Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Marekani Yasema iko tayari kuzungumza na iran bila ya masharti

$
0
0
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo amesema akiwa ziarani nchini Uswisi,nchi yake iko tayari kuzungumza na Iran bila ya masharti.

 Rais Hassan Ruhani wa Iran alisema jana nchi yake iko wazi kuzungumzia mada inayozusha mabishano ya mradi wake wa kinyuklia, lakini "sio kwa amri" ya Washington. 

Mvutano umezidi makali hivi karibuni kati ya Iran na Marekani. Rais Donald Trump, kupitia mkakati wake wa "shinikizo la nguvu",anataka kuilazimisha serikali ya mjini Teheran irejee katika meza ya mazungumzo kuzungumzia mradi wake wa nuklea na sera zake za kikanda.

Iran Yasema Meli zote za kigeni katika Ghuba ya Uajemi ziko katika shabaha ya makombora

$
0
0
Msaidizi na Mshauri Mkuu wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Iran, Yahya Rahim Safavi amesema kuwa meli zote za Marekani katika Ghuba ya Uajemi, ziko katika shabaha ya makombora ya nchi kavu kuelekea baharini ya majeshi ya wanamaji ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC.)

Meja Jenerali Safavi ameyasema hayo katika mahojiano na Shirika la Habari la FARS ambapo sambamba na kuashiria kwamba Wamarekani wana zaidi ya vituo 25 vya kijeshi katika eneo lote la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) ameongeza kwamba Washington inafahamu vyema kwamba meli zao zote katika eneo la Ghuba ya Uajemi ziko katika shabaha ya makombora hayo ya jeshi la IRGC. 

Akibainisha kwamba shambulizi moja tu katika Ghuba ya Uajemi litapandisha bei ya mafuta kufikia dola 100 kwa pipa, amebainisha kwamba kupanda huko kwa bei ya mafuta kutazifanya Marekani, Ulaya na hata washirika wa Marekani kama vile Japan na Korea Kusini, zishindwe kuvumilia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu June 3

Vyama vya Upinzani Vyatangaza Kususia Uchaguzi wa Marudio

$
0
0
Vyama  nane vya upinzani vimesema havitashiriki uchaguzi wa marudio katika kata 32 unaotarajia kufanyika Juni 15, mwaka huu, endapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haitatekeleza agizo la Mahakama la kuwataka wakurugenzi wa halmashauri kutosimamia uchaguzi.

Vyama vilivyosusia ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi,Chauma, UPDP, NLD,CCK na DP.

Wakizungumza kwa niaba ya vyama hivyo nane, viongozi wa vyama vinne vya ACT-Wazalendo, Chauma, UPDP na NLD walisema kitendo cha NEC kuwaruhusu wakurugenzi kuendelea kusimamia uchaguzi huo ni kuidharau mahakama na kwamba hata vyama vyao haviwezi kushiriki kwa kuwa kufanya hivyo ni kushirikiki katika dharau dhidi ya hukumu ya mahakama.

Akisoma tamko la vyama hivyo mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salam, Mwenyekiti wa Taifa wa UPDP, Fahmi Dovutwa, alisema pamoja na kwamba mahakama ilitoa hukumu ya kufuta vifungu vya sheria vinavyowapa wakurugenzi mamlaka ya kusimamia uchaguzi, lakini vyama hivyo vimekuwa vikipokea barua ya mchakato wa uchukuaji na urudishaji wa fomu kutoka kwa wakurugenzi hao.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), ilitangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa marudio katika kata 32, Juni 15, mwaka huu na baada ya tangazo hilo, wakurugenzi wamekuwa wakiviandikia vyama vya siasa juu ya mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu na kutia saini kama wasimamizi wa uchaguzi huo,” alisema Dovutwa.

Aliongeza: “Itakumbukwa kuwa Mei 10, mwaka huu, Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ilitoa uamuzi wa kuvifuta vifungu vya sheria ya uchaguzi ambavyo vilikuwa vinawapa mamlaka wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwa wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo yao. Mara baada ya uamuzi huo wa Mahakama, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema serikali itawasilisha kusudio lake la kukata rufani kupinga uamuzi huo, lakini mpaka tunavyozungumza hivi, hakuna rufani iliyowasilishwa wala ombi la kisheria la kusitisha utekelezaji wa hukumu hiyo.”

Dovutwa alisema vyama hivyo vinaitaka NEC kupitia mamlaka yake iliyopewa, kuteua wasimamizi wa uchaguzi huo wa marudio mara moja na kama itaendelea na msimamo wake wa kudharau amri ya mahakama, vyama hivyo vitachukua hatua ya kutoshiriki uchaguzi huo na vitawasiliana na wanaharakati waliofungua kesi hiyo kupeleka shauri mahakamani la kukazia hukumu hiyo na kuitaka mahakama iichukulie hatua NEC kwa kudharau amri hiyo ya mahakama.

Pia alisema vitaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika madai ya kuhakikisha wanapata tume huru ya uchaguzi ambayo itakuwa na uwezo kamili na mamlaka ya kuandaa na kusimamia uchaguzi huru na haki ikiwa ni pamoja na kuwa na watendaji na wasimamizi wake wasiofungamana na chama chochote cha siasa.

Vyama hivyo vilitumia nafasi hiyo pia, kuikumbusha NEC kutangaza utaratibu wa kuanza kuandikisha wananchi katika daftari la kudumu la wapigakura katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Taarifa rasmi ya Tukio la Mama Mjamzito kujijeruhi Kirando - Rukwa

$
0
0
Kuanzia tarehe 30 Mei, 2019 kuna taarifa zilizosambaa na kutolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu mama mjamzito anayesemekana kujijeruhi maeneo ya tumboni na kupelekea kutoa mtoto tumboni,tukio lililotokea katika kata ya Kirando Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa. 


Baada ya kupokea taarifa hizo timu ya ufuatiliaji iliyoundwa na wataalam wa Afya kutoka ngazi ya Mkoa na Wilaya husika ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa ilifanya ufuatiliaji wa tukio hilo kwa lengo la kupata uhalisia wake na kubaini mambo yafuatayo:

1. Mhusika katika tukio hili ni Bi Joyce Mweupe Kalinda mwenye umri wa miaka 32 anayeishi katika Kitongoji cha Kalya, Kijiji cha Kamwanda, Kata ya Kirando, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa, umbali wa takribani kilometa moja kutoka Kituo cha  Afya Kirando.

 2.Bi Joyce alipokelewa katika kituo cha Afya Kirando kilichopo katika kata ya kirando Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi majira ya saa 09:30 alfajiri ya tarehe 30 Mei 2019 akiwa amesindikizwa na ndugu zake wawili (Wifi na Shangazi yake) kwa lengo la kujifungua ambapo alipokelewa na kufanyiwa uchunguzi wa awali.

Katika uchunguzi huo ilibainika kuwa mama huyo alikuwa na
ujauzito unaokadiriwa kuwa na miezi tisa, akiwa na dalili za
uchungu katika hali ya kawaida kiafya.

4. Baada ya uchunguzi wa awali kukamilika alipelekwa katika wodi ya wazazi wanaosubiri kujifungua kwa ajili ya kupumzika huku watoa  huduma wakiendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wengine.

5. Katika ujauzito huu alikuwa akihudhuria kliniki ya Afya ya Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Kirando ambapo alifanikiwa kufanya mahudhurio matatu na hudhurio la mwisho likiwa ni tarehe 08 Mei, 2019

6. Mnamo saa 10:30 alfajiri wakati watoa huduma wakifuatilia kujua maendeleo yake ndipo walipobaini kuwa Bi Joyce hakuwepo ndani ya wodi na hivyo kuanza kumtafuta katika maeneo mbalimbali ya kituo cha afya na kutoa taarifa kwa mlinzi na uongozi wa kituo cha afya.

7. Wakati juhudi za kumtafuta zikiendelea, majira ya saa 12:30 asubuhi Bi Joyce aliletwa kituoni akiwa amebebwa kwenye godoro na watu watatu (Mojawapo akiwa ni mwenyekiti wa Kijiji cha Kamwanda) huku akivuja damu nyingi.

8. Watoa huduma walimpokea mgonjwa na kumuona akiwa ametapakaa damu, mtoto akiwa nje ya tumbo. Baada ya kumchunguza Bi Joyce alibainika kuwa na jeraha lilililosababishwa na kitu chenye ncha kali tumboni huku sehemu ya utumbo, mfuko wa uzazi, kondo la nyuma na mtoto vikiwa nje na yeye mwenyewe akiwa hajitambui. Baada ya hapo timu ya Kituo cha Afya ikongozwa na Mganga Mfawidhi Dkt. Gideon Msaki iliendelea na huduma za upasuaji wa dharura kwa ajili ya kuokoa Maisha ya Bi Joyce.

Baada ya huduma za upasuaji wa dharura kufanyika timu ya ufuatiliaji iliendelea na ufuatiliaji zaidi wa tukio hili na kubaini ifuatavyo:

1. Bi Joyce alipotoka kituo cha Afya alirudi nyumbani kwake anapoishi yeye,mtoto wake wa kiume aitwaye Linus Sindani anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 12 au 13 na mume wake ambaye siku ya tukio hakuwepo nyumbani. 2. Mara baada ya kurudi nyumbani Bi Joyce alimwagiza mwanaye (Linusi) kwenda kumuita shangazi yake ambaye anaishi maeneo ya jirani na nyumbani kwao. Waliporudi wakiwa na shangazi ndipo walipomkuta Bi Joyce akiwa ameloa damu na hivyo kutoa taarifa kwa majirani na mwenyekiti wa Kijiji kwa ajili ya msaada
zaidi. 

Hitimisho
1. Timu ya ufuatiliaji imejiridhisha kuwa huduma za dharura za upasuaji wa kuokoa Maisha ya Bi Joyce zimefanyika kwa mafanikio makubwa katika kituo cha Afya Kirando na kwamba mama na mtoto ambao kwa sasa wamehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa uangalizi zaidi wanaendelea vizuri 

2. Tunatoa pongezi kubwa kwa watumishi wa Kituo cha Afya Kirando kwa juhudi kubwa walizofanya kuokoa Maisha ya Bi Joyce Kalinda. 

3. Tukio hili limeripotiwa katika jeshi la Polisi kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi zaidi.

Naibu Waziri Kanyasu Awaonya Wananchi Wanaotoa Vitisho Kwa Askari Wanyamapori Wa Vijiji

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewataka Wananchi waache tabia ya kuwatishia maisha  Askari wanyamapori wa vijiji  (VGS) wakati wanapowakataza wananchi hao kuendesha shughuli za kibinadamu katika maeneo ya mtawanyiko na mapito ya wanyamapori (shoroba)

Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amemtaka Mkuu wa wilaya ya Namtumbo,  Mhe. Sophia Mfaume afanye uchunguzi kwa kutumia vyombo vyake vya usalama ili kuwabaini Wananchi hao wanaowatishia Askari  wanapotekeleza majukumu yao  na watakaobainika hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Mhe. Kanyasu, ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya Askari  20 wa  Wanyamapori wa Vijiji  wa kutoka mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Singida waliohitimu mafunzo hayo  katika Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii cha Likuyu Sekamaganga kilichopo katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma

“leo mmehitimu na tumewaapisha, mmekuwa askari kweli  lakini tambueni kuwa kazi za kiuchumi zinapelekea uharibifu mkubwa sana wa mapito ya wanyama, nendeni mkawaelimishe wananchi wasiendelee kuharibu kwa ustawi wa hifadhi zetu"

Amefafanua kuwa  maeneo ya mtawanyiko na shoroba lazima zilindwe ili kuruhusu wanyamapori waendelee  kuzaliana  na pia kwenda  kupata virutubisho maalum ambayo havipo mbugani.

'' Tunazihitaji hizi shoroba, tulikuwa tumejisahau shoroba nyingi zimekuwa mashamba na makazi na wanyama wamekuwa hawana sehemu ya kupita'' amesema Kanyasu

Amesema shoroba na maeneo ya mtawanyiko zisipokuwepo utalii na Hifadhi vitatoweka.

" Lazima tufike mahali tuamue eneo hili ni kwa ajili ya kilimo na eneo hili kwa ajili ya makazi, haiwezekani maeneo yote tukaanzisha kilimo na makazi ilhali wanyamapori hawana mipaka" Alisisitiza Kanyasu .

Amesema uwepo wa shoroba na maeneo ya mtawanyiko husaidia  kupata kizazi imara cha wanyamapori kwani wakifungiwa sehemu moja huzaliana ndugu na kukosa ubora,ikiwamo kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka askari hao kufanya kazi kwa uaminifu kwa kujiepusha kuungana na mtandao wa majangili.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Namtumbo, Mhe. Sophia Mfaume amewahakikishia askari hao kuwa wafanye kazi kwa kufuta sheria na wale watakaowakwamisha  katika kutekeleza majukumu yao hatasita kuwachukulia sheria.

Aidha, Amewataka Wananchi wafuate sheria kwa kuheshimu maeneo ya mtawanyiko na shoroba ili Hifadhi ziendelee kuwepo

Kwa upande wake, Mhitimu wa mafunzo hayo Musa Alfred Wakati akisoma risala, Amemueleza Naibu Waziri kuwa mafunzo waliyopewa yatakuwa chachu katika shughuli za uhifadhi nchini.

Naye Mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Ruvuma, Jaqueline Msongozi amewataka askari hao wa vijiji watekeleze majukumu yao bila kutishwa na mtu yeyote kwa vile maliasili hizo ni za watanzania wote na wao wanazilinda kwa niaba ya Watanzania.

MWISHO

Waziri Mhagama Azindua Baraza La Taifa La Ushauri Kwa Watu Wenye Ulemavu

$
0
0
Na; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amezindua rasmi Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu huku akilitaka baraza hilo kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano ili kuleta tija na mafanikio makubwa kwa Watu wenye Ulemavu nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo alisema kuwa baraza linajukumu kubwa katika kuhakikisha usimamizi wa sekta ya watu wenye ulemavu pamoja na kuishauri Serikali juu ya masuala mbalimbali ya kundi hilo maalumu.

“Mtambue nafasi mliyopewa ni dhamana kubwa katika kuwahudumia watu wenye ulemavu ambao ni takribani asilimia 5 ya watanzania, hivyo ni vyema mkashirikiana na Serikali kubuni mikakati itakayosaidia kutatua changamoto zinazowakabili wenye ulemavu”, alisema Mhagama

Alifafanua kuwa Baraza hilo limeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya Mwaka 2010 na Sheria hiyo imeeleza majukumu ya Baraza ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri.

“Ni matumaini yangu mtakuwa washauri wazuri wa masuala ya watu wenye ulemavu kwa kuzingatia usawa kwa wote na si maslahi binafsi,” alisisitiza Mhagama.

Sambamba na hilo alimpongeza Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Dkt. Lukas Kija kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Wajumbe wengine kutokana na uaminifu na uwezo walionao katika kusimamia masuala ya Watu wenye Ulemavu.

Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha Watu wenye Ulemavu wanapata haki zao za msingi na kwa ajili ya ustawi wao katika Nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, afya, uchumi, kuwa na miundombinu rafiki pamoja na nyenzo za kujimudu.

Aidha Waziri Mhagama alitoa rai kwa watendaji wa Baraza hilo kuwa na miongozo yote inayohusu masuala ya Watu wenye Ulemavu itakayo wawezesha kufanikisha utendaji wao wa kazi.

Kwa Upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amesema kuwa Serikali katika mwaka 2019/2020 itaanza mapitio ya Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 ili kuwawezesha watu wenye ulemavu kwenda sambamba na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija alieleza kuwa wapo tayari kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia haki na ustawi wa Watu wenye Ulemavu.

Aliongeza kuwa Baraza hilo lipo tayari kutoa ushauri na hoja zenye tija kwa Serikali juu ya masuala mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu.

Pia, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe alieleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa Baraza hilo na kufanya kazi pamoja katika kutatua changamoto zinazowakabili Watu wenye Ulemavu nchini ikiwemo migogoro na migongano kwa wadau.

Uzinduzi wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu umefanyika Juni 2, 2019 jijini Dodoma ambapo Baraza hilo litaongoza kwa kipindi cha miaka mitatu (2019 hadi 2021) likiongozwa na Mwenyekiti Dkt. Lukas Kija. Awali Baraza hilo lilikuwa likiongozwa na Dkt. Edward Bagandanshwa ambalo limemaliza muda wake mwaka 2017.

MWISHO

Kitabu Cha Madini Yapatikanayo Tanzania

$
0
0
Serikali kupitia  Wizara ya Madini chini ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imetoa toleo jipya la kitabu cha Madini yapatikanayo Tanzania kuanzia ngazi ya Mikoa, Wilaya na Kata.
 
Toleo hili la nne linaonesha taarifa nyingi zaidi ambapo maeneo mapya yenye madini yameongezeka zaidi ya 2200.
 
GST inatarajia kuwa kitabu hiki kitaongeza uelewa kwa wananchi na wadau mbalimbali kwa ujumla juu ya rasilimali madini yanayopatikana hapa nchini Tanzania na kuchochea uwekezaji katika sekta ya madini.GST inawakaribisha wadau wa sekta ya madini kujipatia nakala ya kitabu hicho kinachopatikana katika ofisi za GST jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma) Hashim Rungwe Aripoti Polisi

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma) Hashim Rungwe ameripoti katika kituo cha polisi Osterbay kuitikia wito wa kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Mussa Taibu.

Rungwe amefika kituoni hapo saa 4.10 asubuhi ya leo Jumatatu Juni 3, 2019  akiwa amevalia kanzu nyeupe akiongozana na mtu mmoja ambao wote wameingia katika ofisi ya Kamanda Taibu.

Mwenyekiti huyo amefika kituoni hapo baada ya jana Jumapili Eugene Kabendera, kwa niaba ya Sekretarieti ya Ushirikiano wa Vyama nane vya Upinzani kutoa taarifa akisema polisi walifika katika ofisi za Chaumma jijini Dar es Salaam na kueleza Rungwe anatakiwa kuripoti leo Jumatatu Juni 3,2019 katika ofisi za Kamanda Taibu.

Katika mkutano huo, viongozi wa vyama hivyo walitoa tamko la kutoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio kwenye kata 32 unaotarajiwa kufanyika  Juni 15, 2019 kwa sababu unasimamiwa na Wakurugenzi Halmashauri za wilaya na Manispaa kinyume na uamuzi wa Mahakama Kuu.

Jeshi la Polisi Kigoma Lafanikiwa Kumkamata kinara wa ubakaji na kujeruhi wanawake

$
0
0
Vyombo vya dola mkoani Kigoma vimefanikiwa kumkamata Hussein Hamis, anayetuhumiwa kuwa kinara wa ubakaji na kujeruhi wanawake nyakati za usiku maarufu kama teleza.

Hamis aliye maarufu kwa jina la Orosho, alikamatwa pamoja na watuhumiwa wengine tisa wakitambuliwa kama teleza, ambao huwaingilia kingono wanawake kwa kuwalazimisha, kuwaibia na kuwajeruhi wakiwa wamejipaka ‘oil’ chafu au mafuta ya mawese ili wanaposhikwa wawe wanateleza.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini, Samson Hanga alisema baada ya kuwapo taarifa hiyo, vyombo vya dola viliendesha  msako mkali kwa kushirikiana na wananchi ili kuwakamata wahalifu.

“Tulitengeneza namna bora ya kuwakamata wahusika, tulifanya kazi ya upigaji kura ya siri tukapata majina, mengine tulipata kupitia vyombo vya dola. Mpaka sasa tumekamata vijana tisa, wapo mahabusu na upelelezi unaendelea,” alisema Hanga.

Alisema katika majina yaliyotajwa na kupigiwa kura, mtuhumiwa mmoja alitajwa na akina mama waliofanyiwa vitendo vya ukatili ambaye ni Hamis.

“Unajua Serikali ina mkono mrefu, macho makubwa, yule kijana alipopata taarifa tunamtafuta alikimbilia kwa mama yake Kijiji cha Kagongo, baadae akakimbilia tena Kijiji cha Kagunga, juzi jioni tukafanikiwa kumkamata wilayani Kasulu na kuletwa hapa kituo cha polisi kwa ajili ya hatua zaidi,” alisema.

Hanga alisema pia wamefanya gwaride la utambuzi kwa waathirika  kuwatambua vijana 10 waliokamatwa.

Alisema msako bado unaendelea na kuonya yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja kabla vyombo vya dola havijambaini na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaobainika.
.

Tangazo la Nafasi za Masomo Kwa Kidato cha Tano Shule ya Sekondari Lake Tanganyika....Changamkia Hii Fursa

Nape Ammwagia Pongezi Waziri Makamba

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Mtama,Nape Nnauye ametoa pongezi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kwa kusimamia suala la katazo la mifuko ya Plastiki.

Katika ukurasa wake wa Twitter leo asubuhi Jumatatu Juni 3, 2019 Nape ameandika ujumbe akisema kazi iliyofanywa na Makamaba ni mfano wa kiongozi na siyo mtawala .

Akiwa ameambatanisha picha yake (Nape) na Makamba wakiwa wamevalia masharti ya rangi ya kijana inayotumiwa na CCM, Nape amendika, “Namna wewe na wenzako mlivyosimamia swala la mifuko ya plastiki ni mfano tosha wa utofauti kati ya kuongoza na kutawala.. Hongera sana!.”

Waziri Makamba ameongoza kampeni hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilotoa bungeni miezi kadhaa iliyopita akisema kuanzia Juni mosi, 2019, itakuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote na matumizi yake yatakoma Mei 31, 2019.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Wizara Ya Fedha Na Mipango Yaomba Kuidhinishiwa Bajeti Ya Shilingi Trilioni 11.94 Mwa 2019/2020

$
0
0

UTANGULIZI


1.            Mheshimiwa Spika,kutokana na    taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, naomba kutoa hoja kwamba, sasa Bunge lako lipokee na kujadili mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2018/19 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/20. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango na Taasisi zilizo chini yake pamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa mwaka 2019/20.

2.           Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutujalia uhai na afya njema na kutuwezesha kukutana tena kushiriki mkutano huu wa Bunge unaojadili Bajeti ya mwaka 2019/20, ambayo ni ya Nne tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani.

3.           Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, napenda nitumie fursa hii kuwapongeza kwa dhati kabisa Viongozi Wakuu wa Serikali, nikianza na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa miongozo yao iliyojaa hekima na uzalendo. Ni dhahiri kwamba, katika kipindi cha takriban miaka mitatu na nusu ya uongozi wao, tumepata mafanikio mengi ambayo kila mmoja wetu anapaswa kujivunia. Naomba Mwenyezi Mungu aendelee kuwajalia afya njema ili dhamira zao za dhati za kuwaletea watanzania maendeleo ziendelee kuleta manufaa kwetu na kwa vizazi vijavyo.

4.           Mheshimiwa Spika, napenda pia nitumie fursa hii, kuwapongeza sana Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb.), kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, pamoja na Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb.), kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Nawaahidi ushirikiano wa hali ya juukatika kutekeleza majukumu yetu ya kumsaidia Mhe. Rais ili shughuli za Serikali ziendelee kufanyika kwa ufanisi zaidi.

5.           Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuendesha vizuri majadiliano ya Bajeti za Wizara mbalimbali. Aidha, napenda kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) na Makamu Mwenyekiti Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (Mb) kwa kuongoza vizuri majadiliano ya Kamati. Vilevile, nawashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Bajeti kwa michango yao mizuri ambayo inatusaidia sana katika kutekeleza majukumu ya Wizara kwa ufanisi. Aidha, Wizara inaahidi kuendelea kuzingatia maoni na ushauri kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge wote wakati wa kujadili taarifa hii ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara yangu kwa mwaka 2018/19 na Mpango na Bajeti ya mwaka 2019/20.

6.           Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, kwa msaada mkubwa na ushirikiano anaonipatia katika kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Wizara.  Aidha, nawashukuru Bw. Doto M. James, Katibu Mkuu HAZINA na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Naibu Makatibu Wakuu Bi. Amina Kh. Shaaban, Dkt. Khatibu M. Kazungu na Bw. Adolf H. Ndunguru kwa kusimamia shughuli za kiutendaji za Wizara kwa ufanisi. Vilevile, nawashukuru Makamishna, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, Wakuu wa Vitengo   na wafanyakazi wote wa Wizara, kwa kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia Watanzania.

7.           Mheshimiwa Spika, baada ya maneno haya ya shukrani, naomba nijielekeze katika hoja yangu yenye maeneo makuu mawili ambayo ni: mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2018/19 na Mpango na Bajeti kwa mwaka 2019/20.

8.           Mheshimiwa Spika,katika mwaka wa fedha 2018/19, bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango inatekelezwa katika mafungu nane ya kibajeti ambayo ni: - Fungu 50 - Wizara ya Fedha na Mipango; Fungu 21 - HAZINA; Fungu 22 - Deni la Taifa; Fungu 23 - Mhasibu Mkuu wa Serikali; Fungu 7 - Ofisi ya Msajili wa HAZINA; Fungu 10 - Tume ya Pamoja ya Fedha; Fungu 13 - Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu; na Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2018/19


9.           Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda na kuwaletea Watanzania maendeleo inafikiwa, Wizara iliandaa Mpango na Bajeti ya mwaka 2018/19 kwa kuzingatia miongozo mbalimbali ya kitaifa, kikanda na kimataifa ambayo ni pamoja na: Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17- 2020/21, Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti 2018/19, Sheria ya Bajeti Na.11 ya Mwaka 2015, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2015, Agenda ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika 2063 na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030. Aidha, Mpango na Bajeti ulizingatia ahadi na maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ushauri na maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti pamoja na Sera mbalimbali za Serikali.

Mapatona Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2018/19


10.        Mheshimiwa Spika, Muhtasari wa mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/19 ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 6 hadi ukurasa wa 9.

UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU


11.        Mheshimiwa Spika, napenda sasa nitumie fursa hii kulieleza Bunge lako tukufu kuhusu majukumu yaliyotekelezwa na Wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake kwa kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi kufikia Aprili 2019 ambayo yameainishwa katika hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 9 hadi ukurasa wa 124.


Kubuni na Kusimamia Utekelezaji wa Sera za Uchumi Jumla


12.        Mheshimiwa Spika, malengo ya uchumi jumla kwa mwaka 2018/19 yalikuwa: kuhakikisha Pato la Taifa linakua kwa asilimia 7.2 mwaka 2018; mfumuko wa bei unabaki katika wigo wa tarakimu moja; mapato ya ndani yanafikia asilimia 15.8 ya pato la Taifa; na mapato ya kodi yanafikia asilimia 13.6 ya Pato la Taifa na nakisi ya bajeti inafikia asilimia 3.2.

13.        Mheshimiwa Spika, uchumi wa nchi yetu umeendelea kuimarika ambapo mwaka 2018, Pato la Taifa kwa kutumia bei ya kizio ya mwaka 2015 lilikua kwa asilimia 7.0 ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka 2017. Sekta zilizokua kwa kasi kubwa ni pamoja na Sanaa na Burudani (asilimia 13.7), ujenzi (asilimia 12.9), usafirishaji na uhifadhi mizigo (asilimia 11.8) na habari na mawasiliano (asilimia 9.1). Ukuaji huu wa uchumi umeenda sambamba na utolewaji wa huduma bora kwa wananchi zikiwemo maji, afya, umeme, elimu na ujenzi wa miundombinu ya reli, bandari, viwanja vya ndege, madaraja na barabara pamoja na kuimarisha usafiri wa anga.
                                      
14.        Mheshimiwa Spika,mfumuko wa bei umeendelea kushuka na kubakia katika kiwango cha tarakimu moja. Kwa mwezi Aprili 2019, mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 3.2 ikilinganishwa na asilimia 3.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2018. Hali hii imetokana na kuimarika kwa upatikanaji wa chakula katika masoko ya ndani na nchi jirani, kutengamaa kwa bei za mafuta katika soko la dunia, usimamizi madhubuti wa Sera za bajeti na fedha na utulivu wa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu nyingine. Utulivu huu wa bei umesaidia wazalishaji, wanunuzi na walaji kuweka mipango na mikakati ya muda mrefu bila kuhofia mabadiliko ya mara kwa mara ya bei ya malighafi na bidhaa.

Uandaaji na Ufuatiliaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa


15.        Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikiwa kufuatilia utekelezaji wa miradi 102 ya maendeleo kati ya 179. Miradi iliyofuatiliwa ilijumuisha sekta za Viwanda, Maji, Kilimo, Nishati, Uvuvi, Afya, Elimu, Madini, Sheria, Ujenzi na Uchukuzi. Ufuatiliaji huo umesaidia kurekebisha upungufu uliojitokeza katika utekelezaji na kuainisha hatua za kuzingatiwa katika kutayarisha mpango wa mwaka 2019/20.

Kusimamia Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali


Mapato ya Kodi na Yasiyo ya Kodi

16.        Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizara ilipanga kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani yakijumuisha mapato ya Halmashauri ya jumla ya shilingi trilioni 20.89. Kati ya hizo, mapato ya kodi yalikuwa shilingi trilioni 18.0, Halmashauri shilingi bilioni 735.6 na mapato yasiyo ya kodi shilingi trilioni 2.16.Hadi kufikia Aprili 2019, mapato ya ndani yakijumuisha mapato ya Halmashauri yalifikia shilingi trilioni 15.46. Kati ya kiasi hicho, mapato ya kodi yalikuwa shilingi trilioni 12.9, sawa na asilimia 87.4, mapato yasiyo ya kodi shilingi trilioni 2.04, sawa na asilimia 122 na mapato ya Halmashauri shilingi bilioni 529.25, sawa na asilimia 72 ya lengo la kipindi hicho.

17.        Mheshimiwa Spika, kati ya mapato yasiyo ya kodi ya kiasi cha shilingi trilioni 2.04 yaliyopatikana hadi kufikia Aprili 2019, jumla ya shilingi bilioni 600.45 zimekusanywa na Wizara ya fedha na Mipango, sawa na asilimia 100.44 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 597.81. Mafanikio haya yametokana na kuimarishwa kwa ufuatiliaji na usimamizi wa mashirika, kampuni na taasisi za umma ambazo Serikali imewekeza.

18.        Mheshimiwa Spika, ili kuendelea kuleta uwazi na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato, Wizara  ilipanga kuunganisha Wizara, Idara na Taasisi za Serikali 300 kwenye Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji na usimamizi wa maduhuli (Government e- Payment Gateway - GePG). Hadi kufikia Aprili 2019, jumla ya Taasisi 210 zimeunganishwa kwenye mfumo wa GePG ikiwa ni asilimia 70 ya lengo. Aidha, hadi sasa jumla ya taasisi 410    kati ya taasisi 667 zimeunganishwa na zinakusanya mapato kupitia mfumo huu.  Mfumo huu unaiwezesha Serikali kuona moja kwa moja miamala ya ukusanyaji wa mapato na kujua kiwango cha mapato kinachokusanywa kwa siku.

Misaada na Mikopo kutoka kwa Washirika wa Maendeleo

19.        Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizara ilipanga kuratibu upatikanaji wa misaada na mikopo nafuu ya kiasi cha shilingi trilioni 2.67 kutoka kwa washirika wa Maendeleo ili kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili 2019, misaada na mikopo ilifikia shilingi trilioni 1.70, sawa na asilimia 86 ya lengo la kipindi hicho.




Mikopo ya Ndani na Nje yenye Masharti ya Kibiashara

20.        Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizara ilitarajia kuratibu upatikanaji wa mikopo ya ndani na nje yenye masharti ya kibiashara ya jumla ya shilingi trilioni 8.90. Kati ya hizo, shilingi trilioni 3.11 ni mikopo ya nje, shilingi trilioni 1.19 ni mikopo ya ndani na shilingi trilioni 4.60 ni mikopo ya ndani ya kulipia hatifungani zilizoiva (rollover). Hadi kufikia Aprili, 2019 kiasi cha shilingi bilioni 692.30 kilikopwa kutoka nje na shilingi trilioni 3.3 zilikopwa kutoka soko la ndani zikijumuisha malipo ya dhamana za Serikali zilizoiva (rollover).

Usimamizi wa Deni la Serikali



22.         Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kufanya tathmini ya Deni la Taifa kila mwaka ili kupima uhimilivu wake. Matokeo ya tathmini iliyofanyika Desemba, 2018 inaonesha kuwa, Deni la Taifa ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu. Tathmini hiyo ilionesha kuwa: uwiano wa thamani ya sasa ya Deni la Taifa (Present Value of Total Public Debt) kwa Pato la Taifa ni asilimia 27.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 70; thamani ya sasa ya Deni la nje pekee (Present Value of External Debt)  kwa Pato la Taifa ni asilimia 22.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55; thamani ya sasa ya  deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 157.3 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 240; na ulipaji wa deni la nje kwa kutumia mauzo ya bidhaa nje ni asilimia 15.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 23.

23.        Mheshimiwa Spika, Serikali ilitenga kiasi cha shilingi trilioni 1.41 kwa ajili ya kulipa riba ya deni la ndani. Hadi kufikia Aprili, 2019 kiasi cha shilingi trilioni 1.06 kimelipwa sawa na asilimia 75.18 ya lengo. Aidha, Serikali ilitenga shilingi bilioni 689.67 kwa ajili ya kulipa riba ya deni la nje. Hadi kufikia Aprili, 2019 shilingi bilioni 588.30 zimelipwa sawa na asilimia 85.30 ya lengo. Vilevile, Serikali ilitenga shilingi trilioni 1.66 kwa ajili ya kulipia mtaji wa deni la nje, ambapo hadi kufikia Aprili, 2019 shilingi trilioni 1.23 zimelipwa sawa na asilimia 74.10 ya lengo. Wizara itaendelea kusimamia Deni la Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada SURA 134 pamoja na Mkakati wa Muda wa kati wa Kusimamia Madeni.

Malipo ya Pensheni na Michango ya Mwajiri kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii


24.        Mheshimiwa Spika,Serikali ilitenga kiasi cha shilingi trilioni 1.19 kwa ajili ya kulipia mchango wa mwajiri kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.  Hadi kufikiaAprili, 2019 kiasi cha shilingi bilioni 797.29 sawa na asilimia 67.0 ya lengo kililipwa ikiwa ni uwasilishaji wa michango ya mwajiri kwa watumishi wote wa Umma walio kwenye “Payroll” ya Serikali na kwa wakati.  

25.        Mheshimiwa Spika,katika mwaka 2018/19, Serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 424.74 kwa ajili ya kulipa mafao ya Kustaafu na mirathi kwa wastaafu wanaolipwa na HAZINA. Hadi kufikia Aprili 2019, kiasi cha shilingi bilioni 314.92 sawa na asilimia 74.14 kilitumika kulipa Wastaafu 4,016, Mirathi ililipwa kwa Warithi 854 na Pensheni kwa kila mwezi kwa Wastaafu 57,055. Katika kurahisisha ulipaji wa mafao ya wastaafu, Serikali imetengeneza mfumo wa ukokotoaji wa Mafao, uhifadhi wa kumbukumbu pamoja na utoaji wa Vitambulisho vya kielektroniki kwa kutumia mfumo wa TPPS (Treasury Pensioners Payment System).

Kubuni na Kusimamia Mifumo ya Taarifa za Fedha


26.        Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikiwa kubuni mfumo wa ufuatiliaji wa Mali za Serikali ujulikanao kama Government Asset Management Information System-GAMIS kwa ajili ya  kurahisisha usimamizi na udhibiti wa Mali za Serikali. Aidha, Wizara imebuni na kuanza kutengeneza mfumo wa usimamizi wa fedha za miradi ya Maendeleo kutoka kwa washirika wa maendeleo zinazopelekwa moja kwa moja kwa watekelezaji (Direct to Projects Funds) ambao unatarajiwa kuanza kutumika Julai, 2019. Lengo ni kutambua miradi yote na kuweka uwazi kuhusu fedha zinazotolewa na Washirika wa Maendeleo bila kupitia Mfuko Mkuu wa Serikali.

27.        Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yaliyotekelezwa chini ya usimamizi wa mifumo ya taarifa za fedha ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 24 hadi ukurasa wa 28.

    

Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali


28.        Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatoa huduma bora kwa Wananchi, Wizara imeendelea kuzijengea uwezo kwa kuzipatia fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati ili ziweze kujitegemea kimapato na kupunguza utegemezi wa ruzuku ya Serikali Kuu. Katika mwaka 2018/19, Wizara imefanya uchambuzi wa Miradi ya Kimkakati 111 yenye thamani ya shilingi bilioni 749.63 kutoka kwenye Halmashauri 67 kwa ajili ya kuzingatiwa katika bajeti ya 2019/20. Matokeo ya uchambuzi huo ni kuwa jumla ya miradi 15 yenye thamani ya shilingi bilioni 137.38 kutoka kwenye Halmashauri 12 ilikidhi vigezo na mikataba kusainiwa.Orodha ya Halmashauri na idadi ya Miradi ni kama ifuatavyo: Halmashauri ya Jiji la Tanga mradi mmoja na Halmashauri ya Jiji la Mwanza miradi miwili; Halmashauri za Manispaa ya Kinondoni miradi miwili, Kigamboni mradi mmoja, Iringa mradi mmoja, Ilemela miradi miwili; Halmashauri ya Mji wa Tarime mradi mmoja; Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mradi mmoja, Biharamuro mradi mmoja, Kibaha mradi mmoja na Hanang mradi mmoja.

29.        Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 28 hadi ukurasa wa 32.

Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi ya Fedha za Umma


30.        Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, imefanya uhakiki wa madeni ya malimbikizo ya mishahara katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali 142; Sekretarieti za Mikoa 24 na Mamlaka ya Serikali za Mitaa 185.  Aidha, Wizara imeendelea kuhakikisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kufanya ukaguzi maalum katika Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila, ambapo mapendekezo ya ukaguzi yaliwasilishwa kwa taasisi husika kwa ajili ya kuyafanyia kazi ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa miradi.

31.        Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yaliyotekelezwa katika kusimamia na kudhibiti Matumizi ya Fedha za Umma ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 33 hadi ukurasa wa 35.

Usimamizi wa Mali za Serikali


32.        Mheshimiwa Spika,Wizara ilifanya uhakiki wa mali na madeni katika taasisi zilizounganishwa ambazo ni Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSPF, GEPF, PPF na LAPF) na mamlaka za maji Dar es Salaam (DAWASA na DAWASCO). Baada ya utambuzi wa mali na madeni ya taasisi hizo, Serikali itahakikisha kuwa inachukua hatua stahiki kulingana na matokeo ya uhakiki. Wizara pia imefanya uhakiki wa majengo yaliyobaki wazi Jijini Dar es Salaam baada ya Serikali kuhamishia shughuli zake Jijini Dodoma kwa lengo la kuandaa utaratibu wa kugawa majengo hayo kwa baadhi ya Taasisi za Serikali ambazo zina uhitaji wa majengo hayo.

33.        Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yaliyotekelezwa katika Usimamizi wa Mali za Serikali ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 35 hadi ukurasa wa 37.

Udhibiti wa Utakasishaji wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi


34.        Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu (FIU) imeendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria za Udhibiti wa Fedha Haramu kwa kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na:  kupokea na kuchambua taarifa 1,305 za miamala shuku kutoka kwa watoa taarifa na kuwasilisha taarifa fiche 32 kwenye vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria kwa ajili ya uchunguzi; kupokea taarifa 5,536 zinazohusu usafirishaji fedha taslimu na hati za malipo mipakani; kuratibu na kusimamia zoezi linaloendeshwa na ESAAMLG la tathmini ya mifumo ya udhibiti wa fedha haramu (AML/CFT Mutual Evaluation); kuimarisha ushirikiano na  FIU za nchi za Djibouti, Sudan, Ethiopia, Somalia, China (Taiwan) na Mauritius na pia kufanya majadiliano ya kuingia katika makubaliano ya ushirikiano na FIU za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamaica, Japan, Trinidad and Tobago, Botswana, Canada, Jamhuri ya Kongo na Kazakhstan. Aidha, Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu imekagua benki nne ili kujiridhisha na utekelezaji wa Sheria za Udhibiti wa Fedha Haramu.

35.        Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yaliyotekelezwa katika Udhibiti wa Utakasishaji wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 37 hadi ukurasa wa 39.

Tume ya Pamoja ya Fedha 


36.        Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Pamoja ya Fedha umeoneshwa kuanzia ukurasa wa 39 hadi ukurasa wa 40.

Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma


37.        MheshimiwaSpika,      katika mwaka 2018/19, Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imefanya Ukaguzi Maalum katika Kampuni 34 ambazo Serikali ina umiliki wa hisa chache. Aidha, Ofisi ya Msajili wa Hazina imeandaa Mpango Kazi wa kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti ya ukaguzi na utekelezaji unaendelea. Utekelezaji wa Mpango Kazi unajumuisha kupitia mikataba ya ubia, uendeshaji na utaalam kwa kampuni husika. Lengo kuu la zoezi hili ni kubaini sababu za Serikali kupata kiwango kidogo cha gawio au kutopata kabisa na kuchukua hatua stahiki ili kuongeza mapato ya Serikali. Aidha, ufuatiliaji wa madeni kwa wawekezaji waliobainika kutomaliza kulipa bei ya ununuzi wa kampuni hizo unaendelea.

38.        Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yaliyotekelezwa katika Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 40 hadi ukurasa wa 47.

Uratibuwa Mikakati ya Kupunguza Umaskini


39.        Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizara imefanya uchambuzi wa awali wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi 2017/18 ambao, unaonesha kuwa umaskini wa mahitaji ya msingi umepungua kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia 26.4 mwaka 2017/18. Kiwango cha umaskini wa chakula kimepungua kutoka asilimia 9.7 mwaka 2011/12 na kufikia asilimia 8.0 mwaka 2017/18.

40.        Mheshimiwa Spika, tathmini ya viashiria vya umaskini usio wa kipato inaonesha tumefanya vizuri katika kuboresha hali ya makazi, umeme, huduma ya maji safi na salama, vyoo, umiliki wa vyombo vya usafiri na mawasiliano. Viashiria vinaonesha kuwa makazi yaliyojengwa kwa kutumia zege, mawe, saruji na vyuma yameongezeka. Vilevile, kaya zinazoishi katika nyumba zenye paa la kisasa zimeongezeka kutoka asilimia 68.0 mwaka 2011/12 hadi asilimia 84.1 mwaka 2017/18. Aidha, asilimia 78.8 ya kaya zinaishi kwenye nyumba zilizojengwa kwa kuta imara mwaka 2017/18 ikilinganishwa na asilimia 46.0 mwaka 2011/12.   Vilevile, asilimia 50.1 ya kaya zinaishi kwenye nyumba zilizojengwa kwa sakafu imara mwaka 2017/18 ikilinganishwa na asilimia 40.0 mwaka 2011/12.

41.        Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yaliyotekelezwa katika kuratibu  Mikakati ya Kupunguza Umaskini ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 48 hadi ukurasa wa 52.

Ununuzi wa Umma


42.        Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikiwa kufanya marekebisho ya Kanuni ya 164 ya Sheria ya Ununuzi wa Ummaili kumpa mzabuni haki ya kupata taarifa ya ukamilishwaji wa mchakato wa ununuzi.Aidha, Kanuni ya 226 ilirekebishwa kumpa mamlaka Mlipaji Mkuu wa Serikali kutoa idhini kwa Maafisa Masuuli kuongeza idadi ya wajumbe wa timu za majadiliano kwenye miradi mikubwa yenye maslahi kwa Taifa. Marekebisho hayo yamezingatia maoni ya wadau juu ya changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura 410.

43.        Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yaliyotekelezwa katika kusimamia Ununuzi wa Umma ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 52 hadi ukurasa wa 60

Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi - PPP


44.        Mheshimiwa Spika, Wizara imepokea mapendekezo ya miradi ya ubia ipatayo 33, kati ya hiyo miradi sita imekidhi vigezo na kufanyiwa kazi. Miradi hiyo ni: Mradi wa Uboreshaji wa Huduma ya Usafiri jijini Dar es Salaam Awamu ya kwanza (Dar- Rapid Transit Project- Phase1);Mradi wa Viwanda Vitatu vya Uzalishaji wa Dawa muhimu na Vifaa Tiba;mradi wa Usambazaji wa Gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam, Lindi na Mtwara; Mradi ya Ujenzi ya Hoteli ya Nyota Nne; Kituo cha Biashara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere; na Mradi wa ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE). Aidha, Wizara imekamilisha uchambuzi wa mawasilisho ya awali ya miradi 22 ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na wahusika watajulishwa kuhusu maeneo ya kufanyia kazi kwa mujibu wa Sheria, mwongozo na taratibu za PPP.

45.        Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yaliyotekelezwa katika eneo la Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 60 hadi ukurasa wa 65.

Utekelezaji wa Majukumu ya Mashirika na Taasisi za Umma


46.        Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa majukumu ya Taasisi na Mashirika yaliyo chini ya Wizara kwa mwaka 2018/19 ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 65 hadi ukurasa wa 114.

          Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

47.        Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali imefanya ukaguzi wa hesabu za: Wizara na Idara za Serikali 65; Vyama vya Siasa 14; Sekretariati za Mikoa 26; Wakala za Serikali 33; Mifuko Maalum 16; Taasisi nyingine za Serikali 42; na Balozi za Tanzania 41. Aidha, ukaguzi ulifanyika kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa 185 na Mashirika ya Umma 176. Vilevile, Ofisi imefanya ukaguzi maalum  kwenye taasisi zifuatazo: Shirika la Usafiri Dar-es-Salaam (UDA); Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF); Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA); Taasisi ya Elimu Tanzania; Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC); Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA); Jeshi la Polisi; na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege.

48.        Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi pia ilifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo 469 na ripoti za ukaguzi zimetolewa. Aidha, katika ukaguzi wa ufanisi, jumla ya taarifa 10 zimetolewa katika kipindi kilichoishia Machi, 2019. Vilevile, hadi kufikia Aprili, 2019 Ofisi imetoa ripoti kuu tano. Taarifa hizo ni muhtasari wa jumla ya taarifa 1,042 za ukaguzi zilizotolewa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2017/18.

          Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

49.        Mheshimiwa Spika, maelezo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyo chini ya Wizara kwa mwaka 2018/19 ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 117 hadi ukurasa wa 121.

CHANGAMOTO NA MIKAKATI YA KUKABILIANA NAZO


Changamoto


50.        Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa bajeti ya Wizara, changamoto zifuatazo zilijitokeza katika mwaka huu wa fedha ambazo ni:

(i)          Masharti yasiyo rafiki ya mikopo kwenye masoko ya fedha duniani;
(ii)         Kupungua na kutopatikana kwa wakati kwa fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo katika kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo; na
(iii)        Mwamko mdogo wa kulipa kodi kwa hiari, kudai au kutoa risiti za kielektroniki.



Mikakati ya Kukabiliana na Changamoto


51.        Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto za utekelezaji wa bajeti kama zilivyobainishwa hapo juu, Wizara inaendelea kuchukua hatua mbalimbali zikiwemo:

(i)          Kuhakikisha kuwa Wizara na Taasisi zote za umma zinatumia Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji na usimamizi wa maduhuli (Government e- Payment Gateway - GePG);
(ii)         Kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa lengo la kupunguza utegemezi;
(iii)        Kuboresha mfumo wa usimamizi wa mashine za kielektroniki za kutolea risiti ili ziweze kutumika kwa kila muamala unaofanywa. Uboreshaji huu utaondoa uwezekano wa kughushi risiti na kupunguza mianya ya ukwepaji wa kodi;
(iv)       Kudhibiti biashara ya magendo kupitia bahari, maziwa, mipaka, na njia zisizo rasmi kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali kama TANROADS, Mamlaka ya Bandari, Jeshi la Polisi, Jeshi la Wanamaji na Usalama wa Taifa;
(v)         Kuongeza jitihada za ukusanyaji wa kodi za majengo kwa kushirikisha wadau muhimu wakiwemo Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, OR-TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu;
(vi)       Kuendelea kusimamia utekelezaji wa bajeti kwa kuzingatia Sheria ya Bajeti Na. 11 ya Mwaka 2015;
(vii)      Kuendelea kuimarisha ushirikiano na Washirika wa Maendeleo kwa kutekeleza Mwongozo wa Ushirikiano (DCF) ili kuhakikisha fedha zilizoahidiwa zinatolewa kwa wakati; na
(viii)     Kuendelea na majadiliano na taasisi za fedha za kimataifa ili kuhakikisha kuwa fedha zinazotokana na mikopo ya kibiashara zinapatikana kwa kipindi kilichobaki.

MALENGO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2019/20


52.        Mheshimiwa Spika, naomba sasa nieleze kuhusu malengo ya mpango na bajeti ya Wizara na Taasisi zake kwa mwaka 2019/20;

MPANGO WA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA


53.        Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Wizara itaendelea kusimamia majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na yafuatayo:


(ii)         Kuratibu uandaaji na ufuatiliaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa;

(iii)        Kusimamia hatua mbalimbali za ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuwezesha utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa ufanisi;

(iv)       Kuratibu upatikanaji wa Misaada na Mikopo kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na kuhakikisha kuwa inaendelea kutolewa kama ilivyoahidiwa na kwa wakati ili kugharamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo;

 

(v)         Kusimamia Deni la Serikali kwa kuhakikisha inakopa kwenye vyanzo vyenye riba nafuu;

(vi)       Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mikopo iliyodhaminiwa na Serikali ili kuhakikisha wadaiwa wanalipa madeni husika kwa wakati kuepusha uwezekano wa kuongeza mzigo kwa Serikali wa kulipa mikopo hiyo;

(vii)      Kusimamia mfumo wa udhibiti wa matumizi ya fedha za umma ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho ya mfumo wa Akaunti Jumuifu ya Hazina (Treasury Single Account) kwa lengo la kuboresha mfumo wa matumizi ya umma ili kuiongezea Serikali uwezo wa kugharamia shughuli zake kwa wakati;


(ix)        Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za umma ili kupata thamani halisi ya fedha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo;

(x)         Kuratibuzoezi la uthamini wa mali katika taasisi za Serikali ili kuwa na taarifa sahihi za mali pamoja na kuendelea kuondosha mali chakavu, sinzia (dormant) na zilizokwisha muda wake;  

(xi)        Kusimamia utekelezaji wa Sheria za Udhibiti wa Fedha Haramu kwa kupokea na kuchambua taarifa za miamala shuku zinazohusu utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi;

(xii)      Kusimamia zoezi linaloendelea la tathmini ya kitaifa ya mifumo ya kudhibiti utakasishaji fedha haramu na ufadhili wa ugaidi (Mutual evaluation). Tathmini hiyo itaijengea nchi sifa na uwezo wa kushirikiana na nchi nyingine duniani kwa kubadilishana taarifa zinazohusu udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa vitendo vya kigaidi;

(xiii)     Kusimamia Mashirika na Taasisi za Umma kwa kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli kutoka katika Taasisi na Mashirika ya Umma na Kampuni ambazo Serikali ina hisa, kuhakikisha viwanda vilivyobinafsishwa vinafanya kazi kwa ufanisi, kurejesha viwanda vilivyoshindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa makubalianona kuwapatia wawekezaji wengine wenye uwezo na nia ya kuviendeleza;

(xiv)     Kuratibu Mikakati ya Kupunguza Umaskini;


(xvi)     Kuratibu shughuli za PPP nchini; na


54.        Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu Mpango wa Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 125 hadi ukurasa wa 145.

Usimamizi na Uratibu wa Taasisi na Mashirika ya Umma Chini ya  Wizara

 

55.        Mheshimiwa Spika,mipango kwa mwaka 2019/20 kwa upande wa Mashirika na Taasisi za Umma zilizo chini ya Wizara ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 147 hadi ukurasa wa 167.

Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi


56.        Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imepanga kutekeleza vipaumbele nane ikiwa ni pamoja na: kufanya ukaguzi wa mafungu ya Bajeti ya Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali, Sekretariati za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mikoa yote nchini, Mashirika ya Umma; kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Wahisani; kufanya kaguzi za kiufundi katika maeneo yenye uwekezaji mkubwa wa rasilimali za Umma kama vile ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege, reli za  kisasa, na Miradi ya umeme; kufanya maboresho ya mfumo wa ukaguzi kwa kutumia TEHAMA; na kukagua ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi; ukaguzi wa ufanisi, kaguzi maalum, na kaguzi za kiuchunguzi (forensic audits) katika maeneo yatakayoainishwa; na kuwajengea Wakaguzi uwezo wa kufanya ukaguzi katika maeneo mapya ya ukaguzi pamoja na ukaguzi katika uhalifu wa kifedha kwa kutumia mtandao (financial crimes auditing).

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2019/20


Makadirio ya Mapato


57.        Mheshimwa Spika, katika mwaka 2019/20, Wizara inakadiria kukusanya maduhuli kiasi cha shilingi 967,042,379,000 (bilioni 967.04) kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na gawio, kodi za pango, marejesho ya mikopo, michango kutoka katika taasisi na mashirika ya umma, mauzo ya leseni za udalali na mauzo ya nyaraka za zabuni. Mchanganuo wa maduhuli yanayokadiriwa kukusanywa kwa mafungu ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na. 6 ukurasa wa 181 wa kitabu cha Hotuba yangu.

Makadirio ya Matumizi kwa Mwaka 2019/20


58.        Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20 Wizara ya Fedha na Mipango, Taasisi zake pamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi inakadiriakutumia kiasi cha shilingi 11,942,986,578,719 (trilioni 11.94). Kati ya fedha hizo, shilingi 11,212,404,636,988 (trilioni 11.21) ni kwa ajili matumizi ya kawaida na shilingi 730,581,941,731 (bilioni 730.58) ni matumizi ya maendeleo. Matumizi ya kawaida yanajumuisha shilingi 608,371,517,988 (bilioni 608.37) kwa ajili ya mishahara na shilingi 10,604,033,119,000 (trilioni 10.60) kwa ajili ya matumizi mengineyo. Aidha, matumizi ya maendeleo yanajumuisha shilingi 677,000,000,000 (bilioni 677.00) fedha za ndani na shilingi 53,581,941,731 (bilioni 53.58) ni fedha za nje.

MAOMBI YA FEDHA KWA MAFUNGU


Fungu 50 – Wizara ya Fedha na Mipango


59.        Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a)Matumizi ya kawaida - shilingi 65,713,430,000 (bilioni 65.71). Kati ya hizo:

(i)        Mishahara - shilingi 37,920,916,000 (bilioni 37.92); na
(ii)       Matumizi mengineyo – shilingi 27,792,514,000 (bilioni 27.79).

(b)Miradi ya Maendeleo – shilingi 34,763,757,000 (bilioni 34.76). Kati ya hizo:

(i)      Fedha za Ndani – shilingi 13,000,000,000 (bilioni 13.00); na
(ii)     Fedha za Nje - shilingi 21,763,757,000 (bilioni 21.76).

 

Fungu 21 – HAZINA


60.        Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

(a)Matumizi ya Kawaida – shilingi 1,272,801,249,988  (trilioni 1.27). Kati ya hizo:

(i)          Mishahara - shilingi 536,520,631,988 (bilioni 536.52); na
(ii)         Matumizi mengineyo – shilingi 736,280,618,000 (bilioni 736.28) ambazo ni kwa ajili ya matumizi ya idara, taasisi zilizo chini ya Fungu hili, pamoja na matumizi maalum.

(b)Miradi ya maendeleo – shilingi 683,717,888,733 (bilioni 683.71). Kati ya hizo:

(i)          Fedha za Ndani - shilingi 656,000,000,000(bilioni 656.00); na

(ii)         Fedha za Nje - shilingi 27,717,888,733 (bilioni 27.71).

Fungu 22- Deni la Taifa


61.        Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

Matumizi ya kawaida – shilingi 9,730,012,708,000 (trilioni 9.73). Kati ya hizo:

(i)          Mishahara - shilingi 8,885,708,000 (bilioni 8.88); na

(ii)         Matumizi mengineyo - shilingi 9,721,127,000,000 (trilioni 9.72)

Fungu  23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali


62.        Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwakiasi cha fedha kama ifuatavyo:

(a)Matumizi ya kawaida - shilingi 44,066,048,000 (bilioni 44.07). Kati ya hizo:

(i)          Mishahara – shilingi 7,029,314,000 (bilioni 7.03); na
(ii)         Matumizi mengineyo - shilingi 37,036,734,000 (bilioni 37.04).

(b)Miradi ya Maendeleo – shilingi 3,300,000,000 (bilioni3.30). Kati ya hizo:

(i)          Fedha za ndani – shilingi 2,000,000,000 (bilioni 2.00);na
(ii)         Fedha za Nje  - shilingi 1,300,000,000 (bilioni 1.30)

Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa HAZINA


63.        Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

(a)     Matumizi ya kawaida – shilingi 40,510,802,000 (bilioni 40.51). Kati ya hizo:

(i)       Mishahara – shilingi 3,281,016,000(bilioni 3.28); na
(ii)      Matumizi mengineyo – shilingi 37,229,786,000 (bilioni 37.23).

(b)         Miradi ya Maendeleo – shilingi 2,300,000,000 (bilioni2.30). Kati ya hizo:

(i)       Fedha za ndani – shilingi 1,000,000,000 (bilioni 1.00); na
(ii)      Fedha za Nje  - shilingi 1,300,000,000 (bilioni 1.30).

Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha


64.        Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
Matumizi ya Kawaida - shilingi 2,207,935,000 (bilioni 2.20)
Kati ya hizo:

(i)    Mishahara - shilingi 649,793,000 (milioni 649.79); na
(ii)   Matumizi mengineyo - shilingi 1,558,142,000 (bilioni 1.55).

 

Fungu 13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu


65.        Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

(i)    Matumizi ya mengineyo - shilingi 2,015,586,000 (bilioni 2.01); na

(ii)   Matumizi ya Maendeleo – shilingi 200,295,998 (milioni 200.29)  ambazo ni fedha za nje.

Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi


66.        Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

(a)Matumizi ya kawaida – shilingi 55,076,878,000 (bilioni 55.07). Kati ya hizo:

(iii)    Mishahara – shilingi 14,084,139,000(bilioni 14.08); na
(iv)    Matumizi mengineyo – shilingi 40,992,739,000 (bilioni 40.99)

(b)Miradi ya Maendeleo – shilingi 6,300,000,000 (bilioni 6.30). Kati ya hizo:

(iii)    Fedha za ndani – shilingi 5,000,000,000 (bilioni 5.00); na
(iv)    Fedha za Nje  - shilingi 1,300,000,000 (bilioni 1.30).

SHUKRANI


67.        Mheshimiwa Spika, napenda nirudie tena kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwasilisha hotuba hii mbele ya Bunge lako Tukufu. Aidha, kwa namna ya pekee kabisa naomba nitumie fursa hii kuwashukuru Washirika wa Maendeleo wote wakiwemo nchi na mashirika ya kimataifa ambao wamekuwa wakisaidia kwa namna mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Vilevile, napenda kuwashukuru Watanzania wote wenye mapenzi mema na uzalendo kwa nchi yao ambao wamekuwa wakilipa kodi stahiki na kwa hiari. Naomba nitumie fursa hii kuwaambia kuwa, mchango wao katika ujenzi wa Taifa letu unathaminiwa sana na utaendelea kukumbukwa hata kwa vizazi vijavyo.

68.        Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, napenda nikushukuru tena wewe binafsi, kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha hoja hii  pamoja na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii inapatikana katika tovuti ya Wizara kwa anuani yawww.mof.go.tz

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

 

Kanuni bora za ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili)....Soma Hapa Uwe Tajiri

$
0
0
Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. 

Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi.

 Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. 

Muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.

Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku
Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
1.  Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.

2. Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe na kufukiwa.

3.  Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.

4.  Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.

5.  Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.

6.  Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.

7.Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.


Magonjwa na kinga kwa kuku wote

1.Ndui ya kuku
Huathiri sana vifaranga wanaokua na ujitokeza kwa wingi wakati wa mvua za muda mrefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na manyoya.

2.Mdondo/kideri
Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari katika magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.

3.Ukosefu wa vitamini A
Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.

4.Kosidiosisi
Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokua. Kuku hudhoofika, manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.

5.Viroboto, chawa na utitiri
Hawa ni wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga na kuatamia.

6.Minyoo
Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo.


Chakula cha ziada
1.Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.

2.Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai).

3.Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kama nyongeza ya protini.

4.Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.

5. Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.

6Mwagia maji hadi kila kilichomo kilowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chungu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuhi, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.

Utotoleshaji wa vifaranga
Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku.

Sifa za jogoo bora
1.  Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.

2.  Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi mueke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.

Sifa za tetea bora
Tetea bora ni yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.

Uhifadhi wa mayai
1.  Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.

2.  Tumia kasha lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.

3.  Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.

4.  Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.

5.  Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.

Kuatamiza mayai
1.  Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.

2.  Mayi 10 hadi 12 yanatosha kuatamia.

3.  Mayai ya kuatamiza yasizidi wiki 2 toka kutagwa.

4.  Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku wa kuyaatamia.

5.  Mayai ya kuatamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu na safi au kilichowekwa spiriti

Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja
1.  Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;

2.  Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.

3.  Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kisha wawekee kuku wote mayai yenye mbegu.

Matunzo ya vifaranga ili kuzuia vifo
Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifaranga wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;

Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine
1.  Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasiende mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.

Chanjo ya mdondo kideri/lufuo
Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.

Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia hadi wakifikisha wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi 3

Kinga dhidi ya kosidiosisi
Kinga ya kosidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.

1.  Wape dawa ya amprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya kosidiosisi.

2.  Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa katika maji au pumba

3.  Kama vifaranga wadogo wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvaa koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;

Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu

Hitimisho
1.  Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku ni visafi kuepusha magonjwa.

2.  Usichanganye kuku na bata katika banda moja

3.  Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.

4.  Kideri, kosidiosisi, ndui na upungufu wa vitamini A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.

5.  Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.

6.  Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri, fuata maelezo kuzuia vifo.

7.  Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.

8.  Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.

Mama Aliyetelekezwa Na Mmewe Baada Ya Kujifungua Mapacha Wanne Atua Bungeni Dodoma

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mama aliyejifungua watoto Mapacha wanne Radhia Solomon[24] mkazi wa Chemchemi  Magomeni  jijini Dar ES salaam na kutelekezwa na mmewe kwa madai ya kukwepa majukumu leo Juni 3,2019 amewasili bungeni jijini Dodoma ambapo bunge limeridhia kila mbunge wa kiume kumchangia Sh.Laki moja na  kila mbunge wa kike kumchangia Sh.elfu hamsini fedha ambazo zitatumika kumsaidia kujikimu na kuwatunza watoto hao.
 
Akizungumza leo Juni,3,Bungeni jijini Dodoma Spika wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema  jukumu la utunzaji wa watoto ni la kila jamii hivyo bunge limeamua kufanya mchango huo kwa wabunge ili kumsaidia mama na watoto huku akiwaasa wanaume kuacha tabia ya kutelekeza familia zao.
 
Ikumbukwe kuwa Radhia Solomon alijifungua watoto mapacha wanne Januari 8,2019 katika  hospitali ya Muhimbili Dar Salaam ,watoto wa kike wawili Faudhia  na Fardhia  pamoja na wa kiume wawili Suleiman na Aiman  ni pacha wanne ambao  kila mmoja alikuwa na mfuko wake wa uzazi  na gharama ya kuwanunulia maziwa ya SMA ya Kopo  ni Sh.Elfu 40 kwa siku  kwani  alipojifungua afya yake haikuwa nzuri kunyonyesha hali iliyosababisha Mmewe kushindwa kumudu gharama na kuwatelekeza .

Waziri Mkuu: Kamilisheni Ujenzi Wa Magereza Za Wilaya

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa Jeshi la Magereza nchini ukamilishe mkakati wa ujenzi wa magereza za wilaya kwa wilaya zisizokuwa na magereza.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Juni 3, 2019) wakati akifungua Gereza la wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Uzinduzi huo umefanyika kwenye viwanja vya gereza hilo.

Waziri Mkuu amesema uwepo wa magereza katika wilaya zote nchini utasaidia kumaliza tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu kwenye magereza ya jirani.

“Kutokuwepo kwa magereza ya wilaya kunasababisha msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza ya jirani, pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa haki.”

Waziri Mkuu amesema kwamba ufunguzi wa gereza la Ruangwa utatatua tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu katika Gereza la wilaya ya Nachingwea

Awali wakazi wa wilaya hiyo waliokabiliwa na tuhuma mbalimbali au waliohukumiwa vifungo walikuwa wakipelekwa katika Gereza la wilaya ya Nachingwea.

Amesema kitendo cha kupelekwa Nachingwea kilikuwa kikiwanyima wafungwa na mahabusu fursa ya kuonana na ndugu au mawakili wao kutokana na umbali uliokuwepo.

“Mbali na ndugu na jamaa kushindwa kwenda kuwaona ndugu zao pia Jeshi la Polisi lilikuwa likilaumiwa kuwa linawachelewesha mahubusu kuja kusikiliza mashauri yao.”

Waziri Mkuu amesema uwepo wa gereza hilo katika wilaya ya Ruangwa umeipunguzia Serikali gharama za kuwasafirisha mahabusu na wafungwa kwenda Nachingwea.

Awali, Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Gereza la Wilaya ya Ruangwa ni nyenzo muhimu katika kuimarisha ulinzi na usalama wa wilaya hiyo.

Amesema gereza hilo ni chachu ya kuimarika kwa uchumi wa wilaya hiyo kwa kupitia sekta ya kilimo kwani kutakuwa na kambi za kilimo, hivyo wananchi nao watajifunza. 

 “Wananchi msilione gereza hili kama adui kwenu, halijaja kuwafunga bali lipo kwa ajili ya kuimarisha amani, ulinzi na usalama wa wilaya yetu pamoja na kutoa elimu mbalimbali.”

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike amesema ujenzi huo umefanywa na kikosi cha ujenzi cha Magereza kwa kutumia nguvukazi ya wafungwa.

Amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa gereza hilo imekamilika na imegharimu sh. bilioni 1.5 hivyo umekamilisha uwepo wa magereza katika wilaya zote za mkoa wa Lindi.

Kamishna huyo amesema ujenzi huo ungefanywa na mkandarasi wa nje ungegharimu sh. bilioni 2.226, hivyo kwa kutumia kikosi cha Magereza wameokoa sh. milioni 635.675.

Amesema kwa sasa gereza hilo lina uwezo wa kuwahifadhi wahalifu 250 hadi 280 na likikamilika itakuwa na uwezo wa kuwahifadhi wahalifu 500.

Kamishna Kasike amesema gereza hilo lina ardhi yenye ukubwa wa ekari 80, ambapo ekari saba zitatumika kwa ajili ya majengo ya gereza, maegezo ya magari na karakana.

“Ekari 56 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 100 za makazi, ekari sita ujenzi wa majengo ya huduma kama zahanati na ekari nane zitatumika katika kilimo cha bustani.”

Baadhi ya wananchi waliohudhuria ufunguzi huo wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuboresha huduma za jamii.

Mmoja wa wananchi hao Zena Selemani amesema kabla ya ujenzi wa gereza hilo walikuwa wanashindwa kuwatembelea ndugu zao walofungwa katika gereza la Nachingwea.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Rais Magufuli akutana na Askofu Gwajima Ikulu

$
0
0
RAIS John Magufuli amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima leo Juni 3, 2019, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo yao, Gwajima amempongeza Magufuli kwa ujenzi wa mradi wa Stiegler’s Gorge akisema umeme wa mradi huo utakuwa mkubwa kuliko umeme wowote ambao Tanzania ilishawahi kuzalisha tangu uhuru, hivyo yatakuwa ni manufaa makubwa kwa taifa letu.

“Tuelewe ili ule chips yai lazima uvunje mayai, namshukuru rais kwa juhudi za Stiegler’s Gorge, tutakapozalisha umeme mwingi kuliko tuliozalisha zamani.  Kama unavyojua watu wengi wa Magharibi wanasema eneo hilo ni la mazingira lakini ukweli ni siasa tu.


Rais Magufuli awapongeza Watanzania kwa kuitikia wito wa kuachana na mifuko ya plastiki......Afanya ziara ya kushtukiza Feri Dar es Salaam.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewapongeza Watanzania kwa kuitikia wito wa Serikali wa kuacha kutumia mifuko ya plastiki ambayo ina madhara makubwa katika mazingira na viumbe hai wakiwemo binadamu.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo June 3,2019 wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko la samaki la Feri Jijini DSM baada ya kufanya ziara ya kushtukiza sokoni hapo na kujionea wafanyabiashara na wanunuzi wa samaki wakitumia mifuko mbadala.

Rais Magufuli amempongeza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wote ambao wamesimamia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa tangu mwaka 2016 kuhusu kuondoa matumizi ya mifuko ya plastiki kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, Rais Magufuli amewataka wafanyabiashara kutotumia mwanya huo kuuza mifuko na vifungashio  mbadala kwa bei kubwa na badala yake amewataka wafanyabiashara hao pamoja na wawekezaji wa ndani na nje kujenga viwanda vya kutengeneza mifuko na vifungashio kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini.

Aidha, Rais Magufuli ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuwa na vifaa vya kubebea bidhaa wanazozinunua madukani na masokoni ili kuepuka gharama kununua vifungashio ama mifuko mbadala.

Rais Magufuli ameziagiza mamlaka zinazohusika, kuhamasisha utengenezaji wa mifuko na vifungashio mbadala hapahapa nchini ili kuongeza ajira katika viwanda vya kutengenezea bidhaa hizo badala ya kuacha wafanyabiashara wakigeuza nchi kuwa mahali pakuingiza bidhaa hizo kutoka nje ya nchi.

Akiwa katika soko hilo la Feri, Rais Magufuli amenunua samaki kutoka kwa wafanyabiashara wadogo wanaotumia vitambulisho vya wajasiriamali na amewapongeza kwa juhudi zao za kujitafutia kipato halali.

Ameiagiza Manispaa ya Ilala kupunguza tozo ya pango kwa wapaa samaki kutoka shilingi 1,000 hadi shilingi 500 kwa siku na ameitaka manispaa hiyo kutenga shilingi Milioni 10 kutoka kwenye makusanyo ya soko hilo kujenga jengo jingine la wafanyabiashara wasiouza samaki kama vile Mama Lishe, Baba Lishe na wauza bidhaa zingine ambao hawanufaiki na jengo la wauza samaki ambalo mwaka jana alichangia shilingi Milioni 20.

Rais Magufuli amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la wauza samaki ambalo alilichangia shilingi Milioni 20 mwaka jana ambapo ameagiza Manispaa ya Ilala ifanye ukaguzi wa gharama zilizotumika kutokana na kuwepo wasiwasi wa matumizi mabaya ya fedha.

Ameiagiza Manispaa ya Ilala na Menejimenti ya soko la Feri kuweka utaratibu wa kuwapokea wafanyabiashara wanaoingiza samaki sokoni hapo kwa muda wote wa saa 24, kuweka umeme na maji katika jengo mojawapo la wafanyabiashara wa samaki ndani ya siku 5 na kuingiza umeme katika jengo la huduma ya Msalaba Mwekundu (Red Cross) lililopo sokoni hapo.

Huku wakimshangilia Wafanyabiashara wa soko la Feri wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa jinsi anavyowapigania Watanzania wanyonge wakiwemo wafanyabiashara wadogo na wamemhakikishia kuwa watatekeleza maagizo yake ya kutotumia mifuko ya plastiki kama inavyoelekezwa katika sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

Taarifa Ya Kusitishwa Kwa Matumizi Ya Pasipoti Za Zamani Zinazosomeka Kwa Mashine (MRP) Ifikapo Tarehe 31 Januari 2020

$
0
0
Kufuatia kuzinduliwa na kuanza kutumika  kwa Pasipoti Mpya za Kielektoniki  (e Passport), Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji inapenda kuufahamisha umma kuwa, tayari imekamilisha  ujenzi wa miundo mbinu ya utoaji wa huduma ya pasipoti hizo katika Mikoa ishirini na tisa (29), Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu, Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar na Ofisi za balozi za Tanzania  Ishirini  na tatu (23) zilizopo nje ya Nchi;

ambazo ni Uingereza (London), Ufaransa (Paris), Marekani (Washington DC na  New York), Canada (Ottawa), Israel (Telaviv), Saudi Arabia (Jeddah na Riyadh), Comoro (Moron), Kenya (Nairobi na  Mombasa), Ujerumani (Berlin), Algeria (Algiers), Italia (Rome), Nigeria (Abuja), Misri (Cairo), Uholanzi (The Hague), Ubelgiji (Brussels), Zambia (Lusaka), India (New Delhi), Malawi (Lilongwe), China (Beijing), Malaysia (Kuala Lumpur).

Nchi ambazo zitafunguwa Mfumo huo hivi karibuni ni Afrika Kusini, Msumbiji na Zimbabwe. Aidha, kwa Balozi zilizosalia, kazi ya ufungaji mitambo ya huduma hiyo inaendelea na itakamilika hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu.

Kwa Msingi huo, Idara ya Uhamiaji inawakumbusha  Watanzania wote Ndani na Nje ya Nchi kuwa matumizi ya Pasipoti za zamani yatasitishwa ifikapo tarehe 31 Januari, 2020.

Aidha, idara inawasisitiza wale wote wenye Pasipoti za zamani (MRP) na wanaokusudia kusafiri nje ya Nchi hivi karibuni, kuhakikisha wanabadilisha Pasipoti zao mapema kabla ya mwezi Julai mwaka huu ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza wa kurejeshwa katika Viwanja vya Ndege na Vituo vya Mipakani wakati wa kutoka Nchini. Ni hitajio la Kisheria kwa Pasipoti kuwa na angalau uhai wa kuanzia miezi sita ili mwenye pasipoti hiyo aweze kuomba Visa ya Nchi anayokwenda na kuruhusiwa kuondoka Nchini kupitia Vituo vya kuingia na kutoka nchini.

Imetolewa na
Ally M. Mtanda (SI)
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji
Makao Makuu, Dar es Salaam
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images