Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Muhimbili Kuanza Kutibu Uvimbe Kwenye Kizazi Bila Kufanya Upasuaji

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanzisha huduma mpya ya kutibu uvimbe kwenye kizazi (uterine fibroids) kwa kutumia njia ya kisasa yaTiba Radiolojia (interventional radiology).

Pia, MNH imeanzisha huduma mpya nyingine ya kuweka mipira maalum kwenye mshipa mkubwa wa damu (permanent catheter insertions) kwa wagonjwa wa figo ambao wapo kwenye mfumo wa kusafisha damu (renal dialysis) au kwa wagonjwa wanaopatiwa tiba ya saratani.

Wataalam wa MNH kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Yale na vyuo shiriki (kama Emory, Dartmouth) vya nchini Marekani wako kwenye programu maalum ya mafunzo ya tiba Radiolojia tangu Octoba mwaka 2018 hospitalini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia wa MNH, Dkt. Flora Lwakatare amesema mgonjwa mwenye uvimbe kwenye kizazi anaingiziwa mpira wenye chembechembe maalum kwenye mishipa ya damu na kwenda kuziba mishipa inayopeleka damu kwenye uvimbe.

“Baada ya mishipa kuziba uvimbe unakosa damu au chakula chake na hivyo kusinyaa na kufa kabisa. Hivyo basi mama mwenye uvimbe kwenye kizazi endapo anapatiwa tiba hii hakuna haja ya kumfanyia upasuaji kubwa wa kuondoa uvimbe,” amesema Dkt. Lwakatare.

Dkt Lwakatare amesema faida ya kutumia njia hii ya kisasa, inamsaidia mgonjwa kutofanyiwa upasuaji mkubwa na pia inampunguzia gharama za matibabu na kuondoa hatari yoyote kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji mkubwa.

Akizungumzia huduma nyingine ya kuweka mipira maalum kwenye mshipa mkubwa wa damu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na figo, Dkt Lwakatare amesema huduma hii inawanufaisha wagonjwa wa figo ambao wako kwenye mfumo wa kusafisha damu (renal dialysis) au wanaopatiwa tiba ya saratani.

Amesema tiba hii inaondoa usumbufu wa kutumia mishipa midogo ya mikononi ambayo mara nyingi ni ngumu kupatikana hasa kama inatumika mara kwa mara na kwa muda mrefu.

“Tiba hii inafaida kubwa kwa kuwa inawezesha kuepeuka upasuaji mkubwa ambao una vihatarishi (risk), kuepeuka mgonjwa kukaa hopsitali kwa muda mrefu na wanaofanyiwa tiba radiolojia mara nyingi wanaweza kurudi nyumbani siku hiyo hiyo, hivyo inapunguza gharama kwa mgonjwa na Hospitali kwa ujumla,” amesema.

Hivyo kujengewa uwezo kwa watalaam wa ndani itasadia kwa kiwango kikubwa kukuza huduma hii hapa nchini ambapo watalaam kutoka Hospitali za hapa nchini watapata fursa ya kujifunza kwa gharama nafuu na kuongeza idadi ya watoa huduma mikoani.

Naye Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory nchini Marekani, Dkt. Janice Newsome amesema tiba radiolojia inahitaji ubunifu na kutoa huduma kwa kushirikiana. Dkt. Janice Newsome amesema wametoa mafunzo ya kutoa huduma ya tiba radiolojia kwa wataalam wa MNH na kwamba wao wamejifunza mambo mbalimbali kupitia wataalam wetu.

“Kuwekeza kwa wataalam ni jambo muhimu na zuri kwa kuwa kazi ya kutoa huduma inahitaji kushirikiana,” amesema Dkt. Newsome. Katika mafunzo haya ya awamu ya nne, wataalam 13 wa MNH wakiwamo madaktari, wauguzi na mafundi sanifu wamepatiwa mafunzo sambamba na kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa mbalimbali.

Mafunzo na huduma za tiba radiolojia zinazotolewa MNH ni mfululizo wa programu mbalimbali za tiba radiolojia yayolianza Novemba 2017 ili kujenga uwezo kwa wataalam wa MNH. Tangu kuanzishwa kwa huduma hii, wagonjwa 339 wamepatiwa huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia na wengi ni wagonjwa wenye uvimbe kinywani.

Tanzania Yapata Heshima Nyingine Kimataifa.....Dkt. Kijazi Ashinda Kwa Kishindo Nafasi Ya Umakamu Wa Tatu Wa Rais Wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)

$
0
0
Na: Monica Mutoni. Geneva
Kwa mara nyingine Tanzania imeingia katika historia ya kimataifa kwa Mkurugennzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na mwakilishi wa kudumu Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kuibuka mshindi wa nafasi ya umakamu wa tatu wa Rais wa WMO. Dkt. Kijazi anachukua nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2019-2022 akiwa mwanamke wa kwanza na mjumbe wa kwanza kutoka nchi zinazoendelea kushika nafasi hiyo. Dkt. Kijazi atakuwa na majukumu makubwa ya kumsaidia Rais kuongoza shirika hilo katika kutekeleza majukumu yenye tija kwa wanachama wake ikiwemo Tanzania

Akizungumzia ushindi wake mbele ya wapiga kura wa mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na wajumbe waalikwa, Dkt. Kijazi alitoa shukrani zake za dhati kwa wote waliomwamini na kumuunga mkono hadi kufika kupata nafasi hiyo na kuahidi kuitumika nafasi hiyo kwa weledi wa hali ya juu ili kufikia malengo ya shirika hilo.

‘ Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote waliokuwa pamoja na mimi kwa kuniunga mkono na kunichagua kwa kura zote, naahidi kuitumikia nafasi hii kwa weledi mkubwa na kuhakikisha WMO inafikia malengo yake’. Alisema Dkt Kijazi

Akizungumzia ushundi huo, Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Atashasta Nditiye alisema ni heshima kubwa sana kwa nchi, Wizara inampongeza sana Dkt. Kijazi na kuamini kuwa ataiwakilisha nchi vizuri, aidha alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano aliouonesha kwa kukubali Tanzania kuwakilishwa na Dkt. Kijazi ambapo kwa jitihada zake katika kuboresha sekta ya hali ya hewa kumeendelea kuiletea sifa nchi kwa ujumla

Kwa upande wa Kaimu Balozi, Ubalozi wa Kuduma Umoja wa Mataifa, Geneva Ndugu. Robert Kahendaguza alisema kuwa ushindi wa Dkt. Kijazi ni kielelezo cha umadhubuti wa kidiplomasia ya Tanzania na sifa zake binafsi ikiwemo uzoefu wa muda mrefu na elimu ya ngazi ya juu katika nyanja ya sayansi ya hali ya hewa, aidha aliongeza kuwa sababu za sifa hizo ziliupunguzia ubalozi kazi ya kumnadi na hata kuwa rahisi kuishawishi nchi ya Sudan kuondoa mgombea wao na hivyo kumfanya Dkt. Kijazi kuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo.

Uchaguzi wa viongozi wa WMO hufanyika kila baada ya miaka minne kwa kuchagua viongozi mbali mbali wakiwemo Katibu Mkuu, Rais, Makamu wa Rais wa kwanza, wapili na watatu, ambapo kwa mwaka huu umefanyika katika mkutano wa 18 wa shirika hilo baada ya muda wa viongozi hao kuisha. Uchaguzi huo ulifanyika kwa haki na kwa mani na kuwapata viongozi hao ambao ni Prof. Petteri Taalas kutoka Finland (Katibu Mkuu), Prof. Dk. Gerhard Adrian kutoka Ujerumani (Rais), Prof. Celeste Saulo kutoka Argentina (Makamu wa kwanza wa Rais), Dr. Albert Martis kutoka Curacao (Makamu wa Pili wa Rais) na Dkt. Agnes Kijazi kutoka Tanzania (makamu wa tatu wa Rais).

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya June 15

Timu Ya Wizara Ya Kilimo Yawasili Kanda Ya Ziwa Kubaini Changamoto Za Zao La Pamba

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo - Simiyu
Uongozi wa Wizara ya Kilimo umewasili katika mikoa ya Kanda ya ziwa ili kubaini changamoto zinazowakabili wakulima wa zao la Pamba na kuzitafutia ufumbuzi.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameongoza timu hiyo ambapo amezuru katika mikoa ya Tabora na Simiyu kwenye Wilaya za Igunga na Meatu.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) anatembelea katika Mikoa ya Shinyanga na Mara huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akizuru katika Mikoa ya Geita na Mwanza.

Akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Imalanguzi Kijiji cha Igurubi Wilayani Igunga, na Kijiji cha Mwabuzo Wilayani Meatu, Mhe Hasunga amesema kuwa wizara ya Kilimo ipo katika mchakato wa kutafuta mfumo madhubuti wa ununuzi wa Pamba.

Alisema mfumo huo punde utakapoelekezwa utatumika lakini ni mfumo ambao utakuwa maalumu kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha sekta ya pamba nchini.

Amesisitiza kuwa ili kuimarisha kilimo nchini ni wazi kuwa wakulima wanapaswa kupatiwa Pembejeo za kilimo ambazo ni Mbegu, Mbolea na Viuatilifu. “Hatuwezi kuwakomboa wakulima kama tutaendelea na uagizaji wa pembejeo feki ambazo zinawarudisha nyuma wakulima” Alikaririwa Mhe Hasunga

Katika ziara hiyo yenye lengo la kutambua changamoto ya zao la Pamba, masoko yake na upatikanaji wa pembejeo, Waziri Hasunga ameeleza kuwa zao la pamba ni sehemu ya mazao makuu ya biashara nchini hivyo ni lazima litafutiwe ufumbuzi.

Aidha, Mhe Hasunga ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi katika mikutano hiyo kuwa Wizara ya Kilimo ipo katika mapitio ya sera ya Kilimo ya mwaka 2013 itakayopelekea kuwa na sheria ya kilimo itakayomnufaisha mkulima na kulinda rasilimali za kilimo ikiwemo ardhi.

Kadhalika, amesema kuwa serikali inaendelea na zoezi la usajili wa wakulima huku akisisitiza umuhimu wa sekta ya umwagiliaji ambayo ikisimamiwa vizuri itakuwa muarobaini wa kilimo pasina kutegemea msimu wa mvua kwa ajili ya kilimo.

Waziri Mkuu Atoa Mwaka Kwa Mikoa Isiyokamilisha Mwongozo Wa Uwezeshaji

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwaka mmoja kwa viongozi wa mikoa ya Dar-es-salaam, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Singida na Shinyanga ihakikishe iwe imekamilisha kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji.

Pia amewataka viongozi wa mikoa na halmashauri zote nchini wahakikishe wanaanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi kama kile cha Kahama ili kuharakisha nia ya Serikali katika kuwezesha wananchi kiuchumi.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumamosi, Juni 15, 2019) wakati akifungua Kongamano la Nne la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. Kongamano hilo limeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) na kauli mbiu yake ni Wezesha Watanzania Kujenga Viwanda.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuliagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuratibu mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo ya Serikali na ile ya binafsi ili kujua ipo mingapi na inamnufaisha nani na je wanufaika wanajijua na ni kweli wananufaika na kisha wampelekee taarifa.

Waziri Mkuu amesema mikoa yote iliyokamilisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji, nayo ifikapo mwakani inapaswa kuonesha hatua za utekelezaji katika kutumia fursa mbalimbali zilizoainishwa pamoja na mikakati ya kutangaza fursa hizo zilizopo katika maeneo yao.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema matokeo ya tafiti ziliyofanywa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuhusu biashara na uwekezaji nchini yanatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uandaaji wa maandiko ya miradi mikubwa inayopendekezwa na shirika hilo.

“Miradi hiyo ni pamoja na ule wa “Harmonized Innovation Solutions for Local Economic Development” ambao upo katika hatua za maandalizi. Lengo la UNDP ni kuhakikisha kuwa miradi inayohusu uwezeshaji wananchi kiuchumi inatekelezwa moja kwa moja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambalo lipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.”

Amesema NEEC ina uwezo mkubwa katika kusimamia miradi mbalimbali ya uwezeshaji ambayo imekuwa ikifadhiliwa na Serikali pamoja na Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo UNDP, ILO, UNCTAD, AfDB na UN-Women, hivyo ameyahakikishia mashirika hayo kuwa Serikali itasimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi yote ili kupata matokeo yaliyo tarajiwa.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuziagizamamlaka zote zishirikiane na NEEC kuhakikisha kuwa fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizobainishwa kupitia tafiti za UNDP zinafanyiwa kazi. “Aidha, hakikisheni kuwa Miradi mikubwa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi inatokana na tafiti hizo”

Amesema anaimani kubwa kuwa kupitia utekelezaji wa miradi hiyo, malengo mbalimbali ya nchi kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi yatafikiwa. Baadhi ya malengo hayo ni pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 - 2020; Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano; Dira ya Taifa ya Miaka 25; na Malengo Endelevu ya Maendeleo ya umoja wa Mataifa (SDGs).

Pia Waziri Mkuu amelitaka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi liendeleekuratibu masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha 2015 - 2020 kuhusu uanzishwaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu.

“Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi iboreshwe sambamba na kuongeza ufanisi ili iweze kuwafikia Watanzania wengi hususan wale wa vijijini. Vilevile, kamilisheni na hakikisheni mnazindua haraka mfumo wa kupima mifuko ya uwezeshaji kwa matokeo ya kiuchumi na kijamii na siyo kwa shughuli walizofanya.”

Amesema uwezeshaji wananchi kiuchumi ni suala mtambuka, sekta mbalimbali za kiuchumi na sekta binafsi zinajihusisha moja kwa moja katika kuwawezesha wananchi kiuchumi, hivyo, amesisitiza kwamba ni muhimu sana masuala ya uratibu, ufuatiliaji na tathimini ya shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi, yakafanywa mara kwa mara ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.
(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Serikali Imepokea Gawio La Sh. Bilioni 6.8 Kutoka Crdb

$
0
0
Na Farida Ramadhani na Peter Haule, Dodoma
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  imepokea kiasi cha shilingi bilioni 6.8 ikiwa ni gawio linalotokana na uwekezaji wa asilimia 21 za hisa katika Benki ya CRDB, ikiwa ni sehemu ya shilingi bilioni 10 ambazo benki hiyo imetoa kama gawio kwa mashirika na taasisi mbalimbali za umma zenye hisa katika Benki hiyo kutokana na faida iliyopatikana Mwaka 2018.

Makabidhiano ya mfano wa hundi za gawio hilo yalifanyika jijini Dodoma ambapo Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) alipokea gawio hilo kwa niaba ya Serikali na kukabidhi baadhi ya mashirika na taasisi za umma zilizopata gawio kutoka Benki hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Mpango, aliupongeza uongozi wa benki hiyo kwa kurudisha fadhila kwa mwananchi na kuzitaka benki na taasisi zote za fedha nchini kuiga mfano wa benki hiyo kwa maendeleo ya nchi.

“Benki ya CRDB na benki zingine muongeze jitihada ili kuongeza gawio kwa Serikali ili iweze kuwahudumia wanachi katika huduma za kijamii ikiwemo afya, elimu na maji”,  alieleza Dkt. Mpango 

Alizitaka benki na taasisi za fedha kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa huduma za benki ili waweze kujikomboa kiuchumi na kuiwezesha nchi kupata gawio kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo.

Dkt. Mpango aliipongeza benki hiyo kwa kuwekeza katika teknolojia hasa katika matumizi ya Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroni (GePG) na kuzitaka benki na taasisi zingine za fedha kutumia mfumo huo.

Aidha, Dkt. Mpango alipongeza taasisi na mashirika ya umma yaliyopata gawio kutoka benki hiyo huku akizitaka Serikali za Mitaa nchini kuiga mfano wa Halmashauri za Lindi, Shinyanga na Mbinga ambazo zimepata gawio, ili ziweze kujiendesha na kukuza uchumi wa nchi.

“Serikali za Mitaa zinaweza kufanya njia nyingine mbadala za kujiongezea kipato kama hii ya kuwekeza kwenye Sekta ya fedha “, alisistiza .

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Bw. Ally Laay alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2018, Benki yake ilitengeneza faida ya shilingi bilioni 64.1 baada ya kukatwa kodi ikilinganishwa na faida ya sh. bilioni 36.2 iliyopatikana Mwaka 2017, huku akichagiza mafanikio hayo na matumizi ya mfumo wa Serikali wa malipo kwa njia ya kielektroniki (GePG).

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela Alisema CRDB imewekeza fedha kwenye mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji katika Mto Rufiji mkoani Pwani na kwamba benki yake iko tayari kuwekeza kwenye ujenzi wa miradi mingine ukiwemo  ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa kiwango cha Kimataifa (SGR).

Mashirika na taasisi za umma zilizopokea gawio ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF (Bil. 2.4), Mfuko wa Hifadhi ya Taifa-NSSF (Mil. 111.5), Mfuko wa Mafao kwa Wafanyakazi wa Serikali-GEPF (Mil. 56,7) , Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar-ZSSF (Mil. 6.5)

Mashirika na taasisi nyingine zilizopokea gawio hilo ambalo ni sehemu ya faida ya shilingi bilioni 34 baada ya kodi kwa mwaka 2018 ni  Mfuko wa Maendeleo Lindi -(Mil. 111.5, Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga (Mil. !.3), Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (Mil. 13.3 na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF (Mil.243.5)

Aidha, Chama cha ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi kimepokea gawio la shilingi milioni 228.

Tume ya Madini ipo teyari kukusanya bilioni 475

$
0
0
Na Issa Mtuwa “WM” – Tunduru, Mbinga na Iringa 
Tume ya madini imesema ipo teyari kukusanya bilioni 475 katika mwaka wa fedha 2019/20 kama walivyopangiwa na serikali na kufikia malengo ya ukusanyaji kama ilivyofikia mwaka 2018/2019 ya kukusanya billion 310 ambapo malengo hayo ilivuka. 

Akiongea kwa nyakati tofauti akiwa wilayani Tunduru, Songea na Mbinga na Iringa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amesema hayo wakati wa vikao  vyake na viongozi wa mikoa, wilaya, maafisa madini wa kaazi, viongozi na wachimbaji wadogo na wanunuzi wa madini kwenye maeneo yao akisisitiza kila mmojja kwa nafasi yake kuwajibika katika suala la usimamizi na ulipaji wa maduhuli ya serikali ili wafikie lengo hilo.  

Amesema serikali imeipangia Wizara ya Madini kukusanya jumla ya Tshs. bilioni 475 na wakusanyaji wa fedha hizo ni Tume ya madini na ili ifikie lengo la kukusanya kiwango hicho lazima wajipange kwa kila mdau anae husika kwa namna moja au nyinge awajibike kutimiza wajibu wake. 

“Ndugu zangu mkisoma jukumu namba moja la Tume ya madini ni kukusanya maduhuli ya serikali, pili kutatua migogoro ambayo ikiachwa inaathiri ukusanyaji wa maduhuli, pamoja na majukumu mengine lakini haya mawili ndio hasa yanayotufanya tuzunguke nchi nzima kuhimiza haya masuala.  

Tume tumesema, ili tufikie haya malengo kila ofisi ya Afisa Madini mkazi iseme imejiwekea malengo ya kukusanya kiasi gani na kila baada ya kipindi gani atakuwa amekusanya kiasi gani, na lazima kila ofisi ifikie hayo malengo. Pamoja na ofisi zetu ofisi zetu kusimamia makusanyo naombeni viongozi wa mikoa na wilaya wasaidieni watu wetu wanapo hitaji msaada wenu kwani tunajenga taifa moja. amesema Prof. Kikula. 

Akisisitizia hoja hiyo mwenyekiti amesema haya yote yanaweza kufikiwa kirahisi kwa kuunganisha nguvu zetu sote na kuzingatia mambo matatu, uwajibikaji, uadilifu hasa kuepuka rushwa na kufuata sheria. Ameongeza kuwa endapo kila mdau kwa nafasi yake atazingatia haya itakuwa rahisi kufikia lengo walilopewa. 

Kwa upande wake Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma ameongeza kuwa jambo lingine la msingi ni lazima kila ofisi ya tume ya madini mikoa yote lazima iwe na mpango kazi unao onesha utaratibu wa utekelezaji wa majukumu kipindi kwa kipindi ili isaidie kujifanyia tathmini kuona ulikotoka, ulipo na unako elekea na muda uliobaki nao katika kufanikisha malengo ya mwaka 

Amesema bila kuwa na mpango kazi inaweza kuwa ngumu kufikia malengo yoyote hata haya ya ukusanyaji wa maduhuli, kwa hiyo amewasisitiza watumishi wa tume kuwa na mpango kazi ambao utawaonyesha kipindi hadi kipindi atakusanya kiasi gani cha maduhuli na kwamba hicho kinaweza kuwa kigezo kikubwa cha upimaji wa utendaji kazi kwa Maafisa Madini wakazi wa Mikoa.

Waziri wa Afya Autaka Uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuweka mashine kwa ajili ya kupimia ugonjwa wa Ebola

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameutaka uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuweka mashine kwa ajili ya kupimia ugonjwa wa Ebola kwa wasafiri wanaoingia nchini.

Waziri Ummy ametoa maagizo hayo leo Jumamosi Juni 15, 2019 wakati akifanya ukaguzi kwenye uwanja huo kuangalia kama kuna mashine  za kupimia ugonjwa huo ambao umeripotiwa kuibuka nchini Uganda.

Amesema Serikali kupitia  wizara yake watatoa mashine kwenye kivuko cha Busisi, Kigongo na kituo cha mabasi cha Nyegezi jijini humo.

Pia,  kwa wasafiri hao wa mabasi kutoka nchi jirani wanaotumia mikoa ya Kigoma na Kagera.

"Kuwepo kwa Ebola sio tatizo hilo linaweza kuthibitiwa ila tatizo ni kusambaa kwa ugonjwa huo," amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake, kaimu meneja wa uwanja huo, Seneth Lyatuu amesema watatekeleza agizo hilo na wanahitaji mashine mbili kwa ajili ya abiria wa ndani na abiria wa nje.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amevitaka vilabu vya soka nchini kutumia vema fursa ya kuwa na mashabiki wengi katika kuvifanya viweze kujitegemea kiuchumi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 15, 2019) katika hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.Ameichangia klabu hiyo sh. milioni 10.

“Natambua kwamba Yanga ni klabu kubwa na kongwe nchini ikiwemo Simba Sport Club ambazo ndizo zina wanachama na mashabiki wasiopungua milioni 20 au zaidi.”

Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuvitaka vilabu vya soka nchini kutafuta njia nzuri na endelevu ya kupata mapato ili kuendesha timu zao na kujiimarisha kiuchumi.

Amesema kwamba, kuimarika kwa vilabu hivyo vyenye ushawishi mkubwa katika soka nchini ni muhimu kwa mustakabali wa soka la Taifa letu.

Waziri Mkuu amesema kufanya vizuri kwa vilabu hivyo kuna uhusiano wa mkubwa na wa moja kwa moja na mafanikio ya timu ya soka ya Taifa.

“Nampongeza kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kwa kazi nzuri aliyoifanya msimu ulioisha na kuiwezesha timu ya Yanga kufanya vizuri ingawa haikupata ubingwa.”

Pia, Waziri Mkuu amesema yeye ni mpenzi wa timu zote zinazoshinda na zinazoshindwa. “Kama kuna timu naipenda sana ni siri yangu, hata nyie hamuijui.”

Waziri Mkuu amesema soka ni mchezo maarufu na una wapenzi wengi duniani na hapa nchini na umejipambanua kwa fursa nyingi ikiwemo biashara, uwekezaji na ajira.

Amesema Serikali imeendelea kusimamia maendeleo ya michezo, ukiwemo mchezo wa soka ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2015-2020.

“Mhe. Rais Dkt. John Magufuli amekuwa akiungana na wanamichezo kuhamasisha kuendeleza michezo na anatamani kuona mkishinda hadi katika ngazi ya Afrika.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amezipongeza timu zote za soka zinazofanya vizuri katika ngazi mbalimbali. “Tumeshuhudia Polisi na Namungo FC zikipanda hadi ligi kuu.”

Ameipongeza timu ya Simba kuwa klabu bingwa, Azam kuwa bingwa wa FA, Serengeti boys na Twiga kuliwakilisha Taifa na Taifa Stars inashiriki AFCON – Misri.

“Kitendo cha Azam kushinda FA na Simba kushiriki vizuri AFCON sasa kumewezesha timu zetu mbili zaidi, Yanga na KMC kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya CAF.”

Kuhusu harambee ya Kubwa Kuliko, Waziri Mkuu amesema ni mwanzo mzuri kuelekea kwenye mabadiliko yatakayoiwezesha Yanga kujitegemea na kujiendesha bila kutarajia michango kama ilivyo sasa.

Naye, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amewataka wanachama wa Yanga warudishe hisia na mapenzi kwa timu yao kama ilivyo kwa timu ya Simba, pia wawe na ubunifu wa kutengeneza mfumo mzuri wa mapato.” Siku hizi Yanga imekuwa baridi sana, viongozi wa Yanga lazima mbadishe hali hii.”

Amesema viongozi wa sasa wa klabu ya Yanga chini ya Uwenyekiti wa Dkt. Mshindo Msolla ni wazuri na wanaujua mpira vizuri, hivyo watengeze mifumo mizuri itakayoinufaisha klabu. Wahakikishe wanawekeza kwenye timu ya watoto badala ya kuangalia wachezaji wa kutoka nje ya nchi pekee.

Amesema wasipowekeza kwenye timu ya watoto siku zote watakua mafahari wa kuwa na wachezaji kutoka nchi za nje jambo ambalo ni sawa na kuwafundishia wenzao. “Leo mnajisifia na akina Makambo, Kagere siku ikicheza timu ya Taifa inakuwaje. Oneni fahari ya kuwa na wachezaji wa ndani hivyo waendelezeni Tanzania kuna vijana wana vipaji.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dkt. Mosolla amesema yeye pamoja na viongozi wenzake watahakikisha wanajenga umoja ndani ya klabu na kuipeleka jirani na wananchi kwa kufufua matawi na kuwa na wanachama wapya wengi.

Pia watawatumia wachezaji wa zamani katika kupata wanachama wengi na pia watakuwa na wiki ya klabu hiyo ambayo wataitumia kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na kurudisha utaratibu wa kwenda mikoani baada ya ligi kuisha kwa ajili ya kutembelea wananchi na kujiongezea wsanachama.

Kuhusu suala la mabadiliko ya katiba amesema watalifanya kwa kufuata utaratibu wa kisheria. Pia Dkt. Msolla amesema uongozi wake utahakikisha unazingatia utawala bora na tayari wametoa matangazo ya nafasi za ajira.

Akizungumza kuhusu hali ya usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu, amesema hadi sasa tayari wamekamilisha kwa asilimia 90 kuwasajili wachezaji wote aliowataka kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera kutoka nje ya nchi na wa ndani ya nchi.

Dkt. Msolla ametumia fursa hiyo kumuomba Waziri Mkuu awasaidie ili Serikali iweze kuwapunguzia changamoto mbalimbali zinazoikabili klabu hiyo ya Yanga ikiwemo ya madeni.
Awali,Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa wa klabu ya Yanga, Anthony Mavunde, alisema kamati hiyo ilikuwa na wajumbe 27 waliofanikisha kupatikana kwa fedha ambazo zimetumika katika kusajili wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Ajira na Vijana alisema walisambaza kadi kwa ajili ya kukusanya fedha za kuimarisha klabu yao ili iweze kujiendesha na kutatua changamoto za wachezaji.

Alisema mbali na kukusanya michango pia kamati yao imependekeza kufanyika kwa mabadiliko ya katiba ili kutengeneza mfumo mzuri utakaoisaidia timu hiyo kuweza kujiendesha na kuweka mfumo mzuri wa kutumia vifaa vya klabu kukuza uchumi.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu ya Yanga na Mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mama Fatma Karume amewataka wananchi wasitumie vilabu vya soka kama njia ya kutaka kujipatia nafasi za kisiasa. Pia amewataka wanachama wampe ushirikiano Mwenyekiti wao mpya.

Naye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alisema hakuna kipindi kigumu kilichompa tabu katika kuongoza wizara hiyo kama kipindi ambacho timu ya Yanga ilipokuwa katika mgogoro wa kiuongozi.

Pia, Dkt. Mwakyembe alionesha kutoridhishwa na upangwaji wa ratiba za michezo mbalimbali ya ligi kuu msimu uliopita, hivyo alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wapenzi wa soka nchini kwamba mambo hayo hayatajirudia tena katika msimu ujao.

(Mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Makamba awatoa hofu Wauza Karanga, Ubuyu, ice cream

$
0
0
Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba imesema hakuna mtu atakayekamatwa kwa kukutwa na vifungashio vya vyakula mfano wa karanga, Ubuyu, kwani kinachokatazwa ni kutumia vifungashio hivyo kubebea bidhaa nyingine.

Kauli hiyo ameitoa siku moja baada ya kusambaa habari kuwa Serikali imepiga marufuku matumizi ya vifungashio vinavyohifadhia vyakula kama ubuyu, karanga, ice cream.

“Vifungashio vya bidhaa za vyakula (karanga, ubuyu, etc) havijazuiwa. Kinachozuiwa ni vi-plastic hivi transparent ambavyo huwa vinafungia karanga, ubuyu etc visitumike kuendea sokoni/dukani kubebea bidhaa. Hakuna mtu atakamatwa kwa kuuza karanga kwenye kifungashio cha plastiki” ameeleza waziri Makamba katika mtandao wa Twitter kuwaeleza wananchi.

Hata hivyo, Makamba ameeleza kuwa zipo bidhaa ambazo lazima zifungwe kwenye mifuko ya Plastiki ili kulinda ubora wa bidhaa hizo kama magodoro, peremende na biskuti hivyo bidhaa kama hizo zitaendelea kuwa kwenye mfumo huo wa kufungwa kwenye vifungashio vya Plastiki.

Matapeli watumia jina la Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi nchini (NEC) Dk. Athumani Kihamia kutapeli watu Facebook

$
0
0
Kundi la matapeli linadaiwa kutumia jina la Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi nchini (NEC) Dk. Athumani Kihamia kwa lengo la kutapeli watu ili kujipatia fedha.

Akizungumza leo, Dk. Kihamia amesema kuna watu wamefungua akaunti feki ya mtandao wa kujamii wa facebook na  kuwatapeli watu kwa kuwatumia ujumbe wa maneno (Messenger), ambapo ametoa tahadhari kwa wananchi kua makini na utapeli huo unaoendelea.

“Kuna baadhi ya watu wamefungua akaunti kwa jina langu na kulitumia kwa kujipatia fedha kwa njia hiyo ya utapeli huku wakijua ni kosa kisheria, baadhi ya jumbe wanazotuma ni pamoja na kwamba Dk. Kihamia anauwezo wa kuwatafutia kazi katika mbuga ya Hifadhi ya Serengeti,”

“Yaani tayari kuna watu wameliwa fedha na hao matapeli hao kupitia sehemu ya ujumbe unaosema sema hivi “angalia kama kuna mtu amemaliza chuo na hajapata kazi uniambie maana kuna kazi shirika la Marekani la Thomson Zoology  kule Serengeti national park na wanahitajika watu wawili wenye diploma au degree kwa ajili ya kazi ya reservations na mshahara milioni moja na laki nane kama kuna mtu aniambie mapema nimpe namba ya huyo mzungu ahsante,” amesema.

Dk. Kihamia amesema aliishawahi kukanusha taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii lakini anaona hali inazidi kuwa mbaya hivyo amewataka wananchi kupuuza ujumbe huo.

Mlima Kilimanjaro Watumika Katika Mapambano Vita Dhidi Ya Ukimwi.

$
0
0
WMU – Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amepongeza juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali kutangaza utalii na uanzishwaji wa kampeni zinazohamasisha mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kupitia vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.

 Dkt. Kigwangalla ametoa pongezi hizo leo mkoani Kilimanjaro wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Wapanda mlima 32 na Waendesha Baskeli 28 kutoka nchi mbalimbali walioshiriki kupanda mlima Kilimanjaro kupitia Kampeni ya Geita Gold Mining Kilimanjaro Challenge 2019 inayolenga kukusanya fedha za kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi na kuwasaidia watoto yatima.

Amesema kampeni hiyo itawawezesha wapanda mlima hao kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro (Uhuru Peak) na waendesha Baiskeli kuzunguka mlima Kilimanjaro takribani Kilometa 500 ikiwa ni sehemu ya kushiriki katika changamoto ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika mwitikio dhidi ya VVU na Ukimwi.

“Ugonjwa wa UKIMWI umeendelea kuwa suala la kipaumbele kwa Serikali, athari zake zinagusa sekta zote ikiwemo wizara ninayoiongoza ya Maliasili na Utalii, bila shaka sote tumeona jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa kupambana na janga hili” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla

Amesema kuwa pamoja na takwimu kuonesha kupungua kwa maambukizo mapya bado jitihada zaidi zinahitajika ili kuutokomeza ugonjwa huo akifafanua  kwamba kila mwananchi ni lazima awe macho kuhakikisha anashiriki kutokomeza ongezeko la maambukizo mapya.

Aidha, amefafanua kuwa programu hiyo imetoa mchango mkubwa katika kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Mlima Kilimanjaro wakati na baada ya msimu wa Kill Challenge kumalizika kwani wageni kutoka ndani nan je ya Tanzania huwataarifu wenzao pindi wanaporudi makwao ili waweze kuja kupanda mlima Kilimanjaro.

“Huu ni uthibitisho tosha kwamba programu hii siyo tu inachangia kudhibiti Ukimwi bali pia inachangia kukuza uchumi wa nchi yetu kupitia mapato ya utalii ya Mlima Kilimanjaro” Amesema.

Dkt. Kigwangalla ameipongeza kampuni ya GGL na wawekezaji wote ambao wamekua wakijitoa kuchangia ustawi wa jamii ya watanzania akitoa wito kwa makampuni mengine kuendelea kujitolea kuchangia program hiyo pamoja na Mfuko wa hisani wa UKIMWI ulioanzishwa na Serikali wa AIDS Trust Fund (ATF).

 Amesema hatua ya GGL kushirikiana na Serikali kupitia TACAIDS ni ya kupigiwa mfano na kwamba inaonesha namna sekta binafsi hususani wafanyabiashara wanavyoendelea kujitokeza kuchangia mwaka hadi mwaka.

Ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa program hiyo takribani shilingi bilioni 13 za Kitanzania zimekusanywa kupitia jitihada hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko amewapongeza wadau wote kwa kuendelea kuchangia kwenye Mfuko wa kupambana na Ukimwi.

Amesema kuwa mujibu wa takwimu zilizopo TACAIDS ugonjwa wa UKIMWI bado ni tatizo nchini kutokana na kuwepo kwa maambukizi mapya ya watu 200 kila siku.

Amesema kazi kubwa inayofanywa na TACAIDS kwa sasa ni kuendeleza kampeni ya kuzuia maambukizi yasitokee ili kuendana na makubaliano ya umoja wa Mataifa ya kufikia maambukizo 0 ifikapo mwaka 2030.

“ Bado tunayo kazi kubwa sana ya kuzuia maambukizi haya, watu 200 kwa siku kuambukizwa VVU ni wengi, tunaendelea kujitahidi na kufanya kazi kubwa ya kuelimisha wananchi na kama ingekua ni ajali ingekua ni watu 200 wanaumia kila siku, tunazungumza hizi takwimu kujikumbusha kwamba Ukimwi bado upo” Amesisitiza Dkt. Maboko.

Ameeleza kuwa kiwango cha maambukizi  hayo kinazidi kuongezeka miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24  akifafanua kwamba kwamba kati ya watu 200 waliopata maambukizi , watu 80 ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24.

“ Kwa ujumla maambukizi mapya  yanazidi kushuka isipokuwa kwa vijana yanazidi kupanda juu, sisi kama Tume kwa kushirikiana na wadau tunaliona na tunaendelea kulifanyia kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kunusuru kizazi cha vijana ambao ndilo tegemeo la Taifa na viongozi wa baadae” Amesisitiza Dk. Maboko.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI Mhe. Oscar Mukasa amesema kuwa kazi yao kama Kamati ni kushirikiana na wadau wote katika masuala ya  Sera, Sheria na usimamizi na kufafanua  kuwa mfuko wa Ukimwi tangu kuanzishwa kwake umekuwa na changamoto ya kupata fedha akiupongeza Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kuendelea kuchangia fedha katika mfuko huo.

Amesema Bunge itaendelea kuishauri Serikali kwa lengo la kupata vyanzo vingine vya mapato vya uhakika ili Serikali iweze kushirikiana na wadau wa ndani wa Sekta binafsi kwa lengo la kujitegemea.

Amesema tukio hilo la wapanda mlima kuchangisha fedha linapeleka ujumbe kwa jamii kwamba kazi ya kupambana na UKIMWI bado ni kubwa na endelevu hivyo jamii yote inapswa kushiriki kikamilifu.

MWISHO.

Kampuni 11 za Uturuki zatafuta fursa za Uwekezaji

$
0
0
Ujumbe wa kampuni 11  kutoka Uturuki upo nchini kwa ajili ya kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji, hususan kwenye sekta ya viwanda vya dawa za binadamu, vifaa vya maabara, vyombo vya ndani,  vifaa vya umeme, ujenzi pamoja na ununuzi wa korosho.

Ziara hiyo imetokana na uratibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Ujumbe huo ambao uliwasili nchini tarehe 10 Juni 2019 ulishiriki mkutano (B2B) uliondaliwa na TPSF tarehe 11 Juni 2019. Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine,  wawakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Ukanda  wa Uwekezaji (EPZA) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) walitoa maelezo kuhusu kanuni, taratibu na mazingira ya kufanya biashara hapa nchini.

Ujumbe huo utatembelea Zanzibar tarehe 13 Juni 2019 na baadaye Dodoma kwa ajili ya kuangalia maonyesho ya masuala ya ujenzi. Ujumbe huo utaondoka nchini tarehe 16 Juni 2019 kurejea Uturuki.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Waziri Kabudi Awapa Neno Wamiliki wa Hoteli Jijini Dar

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amewataka wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli jijini Dar es salaam kutumia fursa ya kibiashara itakayotokana na ujio wa wageni zaidi  ya 1,000 watakaoshiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Agosti  2019.

Profesa Kabudi ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 15, 2019 jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli.

Amesema wizara yake itafanya kazi kwa ukaribu na wadau hao na kuwataka kutoa huduma bora.

Waziri huyo amewataka wamiliki na wafanyabiashara hao wa hoteli kuzingatia mwongozo wa Serikali uliotolewa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhusiana na suala la ubadilishaji wa fedha za kigeni kwa kuwataka kuwaelekeza wageni kubadilishia fedha zao benki na pia katika hoteli ambazo zimeidhinishwa kubadilisha fedha za kigeni.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili June 16

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ampa pole Mkurugenzi Uendeshaji Sport Pesa Tanzania, Tarimba Abbas

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimpa pole, Mkurugenzi wa Uendeshaji Sport Pesa Tanzania, Tarimba Abbas, kwa kufiwa na watoto wake wawili, Maisam na Alliazgar Tarimba Abbas, nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Juni 16.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimpa pole, Mke wa Mkurugenzi wa Uendeshaji Sport Pesa Tanzania, Tarimba Abbas, Warda Tarimba Abbas kwa kufiwa na watoto wake wawili, Maisam na Alliazgar Tarimba Abbas, nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Juni 16.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii atembelea Makumbusho

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda jumamosi tarehe 15 Juni, 2019 alitembelea Makumbusho ya Taifa kujionea urithi na hazina kubwa ya Taifa la Tanzania. Urithi huu wa utamaduni na asili ni pamoja na mafuvu na masalia ya binadamu wa kale au zamadamu, kama Australopithecus afarensis, Zinjanthropus (Paranthropus) boisei, Homo habilis, Homo erectus na Homo sapiens sapiens, yenye umri wa tangu miaka milioni 3.6 had miaka 200,000 iliyopita.

Akiwa Makumbusho ya Taifa, Pof. Mkenda alijadiliana na kuielekeza Menejimenti ya Makumbusho ya Taifa hatua ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii inachukua kuimarisha sekta ya malikale na hususan, Shirika la Makumbusho ya Taifa la Tanzania.

“Wizara inaiimarisha na kuijengea uwezo Makumbusho ya Taifa ili itimize majukumu yake ya msingi ya kutafiti, kuhifadhi, kuonesha na kuelimisha umma juu ya urithi wa Taifa na dunia kwa ujumla”.

Prof. Mkenda, aliyasema hayo alipotembelea chumba maalumu cha kuhifadhia mikusanyo adhimu, na kujionea masalia hayo ya binadamu wa kale, hati ya Uhuru wa Tanganyika, tai ya uhuru, kinyago maarufu cha kimakonde na chungu, mchanga na vibuyu halisi vilivyotumiwa na Baba wa Taifa Mwal. Julius K. Nyerere kuchanganya mchanga kama ishara ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 1964.

Prof. Mkenda alisema kuwa kufika kwake Makumbusho ya Taifa inadhihirisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imejipambanua na inajali na kuthamini urithi wa Taifa na iko tayari kuulinda urithi huu kwa gharama yoyote kwa sababu ukipotea haupatikani tena.

“Vitu hivi ni muhimu na ni urithi wetu, hivyo tunatakiwa kuvitunza kwa gharama yoyote kwani ni utambulisho wa Taifa la Tanzania, vinaleta amani, mshikamano, uzalendo na furaha. Aidha, vinavutia watalii wa ndani na nje na hivyo kuongeza pato la Taifa”, alisema Prof. Mkenda.

Akizungumza na menejemeti na baadhi ya wataalamu wa Makumbusho ya Taifa Prof. Mkenda ameweka wazi kuridhishwa na uhifadhi na kazi iliyofanywa na Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na Ofisi ya Usalama wa Majengo ya Serikali ya kukiimarisha chumba hicho maalumu.

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa na Menejimenti yake kuimarisha zaidi uhifadhi na ulinzi wa urithi huu wa nchi yetu na dunia kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Fuvu la Zinjanthropus lenye umri wa miaka milioni 1.75 iliyopita liligunduliwa kwenye bonde la Olduvai, Ngorongoro tarehe 17 July, 1959 na wataalamu wa Akiolojia Dkt. Louis Leakey na mke wake Dkt. Mary Leakey.

Uguduzi huo ulibadilisha uelewa wa wanasayansi kuhusu mchango wa bara la Afrika katika sayansi ya chimbuko la binadamu duniani. Masalia ya Zinjanthropus (Paranthropus) boisei pamoja na masalia mengine ya binadamu wa kale (kama Homo habilis, Homo erectus), zana zao za mawe na masalia ya mifupa ya wanyama waliyokula bonde la Olduvai miaka milioni 2.0-1.0 iliyopita, vinathibitishia dunia kuwa Tanzania ndiyo nchi pekee yenye taarifa bora na sahihi kuhusu chimbuko la binadamu na utamaduni wake (tabia, teknolojia, chakula na namna ya kupata chakula hicho) katika kipindi hicho; na kwamba bonde la Olduvai ndilo Chimbuko la Binadamu wote duniani (the Cradle of Humankind).

Prof. Mkenda ameitaka Makumbusho ya Taifa kuanzisha kampeni ya kutangaza vivutio mbalimbali ambavyo vinapatikana katika makumbusho zetu yakiwemo masalia ya binadamu wa kale.

“Elimu hii na vitu nilivyoviona leo nimefurahi sana, lakini Watanzania wangapi wanavijua? Serikali ya Awamu ya tano inajipambanua kujali na kujivunia vitu vyetu, lugha yetu ya Kiswahili, maliasili zetu, malikale zetu na utamaduni wetu, alisema Prof Mkenda..

Alisema matangazo kwenye luninga, redio na magazeti kuhusu vitu vinavyotunzwa Makumbusho ya Taifa, yatajenga uelewa kwa wananchi juu ya umuhimu wa makumbusho na hivyo, kufanya watu wengi kuja kutembelea makumbusho zetu.

“Msipotangaza hakuna anayewezea kujua kuwa vitu muhimu kama hivi viko hapa Makumbusho ya Taifa, tunatakiwa tuwaambie wananchi ili waje kuviona,” alisisitiza.

Prof. Mkenda alisema, “tunapoelekea kwenye maadhimisho ya miaka 60 tangu kugunduliwa kwa fuvu la Zinjanthropus, fuvu hilo, halitaondolewa Makumbusho ya Taifa kwenda bonde la Olduvai, bali litaendelea kuhifadhiwa na kutunzwa vizuri Makumbusho ya Taifa na badala yake nakala itatumika pale inapohitajika.

Aidha, amesisitiza kuwa matangazo hayo yawe ya ndani na nje ya nchi (International Promotion) kwa sababu kuna watafiti wengi nje ya Tanzania ambao wangependa kuja kufanya utafiti katika Nyanja za akiolojia na paleontolojia.

Sambamba na hilo, aliwaagiza Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Dkt. Freddy Manongi na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof. Audax Mabulla, kuisimamia Kamati inayohusika na maandalizi ya maadhimisho hayo kubuni na kupanga matukio mbali mbali yatakayoleta hamasa katika kuadhimisha miaka 60 ya ugunduzi wa Zinjanthropus na kutangaza vivutio mbalimbali vilivyoko Tanzania.

Alisisitiza kuwa matukio tofauti yaandaliwe kuanzia mwezi Julai mpaka Desemba mwaka huu kama sehemu ya kumbukumbu ya ugunduzi wa fuvu la Zinjanthropus boisei.

Tume ya Madini yasisitiza uuzaji wa Madini kwenye Masoko

$
0
0
Na Issa Mtuwa “WM” Iringa
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amekemea na kutoa onyo kwa Wachimbaji na wanunuzi wa madini nchini kuacha tabia ya kufanya biashara ya madini nje ya masoko yaliyoteyari na yanayoendelea kuanzishwa mikoa yote hapa nchini.

Prof. Kikula amesema hayo Juni 15, 2019 muda mfupi mara baada ya kukagua soko la madini mkoani Iringa ambako hakuridhishwa na takwimu za uuzaji wa madini ya dhahabu katika soko hilo kuwa spidi ni ndogo akitolea mfano wa takwimu zilizotolewa na Mkaguzi wa Madini kituo cha Iringa Severine Haule kuanzia tarehe 30 Mei, 2019 hadi tarehe 14 Juni, 2019 ni gram 92 tuu za dhahabu zimezalishwa na kupita sokoni hapo.  

Amesema serikali haina mzaha kuhusu suala hilo na yeyote atakae kutwa anafanya biashara ya madini nje ya masoko rasmi atakumbana na mkono wa sheria ikiwemo kutaifishwa madini na kila aina ya raslimali iliyotumika kuwezesha ufanyikaji wa biashara hiyo, hivyo ametoa wito kwa wadau wote kujiepusha na utoroshaji wa madini sambamba na kufanya biashara nje ya Masoko. 

Ameongeza kuwa, jicho la serikali linaona mbali hivyo asijidanganye mtu. Amesema kuwa ziko taarifa za ujanja ujanja kufanya biashara ya kuuziana madini usiku wilayani Tunduru, wengine kutorosha madini kuelekea Malawi kwa wilaya ya Songea na Mbinga, na Iringa wachimbaji wadogo, wanunuzi wa kati (Brokers) na wanunuzi wakubwa (Dealers) kuuziana madini kwa siri kutofikisha madini kwenye soko. 

Amesema taarifa zote hizo serikali inazo hivyo amewaomba wadau wote wanaohusika na michezo hiyo waache mara moja na kama wataendelea wajue siku zao si nyingi hivyo wasijitafutie matatizo wakaacha familia zao bila sababu.  

Wakati huo huo Mwenyekiti ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Tume hiyo mikoa yote nchini kuzingatia uadilifu na kwamba kamwe wasikubali kushawishika kwa rushwa. 

Amesema laiti kama yeye angekuwa mwepesi wa kupokea rushwa pengine asingekuwa anaendelea kumsaidia Rais Magufuli kuwatumikia Wananchi kwani yapo majaribu mengi na majaribio ya watu kumpelekea vifurushi na mabegi ya fedha lakini hajawahi kuingia katika mitego hiyo na hajawahi pokea rushwa hata siku moja katika miaka 46 ya maisha yake yote ya utumishi wa umma. 

Amewambia watumishi hao kuwa wakae wakijua wale watakao waletea fedha hiyo siri haitabaki kwa mtu mmoja lazima itavuja na huo ndio mwanzo wa kuharibu jina lake hivyo wasikubali rusha ni hatari.

Mwenyekiti Prof. Idris Kikula na Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma wamehitimisha ziara yao katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe na Iringa ambako walikuwa wanakagua shuguli za madini, kuhimiza ulipaji wa maduhuli ya serikali, utatuzi wa migogoro, kusikiliza kero na kutatua, kuongea na wafanyakazi wa tume ya madini, wachimbaji, wafanyabiashara wa madini na kuognea na viongozi wa serikali ngazi ya mikoa na wilaya.  

Yaliyojiri kwa ujumla katika ziara hiyo ni pamoja na; kilio cha wachimbaji wadogo katika mikoa mbalimbali kutozwa kodi zaidi na Halmashauri za wilaya na vijiji kinyume cha sheria ya madini, ufinyu wa bajeti, uhaba wa watumishi na vitendea kazi kwa ofisi za tume ya madini mikoani, ucheleweshaji wa utolewaji wa leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo, ulipaji wa maduhuli ya serikali, uuzaji wa madini kwenye masoko rasmi, uadilifu na kuepuka rushwa. 

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Venance Mabeyo Asema dhana ya kulitegemeza Kanisa inatakiwa kufanyika kwa umakini

$
0
0
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Venance Mabeyo amesema dhana ya kulitegemeza Kanisa inatakiwa kufanyika kwa umakini ili lsiathiri shughuli za kiroho za Kanisa Katoliki.

Mabeyo ameyasema hayo leo Jumapili Juni 16, kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Halmashauri ya Walei iliyoongozwa na Kardinali Polycarp Pengo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro, Kamishna wa Uhamiaji, Anna Makakala, Spika mstaafu, Anna Makinda na Rais mstaafu wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela.

Amesema jambo hilo liwe ni la kiimani zaidi na muumini afundishwe kwanini anatakiwa kutoa na asipotoa maana yake ni nini. Amesema hilo litasaidia kuendelea kukuza imani za waumini wa kanisa hilo kwa kufanya wanachokijua.

“Mambo haya yafanyike kwa umakini zaidi ili isionekane Kanisa linapigia chapuo mambo ya fedha kuliko imani,” amesema Mabeyo ambaye ameambatana na mkewe, Tina Mabeyo pamoja na watoto wao.

Sherehe za maadhimisho hayo zimehudhuriwa na mamia ya waumini pamoja na maaskofu wote wa Kanisa Katoliki nchini, mapadri na wawakilishi wa halmashauri za walei kutoka majimboni.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images