Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali kujenga viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi nchini

$
0
0
Serikali inatarajia kujenga viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi nchini kupitia Shirika la Uvuvi Tanzania (Tafico).

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Mei 27 na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati akijibu swali la Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema).

Katika swali lake Kubenea, lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Viti Maalumu, Tunza Malapo (Chadema), alihoji ni lini na ni wapi Kiwanda cha Samaki cha Pwani kitajengwa hapo.

Almasi Yenye Thamani ya Bilioni 3.2 Yaipaisha Sekta ya Madini Tanzania

$
0
0
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
Tanzania imetajwa kuweka historia katika tasnia ya madini baada ya Almasi yenye Karati 512.15 kupatikana hivi karibuni katika eneo la Maganzo Mkoani Shinyanga  na kuuzwa kwa jumla ya shilingi Bilioni 3.2.
 
Akizungumza katika mahojiano maalum kuhusiana na madini hayo,Naibu  Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus  Nyongo amesema kuwa  kutokana na kupatikana kwa almasi hiyo Serikali itapata mapato ya takribani shilingi  milioni 235,000/- kama kodi na tozo mbalimbali ikiwemo mrabaha ambayo yamelipwa Serikalini baada ya mauzo hayo.
 
Kuuzwa kwa jiwe hilo moja la almasi katika soko la madini mkoani Shinyanga ni muendelezo wa tija inayopatikana kupitia masoko hayo toka kuanzishwa kwake nchini,jumla ya shilingi bilioni 34.3 zimepatikana kwenye biashara ya dhahabu iliyofanyika katika kipindi cha mwezi mmoja tu kati ya Machi 17 mpaka Aprili 17 mwaka huu katika masoko ya madini kote nchini, kwa mujibu waziri wa Madini,Doto Biteko, aliyetoa taarifa hiyo hivi karibuni.
 
“Natoa wito kwa wachimbaji wote,madalali na mawakala,kuyatumia ipasavyo masoko hayo kwakuwa kila mmoja atapata stahiki yake tofauti na awali kabla ya kufunguliwa kwa masoko hayo ambapo wachimbaji hawakuwa kwenye mikono salama kufutia kutokuwa na mfumo rasmi wa uuzaji madini yao”.Alisisitiza mhe. Nyongo
 
Akifafanua amesema kuwa kila mchimbaji anapaswa kuzingatia sheria na Kanuni za sekta ya madini ili kuepuka mkono wa sheria na hatua nyingine ikiwa ni pamoja na kutaifishwa kwa madini yao pale watakapobainika kutaka kutorosha madini ama kujihusisha na magendo.
 
Aliongeza kuwa baada ya kupatikana kwa almasi hiyo wataalamu wa Wizara hiyo walifanya tathmini ili kuona ubora wake na kiwango kilichopatikana ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata mapato yake.
 
“ Serikali ya Awamu ya Tano imeweka makazo katika kuimarisha sekta ya madini nchini ili itoe mchango unaostahili katika uchumi wetu ndio maana tunaona kuwa kupitia masoko ya madini tuliyoanzisha hata mchimbaji huyu aliyepata hii almasi pale Maganzo aliiuza kupitia soko letu la madini baada ya kufuata taratibu zote” alisisitiza Mhe. Nyongo

Tanzani ni moja ya nchi zenye utajiri mkubwa wa madini ya aina mbalimbali ikiwemo Almasi, Tanzanite, Dhahabu na mengine mengi.
 
Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo katika kuimarisha sekta ya madini ikiwemo kuimarisha taratibu za uuzaji wa madini yote yanayozalishwa hapa nchini, kuimarisha usimamizi, kuwawezsha wachimbaji wadogo ili waweze kuchimba kwa tija.

Shule za Sekondari 1241 Zajengewa Mabweni

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa ,na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, amesema hadi sasa shule za sekondari 1,241 zimejengewa mabweni kati ya shule za sekondari 3,634 zilizopo kwa kutumia ruzuku kuu.

Jafo amesema hayo leo Jumatatu Mei 27, bungeni jijni Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Azza Hilaly Hamad (CCM).

Katika swali lake, Azza alihoji serikali ina mkakati gani wa kujenga mabweni katika shule za sekondari zilizoanzishwa kitarafa ili kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu bora.

BREAKING: Lazaro Nyalandu Akamatwa na TAKUKURU

$
0
0
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) imemkamata aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu kwa mahojiano. 

Kamanda Polisi mkoani Singida Sweetbert Njewike amethibitisha.

Nyalandu alikua kwenye zoezi la ‘Chadema ni msingi’ ambapo TAKUKURU walifika wakiwa na silaha na kumchukua kwa nguvu na kutokomea nae kusikojulikana.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne May 28

Trump: Marekani haiko tayari kwa makubaliano ya kibiashara na China

$
0
0
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema nchi yake haiko tayari kufikia makubaliano ya kibiashara na China, lakini anaacha wazi uwezekano wa mataifa hayo mawili siku moja kufikia makubaliano.

Akizungumza jana mjini Tokyo, Trump amesema China iko tayari kufikia makubaliano, lakini Marekani haiko tayari.

Mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani yamekuwa katika mzozo wa kibiashara. Trump anatarajiwa kukutana na Rais wa China, Xi Jinping mwezi ujao katika mkutano wa mataifa yenye nguvu kiuchumi, G20.

Aidha, Trump pia amekutana na Mfalme Naruhito wa Japan katika kasri la kifalme. Mfalme huyo pamoja na mkewe Masako wamemkaribisha Trump, kiongozi wa kwanza wa kigeni tangu Naruhito alipotawazwa hivi karibuni. Trump amekutana pia na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe.

Dereva Teksi Afikishwa Mahakamani kwa Tuhuma za Kumteka Mo Dewji

$
0
0
Dereva teksi, Mousa Twaleb (46) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Mei 28, 2019 akikabiliwa  na mashtaka matatu likiwemo la  kumteka mfanyabiashara, Mohamed Dewji ‘Mo’.

Akisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi kwa kushirikiana na Wakili wa Serikali Simon Wankyo, mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mei Mosi mwaka 2018 na Oktoba mwaka huo jijini Dar es Salaam na Johannesburg, nchini Afrika Kusini.

Kadushi amedai mshtakiwa alijihusisha na genge la uhalifu, walimteka Mo katika Hoteli ya Colleseum iliyopo wilayani Kinondoni na kumficha.

Mshtakiwa huyo pia anadaiwa kutakatisha Sh milioni nane ambazo alijipatia huku akijua zinatokana na mazalia ya kosa la uhalifu.

Mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu lolote sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Kesi imeahirishwa hadi Juni 11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Iran Yasema haioni uwezekano wa mazungumzo na Marekani

$
0
0
Iran imesema kuwa haioni uwezekano wa kufanya mazungumzo na Marekani. Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za kigeni wa Iran Abbas Mousavi amesema hayo leo, siku moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema kuna uwezekano wa makubaliano na Iran kuhusu mpango wake wa silaha za nyuklia. 

Mousavi amenukuliwa na shirika la habari la Fars akisema kuwa Iran haitilii maanani maneno bali kile ambacho ni muhimu kwa Iran na mabadiliko ya namna suala hilo linavyoshughulikiwa. 

Hapo jana, Rais Trump alisema anaamini kuwa Iran itapenda kuwa na makubaliano na anafikiri hilo ni wazo zuri na kuna uwezekano wa hilo kufanyika. 

Mzozo umezidi kuongezeka kati ya Marekani na Iran tangu Marekani ilipozipeleka ndege zake za kivita na silaha nyingine za vita Mashariki ya Kati, na Rais Trump kutangaza mipango ya kuwapeleka wanajeshi 1,500 zaidi katika eneo hilo, hali ambayo imeibua hofu ya vita. 

Marekani ilijiondoa kwenye mkataba wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, na ikaongeza vikwazo dhidi ya Iran.

Rais Magufuli atembelea eneo la makaburi ya mashujaa wa Namibia,atembelea kiwanda cha nyama Jijini Windhoek Namibia

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2019 ametembelea na kuweka shada la maua katika eneo la mashujaa (Heros Acre) waliopigania ukombozi wa Namibia, lililopo nje kidogo ya Jiji la Windhoek nchini humo.

Katika eneo hilo wamezikwa mashujaa wa ukombozi wa Namibia ambao baadhi yao walipata mafunzo katika kambi ya Kongwa nchini Tanzania, wengine walikuwa maafisa wa Chama cha SWAPO ambao ofisi zao zilikuwa Jijini Dar es Salaam na wengine ni viongozi wakuu walioendesha mapambano wakiwa nchini Namibia.

Baadhi ya mashujaa waliozikwa katika eneo hilo ni Ndimo Hamaambo, Peter Nanyemba, Theo-Ben Gurirabo na Toiro ya Toire.

Mhe. Rais Magufuli ameongozana na mwenyeji wake Mhe. Rais Hage Geingob.

Baada ya kutembelea eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli ametembelea kiwanda cha nyama cha kampuni Meatco kilichopo Jijini Windhoek na kuelezwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bw. Jannie Breytenbach kuwa kiwanda kina uwezo wa kuchinja ng’ombe 630 kwa siku, kimeajiri wafanyakazi 650 na kwamba kampuni hiyo ipo tayari kushirikiana na Tanzania kuanzisha viwanda vya nyama.

Mhe. Rais Magufuli amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo Barani Afrika na ameikaribisha kampuni ya Meatco kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Kabla ya kuondoka nchini Namibia kwenda nchini Zimbabwe ambako anakwenda kufanya Ziara Rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Pili wa Namibia Mhe. Hifikepunye Pohamba Jijini Windhoek.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Windhoek
28 Mei, 2019

Kesi ya vigogo 11 wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Yapigwa Kalenda

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi inayowakabili vigogo 11 wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) baada ya wakili wa utetezi kuomba muda kupitia jalada.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kukiuka sheria wakati wa ununuzi wa mabehewa 25.

Wakili wa utetezi, Tibita Muganga amedai leo Jumanne Mei 28, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maghela Ndimbo kueleza kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya usikilizwaji na shahidi yupo.

"Kati shauri hili nashiriki kwa mara ya kwanza baada ya wakili, Malamsha aliyekuwepo awali kujitoa nimeshaanza kazi ya kulipitia jalada ninaomba nipewe muda kidogo kwa ajili ya kumalizia kazi hiyo,” amedai wakili Muganga.

Hakimu Shahidi amekubali ombi hilo na kupanga shauri hilo kusikilizwa Mei 29, 2019 na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Vigogo hao ni aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa TRL, Kipallo Kisamfu; mkuu wa kitengo cha makenika na mhasibu mkuu, Jasper Kisiraga; kaimu meneja wa usafiri, Mathias Massae; kaimu mhandisi wa ufundi na meneja ujenzi, Muungano Kaupunda na mkuu wa ufundi na meneja ujenzi, Ngoso Ngosomwiles.

Wengine ni mhandisi mkuu wa ufundi, Paschal Mafikiri;  mhandisi mipango,  Kedmo Mapunda;  kaimu mhandisi wa mawasiliano, Felix Kashaingili; mkuu wa usafiri wa reli, Lowland Simtengu; mkuu wa ubunifu na utengenezaji wa nyaraka, Joseph Syaizyagi na kaimu mkuu wa usafirishaji, Charles Ndenge.

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH ....Anauwezo wa wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani  Mwenye UWEZO wakufanya dua mbali mbali  Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?

Wasilina na Mohamedi Buruhani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO   Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? . Mohamedi Buruhani  Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN  . Anatafsiri Ndoto. , KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na Biashara.


Mawasiliano: (+255 )715971688 au (+255  )756914036

Korea Kaskazini: Tutaendelea kufanya majaribio ya makombora yetu na haturudi nyuma

$
0
0
Serikali ya Korea Kaskazini imesisitiza kwamba, itaendelea kufanya majaribio ya makombora yake na haitorudi nyuma katika suala hilo.

Taarifa iliyotolewa leo na Pyongyang imesema kuwa, kuacha kufanya majaribio ya makombora ya nchi hiyo, kuna maana ya kupuuza haki yake ya kujilinda. 

Kadhalika serikali ya Korea Kaskazini imeyataja kuwa yasiyo sahihi madai ya John Bolton, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani kwamba majaribio hayo yanakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa. 

Ameongeza kwamba, majaribio ya makombora ya nchi hiyo ni jibu kwa vitisho na mashinikizo ya Washington na washirika wake katika eneo dhidi ya Pyongyang.

Imesema kuwa, imeamua kuanzisha majaribio ya silaha zake kutokana na kitendo cha Marekani cha kutofungamana na ahadi zake kwa ajili ya kuiondolea vikwazo Pyongyang na kadhalika hatua yake ya kufanya mazoezi ya kijeshi katika Rasi ya Korea kwa kushirikiana na waitifaki wake ambao ni Korea Kusini na Japan. 

Hivi karibuni pia serikali ya Korea Kaskazini ilitangaza kuwa Washington inapaswa kubadili siasa zake za upande mmoja kama sharti la kurejea kwenye meza ya mazungumzo kati yake na Marekani. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini ilisema kuwa Pyongyang haitarejea kwenye meza ya mazungumzo iwapo serikali ya Marekani haitafutilia mbali matakwa yake ya upande mmoja katika mchakato wa mazungumzo ya kudhibiti silaha za nyuklia.

Serikali yazindua matumizi ya ardhi bomba la mafuta

$
0
0
Serikali  imezindua mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji, wilaya na mikoa itakayopitiwa na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), ikiwa ni hatua nyingine katika utekelezaji wa mradi huo.

Mpango huo umezinduliwa katika Kijiji cha Sojo wilayani Nzega mkoani Tabora juzi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliyeambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry na Meneja Mradi wa EACOP, Mantin Tiffen.

Akizungumza na wananchi wa Sojo, Waziri Lukuvi alisema  mpango huo wa matumizi ya ardhi unahusisha mikoa nane, wilaya 24 na vijiji 226 ambapo vijiji 30 vipo katika Mkoa wa Tabora.

“Mpango huu unazinduliwa katika Kijiji cha Sojo kwa niaba ya vijiji vyote nchini kwa kuwa hapa Sojo ndipo patakuwa na kituo kikubwa cha kutoa huduma katika mradi wa  bomba la mafuta kuliko vituo vingine, kwani kutakuwa na  kambi kuu na kiwanda cha kutayarisha mabomba yatakayotumika kusafirisha mafuta kitajengwa hapa,” alisema Lukuvi.

Katika hatua nyingine, Waziri Lukuvi alitoa onyo kwa wavamizi wa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya mradi huo kuwa tayari mkuza wote ulishapigwa picha za anga, hivyo fidia itatolewa kwa wananchi wanaostahili tu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, alisema kazi za mradi wa EACOP zilizopangwa kufanyika katika kijiji hicho, zina uwekezaji wa Sh bilioni 600 na matarajio ni kuwa kazi hizo zitaanza Septemba mwaka huu.

Alisema kutakuwa na ajira zitakazozalishwa, hivyo alitoa wito kwa wananchi  kuchangamkia fursa zitakazojitokeza kutokana na uwekezaji huo.

“Mpaka sasa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi umeshatoa ajira zaidi ya 200 na matarajio ni kuwa utaendelea kutoa ajira zaidi kwa Watanzania,” alisema Mgalu.

Kuhusu umeme, alieleza kuwa Wizara iko katika mpango wa kusambaza umeme kwenye vijiji vyote vinavyopitiwa na mkuza huo kwa gharama ya Shilingi elfu 27,000 tu ili kuweka mazingira wezeshi ya kutekeleza mradi husika.

MOI Mwenyeji Kongamano la Kimataifa la Madaktari Bingwa wa Mifupa zaidi 150

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dkt Respicious Boniface  jana amefungua kongamano la kimataifa la madaktari wa Mifupa linalofanyika kwa siku tano hapa Tanzania ambapo madaktari zaidi ya 150 kutoka mataifa ya Afrika na sehemu mbalimbali duniani wanashiriki.
 
Dkt Boniface amesema Kongamano hilo limekua likifanyika hapa nchini kila mwaka kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwapa mbinu mpya za matibabu ya mifupa madaktari hapa nchini na nchi nyingine barani Afrika kutokana na MOI kuwa kituo cha mafunzo kutokana na huduma bora za mifupa inazotozitoa.
 
“Madaktari bingwa wetu hapa nchini wamekua wakinufaika sana na kongamano hili, wamekua wakipewa mbinu mpya na zakisasa za matibabu na upasuaji wa mifupa jambo ambalo limepelekea MOI kuweza kumaliza rufaa za nje ya nchi kwa wagonjwa wa mifupa ambapo kwa sasa huduma karibia zote zinapatikana hapa nchini” Alisema Dkt Boniface.
 
Mratibu wa Kongamano hilo Dkt Joseph Mwanga amesema mafunzo yatatolewa kwa njia ya nadharia, vitendo katika chumba cha maabara kwa kutumia mifupa bandia na kwenda kwenye chumba maalum cha kujifunzia kwa kutumia miili ya binadamu (Cadavers).
 
“Kongamano hili limekua na manufaa makubwa sana kwetu, tumekuwa tukipata mbinu mpya kila mwaka kutoka kwa wenzetu wa Marekani jambo ambalo limefanya huduma za mifupa hapa nchini ziendelee kuwa bora ukilinganisha na mataifa mengine barani Afrika” Alisema Dkt Mwanga.
 
Kwa upande wake Profesa Michael Terry ambaye ni mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Calfonia cha San Francisco amesema ushirikiano kati ya Taasisi yake na MOI umejikita katika mafunzo ya namna ya kuwahudumia majeruhi wa ajali kwa lengo la kuwapa huduma bora na za kisasa kwa wakati.
Kongamano hilo limeratibiwa na Taasisi ya MOI kwa kushirikiana na Taasisi za IGOT, SIGN, OTA, AO Alliance na Chuo kikuu cha Calfonia San Fransisco Marekani.
 
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano MOI

Naibu Waziri Kanyasu Aagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Iunde Tume Kuchunguza Kifuta Machozi Wilayani Bunda

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ameiagiza Mamlaka ya  Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) iunde timu ya kuchunguza uhalali wa malipo ya kifuta jasho na kifuta machozi kilichotolewa kwa wananchi  walioathiriwa   na wanyamapori wakali na waharibifu wa mazao katika maeneo mbalimbali nchini.

Mhe. Kanyasu ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea malalamiko na madai kutoka kwa baadhi ya wananchi wa vijiji 4 vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, wilayani Bunda mkoani Mara ambao  mazao yao yaliliwa na kuharibiwa na wanyamapori wakali wamekuwa hawalipwi  huku    wasiostahili ndo wamekuwa wanalipwa .

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Sarakwa, Mariwanda ,Unyali na Kihomboi vinavyopakana na  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Bunda mkoani Mara, Mhe.  Kanyasu amesema  kuwa mara  baada ya uchunguzi kukamilika wale watakaobainika kupokea fidia hiyo wale wasiostahili watachukuliwa  hatua kali za kisheria ikiwemo kuzirudisha fedha hizo.

‘’Nataka niwambie, wale waliopokea kifuta jasho na kifuta machozi kutoka serikalini wakati hawastahili lazima hizo fedha wazitapike” Amesisitiza Mhe. Kanyasu

Aidha, Mhe. Kanyasu amesema licha ya fidia hiyo kuendelea  kulalamikiwa kuwa kidogo ikilinganishwa na hali halisi ya maisha ya sasa,  wananchi ambao  mazao yao  yameharibiwa wanatakiwa kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria  iliyopo na sio vinginevyo.
 
Katika hatua nyingine Mhe. Kanyasu amewataka wananchi wanaoharibiwa mazao yao na wanyamapori wakali na waharibifu  wakiwemo  tembo watoe taarifa ndani ya muda wa siku tatu  katika ofisi za vijiji katika maeneo yao  ili hatua za malipo ziweze kufanyika kwa muda.

Pia, Kanyasu amewaeleza wananchi hao kuwa Serikali imeanza kupitia upya utaratibu wa kifuta jasho na kifuta machozi ili kiweze kuendana na gharama za maisha ya sasa.

Kwa upande wake Bw. Abel Hadawi, mmoja wa wananchi  ambaye mazao yake zaidi ya ekari 20 yaliharibiwa mwaka jana, amemweleza Naibu Waziri huyo  kuwa  amaekuwa akijaza fomu kwa ajili ya kulipwa fidia lakini kila malipo yanapokuja jina lake limekuwa halimo.

Kwa upande wake,  Mkuu wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) kanda ya Ziwa, Emmanuel Nkya amewaeleza wananchi hao kuwa wanachotakiwa kufanya ni  kujaza fomu nne ili kuwe na nakala kuanzia ofisi ya kijiji hadi makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Naye Mbunge wa Bunda vijijini, Boniface Getere amemwomba  Naibu Waziri Kanyasu kuyashughulikia malalamiko ya wananchi wote wanaostahili kulipwa kifuta jasho na kifuta machozi kwa kuwa wengi wao wameathiriwa na kubaki omba omba kufuatia mazao yao kuharibiwa.

Watendaji wa serikali Longido washambuliwa na wafugaji wa mifugo

$
0
0
Na Amiri kilagalila
Mkuu wa wilaya ya Longido Ndugu Frank Mwaisumbe, ameliagiza jeshi la polisi wilayani hapo kuwakamata watu wote walio husika na tukio la kuwapiga watumishi na watendaji wa serikali wakiwa katika utendaji bila kujali vyeo vyao.

Agizo hilo amelitoa jana akiwa katika kijiji cha engarenaibor katika tarafa ya engarenaibor wilayani Longido. Ambapo tukio hilo limetokea na kusababishwa na jamii ya wafugaji walio kuwa wakitorosha mifugo yao kuelekea nchi jirani ya Kenya.

Aidha katika tukio hilo lililosababishwa na wafugaji hao wameweza kufanya uharibifu wa hali ya juu katika ofisi za serikali ya kijiji hicho pamoja na kupelekea kulazwa kwa afisa mmoja wa serikali baada ya kuumizwa na wafugaji hao.

Tukio hilo limetokea wakati wa uthaminishaji wa mifugo hiyo iliyo kamatwa hapo jana ikiwa katika hali ya kutoroshwa kupelekwa nchi jirani ya Kenya bila kulipiwa ushuru, jumla ya mifugo iliyo kamatwa ni ng’ombe 41 na mbuzi pamona na kondoo 521.

 Kwa upande wake mtedaji wa kijiji cha engarenaibor ndugu Tomath Ngobei ameeleza kuwa mifugo hiyo inakamatwa kwa sababu imekuwa ikipitishwa katika kijiji hicho kwenda nchi jirani ya kenya bila kulipiwa hivyo wamekuwa wakishirikiana na wizara ya mifugo na uvuvi kuzuia utoroshwaji huo.

 Aidha Ngobei amesema uharibifu uliofanyika katika sehemu ya eneo la ghala la kuifadhia chakula ni kwa sababu eneo hilo ndilo walilo litumia kama chumba cha kumuhifadhi mmoja kati ya jamii hiyo ya wafugaji walio mkamata wakati wa ghasia hizo.

Utoroshwaji wa mifugo kupitia wilaya ya longido kupelekwa nchini Kenya umekuwa ukifanyika mara kwa mara na hivyo wizira ya mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na serikali ya kijiji, kata pamoja na tarafa wameungana kwa pamoja kuhakikisha swala hilo linafikia tamati.

Ushirikina Njombe wawatesa walimu mashuleni

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Imani za kishirikina mkoani njombe zimetajwa kuwa ndio chanzo cha walimu kukaa kwa muda mfupi katika vituo vya kazi pamoja na wanafunzi  kutokufika mashuleni (utoro).

Aidha imeelezwa kuwa kutokana na uwepo wa imani za kishirikina kwa baadhi ya shule zilipo pembezoni mwa mji inapelekea wanafunzi kufanya vibaya katika masomo yao hali ambayo ina athiri kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.

Hayo yamebanishwa na afisa elimu kata ya mlowa Nitson Damian Mkate halmashauri ya mji wa makambako mkoani njombe wakati akizungumza na mtandao huu mara baada ya kuisha kwa mkutano wa hadhara katika mtaa wa Idofi , amesema kuwa katika kata hiyo kuna mtoto ambaye ameshindwa kuendelea na masomo kutokana na kila anapotaka kwenda shuleni anapatwa na tatizo la kuvimba usoni.

“Ni kweli ushirikina upo lakini ni tofauti na miaka ya nyuma kwa mfano mwaka jana mwalimu mkuu wa shule ya msingi Idofi alichukua walimu wa kujitolea kutoka Lungemba akawaleta hapa lakini usiku walikutana na sintofahamu ambayo hawakujua ni nini,walilala na suruali wakaamka asubuhi suruali zipo nje wengine walilalia mito wakamka asubuhi wakaona mito ina damu lakini hakuna mchubuko wa aina yoyote”alisema afisa elimu

Rajab Shomari ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi idofi amesema licha ya tabia hizo za kishirikina kupungua kwa kiasi kikubwa ikiwa nitofauti na miaka ya nyuma bado kuna tatizo hilo kwa baadhi ya watoto wanao jihusisha na vitendo hivyo pamoja na wazazi.

“Kuna watoto ambao wana tabia hizo na kuna wazazi ambao pia wanatabia hivyo,kwa miaka ya nyuma kulikuwa na asilimia kubwa sana lakini kwa sasa kutokana na kukemea kemea vitendo hivi vimepungua,kwa upande wa wanafunzi mtoto anaweza akaanguka chini anapoulizwa katika hali ile anataja baadhi ya watu wanaofanya vitendo hivyo sasa inakuwa ngumu kuthibitisha lakini huwa inakuwa hivyo”alisema Shomari

Festo Mwalongo ni diwani wa kata hiyo ya mlowa amesema kuwa imani za kishirikina hazipo katani kwake pekee bali zipo kila mahali ambazo zinasababishwa na uelewa mdogo kwa baadhi ya jamii na kuwataka walimu waendelee kumtumikia Mungu.

“Habari ya ushirikina sio inaanzia kwenye kata ya Mlowa,sasa hawa watu wachache wanao jihusisha ni kwa kukosa elimu,sasa hivi watu wengi  wana nguvu ya Mungu itafika mahala hawa washirikina wataenda nyumba nyingine watateketea kwa moto,sasa sihitaji wakafika mahala wakaanza kutaabika, pamoja na ushirikina huo wawaone wachungaji ili wateketeze huo ushirikina wao”alisema Diwani

Wananchi wa mtaa huo wameitaka serikali kufanyia kazi malalamiko yanayotolewa na wananchi hao juu ya uwepo wa imani hizo za kishirikina kwa kuwa zimepelekea kudidimiza shughuli za kimaendeleo katika mtaa huo.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba Aitaka TPRI Kuongeza Juhudi Katika Udhibiti Wa Viuatilifu

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha 220919
Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa viuatilifu ukanda wa Kitropiki-TPRI imekuwa kitovu cha kuunda mifumo mizuri inayosimamia na kudhibiti Biashara ya Viuatilifu.  
 
Zipo baadhi ya nchi za Afika kusini mwa Jangwa la sahara ambazo bado hazijatengeneza mifumo mizuri ya Kisheria na sera za kusimamia biashara za viuatilifu.
 
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba ameyasema hayo leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha wakati akifungua kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI.
 
Mhe Mgumba ameipongeza Taasisi hiyo ya TPRI kwa kushirikiana na wadau wengine kwa kuandaa kongamano hilo Kwani ni sehemu ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali ili waweze kuhakikisha kuwa Visumbufu (Pests) haviwi kikwazo  katika kutimiza azma ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya Viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
 
Alisema kuwa umuhimu wa viuatilifu katika kuzalisha mazao ni jambo la wazi na muhimu katika nchi za Ukanda wa kusini mwa Afrika na maeneo mengine duniani hivyo kongamano hilo litakuwa chachu na taswira chanya katika maendeleo ya kilimo nchini.
 
Alisema matumizi ya viuatilifu kwa tafsiri ya wengi ni kupata mazao mengi na hivyo mapato ya kutosha na kupata uhakika wa chakula. “Suala la madhara ya viuatilifu hivi kwa afya ya binadamu na uchafuzi wa mazingira wengi hawalipi kipaumbele na hawaoni kwamba ni tatizo. Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale ambapo wengi wanatumia viuatilifu bila kuzingatia maelekezo ya watengenezaji” Alikaririwa Mhe Hasunga
 
Kadhalika alisema, Visumbufu vya mazao husababisha upotevu wa karibia ya  nusu  ya mazao katika Bara la Afrika na nchi zinazoendelea hivyo Bara la Afrika likiwa linakusudia kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya watu wake ambao wanaongezeka kwa kasi, hivyo ni lazima wakulima watumie mbinu mbalimbali za kupambana na visumbufu vya mazao.
 
“Ingawa viuatilifu vimeleta mafanikio makubwa sana duniani katika kupambana na visumbufu vya mazao, visumbufu vya mifugo na binadamu, pia vinasababisha madhara kwa binadamu na mazingira kwa upande mwingine” Alikaririwa Mhe Mgumba
 
Aidha, alisisitiza kuwa katika Bara la Afrika tatizo ni kubwa zaidi kuliko maeneo mengine duniani kutokana na uwepo wa matumizi ya viuatilifu hata vile ambavyo vimepigwa marufuku maeneo mengine duniani hivyo kuhisiwa kusababisha madhara kwa maelfu ya watu wengi.
 
Alisema kuwa matumizi ya viuatilifu au biashara zinazohusiana na viuatilifu zinaweza kusababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji wa viuatilifu au kwa jamii na vile vile kusababisha uchafuzi wa mazingira pale ambapo viuatilifu havijatumika kwa njia zilizo sahihi na salama.
 
Tanzania kuna sheria mbili zinazoongoza katika kusimamia na kudhibiti matumizi sahihi na salama ya viuatilifu.
 
Sheria hizi ni sheria ya  udhibiti wa visumbufu vya mimea Namba 13 ya Mwaka 1997 (Plant Protection Act No. 13 of 1997) na kanuni zake za mwaka 1999. Na sheria ya TPRI (The TPRI Act. No. 18 of  1979).
 
Hata hivyo, Baadhi ya nchi za Kiafrika  zinazotumia viuatilifu kwa wingi na zenye sheria hafifu za kusimamia matumizi ya viuatilifu,  madhara ya viuatilifu ni mengi sana kutokana na usimamizi hafifu na pia kutokuwepo kwa huduma ya upimaji wa madhara ya viuatilifu katika afya ya binadamu.

Mbaroni Kwa Kumbaka Mwanafunzi Mwenye Umri Wa Miaka 16 Na Kisha Kumpa Mimba.

$
0
0
Na Salvatory Ntandu
Mkazi wa kijiji cha Nduku wilayani Kahama mkoani Shinyanga SAMORA MASABI amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Kahama kwa Tuhuma ya kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo EVODIA KYARUZI Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi SHABANI MATESO amedai SAMORA aliteda kosa hilo kati ya Disemba 12 mwaka jana na Januari mwaka huu katika kijiji hicho.

Amesema Mtuhumiwa baada ya kutenda Makosa hayo alitoroka kusiko julikana hadi  alipokamatwa na Jeshi la Polisi Mei 20 mwaka huu na kufikishwa mahakamani leo kujibu Tuhuma zinazo mkabili.

Katika Shauri hilo la Jinai namba 190 la mwaka huu MATESO amesema SAMORA anashitakiwa kwa Makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni la kumbaka Mwanafunzi kinyume na kifungu  130(1)(2) na 131  sura 16 ya sheria ya makosa ya jinai marejeo ya mwaka 2002.

Katika shitaka la pili SAMORA anatuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi huyo kinyume na fungu la  60(A) sura 353 ya  sheria ya elimu namba 2 ya mwaka 2016.

SAMORA amekana mashitaka yote yanayomkabili na Shauri hilo limeahirishwa hadi June 10 mwaka huu litakapotajwa tena Mahakamani na amerudishwa Rumande kwa kukosa dhamana.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images