Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TAKUKURU Yatimiza Agizo la Rais Magufuli....Watumishi Hawa Kuburuzwa Mahakamani

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo Jumatatu Juni 10, 2019  imewataja askari polisi wawili na mtumishi mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliohusika na ukamataji pamoja na uzuiaji wa mizigo wa mfanyabiashara Ramadhani Ntunzwe.

Takukuru imewataja watumishi hao ni Charity Ngalawa ambaye ni mwajiriwa wa TRA makao makuu, askari Polisi PC Simon Sungu pamoja na askari polisi PC Ramadhani  Uweza wote wakitokea kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Athuman Diwani imesema watumishi hao wanatuhumiwa kwa kosa la kuomba rushwa ya Sh2 milioni kutoka kwa mfanyabiashara huyo kinyume cha kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya 2007.

Rais Magufuli Amjulia Hali Mke Wa Baba Wa Taifa Mama Maria Nyerere Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli wamemjulia hali mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere anayepatiwa matibabu jijini Dar es Salaam.

LIVE: Rais MAGUFULI Akiwaapisha WAZIRI Mpya na Kamishna wa TRA Pamoja na Kupokea Gawio Toka Airtel

$
0
0
LIVE: Rais MAGUFULI Akiwaapisha WAZIRI Mpya na Kamishna wa TRA Pamoja na Kupokea Gawio Toka Airtel

Ndugai kuwaongoza wabunge kwenda Misri kushuhudia AFCON

$
0
0
Spika wa Bunge Job Ndugai anatarajiwa kuwaongoza Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushuhudia mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) Nchini Misri.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza June 21 mwaka huu nchini Misri ambapo Tanzania imepangwa Kundi C pamoja na Nchi za Kenya, Algeria na Senegal.

Akizungumza leo Juni 10, bungeni mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Spika Ndugai amesema ataenda kushuhudia fainali hizo.

 “Na wale wa awamu ya kwanza kama siku zile nne ni chache na mimi nitalipia nitaenda na wale wa awamu ya kwanza hivyo  tunaweza kuwa pamoja,”amesema.

Akizungumzia utaratibu wa safari na gharama zake, Spika Ndugai amesema kutakuwa na awamu mbili za safari za kwenda Nchini Misri.

“Awamu ya kwanza ambayo itakuwa ya siku nne gharama zake ni Dola za Marekani 720 ikijumuisha tiketi za kwenda na kurudi, usafiri wa kwenda uwanjani na kurudi hotelini na malazi.

“Mwenyekiti wa Bunge Sc Club, William Ngeleja, anaawatangazia na kuwaombeni kwa ambao tunapenda kushuhudia fainali za AFCON nchini Misri mwaka huu tuendelee kujiandikisha kupitia kwake, Ester Matiko, John Kadutu,Venance Mwamoto, Sixtus Mapunda na Cosato Chumi wale ambao tungependa kwenda.

“utaratibu mzima wa safari umeishatolewa kupitia mitandao yetu ya bunge gharama za safari unachagua mwenyewe kama unataka kwenda awamu mbili ama moja,”amesema Ndugai.

Amesema awamu ya pili ambayo itakuwa ya siku sita gharama zake ni dola za Marekani 770 kwa kichwa.

“Awamu ya pili ni ya siku sita hii gharama zake ni dola 770 tu kwa hiyo ukitaka kukaa siku zote ni sawa tu, ‘Atleast’ awamu mojawapo waheshimiwa Wabunge tunaweza tukashiriki, ”amesema.

Aidha Spika amewaomba Wabunge kwenda kuiunga mkono Taifa Stars ili wachezaji wajione wanadeni kwa taifa.

“Tunaomba sana waheshimiwa Wabunge tuunge mkono sana timu yetu ni miaka mingi sana hatujafika AFCON kwahiyo wachezaji wakiwa wanacheza wanaona wabunge wamekuja kuwaunga mkono naamini itawapa  nguvu kubwa zaidi,”amesema.

Askari Polisi wawili na mfanyakazi mmoja wa TRA Waliotajwa IKULU Wapandishwa Mahakamani

$
0
0
Askari Polisi wawili na mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), waliotajwa na mfanyabiashara Ikulu kwamba wamemdai rushwa na kuzuia mzigo wake tangu mwaka 2016 wamepandishwa kizimbani.

Mfanyabiashara huyo aliwataja katika mkutano wa Rais Dk. John Magufuli na wafanyabiashara uliofanyika Juni 7, mwaka huu ikulu jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Juni 10, kwa tuhuma za kushawishi kupewa rushwa ya Sh milioni mbili na mfanyabiashara Ramadhan Ntuzwe.

Washtakiwa ambao ni askari na namba zao ni H 4086 PC Simon Sungu, H 4810 PC Ramadhan Uwezi wa Kituo cha Polisi Osterbay na Mfanyakazi wa TRA, Charity Ngalawa.

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Sophia Gula aliwasomea washtakiwa shtaka linalowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Amedai washtakiwa wanashtakiwa kwa kushawishi rushwa, wanadaiwa Oktoba 29, 2016 maeneo ya Kimara mwisho, wakiwa wafanyakazi wa TRA na Polisi walidai rushwa ya Sh milioni mbili kutoka kwa Ntuzwe.

Washtakiwa wanadaiwa walidai rushwa hiyo kama kishawishi cha kuruhusu mzigo wake ambao unadaiwa ulikadiriwa kodi ndogo jambo ambalo lilikuwa chini ya wakubwa wao.

Washtakiwa walikana kutenda makosa hayo, Jamhuri walidai upelelezi haujakamilika na hapakuwa na pingamizi kwa washtakiwa kupata dhamana.

Mahakama ilikubali kuwapa dhamana kwa masharti ya kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni tano, washtakiwa walitimiza masharti wako nje kwa dhamana.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt.Agnes Kijazi ajitosa kinyang’anyiro cha umakamu wa Tatu wa Rais WMO

$
0
0
Na. Christopher Philemon, Monica Mutoni-Geneva. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt.Agnes Kijazi yupo nchini Uswisi –Geneva kwenye Mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-18 Congress) .Mkutano huu hufanyika kila baada ya miaka 4 ambapo mwaka huu unafanyika jijiji Geneva kuanzia tarehe 3- 14 juni ,2019.

Katika Mkutano huo utafanyika uchaguzi wa viongozi wakuu wa WMO ,ambao ni pamoja na Rais ,Makamu wa Kwanza wa Rais ,Makamu wa Pili wa Rais ,Makamu wa Tatu wa Rais na viongozi wengine wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani(WMO).
 
Tanzania kupitia Dkt Agnes Kijazi amejitosa katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya makamu wa tatu wa Rais wa WMO. Dkt Kijazi anaungwa mkono na wakuu wote wa taasis za hali ya hewa barani Afrika na azimio hili lilipitishwa katika Mkutano wa Mawaziri wenye Dhamana ya Huduma ya Hali ya Hewa Barani Afrika (African Ministerial Conference on Meterology - AMCOMET) tarehe18 - 23 Februari, 2019 Jijiji Cairo Misri  ambapo Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye ambaye kupitia hotuba yake alifanikiwa kuwaombea wajumbe  kumpitisha Dkt Kijazi kama mgombea pekee barani Afrika.

“Kutokana na umuhimu wa nafasi tunayoiomba kwa Taifa na Afrika kwa ujumla, na hasa ukizingatia heshima ambayo tumepewa na Nchi za Afrika kuweka azimio la kumuunga mkono Dkt Kijazi, ili achaguliwe katika nafasi ya makamu wa tatu wa rais ambayo ina wagombea wengine kutoka mabara mengine, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Kushirikiana Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,zinazendelea kushiriki katika kuomba wajumbe  kutoka nchi mbalimbali  hapa mjini Geneva kumpigia kura Dkt.Kijazi ili ashinde nafasi hiyo” alisema Nditiye.

Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iliandaa hafla ya kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania kwa kuwaalika wajumbe mbalimbali wa mkutano wa 18 wa WMO.

 Aidha katika  salamu za viongozi wakuu wa WMO akiwepo Rais wa sasa wa WMO  Bw David Grimes  aliwaomba wajumbe kumuunga mkono Dkt Kijazi kutokana na uchapa kazi wake, kauli ambayo ilirudiwa pia na Katibu Mkuu wa WMO Prof. Petteri Telaas alisema pamoja na utendaji uliotukuka wa Dkt Kijazi, bado shirika hilo halijawahi kupata kiongozi kike kwenye nafasi ya juu kama hiyo hivyo akawaomba pia wamuunge mkono.
 
MWISHO

Waziri Mkuu Majaliwa Afungua Michezo Ya Umiseta Kwenye Uwanja Wa Nangwanda Mjini Mtwara

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagizahalmashauri zote za majiji na miji zihakikishe kuwa kuanzia sasazinatenga maeneo ya michezo na burudani kila zinapopima viwanja.

“Naagiza kuanzia sasa, maeneo yote yanayopimwa na halmashauri na miji yote nchini, lazima yazingatie uwepo wa maeneo ya michezo na burudani,” amesisitiza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Juni 10, 2019)wakati akifungua mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za msingi na sekondari Tanzania, katika Uwanja waNangwanda Sijaona mkoani Mtwara. Zaidi ya wanafunzi 5,400 wanashiriki mashindano hayo.

Pia, amezitaka Halmashauri ziweke mpango madhubuti wa kuyaendeleza maeneo ya michezo na burudani sambamba na miundombinu inayozingatia mahitaji ya wote bila kubagua.

Amesema katika baadhi ya maeneo kumekuwepo na uhaba wa viwanja vya michezo kwa sababu ya mipango miji isiyozingatia mipango endelevu ya sekta mbalimbali.

Hivyo, Waziri Mkuu ameagiza yafanyike marekebisho na hatua za haraka ili kutoa fursa ya ukuaji wa michezo na kusaidia wananchi kushiriki michezo, mazoezi na kupata burudani.

Amesema ifikapo Septemba 30, 2019, kila halmashauri iwe imefanya mapitio ya maeneo yote yaliyokuwa yamepimwa kwa matumizi ya huduma maalum ikiwemo michezo, burudani, shule na ibada na kutoa taarifa kama yanatumika kwa ajili hiyo au vinginevyo.

Wakati huo huo,Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia irudishe na iimarishe mchepuo wa Elimu kwa Michezo Chuo cha Ualimu Butimba ili kupata wataalam zaidi.

“Halmashauri ziendelee kuwaruhusu walimu mbalimbali nchini kuhudhuria mafunzo ya michezo katika chuo cha Mendeleo ya Michezo Malya ili kupunguza uhaba wa watalaam wa michezo katika shule mbalimbali na nchini kwa ujumla.”

Waziri Mkuu amesema michezo ni muhimu kwa wanafunzi kwa kuwa itawaepusha vijana na makundi yasiyofaa yakiwemo matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine visivyoendana na maadili ya Kitanzania.

Amesema michezo itawawezesha vijana kuwa na afya bora na kufanya vema katika masomo yao kwa kuwa ili waweze kusoma vema ni sharti afya zao ziwe njema. Pia sanaa itasaidia katika kuutambulisha utamaduni wetu ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.

“Kwa hiyo, ni vema tukatambua kuwa michezo na sanaa ni sehemu ya elimu bora. Hivyo, ni muhimu kutekeleza dhana ya elimu ya michezo ili tuweze kufikia maendeleo tarajiwa.”

 Kadhalika, Waziri Mkuu amesema sambamba na michezo iliyozoeleka, pia wanaweza kuibua michezo yao ya asili ambayo itautambulisha utamaduni wetu. “Nitoe wito kwa shule zetu, ziendeleze ubunifu wa kuibua vipaji vya sanaa na michezo ya asili katika maeneo yetu kwa lengo la kuenzi utamaduni wetu.”

Akizungumzia kuhusu mashindano ya mwaka huu ambayo yameshirikisha wanafunzi wengi zaidi wenye mahitaji maalumu, Waziri Mkuu amesema waendelee kuwahusisha wanafunzi wote katika michezo, sanaa na burudani bila kujali aina ya ulemavu walionao.

Amesema jambo hilo ni muhimu kwa kuwa vipaji vipo kwa wote na fursa ndizo zitakazowawezesha kuonesha vipaji hivyo na kuvikuza.

Waziri Mkuu amewasisitiza wadau wote wa shule za msingi, sekondari, vyuo, sehemu za kazi na wizara, waweke mipango ya kudumu ya kuwashirikisha watu wenye mahitaji maalumu katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi bila ubaguzi wowote.

“Hakikisheni baadhi ya vikwazo katika kushirikisha watu wenye mahitaji maalumu kwenye michezo vinaondolewa. Vikwazo hivyo ni pamoja na kutokuwepo kwa mipango endelevu katika maeneo mbalimbali na uwepo wa mitazamo hasi ya baadhi ya walimu, wazazi na viongozi katika maeneo yao dhidi ya uwezo wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.”

Aidha, Waziri Mkuu ametuamia fursa hiyo kuupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuwa mmoja kati ya Mikoa ya mfano katika kutekeleza agizo lake la mwaka jana alilolitoa kupitia michezo hiyo la kuanzishwa kwa shule maalumu za michezo.

Mkoa wa Simiyu umejenga Shule ya Sekondari itakayokuwa kituo cha kukuza vipaji vya wanafunzi katika michezo. “Naagiza mwakani wanafunzi wote walioonesha vipaji katika michezo watakaofaulu Mtihani wa Elimu ya Msingi wapangwe katika shule hiyo ili wakakuze vipaji vyao.”

Amesema bila ya kuwa na mipango ya kulea na kukuza vipaji kutoka ngazi za chini Taifa haliwezi kupata mafanikio katika michezo nchini. Kwani katika kipindi ambapo michezo hiyo ilisitishwa kiwango cha michezo ya aina mbalimbali kilikuwa chini sana.

“Tangu tumerejesha shughuli za michezo katika shule zetu tumekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kupata wachezaji wanaofuzu kucheza soka la kulipwa kwenye viwango vya kimataifa kama Mbwana Samatta (Genk –Belgium), Simon Msuva (Difaa El Jadid – Morocco), “

Wengine ni Shiza Kichuya (Enppi –Misri), Thomas Ulimwengu (JS Saoura – Algeria), Hamid Mao (Petrojet – Misri), Adi Yusuph (Blackpool –England), Hassan Kessy (Nkana – Zambia), Yahya Zaydi (Ismaily –Misri), Shabani Chilunda, (Tenerife – Hispania) Rashid Mandawa (BDF- Botswana), Farid Mussa ( Tenerife– Hispania).

Waziri Mkuu amesema pamoja na mafanikio yaliyopatikana, jitihada zaidi zinahitajika ili kuwa na maendeleo ya kutosha katika shughuli za michezo nchini.

Hivyo, Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI wakamilishe tathmini ya shule 56 za Serikali zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya michezo.

Ufunguzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Maafisa Elimu kutoka mikoa yote nchini, walimu wa michezo pamoja na Maofisa wengine wa Serikali.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JUNI 10, 2019.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya LeoJumanne ya June 11


Shahidi kesi ya Malinzi adai fedha za udhamini zilitumika bila nyaraka za uthibitisho

$
0
0
Aliyekuwa Mkaguzi wa Ndani wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL), Richard Magongo, amedai baadhi ya fedha zilizotolewa na TBL kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kwa ajili ya kudhamini timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ zilitumika bila kuwa na nyaraka za uthibitisho wa matumizi.

Magongo amedai hayo jana Juni 10 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde,  wakati akitoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili kutoka Takukuru, Leonard Swai.

Alidai TBL iliingia katika mkataba na hilo wa kuidhamini Taifa Stars mwaka 2012 kwa miaka mitano ambapo jumla fedha za udhamini zilikuwa Dola za Marekani, 10,000,000.

Shahidi anadai walikuwa wakifanya ukaguzi wa fedha hizo kila inapofika robo mwaka na taarifa za ukaguzi zilibainisha kwamba fedha za udhamini zilitumika bila kuwa na nyaraka za kuthibitisha matumizi, kulikuwa na matumizi ambayo hayakuwa ndani ya mkataba na mapungufu yalikuwa mengi kiuhasibu na kiutawala kwa TFF katika utekelezaji wa mkataba.

“Matumizi ambayo hayakuwa na nyaraka za uthibitisho ni mengi, mfano marejesho ya mikopo kwa Jamal Malinzi hayakuwa na nyaraka za kuonyesha lini aliikopesha TFF.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Meneja wa Ofisi TFF, Miriam Zayumba, Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya kula njama, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa dola za Marekani 173,335.

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wanaendelea kusota rumande kwa sababu wanakabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Shehena Ya Magunia 455 Ya Mkaa Yakamatwa Kahama Ikisafirishwa Kwa Lori Kuelekekea Jijini Mwanza

$
0
0
SALVATORY NTANDU
Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwa kushirikiana na Vyumbo vya Ulinzi wilayani Kahama mkoani Shinynga wamefanikiwa kukamata lori aina ya scania  lenye namba za Usajili T 656 AQC  likiwa limebeba shehena ya magunia ya mkaa 455 uliovunwa kwa njia isiyohalali.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Kahama, ANAMRINGI MACHA amesema gari hilo limekamatwa na vyombo vya usalama baada ya kubaini kuwa mkaa huo ulikuwa hauna nyaraka zinazoonesha kuwa ulivunwa kwa uhalali.

Amesema serikali itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu watakaobainika kuvuna mazao ya misitu kiholela kwa manufaa yao binafsi jambo ambalo linasababisha uharibifu wa Mazingira.

MACHA amefafanua kuwa ni vyema watu wanaotaka kuvuna au kusafirisha mazao ya misitu wakafuata sheria na taratibu za uvunaji kwa kupata vibali kutoka ofisi za (TFS) ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwemo kutaifishiwa mali zao.

Kwa upande wake Meneja wa (TFS) Kahama JUMA ALLY amesema  Mmiliki wa lori hilo amejitokeza na kukubali kulipa faini ya zaidi ya shilingi milioni 24 ili aweze kupatiwa gari lake ambapo mpaka sasa anaendelea na taratibu za malipo.

Sanjari na hilo ALLY amesema kwa Mujibu wa sheria namba 14 ya mwaka 2012 kifungu namba 95 kinampa mamlaka ya kufanya tathimini ya mazao ya misitu ambayo yamekamatwa na kumlipisha faini mmiliki wa gari hilo.

Amefafanua kuwa   baada ya kukamilisha taratibu za malipo Mkaa huo gunia 455 zitataifishwa na serikali huku taratibu za kumkabidhi gari lake zitafuata.

Nae ELIAS NKEYE mmliki wa Lori hilo amesema atalipa faini hiyo ili kukomboa gari lake na kusema kuwa dereva na utigo wa gari hilo hawajulikani walipo na mmiliki wa magunia pia hakuweza kujulikana mara moja.

Nimeambatanisha na picha mbili

Mwisho.

Marekani Yakasirishwa na vitisho vya Iran

$
0
0
Marekani haijafurahishwa na vitisho vilivyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif katika mkutano na mwenzake wa Ujerumani Heiko Maas mjini Tehran. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni ya Marekani amesema kuwa Iran inachagua moja rahisi tu, ijionyeshe kuwa nchi ya kawaida au ishuhudie uchumi wake ukisambaratika. 

Zarif aliituhumu Marekani kwa kufanya vita vya kiuchumi kutokana na vikwazo ilivyoiwekea Iran na akaonya kuwa wale wanaounga mkono vita wasitarajie kuwa salama. 

Maas anataka kuyaokoa makubaliano ya nyuklia na Iran, lakini hakupiga hatua zozote za maana wakati wa ziara yake nchini humo. 

Maas alisema jana kuwa Ujerumani itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa mvutano hauongezeki kati ya Marekani na Iran.

Iran yazindua mfumo wa makombora wa Khordad 15

$
0
0
Iran imezindua mfumo wa kujilinda kwa makombora unaoweza kulenga shabaha sita za adui kwa wakati mmoja.

Mfumo huo wa makombora uliopewa jina la Khordad 15 umezinduliwa mbele ya Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Amir Hatami. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Brigedia Jenerali Hatami amesema kuwa, mfumo wa makombora wa Khordad 15 una uwezo wa kugundua ndege za kivita na droni kutoka umbali wa kilomita 150 na kuzifuatilia katika umbali wa kilomita 120.

Ameongeza kuwa mfumo huo wa makombora aidha una uwezo wa kugundua maeneo ya siri na kuyasambaratisha katika umbali wa kilomita 45.

Waziri wa Ulinzi wa Iran ameeleza pia kwamba mfumo wa ulinzi wa Khordad 15 unatumia makombora ya Sayyad 3; na una uwezo wa kugundua, kusambaratisha na kutungua shabaha sita kwa wakati mmoja.

Iran imeeleza kuwa uwezo wake wa kijeshi ni kwa ajili ya kujilinda na si tishio kwa nchi nyingine.

Wabunge Washauriwa Kuwekeza Kwenye Elimu Badala ya Bodaboda na Noah

$
0
0
Spika  wa Bunge, Job Ndugai, ametoa wito kwa wabunge kuwekeza kwenye sekta ya elimu badala ya magari aina ya Noah au pikipiki, akieleza kuwa wanamtia aibu.
 
Ndugai alitoa kauli hiyo jana bungeni jana alipokuwa akitangaza wageni wa Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza (CCM), ambao ni wanafunzi waliofanya vizuri kidato cha nne na darasa la saba mwaka 2018.

Wanafunzi waliotambulishwa ni waliomaliza kidato cha nne mwaka 2018 katika Shule ya Sekondari Sunshine na kupata ufaulu wa daraja la kwanza na pili.

"Pia kuna wanafunzi 59 waliomaliza darasa la saba mwaka 2018 kutoka Shule ya Msingi ya Anne Marie Academy ya jijini Dar es Salaam, kwenye wilaya, hii shule ya ilikuwa ya kwanza na kimkoa ilikuwa ya kwanza na kitaifa ilikuwa ya sita," alisema.

Kutokana na ufaulu huyo, Spika Ndugai alimpongeza Rweikiza ambaye ni mmiliki wa Shule ya Anne Marie kwa kuimarisha elimu.

"Haya ndo mambo ambayo wabunge tunatakiwa tufanye, siyo mbunge unamiliki Noah, unamtia aibu Spika, kila siku unaonekana trafiki huko, mbunge unamiliki bodaboda!

"Tuvuke jamani, bodaboda zikikamatwa, unampigia Spika, Spika bodaboda zangu zimekamatwa huku," Ndugai alisema na kuibua vicheko bungeni.

Kiongozi huyo wa Bunge alitoa rai kwa watunga sheria hao kuwekeza kwenye mambo makubwa, akisema wanapaswa "kuvuka kidogo kwenye uwekezaji".

TECNO Yazindua Boda La Spark 3

$
0
0
Kampuni ya simu ya TECNO mobile inawakaribisha wateja wake kununua simu mpya iliyozinduliwa hivi karibuni aina ya TECNO SPARK 3 na kujishindia zawadi kemkem ikiwemo pikipiki mpya.

Promotion hiyo iliyopewa jina la boda la spark 3 inaanza kwa mkoa wa dar es salaam kisha kuenea mikoa mingine hapo baadae, mteja atakaenunua TECNO spark 3 kwenye maduka maalumu ya TECNO yenye promotion hiyo  atapewa nafasi ya kuondoka na zawadi za papo kwa papo  kama power bank yenye mAh 5000 na pamoja data cable,

TECNO Spark 3 ni simu ya kijanja yenye uwezo mkubwa wa kupiga picha pamoja na kufanya vitu mbali mbali mitandaoni   imezinduliwa takribani mwezi mmoja ikiwa ndio simu inayofanya vizuri zaidi kwa upande wa simu janja za kipato cha kati.

TECNO SPARK 3 ina ubora wa kamera yenye megapixel 13, huku mtumiaji anapata nafasi ya kuifadhi vitu vyake kwenye GB 16  za memory  ya ndani na muonekano wake ni wakijanja na ndio maana inafanya vizuri sokoni,

Angalia zaidi hapa.

Mshindi wa pikipiki atapatikana mwisho wa mwezi wa sita kwa njia ya bahati nasibu itakayo chezeshwa live kupitia mitandao ya kijamii ya TECNO mobile hasa Instagram : https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/

Fika maduka ya TECNO yafuatayo ili kushinda  zawadi kemkem unaponunua simu hii ya SPARK 3, TECNO exclusive mobimart , TECNO exclusive mashreq, TECNO excuslive inorbit, TECNO exclusive hyatt, TECNO smart hub china plaza, maduka haya yanapatikana msimbazi kariako na mtaa wa agrey  lakin kwa upande wa mtaa sa samora posta lipo duka  TECNO Experience centre huku upande wa mlimani Duka la TECNO smart hub,



Wizara ya Ujenzi Yasahauriwa kuongeza kilo za mizigo kwenye boti

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameitaka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kuangalia  namna ya kuongeza kilo zinazopimwa kwa abiria wanaotaka kusafiri na boti kwenda Zanzibar kutoka  kilo 20 za sasa.

Ndugai amedai kwamba kilo hizo ni ndogo hivyo iko haja ya kuliangalia upya suala hilo la mizigo kwani kilo 20 hata begi la mwanafunzi tu linafikisha , hivyo basi  liangaliwe upya ili kuondoa adha kwa wasafiri.

Kauli hiyo ya Spika imekuja baada ya kujibiwa swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Maryam Salum Msabaha, kudai kuwa kuna changamoto bandarini na kwamba hata kilo 10 zinatozwa fedha hali inayosababisha malalamiko kwa wananchi.

Mbunge huyo alihoji ni vigezo gani ambavyo vinatumika kwa mizigo ya biashara na mizigo binafsi kwa wasafiri.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa, alisema vigezo vipo mwongozo wa tozo TPA na kwamba tatizo linaonekana ni uelewa.

"Niwaelekeze Bandari watoe elimu ya kutosha kwa wananchi wanaotumia usafiri kwenda Zanzibar ikiwamo hili la uzito wa kilo 21 na kuendelea ndio unatakiwa kutozwa, sio nia ya serikali kuona wananchi wake wanalalamika," alisema.

Kufuatia majibu hayo, Spika Ndugai, alisema kama kweli kilo 21 ndio kiwango cha chini ipo haja kuangalia kwenye boti.

"Maana kilo 20 hata sanduku la mwanafunzi linazidi, hata baadhi ya mashirika ya ndege yanatoa zaidi ya kilo 20, sasa kwenye boti kilo 20 ni kidogo sana."

Aliongeza "Ipo haja ya kuangalia kama sio sheria ni kanuni tu...Mtu akibeba mihogo mitatu kilo 20 tu anakuwa ameshavuka kwa hiyo tuliangalie, hawa wenzetu wanaotoka Zanzibar wapate raha kidogo na imekuwa kero kwa wananchi serikali iliangalie hili."

Katika swali la msingi, Mbunge huyo alisema abiria wanaokwenda Zanzibar kwa boti hulipishwa ushuru wa Bandari kwa mizigo hata kama boksi la kilo 10 au kilo 20 za mchele kwa Sh. 9,750.

"Je, ni mizigo gani ambayo abiria anapaswa kulipia ushuru huo wa Bandari (Wharfage)," alihoji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Kwandikwa alisema TPA huikusanyi tozo yoyote kwa abiria ambao wana vifurushi binafsi vyenye uzito au ujazo mdogo wanaotumia Bandari kwenda Zanzibar kwa boti eneo la 'Baggage room.

Aidha, alisema abiria wanaotumia Bandari kwenda Zanzibar kwa boti ambao hutozwa ushuru katika eneo la 'Bagage room' ni wale tu wanaokuwa na mizigo mikubwa tena kwa madhumuni ya kibiashara.

Alitoa wito kwa wateja wote wanaotumia Bandari kwenda Zanzibar kwa boti wahakikishe kuwa mizigo yao inapimwa kabla ya kupakiwa ili wajue uzito wake unaostahiki kutozwa ushuru.

Rais Magufuli Ataja Sababu za Kumtumbua Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere

$
0
0
Rais Magufuli ametaja sababu za kumng’oa Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere, huku akitoa pole kwa walioteuliwa kushika nyadhifa hizo.


Rais Magufuli alitaja sababu hizo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni ambao ni Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, Kamishna Mkuu wa TRA, Edwin Mhede na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, Kichere.

Katika mkutano huo, Rais Magufuli alishuhudia Kampuni ya Bharti Airtel ikiikabidhi serikali gawio la Sh. bilioni tatu la miezi mitatu kuanzia Aprili pamoja na fedha binafsi iliyotolewa na mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Sunil Mittal, dola za kimarekani milioni moja (Sh. bilioni 2.2).

Akitaja sababu za kuwaondoa kwenye nafasi zao Kakunda na Kichere, Rais Magufuli alisema: “Tutaambizana maneno mazuri mazuri, lakini maneno mazuri hayasaidii, ukitaka maneno mazuri kaelezwe na mume wako, mke wako basi, lakini sisi tunataka matokeo mazuri basi,” alisema.

Rais Magufuli alisema jukumu lake ni kuteua ili kusudi nia ya Watanzania wanayohitaji ikatimie.

“Ninapotengua mahali siyo kwamba wewe ninakuchukia, nakupenda tu na ninakupongeza mheshimiwa Joseph Kakunda kwa kuja, huku ndiko kukomaa kisiasa, hizi kazi ni muda mfupi, maisha yenyewe ni ya muda mfupi, hakuna kazi ya kudumu,” alisema.

Alisema, “Lakini amejitoa amekuja, safi sana lakini ni ukweli kwenye wizara hakuisukuma ninavyotaka, ni mimi ninataka matokeo na Watanzania walionichagua wakatupigia kura wanataka kuona utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.”

“Changamoto za wafanyabiashara kwani kulikuwa na ubaya gani, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Waziri mwenyewe siwangekuwa wameshapanga mikutano wa wafanyabiashara, palikuwa na dhambi gani? Nani angewakataza? kwamba leo tunazungumza na wafanyabiashara wa Kanda ya Ziwa, leo Kanda ya Kaskazini, leo Kusini, nisikie shida na changamoto zao.”

Rais Magufuli alisema: “Wanasema hawajawahi kumuona, hata ningeuliza hata Manyanya (Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Viwanda) nikasema labda hawajawahi kumuona, kwa sababu Watanzania siyo wanafiki,” alisema.

Kuhusu korosho, Rais Magufuli alisema wamefanya biashara hiyo zaidi ya tani 223,000 na kuhoji ni tani ngapi zimeshauzwa.

“Wizara inaitwa Wizara ya Viwanda na Biashara ni biashara gani inafanya? Wizara ya Kilimo imetimiza wajibu wake, imenunua, wanajeshi wametimiza wajibu wao wamesomba korosho yote wameweka kwenye maghala, Wizara ya Biashara inafanya nini? Ipo tu, korosho zimekaa,” alihoji.

“Wakati huo Tanzania ilikuwa ndiyo wazalishaji peke yetu, tumesubiri hadi mwezi wa tatu mpaka wa nne ukaingia nchi nyingine za Benin, Nigeria, Cote d’Ivoire nazo zikazalisha bado hatujauza, wapo tu, sasa unakuwa unajiuliza wa nini? Kupeperusha bendera barabarani? Haiwezekani,” alisema.

Rais Magufuli alimwambia Bashungwa kuwa inawezekana wamempongeza, lakini alifikiri wangempa pole kwa sababu akiona mambo hayaendi atamtengua.

“Kwa sababu nitaangalia yale ambayo hayaendi, nikiona hayaendi ninatengua nasema ukweli, Prof. Palamagamba Kabudi (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki) na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, wamezungumza tu hapa hawataki kusema, lakini kama ni ‘pumbavu’ kwenye simu wametukanwa mno waulizeni,” alisema na kuongeza:

“Wananizidi umri, lakini neno pumbavu linakuja tu haraka haraka, ndiyo ukweli kwa sababu hii kazi siyo ya kubembelezana, lazima tuipeleke kijeshi, mwanajeshi usiposonga mbele kupigwa risasi na mwenzako siyo tatizo, mpo kwenye vita… hatuwezi kukawa na vita halafu tukawa tunabembelezana na kupeana maneno mazuri tu, lazima tubadilike, wanaotuangalia hawana muda wa kusubiri.”

Rais Magufuli alisema Wizara ya Viwanda na Biashara wamebangua tani 2000, nyingine wanasubiri atelemke nani ndiyo waziuze.

“Na una waziri pale wa biashara ana vyombo vyote vya kufanya biashara nikitakiwa nimpandie kutoka juu mpaka chini, pamoja na wewe Muhende ulikuwa uende huko huko, ukienda kafanye kazi usibembeleze mtu usimchekee mtu nafuu wakuchukue mimi ninayekuteua nikusimamie kinyume na hapo utakwenda kunusa tu pale urudi Karagwe,” alimweleza waziri mpya.

Rais Magufuli alimtaka waziri huyo yale ambayo yamekaa yatatuliwe, viwanda vilivyoshindwa kuendelezwa visiorodheshwe tu, vitafutiwe watu wavichukue.

“Kiwanda kama cha Mbeya cha nguo kinakwenda kubadilishwa kiwe cha pipi, hakiwezekani, tunaonekana tunakula pipi tu, zipo changamoto nyingi kashirikiane na wenzako kuzitatua,” alisema.

Akigeukia kilichomwondoa Kichere, Rais Magufuli alisema Waziri Mpango amezungumza alivyokuwa pale Kamishna wa TRA, aliipandisha kutoka Sh. bilioni 850 hadi trilioni 1.3.

“Nikampandisha cheo kutoka TRA akawa Waziri wa Fedha, sasa wengine mnaokwenda mnasimamia hapo hapo kana kwamba ni fomula, lakini tatizo malalamiko ni mengi na hamchukui hatua, kama kuna ujumbe mfupi nimekutumia kamishna uliyeondoka yawekezana zinazidi 20 au 30 zingine nilikuwa natuma saa nane za usiku, nyingine saa tisa na nyingine saa kumi kwa sababu watu wanapolalamika ninamtumia na jamaa huyu ni kama diplomat (mwanadiplomasia) anasema nimepoka mheshimiwa,”

Aliongeza, “Ukifuatilia hakuna matokeo, ndiyo ukweli, mimi huwa sisahau ndiyo dhambi niliyonayo, haiwezekani mkurugenzi wako wa kukadiria anatoa makadirio ya kijinga kwa wafanyabiashara upo unamwangalia tu wakati una nguvu unashindwa kuitumia, unaona makusanyo ya kodi ya ndani yanashuka, labda huyu wa sasa imepanda kidogo, lakini hakuna hatua inayochukuliwa.”

Rais alisema: “Unaona kuna wafanyabiashara wanapakia mizigo wanaiandika inakwenda Tunduma hadi nchi jirani, wakifika Tunduma wanagongewa mihuri wanarudi kuishusha wakati barabara yote TRA, lori linatembea kilometa 1,300 linasema linakwenda nchi jirani wanachukua nyaraka wanagonga mpakani wanarudi, kama gharama mtu ameamua kusafirisha hadi Tunduma anarudi halafu amehonga za kugonga muhuri, zingejumlishwa zote angetelemsha mizigo yake hapa si mngemsaidia atumie mafuta vizuri.

Rais Magufuli alibainisha kuwa kuna mwekezaji alikuja na vifaa vyake anataka kuchimba dhahabu, lakini vimekaa zaidi ya mwaka alikuwa kiasi kidogo akaongezewa zaidi.

“Badala ya kuangalia huyu atawekeza hiki atatoa ajira na serikali itapata mapato kutoka kwenye dhahabu, utafikiri TRA wote hawakusoma, ndiyo maana nikasema siwezi, ndio maana siku ile walivyokusema nakuuliza unasema hujui unamwangalia mtu wa nyuma yako utamwangalia mpaka lini ukikuta hawapo, nafuu utoke na wewe hapo hapo,” alisema.

Rais Magufuli alimwambia Kichere kuwa amempeleka Njombe akajaribu ukatibu tawala na endapo akiusimamia vibaya atamtoa.

Aliwambia kuwa kuna watu wamebobea pale TRA na kumtaka akawakamate ili kodi ipatikane.

“Hakuna nchi duniani iliyoendelea bila kodi, niache kuwalipa mishahara si nitawakuta Ikulu wamesimama, usicheke na mtu, ni sawa na useme usiende mbinguni tutakuombea wote tunaofaidi utakwenda kwa nguvu tutakusukumiza Watanzania wote milioni 55 uingie mbinguni,” alisema.

Pia alimtaka akashirikiane na wafanyabiashara ili wampe taarifa nyingi na wale walioghushi siku za nyuma kutokana na mazingira akakae nao waseme wanaweza kulipa kiasi gani, kwa sababu anayo mamlaka ya kusamehe asilimia fulani.

Kuhusu watumishi wanaokwenda kwa wafanyabiashara kuwapa makadirio makubwa na kusema wametumwa juu, amemtaka asiogope kuwafukuza, awashike na kuwapeleka mahakamani.

“Kama unawafanyakazi 1000, halafu 200 wakaishia kufukuzwa na kwenda mahakamani sawa tu, lakini ukiwa mtaratibu watakukaribisha na siku ukiingia ofisini watakuletea au karibu wote watakuita bosi hata kama naye ni bosi achana na sherehe, jana nimekutumia ujumbe wa mtu analalamika, kabla sijakuapisha,” alisema.

Alisema kuna makamishna wa TRA katika mipaka, ambapo mpaka wa Rusumu unafanya vizuri lakini Tunduma na Sirari hakufai.

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

$
0
0
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. 

Simu:  +255745495181 au 0682644040  

www.tumainitibaasili.co.tz

Mahakama Yaamuru Wema Sepetu Akamatwe

$
0
0
Muigizaji Wema Sepetu anayekabiliwa na shtaka la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika  mtandao ya kijamii wa Instagram,ameshindwa kufika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili na hivyo mahakama hiyo imetoa amri ya msanii huyo kukamatwa

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde baada ya mshtakiwa kushindwa kufika mahakama kusikiliza kesi inayomkabili.

Kabla ya kutoa uamuzi huo wakili wa Serikali,  Silyia Mitanto amedia kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kusikiliza ushahidi lakini Wema na mdhamini wake wote hawakuwepo mahakamani.

Baada ya kueleza hayo, Ruben Simwanza ambaye ni wakili wa Wema amesema mteja wake alikuwepo katika mahakama hiyo lakini aliugua tumbo na kulazimika kuondoka.

Baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, hakimu Kasonde amesema, “Kama amekuja mahakamani halafu akaondoka bila kutoa taarifa, mahakama itajuaje kama alikuja? Alishindwa nini kutoa taarifa mahakamani.”

Baada ya kueleza hayo hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 4, 2019 huku akitoa hati hiyo ya Wema kukamatwa.

Wakimbizi 66,148 Warudishwa Nchini Kwao

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema wakimbizi 66, 148 kutoka nchi mbalimbali wamerejeshwa katika nchi zao kati ya mwaka 2017 na Aprili 2019, wakiwemo 31,643 wa Burundi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Masauni, Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la  mbunge wa Viti maalum (CUF), Rukia Kassim Ahmed aliyetaka kujua ni lini Serikali ya Tanzania itawarejesha nyumbani wakimbizi waliojaa katika magereza mbalimbali nchini.

Masauni amesema Mkoa wa Kigoma ndio una magereza zenye idadi kubwa ya wakimbizi, “Wapo 91 na kati yao wafungwa ni 38 na mahabusu 53. Wakimbizi ambao wamefungwa gerezani wanarejeshwa katika nchi zao za asili baada ya kumaliza kutumikia vifungo vyao.”

Serikali Yaandaa Mwongozo Wa Msamaha Wa Matibabu Kwa Makundi Tofauti Yasiyokuwa Na Uwezo

$
0
0
Na.Faustine Gimu,Dodoma
Serikali kupitia wizara afya ,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto imeandaa mwongozo wa msamaha kwa makundi tofauti yasiyokuwa na uwezo ikiwa ni pamoja kundi la watu wagonjwa sugu ikiwa ni pamoja na selimundu

Hayo yamesemwa  Juni 10 ,2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii ,jinsia,wazee na Watoto,Dokta Faustine Ndugulile,wakati  akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Taska Mbogo aliyehoji mpango wa Serikali wa kuwasaidia wagonjwa wa Selimundu[Sickle cell] juu ya kupata matibabu bure.
 
Katika Majibu yake,Mhe,Ndugulile amesema wagonjwa wa Selimundu wanahitaji matibabu mfululizo kwani huwa wanapata maumivu na madhara  ya ugonjwa huo mara kwa mara hivyo ,serikali  imeandaa mwongozo wa kutoa msamaha kwa makundi tofauti yasiyo na uwezo  ikiwa ni pamoja na kundi la wagonjwa wa Selimundu na kinachotakiwa ni kuhakikiwa na kupatiwa kibali cha huduma bila malipo.
 
Aidha,Dokta. Ndugulile amesema Serikali imeanzisha mpango wa Taifa wa Udhibiti wa Magonjwa yasiyoambukizwa  ambapo ugonjwa wa  Selimundu [sickle Cell] utakuwa ni moja ya magonjwa yatakayokuwa yanaratibiwa kitaifa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images