Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Makonda atangaza vita na Wamachinga wasio na vitambulisho Dar

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuanzia June 3 mwaka 2019 ni marufuku kwa Wamachinga wote wasio na vitambulisho kufanya biashara katika maeneo yote jijini Dar.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Mei 29, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu mwitikio wa wafanyabiashara kuchukua vitambulisho hivyo vilivyotolewa na Rais John Magufuli kwa wakuu wote wa Mikoa nchini.

Makonda amesema Jiji hilo lilipatiwa vitambulisho 175,000 lakini wapo ambao hawajachukua hadi sasa.

Amesema kuwa atafanya msako mkali kuwatafuta wamachinga wote wasio na vitambulisho hivyo

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

TANESCO Kuanza Kutoa Gawio Serikalini

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa sasa halihitaji ruzuku kutoka serikalini na kuanzia mwaka 2019/20 litaanza kutoa gawio.

Amesema Tanesco  imeanzisha utaratibu mpya wa mawasiliano baina ya wateja na Tanesco kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo kuanzisha makundi ya WhatsApp kwa kila wilaya yanayopatikana saa 24 ili  kuimarisha huduma kwa wateja, kuongeza ufanisi na mapato ya shirika hilo.

Akizungumza  jana Jumanne Mei 28, 2019 akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo alisema Tanesco kwa sasa haihitaji ruzuku ya Serikali katika shughuli zake za uendeshaji kutokana na kujiendesha lenyewe na kuokoa wastani wa Sh143 bilioni zilizokuwa zikitumika kama ruzuku kutoka serikalini kila mwaka.

“Kuimarika kwa mapato ya Tanesco kwa kiwango cha ongezeko la asilimia 1.5 mwaka 2017/18 hadi asilimia 7.6 mwaka 2018/19. Hivyo ni matarajio kuwa Tanesco itaweza kuanza kutoa gawio serikalini katika kipindi cha mwaka 2019/20,” alisema

Alisema imeunganishia umeme wateja wapya 969,431 katika kipindi cha kuanzia Julai 2015 hadi Mei 15, 2019 na kufikia wateja 2,442,648 ikilinganishwa na wateja 1,473,217 waliokuwepo kuanzia nchi ilipopata uhuru hadi Juni, 2015 sawa na ongezeko la asilimia 66 kwa miaka mitatu.

Upendo Peneza ataka REA iunde tume maalumu kusimamia miradi ya umeme

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema), ameitaka Wizara ya Nishati kuunda kitengo maalumu cha kusimamia miradi ya umeme ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano Mei 29 bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Nishati kwa mwaka 2019/20 ambapo amesema kumekuwa na changamoto katika usimamizi wa miradi ya Rea. 

Aidha, mbunge huyo amehoji kuhusiana na mradi wa umeme wa Rufiji kwamba utatumia fedha nyingi wakati fedha hizo zingetumika kwenye miradi mingine kama ya jua.  

“Tumeambiwa itatumia miaka 10 ili lile bwawa liweze kujaa, Mheshimiwa Spika tunatumia hela nyingi kujenga mradi ambao utachukua muda mrefu na hautakuwa na faida.

“Maana yake tunataka kutengeneza historia kwani huo ni uharibifu wa fedha, tusipopata faida, tuna miradi ya jua na upepo, hizo trilioni 6.5 zilizotengwa, tungepeleka kwenye hiyo miradi mingine tungekuwa tuna umeme mwingi,” amesema

Rais Magufuli ataka Jumuiya za Kimataifa kuondoa vikwazo dhidi ya Zimbabwe

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kwa hatua madhubuti za kufanya mageuzi ya kiuchumi katika nchi hiyo na ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akitoa hotuba katika Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Mnangagwa kwa heshima yake na kufanyika Ikulu Jijini Harare.

Rais Magufuli amesema katika kipindi kifupi cha tangu Rais Mnangagwa aingie madarakani hali ya uchumi imeanza kuimarika ambapo kwa sasa uchumi wa Zimbabwe unakua kwa wastani wa asilimia 3.5, mwaka ujao unatarajiwa kukua kwa wastani wa asilimia 4.2 na mwaka unaofuata kuongeza hadi wastani wa asilimi 4.4.

Kufuatia hali hiyo ameisihi Jumuiya ya Kimataifa kuondoa vikwazo mbalimbali vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe kwa kuwa vikwazo hivyo vinawaumiza wananchi wa Zimbabwe wakiwemo watoto na wanawake.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli kwa mara nyingine amewapa pole Rais na wananchi wote wa Zimbabwe kwa kupoteza watu takribani 400 waliofariki dunia katika mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Idai kilichoikumba Zimbabwe Machi 2019. Amesema Watanzania wanaungana na ndugu zao Wazimbabwe katika majonzi ya kuondokewa na jamaa zao na wanawaombea kwa Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi, Amina.

Kuhusu uhusiano wa Tanzania na Zimbabwe ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Mzee Robert Mugabe, Rais Magufuli amesema Tanzania inatambua na inathamini uhusiano huu wa kihistoria na kidugu na amebainisha kuwa jukumu lililopo sasa ni kuelekeza nguvu nyingi zaidi katika uhusiano na ushirikiano wa kiuchumi utakaoziwezesha Tanzania na Zimbabwe kuongeza biashara na uwekezaji.

Rais Magufuli amebainisha kuwa katika mazungumzo yake ya faragha na Rais Mnangagwa leo mchana wamekubaliana kusimamia ipasavyo makubaliano yaliyopo katika Kamati ya Pamoja ya Kudumu (Joint Permanent Commission – JPC) kwa manufaa ya nchi zote mbili.

“Rais Mnangagwa ujio wangu hapa Zimbabwe ni kuthibitisha kuwa urafiki wetu bado upo imara na sisi Tanzania tumejipanga kuuimarisha zaidi, tunataka tufanye biashara zaidi na nyinyi ndugu zetu wa Zimbabwe ili tukuze uchumi wa nchi zetu na kuongeza kipato cha wananchi wetu” amesisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande wake, Rais Mnangagwa amemshukuru Rais Magufuli kwa kukubali mwaliko wake, na amemthibitishia kuwa yeye na wananchi wa Zimbabwe wanatambua kuwa Watanzania ni ndugu zao waliojitolea kwa dhati katika ukombozi wao wakiongozwa na dhamira ya dhati ya Hayati Mwl. Nyerere.

Amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwa kiongozi wa kwanza katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutoa msaada wa chakula, dawa na vifaa vya kujihifadhi wakati Zimbabwe alipokumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Idai mwezi Machi 2019.

Rais Mnangagwa amesema msaada huo uliwagusa Wazimbabwe wengi na kuwakumbusha umuhimu wa kuchukua tahadhari dhidi ya majanga na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesisitiza kuwa daima Zimbabwe itabaki kuwa rafiki na ndugu wa kweli wa Tanzania na hivyo amemhakikishia Rais Magufuli kuwa nchi hiyo ipo tayari kukuza zaidi ushirikiano wa kiuchumi kwa kuongeza biashara na uwekezaji pamoja na kushirikiana katika usafiri wa anga.

Amemshukuru Rais Magufuli kwa kumpa mbinu mbalimbali za kiuongozi ikiwemo kuondoa watumishi hewa ambao wamekuwa mzigo mkubwa kwa Serikali na ameahidi kudumisha ushirikiano kati ya chama chake ZANU-PF na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

PSSSF Yatumia Bilioni 880,000 Kulipa Mafao

$
0
0
Na Frank Mvungi- MAELEZO
Wanachama elfu kumi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wamelipwa takribani Bilioni 880 ikiwa ni malimbikizo ya Pensheni kwa wastaafu  tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo mapema mwaka jana. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Meneja Kiongozi, Uhusiano  wa mfuko huo Bi. Eunice Chiume amesema kuwa dhamira ya  Mfuko huo ni kuhakikisha kuwa wanachama wake wanaendelea kulipwa mafao yao kwa wakati kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwafanya wastaafu wote kuishi maisha bora. 

“Katika kipindi cha miezi 6 Mfuko umeendelea kutoa huduma bora hali iliyowezesha wastaafu wetu zaidi124,000 kuendelea kupata huduma zetu katika ofisi zetu za mikoani pamoja na Zanzibar” alisisitiza Chiume. 

Akifafanua amesema kuwa mfuko huo una wanachama takribani 763,000 kote nchini na unaendelea kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma bora kwa wanachama wake. 

Mfuko huo umeendelea kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kusimamia uwekezaji katika sekta hiyo ikiwemo kiwanda cha viatu Karanga kilichopo Moshi  Mkoani Kilimanjaro kinachomilikiwa kwa ubia na Jeshi la  Magereza. 

Eneo jingine ni uwekezaji katika amana za Serikali, kiwanda cha Tangawizi kilichopo Same Mkoani Kilimanjaro. 

Kwa upande wa zoezi la uhakiki wa wanachama wa mfuko huo amesema kuwa zoezi hilo limefanyika kati ya Desemba 2018 hadi Machi 2019 na ni endelevu. 

Pia alitoa wito kwa wanachama wa mfuko huo ambao wamestaafu kuhakiki taarifa zao kupitia ofisi za mfuko huo zilizopo mikoani ili kuepuka usumbufu ikiwemo kusitishiwa pensheni. 

Aliongeza kuwa dhamira ya kufanya uhakiki huo ni kuwezesha mfuko kuhakikisha kuwa anayelipwa pensheni ni yule anayestahili kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo. 

Kwa upande wa watumishi wa mfuko huo wameaswa kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wa mfuko huo ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza utoaji wa huduma bora. 

Mfuko wa PSSSF ni matokeo ya kuunganishwa kwa mifuko ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi hasa kuchochea ukuaji wa sekta ya hifadhi ya Jamii hapa nchini.

Serikali Yatoa Ufafanuzi Bei Za Taulo Za Kike

$
0
0
Na. Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imesema kuwa nguvu ya soko pamoja na gharama nyingine zimechangia kutoshuka kwa bei ya taulo za kike licha ya Serikali kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika taulo hizo.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Sophia Mwakagenda, alietaka kujua sababu za taulo hizo kupungua bei wakati Serikali iliondoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye taulo hizo katika Bajeti ya Mwaka 2017/2018.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, pamoja na Serikali  kuchukua hatua ya kuondoa kodi za taulo hizo, imebainika kuwa hakuna mabadiliko ya bei katika soko jambo linalodhihirisha kuwa bei inaamuliwa na nguvu ya soko pamoja na gharama nyingine za uzalishaji na uendeshaji.

"Hatua ya kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye taulo za kike (pads) ililenga kupunguza sehemu ya gharama za uzalishaji wa bidhaa na kwamba athari chanya ilitotegemewa ilikuwa ni kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo lakini hadi sasa hakuna mabadiliko ya bei katika soko" alisema Dkt. Kijaji

Alisema kuwa hali hiyo inatokana na sababu mbalimbali ikiwemo gharama za malighafi, mishahara, uwekezaji, mifumo ya uzalishaji, teknolojia, ushindani katika soko, umeme, maji safi na maji taka, usambazaji na ubora wa bidhaa.

"Hivyo basi, kutoshuka kwa kwa bei ya taulo za kike kunabainisha kuwa kodi inachangua sehemu ndogo sana katika kupanga bei ya bidhaa, kama ambavyo Serikali imekuwa ikisisitiza na kutoa ufafanuzi mbele ya Bunge lako Tukufu”, alifafanua Dkt. Kijaji.

Alisema Serikali ina mpango wa kutoa taulo za kike bure  ili kuondoa changamoto ya bei ya taulo hizo inayolalamikiwa kutoshuka na kuwataka wabunge kutolichukulia suala hilo la upatikanaji wa bidhaa hizo kisiasa kwani hata baadhi ya nchi zilizoondoa kodi kama hizo ikiwemo Botswana na Kenya, zoezi hili halikusaidia kushusha bei za taulo hizo.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, kwa sasa mfumo wa uchumi ni wa soko huria na bei ya bidhaa huamuliwa na nguvu ya soko, yaani ugavi na mahitaji ya soko, hivyo fursa iliyopo ni kuhamasisha uwekezaji mkubwa kwa kutumia teknolojia yenye gharama nafuu katika kutengeneza taulo hizo, jambo linalotakiwa kwenda sambamba na  kuchochea ushindani wa bei katika soko na sio Serikali kuondoa kodi na kupanga bei ya bidhaa.

Serikali ilichukua hatua ya kuondoa kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye taulo za Kike ikiwa na lengo la kupunguza sehemu ya gharama za uzalishaji wa bidhaa na hivyo kushuka kwa bei, lengo ambalo halijafikiwa.

Serikali Yaanza Utekelezaji Wa Mkakati Wa Mpango Miji Ambapo Maeneo Yaliyoiva Kuwa Miji Yafikia 455 Hapa Nchini.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imeanza utelekelezaji   wa mkakati wa kupanga miji yote nchini  ambapo maeneo yaliyofikia kuwa miji hadi sasa ni Zaidi ya 455. 

Hayo yamesemwa leo Mei 29,2019 na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi wakati akijibu swali la Mbunge wa Kasulu mjini Daniel Nicodemus Nsanzugwako  aliyehoji kwanini serikali isije na mkakati endelevu  wa kupanga miji  yote iliyotangazwa kwenye gazeti la serikali. 

Katika majibu yake,Waziri Lukuvi amesema serikali imeanza utekelezaji wa mkakati wa kupanga miji yote  ambayo imetangazwa  kwenye gazeti la Serikali  kwa kuandaa mipango kabambe ya majiji,manispaa,na miji. 

Aidha,Serikali imeainisha maeneo yote ambayo yameiva kuendelezwa kimji  kwa ajili ya kuyatangaza kwenye gazeti la serikali  kuwa maeneo mipango ambayo ni Zaidi ya maeneo 455 nchini.

Hata hivyo,Waziri Lukuvi amesema kwa mujibu wa kifungu Na.7[1] na 5 cha Sheria ya Mipango miji  Na.8 ya mwaka 2007,jukumu la kupanga na kupima miji ni la mamlaka za upangaji ambazo ni Halmashauri za majiji,manispaa,miji ,na mamlaka za miji midogo. 

Waziri Lukuvi amebainisha,Serikali imeendelea kuzisaidia halmashauri  kupanga na kupima miji  yao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo  ambapo mwaka 2018/2019 serikali kupitia Wizara  imetoa Jumla ya Shilingi Bilioni 6.4 kwa halmashauri 29 nchini  kwa ajili ya upangaji,upimaji na umilikishaji wa  ardhi .

Pia imewezesha uandaaji wa mipango kabambe ya miji 18  kupitia program ya kuzijengea uwezo  mamlaka za miji [Urban Government Strengthening Program-ULGSP] Chini ya Ofisi ya Rais –TAMISEMI.

Mradi Wa Maboresho Ya Usimaizi Wa Fedha Za Umma Washika Kasi

$
0
0
Na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James amewashukuru Wadau wa Maendeleo kwa kuisaidia Serikali kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha za umma iliyosaidia kuongeza tija katika ukuaji wa uchumi wa nchi na utoaji huduma bora kwa wananchi

Bw. James ametoa shukrani hizo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha mwisho kwa mwaka wa fedha 2018/2019 cha Wadau wa Maendeleo na Serikali kilichojadili maendeleo ya utekelezaji wa Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma  Awamu ya Tano (PFMRP-V) ambao utekelezaji wake umeingia mwaka wa pili na unaotarajiwa kukamilika mwaka wa fedha 2021/2022

Programu ya Maboresho na Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano, utagharimu shilingi bilioni 152.3 katika kipindi cha miaka mitano kuanzia Julai mwaka 2017 hadi Juni, 2022, ambapo unatarajia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kudhibiti mianya yote ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali.

Alisema kuwa katika kipindi cha miaka miwili cha utekelezaji wake, umeonesha mafanikio makubwa ikiwemo usimikaji wa mifumo zaidi ya 7 ya kieletroniki ya kukusanya na kudhibiti mapato ya Serikali.

" Mifumo hii ukiwemo mfumo wa GePG umesaidia sana kuongeza ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali pamoja na kodi, imeongeza udhibiti wa matumizi, misamaha ya kodi na kusaidia upelekaji wa rasilimali fedha kwenye miradi ya kipaumbele ya kitaifa na hatimaye kusaidia usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo" alisema Bw. James

"Wizara ya Fedha na Mipango imejipanga kuendeleza kazi nzuri za programu ili kuendelea kuunga mkono agenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli; katika kusimika mifumo na maboresho ya uhakika katika kusimamia fedha za umma. Hatua hii itachochea maendeleo ya kiuchumi yanayowagusa watanzania wote"

Kwa upande wake, Mwenyekiti mwenza wa kundi la Washirika wa Maendeleo wanaofadhii Program ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma  Awamu ya Tano (PFMRP-V), Bi. Trine Lunde, alielezea kuridhishwa kwao na namna Tanzania inavyotekeleza na kusimamia programu hiyo ambayo amesema imeleta tija katika usimamizi wa fedha za umma nchini.

BAKWATA yatangaza tarehe ya sikukuu ya Idd

$
0
0
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetoa taarifa kuwa sikukuu ya Eid El-Fitr itakuwa siku ya Jumatano Juni 5 au Alhamisi 06 Juni 2019,kutegemeana na kuandama kwa mwezi.

Sherehe za Eid El-Fitr kitaifa zitafanyika Tanga ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Majaliwa .

Waziri Mkuu Majaliwa Aitisha Mkutano Wa Dharura Wa Baadhi Ya Wadau Wa Zao La Pamba

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ana imani kuwa ununuzi wa zao la pamba utaanza mara moja kwa bei ya sh. 1,200 kwa kilo moja katika mikoa yote inayozalisha zao hilo.

Amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya bei kwa takriban ya wiki nne tangu bei elekezi ilipotangazwa Aprili 30, 2019 mkoani Shinyanga kwamba bei hiyo ianze kutumika kuanzia Mei 2, 2019.

Alikuwa akizungumza na wadau wa sekta ndogo ya pamba kwenye kikao kilichofanyika leo (Jumatano, Mei 29, 2019) kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu, jijini Mwanza. Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Mawaziri wa Kilimo na Viwanda, Makatibu Wakuu wa Kilimo na Ofisi ya Rais – TAMISEMI na  Wakuu wa Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita.

Wengine ni wawakilishi wa Wabunge wa mikoa hiyo, Makatibu Tawala wa mikoa, Wakuu wa Wilaya zote za mikoa hiyo, na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya hizo. Pia kilihudhuriwa na wanunuzi wa pamba, wakulima na maafisa wa benki kadhaa.

Waziri Mkuu aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba Serikali bado inaendelea kutafuta njia nzuri ya kuwakutanisha wadau wa mazao ya kibiashara ili yaweze kuwa na tija kwa wakulima. Alisema kazi hiyo inafanywa wa Wizara ya Kilimo. Mazao hayo ni pamba, chai, kahawa, korosho, tumbaku na chikichi.

Pia alisema Bodi ya Pamba iachiwe jukumu la kutoa leseni za ununuzi wa zao hilo na kwamba Wakurugenzi wa Halmashauri waliokuwa wakifanya kazi hiyo waache mara moja. “Kuna baadhi ya Wakurugenzi wanatoa leseni za ununuzi, lakini wenye Mamlaka ni Bodi ya Pamba. Mnunuzi nenda Bodi ukapate leseni yako,” alisema Waziri Mkuu.

Alitumia fursa hiyo kuwakemea baadhi ya wakurugenzi ambao wamekuwa wakizuia wanunuzi wapya kwenye maeneo na kuendelea kuwakumbatia wanaowataka wao. 


“Wakurugenzi baadhi yenu mnazuia wanunuzi wapya, mnamtaka fulani tu. Kwa kufanya hivyo, unapungua kiwango cha kilo ambacho wakulima wako wangeuza,” alionya.

‘Wanunuzi nendeni mkajitambulishe kwa Wakuu wa Wilaya au Wakurugenzi ili watambue kwamba mpo kwenye maeneo yao lakini kila mnunuzi anayo haki ya kwenda kununua pamba mahali popote hapa nchini.”

Kuhusu ubora wa pamba, Waziri Mkuu alitaka wananchi waelimishwe ili waache kuweka maji au mchanga kwenye pamba kwa minajili ya kuongeza uzito kwani kwa kufanya hivyo wanachafua jina la Tanzania pindi inapopelekwa kuuzwa nje ya nchi.

Pia alitaka vyama vikuu vya ushirika vijiridhishe kuhusu ubora wa maghala ya kuhifadhia pamba kwenye vyama vya msingi (AMCOS) kwani kwa kufanya hivyo, itawasaidia wakulima wauze mapema pamba yao mara baada ya kuivuna.

Kuhusu mizani, Waziri Mkuu aliiagiza wakala wa vipimo nchini (WMA) waende wakakague mizani ya kwenye AMCOS na kwenye vinu vya kuchambulia pamba (ginneries) kwa sbabu ya tofauti kubwa ya uzito inayojitokeza na kuwalazimisha wakulima kulipia upotevu wa kilo hizo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe atume wakaguzi kwenye Bodi ya Pamba ili wabainishe matumizi ya sh.100 kwa kila kilo ambazo zimekuwa zikilipwa kwenye bodi hiyo.

“Katibu Mkuu Kilimo lete wakaguzi ndani ya bodi ya pamba, waangalie kwa kipindi cha miaka mitatu toka tulipoanza kukusanya sh. 100 kwa kilo, zimekusanywa shilingi ngapi, na zimetumika kulipia nini.

“Na Mrajisi wa Ushirika nchini ufanye ukaguzi kwenye vyama vikuu vya Ushirika na AMCOS. Uangalie ziko ngapi na zinafanya nini. Kuna AMCOS zina hela, je fedha hiyo imetumika kufanya nini ili kuendeleza zao la pamba. Je zimenunua matrekta au zimelipia posho za vikao,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wanunuzi Binafsi wa Pamba (TCA), Bw. Christopher Gachuma ameshukuru Waziri Mkuu kwa maelekezo aliyoyatoa kuhusu utoaji wa leseni kwani yalikuwa ni kikwazo kikubwa kwa baadhi ya wanunuzi wa zao hilo.

“Suala la utoaji leseni linapaswa lianze mapema lakini kuna wengine hadi sasa bado hawajapata leseni zao.” Aliwataka wanunuzi wa pamba waanze kununua pamba ili msimu wa mauzo uanze kwa kasi.
 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya May 30

Serikali Kuendelea Kutatua Changamoto Za Wawekezaji Nchini.

$
0
0
Serikali imedhamiria kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili wawekezaji nchini ili kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki yatakayowavutia kuwekeza nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki wakati akifungua mkutano wa wawekezaji wa Uingereza waliopo nchini walipokutana kujadili masuala ya Uwekezaji uliofanyika Mei 29, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Coral Beach Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde, Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke pamoja na Mwenyekiti wa Makampuni ya Biashara ya Uingereza Bw.Kalpesh Mehta, viongozi wa makampuni ya uwekezaji nchini, pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi za Sekta ya Umma na Binafsi.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Waziri Kairuki alieleza lengo la kukutana na wawekezaji kutoka Uingereza ni pamoja na kujadili masuala yote yanayowahusu wawekezaji kwa kuzingatia changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kuzitatua ili kuendelea kufikia lengo la kuwa na mazingira bora ya biashara na uwekezaji nchini.

“Tumezingati umuhimu wa wawekezaji nchini, hivyo tumekutana hii leo ili kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili ili kuona namna bora ya kuboresha mazingira na kutambua fursa zilizopo nchini ili kuendelea kuwekeza nchini”, alisema Waziri Kairuki.

Waziri aliongezea kwamba, kwa kuzingatia kuwa mnamo mwezi Machi mwaka 2019 Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli aliutangaza mwaka huu kuwa ni mwaka wa uwekezaji alipokutana na waheshimiwa mabalozi wa nchi za nje ambao wapo nchini ikiwa ni kiashiria cha kufungua mwaka mpya.

Aliongezea kuwa, kwa kuzingatia mchango wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi ikiwemo ongezeko la ajira hivyo tunapaswa kuzingatia na kuboresha mazingira yatakayochochea kuendelea kuchangia katika uzalishaji wa ajira nyingi nchini.

“Sekta binafsi ndiyo kiini cha ukuaji wa uchumi kwa upande wa kuongeza ajira hivyo tunatambua mchango huo ambapo hadi sasa wawekezaji wa uingereza wamechangia katika ukuaji wa ajira kwa kuzalisha ajira laki tatu,”alisisitiza Waziri Kairuki.

Kwa upande wake Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuona umuhimu wa kukutana pamoja kujadili masuala ya uwekezaji na kuendelea kujadili namna ya kuwezesha wawekezaji kutoka uingereza kuendelea kuwa wadau muhimu nchini na kuhakikisha nchi zote mbili zinanufaika.

“Ni kweli tumeenedelea kuwekeza Tanzania kwa kuzingatia mazingira yaliyopo hivyo ni vyema kukawa na maboresho zaidi katika mazingira hayo kwa kuendelea kutatua changamoto zilizopo kwa sasa ili tuendelea kushirikiana pamoja,” alieleza Balozi.Cooke

Aliongezea kuwa nchi ya Uingereza imelenga kuwa kinara cha uwekezaji katika nchi za Afrika hiyo ni wakati sahihi wa kuendelea kutumia fursa zilizopo barani humo ili kufikia malengo.

“Ifikapo mwaka 2022 Nchi yetu imeweka malengo ya kuwa wawekezaji bora barani Afrika hivyo tunaendelea kushirikianana nchi za Afrika ili kuwa na nia moja na kuwa na mahusiano yenye tija hasa katika masuala ya uwekezaji”,alisema Balozi Cooke.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde alieleza kuwa, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara ili kuchangia ongezeko la ajira kwa vijana wa Kitanzania ili kujikwamua kiuchumi.

Aidha alifafanua kuwa, ili kuendelea kukuza ujuzi kwa vijana na kuondokana na changamoto za ukosefu wa ajira Serikali itaendelea kulinda ajira za watanzania na kuboresha mazingira ya sekta binafsi ambao ni wadau muhimu katika kuzalisha ajira nchini.

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni, akata rufaa kupinga hukumu ya kunyongwa

$
0
0
Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Mrakibu wa Polisi (SP), Christopher Bageni, aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kuwaua wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro, amepinga adhabu hiyo katika Mahakama Rufaa jijini Dar es Salaam.

SP Bageni amewasilisha maombi ya mapitio Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambayo yamepangwa kusikikizwa Juni 16, mwaka huu mbele ya jopo la majaji watatu, Stellah Mugasha, Ferdinand Wambali na Rehema Kerefu.

Katika maombi yake ya mapitio, Bageni amewasilisha sababu mbalimbali za kupinga adhabu hiyo ikiwamo kwamba jopo la majaji lilifanya makosa ya dhahiri katika muonekano na hivyo kusababisha haki kutozingatiwa katika kutoa hukumu hiyo.

Septemba 16, 2016 mapema saa 3:45 asabuhi, msajili wa mahakama hiyo (kwa sasa Jaji wa Mahakama Kuu) John Kahyoza alisoma hukumu hiyo baada ya kusikilizwa kwa rufani iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

DPP alipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe na maofisa wenzake watatu akiwamo Bageni mwaka 2009.

Akisoma hukumu hiyo, Kahyoza aliwataja walalamikiwa kuwa ni ACP Zombe, SP Bageni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Alisema Mahakama ya Rufani ilipitia ushahidi uliotolewa Mahakama Kuu na kuona kwamba ilishindwa kuwatia hatiani washtakiwa wa mauaji na kwa kosa la kusaidia mauaji kufanyika.

"Kosa la kuua na kosa la kusaidia kuua ni makosa mawili tofauti, si sahihi kwa mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji kutiwa hatiani kwa kosa lingine ambalo tangu mwanzo mshtakiwa alitakiwa kulijua ili kujitetea," alisema na kuongeza kuwa:

"Washtakiwa wote katika utetezi wao walipinga kuhusika katika mauaji hayo, lakini mlalamikiwa wanne, Rajabu alisema ukweli katika ushahidi wake kwa kueleza tukio la mauaji lilivyofanyika katika Msitu wa Pande, lakini ushahidi wake ulitakiwa kupokewa kwa makini na unatakiwa kuwapo na ushahidi mwingine wa kuunga mkono."

Akifafanua zaidi, Kahozya alisema: “Mlalamikiwa wa kwanza, Zombe, mahakama haikuona kama kuna ushahidi wa kumtia hatiani kwa mauaji wala kwa kusaidia kuua japo kuna jambo kichwani mwake analolifahamu kuhusu mauaji hayo. Ushahidi mwingine unaonyesha wajibu rufani watatu walishuhudia mauaji, lakini hawakuua."

Jopo, kwa mujibu wa Kahozya,  lilisema wamekubaliana kwamba watu wanne waliuawa kwa bunduki na mauaji yalikuwa ya kinyama katika Msitu wa Pande.

Mahakama hiyo ilijiuliza maswali kwamba je, wajibu rufani walikuwapo Pande? Jibu ni kwamba walalamikiwa wa pili, wa tatu na wa nne walikuwapo katika msitu huo na kwamba mlalamikiwa wa nne alisema ukweli mahakamani kuhusiana na tukio hilo.

Ilidaiwa kwamba mauaji hayo yalifanywa na askari Polisi Sadi, lakini mshtakiwa huyo hajawahi kushtakiwa. Mahakama inajiuliza waliouawa walipelekwa Pande kwa amri ya nani.

Kwa mujibu wa ushahidi, mahakama inajiuliza nini nia ya kuwapeleka watu hao Pande sehemu ambayo haina hata nyumba, mlalamikiwa wa pili, Bageni ndiye alitoa amri ya kuua, ushahidi unaonyesha washtakiwa waliwapeleka wakiwa hai Pande na waliwarejesha wakiwa marehemu.

"Marehemu walipelekwa huko ili tukio la mauaji lifanyike bila kipingamizi kwa kibali cha Bageni, ushahidi wa mlalamikiwa wa nne uliungwa mkono na tabia ya Bageni kwamba alikuwa akificha ukweli kuhusu mauaji hayo," alisema.

Hata hivyo, ushahidi wa maofisa watatu wa Jeshi la Polisi, wote walidanganya kwamba mauaji yalitokea Sinza katika majibizano kati ya Polisi na marehemu wakati wengine wa Sinza walisema hawakusikia tukio la aina hiyo kutokea.

"Mahakama hii imeona walalamikiwa wa kwanza, wa tatu na wa nne, rufani dhidi yao inatupwa hakuna ushahidi wa kuwatia hatiani, mjibu rufani wa pili mahakama inatengua kuachiwa kwake kutiwa hatiani na Mahakama Kuu, inamuhukumu kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya watu wanne," alisema Msajili Kahyoza na kusababisha mahakama hiyo kulipuka kwa vilio.

Katika kesi ya msingi, Wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro waliouawa ni Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi, mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Juma Ndugu.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika Msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.

Jumla Ya Miradi 88 Ya Maji Nchini Imejengwa Chini Ya Kiwango

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Jumla ya Miradi 88 ya Maji hapa nchini imejengwa chini ya     Kiwango kwa  kipindi cha mwaka 2010 na 2015 hali iliyosababisha pawe na kero  kubwa ya uhaba wa maji hususan Maeneo ya vijijini hadi sasa.
 
Hayo yamesemwa  Mei 29,2019  bungeni  jijini Dodoma na Waziri wa Maji Prof.Makame Mbarawa  wakati akijibu swali  mbunge Wa Moshi Vijijini  Anthony Komu aliyehoji  serikali inafanya mpango gani wa  kubainisha  waliohusika na mapungufu  yaliyobainika   na kuwachukulia hatua.
 
Katika majibu yake Prof.Mbarawa amesema  kuna miradi 88  ya Maji Tanzania imejengwa chini ya kiwango  kwa mwaka 2010  hadi 2015 na nia ya serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha watanzania wanapata Maji ya Uhakika na kama mradi umejengwa chini ya Kiwango serikali bado inafanya uchunguzi na ikishakamilisha hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya waliohusika.
 
Katika hatua nyingine Prof.Mbarawa amesema serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Moshi  kwa kushirikiana na mkandarasi wa barabara  wameweza kukarabati  na kumaliza tatizo la uvujaji maji barabarani kwa gharama ya Tsh. Mil.1 laki 4 na 37 elfu[1,437,000/=]

Bilioni 107.1 Zimetengwa Katika Utekelezaji Wa Ujenzi Wa Maabara Za Masomo Ya Sayansi Nchini.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika mwaka wa fedha 2019/2020 ,serikali imetenga  Jumla ya Tsh.Bilioni 107.1  katika  kutekeleza  mpango wa ujenzi wa maabara  za masomo ya sayansi kwa shule za sekondari   hapa nchini.
 
Hayo yamesemwa Mei 29,Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Mwita Waitara wakati akijibu swali la mbunge wa Mwanga Prof.Jumanne Maghembe  aliyehoji lini serikali itatenga fedha kwa ajili ya kukamilisha  maabara za sayansi  katika shule zote za kata hapa nchini.
 
Akijibu Swali hilo,Mhe.Waitara amesema serikali inatekeleza  mpango wa ujenzi  wa maabara za Masomo ya sayansi  katika shule za sekondari  kwa kushirikiana na wananchi na wadau  wa maendeleo wa ndani na nje  ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ,serikali  imetenga Tsh. Bil.107.1   katika utekelezaji huo.

Kati ya Kiasi hicho,Tsh. Bilioni 58.2  kupitia mpango wa lipa  kulingana na matokeo [EP4R] na Tsh.Bilioni 48.9  kupitia mpango wa kuboresha  shule za sekondari [SEQUIP] ambapo sehemu ya Fedha hizo  zitatumika kukamilisha  ujenzi wa Maabara  za masomo ya sayansi  kwa shule za sekondari za kata nchini.
 
Hata hivyo,Naibu waziri Waitaraamesema serikali imejipanga namna ya kufanya vizuri katika Masomo ya Sayansi ambapo imeshatoa maelekezo namna ya ufundishaji kwa shule zenye changamoto ya vifaa vya maabara ili ufaulu kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Maagizo Mazito ya Waziri Lukuvi kwa Bodi ya Wakurugenzi NHC

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameipa maagizo mazito Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo ameipa miezi mitatu ya kufanyia maamuzi maagizo yake.

Waziri Lukuvi ametoa maagizo hayo katika Makao Makuu ya Wizara ya Ardhi jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambao wameteuliwa hivi karibuni .

Ameipa bodi hiyo mpya miezi mitatu ya kujifunza yale watakayoyasimamia kwani wengi wao wanatoka katika idara nyingine zisizo za NHC hivyo wapo huru kuchunguza idara yoyote na kama kuna mkurugenzi haoneshi ushirikiano wamlipoti na yeye atamchukulia hatua.

Mei 27 mwaka huu Uteuzi huu umefanyika baada ya kuvunjwa kwa Bodi hiyo Mwaka 2017 ambapo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuri alimteuwa Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Sophia Kongela kufuatiwa na baadae Mhe. Lukuvi kumteua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Maulid Banyani kukaimu nafasi hizo.

Wajumbe hao wapya ni pamoja na Bi. Sauda Msemo Kamishna Msaidizi Sera na Madeni Wizara ya Fedha na Mipango, Abdalla Mwinyimvua Mhasibu, Martin Madekwe Mstaafu kutoka Shirika la Nyumba la Taifa na Mr. Charles Singili Mkurugenzi Mtendaji Benki ya (TIB).

Wengine ni Immaculata Senje Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi, Ndg Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mhandisi Mwita Rubirya ambapo kwa pamoja watashirikiana na Mwenyekiti wa bodi Dkt. Sophia Kongela pamoja na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba Dkt. Maulid Banyani.

Serikali Yawataka Wananchi Waoishi Karibu Na Migodi Mikubwa Ya Dhahabu Kuacha Utegemezi.

$
0
0
Serikali  wilayani Kahama mkoani Shinyanga  imewataka wananchi wanaoishi karibu na Migodi mikubwa ya Madini ya (Buzwagi na Bulyankulu ) kufanya kazi zingine mbadala za kuwaingizia vipato badala ya kutegemea ajira katika  migodi hiyo ili kuondokana na migogoro isiyokuwa na tija baina yao na wawekezaji.

Kauli hiyo imetolewa na jana na Mkuu wa wilaya ya Kahama ANAMRINGI MACHA katika Hafla maalum ya kumtambulisha Mzabuni aliyeshinda Dhabuni ya kuzoa Taka ngumu hususani  vyuma chakavu katika mgodi wa Bulyankulu, AZAN LOGISTIC CO.LTD ya Kahama.

Amesema kuwa baada ya kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji wa madini katika migodi hiyo baadhi ya wananchi wanao ishi karibu Migodi hiyo wamekuwa tegemezi kwa kutojihusisha na kazi zingine  za uzalishaji mali na kuwataka wafanye kazi za ujasiriamali.

Katika Hatua nyingine MACHA ameitaka Kampuni ya AZAN LOGISTIC  kutoa ajira kwa Wazawa pindi atakapoa anza kutoa huduma hiyo katika mgodi huo ili kuwapa hamasa wananchi kupenda kufanya kazi na  wawekezaji wazawa.

 Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo,  AZAN SAID SALUM ameahidi  kutoa ushirikiano kwa wananchi wa Mji mdogo wa  Kakola ambapo Mgodi huo upo  na kuahidi kuwa kampuni yake itaajiri walimu wawili wa sayansi katika shule mbili za sekondari katika Halmashauri ya Mslala.

Mbali na hilo  Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri ya Msalala, SAIMON BEREGE  ametolea ufafanuzi suala la upimaji wa viwanja kwa kusema kuwa tayari Kampuni za upimaji zinaendelea na upimaji  ili kuhakikisha wananchi wanarasimishiwa makazi yao ambapo kwa awali viwanja elfu 10 vitapimwa.

Kampuni ya AZAN LOGISTICS imeshida  dhabuni hiyo ambapo kwa sasa itatoa huduma ya kuzoa vyuma chakavu katika mgodi wa Bulyankulu kwa Muda wa Mwaka mmoja na miezi 10.

Video Mpya: Rich Mavoko - Usizuge

$
0
0
Video Mpya: Rich Mavoko - Usizuge

ATCL yamvuruga Nape, ahoji kucheleweshwa kwa ndege

$
0
0
ATCL yamvuruga Nape, ahoji kucheleweshwa kwa ndege
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images