Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne June 18


Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi Afariki Dunia Ghafla Mahakamani

$
0
0
Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika mahakama ya mjini Cairo.

Rais wa kwanza wa Misri kuchaguliwa kwa njia ya demokrasia ambaye alipinduliwa na jeshi mnamo mwaka 2013 baada ya mwaka mmoja madarakani, Mohammed Morsi, alianguka mahakamani wakati kesi yake ilipokuwa ikisikilizwa na kufariki, televisheni ya taifa na familia yake ilisema.

Morsi aliyekuwa na umri wa miaka 67 alikuwa amemaliza kuihutubia mahakama, akizungumza akiwa katika chumba cha glasi alimowekwa wakati wa vikao vya kusikilizwa kesi yake na kuonya ana 'siri nyingi' ambazo angeweza kuzifichua, afisa wa idara ya mahakama alisema.

Dakika chache baadaye, Morsi alianguka na kupoteza fahamu ndani ya chumba hicho cha glasi, aliongeza kusema afisa huyo aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina kwa sababu hakuwa na amri ya kuzungumza na vyombo vya habari.

Katika kauli zake za mwisho, Morsi aliendelea kusisitiza alikuwa rais halali wa Misri, akidai mahakama maalumu, mmoja wa mawakili wake, Kamel Madour, aliliambia shirika la habari la Associated Press.

Televisheni ya taifa ilisema Morsi alikufa kabla hajapelekwa hospitali. Chama cha Morsi cha Udugu wa Kiislamu kimeilaumu serikali kwa kumuua kupitia mazingira mabaya gerezani. Katika taarifa kundi hilo limetaka uchunguzi wa kimataifa ufanywe kubaini chanzo cha kifo cha Morsi na kuwataka Wamisri waandamane nje ya balozi za Misri kote ulimwenguni.

Morsi, ambaye anafahamika kuugua kisukari, amekuwa gerezani tangu alipopinduliwa mwaka 2013, akitengwa na wafungwa wengine kwa kuwekwa katika chumba chake peke yake na kunyimwa haki ya kuwa na wageni. Familia yake iliruhusiwa kumtembelea mara tatu wakati wa kipindi hicho.

Mwendesha mashitaka mkuu wa Misri amesema mwili wa Morsi utafanyiwa uchunguzi kubaini sababu ya kifo chake.

Tanzania yaongoza kwa amani Afrika Mashariki

$
0
0
Tanzania imeongoza Afrika Mashariki kwa mujibu wa ripoti ya Global Peace Index (GPI) inayotolewa na taasisi ya uchumi na amani (IEP)yenye makao yake makuu mjini Sydney nchini Australia.

Tanzania imeshika nafasi ya 7 kwa kuwa nchi yenye amani kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na duniani ikiwa imeshuka kutoka nafasi ya 51 mwaka 2018 hadi nafasi ya 54 mwaka 2019 kati ya nchi 163, huku Iceland, New Zealand, Uholanzi, Austria, Denmark, Canada, Singapore, Slovenia, Japan, na Jamuhuri ya Czech ni nchi zilizoorodheshwa kuwa na amani zaidi duniani.

Wakati Tanzania ikiongoza Afrika Mashariki, Rwanda imeifuata ikiwa ya pili Afrika Mashariki lakini imeshika nafasi ya 17 kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, ikifuatiwa na Uganda iliyoshika nafasi ya 23 , Kenya ya nne Afrika Mashariki na 28 katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Nchi zilizoshika nafasi za juu katika eneo la jangwa la sahara ni Mauritius, Botswana, Malawi, Ghana, Zambia na Sierre Leone.

Kwa mujibu wa Ripoti hiyo, nchi zilizo na kiwango cha chini cha amani ni Burundi,Chad, Cameroon, Mali, Nigeria, DR Congo, Somalia na Sudani Kusini.

Wizara ya Afya Kenya Yasema kuwa hakuna Ebola...Ni Baada ya Majhibu ya Yule Mgonjwa Aliyehisiwa Kuonesha Hana Ugonjwa Huo

$
0
0
Matokeo ya utafiti wa damu ya mgonjwa aliyeshukiwa kuwa na virusi vya Ebola yameonyesha kwamba hana virusi vya ugonjwa huo.


Katika taarifa rasmi kwa vyombo vya habari, wizara ya afya nchini Kenya imetoa hakikisho kwamba hakuna kisa chochote cha Ebola nchini Kenya.

Waziri wa afya nchini Sicily Kariuki awali alijaribu kutuliza wasiwasi uliopo kwa kueleza kwamba dalili za mgonjwa aliyeshukiwa kuwa na Ebola 'haziambatani na ugonjwa huo'.

Mwanamke aliyeshukiwa kuwa na Ebola alitengwa katika Hospitali ya Kericho, eneo la Bonde la Ufa kusini-magharibi mwa Kenya.
 
"Dalili za mgonjwa haziambatani na ugonjwa wa Ebola ," amewaambia wandishi habari katika uwanja mkuu wa ndege Nairobi alikofanya ukaguzi wa vituo vya udhibiti wa Ebola.

Sampuli za damu za mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 36 zimeonyesha kamba hana virusi vya Ebola.

Mumewe na watu wengine wawili walio karibu naye pia walitengwa.

Maafisa wa afya katika Kaunti ya Kericho wamesema kuwa mwanamke huyo anayekaguliwa alisafiri kutoka Malaba eneo la mpaka kati ya Kenya na Uganda.

Hakuna ripoti yeyote iliyotolewa ya kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola karibu na mpaka wa Malaba:Isipokuwa eneo la Magaharibi mwa Uganda.

Mwanafunzi Chuo Kikuu cha Kampala tawi la Tanzania (KIU) Afariki Dunia Kwa Kuchomwa Visu Nje ya Geti la Chuo

$
0
0
Mwanafunzi wa stashahada ya maabara kutoka Chuo Kikuu cha Kampala tawi la Tanzania (KIU), Anifa Mgaya amefariki dunia  Jumapili usiku baada ya kushambuliwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana.


Anifa alikutwa na umauti majira ya saa 2 usiku jirani na geti la kuingia katika chuo hicho kilichopo GongolaMboto jijini Dar es Dar es Salaam alichokuwa akisoma.

Taarifa zinaeleza baada ya kushambuliwa, wanafunzi wenzake walijitokeza ili kumpatia msaada kwa kumkimbiza hospitali lakini hadi wanafika alikuwa tayari umauti umemfika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Zuberi Chembela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akibainisha vijana waliohusika katika tukio hilo wanasemekana kuwa ni vibaka.

TAKUKURU Yakanusha Taarifa za Upotoshaji Dhidi ya Watumishi Wake

Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji Kufanya Ukaguzi Wa Vifaa Vya Kuzima Moto Katika Magari Yote Nchini

$
0
0
SALVATORY NTANDU
Jeshi la zimamoto na Ukoaji limewataka wamiliki wa Magari ya abiria na Mizigo kuyapeleka magari yao katika vituo vya ukaguzi vilivyopo chini ya jeshi hilo ili kufanyiwa ukaguzi wa vifaa vya kuzimia moto pamoja na kupatiwa elimu na matumizi sahihi ili kuepuka madhara yatokanayo na majanga ya moto.

Hayo yamebainishwa jana na Kamisha Jenerali wa Jeshi la zimamoto na uokoaji (CGF) THOBIAS ANDENGENYI wilayani Kahama mkoani shinyanga katika ziara ya kikazi ya kukagua shughuli zinazotekelezwa na jeshi hilo.

Amesema ni budi kwa wamiliki wa Magari  kutii agizo hilo ambalo ni takwa la kisheria  ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria kwani elimu juu ya matumizi ya vifaa vya kuzimia moto ni muhimu sana na hawapaswi kupuuza agizo hilo.

Mbali na hilo Kamishina ANDENGENYI amesema  kwa sasa Jeshi la zimamoto na Uokiaji  linatarajia kuanzisha vilabu vya marafiki wa zimamoto na uokoaji katika shule za msingi na sekondari nchini kwa lengo la kutoa elimu juu ya kukabiliana na majanga ya moto katika maeneo wanayoishi.

Nae mkuu wa wilaya ya Kahama, ANAMRINGI MACHA amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za Msalala, Ushetu na Mji kuhakikisha kabla ya kujenga  majengo  ya umma ni lazima ramani zake ziwe zimehakikiwa na Jeshi la zimamoto na uokoaji ili kupewa ushauri wa kitalaam ambao utasaidia kuondoa madhara yatokanayo na moto katika majengo hayo.

Wanunuzi Watakiwa Kununua Pamba Kwa Bei Elekezi

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa Kilimo amewaomba wanunuzi wa pamba waliopewa leseni na Bodi ya pamba wanunue pamba kwa wakulima kwa bei elekezi ya shilingi 1200 kama ilivyopangwa na kukubaliwa katika kikao cha wadau wa pamba mwezi Mei, 2019 jijini Mwanza.

Waziri Hasunga ameyasema hayo Juni 15, 2019 wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu wakati alipotembelea viwanda vya kuchambua pamba, vituo vya kununulia pamba na kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.

“Naomba nitumie nafasi kuwaomba wanunuzi wa pamba wenye nia njema na nchi hii waliopewa leseni na Bodi ya Pamba waje kununua pamba kwa wakulima, bei elekezi ya mwaka huu ni shilingi 1200”-alisema Waziri Hasunga.

Aidha, Waziri Hasunga amevitaka vyama vya ushirika vya msingi kuzikagua mizani kwani itakapobainika kufanyika uchakachuaji wakati wa kupima hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, huku akiwahakikishia wakulima kuwa changamoto zote zilizobainishwa na wakulima katika msimu wa 2018/2019 zitafanyiwa kazi.

Mkulima wa Pamba kutoka Luguru wilayani Itilima, Bw. Ngusa Lutenganeja ameishauri Serikali kupanga bei ya pamba wakati wa maandalizi ya msimu ili wakulima walime wakiwa wanafahamu bei na maandalizi ya fedha yafanyike mapema wakulima wasikopwe pamba yao.

Kwa upande wake Mnunuzi wa pamba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga amesema imani yake ni kwamba Serikali itasimamia na kuhakikisha pamba ya wakulima inanunuliwa kwa bei elekezi ya shilingi 1200/= na wananchi wanapata fedha zao kwa wakati.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa wa Simiyu una viwanda vingi vya kuchambua pamba, ambapo ameshauri kuwa ili kuliongezea thamani zao la pamba Wizara ya Kilimo kwa  kushirikiana na wadau wengine kuona uwezekano wa kujenga kiwanda cha  kutengeneza nguo  kwa kuwa uhakika wa soko la bidhaa zitakazotengenezwa upo.

Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa pamba nchini (TCA), Bw. Boaz Ogola ametoa wito kwa Wanunuzi wa pamba kuunga mkono juhudi za Serikali katika viwanda kwa kuwekeza kwenye viwanda vya kuongeza thamani ya pamba ili tusitegemee soko nje ambalo linayumba.

MWISHO

Ujenzi Wa Tawi Jipya La IFM Simiyu Kukamilika Septemba 2019

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof. Tadeo Satta  amewahakikisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kuwa ujenzi wa awali wa  tawi la Chuo hicho mkoani Simiyu ,unatarajia kukamilika  mwezi Septemba mwaka huu na kuanza kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo 2019/2020 .

Profesa  Satta ameyasema hayo Juni 17, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Tawi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Simiyu katika kijiji cha Sapiwi wilaya ya Bariadi.

Profesa  Satta  amesema kujengwa kwa kituo hicho kipya cha mafunzo kutachangia kuongeza udahili na  kubainisha kuwa katika mpango mkakati wa chuo mwaka 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021, chuo kimejipanga kuongeza kutoa mafunzo kwa wateja wake hasa katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Simiyu inayotarajiwa kuchukua mikoa ya kanda ya ziwa mpaka Tabora.

Ameongeza kuwa azma ya chuo ni kuanza kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo 2019/2020 kuanzia ngazi ya cheti  na matarajio ni kuhamisha wanafunzi wa ngazi ya cheti na stashahada kutoka Mwanza kuja Simiyu ili Mwanza zibaki kozi za jioni wanazosoma watu wanaotoka kazini.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amempongeza Makamu Mkuu wa Chuo IFM, Prof. Tadeo Satta kwa kuwa mtendaji wa mipango aliyoipanga na kutimiza ahadi ya kuanza kujenga tawi hilo mwaka huu, huku akitoa wito kwa  wananchi wote kuchangamkia  fursa mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hosteli, migahawa na nyumba za kupangisha watumishi.

“Tawi la Chuo cha IFM linajengwa Sapiwi watu wote wanaalikwa kuchangamkia fursa na wachangamikiaji wa fursa wa kwanza ni wana Sapiwi wenyewe, tungehitaji kupata hosteli, migahawa ya chakula, maeneo ya watu kunywa vinywaji na tutawaambia TANROADS waone namna ya kuweka “stendi” maana hapa Sapiwi kitakuwa kituo kikubwa” alisisitiza Mtaka.

Aidha, Mtaka amewahakikishia viongozi wa Chuo cha IFM kuwa viongozi wa Mkoa wataendelea kushirikiana nao  katika kuhakikisha azma ya kukamilisha ujenzi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwezesha mkandarasi kufanya kazi saa 24 kwa kuhakikisha kuna ulinzi  na miundombinu ya umeme inakuwepo katika eneo la ujenzi.

Naye Mayunga Juma Mkazi wa kijiji cha Sapiwi amesema wananchi wa Sapiwi wanashukuru  uwepo wa ujenzi huo kwani umesaidia kutoa ajira na kuwawezesha kupata fedha za kujikimu kimaisha.

Kwa upande wake Msimamizi wa Ujenzi huo kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) Kagera,   Baluye Mitinje  ameahidi kusimamia na kuhakikisha ujenzi unafanyika usiku na mchana ili ukamilike kwa wakati.

Ujenzi wa awali wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Tawi la Sapiwi utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia tisa na sabini na moja .

MWISHO

Wabunifu wa umeme Njombe wakabidhiwa mamilioni yao na Tanesco

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Shirika la umeme Tanzania Tanesco limewakabidhi kiasi cha shilingi milioni 30 (15mil kila mmoja) wabunifu wawili  wa umeme mkoani Njombe ili ziweze kuwasaidia katika kuboresha miundombinu yao.

Akizungumza wakati akikabidhi fedha hiyo mbele ya wananchi wa kijiji cha Lugenge kilichopo katika halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo,mkurugenzi mtendaji wa Tanesco DK.Tito Mwinuka amesema lengo la kufika katika kijiji hicho ni kutimiza ahadi waliyoitoa mbele ya Rais, huku akiahidi kushirikiana na wabunifu hao ili kuongeza nguvu ya umeme katika vijiji vya wabunifu hao.

“Kama tulivyo ahidi tulituma wataalamu wamefika hapa tangu juzi na wameweza kubaini,ni vitu gani vikifanyika basi vinaweza kusaidia ule umeme upatikane mwingi zaidi  na wananchi waweze kufaidika,kwa hiyo kwa maeneo hayo mawili tumeona kuna uwezekano wa sisi Tanesco kusaidia umeme kupatikana mkubwa zaidi kule msete na hapa Lugenge,uwe salama zaidi na watu waweze kufaidika”alisema Dkt.Mwinuka

John Fute maarufu kwa jina la mzee Pwagu mbunifu wa umeme katika kijiji cha Msete unaozalisha  kilowati 28, mara baada ya kupokea fedha kiasi cha shilingi milioni 15 ametoa rai kwa wananchi kuendeleza vipaji vya watoto wao.

“Mimi langu moja kila mtoto amezaliwa na kipaji chake sasa niwaombe wazazi wenzangu, tujaribu kuwasaidia watoto sio kuwafifisha unaweza kuona siku moja umefanikiwa mfano kama mimi sasa hivi nina miaka 60 lakini nimeanza tangu mwaka 1980 kutengeneza umeme”

Kwa upande wake Lainery Ngailo mbunifu wa umeme katika kijiji cha Lugenge unaozalisha kilowati 15 ameishukuru serikali kwa kuwafikisha wataalamu katika kijiji chake na kuahidi kushirikiana nao ili kuwafikishia nishati wananchi.

Aidha shirika hilo limemkabidhi shilingi milioni moja na laki nne mwandishi wa habari wa  shirika la utangazaji Tanzania TBC Tatu Abdalah kazimoto kwa kuwaibua wabunifu hao.

Nao baadhi ya wananchi katika kijiji cha Lugenge akiwemo bwana John mfyagindza wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt.John Pombe Magufuli kwa kuwaona wataalamu hao kutokana na kuwepo kwa wataalamu wengi vijijini wanaoweza kufanya mambo makubwa lakini wamekuwa wakikosa ushirikiano na baadhi ya taasisi za serikali.

June 13 shirika hilo liliahidi kutoa fedha hiyo kwa wabunifu hao mbele ya Rais Magufuli katika kikao cha wabunifu wa uzalishaji wa umeme nchini kilichofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.

Mkopo wa shilingi milioni 194 watolewa kwa wanawake, vijana na walemavu wilayani Njombe

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Jumla ya vikundi 86 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu halmashauri ya wilaya ya Njombe vimepatiwa mikopo yenye thamani ya kiasi cha shillingi milioni 194 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Mikopo hiyo iliyotolewa kwa awamu mbili,awamu ya kwanza halmashauri hiyo ilitoa mikopo ya thamani ya tsh milioni 66 mnamo mwezi february 2019 katika vikundi 36 huku awamu ya pili ikitolewa tsh milioni 128 katika vikundi 50.

Katika kipindi hicho cha 2018/2019 vikundi vya wanawake vimeonekana kuongoza kupatiwa mikopo kwa kuwa na vikundi 59,vijana 22,watu wenye ulemavu Vikundi 5

Akisoma taarifa ya mikopo ya awamu ya pili katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Ally Juma Ally, amesema kuwa kwa mwaka 2018/2019 halmashauri hiyo imeviwezesha vikundi 59 vya wanawake, vijana vikundi 22 na watu wenye ulemavu vikundi vitano.

Aidha mkurugenzi huyo amebainisha kuwa kati ya shilingi Milioni 194 zilizokopeshwa, milioni 143 ni mchango wa mapato ya ndani ya halmashauri, shilingi milioni 51 zinatokana na marejesho ya mikopo ya awali na kuongeza kuwa halmashauri hiyo imevuka lengo kwa kutoa mikopo kwa asilimia 135 kati ya asilimia 100 zilizowekewa malengo kwa mwaka 2018/2019.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika makabidhiano ya mikopo hiyo amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia ipasavyo katika kujikwamua kiuchumi pamoja na kuirejesha kwa wakati ili Serikali kupitia halmashauri ya Njombe iendelee kutoa mikopo mingine kwa wahitaji.

Baadhi ya Wanufaika wa mikopo hiyo wakiwemo watu wenye ulemavu wameipongeza halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa kutambua umuhimu wa vikundi vyao na kuvisaidi kupata Fedha ili waweze kuendesha shughuli zao za ujasiliamali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Serikali Yawahakikishia Wawekezaji Mazingira Rafiki Ya Uwekezaji Nchini

$
0
0
NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki amewahakikishia wawekezaji kutoka Marekani uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji nchini kwa kuzingatia mchango wao katika masuala ya uwekezaji.

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua kongamano la siku moja la kujadili masuala ya kuboresha mazingira ya biashara pamoja na uwekezaji nchini lililofanyika tarehe 17 Juni, 2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Hyatt Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yaliyolenga kujadili changamoto zinazowakabili na kujadili namna bora ya kukabiliana nazo na hatua mahsusi ambazo Serikali imeendelea kuzichukua ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi wa Marekani kwa kushirikiana na Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania na kuhusisha  wawakilishi wa   Kampuni 47 kati ya 238 za Kimarekani na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi, Maafisa Waandamizi wa Serikali ya Tanzania, Wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani pamoja na Wanachama wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kimarekani.

Waziri Kairuki alieeleza nia ya Serikali ni kuendelea kuwa na mazingira wezeshi yanayowavutia wawekezaji nchini katika kuendelea kuchangamkia fursa zilizopo na kupokea maoni yao ili kutatua changamoto wanazokumbana nazo.

“Serikali itaendelea kuweka mkazo mkubwa wa maboresho katika maeneo mbalimbali yatakayo kuvutia wawekezaji ikiwani pamoja na  uboreshwaji wa sekta ya mawasilino, miundombiu ya barabara na usafirishaji ili kuwa na mazingira mazuri ya wawekezaji kuja kuwekeza nchini,”alisema Waziri Kairuki.

Aliongeza kuwa ifikapo mwezi Julai mwaka huu, serikali itaanza kutekeleza Mpango Kazi wa Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara na Uwekezaji ambao tayari umefanyiwa maboresho na utekelezaji wake utaanza mapema mwaka ujao wa fedha wa 2019/ 2020.

Aidha waziri aliahidi kuendelea kusimamia maeneo muhimu ikiwemo ushiriki wa sekta binafsi katika maeneo ya uwekezaji na kueleza maboresho haya yatatekeleza hasa katika kuboresha mifumo na kuwa na maziringa mazuri yanayotabirika kwa wawekezaji.

“Kwa kutambua umuhimu wa Sekta binafsi, tutaendelea kusimamia ushiriki wao kikamilifu ili kuleta tija pasipo kubagua sekta hiyo na kuendelea kuwa na mifumo inayotabirika kwa ajili ya wawekezaji.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi alifafanua kuwa, jitihada za Serikali ni kuhakikisha kunakuwa na mahusiano mazuri ya kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili kwa kuzingatia zote zinategemeana katika masuala hayo ya uwekezaji.

“Kimsingi tunapaswa kuwa na uelewa wa pamoja kuwa, Tanzania na Marekani zinategemeana katika masuala haya ya uwekezaji kwani mnatuhijai na sisi tunawahitaji hivyo lazima tukae meza moja na kuyajenga endapo tunaona kuna maeneo ya kuboresha yenye tija ya kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo ni vyema tukayafanyia kazi pamoja”, Alisistiza Profesa Kabudi.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dkt. Inmi Patterson katika hotuba yake ya ufunguzi alieleza kuwa, majadiliano hayo ni mwanzo mzuri wa kuendelea kutekeleza mabadiliko ya kisera yatakayosaidia kuongeza uwazi na mazingira rafiki ya ufanyaji wa biashara nchini.

“Majadiliano ya leo ni mwanzo wa utekelezaji wa mabadiliko ya kisera yatakayoongeza uwazi na kuboresha mazingira ya kufanya biashara na tunaunga mkono jitihada hizi za Serikali ya Tanzania kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo sasa,”Alieleza Kaimu Balozi Patterson.

Aliongezea kuwa Serikali ya Marekani itaendelea kuunga mkono ushiriki wa sekta binafsi katika jitihada za maendeleo nchini humo kupitia ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma (Public private partnerships) ambao utaimarisha mazingira ya kibiashara na ubunifu ambao utanufaisha Wananchi wa Tanzania.

Aidha alieleza kuwa nchi yake imeendelea kuwa mstari wa mbele katika uwekezaji, kwa kuzingatia Takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Wafanyabiashara wa Kimarekani wamewekeza zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 4.7 nchini Tanzania na kuzalisha takriban nafasi za ajira 52,000 katika kipindi cha miaka 28 nchini kote Tanzania.

Serikali Yashauriwa Kuunganisha taasisi zote zenye majukumu yanayofanana ikiwa ni pamoja naTBS, OSHA na TFDA

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Kamati ya bunge ya bajeti imeishauri serikali kuhakikisha inaunganisha taasisi zote zenye majukumu yanayofanana ikiwa ni pamoja na TBS, OSHA, TFDA na Fire ili kuondoa kero na usumbufu kwa wafanyabiashara

Hayo yamesemwa  Juni 17,2019 bungeni jijini Dodoma na mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Bajeti George  Simbachawene  wakati akiwasilisha taarifa ya kamati ya bajeti kuhusu hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018 na mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20 pamoja na  tathmini ya utekelezaji wa bajeti ya serikali  kwa mwaka 2018/20 na mapendekezo ya mapato na matumizi ya serikali  kwa mwaka 2019/20.
 
Mhe.Simbachawene amesema ilikurahisisha utekelezaji katika maeneo mbalimbali ni vyema kuunganisha taasisi hizo ili kuondoa kero  na usumbufu unaojitokeza    pindi taasisi hizo zinapotembelea na kufanya ukaguzi  kwenye viwanda mbalimbali hapa nchini.
 
Aidha,Mhe.Simbachawene amesema pamoja na nchi yetu kuwa na Rasilimali kubwa ya mifugo  na samaki  bado haijaweza kunufaisha wananchi na taifa kwa ujumla hivyo ni wakati umefika kuacha kujipongeza kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo na badala yake kujielekeza kuongeza kasi ya kutumia Baraka hizo kwa kunufaisha watu wa Taifa la Tanzania Pamoja na kunufaisha sekta ya kilimo.

Kuhusu suala la Madini Mhe.Simbachawene amesema bado kuna tatizo kwa baadhi ya wafanyabiashara  kutorosha dhahabu kwenda nje ya nchi kwani kiwango cha kilo 600 za dhahabu  zilizouzwa katika soko la Geita  ni kidogo.

Wakichangia maoni juu ya taarifa ya bajeti kuu ya serikali baadhi  ya wabunge akiwemo mbunge wa Sumve Kwimba Richard Ndassa wamesema kuna haja kubwa  ya serikali kuangalia  upya sekta ya kilimo hususan Soko  ili kuinua wanyonge.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

BUNGE LIVE: : Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka Bungeni Dodoma

$
0
0
BUNGE LIVE: : Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka Bungeni Dodoma

Lori Lagonga treni Dodoma....Watu 29 Wajeruhiwa

$
0
0
Watu 29 wamejeruhiwa baada ya lori kugonga treni jijini Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Protas Katambi amesema leo asubuhi Jumanne Juni 18, 2019 kuwa ajali hiyo imetokea jana saa 5.30 usiku.

Amesema ametoa maagizo kwa vyombo vya usalama kumsaka dereva wa lori ambaye inasemekana aliruka kutoka kwenye lori baada ya ajali hiyo kisha kutokomea kusikojulikana.

Shughuli ya kuondoa mabehewa ya treni inaendelea huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika eneo la tukio huku polisi waliokuwa na silaha wakiwa wameimarisha ulinzi katika tukio.

Askari Atakayekamata Bodaboda Na Kupeleka Kituoni Nje Ya Makosa Matatu Yanayotambulika Kukiona Cha Moto.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,Kangi Lugola amewataka askari kote nchini kuacha tabia ya kukamata ovyo waendesha bodaboda na kuziweka kizuizini pikipiki zao katika vituo vya polisi bila sababu na makosa ya Msingi.
 
Waziri Lugola amesema hayo  Juni 17,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu  maswali mbalimbali ya  yaliyoelekezwa katika Wizara yake ambapo  wamedai pamekuwepo na changamoto ya baadhi ya askari wa vikosi vya usalama barabarani kuonekana kuwa kero kwa waendesha bodaboda kutokana na kukamata pikipiki  na kuziweka kizuizini kwa muda mrefu  licha ya makosa hayo kuwa na uwezekano wa kutatulika  kwa utaratibu maalum.
 
Akijibu Maswali hayo,Waziri Lugola amesema pikipiki inaweza ikakamatwa na kuwekwa kizuizini katika kituo cha polisi kwa makosa matatu  ambayo ni endapo imehusika kwenye uhalifu,imeokotwa  na haina mwenyewe  na sababu  ya tatu imesababisha ajali kinyume na hapo hairuhusiwi  kukamatwa na kupelekwa kituoni.
 
Aidha,Waziri Lugola amesema ajali za barabarani zimekuwa zikitokea mara kwa mara hapa nchini ,hivyo watanzania       wanatakiwa kufuatilia bima pindi wanapopata ajali.
 
Awali  akijibu Swali  la Msingi la Subira Mwaifunga,Mbunge wa viti Maalum,lililohoji juu ya tishio la ajali za barabarani,Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni  amesema   serikali ina mkakati madhubuti ya kupambana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja kuongeza wigo wa elimu kwa njia ya redio ,luninga na machapisho ya vipeperushi.

Mohammad Morsi azikwa kimya kimya Cairo, Misri

$
0
0
Rais wa zamani wa Misri Mohammed Morsi amezikwa leo, baada ya hapo jana kuanguka mahakamani na kuaga dunia. 

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yametaka kufanyika uchunguzi huru, kufahamu sababu halisi ya kifo chake.

Wakili wa rais huyo wa zamani amesema Morsi amezikwa leo asubuhi katika makaburi ya Medinat Nasr Mashariki mwa mji mkuu, familia yake ikiwepo. Televisheni ya taifa imesema kifo chake kilisababishwa na mshituko wa moyo.

Morsi, rais wa kwanza wa kiraia wa Misri, ambaye ni wa kwanza pia kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, alianguka katika kizimba chake mahakamani baada ya kujieleza, na aliwahishwa hospitalini ambako ilitangazwa kuwa alikuwa tayari amekata roho.

Tangu alipoangushwa katika mapinduzi ya kijeshi Julai 2013, aliyekuwa waziri wake wa ulinzi Abdel Fattah al-Sisi amechukua hatamu, na amefanya ukandamizaji mkubwa dhidi ya maelfu ya wanachama na wafuasi wa kundi la Udugu wa Kiislamu, mamia miongoni mwao wakikabiliwa na hukumu ya kifo.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Misri wamesema yumkini mazingira mabaya gerezani yamesababisha kifo cha Morsi, hali ambayo wanasema ni ukiukaji wa haki za binadamu. 

Marekani kutuma askari 1,000 Mashariki ya Kati kuikabili Iran

$
0
0
Serikali ya Marekani imesema itatuma askari 1,000 zaidi kwenye avikosi vyake vilivyopo Mashariki ya Kati kufuatia kushamiri kwa sintofahamu na taifa la Iran.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani, The Pentagon, imeeleza kwamba Ikulu ya Marekani na Kamati ya Wakuu wa Vikosi vya ulinzi na Usalama tayari imekwisha ridhia kupelekwa kwa askari wa majini, ardhini na anga watakao fikia 1,000 ili kuongeza nguvu zaidi kwa vikosi vilivyopo.

Kaimu Waziri wa Ulinzi Patrick Shanahan, amenukuliwa akisema kwamba nyongeza ya askari hao inafuatia kushamiri kwa vitendo vya chuki na uhasama vinavyo fanywa na serikali ya Iran hivyo kuhatarisha maslahi ya Marekani na Washirika wake Mashariki ya kati.

Pierre Liquid kuongozana na wabunge hadi Misri kuishangilia Taifa Stars

$
0
0
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema wabunge 48 watakwenda kuishangilia timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’  katika Fainali za Mataifa ya Afika (AFCON) zinazofanyika nchini Misri wakiambatana na Peter Mollel maarufu Pierre Konki Liquid.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Juni 18, 2019 Ndugai amesema wataambatana na mchekeshaji huyo katika fainali hizo huku akiwataka wabunge zaidi kujiandikisha ili kwenda Misri.

Katika fainali hizo zitakazoanza Juni 21 hadi Julai 19, 2019, Taifa Stars imepangwa kundi moja na Algeria, Senegal na Kenya.

Msafara wa wachezaji 32 wa Taifa Stars uliondoka nchini Juni 7, 2019  kwenda Cairo kuweka kambi ya maandalizi ya mwisho ya fainali hizo na tayari timu hiyo imeshacheza mechi mbili za kirafiki na Misri na Zimbabwe.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images