Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Sikukuu ya Pasaka yamponza Daktari, ashushwa cheo

$
0
0
Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dkt Maulid Madeni amefikia uamuzi wa kumshusha cheo Mkuu wa Kituo cha Afya cha Ngarenaro, Japhet Kivuyo, kwa kosa la kutokuwepo kazini siku ya pasaka kwa kile alichokidai alikuwa mapumzikoni.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Mkurugenzi huyo amesema kitendo kilichofanywa na mkuu huyo wa kituo kilikuwa kinyume na utaratibu wa utendaji kazi.

"Ofisi yangu inafanya uchunguzi na itachukua hatua stahiki, pia tunatoa taarifa kwa umma kuwa tunamvua uongozi Dkt Japhet Kivuyo kuwa Daktari wa kawaida, na nafasi yake itachukuliwa na Daktari David Mng'anya, mwisho tunawaomba radhi wananchi walioathirika kwa hili", amesema Mkurugenzi.

"Siku ile ya tukio ambayo ilikuwa Ijumaa, Daktari yule alitoa majibu ambayo si ya kiuongozi kwa sababu huwezi ukaondoka kwenye kituo cha afya, halafu hujaacha mbadala wowote, halafu unapigiwa simu unatoa majibu kwamba hauwezi kurudi ofisini", ameongeza Mkurugenzi huyo.

Mwishoni wa wiki iliyopita Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilayani Arusha, ilifanya ziara katika Kituo cha Afya cha Ngarenaro na kukuta wagonjwa wakiwa peke yao bila daktari yoyote wa kuwahudumia.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Mwakyembe Apangua Hoja Ya Musukuma Kuhusu Wasanii Kumiliki madanguro na kula fedha za misiba

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema hoja ya mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Musukuma kuwa wasanii nchini wanamiliki madanguro na kula fedha za misiba, si ya kweli.

Dk Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 23, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya wizara hiyo.

Alhamisi iliyopita Aprili 18, 2019 naibu Spika, Dk Tulia Ackson aliitaka Serikali leo kujibu madai ya wasanii wa filamu nchini kumiliki madanguro sambamba na kuchangisha fedha katika misiba na kuzitumia katika mambo mengine.

Suala la wasanii kumiliki madanguro na kutafuna fedha za misiba liliibuliwa na Musukuma katika mjadala huo na kumfanya Dk Tulia kutaka maelezo ya Serikali kwa kuwa kauli hiyo ikiachwa hivyo inaweza kuleta picha mbaya kwa wasanii.

Katika majibu yake Dk Mwakyembe amesema, “Vitendo hivyo havikubaliki kisheria na ni kosa la jinai nimuombe tu Waziri wa Mambo ya Ndani asilichukulie kwa nguvu suala hili (la madanguro na fedha za misiba) maana Musukuma alizungumza tu pengine kutaka kusikika tu.”

Katika maelezo yake ya Alhamisi iliyopita Dk Tulia alisema,“Kuna mchango ulitoka hapa naamini utakapopewa fursa ya kuhitimisha hoja yako utaliweka vizuri zaidi. Umekuja mchango kuhusu wasanii kuwa ndio wamiliki wa madanguro mengi Dar es Salaam.”

“Nadhani hili uliweke sawa halitakuwa jambo jema kama halina ukweli wowote kuwadhalilisha wasanii wetu.”

Kuhusu fedha za misiba, naibu Spika alisema, “ Pia kuna hoja ya ushiriki wa wasanii kwenye misiba kwamba wanakusanya michango na wanaweza kuitumia si kwa makusudi ya

Marekani yatishia kuiwekea Uturuki vikwazo vipya ikinunua mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Urusi

$
0
0
Uhusiano wa Marekani na Uturuki umekumbwa na msuguano mkubwa hasa baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli ya Julai 2016. 

Baada ya Uturuki kusambaratisha mapinduzi hayo, ilisema kuwa Marekani ilihusika katika njama hiyo na kwa msingi huo uhusiano wa nchi hizo mbili uliingia baridi.

Kinyume na matumaini ya wakuu wa Uturuki kuhusu kuboreka uhusiano wa pande mbili katika urais wa Donald Trump, hitilafu za nchi hizo mbili zinaonekana kushadidi.

Moja ya nukta muhimu za hitilafu baina ya Marekani na Uturuki ni sisitizo la wakuu wa Ankara kuhusu kununua mfumo wa makombora ya kujihami angani ya S-400 kutoka Urusi.

Disemba 2017, Uturuki na Urusi zilitiliana saini mapatano ya kununua mfumo huo wa S-400 na punde baada ya hapo Marekani ilianza kuwashinikiza wakuu wa Ankara wabatilishe mkataba huo. 

Hatua ya Uturuki ya kununua silaha hiyo muhimu ya  Urusi si tu kuwa ilipingwa vikali na Bunge la Marekani, Congress, na wizara ya ulinzi ya nchi hiyo, Pentagon, bali pia Washington imesonga mbele na kuchukua hatua za kivitendo kuizuia Uturuki kununu mfumo huo wa kujihami.

Uturuki ni mwanachama wa Muungano wa Kijeshi wa Atlantiki ya Kaskaizni (NATO)  ambao unaongozwa na Marekani na unaoitazama Urusi  kama hasimu wake mkuu.

Kwa msingi huo Marekani imedai kuwa kuingiza mfumo wa S-400  katika mtandao wa kujihami angani wa nchi ya NATO ni jambo ambalo litapelekea Urusi  igundue siri za udhaifu wa ndege za kivita za nchi wanachama wa NATO hasa udhaifu wa ndege ya kivita ya Marekani ya kizazi cha tano ya F-35.
 
Aidha utawala wa Trump una wasiwasi kuwa iwapo Uturuki itanunua silaha za kistratijia za Russia, hatua kwa hatua nchi hiyo itajikurubisha zaidi kwa Moscow.

Pamoja na kuwepo mashinikizo hayo ya Marekani, lakini Uturuki inasisitiza kuwa itanunua mfumo huo wa makombora ya kujihami kutoka Russia.

 Mevlüt Çavuşoğlu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki hivi karibuni aliashiria vitisho hivyo vya Marekani dhidi ya nchi yake na kusema: "Russia na Uturuki zimeshakamilisha mkataba wa mfumo wa S-400 wa makombora na hakuna yeyote anayeweza kuiambia Ankara ichague baina ya Magharibi na Russia."

Marekani imetupilia mbali sababu zilizotolewa na Uturuki kuhusu kununua mfumo wa S-400, na sasa inachukua hatua za kutaka kuilazimisha ibatilishe uamuzi wa kununua silaha hiyo.

Katika hatua ya kwanza, utawala wa Trump umekataa kuikabidhi Uturuki ndege za kizazi cha tano za F-35  mbali na kutoa vitisho vipya dhidi ya Ankara. 

Kwa mujibu wa mapatano, Marekani inapaswa kuikabidhi Uturuki ndege za kivita za F-35 mwaka huu wa 2019.

Marekani pia imetoa tishio la kuondolewa Uturuki katika muungano wa kijeshi wa NATO. 

Mike Pence, Naibu Rais wa Marekani akizungumza Aprili 3 aliitahadahrisha Uturuki kuhusu sisitizo lake la kununua makombora ya S-400 kutoka Russia na kusema: "Uturuki inapaswa kuchagua mawili, ima ibakie NATO au inunue S-400. Tishio hilo lilikabiliwa na jibu kali la wakuu wa Uturuki.
 
Katika tishio jipya dhidi ya Uturuki,  Robert Menendez  ambaye ni seneta wa ngazi za juu wa chama cha Democrats nchini Marekani amesisitiza kuwa, iwapo Uturuki itaendeleza mchakato wa kununua mfumo wa S-400 kutoka Russia, basi Marekani itaiwekea nchi hiyo vikwazo na haitaikabidhi ndege za kivita za F-35.

Kwa mtazamo wake, hatua ya Uturuki ya kununua S-400 ni sawa na kununua zana muhimu ya kijeshi kutoka Russia na jambo hilo litapelekea Ankara ikumbwe na vikwazo vya Marekani. Amesema nchi yoyote itakayonunua silaha kama hiyo ya Russia pia itawekewa vikwazo.

Mendez amesisitiza kuwa: "Hatuwezi kuweka ndege ya kivita ya F-35 pembeni mwa mfumo wa makombora wa S-400 kwani jambo hilo litapelekea siri za F-35 kugundulika.

Mwanamke Auawa Katika Harakati za Kutaka Kubakwa

$
0
0
Regina Manday (35), aliyekuwa anafanya kazi kwenye shamba la mwekezaji Rift Wall Plantation Kijiji cha Magara Halmashauri ya Babati, ameuawa katika harakati za kubakwa.

Taarifa ya mama huyo kuuawa ilitolewa mwishoni mwa wiki na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Augustino Senga, na kusema tukio hilo lilitokea Aprili 15, mwaka huu saa 1:00 usiku,  baada ya kupigwa mweleka na kuanguka chini.

Kamanda Senga alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo ni Claud Swedi maarufu kama Claud Safari (35), mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Moya, na amekamatwa.

“Chanzo cha mauaji haya marehemu alikuwa anakwenda kulala kambini kutokana na kufanyakazi za kibarua… wakati anapita maeneo ya korongoni kwenye  mto, ndipo alipigwa mtama na kuangukia kisogo na kufariki dunia,” alisema Senga.

Spika Ndugai Ataka Walimu wa Sayansi Wapewe Kipaumbele Wakati wa Kutoa Ajira

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Spika wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai ameishauri Serikali  kuwa na mpango wa kutoa kipaumbele cha kwanza katika kuajiri walimu wa  Masomo ya Sayansi  ili kupunguza uhaba wa walimu hao hapa nchini.
 
Mhe.Ndugai ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akitoa mchango wa nyongeza  baada ya Mbunge wa Buhigwe Mhe.Albert Obama aliyehoji mpango wa Serikali kuongeza walimu wa Masomo ya Sayansi.
 
Mhe.Ndugai katika Msisitizo wake amesema kuna baadhi ya shule katika jimbo lake  unakuta kuna mwalimu mmoja tu wa Masomo ya Sayansi hususan somo la hesabu hivyo kuna haja ya serikali katika awamu nyingine ya ajira ikaajiri walimu pekee wa Masomo ya Sayansi hata kama ni elfu nne huku Mbunge wa Buhigwe Alrbert Obama  Ntabaliba akihoji pia juu ya kuongeza vifaa vya Maabara.
 
Akijibu Maswali hayo,Naibu Waziri wa  nchi,Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa Mwita Waitara amesema serikali inafanya mchakato wa kuajiri zaidi ya walimu elfu nne kwa kuzingatia maeneo yenye upungufu zaidi na awamu ya pili  ya kutoa ajira serikali itazingatia maeneo yenye mapungufu zaidi  walimu wa Masomo ya Sayansi.
 
Hata hivyo Naibu Waziri,Waitara amesema kwa mwaka wa fedha 2018/2019  serikali inatarajia kununua na kusambaza vifaa  vya Maabara katika  shule za sekondari 1250 zilizokamilisha vyumba vya maabara hapa nchini.

Profesa Lipumba Amkumbuka Kikwete....Aitaka Serikali Iruhusu IMF Ichapishe Ripoti ya Hali ya Uchumi wa Tanzania

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Civic Union Front (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba,  amesema kitendo cha serikali kukataa taarifa ya Shirika la Fedha  Duniani (IMF) isichapishwe ni sawa na serikali kujipiga risasi yenyewe kwani maswali ni mengi yanayohusu kwa nini serikali inazuia taarifa hizo kuchapishwa.
 
Prof. Lipumba amesema hayo katika mkutano wake na wanahabari leo Aprili 23, ambapo amebainisha kuwa kuzuiwa kwa ripoti hiyo kutazorotesha mahusiano ya taifa na shirika hilo na kudai kuwa wakati wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete hakukuwepo na zuio lolote.

“Ni vyema taarifa ya Shirika la Fedha la Dunia (IMF) ikachapishwa ili wabunge wakaisoma na kama kuna mapungufu wakasema ni wapi kuna mapungufu ili irekebishwe. Riba za mikopo katika mabenki bado ziko juu sana, hii inapunguza kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

“Namshauri Waziri wa Fedha, Dkt. Mpango aruhusu taarifa hiyo ichapishwe ili Watanzania na wabunge waisome na kama kuna matatizo serikali inaweza ikatoa msimamo wake. 


"Huenda katika taarifa yao, IMF wanatoa sababu za kwa nini uchumi wa Tanzania utaporomoka, ni vyema serikali ikaruhusu huu uchambuzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa ili tujue watu wengine wanatazamaje uchumi wetu na kama kuna ubovu basi turekebishe.

“Rais Jakaya Kikwete aliendeleza mahusiano mazuri na IMF, japo watu walikuwa wanamsema kuwa ni mzee wa kutembea nchi za nje lakini IMF waliweza kuja kufanya mkutano mkubwa hapa kwetu mwaka 2009. 


"Wakati huu tunaojadili bajeti bungeni ni vizuri ripoti ya uchambuzi wa IMF ichapishwe ili wabunge wapate kuisoma na kujua kama sera zetu zinakidhi mahitaji ya maendeleo ya uchumi wetu au la!

“Katika utawala huu kumekuwa hakuna programu yoyote ya Shirika la Kimataifa, programu ya mwisho ilikuwa mwaka 2014 wakati Rais alikuwa Jakaya Kikwete. Unapokuwa hauna programu kubwa za kimataifa kama hii ya IMF, wale wanaotaka kukukopesha wanakuwa na mashaka kidogo, na wakitaka kukukopesha wanakupa mikopo yenye riba kubwa.

“Siyo kwamba unalazimishwa kutekeleza jambo fulani, ni suala la uchambuzi wa hali ya kiuchumi, sasa kusema ni suala la ubeberu siyo sahihi kwani mpaka sasa sarafu ya China imeingizwa kwenye kikapu cha IMF,” amesema Lipumba.

 
Aidha wakati hayo yakijiri, Waziri wa Fedha, Dkt. Phillip Mpango amelieleza Bunge leo  April 23, 2019 mjini Dodoma kuwa Serikali iko katika majadiliano na IMF kuhusu ripoti ya Tanzania na kuna siku 14 za kujadiliana kufuatia wataalamu waliotumwa awali kutozingatia hoja za upande wa Serikali kama ulivyo utaratibu.

Serikali Yasema Haijaizuia IMF Kuchapisha Hali ya Uchumi wa Tanzania

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango, amesema Serikali haijalizuia Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuchapisha ripoti ya uchumi wa Tanzania isipokuwa kinachofanyika ni mazungumzo kati ya serikali ya Tanzania na shirika hilo kabla ripoti hiyo haijachapishwa.
 
Dk. Mpango ametoa taarifa hiyo bungeni leo Jumanne aprili 23, alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maelezo ya Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema), aliyesema Serikali imelizuia shirika hilo kutoa ripoti ya uchumi wa Tanzania.

Katika maelezo yake Mwakajoka alipokuwa akichangia makadirio ya bajeti ya Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na  Michezo kwa mwaka wa fedha 2019/20, alisema waandishi wa habari wamejaa hofu ya kuripoti mambo mbalimbali yakiwamo hali ya uchumi wa Tanzania.

Kutokana na hali hiyo alishauri waandishi wa habari waachwe huru ili waripoti mambo mbalimbali kwa maslahi ya umma.

Serikali yatolea ufafanuzi umiliki wa laini za simu zaidi ya moja

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Astashata Nditiye amesema Serikali haijatoa tamko la kupiga marufuku kumiliki laini nyingi za simu badala yake imelenga kuzuia mwananchi mmoja kutumia laini zaidi ya moja, kwa mtandao mmoja.

Naibu Waziri Nditiye ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ambaye alihoji kuhusiana na kauli hiyo iliyotolewa na serikali hivi karibuni.

Mbunge Selasini amehoji kuwa, "Waziri amesema Mei 1, utaanza usajili wa laini za simu kwa alama za vidole, akasema hakuna kumiliki laini 2 mpaka uruhusiwe, haudhani mtawatesa wananchi kwa maeneo ambayo mitandao mingine haipatikani?".

Akijibu swali hilo ndani ya Bunge Naibu Waziri amesema kuwa, "nilichosema ninatamani kila mtanzania awe na laini moja kwaa kila mtandao, akitaka laini nyingine aseme tu, tunaepuka utitiri wa laini nyingi, mfano ' Zile laini za tuma kwa namba hii ni laini zisizo na tija'".

==>>Msikilize hapo chini

Kufanya vibaya kwa Serengeti Boys, Waziri Mwakyembe awalaumu mawakala

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amedai miongoni mwa sababu za timu ya Serengeti Boys kufanya vibaya ni baadhi ya Mawakala wa wachezaji wa nchi za nje kuwaahidi baadhi ya wachezaji kiasi kikubwa cha pesa na kutakiwa timu kubwa.

Mwakyembe alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia wakati wa mjadala wa Wizara hiyo aliyehoji kitendo cha Serengeti Boys kutofanya vizuri kwenye michuano ya AFCON chini ya miaka 17 kwa kuambuliwa kichapo katika mechi zote tatu walizocheza na kutupwa nje ya michuano.

Akihoji suala hilo Mbunge Mkamia amesema kuwa, "huwezi ukaandaa mashindano ukashika nafasi ya mwisho hata Korea aliishia robo fainali, nilishangazwa pale kamati ilipotangaza wakichukua ubingwa watawapa magari na milioni 20, ni sawa na mtoto wa miaka 8 ana birthday, unamwambia nitakununulia gari, hatukuiandaa timu vizuri hata mashindano waliofanya vizuri yalikuwa ni bonanza."

Akijibu hoja hiyo Waziri Mwakyembe amesema kuwa, "vijana wetu walikuwa na presha ya kuibeba Tanzania, pia nawalaumu Mawakala waliokuja  nchini wakina Diouf, Etoo waliwaambia watoto wadogo tunawahitaji kwenye timu yetu tutakulipa milioni 100, wakawa wanacheza kwa kuangalia zile hela. Baadhi ya  wazazi wakawaambia watoto wao wasicheze watavunjika mguu."


Msikilize gapo chini akiongea

Rais Magufuli Aiongezea muda wa miaka 3 Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameongeza muda wa miaka 3 kwa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iliyokuwa imalize muda wake leo tarehe 23 Aprili, 2019.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa bodi hiyo  wameongezewa muda hadi tarehe 23 Aprili, 2022.

Bodi hiyo inaongozwa na Mwenyekiti, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na wajumbe 6 kama ifuatavyo;
  1.     Bw. Augustine Kungu Olal.
  2.     Bi. Zabein Muhaji Mhita.
  3.     Bw. Richard Rugimbana.
  4.     Bw. Mark Leveri.
  5.     Bw. Ally Hussein Laay.
  6.     Bw. Ibrahim Mussa.

Waziri Mkuu Akagua Ofisi Za Serikali Mtumba

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ofisi mpya za wizara saba katika mji wa Serikali ulioko Mtumba, Dodoma na kusisitiza waweke vibao vya ofisi na kukamilisha mazingira ya nje.

“Kuna wizara hazina majina kwa nje. Hakikisheni majengo yote yanawekwa majina haraka ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wanaokuja huku kutafuta huduma. Kama kuna wizara mbili ziko jirani, pale njia panda wekeni kibao kuonesha majina ya wizara zote mbili. Nia ya Serikaili ni kutoa huduma zote kutokea hapa Mtumba,” amesema.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumanne, Aprili 23, 2019) wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo fupi kwa maafisa wa Serikali waliokuwepo kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara ya nishati ambako ndiko alimalizia ziara yake.

Waziri Mkuu ametembelea wizara saba ambazo ni Maliasili na Utalii; Ofisi ya Rais - TAMISEMI; OWM - Sera, Uratibu na Bunge; Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora; Mifugo na Uvuvi, Ulinzi na JKT na ya mwisho ilikuwani ni Wizara ya Nishati.

“Nimefurahi kukuta Mawaziri, Naibu wao na Makatibu Wakuu pamoja na wakuu wa idara wako huku na kazi zinaendelea, lakini ni lazima nisisitize kwamba idara zinazohamia huku ziwe ni zile zenye kutoa huduma za kila siku kwa wananchi,” amesema.

“Ni lazima tuwaeleze wananchi na wadau wetu ili watambue kwamba Serikali imehamia huku, lakini wakija kutaka huduma wasikute idara inayowahusu iko mjini au wengine wako huku na wengune wako kule.”

Kuhusu miundombinu ya barabara, umeme na TEHAMA, Waziri Mkuu amesema Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma inasimamia kazi hiyo ikiwemo suala la ujenzi wa kituo kikubwa cha afya ambacho kitakuwa na huduma zote kwa viongozi lakini pia pia kitatoa huduma kwa wananchi waishio vijiji vya jirani.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka mawaziri walioko Mtumba wajiandae kwani kuna siku atakwenda kufanya vikao vyake kwenye wizara zao kwa sababu amebaini kuwa kila wizara ina ukumbi mkubwa wa mikutano.

Mapema, akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema jumla ya watumishi 64 wameshamia kwenye ofisi za wizara hiyo ambapo kuna vyumba 25 vya ofisi na ukumbi mmoja wa mikutano.

Pia alisema waligawa miche ya miti 13,570 kwa wizara mbalimbali na kwamba katika ofisi yake, wamepanda miti 980.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi (OR-TAMISEMI), Bw. Suleiman Jafo alisema wamekwishahamia tangu Jumatatu iliyopita na kwa sasa wanatumia ofisi za muda ambazo ni za mabati huku wakisimamia ujenzi wa ghorofa yao hadi ukamilike.

Akielezea kuhusu ujenzi wa ofisi hizo ulipofikia, Bw. Jafo alisema ifikapo mwishoni mwa wiki watakuwa wamekamilisha kazi ya kuweka mabati na kupiga plaster. “Tunatarajia kukamilisha kazi ya ujenzi Mei 30, kama ilivyopangwa. Jengo lilikamilika litakuwa na kumbi mbili za mikutano na ofisi za kuchukua watumishi 88,” alisema.

Naye Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alisema kuwa hadi sasa watumishi 73 kati ya 153 ndiyo wamehamia kwenye ofisi mpya za Mtumba.

Alisema kwa sasa wanatenegeza eneo la maegesho ya magari na wameshatenga eneo la mgahawa kwa ajili ya wafanyakazi wa wizara hiyo.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Serikali Yakusanya Mabilioni Ya Kodi Taulo Za Kike

$
0
0
Serikali imesema kuwa imekusanya Sh. Milioni 3,010.5 kwa mwaka fedha 2016/17 na Sh. Milioni 2,545.6 kwa mwaka wa fedha 2017/18 za     Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika taulo za kike(sanitary pads) zilizozotengenezwa nchini na zilizoingizwa kutoka nje ya nchi.  

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Upendo Peneza (Chadema) aliyetaka kujua Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokusanywa na Serikali katika mwaka wa fedha wa 2016/17 na 20017/18.  

Dkt. Kijaji alisema kiasi hicho cha kodi kilikusanywa kabla ya kuondolewa kwa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)Juni, 2018. 

Katika maswali ya nyongeza, yaliyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Dkt. Immaculate Swale kwa niaba ya Mhe. Peneza, alisema pamoja na Serikali kuondoa baadhi ya kodi katika uzalishaji wa taulo za kike lakini bado bei ya bidhaa hiyo ipo juu, na kutaka kujua mkakati wa Serikali kushusha bei ya bidhaa hiyo ili kuhakikisha inawafikia walengwa.  

“Kama Serikali imeshindwa kusimamia kushuka kwa bei, haioni kwamba iendeleze zile kodi za awali lakini kodi hii ikusanywe na iwe refinance ili kuweza kununulia hizi taulo za kike na izigawe bure mashuleni”, aliongeza Dkt. Swale. 

Akijibu maswali hiyo, Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali haijashindwa kusimamia bei ya bidhaa hizo na kwa sasa inaendelea kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi ili kuona namna bora ya kuwafikia walengwa.  

Alisema Serikali inaendelea kufanya tafiti mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuona namna ya kuwasaidia watoto wa kike ila kuna changamoto kodi inakusanywa ikiwekwa kwa ajili ya kununua na kugawa taulo za kike mashuleni. 

“Yapo makundi mengine ambayo kodi zinazotozwa kwenye bidhaa zinazotumika na makundi hayo, tutatengeneza ombwe la kila kundi kuja kuomba kodi inayotozwa kwenye makundi hayo waweze kupewa wao”, alisema Dkt. Kijaji. 

Aidha, Dkt. Kijaji alishauri kuwa kinachotakiwa kufanywa ni kubuni njia nyingine ili kuona watoto wa kike wanaweza kupata bidhaa hii bila kuhusisha kodi, au tozo zozote zinazotozwa katika bidhaa hii kwasababu imebainika kuwa inapoondolewa kodi wanaonufaika ni wazalishaji kwa kuwa taifa lipo katika soko huria.  

Imetolewa na;
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

Mwakyembe awataka watu waache kumuulizia Azory Gwanda

$
0
0
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewashangaa watu wanaofuatilia mahali alipo mwandishi wa habari Azori Gwanda.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Amesema kwamba pamoja na kwamba watu wengi wanataka kujua alipo Gwanda lazima waelewe kwamba eneo alilopotelea mwandishi huyo walipotea watu wengi wakiwamo viongozi wa Serikali.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo amesema  watu wasiendelee kufuatilia mahali alipo mwandishi huyo kwa kuwa hilo ni suala dhaifu.

Dk Mwakyembe aliyasema hayo bungeni leo alipokuwa alihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/20.

“ Pamoja na hayo Serikali itaendelea kudhibiti watu wanaokiuka utoaji wa maoni kwa kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,”amesema Dk Mwakyembe.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amewataka watu wanaokashifiwa na magazeti wakalalamike mahakamani kwa kuwa ndiko haki inakopatikana.

Hakimu Aagiza Wafuasi 18 wa CHADEMA Wasakwe

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuwasomea maelezo ya awali (PH) washtakiwa 31 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema kutokana na washtakiwa wengine 18 kutofika mahakamani.

 Washitakiwa hao wanakabiliwa na shtaka moja la kufanya mkusanyiko usio halali.

Wakili wa Serikali, Faraji Nguka alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Agustin Rwizile kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusoma maelezo ya awali (PH) lakini kuna washtakiwa ambao waliomba hati za kuwakamata na bado wanaendelea kuwatafuta.

"Tupo tayari kuendelea na hoja za awali licha ya wafuasi 18 kutokuwepo mahakamani, tulishaomba hati za kuwakamata bado tunaendelea kuwatafuta," amedai Faraji Nguka.

Wakili wa kujitegemea, Majura Magafu amedai kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, huwezi kuendelea kama mshtakiwa hayupo mahakamani bila taarifa yoyote ya maandishi.

"Kesi inaruhusiwa kuendelea bila kuwakilishwa kama mshtakiwa atakuwa amewasiliana na wakili wake na kumpa taarifa tena kwa njia ya maandishi" amedai Wakili Magafu.

Wakili wa Utetezi, Alex Massaba amedai licha ya mahakama kutoa hati za kuwakamata washtakiwa, kumekuwa hakuna jitihada zozote za kuwatafuta.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 17,mwaka huu kwa ajili ya kutolea uamuzi kama kesi hiyo iendelee na hoja za awali.

DC Iringa akanusha uwepo wa kiwanda cha kutengeneza Uume Bandia

$
0
0
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Siku chache baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa ameshika viungo bandia vya kiume na kuzua Taharuki katika jamii, Mkuu huyo wa Wilaya ametolea ufafanuzi.

Akizungumza na Wandishi wa habari ofisini kwake leo Kasesela amesema kuwa taarifa zilizosambaa mtandaoni juu ya uzalishaji wa viungo bandia vya kiume, zimeleta changamoto huku akiwataka wananchi  kuondokana na dhana potofu za kuchukua habari za mitandaoni na kuupotosha umma.

“Naomba niendee kuwaomba radhi watanzania kwa ajili ya jambo ambalo lilileta taharuki kwenye mitandao ya kijamii hasa nchi ya jirani zetu hapo Kenya lilipokelewa tofauti na nilivyokuwa hapo awali” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka watanzania kuacha kufuatia mambo ya ajabu na kuyapa nafasi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kupata mambo ya kujenga nchi na yenye tija.

“Jamni ile habari ilitungwa na ni habari ya hovyo sana kwa kuwa nililishwa habari ambayo mimi sijaisema kwenye chombo chochote kile kwenye vyombo vya habari hivyo hiyo habari ni ya kupuuza tu” alisema Kasesela

Kasesela amewashauri watanzania kuhakikisha wanafatilia taarifa zenye kuleta maendeleo na zenye kujenga katika jamii inayomzunguka.

“Kwa sasa habari nyingi ambazo zinazungumzwa hivi sasa ni habari ambazo ni za hovyo hovyo mno ndio maana leo wamesema kuwa wilaya ya Iringa kuna kiwanda hicho kitu ambacho sio kweli” alisema Kasesela

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amelaani kitendo cha Dawson Kagine   kusambaza taarifa zisizo za kweli na kuongeza kuwa mkoani Iringa kuna kiwanda cha kuzalisha vifaa vya elimu ya mapambano dhidi ya Ukimwi.

Utabiri wa Hali ya Hewa: Taarifa Ya Uwepo Wa Mgandamizo Mdogo Wa Hewa Kaskazini Mwa Kisiwa Cha Madagasca.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano April 24

Nafasi za Ajira Katika Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwahimiza Watanzania wenye sifa kuomba fursa ya ajira iliyotangazwa na Sekretarieti ya Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (Organization for the Prohibition of Chemicals Weapons-OPCW) iliyopo The Hague, Uholanzi. 

Nafasi hiyo ni ya Technical Support Officer-P3 ambapo mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 06 Juni 2019.

Wenye sifa zinazohitajika, wanashauriwa kufanya maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya sekretarieti; www.opcw.org

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Rais Magufuli Atanya Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala Wa Meli Tanzania (TASAC)

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images