Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yasema biashara ya kuni na mkaa ni halali,rasmi na haina kizuizi kwa mwananchi yeyote

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Serikali imelieleza bunge kuwa biashara ya kuni na mkaa ni halali,rasmi na haina kizuizi  kwa mwananchi yeyote ili  mradi anafuata mwongozo wa uvunaji wa mazao ya misitu wa mwaka 2007 na marekebisho yake ya mwaka 2015.

Hayo yamesemwa Juni 10,2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Costantine Kanyasu wakati akijibu swali la mbunge wa viti Maalum Zubeda Sakuru aliyehoji ongezeko la gharama za nishati nchini hasa umeme na gesi zimepelekea kuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya kuni na mkaa je,lini serikali itarasmisha biashara ya mkaa ili kupunguza makali ya maisha.
 
Akijibu Swali hilo,Mhe.Kanyasu amesema biashara ya kuni na mkaa inafanyika kwa mujibu wa sheria na kanuni za misitu ,pamoja na tangazo la serikali Na.324  la  14/08/2016  na mwongozo wa uvunaji wa mazao ya misitu wa mwaka 2007 uliofanyiwa marekebisho mwaka2015.
 
Kutokana na hilo,Naibu Waziri Kanyasu amesema biashara ya kuni na mkaa ni rasmi na haina kizuizi chochote kwa mwananchi na kinachotakiwa ni kufuata sheria  na taratibu za biashara za uvunaji  wa mazao ya misitu.
 
Aidha,Mhe.Kanyasu amezitaja baadhi ya taratibu ambazo zinatakiwa kufuatwa na kuzingatiwa wakati wa kutaka kufanya biashara ya mkaa na kuni ni pamoja na kutenga maeneo ya misitu kwa ajili ya kutengeneza mkaa,kusajiliwa na meneja wa misitu wa wilaya,kutuma maombi ya usajili kwa afisa misitu wa wilaya na kila mfanyabiashara kulipia mrabaha .
 
Hata hivyo,serikali imehimiza watanzania kuanzisha mashamba ya miti kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na nishati.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Waziri Kigwangalla Aingilia Kati Na Kumaliza Mgogoro Wa Ardhi Hifadhi Ngorongoro Na Wananchi

$
0
0
WMU – Ngorongoro, ARUSHA.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro uwaruhusu wananchi wa Kata ya Alaitole wajenge  shule ya wasichana ya bweni katika eneo la Esere lililo ndani ya Mamlaka hiyo ili waweze kupata elimu kufuatia wananchi hao kuzuiwa kwa muda mrefu kutekeleza mradi huo.

Aidha, ameutaka uongozi wa Mamlaka hiyo utoe kibali cha kuwawezesha wananchi kata hiyo kuanza ujenzi haraka iwezekanavyo ili fedha zilizotolewa na Serikali shilingi milioni 298 zianze kutumika.

Dkt. Kigwangalla ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Kata Alaitole wilayani Ngorongoro kwenye mkutano wa hadhara uliowashirikisha viongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, viongozi serikali wa kata hiyo, viongozi wa mila wa kabila la Masai na madiwani na Mbunge wa jimbo la  Ngorongoro Mhe. William Ole Nasha.

Amesema Serikali inaunga mkono juhudi zote za wananchi za kujiletea maendeleo akifafanua kwamba hatua ya wananchi hao kuamua kujenga shule ya Sekondari ya Bweni ni jambo la linalopaswa kupongezwa na kila mpenda maendeleo.

“Mnacho kitaka kiko wazi, mnataka maendeleo ya watoto wenu, katika hili mmesema kila baba anatoa elfu hamsini na wanawake wanatoa elfu ishirini, hili ni jambo kubwa  achilia mbali nguvu kazi mnayojitolea na tayari serikali imeshaleta milioni 298, haiingii akilini eneo linalochangia kuleta na kuingiza mapato mengi Serikalini kiasi cha bilioni 126 likose shule” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Dkt. Kigwangalla ameeleza kuwa ujenzi shule hiyo utawaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wananchi hao kwenye mipango yao ya utekelezaji miradi ya maendeleo.

Amesema jamii hiyo pamoja na mazingira wanayoishi kuwa ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wanahitaji elimu. Aidha, amesema pia ni muhimu katika sekta ya utalii kupitia utamaduni wao akiongeza kuwa kazi ya Wizara ni kuona mafanikio ya sekta ya utalii yanakuwa kwa kuongeza mapato na sio migogoro.

Dkt. Kigwangalla amesema Hifadhi ya Ngorongoro ni hifadhi mseto inayoruhusu binadamu na wanyama kuwepo katika eneo moja na kwamba hiyo ipo kwa mujibu wa sheria akiitaka Mamlaka hiyo kuyatazama vizuri majukumu yake ya kuendeleza Utalii, Kulinda rasilimali zililizopo kwa maana ya kuhifadhi na kuhudumia jamii iliyo ndani ya hifadhi hiyo.

Katika hatua nyingine ameutaka uongozi wa Mamlaka hiyo uendelee kufanya mazungumzo na wananchi hao badala ya kujielekeza katika matumizi ya nguvu ili kupata uelewa wa pamoja akitolea mfano wa eneo la Loliondo ambalo hivi sasa lina utulivu.

“ Viongozi wa Mamlaka mnalo jukumu la kuwasikiliza wananchi na kuamua kwa pamoja, eneo la Ngorongoro ni Urithi wa dunia na litaendelea kuwa hivyo kwa kuheshimu na maslahi ya Taifa na maslahi ya walio walio wengi” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Kuhusu mahusiano baina ya wananchi na wahifdhi Dkt. Kigwangalla amesema kuwa kupitia mkutano wake na wananchi amebaini kuwepo kwa tatizo la mawasiliano na mahusiano baina ya wananchi wa eneo hilo na  watumishi wa Serikali walio chini ya  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro akibainisha kwamba tayari serikali imeliona jambo hilo na inaendelea kulifanyia kazi.

Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe. William Ole Nasha akizungumza wakati wa mkutano huo amempongeza na kumshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha ulinzi wa rasilimali za Taifa katika maeneo mbalimbali nchini.

Amemwomba aeendelee kutembelea maeneo mengine ya jimbo hilo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi wa kata za wilaya hiyo kwa lengo la kudumisha mahusiano mema.

Mhe. Ole Nasha ameeleza kuwa hatua ya Wizara kutafutia ufumbuzi mgogoro huo wa ujenzi wa shule ya wasichana ya bweni, vile vile uamuzi wa serikali kutoa eneo na fedha kiasi cha shilingi milioni 298 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo katika eneo lililokubaliwa ni ishara tosha kwamba Serikali inawalinda na kuwajali wananchi wake.

Amesema wananchi wa jimbo la Ngorongoro pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wako ni wasikivu na wako tayari muda wote kushirikiana na Serikali ikiwemo ulinzi wa rasilimali zilizopo na kuendeleza uhifadhi katika hifadhi ya Ngorongoro.

Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Alaitole wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemshukuru Dkt. Kigwangalla kwa kuamua kuwafuata na kuzungumza nao katika makazi yao wakimpongeza kwa juhudi zake za kutatua changamoto mbalimbali kwa maslahi ya wananchi na uhifadhi.

Aidha, wamemwomba kuendelea kuisimamia sekta ya uhifadhi nchi wakitoa wito wa kudumisha mahusiano mema baina ya wananchi na wahifadhi.



MWISHO

Kaka wa Kambo wa Kiongozi wa Korea Kaskazini aliyeuawa alikuwa jasusi wa CIA

$
0
0
Kaka wa kambo wa Kiongozi wa Korea Kaskazini aliuawa baada ya kubainika kuwa ni jasusi wa shirika kuu la kijasusi la Marekani CIA.

Kwa mujibu wa gazeti la Wall Street Journal,  Kim Jong-nam, kaka wa kambo wa Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un aliuawa kwa sumu akiwa safarini nchini Malaysia mwaka 2017.

Gazeti hilo limechapisha ripoti hiyo Jumatatu na kusema limedokezewa hayo na mtu mwenye taarifa kamili kuhusu tukio hilo. Gazeti hilo limedokeza kuwa, kulikuwa na mawasiliano baina ya CIA na Kim Jong-nam.

Uchunguzi uliofanywa na Malaysia kuhusu kesi hiyo mwaka jana uligundua kuwa, kaka wa kambo wa Kiongozi wa Korea Kaskazini alikutana an raia mmoja wa Marekani, aliyeshukiwa kuwa ni jasusi, katika hoteli moja nchini Malaysia siku nne kabla ya kuuawa tarehe 9 Februari 2019. 

Kabla ya hapo, raia mmoja wa Indonesia  Siti Aisyah na raia mmoja wa Vietnam, Doan Thi Huong walikuwa wamekamatwa kwa tuhuma za kumpa sumu Kim Jong-nam katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, lakini waliachiliwa huru mapema mwaka huu nchini Malaysia baada ya kukosekana ushahidi.

Marekani na Korea Kaskazini zina historia ndefu ya uhasama na uadui. Mwaka jana Rais Donald Trump wa Marekani alikutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un nchini Singapore kwa ajili ya mazungumzo ya nyuklia.

 Walifanya mkutano wa pili mjini Hanoi Vietnam mapema mwaka huu lakini mazungumzo hayo yaligonga mwamba baada ya Korea Kaskazini kuituhumu Washington kuwa imepoteza fursa nadra ya kupunguza uhasama.

Tanzania Kutumia Zoezi La Kupima Utayari Wa Kukabili Magonjwa Ya Mlipuko Mipakani, Kuchagiza Utekelezaji Wa Dhana Ya Afya Moja Nchini.

$
0
0
Kufuatia nchi za Kanda ya Afrika Mashariki kuwa katika hatari ya kuathirika na magonjwa ya mlipuko kama Homa ya Bonde la Ufa, Mafua Makali ya Ndege na Ebola, na kwa kuwa magonjwa hayo husambaa kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine, Tanzania kwa kushirikiana na Kenya wameanza kutekeleza zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, lilofunguliwa leo  mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga,  kuanzia tarehe 11 hadi 14 Juni mwaka huu.

Zoezi hilo, linazingatia Dhana ya Afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu. Jumla ya washiriki 150 ambao wanatoka Sekretarieti ya Afrika Mashariki, Kenya na Tanzania washiriki 130 kutoka ngazi ya taifa, mkoa na wilaya katika mpaka wa Namanga; pamoja na nchi nyingine wanachama ambapo watakuwa watazamaji ikiwa ni Uganda, Burundi, Rwanda na Sudani Kusini wanatarajiwa kushiriki zoezi hilo.

Akiongea leo tarehe 11 Juni, 2019, wakati wa Kufungua rasmi zoezi hilo  la siku nne, mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga,  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, amefafanua kuwa, serikali kupitia Wizara hiyo inatumia zoezi  hilo kufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mipango ya Dharura ya Taifa na Kanda, Miongozo ya Utendaji na kuwapa washiriki fursa ya kujifunza namna sekta zingine zinavyotekeleza majukumu katika kuzuia na kupunguza madhara pamoja na kujiandaa kukabiliana na maafa ya magonjwa ya mlipuko.

“Hapa nchini Tanzania tunalo Dawati la Kuratibu masuala ya Afya Moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati hilo sisi kama wizara ya Afya tunasubiri tu ripoti ya zoezi hili na tutaitekeleza mara moja. Utekelezaji wa ripoti hiyo tutahakikisha unakuwa wa ufanisi na tija kwa nchi ili tuweze kusaidia kuimarisha ushirikiano wa sekta za Afya hapa nchini  kwa kuzingatia dhana ya  Afya moja.” Amesisitiza Waziri  Ummy.

Aidha, Waziri Ummy, ameongeza kuwa zoezi hilo linalenga kutathmini utaratibu wa kutumia kikosi cha taifa cha dharura cha kukabili lakini pia  kuhakiki matumizi ya maabara zinazohamishika, kutathmini uwezo wa uchunguzi na usimamizi wa magonjwa ya mlipuko kwa vituo vilivyopo mpakani kwa magonjwa ya mifugo na binadamu; kupima hatua za kujiandaa kukabiliana katika viwanja vya kimataifa vya Jomo Kenyatta na Kilimanjaro.

Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akiongea kwa niaba ya Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana  na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, ameeleza kuwa Serikali kupitia ofisi hiyo, itaendelea kuratibu sekta zote za Afya nchini kwa kutumia Dhana ya Afya moja,  ili kuhakikisha Afya za wananchi zinakuwa imara na salama kwa kudhibiti magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kusababisha maafa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, akiongea kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina, amebainisha kuwa,  kwa kutambua umuhimu wa Dhana ya Afya moja, Wizara inafahamu kuwa mifugo huwa ni chanzo cha  vimelea  vya magonjwa ambayo huambukizwa binadamu, hivyo serikali imeendelea kuboresha maabara za Mifugo nchini ili kuweza kutambua vimelea kwa haraka na wakati ili visisababishe magonjwa ya mlipuko kwa  binadamu.

Naye, Waziri wa Afya wa Kenya, Mhe. Sicily Kariuki, amebainisha kuwa zoezi hilo ambalo linahusisha  mlipuko wa virusi vinavyo shabihiana na Homa ya Bonde la Ufa katika eneo la mpakani, ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa sekta za Afya, kwa kuwa  washiriki watahitajika kuonesha utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo kwakuzingatia Dhana ya  Afya Moja.

Zoezi hilo linafanyika nchini Tanzania kufuatia Kikao cha 11 cha Kawaida cha Mawaziri wa Sekta ya Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika mwezi Machi, 2015, ambapo kilielekeza Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuandaa Zoezi la Nadharia la kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika mpaka wa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga.

Zoezi hilo ambalo linafanyika mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga, linaratibiwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na nchi wanachama kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani la GIZ na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa.


IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILINO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU

 

Polisi Kenya wamjeruhi vibaya kwa risasi kijana aliyetaka kuingia Ikulu kwa nguvu

$
0
0
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) nchini Kenya, Brian Kibet Bera, amepigwa risasi na polisi baada ya kuingia Ikulu ya Nairobi kinyume cha sheria.

Kibet wenye umri wa miaka 25, alipigwa risasi na kujeruhiwa bega la kushoto na polisi waliokuwa wakifanya doria katika eneo hilo hilo baada ya kuchomoa kisu alipoagizwa asimame.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu, Kanze Dena-Mararo tukio hilo litokea Jumatatu na mtuhumiwa alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kwa ajili ya matibabu.

Siku moja kabla ya tukio hilo kutokea Kibet aliandika katika mtandao wake wa Facebook kuwa atavamia Ikulu.
Ikulu ya Nairobi Kenya

Tukio hilo limezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii nchini humo huku baadhi watu wakiamini huenda mwanafunzi huyo alichukua hatua hiyo baada ya kutumia kilevi chochote kwasababu mtu aliye na akili timamu hawezi kufanya hivyo.

Kwa sasa Kibet anaendelea na matibabu katika katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta nchini humo.

Benchi La Ufundi Taifa Stars Laongeza Nguvu Mashindano Ya Afcon

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano June 12


Nditiye:Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) linamchango Mkubwa Katika Huduma Za Hali Ya Hewa Tanzania.

$
0
0
 Na: Christopher Philemon, Monica Mutoni. Geneva
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsailiano Mhandisi Atashasta Nditiye ameeleza namna ambavyo Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) linavyochangia katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa Tanzania.Amezungumza hayo wakati akihutubia mkutano wa 18 wa WMO, unaoendelea jijini Geneva, Uswisi.

‘WMO ina mchango mkubwa katika huduma za hali ya hewa nchini kama vile miongozo maalum iliyowekwa kwa ajili ya uandaaji na utoaji wa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa maeneo ya ziwa Viktoria ambapo TMA inatoa miongozo ya tahadhari kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, utekelezaji wa Mfumo wa Kidunia wa Huduma za Hali ya Hewa (Global Framework for Climate Services-GFCS) ambao ndani yake Tanzania kupitia TMA inanufaika masuala mbalimbali kama vile mafunzo ya muda mrefu na mfupi, upatikanaji wa baadhi ya vifaa vya hali ya hewa  alisema’ Alisema  Nditiye. 

Aidha, katika hotuba yake, naibu waziri  Nditiye aliwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kuelezea namna Serikali inavyoweka jitihada kubwa kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini zinakuwa za kisasa kwa kufanikisha ununuzi wa rada tatu za hali ya hewa pamoja na kuifanya TMA iweze kukidhi zaidi matakwa ya watumiaji kwa kuibadilisha TMA kutoka kuwa Wakala na kuwa Mamlaka kamili.

Wakati akimalizia hotuba yake, Naibu waziri  Nditiye alitumia nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kumnadi mgombea wa nafasi ya makamu wa tatu wa Rais wa WMO Dkt. Agnes Kijazi kutokana na uwezo na uzoefu alionao WMO akiwa mjumbe wa kamati kuu wa shirika hilo kwa miaka saba.  

MWISHO.

Rais Magufuli atangaza wawakilishi wa Serikali ndani ya Bodi ya Airtel

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mohammed Abdallah Mtonga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Mtonga anachukuwa nafasi ya Dkt. Omari Rashid Nundu ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania.

Uteuzi wa Dkt. Omari Rashid Nundu katika nafasi hiyo unafuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel International juu ya uendeshaji wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania anapaswa kuteuliwa na Serikali ya Tanzania.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo Afisa Mkuu wa Ufundi (Chief Technical Officer – CTO) pia anateuliwa na Serikali ya Tanzania, na aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo ni Dkt. Prosper Godfrey Mafole.

Wajumbe wengine watakaoiwakilisha Serikali katika Bodi ya Airtel Tanzania ni John Marato Sausi na Lekinyi Ngariapusi Mollel.

Uteuzi huu unaanza leo June 12, 2019.

Serikali Yatenga Zaidi Ya Tsh.bilioni 82 Kuendesha Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Mwaka Huu 2019.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imeandaa kiasi cha Sh.Bilioni 82,milioni 975 laki 9,na 94 elfu ,na mia 148 kwa ajili ya kuendesha uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu 2019. 

Hayo yamesemwa leo bungeni jijini Dodoma na Naibu waziri wa Ofisi ya Rais,TAMISEMI,Mwita Waitara wakati akijibu swali la mbunge wa Mtambile Masoud Salim aliyehoji ,mwaka 2019 utafanyika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Sheria ,je,serikali ina mkakati gani unaoendelea  katika maandalizi ya mchakato wa Uchaguzi huo. 

Katika Majibu yake Naibu waziri  wa Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mhe.Mwita Waitara amesema katika kuhakikisha uchaguzi waserikali za mitaa unafanyika kwa ufanisi ,serikali imekamilisha maandalizi ya kanuni hizo zilizotangazwa kwenye gazeti la serikali la tarehe 26/April/2019   tangazo Na.371,tangazo Na.372 , tangazo  Na.373,  na tangazo 374. 

Hivyo Naibu Waziri Waitara amesema ,serikali imehakiki maeneo ya Utawala na kufanya mafunzo na mikutano kwa wadau wa uchaguzi  ambapo serikali inaendelea na maandalizi ya ununuzi ya ununuzi wa vifaa vya uchaguzi na imetenga kiasi cha Sh.Bilioni 82,milioni 975,laki 9,94 elfu ,na 148  kwa ajili ya kuendesha uchaguzi huo.

Kortini kwa kumshika sehemu za siri mtoto wa miaka mitatu

$
0
0
Mkazi wa Mbezi, Vicent Marseli (37), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam, akikabiliwa na shtaka la kumshika sehemu za siri mtoto wa miaka mitatu ili kujiridhisha kimapenzi.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Neema Moshi, alidai Februari 18 eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa alifanya shambulio la aibu kwa kumshika mtoto huyo sehemu za siri ili ajiridhishe kimapenzi.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na mwendesha mashtaka wa Jamhuri alisema upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Kiliwa alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya Sh 50,000 kila mmoja.

Hata hivyo, alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakaposomwa Juni 25, mwaka huu.

Serikali Yataifisha Mali Za Wahalifu Zenye Thamani Ya Tsh Bilioni 93.16

$
0
0
Na Grace Semfuko,MAELEZO
Serikali imesema kuwa kati ya kipindi cha mwaka 2013 hadi Mei 2019 imetaifisha mali za wahalifu zenye thamani ya Tsh. Bilioni 93.16 zilizokamatwa kwenye sekta za Madini, Maliasili na Sekta ya fedha (Upatu) ikiwa ni sehemu ya kudhibiti uhalifu kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Uhalifu huo unaodaiwa kukithiri katika miaka ya nyuma na ambao sasa unaendelea kudhibitwa unatajwa kuliingizia Taifa hasara ya Mabilioni ya fedha, hatua iliyoifanya Serikali kuudhibiti kwa kutaifisha mali za wahusika wa uhalifu huo.

Hayo yalibainishwa leo (Jumatano Juni 12, 2019) Jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati akifungua mkutano wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Urejeshaji wa Mali Zinazohusiana na uhalifu wenye jumla ya nchi  wanachama 16.

Samia alisema hivi sasa Serikali ya Tanzania inapanga mikakati ya kuondokana kabisa na uhalifu huo kutokana na sera ya kudhibiti Rushwa pamoja na kuanzisha mahakama maalum zitakazoshughulikia ufisadi Nchini Tanzania.

“Sisi Tanzania tunaimarisha Sera zetu za kupambana na Rushwa na Ufisadi, tunaenda sambamba na umoja wetu huu wa ARINSA hivyo tunazishauri nchi zingine ambazo zipo kwenye umoja huu na bado hazijatunga Sera na Sheria ziharakishe mchakato ili twende sawa” alisema Samia.

Kwa upande wake Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Augustine Mahiga alisema mkutano huo pamoja na mambo mengine utazungumzia mikakati ya pamoja ya kudhibiti uhalifu wa mipakani hasa kwenye udhibiti wa uingizwaji wa bidhaa haramu ikiwepo dawa za kulevya.

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Biswalo Maganga alisema mkakati wa kutaifisha mali za wahalifu umekuja kufuatia kuona vifungo gerezani kwa wahalifu hao havitazinufaisha nchi hizo na badala yake kuchukua mali zao ili kukomesha kabisa suala hilo.

Aidha alisema tayari wataalamu kadhaa wa upelelezi wa kufuatilia mali na kuzitaifisha wameshapata mafunzo na kwamba zoezi hilo linaendelea ili kuhakikisha linafanyika kikamilifu na kwa usiri mkubwa.

ARINSA ni umoja wa urejeshaji wa mali zinazohusiana na uhalifu wenye Nchi  wanachama 16 zilizopo Barani Afrika ambao kwa pamoja wanakusudia kukabiliana na uhalifu hususan kwenye mipaka ya nchi hizo.

MWISHO.  

Mgogoro Wa Uendeshaji Kinu Cha Nafaka Cha Arusha Wamalizika

$
0
0
HATIMAYE mgogoro wa muda mrefu wa uendeshaji wa kinu cha kusagisha nafaka kilichopo Arusha kati ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko na Kampuni ya Monaban Trading and Farming ya jijini Arusha umemalizika baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuingilia kati.

Kufuatia kumalizika kwa mgogoro huo na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kukabidhiwa uendeshaji wa kinu hicho, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri Kilimo, Japhet Hasunga aisimamie Bodi hiyo na kuhakikisha inaendeleza kinu hicho ili kiwe na tija kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Juni 12, 2019) wakati alipokutana na Waziri wa Kilimo pamoja na Viongozi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma. Awali kinu hicho kilikuwa kinamilikiwa na Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC).

Amesema Waziri wa Kilimo ahakikishe kuwa kinu hicho kinasagisha nafaka kwa wingi kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi na ziada ya unga utakaozalishwa kuuzwa nje ya nchi ili nchi iweze kupata faida zaidi kwa kuuza unga utaotokana na kinu hicho.

Uamuzi wa kukabidhi kinu hicho cha kusagisha nafaka kilichokuwa kikiendeshwa na Kampuni ya Monaban Trading and Farmning kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ulitolewa na Baraza la Mawaziri katika kikao kilichofanyika mwaka 2008.

Mgogoro huo wa uendeshaji wa kinu hicho ulitokea baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Monaban Trading and Farming, Dkt. Philemon Mollel kutoelewana na uongozi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kuhusu uendeshaji wa kinu hicho hali iliyosababisha Waziri Mkuu kuingilia kati.

Waziri Mkuu amesema bodi hiyo inamiliki vinu vinne vilivyopo Arusha, Dodoma, Iringa na Mwanza. Kinu cha Arusha pekee ndicho kilichokuwa na migogoro ya mara kwa mara ambayo haikuwa na utatuzi kwa muda mrefu licha ya jitihada za Serikali kutatua mgogoro huo.

“Viongozi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko waliwahi kufungiwa milango na mwekezaji aliyesaini mikataba ambayo haieleweki na akawa anaonekana anataka kukirasimisha Kinu cha Arusha kiwe mali yake na ndipo tukalazimika kuunda Timu ya uchunguzi ili kubaini uhalali wake na kuchukua hatua stahiki”


(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

Kiingereza kuendelea kuwa lugha ya kufundishia - Waziri Ndalichako

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce amesema Kiingereza kitaendelea kuwa lugha ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi ya elimu ya sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu.

Akijibu swali la mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Athuman Maige leo, Ndalichako amesema Kiingereza kitaendelea kutumika kwa sababu ya umuhimu wake kitaifa, kikanda na kimataifa kwa mawasiliano na biashara ili kuwajengea wanafunzi ufahamu na umahiri wa lugha hiyo.

“Suala la matumizi ya lugha ya kufundishia na kujifunzia ni la kisheria kama ambavyo sheria ya elimu sura 353 inavyoelekeza. Sheria hiyo inabainisha matumizi ya lugha mbili za kufundishia na kujifunzia ambazo ni Kiswahili na Kiingereza.”

“Kwa sasa Kiswahili kinatumika kufundishia katika ngazi ya elimu ya awali na msingi, vyuo vya ualimu ngazi ya cheti na vyuo vya ufundi stadi,” amesema Profesa Ndalichako.

Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi Wanachama wa SADC....RC Makonda Apewa Maagizo Mazito

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametakiwa na Waziri wa Mambo ya  Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki,  Profesa Palamagamba Kabudi kuzitafuta na  kuzitambua nyumba na ofisi zote zilizotumiwa na wapigania uhuru katika nchi mbalimbali za Afrika zilizopo Tanzania.

Profesa Kabudi ametoa agizo hilo leo, wakati akizungumza na wamiliki na wakuu wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

“Wakuu wa nchi 16 watahudhuria mkutano huu na kuleta  ombi maalumu kufanya kumbukizi ya Nyerere watakapokuwa. Hii ni fursa kwetu kuweka kumbukumbu na ku identify (kutambua) maneno yote ambao wapigania uhuru wa nchi mbalimbali walikaa.”

“Tupitie nyumba zote walizokaa mfano Jacob Zuma (rais mstaafu wa Afrika Kusini) aliishi hapa,  Sam Nujoma (Rais mstaafu wa Namibia) na wengine wengi tuzitambue hizo nyumba na ofisi zao,” amesema Profesa Kabudi.

Aidha alisema kuwa Agosti 17, 2019  Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) , ugeni aliodai pamoja na mambo mengine utafanya kumbukizi ya Julius Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi June13

Serikali Kuendelea Kutekeleza Mikakati Ya Kupiga Vita Utumikishwaji Dhidi Ya Watoto

$
0
0
Serikali imekua na mikakati mikubwa ambayo imesaidia kuwatoa Watoto katika suala zima la utumikishwaji katika kazi na mazingira mbalimbali. 

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu 
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Bungeni kuhusu maadhimisho ya siku ya kupiga vita utumikishwaji dhidi ya  

Watoto. Waziri Mhagama alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa  na Dkt. John Pombe Magufuli imekua ikichukua hatua mbalimbali dhidi ya  tatizo hilo. 

“Jamii inatakiwa kutambua maana ya utumikishwaji wa Watoto na kazi  hatarishi zinazowakabili ili kuwa walinzi wa watoto,” alisisitiza Mhagama. 

Aliongeza kuwa Watoto hawatakiwi kutumikishwa bali wasaidiwe kutimiza  ndoto zao kwa kuwaandaa kuwa raia wema na wajenzi wa Taifa la kesho. 

Alieleza juu ya Sheria na mikakati mbalimbali inayosimamia haki za Watoto ikiwemo Sheria ya elimu ambayo inataka Watoto wote kupata fursa ya  elimu, Sheria Na. 1 (2009) ambayo inalinda haki na ustawi wa mtoto,  Sheria Na. 6 (2004) ya Ajira na Mahusiano Kazini inelezea mazingira  ambayo mtoto hatakiwi kutumikishwa kazi ambazo hazipo kwa mujibu wa taratibu.

Pamoja na hilo alielezea pia juu ya mpango ya taifa wa kupiga vita ukatili  dhidi ya Wanawake na Watoto ambao umesaidia katika kuwaondoa Watoto kwenye mazingira hatarishi na Mpango Mkakati wa taifa wa kupambana na  ajira dhidi ya Watoto. 

“Ofisi ya Waziri Mkuu inasimamia viwango vya kazi na imekuwa ikisisitiza  waajiri kufuata sheria za kazi kwa kutowahusisha Watoto katika   mazingingira hatarishi au kwenye kazi zisizo na staha ambazo zinafanya   Watoto waingie kwenye utumikishwaji,” alisema Mhagama 

Aidha, Waziri Mhagama alitoa wito kwa jamii kuwapa Watoto kazi   zinazozingatia umri, ukubwa wa kazi na zinazolinda afya yao. 

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILINO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU

Ebola Yaua Uganda, Tanzania Yatoa Tamko

$
0
0
Kijana aliyekuwa na umri wa miaka mitano ameaga dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola, hii ikiwa ni kesi ya kwanza ya maradhi hayo hatari kuthibitishwa nchini Uganda.

Duru za habari zimearifu kuwa, kijana huyo alikuwa akitibiwa katika kituo kimoja cha afya mjini Kasese, katika mpaka wa magharibi wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Jana jioni, Shirika la Afya Duniani WHO bila kutoa maelezo ya kina, lilithibitisha kesi ya kwanza ya ugonjwa huo nchini Uganda.

Haya yanaripotiwa chini ya mwezi mmoja baada ya Uganda kutangaza kuwa imechukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kuzuia ugonjwa hatari wa Ebola usiingie nchini humo ukitokea nchi jirani ya DRC, hasa kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kumiminika nchini Uganda.

Hii ni katika hali ambayo siku chache zilizopita, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema karibu robo ya watu walioambukizwa Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yumkini hawajui kwamba wanaugua ugonjwa huo hatari.

Tayari Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, imeshatoa taarifa kwa wananchi wake kuchukua tahadhari za ugongwa huo.

“Tumepokea kwa tahadhari ya uwepo wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda. Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuwa ikichukua hatua za utayari (preparedness) za kukabiliana na ugonjwa huu. Wananchi wasiwe na hofu. Tutatoa taarifa kwa umma siku chache zijazo.” Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Viongozi CCM Watakiwa Kutokuwa Chanzo cha Migogoro

$
0
0
Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humfrey Polepole, amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia chama hicho kutokuwa chanzo cha migogoro na majungu badala yake wawe suluhisho kwa kufuata malengo ya chama ambayo ni kusimamia serikali na kuwaletea watanzania Maendeleo.

Ameyasema hayo  Juni 12 katika semina ya kuwafunda makatibu wa uenzi wa ngazi zote mkoani Iringa ambapo amesema kuwa chama hicho kimejengwa kwenye misingi bora ya kutumikia wananchi na kuwasikiliza ili kujua shida zao.

“Hii ni CCM mpya chini ya mwenyekiti rais John Magufuli na hana utani anataka kazi tu na wale ambao wanaona wameshindwa watupishe maana unapoacha sumu ndani kuna siku itakudhuru tunapogombana wanaoumia ni watanzania waliotupa dhamana ya kusimamia serikali ”amesema.

Amesema kuwa kwasasa mlango uko wazi na kwamba endapo kuna mtu anaona atashindwa kupelekana na kasi ya chama hicho chini ya rais Magufuli ni vyema akapisha na kuacha wanaojua kufanya kazi.

Pia amewataka viongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa huku akimtaka katibu wa itikadi na uenezi mkoani humo, Ramadhani Baraza kuendelea kuwatumikia wananchi vizuri kwa kueleza mambo mazuri yanayofanywa na serikalia ya CCM.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images