Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli arejea nchini akitokea Zimbabwe

$
0
0
Rais John Magufuli amerejea nchini kutoka Zimbabwe ambapo amepokelewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen.  Venance Mabeyo.

Rais  Magufuli kwa takribani wiki moja sasa amekuwa ziarani katika nchi kadhaa za Afrika, ziara hizi za wanachama wa SADC zilikuwa muhimu kwa sababu ya uhusiano wa kipekee na kihistoria wa Tanzania na nchi hizo 

Serikali yakanusha kuwalazimisha wafanyakazi wake kuwa na laini ya TTCL

$
0
0
Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema hakuna agizo la Serikali linalolazimisha mfanyakazi wa Serikali kuwa na laini ya TTCL isipokuwa viongozi wanaowekewa vocha za Serikali kwamba ni muhimu kuwa na laini hizo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo amesema taarifa inayosambaa kwenye mitandao kuhusu hilo ni ya upotoshaji na kuwataka wananchi kuipuuza.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Msemaji wa Serikali: Maono Na Mtazamo Wa Rais Magufuli Yazidi Kupaisha Makusanyo Ya Mapato Ya Madini

$
0
0
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
SERIKALI imesema maono na mtazamo yakinifu wa Rais Dkt. John Magufuli katika usimamizi na ufuatiliaji wa sekta ya madini, umewezesha ongezeko maradufu la makusanyo ya mapato ya sekta hiyo kutoka Tsh Bilioni 210 mwaka 2015/16 hadi kufikia Tsh Bilioni 302 kwa mwaka 2018/19 na kuifanya Tanzania kuzidi kujijenga Kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari leo Alhamisi (Mei 30, 2019) Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, alisema Serikali ya Awamu ya Tano inafanya kazi kisayansi na itahakikisha rasilimali za nchi zinaendelea kulindwa ili ziweze kuleta manufaa kwa Watanzania wote.

Dkt. Abbasi alisema mara baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani Novemba 2015, ilifanya mageuzi mbalmbali katika usimamizi na ufuatiliaji wa rasilimali za madini, kwani huko nyuma Serikali ilikuwa ikipoteza kiasi kikubwa cha fedha na kuamua kuchukua hatua stahiki ikiwemo kufanya mabadiliko katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010.

“Tulipofanya marekebisho katika sheria yetu ya madini mwaka 2017, matokeo tumeanza kuyaona kwani tumedhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato yetu na kuanza kusimamia kwa umakini mkubwa utoroshaji mkubwa wa madini ambapo ilisababisha Serikali kupoteza kiasi kikubwa cha mapato” alisema Dkt. Abbasi.

Akitolea mfano Dkt. Abbasi alisema kufuatia agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kuanzishwa kwa masoko ya madini ambayo ni utekelezaji wa sheria ya madini ya mwaka 2017, hadi sasa kuna jumla ya masoko 24 ambayo yamekuwa yakithibiti ubora, thamani na takwimu za madini nchini, ambapo soko la kwanza lilianzishwa Mkoani Geita, mwezi Machi mwaka huu.

Aidha Dkt. Abbasi alisema Takwimu za jumla za uzalishaji wa dhahabu katika kipindi cha miezi miwili , mkoani Geita kuanzia mwezi Machi hadi Mei, mwaka huu zinaonyesha kuwa uzalishaji umeongezeka kwa kiasi kikubwa na kufikia kilo 312.65 za dhahabu ukilinganisha na uzalishaji wa dhahabu  kilo 259.12 zilizokuwa zikizalishwa kabla ya masoko hayo.

“Mwezi April, pekee uliweka rekodi ya Geita kwa kuzalisha kilo 200 ambazo hazijapata kufikiwa mkoani humo kwa wachimbaji wadogo na wa kati na kwa Takwimu za Mei mwezi mwaka huu zinazidi kuthibitisha kuwa Watanzania wanapaswa kuendelea kumuombea na kumuunga mkono Rais Magufuli” alisema Dkt Abbasi.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema eneo lingine la mageuzi yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika sekta ya madini ni pamoja na maamuzi iliyochukua ya kujenga ukuta kuzunguka eneo la wachimbaji wa Madini ya Tanzanite Mkoani Manyara ambao Serikali iliweka mifumo ya masoko na ukaguzi, na hivyo kuchangia ongezeko la mapato ya wachimbaji wadogo na Serikali kwa ujumla.

Akifafanua zaidi Dkt. Abbasi alisema uzalishaji wa madini ya Tanzanite kutoka kwa wachimbaji wadogo ulioripotiwa kwa mwaka 2016 ulikuwa kilo 164.6 na kilo 147 kwa mwaka 2017, ambapo Serikali iliweka kukusanya kiasi cha Tsh Milioni 71 (2016) na Tsh Milioni 166 (2017), lakini uzalishaji huo uliongezeka maradufu mara baada ya Serikali kujenga ukuta huo.

“Uzalishaji uliongeza sana mara baada ya ujenzi wa ukuta kwani Kilo 781.2 zilizalishwa mwaka 2018 na kuiingizia Serikali mapato ya Tsh Bilioni 1.43 na uzalishaji kwa mwaka 2019 katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Mei ulikuwa kilo 1086.05 zenye thamani ya Tsh Bilioni 1.422” alisema Dkt. Abbasi.

Aliongeza kuwa mabadiliko hayo yameanza kuleta faida kwa nchi ambapo kwa sasa nchi nyingi za Afrika zimeanza kuiga mageuzi yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ikiwemo kupitia upya mikataba na wawekezaji na pia watafiti mbalimbali wanairejea Tanzania inayogeuza “laana” ya madini kuwa “Baraka” ya Madini.

Naibu Waziri Nditiye Awataka Watanzania Kusoma Kwanza Maelekezo Ya Tiketi Kabla Ya Kukata Tiketi Ili Kuondoa Migogoro.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye amewataka watanzania  Kuwa na desturi ya kusoma kwanza maelekezo yaliyopo kwenye tiketi  ya kusafiria  pindi wanapotaka kusafiri ili kuondoa migongano na migogoro baina yao na Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri. 

Mhe.Nditiye ameyasema hayo Mei 30,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa ShauriMoyo  Mhe.Mattar Ali Salum  aliyehoji juu ya  baadhi ya kampuni za usafiri hususan Usafiri wa Majini kwa njia ya Boti  kuuza tiketi kwa abiria  kwa ajili ya Safari  lakini abiria anapochelewa safari tiketi hiyo  huwa haitumiki  na hivyo kusababisha hasara na usumbufu kwa abiria . 

Katika Majibu yake Mhe.Nditiye amesema tiketi ni moja ya mkataba kati ya abiria na mmiliki wa chombo cha usafiri hivyo abiria  anatakiwa kusoma kwanza maelekezo yaliyo kwenye tiketi na kama hatoridhika na maelekezo hayo ana ruksa ya kusitisha kukata tiketi ili kuondoa usumbufu.

Hata hivyo,Mhe.Nditiye amesema ufuatiliaji wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano  kupitia TASAC Umebaini kuhusu changamoto hizo na serikali inalifanyia uchunguzi.

Mageuzi ya Kisayansi Yazaa Matunda Sekta ya Madini, Mapato

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Hatua za serikali kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali za nchi yao na kuongeza mapato zimeanza kuzaa matunda licha ya kupingwa vikali hapo awali.  

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar-es-Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, amesema hatua zilizochukuliwa kwenye sekta ya madini  na kuboresha mifumo ya kukusanya mapato ya serikali imechangia kuongeza mapato maradufu. 

    Akieleza hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano, Dkt. Abbasi amesema ni pamoja na ujenzi wa ukuta kwenye eneo la migodi ya madini ya Tanzanite Mirerani, kuanzishwa kwa masoko ya madini kwenye mikoa na wilaya nchi nzima na kuundwa kwa mifumo ya kisasa ya kijiditali ya kurekodi mapato ambayo licha ya kuongeza mapato, lakini pia imeongeza ufanisi. 

    Dkt. Abbasi amesema kuwa hadi kufikia mwezi Mei 2019 sekta ya madini kwa kipindi cha miezi kumi na moja ya mwaka wa fedha 2018/19 mapato yamefikia Shilingi bilioni 302.63 kiasi ambacho ni zaidi ya mapato yote kiasi cha Shilingi bilioni 301.6 yaliyopatikana kwenye mwaka wa fedha 2017/18. 

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Dkt. Abbasi mapato kwenye sekta ya madini katika kipindi cha miaka minne yamekuwa yakiongezeka mfululizo, akitolea mfano amesema mwaka 2016/17 makusanyo ya maduhuli yalikuwa bilioni 214.5 wakati mwaka 2015/16 maduhuli yalikuwa Shilingi Bilioni 210 na mapatao ya mwaka 2017/18 yalikuwa Shilingi bilioni 301.6 

    Aidha, aliongeza kuwa mapato yanayotokana na mauzo ya madini ya Tanzanite tangu ujenzi wa ukuta wa Mirerani ujengwe kuzunguka migodi ya madini hayo mapato yameongezeka maradufu kutoka kiasi cha shilingi milioni 71.8 mwaka 2015 hadi kufikia bilioni 1.43 mwaka 2017.  

Akieleza mafanikio yaliyopatikana kutokana na uboreshaji wa mifumo ya kukusanya mapato Dkt. Abbasi amesema mifumo hiyo sio tu imeongeza mapato, lakini pia imeongeza ufanisi.   

“Kabla ya Mfumo wa TTMS Serikali ilikuwa haipati kitu kabisa katika miito ya simu za nje wala kuwa na uwezo wa kuhakiki mapato ya simu za ndani lakini tangu mfumo huo ulipofungwa kwa eneo la mapato ya simu za nje tu Serikali imekwisha kusanya Shilingi bilioni 97.16 ikiwa ni malipo ya kodi zitokanazo na mapato ya kampuni za simu kwa simu kimataifa zinazoingia na kuishia hapa nchini” alifafanua Dkt. Abbasi. 

Kuhusu ziara ya Rais Magufuli kwenye nchi za Afrika Kusini, Namibia na Zimbabwe Dkt. Abbasi ameeleza ziara hiyo licha ya kuwa na lengo la kuimarisha ushirikiano wa kihistoria, lakini pia ilikuwa na lengo la kutafuta fursa za kibiashara.

 “Kwenye ziara hiyo Rais Magufuli ameweza kufikia makubaliano ya kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kwenye sekta ya utalii, usafiri wa anga na miundombinu pia Tanzania imeweza kupata soko la mahindi tani 700,000 nchini Zimbabwe”. 

Aidha, Dkt. Abbasi amewasihi Watanzania wenye ujuzi wa kufundisha Lugha ya Kiswahili kuitumia vyema fursa ya kufundisha lugha hiyo nchini Afrika Kusini kwa kujisajili kwenye kanzi data ya wataalamu wa Kiswahili Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ili wapate ithibati na kutambulika rasmi. 

    Kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Msemaji Mkuu wa Serikali amewahakikishia Watanzania majadiliano juu ya mrad huo bado yanaendelea na Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha maslahi ya nchi yanawekwa mbele ili wanufaike na rasilimali za nchi yao.      

    Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na vyombo vya habari umelenga kueleza  utekelezaji wa serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo madini, miundombinu, mawsiliano na sekta nyingine.

Wananchi Watakiwa Kutembelea Ofisi Za TRA Kuwasilisha Maoni Na Kero Za Kikodi

$
0
0
Na. Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imetoa wito kwa wananchi kutembelea ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilizopo katika maeneo yao na kuhudhuria vikao vinavyoitishwa na wakuu wa Mikoa na Wilaya ili kuwasilisha maoni na kero zao zinazohusu kodi.

Wito huo umetolewa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Jaku Hashimu Ayoub, alietaka kujua ni lini TRA itakaa na Wafanyabiashara kusikiliza vilio vyao kwa kuwa kila mkoa una ofisi za Mamlaka hiyo.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, TRA ina ofisi katika mikoa yote ya Tanzania pamoja na baadhi ya wilaya zake, na baadhi ya mikoa ina vituo maalum vya huduma za kodi (Tax Centres), hususani Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya, pia kila Mkoa una Mwanasheria na Afisa Elimu ya Kodi  kwa ajili ya kutoa elimu, kusikiliza na kutatua kero za walipakodi.

“TRA imeweka utaratibu kwa meneja wa mikoa ya kikodi kukutana na walipakodi kila Alhamisi ili kusikiliza kero zao na kuzitatua, hatua ambayo ina lengo la kujenga imani , kutatua kero na kukuza ridhaa ya ulipaji kodi kwa hiari”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa miongoni mwa kazi za kila siku za TRA ni kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara ili kuwawezesha kufanya biashara zao bila usumbufu, hivyo hufanya biashara katika ngazi ya wilaya, mikoa na Taifa ili kutoa elimu, na pia hurusha vipindi maalum katika runinga na redio kuhusu elimu ya kodi kwa wananchi na kujibu kero za wafanyabiashara.

Dkt. Kijaji alieleza kuwa Wenyeviti wa Kamati za Mapato za Mikoa na Wilaya ambao ni wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwa wakisikiliza kero za walipa kodi kwa kushirikiana na TRA na kwamba Mamlaka hiyo hubuni na kuanzisha mifumo, vituo na vilabu rafiki vya kikodi ili kujibu vilio vya wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

Aidha Dkt. Kijaji alikanusha kuwepo kwa usumbufu wa utoaji wa mizigo kutoka Zanzibar ikilinganishwa na mizigo mingine inayopitia bandari ya Dar es Salaam kwenda nchi za nje kama Zambia, Uganda, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo akifafanua kuwa bidhaa zote zinatakiwa kufuata utaratibu wa forodha.

Alisema bidhaa zinazoingia Tanzania Bara kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa Afrika (SADC), hupata msamaha wa ushuru wa Forodha lakini hulipiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani pamoja na ushuru wa bidhaa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa May 31


NEC yatangaza nafasi za ajira za muda za uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura

$
0
0
 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi za kazi za muda kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura.

Kwa mujibu wa tangazo la maombi ya ajira hizo lililosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Mabamba Rajabu Moses, Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na wasiozidi miaka 45 wametakiwa kuomba.

Sifa zingine za waombaji ni kuwa na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

“Awe  na uwezo wa kutambua matatizo ya kompyuta ya hardware na software an kuyatatua” ilisema sehemu ya tangazo hilo na kuongeza kuwa:.

“Awe na uwezo wa ku-istall programu za kompyuta an kutoa msaada wa kuifundi wa TEHAMA kwa watumiaji. Awe hajawahi kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai an awe na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yenye usimamizi mdogo”.

Sifa nyingine za ziada za kazi hiyo zimetajwa  kwenye tangazo hilo linalopatikana kwenye Tovuti ya NEC ya www.nec.go.tz na mitandao ya kijamii ya NEC.

Orodha kamili ya washindi wa MO Simba Awards 2019

$
0
0
Usiku wa kuamkia leo kulitolewa tuzo za Mo Simba Awards 2019 katika hoteli ya Hyatt Regency - The Kilimanjaro iliyopo Jijini Dar es Salaam. Chini ni majina ya washindi.

Waziri Jafo atoa maelekezo maalumu kwa Ma-RC, Ma DC na Wakurugenzi.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Suleiman Jafo amewaagiza wakuu wa Mikoa minne iliyopo kwenye mradi wa “lishe Endelevu” kuhakikisha kuwa mikataba hiyo ya utekelezaji wa afua za lishe inawashukie wakuu wa Wilaya, nao wasainiane na wakurugenzi wa halmashauri, nao pia waishushe kwa watendaji wa kata na watendaji hao  wasainiane na watendjai wa vijiji na mitaa ili utekelezaji wa mikataba hiyo kuwa shirikishi bila ya kubagua eneo lolote la utawala.

Amesema kuwa pamoja na utekelezaji wa mradi huo, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa niaba ya Makamu wa Rais alisainishana mkataba wa utekelezaji wa afua za lishe na wakuu wa Mikoa yote nchini ili kuchochea utekelezaji wa shughuli za lishe hapa nchini, mkataba ambao una viashiria kumi ambavyo vinampima Mkuu wa Mkoa kila baada ya miezi sita na utadumu kwa kipini cha miaka minne kuanzia januari 2018 hadi 2021

“Kwa vile eneo hili ni eneo la mradi maalum, nitatamani sana niweze kuona katika mbao za vijiji vyetu ambavyo miradi hii inatekelezeka, tuwe na taarifa licha ya taarifa ya mapato na matumizi, kuwe na taarifa ambayo inasema katika Kijiji X, Kijiji cha Milepa, Kijiji cha Wampembe ama Kijiji kingine inaonesha watoto wenye udumavu ni wangapi na watoto wenye upungufu wa damu ni wangapi, hili jambo ninlazima tushikane kila mtu atomize wajibu wake kuhakikisha ajenda ya lishe tunaisimamia kwa nguvu zote,” Alisisitiza.

Ameyasema hayo alipokuwa akizindua mradi wa Lishe Endelevu unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) unaotekelezwa katika Mikoa minne ya Iringa, Dodoma, Morogoro pamoja na Rukwa ikiwa ni mchango wa Serikali ya Marekani katika kuisaidia Serikali ya Tanzania kufikia lengo la kupunguza tatizo la udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano kutoka asilimia 34 hadi asilimia 28 ifikapo mwaka 2021.

Akitoa salamu za mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alitaja baadhi ya mambo yanayopelekea wananchi wa Mkoa wa Rukwa, hususan watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kuwa na hali duni ya lishe huku akisistiza Utamaduni na mazoea ya wananchi wengi kutumia aina fulani za vyakula hususan nafaka kwa muda mrefu bila kuchanganya na makundi mengine ya vyakula, hivyo kukosa virutubishi muhimu.

“Wananchi wengi hasa wanaoishi Vijijini kutokuwa na Elimu ya kutosha kuhusu masuala ya lishe bora.Baadhi ya akinamama na familia kwa ujumla, kutozingatia taratibu za unyonyeshaji na ulishaji bora kwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili. Baadhi ya akina mama wenye watoto wadogo kukosa muda wa kutosha wa kuwahudumia watoto wao kwa lishe bora,” Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirila la Maendeleo la Watu wa Marekani Andrew Karas aliishukuru serikali kwa kuweka kipaumbele juhudi za kuhakikisha inapunguza hali ya udumavu nchini kwa kutekeleza afua mbalimbali kuanzia ngazi ya kitaifa hadi kwenye halmashauri huku akimpongeza mgeni rasmi wa shughuli hiyo Mh Suleima Jafo na Wizara ya TAMISEMI kwa kutoa kipaumbele maboresho ya lishe.

“Sisi sote tunatambua mchango wa Lishe katika maendeleo jumuishia na maendeleo endelevu, tunavyojua Tanzania inaendelea kukumbwa na viwango vya juu vyua utapiamlo Mkoani Rukwa zaidi ya nusu ya watoto waliochini ya miaka mitano wana udumavu ambayo ni asilimia kubwa zaidi nchini, utapiamlo una athari mbaya kwa mtu binafsi, familia na taifa, unaathiri maendeleo ya Kimwili na pia kiakili, lishe duni huchangia kuwa na uwezo mdogo wa kujifunza,” Alisema.

Mradi huu unalenga kuongeza na kuboresha upatikanaji na utoaji wa huduma bora za lishe katika vituo vya afya na jamii, uzalishaji na ulaji wa vyakula vyenye virutubishi kwa wingi katika ngazi ya kaya, udhibiti wa usawa wa kijinsia katika mapato na matumizi ya rasilimali za nyumbani ili kuhakikisha upatikanaji wa vyakula mchanganyiko.

Shirika la maendeleo la Watu wa marekani limetenga zaidi ya dola za kimarekani milioni 19 ili kutekeleza mtadi wa lishe Endelevu kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 katika Mikoa minne na Halmashauri 22 za Tanzania Bara na kulenga kufikia zaidi ya wanawake milioni 1.5 walio katika umri wa kuzaa, watoto milioni 1.1 walio chini ya umri wa miaka mitano na vijana walio katika rika la baleghe 330,000 wenye umri wa miaka 15-19.

Serikali Kuja Na Mbinu Za Ziada Kukabiliana Na Ugonjwa Wa Mnyauko Wa Migomba

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Kwa kipindi cha Mwaka 2006 - 2014, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Kagera umetoa mafunzo ya kutokomeza ugonjwa wa mnyauko wa migomba kwa wakulima na maafisa ugani kwenye wilaya zote zilizoathirika.

Serikali imekuwa ikiendesha kampeni ya kung’oa migomba yote iliyoathirika, kukata Ua Dume na kuiteketeza. Halmashauri zote za Wilaya za Mkoa wa Kagera ziliweka sheria ndogo ndogo za kuwataka wakulima kung’oa na kuchoma au kuzika migomba yote iliyoathirika. Zoezi hilo lilipunguza ueneaji wa ugonjwa huo kwa asilimia 70.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 31 Mei 2019 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe Jasson Samson Rweikiza Mbunge wa Bukoba vijijini aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani kuchukua hatua za makusudi za kupambana na ugonjwa huo na kutokomeza kabisa.

Bashungwa alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya tafiti za kuzalisha miche bora ambayo haina vimelea vya ugonjwa wa unyanjano kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ikishirikiana na Shirika la Belgium Technical Cooperation.

Aidha, hadi sasa miche bora milioni sita (6) imezalishwa na kusambazwa kwa wakulima katika Mikoa ya Kagera na Kigoma.

Bashunwa ametoa wito kwa wakulima kote nchini kutumia mbegu bora za migomba aina ya Shia 17, Shia 23, Nshakara, Nyoya, na Kinohasha zinazozalishwa katika taasisi za utafiti kama Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine, Mikocheni, Uyole, Kibaha, Maruku na Tengeru ili kuongeza tija katika uzalishaji na kutosafirisha ndizi zilizofungashwa na majani ya migomba kutoka mashamba yaliyoathirika.

Aliutaja ugonjwa huo wa Mnyauko wa migomba ambao kitaalamu unaitwa unyanjano wa migomba kuwa husababishwa na vimelea aina ya bacteria ambao hushambulia aina zote za migomba na jamii yake.

Ugonjwa huo husambazwa na ndege, nyuki, binadamu, ngedere na tumbili; miche iliyoathirika; vifaa vya shambani vilivyotumika kwenye migomba iliyoathirika na vifungashio vya kusafirishia ndizi.

Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha AICC Chaingiza Mapato Zaidi Ya Shilingi Bilioni 11

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imewasilisha hotuba ya mpango na Makadirio ya Bajeti ya wizara kwa mwaka  wa fedha  2019/2020 ,  bungeni jijini Dodoma  ambapo kituo cha kimataifa cha mikutano  Arusha  AICC  kimeendelea kuwa kitovu cha diplomasia  ya mikutano hapa nchini na kuchangia katika uchumi wa taifa.
 
Akiwasilisha hotuba  ya Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mei 30, 2019 bungeni jijini Dodoma  ,Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi amesema hadi kufikia Mwezi April ,2019  kituo cha mikutano ya kimataifa cha Arusha AICC  Kimeingiza  mapato ya Sh.Bil.11,Mil.428  laki 8  ,68 elfu na mia 998.
 
Kati ya Fedha hizo,Sh.Bilioni 2 ,Mil.76,laki 7 ,71 elfu na 27[2,076,771,027] zimetokana na huduma  za mikutano 342  iliyofanyika katika kituo cha AICC  ambapo mikutano 32 kati ya hiyo ni ya kimataifa na 310 ni ya kitaifa.
 
Prof.Kabudi amefafanua kuwa ,Sh.Bilioni 2,Milioni 244 , laki 5,na 32 elfu  na mia 662 [2,244,532,662] zimetokana na huduma za mikutano  katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere ,Sh.Bil.3,mil 556,laki 5  na 96 elfu na mia 819[3,556,596,819] na Sh.bil.3,mil.550,laki 9,na 68 na mia 490 [3,550,968,490]ni kutokana na huduma za hospitali.
 
Aidha,Prof.Kabudi amesema ,kuhusu usimamizi wa kiuchumi Ripoti inaonesha kuwa Tanzania imeendelea kutekeleza mipango ya Maendeleo ikiwianishwa na mpango wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa [2030] na Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika,Mpango wa Miaka mitano[FYDP  II 2016/17-2020/21] unaweka mkazo katika mageuzi ya viwanda na maendeleo ya Rasilimali watu kama njia sahihi ya kuifikisha nchi katika uchumi wa kati ifikapo 2025.
 
Hata hivyo,Successor Strategy ya Zanzibar 2016/17-2020/21 imepatia ufumbuzi  maeneo mengi yaliyokuwa yameainishwa   kama mapungufu  kama mpango kazi wa  APRM.
 
Katika hatua,nyingine Prof.Kabudi katika hotuba yake amesema chuo cha Diplomasia kimeendelea kutoa mafunzo  na kufanya tafiti katika masuala ya Diplomasia ,uhusiano wa kimataifa na usuluhishi wa Migogoro na kulinda Amani.
 
Chuo cha Diplomasia kinatoa Mafunzo ya Lugha saba [7] za kigeni  ambazo ni kiarabu,kichina,Kifaransa,kiingereza,Kireno,Kihispania,na Kikorea na hadi sasa kinafanya Mazungumzo na Serikali ya Kirusi  ili kufadhili mafunzo ya Lugha ya Kirusi na Mwaka 2018/2019 kilidahili Jumla ya wanafunzi  1,029  katika ngazi za cheti,Stashahada,Shahada na Shahada ya Uzamili.

Waziri Kabudi: Hatuwezi Kupiga Magoti Kuomba Misaada

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haikupiga magoti katika kipindi cha utawala wa Awamu ya pili chini ya Ali Hassan Mwinyi, ilipokuwa na hali ngumu, hivyo haiwezi kufanya wakati huu ikiwa na hali nzuri zaidi.

Profesa Kabudi aliliambia Bunge jana jioni alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliochangia mjada wa bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.

Alisema licha nchi kutokuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni wakati huo wa Awamu ya pili (1985-1995), Tanzania haikupiga magoti kuomba msaada lakini sasa, Taifa lina akiba ya fedha za kigeni za miezi mitano.

“Kama tuliweza kwa wakati huo hatuwezi kushindwa katika awamu hii ya (Rais John) Magufuli. Tumeamua kujitegemea,” alisema Kabudi.

Profesa Kabudi alisema Tanzania ndiyo nchi pekee Afrika ambayo haijawahi kushindwa vita na ndiyo nchi iliyowarudisha wapigania uhuru katika nchi zao.

Alisema ndani ya Tanzania kuna watu aliowaita mabarakuli ndani ya nchi wanaofanya kazi za vibaraka wa kubeza juhudi za Serikali wanapoona mafanikio.

Alisema hiki ndicho kizazi cha mwisho kwa fedheha lakini kwa wajukuu wanaokuja hawatakiwi kuona fedheha hiyo.

Korea Kaskazini Yamuua mjumbe wake maalumu kwa ajili ya Marekani Kim Hyok Chol kufuatia kushindwa kwa mkutano wa pili wa Kim Jong Un na rais Donald Trump.

$
0
0
Vyombo vya habari vya Korea Kusini hii leo vimeripoti kwamba Korea Kaskazini imemuua mjumbe wake maalumu kwa ajili ya Marekani Kim Hyok Chol kufuatia kushindwa kwa mkutano wa pili wa kilele kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais Donald Trump. 

Gazeti la Chosun Ilbo limeandika Chol aliyeuandaa mkutano huo wa Hanoi na kumsindikiza Kim kwenye treni yake binafsi ameuawa kwa kupigwa risasi kwa kile kinachotajwa kumsaliti kiongozi huyo wa juu baada ya kufanikiwa kuishawishi Marekani wakati wa majadiliano ya kabla ya mkutano huo wa kilele. 

Gazeti hilo lililonukuu chanzo ambacho hakikutambulishwa limesema Chol, aliuawa mwezi Machi, katika uwanja wa ndege wa Mirim pamoja na maafisa wanne waandamizi wa wizara ya mambo ya nje baada ya uchunguzi. 

Mkalimani wa Kim kwenye Umoja wa Mataifa naye ametiwa kizuizini baada ya kufanya makosa kwenye mkutano huo wa kilele.

Video: Young Dee Ft. Abbah - Gari Yangu Remix

$
0
0
Video: Young Dee Ft. Abbah - Gari Yangu Remix

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH ....Anauwezo wa wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani  Mwenye UWEZO wakufanya dua mbali mbali  Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?

Wasilina na Mohamedi Buruhani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO   Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? . Mohamedi Buruhani  Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN  . Anatafsiri Ndoto. , KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na Biashara.


Mawasiliano: (+255 )715971688 au (+255  )756914036

Video: Gigy Money Ft. Tushynne - Changanya

$
0
0
Video:  Gigy Money Ft. Tushynne - Changanya

Thamani ya Mfuko wa Pensheni Kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Yafikia Trilioni 5.8

$
0
0
Na Frank  Mvungi- MAELEZO
Thamani ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) imefikia Trilioni 5.8 hali inayoonesha kuwa mfuko huo unaendelea kuimarika na hivyo kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wake.
 
Akizungumza katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo  Bw. Hosea  Kashimba  amesema kuwa  kuunganishwa kwa mifuko ya GEPF, LAPF, PSPF na PPF kunatoa  fursa ya kuimarisha zaidi sekta ya hifadhi ya Jamii hali iliyochangia thamani ya mfuko mpya wa PSSSF kuendelea kukua hata katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwake.
 
“Tumeshatumia zaidi ya Trilioni moja kulipa mafao kwa wanachama wetu hali inaonesha kuwa mfuko upo katika hali nzuri hivyo niwatoe hofu wanachama wetu kwani tumejipanga kuhakikisha tunawahudumia vizuri kwa mujibu wa sheria na kanuni za hifadhi ya jamii “ Alisisitiza Kashimba

Akifafanua Kashimba amesema kuwa,  wastaafu elfu kumi wameshalipwa mafao yao tangu kuanzishwa kwa mfuko huo na wachache ambao hawajalipwa ni wale ambao hawajahakiki taarifa zao kwa muda  uliotolewa hivyo aliwataka kujitokeza na kuhakikiwa ili warejeshwe katika daftari la malipo.
 
“Ukishahakikiwa tunakurejesha kwenye daftari la malipo na utalipwa malipo yako yote ambayo hukuwa umelipwa hapo awali kabla ya kuhakikiwa hivyo niwatoe hofu wanachama wetu na kuwataka wajitokeze kuhakiki taarifa zao” Alisisitiza Kashimba
 
Alieleza kuwa,takribani wastaafu 113,000 wamehakikiwa kati ya wastaafu 124,000 waliotakiwa  kuhakikiwa hivyo kuwaomba wanachama wa mfuko huo nchini kuendelea kujitokeza kuhakikiwa kupitia ofisi  za mikoani kwa kuwa huduma zinazotolewa makao makuu  zinatolewa pia mikoani.

Akizungumza kuhusu ujenzi wa uchumi wa viwanda Bw. Kashimba amesema kuwa mfuko huo umejipanga kikamilifu kuendelea kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kuwekeza  katika sekta mbalimbali kulingana na miongozo ya Serikali.
 
“Tumewekeza katika Kiwanda cha viatu Karanga Moshi kwa ubia na Jeshi la Magereza na tunatarajia Kiwanda hiki kitatoa ajira  elfu nne na kuzalisha jozi milioni 1. 2 kwa mwaka, tunawekeza kwenye kiwanda cha kuchakata tangawizi kilichopo Wilayani Same, Kiwanda cha nyama Morogoro na vingine kulingana na miongozo ya uwekezaji na maagizo ya Serikali “Alisisitiza Kashimba
 
Aidha, Mitambo ya kuzalisha viatu katika  kiwanda cha Karanga inatarajiwa kuwasilisi nchini na kufungwa katika kiwanda hicho kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kutekeleza azma ya sekta hiyo kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi jumuishi kupitia viwanda.
 
Hata hivyo Kashimba aliwataka wanachama wote kuhakikisha kuwa waajiri wanawasilisha michango yao kwa wakati ili kuepuka usumbufu wakati wa kustaafu.
 
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa mfuko huo Bw. Victor Kikoti amesema kuwa baadhi ya mafao yanayotolewa ni yale ya muda mfupi na muda mrefu lengo likiwa kuwawezesha wanachama wote kuishi maisha bora hata baada ya kustaafu.
 
“Wanachama wetu wataendelea kunufaika na huduma zetu na hata pale inapotokea bahati mbaya mwanachama wetu amefariki basi haki zake hazitapotea na zinalindwa kwa mujibu wa sheria ili ziwanufaishe warithi wake” Alisisitiza Kikoti
 
Naye Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Bw. Gilbert Chale amesema kuwa mfuko huo umejenga mifumo bora inayounganisha Ofisi zote na makao makuu ya mfuko ili kuimarisha huduma na tija kwa wanachama.
 
Kuunganishwa kwa mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSSSF, GEPF, LAPF na PSPF kumewezesha kuanza rasmi kwa mfuko mpya wa Hifadhi ya Jamii katika Utumishi wa Umma (PSSSF) mwaka 2018.


Naibu Waziri Mhe.kanyasu Aahidi Mageuzi Kwenye Jumuiya Za Hifadhi Za Wanyamapori

$
0
0
Serikali imewahakikishia Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za  Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) kuwa itaendelea kufanya mageuzi pamoja kuwapa ushirikiano kwa  kuendeleza dhana halisi  ya uhifadhi wa wanyamapori  shirikishi katika jamii.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma  na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu wakati akizungumza na wenyeviti hao kwenye mkutano wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya wizara na wadau hao wa uhifadhi nchini.

Amesema Wizara itaendelea kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kwa kuwa inatambua mchango mkubwa wanaoutoa katika shughuli za uhifadhi wa wanyamapori nchini.

Aidha,  Mhe.Kanyasu ameziagiza WMAs zinazotegemea kufanya uchaguzi hivi karibuni  ziendelee na utaratibu wa zamani wa kutumia kigezo cha elimu ya kuanzia darasa la 7 na kuendelea.

 Amesema lengo la  kuruhusu kutumika kwa kigezo hicho cha elimu  ya darasa la saba na kuendelea ni kutoa fursa kwa  wagombea wengi wenye uwezo kuweza kujitokeza.

 Amezitaka WMAs hizo  kuchagua viongozi watakaokua na uwezo wa  kutekeleza  mipango mbalimbali kwa ufanisi.

Hata hivyo, amesema kuwa yapo baadhi ya mambo ya msingi ambayo Wizara imeanza kuyaboresha kwenye kanuni za WMAs  likiwemo suala la kiwango cha elimu kwa viongozi wa WMAs nchini ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima inayojitokeza mara kwa mara ndani ya WMAs hizo.

Kwa upande Mwenyekiti wa Muungano huo, Bw. Christopher Mademula amemueleza Mhe.Kanyasu kuwa suala la kigezo cha elimu liangaliwe kwa mapana yake kwa kigezo kuwa ikiwa wagombea wa darasa la saba hawataruhusiwa kugombea nafasi za uongozi kwenye WMAs, kitendo hicho kitachochea ujangili kwa kuwa wao wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa za kiinteligensia za ujangili kwenye maeneo yao.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images