Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wabunge CHADEMA Walivyotimuliwa Bungeni Jana Jioni

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson jana jioni aliwatoa ndani ya ukumbi wa Bunge wabunge watatu wa Chadema walioibua zogo bungeni kuhusu uamuzi uliochukuliwa dhidi ya mbunge wa Kasulu Vijijini (CCM), Augustine Vuma aliyechana kitabu cha hotuba mbadala ya bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni mwaka 2019/2020.

Wabunge hao ni Esther Matiko (Tarime Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Dk Emmaculate Sware (Viti maalum), ambao walipinga uamuzi wa Dk Tulia kumtaka Vuma kuomba radhi kwa alichokuwa akizungumza wakati akichana kitabu hicho, si kitendo chake cha kuchana kitabu.

Dk Tulia alichukua uamuzi huo kwa maelezo kuwa taarifa iliyoombwa na mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka baada ya Vuma kuchana kitabu hicho, inazungumzia mbunge kutamka maneno yasiyoruhusiwa bungeni.

Vuma wakati akizungumza utekelezaji mzuri wa miradi ya Serikali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), alishika kitabu hicho cha upinzani na kusema kina maneno yasiyofaa na kinafaa kuchanwa kisha kukichana.

“Mchangiaji wakati akizungumza amechana hotuba ya upinzani ndani ya Bunge nafikiri jambo hili ni dharau kubwa. Ni kutojielewa kwa mbunge na hajui kwa nini vitabu hivi amepewa. Achukuliwe hatua maana tumemuona kama kichaa fulani hivi ndani ya Bunge,” alisema Mwakajoka aliyetumia kanuni ya 64 ya Bunge kutoa taarifa hiyo.

Katika majibu yake Dk Tulia alisema, “Ameitaja kanuni ya 64 japokuwa ufafanuzi wake haukuwa haswa katika kifungu gani ambacho kimevunjwa, kanuni hii inazungumzia mambo yasiyoruhusiwa bungeni na ukiisoma fasili ya kwanza inazungumza kuhusu kutotumia lugha ya kuudhi au inayodhalilisha watu wengine.”

“Kwa mchango wa Vuma hoja iliyopo itakuwa si kuchana kitabu maana amezungumza wakati akichana kitabu. Vuma maneno ya kuhusu kukichana kitabu nitakupa fursa ya kuyafuta na jambo hili lisirudiwe tena.”

Baada ya kupewa fursa hiyo Vuma alifuta maneno hayo na kusisitiza, “ila  ilikuwa ni kuonyesha namna gani ambavyo hotuba hii haina maslahi kwa umma.”

Kauli hiyo iliwanyanyua Heche na Matiko na kutaka mbunge huyo kuchukuliwa hatua zaidi.

“Waheshimiwa wabunge ndio maana huwa nasisitiza anapozungumza mmoja wetu kumsikiliza, Vuma ameonyesha kitendo ambacho mimi nimeshakitolea ufafanuzi, wakati amesema kitabu hiki kinapaswa kuchanwa. Vuma ameshaambiwa afute hayo maneno,” alisema Dk Tulia ambaye kabla hajamaliza wabunge wa upinzani walitaka achukue hatua zaidi.

“Naomba mtoke nje maana hatuelewani. Matiko na Heche namba mtoke nje. Matiko simama uende nje,” alisema Dk Tulia.

Dk Sware aliposimama na kutaka kutoa taarifa naye alitakiwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

$
0
0
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. 

Simu:  +255745495181 au 0682644040  

www.tumainitibaasili.co.tz

Wahamiaji Haramu Sita Na Watu Wengine 29 Wanaojihusisha Na Uhalifu Wakamatwa Chalinze

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
JESHI la polisi mkoani Pwani, linawashikilia wahamiaji haramu sita ambao ni raia kutoka nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali, huku likikamata watu wengine 29 kwa kujihusisha na matukio ya uvunjaji nyumba usiku na kuiba.

Watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia msako mkali na oparesheni dhidi ya vikundi vya vijana wa mitaani wanaojihusisha na wizi kwa kuvunja, kupora na kukaba raia wema huko wilaya ya kipolisi Chalinze .

Akielezea kuhusiana na matukio hayo,kamanda wa polisi mkoani Pwani Wankyo Nyigesa alisema baadhi yao walikamatwa wakiwa na mali kadhaa,madawa ya kulevya aina ya bangi kete 142,puli nne,pombe haramu ya moshi lita 25 na pikipiki moja.

Anabainisha kwamba, pia kumekamatwa magunia 90 ya mkaa uliovunwa bila uhalali ,mashuka,raba,vitenge,mafuta ya pikipiki na mafuta ya kula yanayodaiwa kuingizwa kwa kukwepa ushuru lita 300.

Akizungumzia kuhusu wahamiaji haramu alisema ,watafikishwa katika idara ya uhamiaji kwa taratibu nyingine za kisheria. Kamanda huyo alitoa rai kwa jamii ,kuwa itambue uhalifu haulipi na hauna faida kwani siku za mwizi ni arobaini na akishikwa mtu akijihusisha na uhalifu atakiona.

Vilevile anawataka walioibiwa kufika katika kituo cha polisi Chalinze kutambua mali zao .

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

VIDEO: Kauli ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Juu ya ombi la DRC kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

$
0
0
Kauli ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga juu ya ombi la DRC kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

VIDEO: Tahadhari yatolewa kwa wanaotikisa mitungi ya gesi

$
0
0
Jeshi la Zimamoto na uokoaji nchini limesema kuwa ni hatari sana ikiwa mtu atatikisa tikisa mtungi wa gesi kuangalia kama bado gesi ipo ndani, kwani inaweza kutokea mlipuko mkubwa wa moto.

Tahadhali hiyo imetolewa leo juni 19, na Mkuu wa Jeshi hilo, Kamishina Jenerali Thobias Andengenye, wakati wa zoezi la kufunga mitungi ya kuzimia moto katika Shule ya Sekondari Simiyu mjini Bariadi.

Jenerali Andengenye amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakitikisa mitungi hiyo kuangalia kama bado gesi ipo, ambapo inaweza kusababisha kuongezeka kwa presha ya gesi na kulipuka.

“ Ukitikisa gesi presha yake inaweza kupanda na msukumo mkubwa na kulipuka, ni kama ilivyo kwenye soda au bia ambavyo ukatikisa unaona presha inavyopanda, ndivyo hata kwenye gesi ilivyo tunawashauri watu wasifanye hivyo ni hatari mno,” amesema Jenerali Thobias.

Aidha amewashauri watu ambao wanataka kuangalia kama mtungi una gesi, watumie maji kwa kuweka  mtungi wa gesi kwenye maji kisha utolewe na sehemu ambayo itakauka haraka hiyo inaashiria hakuna gesi na ambayo itabaki na maji ndipo gesi ilipo.

==>>Msikilize hapo chini

Serikali Yapata Dola za Marekani Milioni 500 Kutoka India Kwa Ajili ya Kutekeleza Miundombinu Ya Maji

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Serikali imepata fedha kutoka serikali ya india kiasi  cha dola za marekani milioni 500 kwa ajili ya kuboresha huduma ya miundombinu ya maji  katika miji 28 ya tanzania na Zanzibar.
 

Hayo yamesemwa leo Juni 19,2019  bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso  wakati akijibu swali la mbunge wa Kilombero,Peter Lijualikali  aliyehoji,serikali ina mpango gani wa kuongeza mtandao wa Maji.

Akijibu Swali hilo,Naibu waziri wa maji Mhe.Aweso amesema Katika mpango wa Muda Mrefu,serikali imepata fedha kutoka serikali ya India kiasi  cha Dola za Marekani Milioni 500 kwa ajili ya kuboresha huduma ya miundombinu ya maji katika miji 28 ya Tanzania bara  na Zanzibar ambapo mji wa Ifakara ni miongoni mwa miji itakayopata maji kupitia fedha hizo na sasa taratibu za kuwapata wataalam washauri watakaofanya usanifu  wa kina na maandalizi ya makabrasha unaendelea.

Hata hivyo ,Mhe Aweso amesema kukamilika kwa mipango hiyo kutaboresha hali ya upatikanaji wa Maji kwa asilimia 90%.

Rais Magufuli Ang’ara Jarida la Forbes.... Aendelea kukubalika Kimataifa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, ameendelea kukubalika kimataifa baada ya Jarida maarufu Duniani la Forbes kubashiri kwamba ataivusha Tanzania na kuwa nchi yenye kipato cha kati kupitia ajenda yake ya Tanzania ya viwanda chini ya mpango wa maendeleo wa 2025.

Katika jarida hilo la Forbes Afrika la Julai mwaka huu ambalo lilikuwa mahsusi kwaajili ya kelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano na uongozi wa Rais Magufuli kwa ujumla, imeelezwa maono yake kama kiongozi wan chi yameifanya  Tanzania kupiga hatua kubwa za maendeleo na inatarajiwa kuwa miongoni mwa nchi chache sana za Afrika zenye maendeleo yanayoonekana na yanayopatikana kwa muda mfupi.

Kwamujibu wa Jarida hilo ambalo limemwelezea Rais Magufuli kama Tingatinga katika kusimamia kile anachokiamini, miongoni mwa mambo makubwa yanayomfanya ang’ae kimataifa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya standard Gauge SGR, upanuzi wa bandari na ujenzi wa miundombinu ya barabara zinazounganisha nchi nzima ambazo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo hapa nchini.

Aidha Rais Magufuli ameelezewa kuwa ni mtu asiye na masihara katika kusimamia masuala ya maendeleo, mfano  jinsi alivyosimamia na kuhakikisha uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere terminal three unakamilika kwa wakati na kwa kiwango cha kimataifa.

Jarida la Forbes limeendelea kumwelezea Rais Magufuli kuwa, mafanikio mengi anayopata ni kutokana na kuongozwa na mpango wa maendeleo  wa 2025 pamoja na ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015.

Miradi mingine iliyoainishwa kuonyesha utendaji wake ni ile ya umeme ya Kinyerezi  awamu ya kwanza ya pili nay a tatu, pamoja na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika maporomoko yam to Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge,ambayo lengo lake ni kumaliza kabisa tatizo la umeme hapa nchini hasa kwa wananchi wa vijijini.

Kuhusu ukuaji wa uchumi Jarida la Forbes limeelezea kuwa katika kipindi cha utawala wake tangu aingie madarakani mwaka 2015, uchumi umeendelea kukua kwa kasi kwa kiwango cha asilimia 7 ambao ni ukuaji wa mfano na wakuridhisha   kwa nchi za Afrika ikilinganishwa na miaka mingi iliyopita.

Katika uwekezaji Rais Magufuli amenukuliwa akiwahakikishia wawekezaji na dunia kwa ujumla kwamba, Tanzania ni nchi salama na kwa uwekezaji na akawakaribisha kuja kuwekeza kwani ameendelea kufanya mapinduzi makubwa katika uwekezaji lengo kuu ikiwa ni kuvutia wawekezaji wengi zaidi.

Mahojiano ya Rais Magufuli yaliyotolewa na Jarida la Forbes Africa,  yalifanyika mapema mwaka huu ambapo Jarida hilo lilikuwa na toleo maalum la Tanzania kuhusiana na mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali.

Credit: Michuzi

Mahakama ya Afrika Mashariki Yaanza kusikiliza kesi ya kupinga Sheria ya vyama vya siasa iliyofunguliwa na Freeman Mbowe, Zitto Kabwe na Wengine

$
0
0
Mahakama ya Afrika Mashariki imeanza kusikiliza kesi ya kupinga Sheria ya vyama vya siasa iliyofunguliwa na Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, Maalim Seif, Rungwe na Salum Mwalimu kwa niaba ya Vyama 8 vya upinzani Tanzania  wakiiomba EACJ isimamishe matumizi ya sheria hiyo hadi kesi ya msingi itakapoamriwa.

Katika kesi hiyo ambayo viongozi wa upinzani wanawakilishwa na Mawakili Fatuma Karume, John Mallya na Jebra Kambole wanaomba mahakama kusitisha sheria hiyo.

Wakili Karume  ameeleza majaji wa mahakama hiyo leo Jumatano Juni 19, 2019 kuwa sheria hiyo inakiuka mkataba wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika masuala ya haki na demokrasia.

Amesema miongoni mwa upungufu katika shauri hilo ni kuzuia viongozi wa upinzani kutoa elimu ya mpiga kura bila idhini ya msajili wa vyama vya siasa, kuzuia walinzi binafsi wa vyama na kuingiliwa uhuru wa vyama

Majaji wa mahakama hiyo bado wanasikiliza maombi ya upinzani kutaka mahakama hiyo kutoa uamuzi wa dharura kuzuia baadhi ya vifungu vya sheria hiyo.

Serikali Yatoa Orodha ya wadaiwa sugu wa madeni ya Commodity Import Suport....Yumo Mo Dewji, Yusuph Manji Na Wengine

$
0
0
Wizara ya Fedha na Mipango inawataka wadaiwa sugu wa madeni ya Commodity Import Suport (CIS)na FACF, walipe madeni yao mara moja. 

Madeni haya ni mkopo wenye masharti nafuu yaliyotolewa kwa Taasisi, Kampuni, Viwanda na Wafanyabiashara,  ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni bila kutozwa riba katika kipindi cha Miezi 18 tangu walipopewa mikopo hiyo. 

Kwa mujibu wa sheria ya CIS (The Commodity Import Support Regulation Act, CAP 261 R. E. 2002 (s.8 (1)(b), Mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18 tangu kupatiwa mkopo, atapaswa kulipa riba ya asimilia sawa na kiwango kinachotozwa na Benki Kuu ya Tanzania inapoikopesha Serikali katika kipindi husika. Zaidi ya makampuni 980 yalikopeshwa chini ya utaratibu huu.

Serikali inatangaza kwa mara ya Mwisho kufuatia baadhi ya wadaiwa ambao wameshindwa kuitikia wito wa matangazo ya awali ya tarehe 30/12/2015 na 05/04/2018. Hatua za kisheria zitachukuliwa mara baada ya kutoka kwa tangazo hili.

ORODHA YA KWANZA YA WADAIWA SUGU WA MADENI YATOKANAYO COMMODITY IMPORT SUPPORT(CIS) NA FOOD AID COUNTERPART FUND (FACF).

1. Yusuph Manji

·         Farm Equipment Tanzania Ltd

·         Quality Group Ltd

·         Dunhill Motors Ltd

·         Quality Seed Ltd

·         Quality Garage Ltd

2. Mohamed Dewji

·         21st Century Textiles Ltd

·         Afritex Ltd

2. S. S Rashid

·         Pwani Tours and Safari Ltd

·         Pwani Investment Ltd

5. Issack Bugali

·         Dar es Salaam International School Trust Fund

·         Upoloto Farm  Ltd

6. K.B Medicare Ltd (Prof. Bernard Kirei)

7.Siza Cold Storage Co.Ltd (Stephen Wasira)

8. Sorority Co. Ltd (Martha Lyimo)

9. 21st Century, Afritex Ltd,

10. Kichonge Miller (Bokeye Kangoye)

11. Rela Investment Company Ltd (Ahiya E. Lukumayi)

12. Bahari Motor Co Ltd (Hashim Rungwe)

13. Andrew Traders Co Ltd (Andrew Richard Kisenge)

14. Oth Investment Co Ltd (Boniventure Boniventure)

15. Kiomboi Kisiriri Pharmacy Ltd (Dkt Kingu)

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Kikosi Kazi, Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es Salaam, chumba Na. 352, Simu Na. +255 739403025/ 2122282285

KATIBU MKUU
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Serikali Kutoa Tamko Rasmi Kuhusu Ugonjwa wa Dengue

$
0
0
Serikali imeeleza kuwa inatarajia kuja na utaratibu mpya wa kutibu ugonjwa wa Dengue ambao umezuka katika baadhi ya mikoa nchini ikiwemo Dar es Salaam na kupelekea vifo kwa baadhi ya watu na wengine kuugua.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Waziri Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mbunge wa Ilala Mussa Zungu ambaye alihoji juu ya Serikali kugawa dawa mpya zitakazomaliza mbu wa ugonjwa wa Dengue.

Akiuliza swali hilo Bungeni, Mbunge Zungu amesema kuwa, "bado kuna changamoto kwenye upambanaji wa Dengue, Serikali itabadilisha dawa zinazotumika ili wananchi washiriki wazimwage kwenye maeneo yao, Mheshimiwa Naibu Spika ni kwamba sasa hivi Mbu wa Dengue wameanza kuingia kwenye daladala".

Akijibu swali hilo Bungeni, Waziri Ummy amesema "suala hili limeanza kufanyiwa kazi na Serikali, ndani ya siku 2 tutatoa kauli rasmi jinsi gani tumechukua hatua za kupambana na Dengue".

"Niwaambie pia wananchi hakuna njia nyingine ya kujikinga na ugonjwa Dengue zaidi ya kuwatokomeza mbu hao," ameongeza.

PICHA: Pierre Liquid A.KA "Konki Fire" Katua Tena Bungeni....Tazama Hapa Akisalimiana na Waziri Mkuu

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Msanii Pierre Liquid kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 19, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Msanii Pierre Liquid kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 19, 2019.  Wa pili kulia ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Mhandisi Ramo Makani.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi June 20

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yasema Haitatumia Wakurugenzi Kusimamia Uchaguzi

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesisitiza vifungu vya sheria vilivyokuwa vikiruhusu wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, miji na majiji kusimamia uchaguzi ambavyo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imevitengua, havitatumika katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Kauli hiyo ya NEC imekuja wakati kukiwa na sintofahamu, hasa baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Aderladus Kilangi, kuwasilisha kusudio la kukata rufaa kupinga utekelezaji wa hukumu hiyo.

Katika hoja zake, AG alisema utekelezaji wa hukumu hiyo unasimama hadi pale rufaa ya Serikali itakapoamriwa.

Hata hivyo, akizungumza katika mkutano wa NEC na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura ambao uandikishaji wake unatarajiwa kuanza Julai, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage alisema katika kutekeleza majukumu yao, vifungu hivyo vya Sheria ya Uchaguzi 7(1) na 7(3) havitatumika.

Mkutano huo ulifanyika jana katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Jaji Kaijage ambaye alikuwa akijibu swali aliloulizwa na mwandishi aliyetaka kujua msimamo wa NEC baada ya mahakama kuondoa vifungu hivyo, alisisitiza pasipo kueleza kwa kina kuwa “vifungu vingine vya sheria hiyo ambavyo havikulalamikiwa vitaendelea kutumika kama kawaida”.

Pamoja na hayo, Jaji Kaijage  hakufafanua ni nani ambao watasimamia uchaguzi baada ya wao kuamua kutotumia vifungu hivyo.

Mei 10, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam katika hukumu yake iliyotolewa na jopo la majaji watatu – Dk. Atuganile Ngwala, Dk. Benhajj Masoud na Firmin Matogolo, ilibatilisha kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Uchaguzi kinachoipa mamlaka NEC kuwateua wakurugenzi wa majiji, manispaa na miji kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa kuwa kinapingana na sheria mama, yaani Katiba.

Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bob Wangwe, aliyekuwa akitetewa na Wakili Fatma Karume, pia mahakama hiyo ilibatilisha kifungu cha 7(3) kinachoipa NEC mamlaka ya kuteua mtu yeyote miongoni mwa watumishi wa umma kuwa msimamizi wa uchaguzi.

 Mahakama ilisema vifungu hivyo ni kinyume cha Katiba ya nchi ikibainisha kuwa wakurugenzi hao ambao si waajiriwa wa NEC, huteuliwa na rais aliyeko madarakani, ambaye hutokana na chama tawala na kwamba wengine ni wanachama wa chama cha mamlaka inayowateua jambo ambalo huathiri utendaji wao katika kutenda haki.

Alisema kifungu cha 7(1) kinasema kila Mkurugenzi wa Jiji, Manispaa na Halmashauri anaweza kusimamia uchaguzi wakati viongozi hao ni wateule wa Rais na si waajiriwa wa NEC wakati Katiba inasema NEC inapaswa kuwa huru na haki.

Jaji Ngwala alisema kutokana na hali hiyo, kifungu hicho kinakinzana na sheria mama ambayo inasimamia nchi. Pia kifungu cha 7(3) kinasema kuwa NEC inaweza kuteua mtu yeyote kuwa msimamizi wa uchaguzi bila ya kuainisha ni mtu wa aina gani.

Jaji Ngwala alisema, lakini Katiba inasema kuwa mtu yeyote anayekuwa msimamizi wa uchaguzi hapaswi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.

Mei 13, AG Dk. Kilangi alisema Serikali imewasilisha katika Mahakama ya Rufani kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kuwazuia wakurugenzi kusimamia uchaguzi kwa niaba ya NEC.

Dk. Kilangi alisema tayari Serikali kupitia kwa Wakili Mkuu wa Serikali (SG) imewasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Alisema kuwapo kwa hukumu hiyo hakuathiri chaguzi nyingine zijazo, zikiwemo ndogo, kwani baada tu ya kuwasilisha taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa utekelezaji wa hukumu hiyo husimama, hadi pale rufaa itakapoamuliwa.

IGP Sirro awatoa hofu wananchi tishio la shambulizi la Kigaidi

$
0
0
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limewatoa hofu wananchi juu ya tishio la ugaidi katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam, likisema taarifa hizo zimeshaanza kufanyiwa kazi.

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro amesema kuwa jeshi lake lilishapata fununu za shambulio hilo kabla Ubalozi wa Marekani kutoa tahadhari juu ya tukio hilo kupitia tovuti yake Juni 18, 2019.

Akizungumzia taarifa hiyo ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, IGP Sirro amesema, “hiyo ni taarifa kama taarifa nyingine, inaweza kuwa ya kweli au uongo, lakini sisi kama vyombo vya ulinzi huwa hatupuuzi jambo. Tangu  Jumanne Juni 17, 2019 tulipata hiyo taarifa kwa hiyo tuko vizuri, timu zetu za operesheni na intelijensia na wengine tunaifanyia kazi.”

Katika tangazo lake Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania inaeleza kuwapo kwa uvumi wa kutokea kwa shambulio la kigaidi katika eneo la Masaki hususan hoteli za kitalii na maduka ya maeneo hayo ya ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Ubalozi huo umewataka wakazi kuwa makini na maeneo hayo, kujiepusha na makundi na kufuatilia taarifa kupitia vyombo vya habari.

Rugemalira Ajaribu Tena Bahati Yake Ya Kupewa Dhamana Mahakama ya Rufaa

$
0
0
Mshtakiwa wa kesi ya uchotaji fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, James Rugemalira kwa mara  nyingine tena amejaribu bahati yake ya kupata dhamana katikati ya mashtaka yasiyo na dhamana yanayomkabili yeye na mwenzake, baada ya kuiomba Mahakama ya Rufani nchini Tanzania imwachie huru kwa dhamana.

Rugemalira ambaye anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi  yenye mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana, ametoa maombi hayo  Jumatano Juni 19, 2019, wakati wa usikilizwaji wa rufaa yake.

Katika rufaa hiyo Rugemalira anapinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, (Mahakama ya Ufisadi) kumnyima dhamana, uliotolewa na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahaka hiyo Firmin Matogolo, Agosti 30, 2019.

Rufaa hiyo imesikilizwa jana na  jopo la majaji watatu, Richard Mziray (kiongozi), Winfrida Korosso na Ignas Kitusi, ambapo Rugemalira licha ya kuwa na mawakili wawili, ameomba na akaruhusiwa kutoa hoja zake za rufaa yeye mwenyewe, kabla ya mawakili wake.

Baada ya kusikiliza hoja hizo, Jaji Mziray ameahirisha shauri hilo hadi tarehe nyingine itakayopangwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani kwa ajili ya uamuzi.

Rugemalira licha ya kukabiliwa na mashtaka hayo ambayo hayana dhamana alikimbilia mahakamani hapo kuomba afutiwe mashtaka ya utakatishaji fedha kisha aachiwe huru kwa dhamana kwa madai hati ya mashtaka yanayowakabili ina kasoro za kisheria, kwa kutokuwa na  maelezo yanayoonyesha kosa la utakatishaji fedha.

Hata hivyo  Jaji Matogolo alitupilia mbali maombi hayo akisema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpa nafuu alizokuwa akiziomba.

Marekani yakiri ndege yake kutunguliwa na majeshi ya Iran ambayo yamedai kuishambulia ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya Marekani

$
0
0
Jeshi la Marekani limekiri Ndege yake kutunguliwa na jeshi la Iran ilipokuwa kwenye anga ya kimataifa kwenye eneo la mpaka kati ya ghuba ya Oman na Uajemi, maafisa wa Marekani wameeleza.

Awali vikosi vya kijeshi vya Iran vilidai kuwa vimeshambulia ndege ya kijasusi isiyo na rubani kwenye anga la Iran.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti tukio hilo dhidi ya ndege isiyo na rubani walioiita RQ-4 Global Hawk, kusini mwa jimbo la Hormozgan.
 
Jeshi la Marekani awali halikuthibitisha kama ndege yake imeangushwa, huku msemaji akikana taarifa kuwa ndege ya Marekani ilikua kwenye anga la Iran.

Tukio hilo limetokea siku kadhaa baada ya wizara ya ulinzi ya Marekani kusema kuwa watapeleka vikosi 1,000 zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati baada ya kutokea mvutano kati ya Marekani na Iran.

Marekani iliishutumu Iran kushambulia kwa mabomu meli za mafuta katika Ghuba ya Oman.

Mzozo huo ulishika kasi siku ya Jumatatu wakati Iran iliposema kuwa itazidisha kiwango cha urutubishaji wa madini ya Urani kinyume cha makubaliano na mataifa yenye nguvu duniani mwaka 2015.

Iran imefikia uamuzi huo baada ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani.

Lugola: Hakuna Tishio Lolote la Ugaidi Nchini

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Watanzania wasiwe na hofu juu ya tishio la ugaidi kwani nchi ina usalama wa hali ya juu.

Akizungumza leo Juni 20, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani, amesema vyombo vya ulinzi vinaendelea na uchunguzi juu ya suala hilo.

“Serikali iko imara na vyombo vya ulinzi na usalama viko imara vimejipanga vizuri kwa jambo au tishio lolote la usalama.

“Tahadhari ambayo imetolewa na wenzetu wa Marekani hizi ni sehemu ya taarifa za kawaida na tumeweza kuwasiliana nao kupitia jeshi la polisi.

“Watanzania wasiwe na hofu wala wasiwasi nchi iko imara  ina usalama wa hali ya juu na vyombo vinaendelea kufanya kazi yake,” amesema Lugola.

Awali, Mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania, Chansa Kapaya anasema siku ya wakimbizi inatoa nafasi ya kutafakari na kukumbuka kwamba wakimbizi ni watu na wanatamani nchi zao ziwe na amani waweze kurejea.

"Tunaunga mkono Serikali ya Tanzania katika kutoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na chakula, mavazi, maji safi na makazi," amesema.

Mpaka Mei 2019 Tanzania ilikuwa inahifadhi wakimbizi 312,152 wengi wao walitokea Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jana Jumatano Juni 19, 2019 Ubalozi huo ulieleza kuwapo kwa uvumi wa kutokea kwa shambulio la kigaidi katika eneo la Masaki hususan hoteli za kitalii na maduka ya maeneo hayo ya ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Ubalozi huo uliwataka wakazi kuwa makini na maeneo hayo, kujiepusha na makundi na kufuatilia taarifa kupitia vyombo vya habari.

Serikali Ya Tanzania Yajipanga Kuteka Soko La Watalii China

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kwa sasa muelekeo wa soko la Utalii nchini umelenga kupata watalii wengi kutoka nchini China na kama Wizara inayoshugulikia masuala ya Utalii,  suala la  kujifunza lugha ya kichina kwa baadhi ya watumishi na wadau wa utalii ili kuteka soko hilo ni jambo lisiloepukika.

Imesema nguvu nyingi kwa sasa zinaelekezwa nchini China hivyo  ni muda muafaka wa kuandaa timu ya wataalamu mbalimbali wakiwemo  waongoza watalii watakaoweza kuzungumza lugha ya kichina ili kuweza kulimudu soko hilo.

Hayo yamesemwa leo  jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu  wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa  Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii  cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS

Amesema  lengo mkutano huo ni  kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya

China na Tanzania katika suala la kuwajengea uwezo watumishi na wadau wa Utalii nchini.

Mkutano huo  umehudhuriwa na ujumbe kutoka China ukiongozwa na Makamu wa Chuo hicho,Prof.Xiong Nanyong,Kaimu huku kwa upande wa Wizara  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.Lucius Mwenda pamoja na ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara.

Amesema ni muhimu kwa watumishi wa wizara pamoja na wadau wa utalii kujiandaa ili kuweza kuzungumza lugha ya kichina badala ya vifaa maalum vya kutafsiri lugha ilhali kuna uwezekano kwa Watanzania kujifunza.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Xiong Nanyong amesema wamejipanga kutoa mafunzo mbalimbali likiwemo suala la lugha ya kichina pamoja na utalii ili kuwajengea uwezo Watumishi hao

Ameongeza kuwa tayari wameshaomba kibali kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa umma na Utawala Bora  kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lucius Mwenda  ameahidi kutoa ushirikiano kwa Uongozi wa Chuo hicho ili  kujengeana uwezo  baina ya Serikali ya  Tanzania na China

Mbunge Aishauri Serikali Ifute Tozo Ya Maiti Kwenye Chumba Cha Kuhifadhia Maiti [mortuary]

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Michango ya Wabunge ya kuchangia maoni mbalimbali  juu ya bajeti kuu ya Serikali imeendelea bungeni jijini Dodoma ambapo mbunge wa Kahama mkoani Shinyanga,Jumanne Kishimba maarufu kwa jina Prof.Kishimba ameitaka serikali kufuta tozo la Maiti kwenye chumba cha kuhifadhia  maiti [Mortuary]
 
Mhe.Kishimba ameshangaa  kufuta na kusamehe  tozo kwenye unga wa  ngano huku tozo la Maiti kwenye Mortuary ambayo ni Tsh.Laki tano  ikiwa inaendelea hivyo ameishauri serikali kurudisha tozo ya keki na kuweza kufuta tozo ya maiti.
 
Mhe.Kishimba amesema ni jambo la kushangaza kwa watu wanaofariki kwa waganga wa jadi hawadaiwi bili yoyote  na hupewa huduma ikiwa ni pamoja na sanda lakini mtu anapofariki akiwa hospitalini anadaiwa bili kubwa hivyo ni vyema serikali ikaangalia upya suala hilo kwani hali hiyo husababisha baadhi ya maiti hukosa ndugu wa kuichukua hospitalini kwa kukwepa kulipa bili  na tozo ya Mortuary kutokana  na hali ngumu ya Maisha na kusababisha kuzikwa ovyo.
 
“Mnajua waheshimiwa wabunge sisi ni  marehemu watarajiwa ,kasoro itakuwa  muda,tarehe na wakati,tumesamehe tozo ya keki lakini kwenye tozo ya maiti inabaki palepale,haiwezekani mtu apoteze mtu halafu atozwe bili na fedha ameitoa wapi”Amesema.
 
Mbunge Kishimba amesema yawezekana watengeneza Bajeti wanaishi Osterbay hawajui hali ngumu za watanzania kwa kufuta tozo ya keki ambayo kwa watanzania walio wengi amedai haina tija kwao na hivyo kuna haja ya  serikali kurudisha tozo hiyo na kufuta tozo ya Maiti kwenye Mortuary.
 
Aidha ,Mhe.Kishimba ameiomba serikali iruhusu wananchi pindi wanapoenda kutibiwa ikiwa  hawana fedha waende na mifugo yao hospitalini kama dhamana ili kutibiwa haraka na kuokoa Maisha yao  kwani  bado kuna dhana ya baadhi ya jamii  kanda ya ziwa kutokuwa na uelewa juu ya bima kwani  hudhani kuwa kukata bima ni kujitakia ugonjwa au kifo na elimu inatakiwa itolewe  zaidi.
 
Sambamba na hayo,Mhe,Kishimba amesema kuna haja kubwa ya serikali kupunguza tozo za X-RAY  ili watu wengi wanunue na kupekeka hospitalini  hali itakayosaidia kupata huduma za X-Ray kwa bei nafuu.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images