Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tanzania Yaungana Na Mataifa Mengine Barani Afrika Wanachama Wa Umoja Wa Afrika Kuadhimisha Wiki Ya Utumishi Wa Umma Kuanzia Leo Juni 16 Hadi 23-2019.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Tanzania inaungana na Mataifa mengine wanachama wa Umoja wa Afrika katika  kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma barani Afrika   ambayo yameanza leo Jumapili Mwezi Juni 16  ambapo kilele chake itakuwa Juni 23,jijini Nairobi nchini Kenya kwa Bara zima la Afrika. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi  wa Umma Kapt.George Mkuchika alisema katika wiki  ya utumishi wa Umma mwaka 2019,Ofisi yake imewalekeza watendaji wa taasisi za Umma kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma katika maeneo yao ya kazi  ili kusikiliza maoni na changamoto  wanazokutana nazo  katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na kukutana na wadau wa nje  kwa lengo la kupata mrejesho wa huduma wanazozitoa. 

Aidha,Waziri Kapt.Mkuchika alisema ili kujenga mahusiano mazuri na jamii ,Taasisi za umma zinaweza kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya shughuli za kijamii kama vile usafi wa Mazingira katika maeneo mbalimbali hususan hospitalini,sokoni na katika fukwe za mito na bahari zilizo jirani na maeneo yao ya kazi. 

Waziri Kapt.Mkuchika ameyataja baadhi ya Malengo ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika ni kutafakari juu ya wajibu ,dhima,dira,malengo ya utumishi wa umma ,mikakati,mchango na umuhimu wa watumishi wa umma,changamoto zao na kuhamasisha kuendelea kufanya kazi nzuri  katika ujenzi wa  Taifa pamoja na kupata mirejesho kutoka kwa wananchi na wadau wanaohudumiwa na taasisi za umma ili kurekebisha kasoro za utendaji zinazosababisha malalamiko ya wateja. 

Waziri Kapt.Mkuchika mara baada ya kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma ameziagiza Sekretarieti za mikoa ,Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zote za Umma kuwasilisha taarifa ya namna walivyoshiriki kwa makatibu wakuu wa Wizara zao  ambao wataunganisha taarifa zote  na kuziwasilisha kwa  katibu mkuu  ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili Serikali iweze kutumia taarifa hizo  kuboresha utendaji kazi. 

Kwa Mwaka 2019 Tanzania ni Kinara maadhimsho ya Wiki ya Utumishi wa Umma barani Afrika yatakayofanyika Nairobi Kenya kuanzia tarehe 21 hadi 23,2019  na shughuli zitakazofanyika ni pamoja na maonyesho ya shughuli za ubunifu  huku taasisi zitakazoshiriki  katika maadhimisho hayo ni zile huduma zake zinazolenga moja kwa moja kauli mbiu ya mwaka huu. 

Chimbuko la  maadhimisho ya  wiki ya utumishi wa Umma   ambayo huadhimishwa kila baada ya miaka miwili barani Afrika ni uamuzi wa mkutano wa Mawaziri  wenye dhamana ya utumishi ,uliofanyika Tangiers nchini Morocco mwaka 1994  ambapo ulizitaka nchi za Afrika kusherehekea kwa kauli mbiu moja katika bara zima la Afrika ambapo kwa kauli mbiu mwaka 2019 ni “Uhusiano kati ya Uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa Masuala ya Uhamiaji,Kujenga Utamaduni wa Utawala Bora ,Matumizi ya TEHAMA  na Ubunifu  katika utoaji Huduma Jumuishi.”
MWISHO.

Ripoti kifo cha Kabote, kutoroka kwa wafungwa zatua kwa Lugola

$
0
0
Na Veronica Mwafisi, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amepokea ripoti mbili za uchunguzi ikiwemo ya kifo chenye utata cha Isululu Kabote (85), mkazi wa Kijiji cha Buhungukila, Kata ya Bugarama, Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu. 

Kabote alidaiwa kuuawa akiwa mikononi mwa polisi Mei 17, mwaka huu, saa 8:00 usiku. Pia Lugola alipokea ripoti ya uchunguzi wa tukio la kutoroka mahabusu 17, Mei 21, mwaka huu, mkoani Geita. 

Mahabusu hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali na kuwekwa kwenye Ukumbi wa Jengo Jipya la mahakama wakisubiri kusomewa kesi zao. 

Ripoti ya uchunguzi wa kifo cha marehemu Kabote iliwasilishwa na Lalph Meela (Mwenyekiti), kutoka Dawati la Malalamiko Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Wajumbe ni Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Ibenze Ernest, Kefa Kaswamila kutoka Dawati la Malalamiko Kitengo cha Upelelezi Wizara ya Mambo ya Ndani na Mzee Mzee kutoka Ofisi ya Ofisa Usalama, Mkoa wa Simiyu. 

Kamati hiyo ilifanya uchunguzi huo kuanzia Juni 4-10, mwaka huu ambapo ripoti ya uchunguzi wa tukio la kutoroka wafungwa ilikabidhiwa na Mwenyekiti wake, Alex Mfungo. 

Baada ya kupokea ripoti hizo, Lugola alisema ameridhishwa na matokeo ya uchunguzi huo ambapo wajumbe wa kamati zote walipata fursa ya kuzichambua ripoti hizo sambamba na kutoa mapendekezo. 

Viongozi wengine waliokuwepo wakati Lugola akipokea ripoti hizo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. 

Kamati ya uchunguzi wa kifo cha Kabote iliundwa baada ya wananchi wa kijiji hicho kudai kabla ya kukumbwa na mauti, alikamatwa na polisi, kupigwa akidaiwa hajatoa mchango wa maendeleo sh. 50,000 madai ambayo Jeshi la Polisi liliyakanusha. 

Mmwili wa marehemu Kabote ulikaa siku 20 katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya uchunguzi wa kidaktari.
MWISHO.

Serikali Yasema Jukumu La Kulinda Watoto Ni La Wazazi Na Jamii Nzima

$
0
0
SALVATORY NTANDU
Serikali mkoani Shinyanga  imesema kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto unachangiwa na  wazazi/wazazi kutotimiza wajibu wao katika malezi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Kahama ANAMRING MACHA katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa afrika ambayo kimkoa imefanyika wilayani kahama na kusema kuwa wazazi wamejitoa katika malezi na kusababisha kuongezeka kwa matukio hayo.

Amesema Watoto wengi katika jamii wanakosa malezi kutokana kuwepo kwa dhana kuwa jukumu hilo lipo kwa serikali hali ambayo inasababisha watoto kukosa haki zao za msingi ikiwemo elimu,afya, chakula na malazi bora.

MACHA amefafanua kuwa Jukumu la kumlinda mtoto ni la mzazi/mlezi na jamii kwa ujumla hivyo ni budi wakatimiza wajibu wao ili kuhakikisha watoto wanatimiza malengo yao na kutokomeza vitendo vya ukatili kwa kundi hilo muhimu.

Sanjari na hilo             macha amesema  kuwa, wazazi wamekuwa chanzo cha kuwakwamisha watoto wao katika kutimiza ndoto zao hasa wanafunzi wakike kwa kuwaozesha wakiwa na mri mdogo ambao anahitajika kuwa shuleni nakuongeza serikali haitavumilia vitendo hivyoa ambavyo vimekuwa vinafanywa na wazazi wasiowadilifu.

Nae        Mwenyekiti wa baraza la watoto Mkoa Shinyanga VICTORY CHACHA Wakati akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wa mkoani humo amesema kuwa,upungufu wa walimu wa masomo ya hesabu na sayansi ndio imekuwa chanzo cha kushusha ufaulu wa wanafunzi.

Amefafanua kuwa  kuwa,wazazi na walezi wamekuwa na tabia ya kuwafungia watoto kike na wakiume walemavu na kuwanyima frusa ya kusoma kwa kuwa na imani potofu kuwa watachekwa kwenye jamii,nakuomba serikali kuliingilia jambo hilo kati ili kila mmoja awe kupata elimu bila kujali matabaka.

Mwisho

Waziri Mkuu Awashauri Watanzania Kujiwekea Akiba Kupitia Hisa

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ni wakati muafaka kwa Watanzania kuanza kujiwekea akiba kwa kununua hisa kupitia taasisi za kifedha nchini ikiwemo benki ya CRDB.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Juni 16, 2019) wakati wa bonanza kati ya Wabunge na watumishi wa benki ya CRDB lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema suala la wananchi kujiwekea akiba ni muhimu kwa ajili ya maendeleo yao. "Nashauri wananchi tutumie taasisi za fedha kujiwekea akiba pamoja na kukopa mikopo kwa ajili ya maendeleo yetu."

Akizungumzia kuhusu bonanza hilo lililoandaliwa na benki ya CRDB, Waziri Mkuu amesema michezo ni sehemu nzuri kujenga afya, furaha na kujenga mshikamano wa karibu baina ya benki hiyo na wananchi ambao ni wateja.

Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu ambapo timu ya CRDB ilishinda baada ya kuifunga timu ya Bunge penati tatu kwa moja na kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuibugiza CRDB magoli 35 kwa mawili.

Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za CRDB. Upande wa mchezo wa basketball timu ya Bunge ilishinda vikapu 53 kwa 51.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Kigwangallah Atoa Shukran Kwa Madaktari na Wauguzi Baada ya Kunusurika Kufa Ajalini

$
0
0
WMU – Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amewashukuru Madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ya jijini Arusha kwa huduma na matibabu waliyoyatoa kwake na kwa wasaidizi wake alipopata ajali mbaya ya gari Agosti 4, 2018 katika eneo la Magugu mkoani  Manyara.  

Dk. Kigwangalla ametoa shukrani hizo wakati akizungumza na Madaktari, Wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre, jijini Arusha.

Akiwa ameambatana na mkewe Dk. Bayoum Awadh, amewashukuru na kuwapongeza madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo kwa matibabu waliyompatia kwa kipindi chote alichokuwa hospitalini hapo na kuwaomba waendelee kuwahudumia wananchi wenye shida.

Amesema kazi ya udaktari, uuguzi na fani zote zilizo katika sekta ya afya ni za wito na kila anayezifanya inampasa azifanye kwa wito kutoka ndani ya moyo wake.

“Kazi ya udaktari, uuguzi na fani zote zilizo katika sekta ya afya kwa kiasi kikubwa ni kazi ambazo mtu anazifanya kutoka ndani ya moyo wake kuwahudumia wengine ambao wako katika madhira mbalimbali ya kiafya” Amesema Dkt. Kigwangalla.

 Amesisitiza kuwa hakuna namna ambayo Daktari au Muuguzi anayetoa huduma ya kumtibu mtu, kumwondolea maumivu, au kumpa faraja mgonjwa anaweza kulipwa na malipo hayo yakalingana na kazi aliyoifanya.

Amesema kazi ya Udaktari na Uuguzi inafanywa na watu wachache ambao kwa kiasi kikubwa wanakua wameitika wito ama wametumwa na Mungu na kwamba mtu yeyote hawezi kusema kuna kipato au kitu utakachoweza kumlipwa kikamtosheleza au kukidhi umuhimu na ugumu wa kazi anayoifanya.

“Kwa dhati ya moyo wangu ninatoa shukrani zangu za dhati lakini pia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye kwa muda wote toka tulipopata ajali alikua akifuatilia afya zetu, ninaomba nifikishe kwenu shukrani za Serikali anayoiongoza ya kwamba tunatambua mchango wenu mkubwa” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla

Ameeleza kuwa yeye na wasaidizi wake waliopata ajali Agosti 4, 2018 walipita katika hospitali hiyo wakiwa na hali ngumu kiafya lakini kutokana na juhudi na upendo uliooneshwa na madaktari wa hospitali hiyo wakishirikiana na madaktari wa hospitali ya mkoa wa Arusha na KCMC waliweza kushughulika afya zao na kuokoa maisha yao.

 “Tunawashukuru sana kwa yote mliyotenda, tunawaombea dua madaktari, wauguzi na watumishi wa kada zote zilizo katika sekta hii ya tiba hatuna cha kuwalipa zaidi ya kusema Mungu awabariki katika maisha yenu, awape mafanikio makubwa na ujuzi zaidi ili muendelee kuwasaidia wengine” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya magonjwa ya dharura cha Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC), Dk. Peter Mabula akizungumza kwa niaba ya uongozi wa hospitali hiyo amesema kuwa kitendo cha Dkt. Kigwangalla kupanga muda wa kwenda kuwashukuru kimewapa nguvu na moyo wa kuendelea kufanya kazi vizuri zaidi.

Dk. Mabula amemwomba Mhe. Kigwangalla atenge muda mwingine wa kuitembelea hospitali hiyo pia afikishe salam zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwamba wataendelea kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu June 17

Kamishna wa Uhamiaji afanya mabadiliko kwa Maafisa wa Mikoa

Taarifa kutoka nchini Kenya kuhusu mwanamke aliyeonesha dalili za ugonjwa wa Ebola

$
0
0
Imeripotiwa kuwa mtu mmoja nchini Kenya amepatwa na ugonjwa wa Ebola na tayari amelazwa katika Hospitali ya Kericho,nchini humo.

Taarifa za awali kutoka kwa Maafisa wa afya katika Kaunti ya Kericho wamesema kuwa, Mgonjwa huyo siku chache zilizopita alisafiri kutoka Malaba eneo la mpaka kati ya Kenya na Uganda.

Tayari Sampuli za damu za mgonjwa huyo zimechukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya uchunguzi zaidi, kujua kama kweli ameathirika na virusi vya Ebola.

Kwa upande mwingine, Idara ya huduma za afya na serikali ya kaunti ya Kericho imesema inafuatilia kwa karibu suala hili na kuwahakikishia wananchi kuwa hatua madhubuti zinafuatwa kuhakikisha usalama wa kiafya kwa wengine.

Hili linakuwa ni tukio la pili kwa nchi za Afrika Mashariki kukumbwa na kisa cha mgonjwa wa Ebola, Baada ya wiki iliyopita kupatikana kwa mgonjwa mmoja nchini Uganda.

Omar al-Bashir aonekana mara ya kwanza baada ya mapinduzi ya kijeshi

$
0
0
Aliyekuwa Rais wa Sudan, Omar al-Bashir amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa kwake madarakani mwezi Aprili.

Bwana Bashir alikuwa akitolewa gerezani katika mji mkuu, Khartoum kwenda kwenye Ofisi ya mwendesha mashtaka ambaye alimsomea mashtaka ya rushwa yanayomkabili

Akiwa amezungukwa na askari wa usalama, Kiongozi huyo wa zamani mwenye miaka 75 alikua amevaa vazi lake jeupe na kilemba.

Bwana Bashir alipinduliwa madarakani baada ya miezi kadhaa ya maandamano nchini humo.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa maburungutu ya fedha za kigeni yalikutwa kwenye magunia nyumbani mwake baada ya kuondolewa madarakani alikohudumu kwa takribani miaka 30.

Bashir alionekana akishuka kwenye gari kuingia kwenye ofisi ya mwendesha mashtaka, akitabasamu na kuzungumza na walinzi, lakini baadae alirejea akiwa na uso usio na furaha, Shirika la Reuters limeeleza.

Bwana Bashir pia anatakiwa na mahakama ya kimataifa, ICC, akishutumiwa kuongoza vitendo vya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu katika eneo la Darfur, shutuma ambazo amezikana.

Naibu Waziri wa Ardh, Angeline Mabula agiza mkataba nyumba 4,000 Dar upitiwe upya

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula, ameagiza kupitiwa upya mkataba wa mauziano ya nyumba 4,000 kati ya Kampuni ya PMM 2001 Ltd na wakazi wa Vingunguti, Dar es Salaam.

Uamuzi huo unafuatia kutozingatiwa kwa masharti ya mkataba ulioingiwa awali, ambao umeonekana kuwa na upungufu wa kisheria na hivyo kusababisha PMM 2001 Ltd kushindwa kuwalipa wamiliki wa nyumba katika eneo la Vingunguti kwa karibu miezi tisa kama walivyokubaliana jambo lililozua taharuki.

Dk. Mabula alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki, baada ya kukutana na pande zote mbili za kamati inayosimamia makubaliano ya uuzaji nyumba 4,000 katika mitaa minne ya Vingunguti ambayo ni Mnyamani, Mtambani, Mtakuja na Faru, Kampuni ya PMM 2001 Ltd na Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli katika ofisi za wizara hiyo, jijini hapa.

Alisema baada ya kupitia mkataba wa mauziano ya nyumba katika eneo la Vingunguti, kati ya PMM 2001 Ltd na wamiliki wa nyumba, wamebaini kutofuata taratibu za kisheria na kubainisha kuwa wamiliki ambao hawajalipwa fedha yoyote hawabanwi na mkataba huo na wanaweza kuzifanyia shughuli yoyote nyumba zao.

DNA yatatua kitendawili cha mapacha wawili Melon na Sharon

$
0
0
Majibu ya vipimo vya vinasaba (DNA) vimetatua kitendawili kikubwa ambacho wengi walikuwa wakisubiri jibu lake, la iwapo mabinti wawili Melon na Sharon kutoka Kakamega nchini kenya, ni mapacha ama la

Majibu ya vipimo hivyo yamethibitisha kuwa Sharon Mitekwa na Melon Lutenyo walizaliwa na mama mmoja, ambaye ni Bi Rosemary Khaveleli.

Matokeo hayo pia yameonesha kuwa msichana Mevis Imbaya aliyekuwa akiishi na Melon kama pacha mwenzake, si dada yao halisi, na Bi Angeline Omina, aliyekuwa akiishi na Sharon kama mama yake mzazi katika mtaa wa Kangemi, Kaunti ya Nairobi ndiye mama mzazi wa Mevis.

Uchunguzi huo uliendeshwa na Dkt Ahmed Kalebi kutoka maabara ya Lancet, juu ya  mapacha ambao walitenganishwa katika hali tatanishi mnamo 1999, mara tu baada ya kuzaliwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kakamega, na kuonesha kuwa chembechembe zao za DNA zinalingana kwa asilimia 100, hali inayothibitisha kuwa ni pacha halisi.

Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza mnamo Aprili kupitia mtandao wa Facebook miaka 19 baada ya kuishi katika makazi na maisha tofauti, baada ya pacha mmoja kuona mtu aliyefanana naye kwa kila kitu na kuamua kumuomba urafiki, na ndipo alipobaini kuwa anafanana na si kwa bahati mbaya bali kuna kitu zaidi na kuanza kufuatilia, ndipo ikagundulika walizaliwa siku moja na hospitali moja.

Walijikuta wakilelewa na mama tofauti, jamboa mbalo mpaka sasa halijajulikana kilichotokea mpaka watoto hao kubadilishiwa wazazi, na kulelewa na watu ambao si wazazi halisi.

Mahakama Yaamuru Wema Sepetu Aende Gerezani Siku 7

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemuamuru Msanii Wema Sepetu kwenda gerezani siku saba mpaka Juni 24  akisubiria uamuzi wa mahakama wa kumfutia dhamana. 

Nyota huyo wa filamu anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono mitandaoni kupitia simu yake ya kiganjani.

Uamuzi huo wa Mahakama umefikiwa leo Juni 17,  mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wakati mshtakiwa huyo alipofikishwa mbele yake.

Wakili wa Serikali Glory Mwenda amedai mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa hapo baada ya mahakama wiki iliyopita kutoa hati  ya kumkamata Wema kwa kosa la kuruka dhamana.

Hakimu Kasonde alimtaka Wema kujieleza kwanini asifutiwe dhamana kwa kushindwa kufika mahakamani kwa tarehe mbili tofauti.

Akijieleza Wema alidai Mei 14 mwaka huu hakufika sababu alikuwa safarini mkoani  Morogoro na Juni 11 mwaka huu aliumwa akashindwa kupandisha mahakamani.

Mshtakiwa aliomba msamaha na Wakili wa Serikali, Mwenda aliomba Mahakama impe onyo mshtakiwa ili asirudie kufanya kitendo hicho chenye usumbufu.

Hakimu Maira alisema kasikia hoja zilizowasilishwa na atapitia kiapo cha mshtakiwa kisha atatoa uamuzi Juni 24 mwaka huu na akaamuru katika kipindi cha kusubiri uamuzi mshtakiwa akae rumande.

Wema anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa hazina maudhui.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Watuhumiwa1842 wa Madawa ya Kulevya Watiwa Mbaroni

$
0
0
  Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mpaka kufikia  mwezi januari 2019 hadi  machi 2019 jumla ya makosa  113  dawa za kulevya yaliripotiwa  hapa nchini na watuhumiwa 1,842 wa makosa ya dawa za mirungi na bangi..  . 

Hayo yamesemwa leo Juni 17,2019 bungeni jijini  Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa viti Maalum ,Zainabu Katimba aliyehoji serikali ya    awamu ya tano tangu iingie Madarakani  imebaini na kuwachunguza watu wangapi wanaojihusisha na mtandao wa dawa za kuleya. 

Katika majibu yake Yake,Mhandisi Masauni amesema tokea serikali ya awamu ya tano iingie Madarakani  imewabaini  makosa 679  na kuwakamata watuhumiwa  1,269 kwa mwaka 2016,Makosa 902, na watuhumiwa 1,578  mwaka 2017,Makosa 702 na watuhumiwa 886 kwa mwaka 2018 ,makosa 113 na watuhumiwa 1,842  kwa mwaka 2019. 

Aidha,Mhandisi Masauni  amesema madawa mashambani Mirungi na bangi yaliyokamatwa kwa mwaka 2016 ni  jumla ya makosa 10,375 na  watuhumiwa 26,031,makosa  8,956 na watuhumiwa 12,529 kwa mwaka 2017,makosa  7,539  na watuhumiwa 9,987 kwa mwaka 2018. 

Baadhi ya watuhumiwa  wamepelekwa mahakamani na wengine upelelezi wa Mashauri yao unaendelea huku Jeshi la polisi kupitia Programu ya kuzuia uhalifu limeendelea kutoa huduma ya urekebishaji kwa waathirika wa dawa za kulevya.
 
Kwa upande wake Waziri wa Ofisi ya Waziri mkuu ,vijana,ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amesema ofisi ya Waziri mkuu imefanikiwa kudhibiti dawa za kulevya kwa asilimia 95%  huku waathirika wote wa dawa za kulevya  wakipewa elimu pamoja na kufanya kazi ili kurejea katika hali yao ya kawaida.

Serikali Yaipatia Tume Ya Madini Na Kampuni Ya Huduma Za Meli Shi. Bil. 17 Kuboresha Mapato

$
0
0
Na Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali, kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, imetoa Sh. billion 10.7, kwa Tume ya Madini nchini na Sh. billion 5.9, kwa Kampuni ya Huduma za Meli (Marine Service Company Limited -MSCL) kwa ajili ya kutekeleza Miradi  ya kimkakati, yenye lengo kuongeza mapato yanayotokana na madini pamoja na kuiwezesha Kampuni ya Huduma za Meli kujiendesha kibiashara.

Hafla ya utiaji saini mikataba ya fedha hizo umefanyika Jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Doto James na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamriho.

Bw. James alisema kuwa  Sekta ya Madini na Kampuni ya Huduma za Meli,  wajifunze kupitia miradi mingine ya kimkakati katika Halmashauri zilizopewa fedha, ili kuepuka changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwa baadhi ya Halmashauri kushindwa kufikia malengo.

“Fedha hizi sio za bure tutazifuatilia mpaka shilingi ya mwisho, ili kupata mrejesho wa kuchangia maduhuli katika Mfuko Mkuu wa Serikali, hivyo fedha hizo  zinatakiwa kutumika kwa ufanisi  kwa lengo lililo kusudiwa”, alisisitiza Bw. James.

Alisema Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imeunda kikosi kazi maalum ambacho kitakuwa kinafuatilia maendeleo ya miradi hiyo na kutoa taarifa Serikalini.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Pro. Simon Msanjila aliishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha hizo na kuahidi kuwa watazitendea haki na kuongeza mapato ya Serikali.

"Tumepewa lengo la kukusanya maduhuli ya kiasi cha shilingi bilioni 475 katika mwaka huu wa fedha 2018/2019, nina kuhakikishia kuwa lengo hili tutalifikia kwasababu ya uwezeshaji huu wa Serikali na mwitikio mzuri wa wadau wa sekta ya madini katika kulipa kodi kwa hiari" alisema Prof. Msanjila

Alisema kuwa Sekta ya madini ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi, uwezeshaji huo utawezesha kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiikumba Tume ya Madini kwa lengo la kuongeza ukusanyaji wa mapato yanayotokana na madini.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula, alisema kuwa uwezeshaji huo utaiwezesha Tume hiyo kufikia lengo na kuahidi kuendelea na juhudi za kuhakikisha maduka ya madini nchini yanaboreshwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamriho, aliishukuru Serikali kwa kuipatia Kampuni ya Meli nchini (MSCL) kiasi cha shilingi bilioni 5.9 zitakazotumika kukarabati baadhi ya meli  zilizopo pamoja na kuweka mifumo ya kieletroniki ya kukusanya maduhuli ya Serikali.

Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Bw. Eric Hamissi, aliahidi Serikali kuwa hawatoiangusha na kubainisha kuwa kampuni hiyo ni ya kimkakati na inaweza kuchangia uchumi wa nchi.

Mwisho.

Watumishi wanaotarajia kustaafu waaswa kuzingatia mabadiliko ya maisha

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
 Watumishi wanaotarajia kustaafu wameaswa kuzingatia mabadiliko ya maisha kutoka katika utumishi wa umma kwenda katika mfumo wa maisha ya  kawaida na kujiepusha kufanya miradi ambayo hawana ujuzi wa kutosha kuihusu. 

 Akizungumza katika mafunzo kwa yakuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni ili wawe na mbinu za kuendana na mazingira hayo, Katibu Mkuuu wa Ofisi hiyo anayeshughulikia (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Doroth Mwaluko amesem kuwa Ofisi hiyo inatambua umuhimu wa wastaafu na faida za kujiandaa kustaafu. 

“ Kuna umuhimu mkubwa wa kutambua kuwa suala la kustaafu ni la kila mmoa wetu na ni muhimu kujiandaa vyema na maisha mapya ambayo kimsingi yatakuwa tofauti na haya ya utumishi wa umma mliyo nayo  kwa sasa” Alisisitiza Mwaluko 

Akifafanua amesema kuwa kila mtumishi wa umma lazima atambue kuwa ni mstaafu matarajiwa hivyo kujiandaa kwake ni jambo  muhimu. 

Kwa upande wake Muwezeshaji Kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni Jijini Dar es Salaam Bw. Peter Seme amesema kuwa watumishi hao wanaotarajia kustaafu watajifunza mambo mengi yakuwawzesha kuendelea na maisha yao kama kawaidia hata baada ya kustaafu. 

Alitaja baadhi ya mada kuwa ni pamoja na utayari wa kupokea mabadiliko baada ya kustaafu, Stadi za kuongeza kipato, Mtindo wa maisha bora baada ya kustaafu, Namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu. 

Kwa upande wake mmoja wa watumishi hao  Bw. Esamo Sawaki amesema kuwa  wanaipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa mafunzo hayo kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi hiyo ili waweze kukabiliana na changamaoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu. 

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kupata uzoefu kutoka kwa wastaafu wengine ambao tayari wana uzoefu katika kukabiliana na changamoto za kustaafu na hata kuelewa kazi ambazo ni za uzalishaji wanazoweza kuzifanya kama wastaafu ili kuwaletea tija. 

“Tutapata maarifa sahihi ya namna ya kutumia kiinua mgongo tutakachopewa baada ya kustaafu kutoka katika utumishi wa umma” Alisisitiza  Sawaki 

Mafunzo yakuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni yanafanyika Jijini Dodoma kwa siku tano yakiwashirikisha watumishi hao kutoka kada mbalimbali.

Taasisi Za Kidini Na Jumuiya Za Kijamii Kuhakikiwa Kuanzia Juni 23 Hadi Julai 02, 2019

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MOHA
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini, itaanza kufanya uhakiki wa jumuiya na taasisi hizo kuanzia Juni 23 hadi Julai 2, mwaka huu. 

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, alisema uhakiki huo awamu ya pili utaanza Juni 23 hadi Julai 2, katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida na Manyara. 

Meja Jenerali Kingu alisema uhakiki utafanyika kwenye Kituo cha Uhakiki cha iliyokuwa ofisi ya zamani ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 10 jioni. 

Alisema wakati wa uhakiki, jumuiya na taasisi zinapaswa kuwasilisha nyaraka mbalimbali kikiwemo cheti cha usajili na kivuli cha cheti hicho, stakabadhi ya mwisho ya malipo ya ada iliyolipwa hivi karibuni pamoja na katika ya jumuiya, taasisi husika iliyopitishwa na Msajili. 

Nyaraka nyingine nib aria inayothibitisha uwepowa jumuiya, taasisi husika kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa, kata mahali ilipo ofisi ya jumuiya ama taasisi, taarifa za Mkutano Mkuu wa Mwaka pamoja na taarifa ya fedha ya mwaka . 

“Fumu ya uhakiki inapatikana kwenye tovuti ya Wizara sambamba na kwenye kituo cha uhakiki, taasisi ambazo zitashindwa kuhakikiwa kwa mujibu wa ratiba ya eneo husika zitalazimika kwenda Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma ili kuhakikiwa. 

“Na kama zitashindwa kufanya uhakiki kwa muda uliopangwa zitaondolewa kwenye orodha ya Msajili, pia taasisi na jumuiya ambazo hazijasajiliwa zinatakiwa kufika wakati wa uhakiki ili kupewa utaratibu wa kupata usajili,” alisema Meja Jenerali Kingu. 

Alifafanua kuwa, malipo ya ada yatafanyika wakati wa uhakiki kupitia mfumo wa malipo ya Serikali kwa njia ya kielektroniki (Governmment Electronic Payment Gateway System).
MWISHO.
 

Mwigulu Nchemba ataka Staili yake ya Kuvaa Skafu Shingoni itambuliwe kama vazi rasmi la Taifa

$
0
0
Mbunge wa Iramba Magharibi Dr. Mwigulu Nchemba amependekeza kuwa mtindo wa mavazi ambao yeye amekuwa akiuvaa mara kwa mara utumike kama vazi la taifa kwa kile alichokieleza umekuwa ukiwatambulisha watanzania hasa wanapokuwa nje ya nchi.

Dr. Mwigulu ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo juu ya vazi rasmi la taifa.

Mwigului Nchemba ameuliza kuwa "watanzania wakienda nje ya nchi wanatumia skafu, tai bendera ya taifa yani Mwigulu style na wanatambuliwa ni Watanzania, kwanini Serikali isiseme hili ndilo vazi la taifa?.

Akijibu swali hiyo, Naibu Waziri Juliana Shonza amesema kwa sasa mchakato wa kulipata vazi la taifa ulishaanza upya hivyo watahakikisha wanapokea maoni ya watu mbalimbali.

"Kwa sababu mchakato umeshaanza, nimwambie tu maoni ambayo ameyatoa tunayachukua na tutayafanyia kazi", amesema shonza.

Waziri Mwakyembe Azindua Kampeni ya Kuichangia Timu Ya Taifa “Taifa Stars”

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua rasmi kampeni maalumu ya kuchangia timu ya Taifa “Taifa Stars” inayoshiriki mashindano ya Kombe la Maifa ya Afrika (AFCON) yanayotarajiwa kuanza Juni 21 nchini Misri.

Waziri Mwakyembe amesema watanzania hawana budi kuchangia kiwango chochote na kwamba fedha hiyo itakuwa salama na itawafikia wachezaji hao bila ya mizengwe yoyote.

"Watanzania kote nchini wanaweza kuichangia timu yao  kupitia akaunti zifuatazo BMT N BC 011101000978, Sport Development Fund, CRDB 01J1019956700 na Voda *150*00#5595298. Ukichangia, ujumbe unaopata utume  kwenda 0735 414043 jina litakuja Oscar Zabloni ambye ni mweka hazina ,'' amesema Dkt. Mwakyembe.

Amesema wote watakaochangia watapewa cheti  maalumu na  kiongozi wa kitaifa ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika kuhakikisha timu yetu ya Taifa inafanya vizuri katika mashindano hayo.

Naye mwenyekiti wa kamati ya kusaidia Taifa Stars, Paul Makonda amesema siku ya Jumamosi Juni 22, 2019 mkoa wa Dar es Salaam utafanya maombi maalum kwa ajili ya  kuiombea timu ya Taifa Stars ambayo inatarajia kushuka dimbani siku ya Jumapili Juni 22 dhidi ya timu ya Taifa ya Senegal.

Pamoja na mambo mengine Makonda amezitaka kampuni 41 zilizoahidi kuchangia Taifa Stars kutoa michango hiyo.

"Jumamosi ya Juni 22,2019 Mkoa wa Dar es Salaam tutafanya maombi maalum kuiombea timu ya Taifa Stars, na pia nitumie nafasi hii  kuyakumbusha  makampuni  yaliyoahidi kuichangia Taifa Stars sasa wachangie kupitia akaunti hizo,'' amesema Makonda.

Timu ya Taifa Stars iko kundi C, pamoja na timu za Senegal, Algeria na Kenya ambapo siku ya Jumapili inatarajia kutupa karata yake ya kwanza dhidi Senegal.

Tayari Stars imeshacheza mechi mbili za kirafiki za kujipima nguvu, huku ikipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Misri 1-0 na kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Zimbabwe.

Rais Magufuli Atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala ya Nishati ya Umeme Vijijini (REA)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala ya Nishati ya Umeme Vijijini (REA), Michael Pius Nyagoga.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,  Ikulu Gerson Msigwa, utenguzi huo umeanza leo Juni 17, 2019.

Aidha kutokana na uamuzi huo, Rais Magufuli amemteua Wakili Julius B. Kalolo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala ya Nishati ya Umeme Vijijini (REA), kuanzia leo Juni 17, 2019.

 
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>