Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Polisi Kilimanjaro wakamata ndoo 60 za samaki Wachanga Bwawa la Mungu

$
0
0
Polisi mkoani Kilimanjaro wamekamata ndoo 60 za samaki wanaodaiwa kuvuliwa kinyume cha sheria katika Bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani Mwanga  wakiwa wanafirishwa kwenda Arusha.

Samaki hao wamekamatwa leo Juni 18 majira saa tisa usiku katika kata ya Lag’ata wilayani Mwanga ambapo Kamanda wa polisi wa Mkoa huo, Hamis Issah, amewambia wandishi wa habari kuwa samaki hao walikamatwa wakiwa kwenye aina ya Mistubishi pajero yenye namba za usajili T. 527  AEQ na kwamba wanawashikilia watuhumiwa wawili waliokutwa na samaki hao.

Amewataja watuhumiwa hao ni mfanyabishara Godlisen Mfinanga (37), mkazi Mrombo Arusha na Mwidini Seleman (30) mkazi wa kisongo Arusha na kwamba watafikishwa Mahakamani.


Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

$
0
0
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. 

Simu:  +255745495181 au 0682644040  

www.tumainitibaasili.co.tz

Naibu Kamishna Mkuu TRA Atembelea Bandari Kavu Za ICD

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo ametembelea bandari kavu ya Said Bakhresa (SSB-ICD) na African ICD ambapo amewataka Maofisa Forodha wa Mamlaka hiyo kuzingatia uwajibikaji, weledi na uadilifu wakati wote wanapotimiza majukumu yao ya kila siku.

Akizungumza na maofisa hao kabla ya kukagua mizigo iliyopo katika bandari hizo, Naibu Kamishna Mkuu huyo amesema kwamba, uzingatiaji wa maadili katika sehemu za kazi utasaidia kuondoa malalamiko na kero kwa walipakodi ambao ni wadau wakuu wa TRA.

“Jukumu la kujenga taswira ya mamlaka ni la kila mtumishi wa TRA. Hivyo, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anafanya kazi bila upendeleo, anawajali wateja ikiwa ni pamoja na kutumia lugha yenye staha, alisema Naibu Kaimshna Mkuu Mbibo.

Kwa upande wake Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Ben Usaje amewasisitiza watumishi hao kutojihusisha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaichafua Mamlaka ya Mapato Tanzania.

“Sote humu ndani tunajua kuwa, kupokea au kutoa rushwa ni kinyume cha sheria ya nchi yetu na yeyote atakayebainika akifanya hivyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Hivyo, hakikisheni mnaepuka kabisa vitendo hivyo vya rushwa kwani vitawasababishia kupoteza kazi na kufikishwa mahakamani”, alisema Usaje.

Baadhi ya majukumu ya Ofisi za Forodha zilizopo katika bandari kavu hapa nchini ni kuhakikisha kuwa taratibu zote za kuingiza mizigo ndani ya nchi zinafuatwa pamoja na kuhakikisha kwamba kodi stahiki inalipwa na wenye mizigo kabla ya kutoa mizigo yao katika bandari hizo.

MWISHO.

Jeshi La Polisi Pwani Lawashikilia Watumishi Saba Wa NIDA Kwa Tuhuma Za Wizi Wa Vifaa Na Vitambulisho.

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
WATUMISHI Saba wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Pwani, wakidaiwa kuiba raslimali vifaa vyenye thamani ya sh.mil.15 ambavyo walikuwa wakivichepusha ,kisha kuuza kwa maslahi yao binafsi.


Kati ya watumishi hao walipopekuliwa kwenye makazi yao ,pia walikutwa na vitambulisho vya Taifa boksi moja ambalo ndani vimo vitambulisho 15,000 pamoja na komputa mpakato mbili na nyaya za komputa.

Akielezea juu ya tukio hilo ,kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa alisema ,kati ya watuhumiwa hao wanaodaiwa kufanya tuhuma hizo sita ni wanaume na mmoja mwanamke ambapo majina yao yanehifadhiwa kwa uchunguzi zaidi.

Hata hivyo,kamanda huyo alibainisha,taarifa za tukio hilo zilipokelewa kutoka kwa uongozi wa juu wa NIDA kwenda jeshi la polisi mkoa Juni 14 mwaka huu na mara moja lilifuatilia na kuwakamata watuhumiwa saba na gari T.365 DFS aina ya Toyota spacio rangi ya silver ambayo ilikuwa imebeba jenereta moja mali ya NIDA.

“Awali watumishi wa NIDA waliokuwa wanafanya kazi mkoani hapo walikuwa wanatumia ofisi za kilipokuwa kiwanda cha kubangua korosho TANITA KwaMatias Kibaha na baadae serikali iliwajengea ofisi mpya za kisasa eneo la Machinjioni huko Loliondo Mjini Kibaha.”

“:Baaada ya majengo kukamilika walitakiwa kuhamia katika ofisi hizo mpya wao wenyewe na vitendea kazi vyao kama komputa,meza,scanner,camera,stationaries,BVR kits na vingine”alifafanua Wankyo.

Wankyo alielezea,watumishi wanaoshikiliwa na polisi waliteuliwa na uongozi wa mamlaka hiyo kuhamisha raslimali vifaa kutoka TANITA kwenda Loliondo ambapo wakiwa njiani walikosa uaminifu na kuanza kuvichepusha ,kuviuza na kujipatia pesa kwa manufaa yao binafsi .

Wankyo alitoa rai kwa watumishi wa umma , taasisi na mashirika ya watu binafsi wanapokabidhiwa madaraka na mali za serikali wawe waaminifu ,watiifu kwa kuzilinda kama mboni ya jicho lao na amekemea kuacha ubadhilifu wa mali za umma kwa maslahi ya matumbo yao.

Serikali Yaokoa Mabilioni Uendeshaji Mashauri Ya Madai

$
0
0
Na. Mwandishi Wetu
Serikali imesema mabadiliko kwenye sekta ya sheria nchini hususani Ofisi ya Mwanasheria Mkuu yameanza kuleta tija baada ya kuongeza ufanisi na kuokoa fedha ambazo hapo awali zilikuwa zikitumika kuwalipa mawakili binafsi.   

Akijibu swali la Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kuebenea ambae alitaka kujua kiasi cha fedha ambacho serikali imeokoa tangu maboresho kwenye sekta hiyo yaanze kutekelezwa, ambapo pamoja na mambo mengine yalianzisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia, kuendesha na kuratibu mashauri yote ya madai kwa niaba ya Serikali nchini. 

Kwenye majibu yake Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga alimueleza mbunge hyo kuwa kwenye Mwaka wa Fedha 2018/19 pekee Serikali imeweza kuokoa zadi ya shilingi bilioni tisa (9,018,957,011), ambazo kama sio maboresho kwenye sekta hiyo zingetumika kulipa makampuni binafsi ya uwakili.  

Aidha, Dkt. Mahiga aliendelea kulieleza Bunge kuwa Serikali itaendelea kutumia Mawakili binafsi kwa kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali pale itakapothibitika kuwa ni lazima kufanya hivyo. Alitoa mfano wa vigezo vinavyotumika kutumia mawakili binafsi ni shauri kufunguliwa kwenye mahakama ambazo sio za kimataifa na sheria za nchi husika haziruhusu uwakilishi wa mwanasheria kutoka nje ya nchi hiyo.  

Kuhakikisha maslahi ya taifa yanalindwa Dkt. Mahiga ameliambia bunge kuwa uendeshaji wa mashauri hayo utendelea kuishirikisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye kila hatua ya mwenendo wake tofauti na hapo awali.
 
Kuhusu baadhi ya mashirika ya umma kuendelea kutumia mawakili binafsi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi amelieleza Bunge kuwa mashirika hayo ni yale ambayo mashauri yake yalianza kabla ya maboresho kwenye sekta hiyo hayajaanza kutekelezwa na uendeshaji wa mashauri utatekelezwa kwa kushirikiana na Wakili Mkuu wa Serikali.

Serengeti Breweries yatangaza mabadiliko ya uongozi wa juu

$
0
0
Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa bia nchini, Serengeti Breweries Limited (SBL) imemteua Mark Ocitti kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya kuchukua nafasi ya Helene Weesie anayeondoka.

Helene amekuwa na SBL kwa miaka minne kuanzia mwaka 2015, kipindi ambacho kampuni imeweza kuzindua bidhaa muhimu zilizosababisha ukuaji wa biashara kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kampuni kupata tuzo za ubunifu na kuongezeka kwa uwekezaji. 

Helene anaondoka kwenda kuchukua nafasi nyingine ndani ya Diageo barani Ulaya. Akiwa nchini Tanzania atakumbukwa, bali na mambo mengine, kwa kuibua na kuendeleza vipaji vya ndani ya nchi.

Mkurugenzi mtendaji mpya, Mark Ocitti, kwa sasa anahudumu katika nafasi sawa na hiyo katika kampuni ya Uganda Breweries Limited (UBL) ambayo pia ni sehemu ya kampuni mama ya East Africa Breweries Limited (EABL) inayoongoza kwa uzalishaji wa vinywaji katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ocitti, chini ya uongozi wake, UBL imeweza kupiga hatua kubwa katika utendaji wake na kupelekea kukua kwa biashara.

Akizungumzia uteuzi wa Ocitti, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa EABL, Andrew Cowan amesema: “Mark amefanya mageuzi makubwa katika biashara yetu nchini Uganda; ameongeza nafasi yetu kiushindani na kukuza faida ya UBL kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Sina shaka kwamba kutokana na uzoefu wa uongozi wa Mark, maono, pamoja na mipango mikakati yake shupavu, itaifanya biashara ya SBL, inayokua kwa kasi kukua hata zaidi.”

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne June 18

Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma Yaendelea na Zoezi la Kuhakiki Mali Za Viongozi Wote Wa Umma

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inaendelea na zoezi la kuhakiki  kwa viongozi wote wa Umma wanaojaza fomu  za tamko la rasilimali na madeni  ili kuepusha mgongano  wa maslahi miongoni mwao.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Kamishna wa  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati wa Mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.

Aidha Mh Nsekela amewata Viongozi hao kufanya kazi kwa Uadilifu kwa kufuata Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 ambayo inawataka Viongozi wa Umma kutekeleza Majukumu yao kwa Maslahi ya Taifa.

Alisema lengo ni kutaka viongozi wa umma wafanye kazi kwa kuzingatia maadili na kuweka maslahi ya Taifa mbele badala ya maslahi binafsi.

Mh Jaji Nsekela katika hotuba yake aliongeza kuwa mgongano wa maslahi kwa baadhi ya viongozi wa umma unaweza kulisababisha Taifa hasara ya kuwa na miradi inayotekelezwa chini ya viwango.

Katika hatua nyingine Kamishna huyo wa  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma aliwataka viongozi wote wanaohusika katika ujazaji wa fomu  za tamko la rasilimali na madeni  kutenga muda wa kutosha kujaza fomu zao kwa ufasaha.

Alisema mara nyingi Viongozi wanaojaza fomu  za tamko la rasilimali na madeni wamekuwa wakisubiri siku za mwisho ndio wanaanza kujaza , jambo ambalo linaweza kusababisha kuachwa baadhi ya mali bila kuorodheshwa katika fomu hiyo ya Tamko.

Aliongeza kwamba Kiongozi wa Umma kujaza fomu za Tamko la Raslimali na Madeni ni takwa la Kisheria na ni lazima wala sio ombi. Na kwamba Kiongozi asipojaza fomu hizo na kuzirejesha kwa Kamishna wa Maadili kwa wakati ni kosa la kimaadili kisheria.

Alifafanua kwamba Kiongozi wa Umma anatakiwa kutoa Tamko lake la Raslimali na Madeni yake kila mwaka ifikapo mwishoni mwa Mwaka yaani tarehe 31 Desemba ya kila mwaka.

Mafunzo haya ya Maadili yamehudhuriwa na  Viongozi wa Umma wa Manispaa  zaidi ya Tabora  zaidi ya 200 wakiwemo Wakurugenzi, Makamanda wa polisi na jeshi la wananchi, wakuu wa wilaya, Madiwani, wakuu wa Idara na Vitengo.s

Habari Zilizopo KatikaMagazeti ya Leo Jumatano June 19

China yaionya Marekani dhidi ya kutuma wanajeshi Mashariki ya Kati

$
0
0
China  imeionya Marekani baada ya kutangaza kutuma wanajeshi 1,000 wa ziada katika eneo la Mashariki ya Kati huku mvutano na Iran ukiwa unazidi kuongezeka. 

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa China Wang Yi pia ameisihi Iran kutojitenga na makubaliano ya nyuklia kiurahisi, baada ya nchi hiyo kusema itarutubisha madini ya Urani kwa kiwango kikubwa iwapo nchi zenye nguvu duniani zitashindwa kutimiza ahadi zake chini ya makubaliano hayo katika siku 10 zijazo.

 "Katika hali ya hivi sasa, tunatarajia kuwa Iran itafanya maamuzi ya busara na sio kuachana makubaliano kwa urahisi.  Wakati huo huo tunatarajia pande nyingine zitaheshimu haki na maslahi ya upande wa Iran na kuchukua hatua za kweli za kuilinda nchi hiyo." amesema Wang. 

Marekani iliongeza shinikizo lake dhidi ya Iran hapo jana, kwa kutangaza kutuma wanajeshi zaidi katika Mashariki ya Kati pamoja na kutoa picha kadhaa ambazo inasema ni ushahidi mwingine kwamba Iran inahusika na mashambulizi dhidi ya meli za kubebea mafuta yaliyotokea katika Ghuba ya Oman wiki iliyopita. Iran inakanusha vikali madai hayo.

Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Agustine Mahiga Atoa Ufafanuzi Kuhusu Sheria ya Mirathi

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Agustine Mahiga amesema kuwa hakuna sheria inayompa mgane haki zaidi ya mjane au kwa namna yoyote kuonesha ubaguzi na kwamba sheria zinaeleza namna mali inavyopaswa kugawiwa kwa wanufaika huku ikiainisha kila mnufaika na kiwango anachopata.

Ametoa kauli hiyo bungeni jana Juni 18, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Silafu Maufi (CCM) aliyetaka kujua ni kwa nini mjane asiandikwe jina lake kwenye hundi na asimame na watoto wake kwa kupewa haki ya kusimamia mirathi.

Akijibu, Dk Mahiga alisema utaratibu unaofanyika unamtaka msimamizi wa mirathi kuwasilisha mchanganuo wa malipo na hundi huandikwa kwa wanufaika wote pasipo kujali jinsia zao.

Alisema pamoja na kuwa na Sheria nzuri, kumekuwa na uelewa mdogo miongoni mwa baadhi ya wananchi kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazohusu utaratibu wa mirathi.

“Wizara yangu kupitia RITA na wadau mbalimbali imekuwa ikitoa elimu kwa makundi mbalimbali kuhusu mirathi na itaendelea kubuni mbinu zitakazosaidia ili elimu ya hiyo iwafikie wananchi wengi zaidi” alisema.

Aliongeza kuwa sheria za nchi zinatambua kuwa mirathi na usimamizi wake unaweza kuongozwa na sheria ya kiislamu au Sheria ya India ya mwaka 1885 kwa wasiokuwa waislamu na kwamba matumizi ya sheria hizo yanaangalia maisha ya marehemu, dini na namna marehemu alivyozikwa.

Serikali kufikisha umeme katika vijiji vyote visivyo na umeme nchini ifikapo Juni 2021

$
0
0
Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini imedhamiria kufikisha umeme katika vijiji vyote visivyo na umeme nchini ifikapo Juni 2021.

Hayo yameelezwa bungeni jana  Juni 18, na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Monduli Julius Laizer (CCM) aliyetaka alitaka kujua ni lini Serikali itapeleka umeme katika shule ya Sekondari Oldonyolengai ambapo lami imefika toka mwaka 2015 lakini mpaka sasa hakuna umeme.

Akijibu swali hilo Subira alisema kulingana na mpango wa kupeleka umeme katika vijiji 64 wilayani Monduli, vijiji 16 vilishapatiwa umeme kupitia awamu ya pili ya miradi ya kusambaza umeme vijijini (REA-11), vikiwemo vijiji vya Arkatani na Mti.

Alisema kazi za mradi zinahusisha ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilometa 48.75 na njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 0.4 yenye urefu wa kilometa 40.

Chiza Afichua Udhaifu wa Mashine za risiti za kielektroniki (EFDs)

$
0
0
Mbunge wa Buyungu (CCM) Christopher Chiza amesema risiti za kielektroniki (EFDs) hasa zinazotolewa kwenye vituo vya mafuta hufutika baada ya muda na hivyo kuwafanya wafanyabiashara washindwe kutunza kumbukumbu.

Chiza alikuwa akichangia mapendekezo ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni bungeni jijini Dodoma jana Jumanne Juni 18, 2019.

Alisema Serikali inapendekeza kupunguza ushuru wa mashine za EFDs kutoka asilimia 10 hadi asilimia sifuri akisema ni jambo jema kwa sababu mashine hizo zinatumika katika kukusanya ushuru.

Alisema alihudhuria mkutano wa Chama cha wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo, (TCCIA)  kwa ajili kufundisha jinsi mashine za EFDs zinavyoagizwa.

Chiza alisema walisema mashine hizo kama ilivyo kwa bidhaa nyingine wanaweza kucheza nazo hivyo wakati mwingine mashine hizo zinaweza zikawa hazitoi taarifa sahihi.

“Mashine nyingi hasa kwenye vituo vya mafuta  ukiiweka nyumbani baada ya miezi mitatu minne hazisomeki tena yamefutika yote kama hujapiga picha basi hizo taarifa na kumbukumbu utakuwa hauna tena,” alisema.

Watiwa Mbaroniu kwa Kutaka Kumuua Mtoto kwa Imani za Kishirikina

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma linawashikilia watuhumiwa wanane wakiwemo wanne wa kutoka mkoani Njombe wakitaka kumtoa mtoto mdogo kafara katika mlima Mgwijima wilayani Namtumbo kwa mganga Faraji Panjapi.

Watuhumiwa hao, wanne kutoka mkoani Njombe na wanne kutoka mkoani Ruvuma wanashikiliwa na Polisi wilayani Namtumbo kwa kufanya ramli chonganishi na kutaka kumtoa kafara mtoto mdogo.

Walikamatwa katika Mlima Mgwijima wakiwa na mtoto mdogo  na vifaa mbalimbali vinavyodaiwa kutumika katika kafara wakiwemo mbuzi mmoja mweusi, kuku wawili (mmoja mweusi na mwingine mweupe).

Inadaiwa Polisi baada ya kupata taarifa za kiintelijensia walifika katika mlima huo na kuwakamata watuhumiwa hao ikiwa ni pamoja na mganga wa kienyeji, lakini baada ya mahojiano walikana madai hayo.

Awali, mmoja wa watuhumiwa, mwanamke ambaye alikuwa na  mtoto huyo akiwa ametokea Njombe, baada ya kufika kituo cha polisi  ‘alipandisha mashetani’ na kuanza kujigaragaza akisema wale wengine hawana makosa ila yeye.

Baadaye alipotulia na kuhojiwa alikana madai hayo na kudai kuwa yeye ni mgonjwa, hivyo alioteshwa kutoka Njombe kwenda kwenye mlima huo ili kupona. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Mbunge Alalamikia Kushuka Biashara Kariakoo

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Seleman Sadiqq, amesema  ukadirio wa kodi unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na kutokuruhusiwa wafanyabiashara wanaonunua bidhaa China na Dubai kwenda na fedha taslimu umekuwa ni tatizo.

Akichangia mjadala wa Bajeti kuu ya Serikali  jana June 18 bungeni Sadiqq alisema tatizo lipo kwenye ukadiriwaji wa kodi na kwamba biashara za Dubai na China zimetawaliwa kwa kulipa fedha taslimu.

“Ni muhimu kwa Benki Kuu (BOT), ueleze utaratibu wa kupeleka fedha taslimu ukoje. BOT wasaidie kuhakikisha biashara inarudi Kariakoo, kwa sasa imepotea katika ramani ya biashara.

“Tulikuwa na Kariakoo ya wafanyabiashara kutoka Malawi, Kariakoo, Burundi, Congo, Uganda na Rwanda, BOT na TRA lazima wajiuelize kuna nini na sababu zipi tulizopoteza biashara Kariakoo,” alisema.

Aidha Mbunge huyo alisema sera ya Tanzania ya viwanda kwa sasa inatekelezeka kwa vitendo kutokana na ujenzi wa viwanda unaofanyika katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri Mpina Afunga Kilele Cha Maonesho Ya Kwanza Ya Ng’ombe Bora Wa Maziwa Tanzania , Jijini Dodoma

$
0
0
Na.Fasustine Galafoni,Dodoma
Imeelezwa kuwa  idadi ya ng’ombe wa Kisasa waliopo Tanzania  kwa sasa ni zaidi ya Milioni Moja ambapo wana uwezo wa kuzalisha lita za Maziwa  zaidi ya Milioni 900  hivyo wafugaji wametakiwa kujikita katika ufugaji wa kisasa zaidi na wenye kuleta tija.
 
Akizungumza katika  Kilele cha maonyesho ya  kwanza  ya ng’ombe  bora  wa Maziwa tangu Tanzania ipate uhuru yaliyofanyika katika viwanja vya nanenane jijini Dodoma Juni 18,2019  ,Waziri wa  Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Mpina amesema ufugaji wa kisasa una tija kubwa katika maisha ya  Mfugaji kwani uhitaji mifugo wa chache huku wakitoa mazao mengi tofauti na ufugaji wa kienyeji ambapo umekuwa na mlundikano wa mifugo wengi na uzalishaji usiokuwa na tija katika kumwinua kiuchumi mfugaji.

Aidha,Waziri Mpina  amesema Zaidi ya Lita za Maziwa Milioni 20 kwa mwaka huagizwa kutoka nje ambapo hutumia zaidi ya Tsh.Bil.30 katika ununuzi huo hivyo kuna haja kubwa kwa Watanzania kujikita katika ufugaji wenye tija hali itakayosaidia upatikanaji wa maziwa kwa wingi hapa nchini kwani uzalishaji wa mbegu wan g’ombe wa Maziwa ni himilivu.
 
Waziri Mpina amesema kiwango mifugo 40  bora wa maziwa    ambayo imefanyiwa utafiti na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo International Livestock Research Institute (ILRI) bado ni michache hivyo kuna uhitaji mkubwa wa kuzalisha ng’ombe wa Maziwa.

Uzalishaji wa maziwa nchini kwa mwaka unakadiriwa kuwa lita bilioni 2.4. Wastani wa uzalishaji wa maziwa kwa ng’ombe bora mwenye damu mchanganyiko ni takribani lita 1,400 kwa msimu wa uzalishaji (lactation); wakati ambapo ng’ombe wa asili wanatoa wastani wa takribani lita 400 kwa msimu wa uzalishaji.

Hata hivyo,Waziri Mpina amesema Wizara yake ya Mifugo ina upungufu wa Watumishi ambapo kuna   kuna watumishi 3795 pekee katika halmashauri na amemwagiza katibu mkuu wa Wizara kufanya mchakato wa mgawanyo wa watumishi katika maeneo yaliyo na watumishi wachache huku pia akizitaka taasisi za kifedha kuchangamkia fursa ya kuwakopesha wafugaji  ili waweze kukuza tasnia yao ya ufugaji.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo International Livestock Research Institute (ILRI) Bw.Gimmy Symith amesema Kila nchi ambayo inafanya mchakato wa mabadiliko  kuwekeza katika viwanda vya kuzalisha maziwa  imeweza kubadilisha uchumi pia.

Programu ya Kuboresha Mbari za Ng’ombe Bora wa Maziwa (African Dairy Genetic Gains, ADGG) inafadhiliwa na Wakfu wa Bill & Melinda Gates, na ina nia ya kukuza ushirikiano kati ya wafugaji wa ng’ombe wa maziwa nchini Tanzania pamoja wadau ili kupambana na changamoto za ufugaji na kuongeza uzalishaji na
tija.

Maonyesho ya ng,ombe bora wa Maziwa yalianza tarehe 17  hadi 18 ,2019 ambapo ng,ombe 40  bora  hapa nchini wamebainika kuwa za uwezo wa kuzalisha zaidi ya  lita 30 kila mmoja kwa siku kwa mujibu wa tafiti za taasisi ya utafiti wa Mifugo Tanzania TALIRI Kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti ya Mifugo ya kimataifa ILRI ambapo kaulimbiu ni”ng’ombe bora kwa Maziwa zaidi.

Afikishwa mahakamani kwa kutoa ushahidi wa uongo

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Njombe imemfikisha mahakamani bwana Osward evance Mbilinyi mkazi wa wilaya ya Makete kwa kutoa ushahidi wa uongo katika kesi ya hongo namba 2/2019 iliyokuwa ikiwakabili Christian batholomeo Sanga na Zabron Mwakagile iliyofunguliwa katika mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya ya Makete.

Kwa mujibu wa takukuru mkoani njombe taarifa zinasema kuwa mshitakiwa akiwa ni shahidi wa upande wa jamhuri anadaiwa tarehe 27/2/2019 wakati wa kesi ya hongo dhidi ya Christian sanga na Zabron mwakagile mshitakiwa alitoa ushahidi wa uongo huku akikana kutotambua maelezo yake aliyoyatoa ofisini kwa hiari yake akiwa kama shahidi katika kesi hiyo ya hongo iliyokuwa ikimkabili Christian batholomeo sanga na Zabron mwakagile.

Katika kesi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na mwanasheria wa takukuru baada ya mshitakiwa kutoa ushahidi wa uongo,mwendesha mashtaka aliomba mahakama kumtambua shahidi huyo kama shahidi aliyebadilika.

Kamanda wa takukuru mkoani Njombe Charles mulebya ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa umma kuwa wasikubali kurubuniwa na washtakiwa hasa pale ambapo wameamua kuungana na serikali katika vita dhidi ya rushwa kwa kutoa ushahidi wa uongo ili mshitakiwa aonekane hana hatia mbele ya mahakama kwa kuwa kufanya hivyo ni kuhujumu jitihada za takukuru katika mapambano dhidi ya rushwa.

Aidha katika hatua nyingine takukuru mkoani Njombe imemfikisha katika mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya ya Makete Leuteli amanyise Malila ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Ludihani kwa kutumia cheti cha mtu mwingine ambaye ni Festo amanyise Ngogo na kujipatia ajira kupitia cheti cha mtu mwingine.

TAKUKURU Yawasha Moto Waliopiga Bilioni 46 za Libya

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), imetangaza kuwasaka watu wanne wanaodaiwa kutoweka na zaidi ya Sh bilioni 46, ambazo ni mkopo kutoka Serikali ya Libya ili kujenga Kiwanda cha Saruji mkoani Lindi.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari jana, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo, alisema fedha hizo kwa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Libya, kama mkopo wenye riba.

Alisema kwa kuwa Serikali haifanyi biashara, fedha hizo zilikabidhiwa kwa kampuni ya MEIS Industries Ltd mwaka 2009 kwa ajili ya kujenga kiwanda hicho, lakini hadi sasa hakijawahi kuonekana na wahusika hawajulikani walipo.

“Mwaka 2009 Serikali hizi mbili zilitia saini mkataba ulioitaja kampuni ya MEIS Industrial Limited kama kampuni itakayopewa dola milioni ishirini za Marekani kwa ajili ya uwekezaji wa ujenzi wa kiwanda cha Saruji eneo la Machore mkoani Lindi.

“Fedha hizo zilitolewa kwa kampuni ya MEIS kama mkopo uliopaswa kurejeshwa kwa riba nafuu na kwa mujibu wa mkataba, mkopo huo ulipaswa kurejeshwa ndani ya miaka sita, yaani 2011 hadi 2017. Hata hivyo, hadi mwaka 2019 kampuni hiyo haijarejesha mkopo huo wala kiwanda cha saruji kilichokusudiwa kujengwa bado hakijajengwa,” alisema.

Alisema uchunguzi uliofanywa na Takukuru umebaini kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo imetumika kwa matumizi mengine kinyume na makusudio ya Serikali jambo ambalo ni kosa.

Brigedia Jenerali Mbungo alisema wahusika wa kapuni ya MEIS ambao wanatafutwa ni Islam Ally Saleh Balhabou, Merey Ally Awadh Saleh, Sabri Ameir Kuleib na Abdallah Said Abdallah bin Aliya, ambao hadi sasa hawajulikani walipo.

Alisema zipo taarifa kuwa huenda wengine walikimbilia Visiwa vya Comoro na wengine nchini Uingereza, hivyo juhudi za kuwatafuta zinaendelea.

“Tunatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa sahihi za mahali watuhumiwa hawa wanapoweza kupatikana wawasiliane nasi ili wakamatwe na kuja kujibu tuhuma hizi zinazowakabili kwa kuwa kosa hili liko chini ya kifungu cha 28(2) cha Sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007,” alisema.

Akitoa ufafanuzi kuhusu mikopo iliyotolewa na Serikali ya Libya kwa Tanzania, alisema Serikali ya Libya katika miaka ya 1980 iliikopesha Serikali ya Tanzania mafuta ya petrol na dizeli kiasi cha tani 200,000 za ujazo ambayo kufikia mwaka 2005 ilikuwa ikiidai Serikali ya Tanzania Dola 201,000,000.

Alisema kutokana na fedha hizo, Serikali ya Libya ilisamehe nusu ya deni ambapo Seriali hizo mbili zilikubaliana namna ya kulipa dola 101,000,000 zilizobaki.

“Katika makubaliano haya, dola milioni 61 zilitakiwa kulipwa kwa mtindo wa madeni ya kitaifa, dola milioni 20 zilipwe kwa mpango maalumu na dola 20 milioni zifanye uwekezaji nchini Tanzania na baadaye zirudishwe Libya kwa riba nafuu,” alisema.

Alieleza katika mpango huo, kampuni hiyo ya MEIS ilipopewa fedha hizo kwa ajili ya kufanya uwekezaji nchini ambao ulitakiwa uwe umeshakamilika na urejeshaji wa fedha hizo nchini Libya kwa riba nafuu uwe umeshakamilika kufikia mwaka 2017.

Kanuni bora za ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili)....Soma Hapa Uwe Tajiri

$
0
0
Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. 

Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi.

 Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. 

Muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.

Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku
Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
1.  Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.

2. Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe na kufukiwa.

3.  Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.

4.  Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.

5.  Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.

6.  Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.

7.Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.


Magonjwa na kinga kwa kuku wote

1.Ndui ya kuku
Huathiri sana vifaranga wanaokua na ujitokeza kwa wingi wakati wa mvua za muda mrefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na manyoya.

2.Mdondo/kideri
Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari katika magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.

3.Ukosefu wa vitamini A
Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.

4.Kosidiosisi
Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokua. Kuku hudhoofika, manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.

5.Viroboto, chawa na utitiri
Hawa ni wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga na kuatamia.

6.Minyoo
Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo.


Chakula cha ziada
1.Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.

2.Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai).

3.Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kama nyongeza ya protini.

4.Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.

5. Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.

6Mwagia maji hadi kila kilichomo kilowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chungu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuhi, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.

Utotoleshaji wa vifaranga
Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku.

Sifa za jogoo bora
1.  Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.

2.  Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi mueke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.

Sifa za tetea bora
Tetea bora ni yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.

Uhifadhi wa mayai
1.  Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.

2.  Tumia kasha lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.

3.  Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.

4.  Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.

5.  Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.

Kuatamiza mayai
1.  Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.

2.  Mayi 10 hadi 12 yanatosha kuatamia.

3.  Mayai ya kuatamiza yasizidi wiki 2 toka kutagwa.

4.  Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku wa kuyaatamia.

5.  Mayai ya kuatamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu na safi au kilichowekwa spiriti

Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja
1.  Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;

2.  Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.

3.  Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kisha wawekee kuku wote mayai yenye mbegu.

Matunzo ya vifaranga ili kuzuia vifo
Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifaranga wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;

Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine
1.  Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasiende mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.

Chanjo ya mdondo kideri/lufuo
Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.

Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia hadi wakifikisha wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi 3

Kinga dhidi ya kosidiosisi
Kinga ya kosidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.

1.  Wape dawa ya amprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya kosidiosisi.

2.  Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa katika maji au pumba

3.  Kama vifaranga wadogo wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvaa koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;

Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu

Hitimisho
1.  Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku ni visafi kuepusha magonjwa.

2.  Usichanganye kuku na bata katika banda moja

3.  Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.

4.  Kideri, kosidiosisi, ndui na upungufu wa vitamini A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.

5.  Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.

6.  Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri, fuata maelezo kuzuia vifo.

7.  Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.

8.  Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.

Kuwa Wakwanza Kupokea Habari Zetu....Download App Yetu Kwa Kubonyeza Hapa, Huhitaji tena kuwa na Computer

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images