Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wataalam Wa Sheria Waitaka Sheria Mpya Ya Kudhibiti Vimelea Hatarishi Nchini

$
0
0
Na. OWM, ARUSHA
Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri kutungwa kwa sheria mpya itakayohusika na  ulinzi na usalama wa  vimelea hatarishi ili kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo kutoweza kueeneza  magonjwa  kwa binadamu.

Sheria hiyo imeshauriwa kuzingatia dhana ya Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu, lengo nikusaidia katika kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa kuvichukua  vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kuvisafirisha na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, uliofanyika kwa siku tatu na kufungwa leo  tarehe 31 Juni, 2019, Jijini Arusha, kwa pamoja,  wataalam wa sekta za Afya  na wanasheria wa sekta hizo wamebainisha kuwa uwepo wa sheria hiyo utasaidia kuimarisha usalama  na ulinzi kwa wanaohusika na shughuli za vimelea hivyo, mafunzo kwa wataalamu hao, miundo mbinu  ya maabara, pamoja na kuainisha orodha ya vimelea hivyo.

Wataalamu wa sekta za Afya walioshiriki mkutano huo, wamebainisha kuwa, sheria hiyo ni ya muhimu kwa kuzingatia kuwa, Dunia imekuwa na tishio kubwa la magonjwa ya kuambukiza yanayoweza kusambaa kwa muda mfupi na kusababisha madhara makubwa kwa binadamu, mifugo, wanyama pori na kuleta uharibifu wa mazingira. Wamefafanua kuwa,  Tafiti zinabainisha kuwa kila mwaka huibuka magonjwa ambukizi mapya kati ya matano hadi Nane duniani. Hivyo inakadiriwa ifikapo mwaka 2030, dunia itakuwa na magonjwa ambukizi mapya 30.

Aidha, wamebainisha kuwa, Tafiti mbalimbali duniani zinaonesha pia, kuwa asilimia 60% ya vimelea vya magonjwa ambayo huambukizwa binadamu vinatoka kwa wanyama hususani  wanyamapori na baadae kusababisha magonjwa kwa binadamu.Tayari Tanzania kupitia Dhana ya Afya Moja,  imeainisha magonjwa sita ya kupewa kipaumbele ambayo ni; Kimeta, Kichaa cha mbwa, Mafua ya ndege, Homa ya Bonde la ufa, Malale na Ugonjwa wa  kutupa mimba  wanyama.

 Akiongea wakati wa akifunga mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe amebainisha kuwa serikali imedhamiria kuijenga jamii ya watanzania yenye Afya bora kwa kuikinga na majanga yatokanayo na magonjwa ya mlipuko,  hivyo ushauri huo wa wanasheria na wataalam wa sekta hizo za afya  utaratibiwa kwa uhakika ili kuweza kuijenga jamii salama.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini.

Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Yafanyika kwa Mara ya Kwanza.

$
0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Vyuo na Taasisi za Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mara ya kwanza limeandaa Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ambayo yamefanyika Jijini Dodoma tarehe 27 hadi 30 Mei, katika uwanja wa Jamhuri.
 
Maonesho hayo yaliyofanyika kwa takribani siku tano na kufungwa leo na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ambapo kabla ya hotuba ya kufunga maonesho hayo, Ole Nasha aliweza kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Vyuo na Taasisi za Elimu na Mafunzo.
 
Ole Nasha amesema kuwa, maonesho hayo yametoa fursa kubwa kwa wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ambapo wameweza kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Vyuo na Taasisi na Ufundi za Elimu ya Mafunzo na Ufundi. Vile vile kufahamu huduma na bidhaa zinazotolewa na Taasisi hizo.
 
Vile vile amesema kupitia maonesho hayo Vyuo na Taasisi zilizoshiriki zimeweza kukutana pamoja na wadau hao, hivyo kupata fursa ya kujibu changamoto pamoja na kupokea ushauri kutoka kwa wadau wao.
 
Aidha amesema, maonesho hayo yametoa fursa kwa wanafunzi na wazazi kufahamu vyuo na masomo wanayotoa  pamoja na kupata ushauri wa chuo gani mwanafunzi anaweza kujiunga kutokana na ufaulu wake.
 
Ole Nasha ameitaka NACTE kuhakikisha maonesho hayo yanafanyika kila mwaka ili wadau wa elimu ya ufundi na mafunzo waendelee kunufaika na kupata uelewa wa shughuli zinazofanywa na vyuo na taasisi za elimu ya ufundi na mafunzo.
 
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa NACTE Dkt. Adolf Rutayuga amesema jumla ya Taasisi 100 zimeshiriki maonesho hayo ambapo kati ya Taasisi hizo 71 ni vyuo vya ufundi na mafunzo, 11 ni vyuo vikuu. 5 kampuni kupitia elimu ya mafunzo na ufundi na 13 ni kampuni za biashara.
 
Kauli mbiu ya maonesho hayo ni Elimu ya Ufundi na Mafunzo kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda Tanzania.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya June 1

BREAKING: Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Elimu ya Kati na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka wa Masomo 2019 .

Ujenzi wa stendi,soko la kisasa Njombe wamkosha Jafo

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa OR Tamisemi Selemani Jafo amepongeza kuanza kutumika kwa kituo kipya cha mabasi Njombe mjini kinacho iwezesha halmashauri hiyo kukusanya shilingi laki nane kwa siku licha ya kuanza kutumika wiki tatu zilizopita.

Jafo ametoa pongezi hizo mkoani Njombe mara baada ya kufika na kukagua maendeleo ya ukamilishwaji wa kituo hicho  kipya cha mabasi kilicho anza kutumia mei 11 huku baadhi ya maeneo ndani kituo hicho yakiendelea kukamilishwa.

“Ninachofahamu kama mmeanza kukusanya shilingi laki 8 kwa siku,tena stendi ndio kwanza ngeni inaanza na mmeniambia ndani ya wiki moja mmekusanya milioni tano maana yake kwa mwezi mnawastani sio chini ya shilingi ya milioni 20 na kwa mwaka mkiendele itakuwa sio chini ya milioni 240 kwa kitega uchumi hiki kimoja na maana yake  itakapoanza kufanya kazi vizuri itafika muda mnaweza mkakusanya hata milioni 20 kwa wiki”alisema Jafo

Kuhusu ujenzi wa soko kuu la mjini Njombe Waziri amesema kuwa soko hilo ndio litakuwa lakisasa kwa kanda nzima na limejengwa kisasa na kumtaka mkandarasi kukamilisha kwa muda ili liweze kukamilika.

“Hapa ninyi soko mnatengeneza zuri sana tunajenga masoko haya maeneo kadhaa,tunajenga Dodoma tunajenga Mtwara  lakini kwa hili nimeridhika isipokuwa nendeni kwa mda huo, mwezi wa kumi kazi iwe imekamilika,Naomba niwaambie katika hii kanda, Njombe ninyi ndio mtakuwa na soko zuri tena la kisasa na mkandarasi amefanya kazi nzuri mimi nimeridhika nalo sana”aliongeza Jafo

Kwa upande wake msimamizi wa mradi wa stendi mhandisi Tembo David amesema stendi hiyo imekamilika kwa zaidi ya asilimia 96,huku akiahidi kukamilisha sehemu zilizobakia za ujenzi kabla ya june 30.huku changamoto kubwa kwa sasa ikiwa ni msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani VAT kwa kuwa mpaka sasa wakandarasi hawajapata.

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminata mwenda ameahidi kusimamia kazi kwa nguvu ili kuikamilisha miradi hiyo kwa wakati.

“Mheshimiwa waziri ameona kazi zetu na tumemueleza changamoto na ametoa maelekezo ya muda wa kumaliza kazi na sisi kuanzia sasa tutasimamia hii kazi kwa nguvu sana”alisema Iluminata Mwenda.

Wizara Ya Ardhi ,nyumba Na Maendeleo Ya Makazi Yatarajia Kukusanya Sh.bilioni 180 Kwa Mwaka Wa Fedha 2019/2020

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo Mei,31,2019 imewasilisha hotuba ya Makadirio ya  Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 ambapo inatarajia kukusanya Sh.Bilioni 180 .
 
Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara 2019/2020, bungeni jijini Dodoma,Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mhe.William Lukuvi amesema Wizara yake inatarajia kukusanya Sh.Bilioni 180 kutokana na kodi ya pango la ardhi,ada na tozo mbalimbali zinazohusiana na sekta ya ardhi.
 
Waziri Lukuvi amesema lengo la ukusanyaji wa fedha hizo litasaidia kufanikisha mikakati mbalimbali ya wizara ikiwemo kuimarisha  mifumo ya TEHAMA ya Utunzaji wa kumbukumbu na kuboresha taarifa za ardhi,kurahisisha ukadiriaji wa pango la ardhi na tozo mbalimbali,kutumia mfumo wa kielektroniki na kuendelea kutoa elimu kwa umma.

Aidha,Waziri Lukuvi amesema,katika mwaka 2018/2019 Wizara iliidhinishiwa Sh.Bilioni 65.98 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya Maendeleo ,kati ya hizo,Sh. Bilioni  17.68 ni kwa ajili ya mishahara ,sh.bilioni 17.76 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo n ash.bilioni 30.54 kwa ajili ya miradi ya Maendeleo.
 
Waziri Lukuvi amefafanua,baada ya uhakiki wa Madeni  uliofanywa na Wizara ya Fedha na Mipango ,Wizara ilipewa Sh.bilioni 12.8 kwa ajili ya kulipa madeni ya wazabuni  na hivyo kuifanya bajeti  ya Wizara  kuwa Jumla ya Sh.Bilioni 78.8 hadi kufikia tarehe 15 Mei,2019.
 
Katika hatua nyingine,Waziri Lukuvi amesema hadi kufikia tarehe 15,Mei,2019 ,wizara imeandaa na kusajili  hati za hakimiliki 47,688  na kusajili nyaraka nyingine za kisheria 25,045 chini ya sheria ya usajili wa Ardhi  huku Wizara ikitarajia kusajili Hatimiliki na nyaraka za kisheria 152,000.
 
Katika utatuzi wa Migogoro ya Ardhi hapa nchini kupitia kauli mbiu  ya Funguka na Waziri , Waziri Lukuvi amesema Jumla ya Malalamiko  13,055 yalipokelewa na  malalamiko 10,174  yamefanyiwa kazi  na 2,719 yanaendelea kufanyiwa kazi.

Wananchi Dodoma Wasalimisha Mifuko Ya Plastiki

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kufuatia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililotelewa na Waziri mkuu wa jamhuri ya muungnao wa Tanzania Mh Kasim Majaliwa wananchi jijini Dodoma wamejitokeza kusalimisha mifuko ya plastiki  katika kampuni ya usafi ya Green waste  tawi la Dodoma ambayo imefanya uzinduzi wa vituo vya kukusanya mifuko ya  plastiki.

Akizungumza katika uzinduzi wa vituo vya kupokea mifuko ya plastiki  mkurugenzi wa Halmashauri ya  Jiji la Dodoma Bwana Godwin Kunambi amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutii sheria kwani  wameunda kamati mbalimbali ambayo itapita kila nyumba na maduka ili mifuko ya plastiki .
 
Aidha kunambi ameongeza kuwa Jiji la Dodoma limetoa elimu ya mifuko ya plastiki katika ngazi ya Mtaa,Kata,Wilaya na Taasisi zote za jiji huku akisema zipo baadhi ya taasisi zinashindwa kulipa hela ya usafi
 
Akizundua vituo vya kupokea mifuko  ya plastiki Mkuu wa Wilaya ya Dodoma  Bwana Patrobas Katambi Ambaye ndiye mgeni rasmi katika uzinduzi huo amesema kuwa wajibu wa kutunza mazingira ni jukumu la kila mwananchi ambpo amesema kuwa kwa taasisi ambazo hazilipi tozo za taka watachukuliwa sheria.

Kwa upande wake Ally Mfinanga ambaye ni Afisa Mazingira wa Jiji la Dodoma amesema kuwa kwa  atakaye bainika kuzalisha na kuingiza mifuko faini yake itakuwa ni shilingi  milioni 20.

Hatahivyo, Katambi amesema kuwa  jiji la Dodoma halitakuwa na msamaha kwa mtu yeyote atakaye kutwa na mfuko wa plastiki huku akisema kuwa watu ambao wanauza mifuko hiyo waisalimishe katika vituo ambavyo vinapokea mifuko hiyo.
 
Ikumbukwe kuwa Mwisho wa Matumizi ya Plastiki hapa nchini ilikuwa jana  Mei.31 2019 na atakayebainika anauza au kutumia mfuko wa Plastiki kuanzia  leo  Juni 1,2019 hatua kali za  kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Dkt. Magufuli Kuapishwa Kwa Rais Wa Malawi

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehudhuria sherehe za kumwapishwa Rais wa Malawi, Profesa, Arthur Peter Mutharika zilizofanyika jijini Blantyre.

Amehudhuria sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzi, Blantyre. jana (Ijumaa, Mei 31, 2019) kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

Akizungumza baada kuapishwa, Rais Mutharika aliwaahidi wananchi wa Malawi kuwa atawatumikia bila ubaguzi wa itikadi za kisiasa, kidini au ukabila.

Pia alisisitiza kuwa hatavumilia kuona vyama vya siasa, madhehebu ya dini au mtu yeyoye anaanzisha vurugu kwa nia ya kuikwamisha Serikali.

Rais Mutharika alisema kuwa waliomchagua na wasiomchagua wote ni rafiki zake na amedhamiria kuwatumikia kwa moyo wa upendo na haki.

“Uchaguzi umekwisha mshindi amepatikana, hivyo mnapaswa kuiunga mkoano serikali iliyodhamiria kuwaletea maendeleo wananchi wa Malawi.”

Alisema wananchi wa Malawi wameamua kumchagua Profesa Mutharika na Chama cha Democratic Progressive Party (DPP) hivyo lazima waheshimiwe.

Awali, Waziri Mkuu alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chileka alipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Ben Botolo.

Viongozi wengine waliokuwepo uwanjani hapo ni pamoja na Balozi wa Tanzani nchini Malawi, Ben Mashiba na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Chembe Muntali.

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais Mstaafu wa Malawi, Bakili Muluzi. Mheshimiwa Majaliwa amerejea nchini leo jioni.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Hasunga aanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kuiuzia Zimbabwe mazao ya kilimo

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb)  tarehe 31 Mei 2019 ameitisha kikao cha dharura na Wakurugenzi wa Taasisi na Idara mbalimbali za Wizara ya Kilimo lengo ni kuanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuiuzia nchi ya Zimbabwe mahindi na mazao mengine kiasi cha Tani Laki Nane (800,000).

Itakumbukwa mapema wiki hii, Rais John Pombe Magufuli alipoitembelea Zimbabwe kwa mwaliko wa Mwenyeji wake Rais Emmerson Mnangagwa. Rais Mnangagwa alimweleza Rais Magufuli kuwa Zimbabwe inakabiliwa na upungufu wa chakula na kuiomba Tanzania iiuzie sehemu ya chakula chake cha ziada ombi ambalo Rais Magufuli alilikubali.

Waziri Hasunga amesema ujumbe kutoka Serikali ya Zimbabwe utawasili nchini kuanzia Siku ya Jumanne ya Tarehe 3 Juni na unatajiwa kuwa nchini mpaka tarehe 7 ya Mwezi Juni, 2019.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa ujumbe huo kutoka Zimbabwe unakuja kwa ajili ya kuangalia na kujiridhisha kuhusu mambo ya msingi kama ubora wa chakula na mambo mengine ya awali.

Waziri wa Kilimo amesema kimsingi Serikali zote mbili zimekubaliana kuwasaidia Wananchi kwa njia ya biashara na kuongeza kuwa huu ni mwanzo kwa kufanya biashara endelevu baina ya nchi hizi mbili na kuongeza kwa biashara hiyo, itakuwa endelevu mwaka hadi mwaka.

Mhe. Hasunga amesema Zimbabwe imefikiria pia kuanza kununua mazao mengine kama korosho kwa kuwa imeona fursa ya kupata mazao yenye ubora na kwa bei nzuri ipo Tanzania kwamba baadae mazao mengine ya mbegu za mafuta, jamii ya mikunde, mboga na matunda yataanza kununuliwa na Taifa hilo la Kusini mwa Afrika.

Serikali Yaendelea na ukarabati mkubwa wa reli ya kati inayoanzia Dar Es Salaam kwenda mikoa ya Tabora,Kigoma hadi Mwanza

$
0
0
Na  Christopher Philemon
Serikali imesema inafanya ukarabati mkubwa wa reli ya kati inayoanzia Dar Es Salaam kwenda mikoa ya Tabora,Kigoma hadi Mwanza ambao itagharimu takribani dola 300 za kimarekani.
 
Ukarabati huo umeanza mwaka 2018 utakamilika ifikapo mwaka 2021 na hivyo kurahisisha huduma kwa watumiaji wa usafiri huo wa gari moshi(treni).
 
Akiongea na waandishi wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa eneo la Kilosa hadi Itigi naibu waziri  wa Ujenzi ,uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye,alisema kuwa ukarabati huo mkubwa unaofanywa  ili kuweza kusafirisha mizigo kutoka Dar  es Salaam kwenda nchi za jirani kama Uganda na Rwanda.
 
Nditiye alisema ukarabati huo pia utasaidia  kusafirisha abiria kwenda mikoa ya Kigoma na Tabora kwa siku mbili kutoka Dar es Salaam_kigoma ambapo itakuwa tofauti na hivi sasa gari moshi(treni)hutumia siku tatu.
 
Naibu waziri alitoa wito kwa wananchi na madereva wa magari wanaopita kukatisha reli kuwa makini kwa sababu  ukarabati huo treni itakuwa inakimbia kwa kasi ya kilometa 72 kwa saa.
 
Naye Mhandisi ,Uboreshaji wa Reli ya kati kutoka shirika la Reli Tanzania (TRC) Edwin Leonard alisema  uboreshaji wa reli hiyo unafanywa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC)  inatekelezwa katika  vipande vinne ambayo ni Dar es Salaam- Ngerengere- Kilosa – Itigi hadi Isaka na watanzania zaidi ya elfu mbili na wageni miambili na ishirini  wamepata ajira.
 
Baadhi ya wafanyakazi wa kitanzania walioajiriwa katika kampuni hiyo walisema kuwa kazi hiyo inawasadia kupata kipato cha kuendesha maisha yao.
 
"Kwa kweli tunashukuru ukarabati huu umetupatia kazi na inatusaidia sana sisi kuweza kuendesha maisha yetuna pia tumepeleka watoto shule kwa kazi hii hii"alisema Hamisi Omary

Ukarabati wa reli hiyo unakwenda sambamba na Ujenzi wa madaraja,uinuaji wa tuta la reli  pia kujenga vituo vya kudumu vya kusimama trein pindi lifanyapo Safari zake.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521

Taarifa Toka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi

Waziri Mkuu Awatangazia Neema Wakulima Wa Korosho

$
0
0
*Asisitiza kwamba madai yote kumalizwa ndani ya mwaka huu wa fedha

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa kuwa Serikali italipa fedha hizo ambazo ni zaidi ya bilioni 20 mwaka huu.

Amesema wakulima ambao bado hawajalipwa au kumaliziwa malipo yao baada ya Serikali kumaliza uhakiki majina yao yatapelekwa TADB kwa ajili ya malipo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 1, 2019) katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Lindi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa.

“Wakulima wote wanaodai malipo yao ya korosho watalipwa katika mwaka huu wa fedha kwa kuwa ni haki yao na kwamba Serikali haitodhulumu haki ya mkulima yeyote.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesisitiza suala la uboreshwaji wa miundombinu mbalimbali ya kutolea huduma zikiwemo barabara ili ziweze kupitika kwa urahisi wakati wote.

Amesema uboreshwaji wa mbiundombinu pamoja na huduma nyingine za jamii ni jukumu la watendaji, hivyo wahakikishe wananchi wote wanahudumiwa bila ya kubaguliwa.

“Kila aliyepewa jukumu ahakikishe analitekeleza ipasavyo. Watendaji hakikisheni mnawatumikia Watanzania wote vizuri, kusiwe na ubaguzi wa kisiasa, kidini na kikabila.”

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesema zoezi la malipo ya fedha za korosho zilizohakikiwa linaendele.

Amesema hadi Mei 31 mwaka huu kilo 51,990,999.97 zenye thamani ya sh. bilioni 171,570,299,912 ambazo ni sawa na asilimia 87.6 zimeshalipwa kwa wakulima husika.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kiasi cha bilioni 23,404,086,508 bado hazijalipwa kwa wakulima wa korosho wa mkoa wa Lindi. Korosho hizo zilihakikiwa kituo cha Mtwara.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wabunge wa mkoa wa Lindi, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa pamoja na Wakuu wa Idara.

 (mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Katibu Mkuu Ofisi Ya Makamu Wa Rais Aongoza Oparesheni Ya Ukaguzi Wa Mifuko Ya Plastiki Jijini Dodoma

$
0
0
Wito umetolewa kwa Wakazi wa Dodoma na Wilaya zake  kuacha kabisa kautumia mifuko ya plastiki na kuanza mara moja matumizi ya mifuko mbadala ikiwa ni kutii agizo la Serikali la kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.  

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo wakati wa uzinduzi wa operesheni ya kukagua mifuko ya plastiki katika jiji la Dodoma ambapo ni kutii agizo la Serikali la ukomo wa matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia juni 1. 

Akiongea katika oparesheni hiyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais ndiyo Wasimamizi wakubwa wa mazingira Nchini, hivyo amefurahi kuona elimu juu ya katazo la mifuko ya plastiki kwa jiji la Dodoma imefika kwa Wananchi kwa sababu ambao wamekutwa na mifuko ya plastiki ni wachache sana kulinganisha na Wananchi wanaotumia mifuko mbadala kwa siku ya leo. ‘Elimu imefika kwani kila Mwananchi namuona kabeba mfuko mbadala, vikapu n.k” alisema Injinia Malongo 

Naye Mkuu wa Wilaya wa jiji la Dodoma Mh. Protabas Katambi amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na anawaagiza Wananchi na Wafanyabiashra wa jiji laDodoma  kutii agizo la Serikali na kuachana kabisaa na matumizi ya mifuko ya plastiki.

 ‘Mwananchi atakayekutwa na mfuko wa plastiki hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yake, hili suala syo mchezo mchezo nia agizo la Serikali” alisema Katambi 

Operesheni hiyo ya kukagua mifuko ya plastiki imekuja baada ya Waziri Mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kutoa agizo bungeni kuwa ifikapo juni 1 hakuna Mwananachi atakayeruhusiwa kutumia mifuko ya plastiki Nchini Tanzania. 

Waziri Mkuu Majaliwa Aikabidhi Azam Kombe La Ubingwa Wa Kombe La Shirikisho La Azam

$
0
0
TIMU ya Azam FC imefuzu michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika msimu ujao baada ya kuifunga Lipuli FC bao 1-0 kwenye fainali za Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Mbali na kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, timu ya Azam imeondoka na kitita cha sh. milioni 50, medani pamoja na kombe.

Fainali hizo zimefanyika leo (Jumamosi, Juni 1, 2019 katika uwanja wa Ilulu, Manispaa ya Lindi ambapo ushindi huo unaifanya Azam FC kuungana na Simba kuliwakirisha Taifa kwenye michezo ya Kimataifa itakayoanza Novemba mwaka huu.

Mshambuliaji wa Azam Obrey Chirwa ndio aliyeiwezesha timu yake ya Azam kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya kufunga bao la ushindi katika kipindi cha pili.

Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, timu ya Lipuli FC iliyong’ara kwa kutawala mchezo kwenye kipindi cha kwanza, ilishindwa kutumia nafasi nyingi ilizozipata kuifunga Azam.

Mbali na timu ya Lipuli kuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo, pia timu hiyo imetoa mchezaji bora wa mechi ya fainali, Paul Ngalema pamoja na mfungaji bora wa mashindano hayo Seif Rashid.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Serikali Yaja na Mfumo Mpya wa Ajira ‘Ajira Portal’ Kukabiliana na Vitendo vya Rushwa na Upendeleo

$
0
0
Na Mwandishi Wetu- MAELEZO, Dodoma
Serikali  imewataka Waajiri katika Utumishi wa Umma kuhakikisha kuwa wanatumia mfumo mpya wa Maombi ya Kazi ‘ Ajira Portal’ uliopo chini ya Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira ili kuondoa changamoto zilizokuwepo awali kabla ya kujengwa kwa mfumo huo. 

Akizungumza wakati akifungua  mafunzo kwa waajiri leo Jijini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Kapteni (Mstaafu) George Mkuchika (Mb) amesema kuwa  Waajiri  wote watapaswa kutumia mfumo huo unaowashirikisha waajiri, muombaji wa ajira na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira. 

“ Hakuna sababu ya kila Taasisi kujenga mifumo ya kuendesha michakato ya ajira wakati tayari Serikali imeshawekeza katika ‘ Recruitment Portal’ kupitia Sekretarieti ya ajira” Alisistiza Mhe. Mkuchika 

Akifafanua amesema kuwa Serikali inahitaji watumishi wenye weledi unaoendana na mahitaji ya wakati hasa wakati huu Taifa linaposisitiza ujenzi wa uchumi wa viwanda. 

“Mfumo huu ni muarobaini dhidi ya vitendo vya rushwa,utashi  na upendeleo kwa kuwa utakuwa na uwezo wakuchagua waombaji wa ajira kulingana na sifa zao na nafasi walizoomba” Alisisitiza mhe. Mkuchika 

Aliongeza kuwa mfumo huo utasaidia kupunguza gharama zilizokuwa zikitumika kutangaza nafasi za Ajira kupitia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari . 

Pia alibainisha kuwa mchakato wa kuendesha zoezi zima la kutangaza nafasi za ajira hadi kukamilisha usaili litafanyika kwa muda mfupi tofauti na ilivyokuwa awali na kuchelewesha upatikanaji wa majibu kwa waombaji wa nafasi za ajira. 

Aidha, alizitaka Taasisi zilizopo chini ya Msajili wa Hazina kutumia mfumo wa maombi ya kazi kuendesha michakato ya ajira ili kuwa na uhakika na takwimu sahihi, kumbukumbu na uhakika kwamba wanaoajiriwa Serikalini ni wale waliohakikiwa kupitia Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) na Baraza la Mitihani (NECTA). 

Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amesema kuwa mfumo huo una maeneo makuu matatu lakwanza likiwa ; Eneo la mwombaji wa kazi (Applicant), Eneo la Mwajiri (Employer), Eneo la Sekretarieti ya Ajira( Handling Interview Process and Placement/ Administrator). 

“ Mafunzo haya yamejikita kwenye eneo moja la Mwajiri (employer) ambao kwa mujibu wa mfumo wanajukumu kubwa kuandaa rasimu ya tangazo la ajira kwa mujibu wa muundo, kuingiza kibali cha ajira, kufuatilia maendeleo ya kibali husika na kupokea Watumishi wanaopangwa kwenye sehemu au Taasisi zao za Kazi” Alisisitiza  Bw. Daudi. 

Akizungumzia baadhi ya mafanikio ya Taasisi hiyo  Bw. Daudi amesema kuwa ni pamoja na kuokolewa kwa kiasi kikubwa cha fedha za Serikali zilizokuwa zikitumika kwenye matangazo na pia kupunguza muda wa usaili na uendeshaji wa mchakato mzima wa maombi ya ajira. 

Pia kuongezeka kwa maombi ya kazi, kuongeza uwazi na pia mifumo ya TEHAMA imerahisisha utunzaji wa Taarifa na nyaraka mbalimbali za waombaji kazi. 

Mafunzo haya yaliyotolewa kwa siku mbili kuhusiana na mifumo ya Ajira licha ya kurahisisha utendaji kazi wa ofisi moja moja, pia yataondoa urasimu wa upatikanaji wa taarifa na yatawezesha taarifa kupatikana kwa wakati.

Polepole Asema Wabunge Wa Ccm Wanaoleta Nongwa Kwenye Ununuzi Wa Korosho Watakatwa Majina Yao Uchaguzi 2020.

$
0
0
Na Bakari Chijumba, Mtwara.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg.Humphrey Polepole amesema wabunge wa CCM wenye nongwa kila serikali inapotatua tatizo, ikiwemo mchakato wa kununua korosho,watakuwa na hali mbaya Uchaguzi wa 2020, huku akiwataka watafute kazi nyingine kwakuwa watakatwa majina yao.

Akizungumza mjini Mtwara, kwenye Mahafali ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo na vyuo vikukuu (UVCCM) mkoani Mtwara, June Mosi,2019, Polepole amesema  Korosho ni zao linaloleta pesa nyingi nchini lakini mabeberu wanalitumia kama fimbo ya kuwachapia Watanzania.

"Korosho ni zao linaloleta pesa nyingi,ila nalo haliko salama dhidi ya Mabeberu wanatumia kama fimbo ya kutuchapia,Rais Magufuli ameamua vizuri tumenunua, ila kuna Wabunge wanazingua 'ooh hela ya kununulia korosho imetoka wapi'..hawa upinzani 2020 wajipange tutawachapa watafute kazi nyingine" amesema Polepole na kuongeza kwamba;

"Na nyie Wabunge wa CCM acheni kuwa sehemu ya tatizo,Kama wewe ni mbunge wa CCM na unashiriki kuweka Nongwa kwenye suala hili la korosho jipange mapema...Mwaka 2020 kuna michakato kadhaa ya kukata majina ya watu na kwenye michakato yote ya ukatataji mie nimo"

Polepole amesema wapo baadhi ya wabunge wa CCM  ambao wanaongeza matatizo badala ya kutatua na kusema mtu ambaye ataonesha utovu wa nidhamu hana nafasi  kwenye chama cha mapinduzi.

"Kuna wabunge wa CCM hawana nidhamu na kuna baadhi yao tunawalia Timing tu,kama kumchinja kobe acha waendelee kuruka ruka kama Bisi..Haiwezekani kila mtu anainua kichwa kama kambare kujifanya ana ndevu,Kama haufuati utaratibu kwenye CCM hauna nafasi" amesema Polepole huku akitoa msisitizo  kwa wizara kupeleka pembejeo mapema kwa wakulima.

"Sasa hivi watu wanafanya parizi ya Korosho watu wa bodi ya mazao mchanganyiko na Wizara ya Kilimo,hakikisheni Sulphur isichelewe,Pembejeo ni muhimu sana kwa Korosho zetu..Zile korosho tulizonunua bado tunaendele kuzitafutia utaratibu" amesema Polepole.

Katika hatua nyingine Polepole amezungumzia kukosekana kwa uwepo wa safari za Ndege kutoka ATCL  na kusema amewasiliana na Mkurugenzi na zitaanza kutua hivi karibuni.

"Nimempigia simu Mkurugenzi wa Air Tanzania nimemuambia nipo Mtwara ndege haziji hapa, tickets unakatia ofisi za ATCL halafu unafaulishwa kwenda Precion Air..Nimemuambia kabla ya wiki hii Ndege zianze safari za Mtwara na amelipokea, hivi Punde zitatua" amesema Polepole huku akiwapiga dongo wapinzani akidai wanapinga kila kitu ikiwemo mchakato  wa manunuzi ya Ndege.

"Bombadier inabeba watu 84 ila bado upinzani wazee wa kupinga kila kitu wakaziita bajaji..Tukanunua nyingine wakasema injini yake mbovu ndio maana ilipoinga uwanjani ikapigwa maji na magari ya fire kuipoza,wakati ni  kawaida Ndege mpya kupokelewa kwa kumwagiwa Maji".

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili June 2

Waziri Mkuu Aushukuru Uongozi Wa Kanisa ......Ni Baada Ya Kutoa Sehemu Ya Eneo Lake Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Shule

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameushukuru uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Lindi kwa kutoa sehemu ya eneo lake na baadhi ya majengo kwa ajili ya ujenzi wa shule.

Jimbo Katoliki la Lindi limetoa eneo hilo lilipo katika Parokia ya Mnacho wilayani Ruangwa ambalo awali ilikuwa shule ya msingi ya Mnacho sasa imebadilishwa na kuwa sekondari.

Waziri Mkuu ametoa shukurani hizo leo (Jumapili, Juni 2, 2019) alipokwenda kwenye kanisa Katoliki la Theresia wa Mtoto Yesu, Parokia ya Mnacho kuwasalimia waumini.

Amesema lengo la kuibadilisha shule hiyo kuwa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia ni kuwawezesha watoto wa kike wa Wilaya hiyo kusoma katika mazingira mazuri.

Waziri Mkuu ambaye ameambatana na Mkewe Mary amesema shule hiyo ya bweni itawapunguzia vishawishi watoto wa kike, hivyo kuwawezesha kutimiza malengo yao.

Awali, uongozi wa Parokia hiyo uliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuboresha huduma za jamii zikiwemo za afya, elimu pamoja na miundombinu katika wilaya hiyo.

Naye, Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa amewaomba viongozi wa dini washikamane na wahakikishe wanatatua changamoto ya mmomonyoko wa maadili.

Amesema changamoto ya mmomonyoko wa maadiji katika jamii hususani kwa vijana ni kubwa, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha kwamba wanawarejesha kwenye maadili bora.

Kadhalika, Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia na amesema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.

Shughuli zinazoendelea katika shule hiyo ni pamoja na ujenzi wa mabweni, vyumba vya madarasa, maabara na nyumba nne za walimu ambazo tayari ujenzi wake umekamilika.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images