kuhakikisha Hoja zote za CAG zinapatiwa majibu, kuhakikiwa na kufungwa, ushirikiano unatolewa kwa CAG na taratibu za kufunga hoja zinazingatiwa.

Halkadhalika  Mhe. Kandege alimpongeza aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Ndugu Mohamed A. Mtonga kwa kustaafu utumishi wa umma na kazi kubwa aliyoifanya katika kada hii ya ukaguzi.

“Ndugu Mohamed nakutakia Afya njema, naamini bado una nguvu za kuendelea kutoa mchango wako kwenye shughuli za kiuchumi za kujenga Taifa letu endelea kuwa Mwalimu kiongozi kwa wakaguzi wa ndani, ukiendelea kuwafundisha na kutoa ushauri, nakutakia kila la Kheri.  Alisema Kandege.

Akizungumza wakati wa Mkutano huo Karibu Mkuu OR-TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga amesema  kutokana na umuhimu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani fedha zilizotengwa kwenye bajeti kwa ajili ya Kitengo hiki zitalindwa na kuhakikisha zinatumika kwa ajili ya kazi za kitengo hiki pekee.

“Umefika muda sasa vitengo vya wakaguzi wa ndani kuimarishwa na Kila Mkoa na Halmashauri kuviwezesha vitengo hivi rasilimali fedha, watu na vitendea kazi vya kutosha wakati wote” Alisema Nyamhanga.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Ukaguzi na Ufuatiliaji Ofisi ya Rais TAMISEMI Miriam Mbanga amesema Mkutano wa kazi kwa wakaguzi wa ndani wa Mikoa na Halmashauri wa kwanza kufanyika na unalenga kujifunza, kubadilishana uzoefu, kushirikishana namna mbalimbali ya kutatua changamoto za kiukaguzi na kujiwekea malengo ya namna ya kufanya kazi ya ukaguzi wa ufanisi.

Mkutano huu umehudhuriwa na Wakaguzi wa Ndani zaidi ya mia moja na hamsini kutoka katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. 

Spika Ndugai Atembelea Timu Ya Taifa Stars Nchini Misri

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amekutana jana na wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars katika kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Misri.

Katika mazungumzo na wachezaji hao Spika alifikisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kuwataka vijana hao kupambana kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa katika mashindano ya Afrika yanayotarajia kuanza Juni 21 nchini Misri.

Spika aliwataka wachezaji hao kuingia uwanjani wakiwa wamejua wamebeba matumaini makubwa kwa Watanzania ambao macho na masikio yao wameyaelekeza kwao.

Kwa upande wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alimuahidi Spika kuwa wamepokea salamu za  Rais Magufuli na wamemuahidi kuwa wataingia uwanjani kupambana na kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa.

Alisema hawataki kumuahidi kitu kikubwa,ila watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha wanapambana na kupata ushindani katika mechi zote za makundi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa June 21


Trump Atengua Kauli ya Kuishambvulia Iran Dakika za Mwisho.....Awali Alikuwa Ameshaamrisha Majeshi Kuivamia Iran Usiku wa Kuamkia Leo

$
0
0
Rais wa Marekani Donald Trump amesitisha hatua ya kuishambulia Iran muda mfupi baada ya kutoa idhini ya kufanya hivyo kujibu shambulio la Iran lililoidungua na kuiangusha  ndege isiyo na rubani ya jeshi la Marekani.

Gazeti la New York Times limeripoti likiwanukuu maafisa wa ngazi ya juu wa utawala wa Marekani, wakisema kuwa rais trump aliidhinisha kufanywa mashambulizi kwa kuyalenga maeneo kama rada za jeshi na mizinga ya kufytua makombora.

Mashambulizi hayo yalipangwa kufanyika kabla ya mapambazuko ya siku ya leo Ijumaa kujibu shambulio la Iran la kuiangusha ndege  ya jeshi la Marekani kwa madai ya kuingia kwenye eneo lake la bahari.

Kulingana na gazeti hilo, afisa mmoja wa utawala wa Trump amesema ndege za kivita zilikuwa angani na meli zilijiweka tayari lakini hakuna kombora lililofyatuliwa wakati amri ya kusitisha mashambulizi hayo ilipotolewa.

Uamuzi huo wa ghafla wa kusitisha kuishambulia Iran umezuia kile ambacho kingekuwa hatua ya tatu ya kijeshi ya utawala wa Trump katika eneo la mashariki ya kati baada ya kuvishambulia vituo vya jeshi la Syria mwaka 2017 na 2018.

Hatahivyo haijafahamika mara moja iwapo mashambulizi dhidi ya Iran yataendelea na haijawa wazi uamuzi huo wa Trump wa kuyasitisha umechochewa na kitu gani.

Hapo jana rais Trump alisema Iran imetenda kosa kubwa kwa kuiangusha ndege ya Marekani katika anga ya mlango bahari wa Hormuz.

Rais Trump alipooulizwa kuhusu hatua atakazochukua  alisema kwa mkato "mtafahamu hivi karibuni".

Lakini pia Trump aliashiria kuwa huenda shambulio hilo huenda lilifanywa kimakosa na mtu aliyepewa maelekezo na mamlaka za Iran.

Iran yalalamika kwa Umoja wa Mataifa
Wakati huo huo Iran imesema imeyapata mabaki ya ndege isiyo na rubani ya jeshi la Marekani katika eneo lake la bahari baada ya kuidungua

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Mohamed Javed Zarif amesema kupitia ukurasa wa Twitter kuwa ndege hiyo ilidunguliwa baada ya kukiuka utaratibu na kuingia kwenye anga la Iran.

Katika barua kwenda Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kwa Katibu mkuu wa Umoja huo, Iran imelalamika dhidi ya kile ilichoita kuwa vitendo hatari na vya uchokozi vya jeshi la Marekani kwenye eneo lake la bahari.

Marekani kwa upande wake imesema ndege  iliyoangushwa ilikuwa kwenye eneo la maji ya kimataifa.

Katika hatua nyingine viongozi wa bunge la Marekani wametoa wito wa kuchukuliwa tahadhari kuepusha kuongezeka mvutano na baadhi ya wabunge wamesisitiza kuwa Ikulu ya Marekani inapaswa kuliarifu bunge na kupata idhini yake kabla ya kuchukua hatua ya yoyote dhidi ya Iran.

Habari Njema Kwa Wanafunzi Wote Wanaotaka Kujiunga Kidato cha Tano na Sita .......Southern Highland School Wanakutangazia Nafasi za Masomo, Shule ni Nzuri na Ada zao ni Nafuu

Serikali Yatangaza Oparesheni Maalumu Nchi Nzima juu ya marufuku ya Mifuko ya Plastiki

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katibu mkuu wa Ofisi ya Makamu wa  Rais ,Mhandisi Joseph Malongo ametangaza operesheni   maalum ya Nchi nzima ya uzingatiaji wa Sheria ya usimamizi wa Mazingira juu ya marufuku ya Mifuko ya Plastiki  na Matumizi endelevu ya mifuko mbadala .
 
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dodoma Mhandisi Malongo amesema kanuni za usimamizi wa Mazingira za kupiga marufuku mifuko ya Plastiki  za mwaka 2019 zimeanza kutekelezwa kuanzia tarehe Mosi ,Juni,2019 hivyo kwa mujibu wa kanuni hizo ,ni marufuku kuzalisha,kusambaza kuingiza nchini ama kusambaza nje ya nchi na kutumia Mifuko ya Plastiki iliyotajwa katika katazo hilo .
 
Mhandisi Malongo amebainisha ,kiwanda,kikundi cha watu au mtu binafsi atakayebainika  kukiukwa matakwa ya kanuni hizo atakuwa ametenda kosa la  jinai na hivyo sheria itachukua mkondo wake.
 
Hata hivyo,amesema baada ya kuanza kwa utekelezaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki,baadhi ya wazalishaji na wasambazaji wamebadilisha matumizi ya mifuko laini ya plastiki isiyokuwa na mishikio na kuitumia kama vibebeo vya bidhaa  kinyume na kanuni ya 8 ya kanuni za usimamizi wa Mazingira.
 
Mhandisi Malongo ameendelea kufafanua kuwa kanuni ya 9 inatoa Msamaha kwa baadhi ya vifungashio vya plastiki kwa ajili ya huduma za afya  au kwa vifungashio vinavyotumika kufungashia bidhaa za  viwandani ,sekta  za ujenzi ,sekta ya kilimo,vyakula au usafi na   udhibiti wa taka.
 
Shirika la viwango Tanzanzia TBS linaandaa   viwango vya vifungashio  ambavyo vitalazimisha kiwango cha unene,uwekwaji   lakiri na kutambulisha bidhaa iliyofungashwa kabla ya kuuzwa.
 
Katika kuhakikisha suala hilo linatekelezwa kwa  ufanisi zaidi,Mhandisi Malongo  amesema Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi  wa Mazingira nchini,[NEMC] linaendelea na Operesheni kabambe   nchi nzima ya kusaka  mifuko ambayo imebadilishiwa matumizi  yake na kukiuka sheria  ambapo operesheni hiyo itahusisha vyombo vya ulinzi  na usalama,kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya,mamlaka za  serikali za mitaa.
 
Vingine ni  mamlaka ya maabara ya mkemia  mkuu wa serikali,shirika la viwango Tanzania TBS,Mamlaka ya Chakula na Dawa ,TFDA,Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,Pamoja na mamlaka ya viwanja vya ndege,bandari ,Forodha,uhamiaji na usafiri wan chi kavu.
 
Ikumbukwe kuwa ni makosa kisheria kubadili matumizi ya vifungashio na kuwa mifuko ya kubebea bidhaa na adhabu stahiki zitatolewa  kwa watu watakaobadili matumizi ya vifungashio na kuwa vibebeo vya bidhaa huku Ofisi ya Makamu wa Rais ikiendelea kuelimisha umma  pia  ikisisitiza kutumia mifuko mbadala.

Taarifa muhimu kutoka Wizara ya Ardhi

$
0
0
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inawatangazia wananchi wote waliopewa viwanja katika eneo la Pemba Mnazi kukamilisha malipo ya viwanja kabla ya Julai 31 2019.

Kwa wananchi ambao watashindwa kukamilisha malipo kwa muda uliotolewa viwanja vyao vitagawiwa kwa waombaji wengine bila taarifa yoyote. 

Tangazo hili pia litawahusu wale waliolipia sehemu ya gharama za umilikishaji lakini hawajakamilisha malipo.

Serikali Yaanza Ukarabati Mkubwa wa barabara ya Dar es salaam,Morogoro hadi Dodoma

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Serikali imesema imeanza ukarabati wa mashimo na kupanua barabara ya Dar es salaam,Morogoro hadi Dodoma ambayo ni kiungo muhimu kwa uchumi wa tanzania.

Naibu waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe,Elias Kwandikwa amebainisha hayo Juni 20,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la  mbunge wa Wingi Juma Kombo aliyehoji serikali ina mpango gani wa kukarabati mashimo  pamoja na kuipanua barabarahiyo.
 
Katika Majibu Yake Naibu waziri wa ujenzi ,uchukuzi na mawasiliano Elias Kwandikwa amesema Serikali  imeanza     ukarabati   mashimo  na   kupanua  barabara   ya   Dar eS Salaam,Morogoro  hadi Dodoma  ambayo ni kiungo muhimu kwa uchumi  Wa Tanzania ambapo mkataba  wa kazi ya upanuzi wa madaraja ya Kibamba,Kiluvya na Mpiji ulishasainiwa tangu tarehe 13,Julai,2018 na  mkandarasi ESTIM Construction.Co.Ltd kwa  gharama ya Sh.Bil.440,Mil.449 ,laki  5 na 21elfu.
 
Aidha,Mhe.Kwandikwa amesema Ukarabati wa maeneo yaliyoharibika unafanyika kwa kuondoa lami  ya zamani  na kuweka tabaka jipya  katika  maeneo ya Kibaha   hadi  Chalinze  ambapo  mkoa wa Pwani imetenga Tsh.Bil.2.5.

Hata hivyo Serikali imetenga Tsh.Milioni 800 katika mwaka wa Fedha 2018/2019 ili kufanya upembuzi yakinifu  na usanifu wa kina  kwa ajiliya ukarabati  Barabara ya  Morogoro  -Dodoma [km 256]
 
Katika  hatua nyingine   Mhe.Kwandikwa  amesema mkandarasi yeyote atakayechelewesha kazi atachukuliwa hatua na lipia gharama za usumbufu ambapo kuna mashauri 20 ya Makandasi waliofanya uzembe

Serikali Yatangaza Kutoa Bure vipimo kwa ajili ya Homa ya Dengue

$
0
0
 Serikali imelieleza Bunge kuwa vipimo kwa ajili ya Homa ya Dengue vitatolewa bure kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya umma wakati huu wa mlipuko.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuanzia mwezi Januari hadi Juni 19 mwaka huu, jumla ya wagonjwa 4,320 na vifo vinne vilivyotokana na homa ya dengue vimetolewa taarifa

“Mkoa wa Dodoma wagonjwa walikuwa watatu na kifo kimoja. Tanga wagonjwa 207, Pwani 57, Morogoro 16, Arusha wagonjwa watatu, Singida wawili, Kagera pia wawili. Vifo vimetokea katika hospitali ya rufaa Dodoma na Dar es Salaam katika hospitali ya Hindu Mandal na Regency,” amesema Ummy.

Akizungumzia kuhusu changamoto, Ummy amesema ya kwanza ni gharama za kupima. Amesema Ingawa Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imenunua vipimo moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji na kuviuza kwa bei nafuu ikilinganishwa na gharama inayotozwa kwenye baadhi ya hospitali binafsi, bado wananchi wanashindwa kumudu gharama za uchangiaji matibabu ya ugonjwa huu.
 

Pia amesema jamii haijaweza kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa kampeni ya usafi wa mazingira ambayo ni njia kuu ya kudhibiti mazalia ya mtu na watoa huduma za afya hawafuati  kikamilifu miongozo ya matibabu ya ugonjwa huu.

Taarifa Toka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi


Je wewe ni Mmiliki wa Gari? Ni Fundi Magari au Muuza Spea? ...Hapa Tunahabari Njema Inayokuhusu

$
0
0
Habari njema kwa wamiliki wa Magari, mafundi na Wauza Spea za Magari. EDRIVE PRO wamekeletea mfumo ambao unawaunganisha pamoja na pindi gari lako likiharibika popote ulipo hutapata tena tabu ya kuhangaika kutafuta fundi au maduka ya spea

www.edrivepro.co.tz ni mfumo wa kufanya na kusimamia utengenezaji wa magari online.

1. Katika mfumo huu wamiliki wa magari, maduka ya spare, na mafundi wanajisajiri ama wanaweza kusajiliwa kwa kuwasiliana na mtoa huduma wetu kwa e-mail edriveprotz@gmail.com

2. Baada ya kujisali kulingana nafasi yako [ mmiliki wa gari, muuza spare, fundi ama mwandika makala juu ya magari] msimamizi wa mfumo atakuthibitisha katika mfumo na utatumiwa e-mail na mfumo.

Baada ya kudhibitishwa utaweza kupata huduma za uuzaji wa spare, matengenezo ya magari kwa wamiliki wa magari na mafundi kupata fursa za mateja wapya mtandaoni nchi nzima.

3. Kutokana na wahusika wote katika mfumo huu kuwa wamesajiliwa, huduma katika mfumo huu ni nafuu na za uhakika.

Karibuni mjisajili katika www.edrivepro.co.tz


NB: Weekend hii kuna ofa kabambe kama unahitaji matengenezo ya Gari yako.  Hii si ya kukosa, Jisajili sasa.

Mahakama ya Mafisadi Yamhukumu Mnigeria Kifungo cha Miaka 30 Jela

$
0
0
Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumi Uchumi maarufu kama ‘Mahakama ya Mafisadi’ imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela raia wa Nigeria, Christian Ugbechi baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha Pipi 56 za Dawa za Kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

Adhabu hiyo imetolewa leo June 21, 2019 na Jaji Sirillius Matupa baada ya mshitakiwa huyo kutiwa hatiani June 19, 2019 ambapo Jaji alishindwa kutoa adhabu kutokana na mvutano wa kisheria.

Mshtakiwa huyo anadaiwa January 28, mwaka jana maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) Wilayani Ilala Mkoani DSM, raia huyo alikamatwa akisafirisha dawa hizo zenye uzito wa gramu 947.57.

Madaktari waliosomweshwa na serikali kupangiwa vituo

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema madakatari wote waliosoma kwa fedha za serikali watapangwa katika vituo vya kazi na serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Faustine Ndugulile alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nanyamba Abdalah Chikota (CCM) ambaye alitaka kujua mpango wa muda mfupi wa serikali wa kupeleka madaktari bingwa katika Hospitali ya Mkoa ya Ligula (Mtwara).

Ndugulile amesema katika wakati huu wa mpito wakiwa wanasubiri kupeleka madaktari hao Serikalini pamoja na Mfuko wa Bima ya Afya NHIF wamekuwa wakiweka kambi mabalimbali wakiwa na madaktari bingwa ili kutoa huduma za kibingwa.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mtwara Mjini, Hawa Ghasia (CCM) aliyetaka kujua mikakati ya serikali katika kupeleka madaktari bingwa katika hospitali ya Ligula, Ndugulile amesema Wizara imefanya tathimini ya mahitaji ya madaktari bingwa na fani zao katika Hospitali zote za mikoa, Kanda maalum na Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwamba tathmini hiyo itawezesha utekelezaji wa uamuzi wa kuwapanga upya madaktari Bingwa kwa uwiano kulingana na mahitaji ya kila Hospitali hizo.

“Lengo ni kuwa kila Hospitali hizi zinakuwa na madaktari bingwa wa fani nane, fanio hizo ni pamoja na Daktari bingwa magonjwa ya uzazi na wanawake , Watoto, Magonjwa ya Ndani, Upasuaji, Upasuaji wa mifupa, Daktari wa huduma za dharura na magonjwa ya ajali “ amesema.

Pia amesema madaktari wengine bingwa wanaohitajika katika Hospitali hizo ni pamoja na Daktari bingwa wa huduma za usingizi na daktari bingwa wa huduma ya Radiolojia.

Kwa mujibu wa Ndugulile amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2017/2018 Wizara iliwapeleka madaktari bingwa wa fani za upasuaji wa kawaida na upasuaji wa mifupa 125 katika Chuo cha MUHAS na wanatarajia kumaliza masomo yao katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Yafungua Ofisi Ya Kanda Mpya Ya Ziwa Mashariki Simiyu

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imefungua rasmi Ofisi ya Kanda mpya ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambapo makao makuu ya kanda hiyo yatakuwa Mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama amesema mamlaka hiyo imeanzisha Kanda Mpya ya Ziwa Mashariki inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ili kusogeza huduma kwa wananchi na kuharakisha ukuaji wa uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Amesema ofisi hii itajishughulisha na usajili wa maeneo yanayo jihusisha na uzalishaji na uuzaji wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba, kupokea maombi ya usajili wa bidhaa za vyakula vinavyofungashwa, kufanya ukaguzi wa bidhaa za vyakula katika soko kuwalinda walaji na  kudhibiti usindikaji wa chakula dawa na vipodozi.

Kazi nyingine zitakazofanywa na kanda hii ni kutoa vibali vya uingizaji nchini na usafirishaji wa chakula nje ya nchi, kufanya ufuatiliaji wa bidhaa za vyakula katika soko, kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa, vipodozi na vifaa tiba pamoja na kuelimisha na kutoa taarifa kwa wadau na wananchi kwa ujumla kuhusu bidhaa zinazothibitiwa na mamlaka.

Aidha, Mwasulama amesema Ofisi ya kanda hii itatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ambapo wataalam waliopo kwenye wilaya, manispaa, miji na majiji watasimamia sheria ya chakula na dawa kwa mujibu wa kanuni ya kukasimu baadhi ya majukumu na madaraka ya TFDA katika  Halmashauri.

Akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa wa Simiyu na TFDA katika ufunguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema Taasisi nyingine zinazohitajika katika uwekezaji wa viwanda na maeneo mengine ya uwekezaji zikaiga mfano wa TFDA  kwa kusogeza huduma karibu na wananchi ili waweze kupata huduma kwa wakati.

“Hiki kilichofanywa na TFDA ni vizuri taasisi nyingine nazo ziige, kama leo TFDA ipo Simiyu kama Kanda ya Ziwa Mashariki ningetamani kuwaona TBS, NEMC, OSHA wako Simiyu kama Kanda ya Ziwa Mashariki na Taasisi zote ambazo kwenye uwekezaji wa viwanda na maeneo mengine ya uwekezaji zinakuwa karibu na maeneo ya kutolea huduma” alisisitiza Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaotekeleza majukumu waliyokasimiwa na TFDA kufanya majukumu hayo kwa mujibu sheria huku akiwaasa  kuacha tabia ya kufungia biashara za wananchi bila kuwaelimisha badala yake wawasaidie kuwapa elimu ili wazalishe bidhaa bora kwa walaji.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Dkt. Mike Mabimbi akizungumza kwa niaba ya waganga wakuu wa wilaya ambao ni Makatibu wa kamati za ukaguzi wa chakula na dawa amesema watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa majukumu wanayokasimiwa  na TFDA kwa mujibu wa sheria na akashukuru TFDA kusogeza huduma karibu na wananchi.

MWISHO

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images