Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka Bundeni Dodoma

$
0
0
LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka Bundeni Dodoma

Kim Jong Un na Rais wa Urusi Vladmir Putin Kukutana Kesho Alhamisi

$
0
0
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais wa Urusi Vladmir Putin watakutana Alhamisi katika mji wa bandari wa Vladivostok kuujadili mkwamo wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini. 

Mshauri wa siasa za kimataifa  katika Ikulu ya Urusi Yuri Ushakov amewaambia wanahabari katika miezi michache iliyopita hali katika rasi ya Korea imetulia, kwa kiasi kikubwa kutokana na juhudi za Korea Kaskazini za kusitisha majaribio ya makombora na kufunga kituo chake cha kufanyia majiribo ya nyuklia. 

Kwa hiyo Urusi inataka kusaidia kwa njia yoyote ile kuyaendeleza mafanikio hayo. 

Wachambuzi wanasema ziara ya Kim nchini Urusi ni ya kutafuta uungwaji mkono wa mataifa ya kigeni, baada ya kuvunjika kwa mkutano wa pili wa kilele kati ya Marekani na Korea Kaskazini mjini Hanoi Februari mwaka huu.

Rais Magufuli Aondoka Nchini Kwenda Malawi Kwa Ziara Ya Siku Mbili

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Aprili, 2019 ameondoka kwenda nchini Malawi ambapo anatarajiwa kufungua msimu wa Soko la Tumbaku nchini humo.

Putin adai ni mapema mno kupongeza uchaguzi Ukraine

$
0
0
Msemaji wa ikulu ya rais nchini Urusi  Dmitriy Peskov amesema ushirikiano na mchekeshaji Vladimir Zelenskiy, mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Ukraine, unaweza kutathminiwa kulingana na juhudi zake.

Peskov amekumbushia kuwa matokea rasmi hayajatangazwa bado hivyo ni mapema sana kwa rais wa Urusi Vladmir Putin kumpongeza Zelenskiy kama mshindi rasmi wa uchaguzi wa Ukraine

"Ni mapema mno kuzungumza juu ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kumshukuru Zelensky." alisema.

Peskov, akizungumza kuhusu Putin kufanya kazi na Zelenskiy..."Atatathminiwa kulingana na kazi halisi ambayo atafanya." alisema

Peskov pia amesema kuwa Urusi inaheshimu uchaguzi wa Ukraine.

Watatu Wafariki Dunia Baada ya Kufukiwa na kifusi kwenye machimbo ya moram jijini Arusha

$
0
0
Watu watatu wamefariki dunia na wawili wamejeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Mkoa Mount Meru, baada ya kufukiwa na kifusi kwenye machimbo ya Moram inayotumika kwa ajili ya shughuli za ujenzi, yaliyopo eneo la Moivaro Kata ya Moshono.

Tukio hilo limetokea umbari wa Kilometa nane kutoka katikati ya Jiji la Arusha, baada ya mabonge makubwa ya Moram kuporomoka, wakati watu hao wakiwa kwenye shughuli ya uchimbaji.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana, alisema tukio hilo lililotokea jana asubuhi.

Alisema tangu kutokea ajali hiyo vikosi vya uokoaji, kutoka mamlaka za ulinzi na usalama vilikusanyika eneo la tukio na kuendelea na shughuli ya kufukua udongo, kuwatafuta watu waliofukiwa.

“Lakini pia vifaa mbalimbali vya uokoaji viliwasili mara moja ili kufanikisha zoezi la ufukuaji kifusi linaenda kwa haraka na vizuri,” alisema.

Shana alisema watu watatu waliofariki walikuwa wamefunikwa na gema lililobomoka kutoka na mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia siku hiyo na wawili walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Diamond: Zari Alikuwa Akinisaliti kwa Peter wa P Square

$
0
0
Msanii Diamond Platnumz ameeleza kile kilichotokea kati yake na mzazi mwenzie Zari The Bosslady hadi kuachana kwao. .

Muimbaji huyo kwenye kipindi cha Block 89 kupitia Wasafi FM amesema kuwa Zari alikuwa akimsaliti.

"Namheshimu Zari ni mzazi mwenzangu, alikuwa wife material, alikuwa anataoka na Peter wa Psquare, niliwahi kukuta sms nikamuuliza. Alikuwa anachepuka pia na Trainer wake na alikua anamleta hadi kwangu, lakini sijawahi kufunguka"

Ameendelea kwa kueleza kuwa, "Na ukweli sijawahi kuachwa na Mwanamke, Ukizingua nitakupiga matukio utaondoka mwenyewe".

“Mpaka nyumbani kwangu na mpaka picha pia ninazo ila mimi sio mtu wa kujifanya, mimi siongei mpaka naulizwa kwa nini sizungumzi,  na kiukweli licha ya mambo yote hayo labda mimi nilikuwa ni chanzo kwa sababu mimi nilikuwa mwendawazimu kwelikweli na yeye alikuwa ananipenda sana ila mimi nilikuwa nampenda lakini sio kama yeye alivyokuwa ananipenda mimi”.

Wimbo Mpya: Rossa Ree X Timmy T dat - Asante Baba Remix

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Rosa Ree ametuleta video mpya ya wimbo wake uitwao Asante Baba Remix

Video Mpya: Barnaba Classic - Nyang'a Nyang'a

$
0
0
Video Mpya:  Barnaba Classic - Nyang'a Nyang'a

Wimbo Mpya wa Aslay: Nichombeze

$
0
0
Msanii Aslay katoa  video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Nichombeze. Utazame hapo chini

Diamond Ataja Sababu za Kuacha Kuwahudumia Watoto Wake Aliozaa na Zari

$
0
0
Msanii Diamond Platnumz ameeleza kile kinachoendelea kati yake na mzazi mwenzie Zari The Bosslady kuhusu watoto wao.

Muimbaji huyo kwenye kipindi cha Block 89 kupitia Wasafi FM amesema Zari amekuwa akizuia pindi anataka kuwaona watoto wake.

Amesema kila mwezi alikuwa akitoa dola za Marekani 2,000 ambazo ni wastani wa Sh5 milioni kwa ajili ya matunzo ya watoto. 

“Niseme ukweli kabisa, nina kama miezi mitatu hivi sijapeleka fedha za matunzo ya watoto kwa sababu mwenzangu hataki hata niongee na watoto, hebu fikiria hata kupitia mfanyakazi wa ndani amegoma nisiongee nao.

“Nilijaribu kuwasiliana na mtoto wake wa kiume, yule mkubwa  lakini mwenzangu ameniwekea ngumu,” amesema.

Jitihada nyingine anazosema mwenzake amekuwa akizizima ni za kuwaleta watoto nchini akisema amemuwekea masharti kuwa lazima aje nao.

“Zari anataka aje na watoto, mimi nimemwambia mama nina mahusiano mengine nikamshauri mama yangu mzazi awafuate watoto lakini akakataa akasema labda niende kuwaangalia Sauzi (Afrika Kusini),” amesema.


Ameendelea kueleza kuwa, "Kuna kipindi Tiffah alizidisha muda wa kukaa South kwasababu anapassport ya Tanzania, ningekuwa nataka matatizo ningeweza kupiga simu mtoto akarudishwa Tanzania".

Zari Apangua Tuhuma za Kumsaliti Diamond

$
0
0
Mzazi mwenza wa mwanamuziki Diamond Platnumz,  Zari the Boss Lady,  amefunguka baada ya msanii Diamond kuongea mengi kuhusu mahusiano yao yaliyopita ndani ya kituo chake cha redio cha Wasafi FM jana,  April 23, 2019.

Diamond alifunguka mambo mengi ikiwemo Zari kumsaliti kwenye mahusiano, kuhusiana na kutoa sapoti kwa wanaye, na mambo mengine yaliyokuwa yanawahusu walipokuwa kwenye mahusiano.

Zari amejibu kwa kusema; “Sasa yale magoti mpaka Sauzi yalikuwa ya nini? Kule  kuomba msamaha kwote kwa radio kwa nini? Kwani umekuwa comedian sasa? Usinichafulie maisha bro. Yameisha zamani kubali tu. Kiki zimekuwa ngumu mjini. Niheshimu tafadhali nakulelea watoto tena vizuri.

"Mimi sijawahi kuchepuka wakati nipo naye na ninajiapiza kama nimewahi kufanya hivyo basi lolote liwatokee watoto wangu.

“Sasa kama mtu amewahi kuikana damu yake kuna uongo gani mwingine anaweza kuacha kusema? Ni vyema kukiri makosa yako na kuyatumia kukua, bado unayo nafasi,”  Amesema Zari

Mafuriko yaua zaidi ya 51 Afrika Kusini

$
0
0
Mafuriko na mmomonyoko wa udongo umepelekea watu wasiopungua 51 kupoteza maisha katika mkoa wa KwaZulu-Natal, mashariki mwa Afrika Kusini.

Maafa hayo yamesababishwa na mvua kubwa ambazo zinaendelea kunyesha katika mkoa huo tokea siku ya Jumatatu. Mafuriko hayo pia yameharibu maeneo mengi ya makazi pamoja na maelfu ya hekari za ardhi ya kilimo.

Kiwango cha maji kimekuwa kikiongezeka katika mkoa huo na kuwalazimisha baadhi ya wakazi wa viunga vya mji wa Durban ulioko kwenye mkoa huo kuyahama makazi yao.

Ripoti zinasema kuwa miili ya wahanga wa mafuriko hayo inaendelea kuopolewa kutoka kwenye maji ya mafuriko ambayo hadi sasa yamewasababishia wakazi wa maeneo yaliyoathirika maafa na hasara kubwa.

TCRA yawatoa hofu Wananchi Kuhusu Zoezi la Kusajili Upya Line za Simu

Serikali Kuweka Bei Elekezi Ya Pembejeo Za Kilimo

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha pembejeo za kilimo (mbegu, mbolea, viuatilifu na zana za kilimo) zinapatikana kwa wakati na kwa bei nafuu.

Hatua hizo ni pamoja na uagizaji wa pamoja, ruzuku, kufuta au kupunguza tozo na kodi zinazochangia kuongezeka kwa bei ya pembejeo na kufanya tafiti katika mnyororo wa thamani wa mazao.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 24 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Ndanda Mhe Cecil David Mwambe aliyetaka kufahamu kwanini Pembejeo za kilimo ni ghali sana, hivyo wakulima wengi hushindwa kununua na kusababisha kupata mavuno haba na kama Serikali ipo tayari kupunguza au kuweka bei elekezi iliyo nafuu kwa mkulima ili aweze kupata pembejeo za madawa, mbolea na zana za kilimo.

Alisema kuwa Serikali ina utaratibu wa kuweka bei elekezi ya mbolea kupitia Mfumo wa Ununuzi wa pamoja nchini kwa mbolea za kupandia aina ya DAP na kukuzia aina ya Urea. Utaratibu huu unalenga kuhakikisha upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu.

Mhe Mgumba aliongeza kuwa katika jitihada za kuongeza uzalishaji na kipato cha mkulima, Serikali hununua  na kusimamia uthibiti na usambazaji wa viuatilifu vya kupambana na milipuko ya visumbufu vya mazao na mimea kama vile kweleakwelea, viwavijeshi, viwavijeshi vamizi, panya, nzige wekundu na nzi wa matunda.

Kadhalika, ili kumpunguzia mkulima harubu katika uzalishaji na uongezaji thamani ya mazao, Serikali imeendelea kutoa mikopo nafuu ya zana za kilimo kupitia Mfuko wa Taifa wa Pambejeo za Kilimo, Benki ya Maendeleo ya Kilimo na Shirika la Maendeleo la Taifa.

Kwa upande wa mbegu na viuatilifu, Mhe Mgumba alisema kuwaserikali inafanya utafiti wa kubaini gharama za uzalishaji wa mbegu kwa kulinganisha na bei za mbegu zilizopo sasa ambao utaiwezesha Serikali kuamua endapo kuna ulazima wa kuweka bei elekezi.

Aidha, Mhe Mgumba pamoja na hatua hizo, Serikali inahamasisha ujenzi wa viwanda vya mbolea, viuatilifu, zana za kilimo na uwekezaji katika mashamba ya mbegu ili kupunguza gharama za pembejeo hizo.

Serikali Yatoa Tamko Usajili wa Line za Simu Kwa Wasio na Vitambulisho Vya Taifa

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema  vyombo vya dola vitandelea kuimarisha amani na utulivu wa Tanzania ili kuhakikisha shughuli za maendeleo zinazoendelea hivi sasa.

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akitoa hoja kuhusiana na taarifa ya makadirio ya bajeti kwa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020, ambapo amesema atahakikisha amani inalindwa.

"Wizara itaendelea kulinda amani na usalama wa nchi hii kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wadau wengine, kuwepo kwa utulivu ambao watanzania wanauona utaendelea kuwezeshwa na hakika shughuli za maendeleo zitaendelea kuimarika." amesema Kangi

Aidha kuhusiana na zoezi la usajili walaini kupitia vitambulisho vya taifa, Waziri Lugola amesema watanzania milioni 16 ambao wana namba za vitambulisho vya NIDA wana sifa za kusajili kadi za simu ya mkononi   na wasio na vitambulisho hivyo watawekewa utaratibu maalum.

“Mtanzania huyu tutampa utaratibu kwa sababu si kosa lake kutosajiliwa simu kwa sababu Serikali tupo kwa ajili ya kuwalinda Watanzania.

“Watanzania hawapaswi kuwa na maisha ya wasiwasi, lazima waendelee kutumia simu kuanzia anainunua mpaka pale atakapoacha kuitumia. Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa) tulikuwa na lengo la kutambua na kutoa vitambulisho milioni 24.5, hayo ndiyo malengo.

“Lakini mpaka sasa Nida tumekwishafanya utambuzi, usajili wa Watanzania wenye sifa milioni 16, tulipoona kwamba wenzetu wa TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania)  wanataka kubadilisha masuala ya kusajili simu ili waweze kutumia alama za vidole na kwamba mwenye kitambulisho cha taifa ndio atakayesajiliwa,sisi kupitia Nida tuliweka utaratibu.

 “Watanzania  ambao wamekwishapata vitambulisho watatumia  vitambulisho vyao. Watanzania milioni 16 tayari wameshapatiwa namba inaitwa NIN yaani National Identification Number, kwa hiyo namba hiyo ambayo anasubiri apewe kitambulisho chake ndiyo atakayoiwasilisha NIDA,” amesema.

Lugola amesema namba hiyo itawasilishwa TCRA na mhusika ataitumia kusajiliwa.

Tahadhari ya Kimbunga Kikubwa Nchini Tanzania

$
0
0
Taarifa hii inatoa mrejeo wa mwenendo wa mgandamizo mdogo wa hewa uliopewa jina la “Kenneth” katika bahari ya Hindi na athari zake kwa maeneo mbalimbali hapa nchini.

Katika kipindi cha saa 24 zilizopita, mgandamizo mdogo wa hewa (Kenneth) umeendelea kuimarika kwa kasi hadi kufikia kiwango cha kimbunga kamili. 

Kimbunga Kenneth kwa sasa kipo umbali wa takribani kilometa 700 mashariki mwa Mtwara. Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kimbunga Kenneth kilichopo eneo la kaskazini magharibi mwa kisiwa cha Madagascar kinaambatana na mvua kubwa na upepo mkali katika eneo hilo.

 Aidha, vipindi vya upepo mkali unaofikia na kuzidi kasi ya kilometa 80 kwa saa vinatarajiwa kujitokeza katika ukanda wa pwani ya kusini (Lindi na Mtwara). 

Kimbunga hicho kinaendelea kutawala mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini, hivyo kusababisha ongezeko la mvua zinazoambatana na ngurumo za radi pamoja na upepo mkali kadri kinavyokaribia maeneo ya ukanda wa pwani.

Kimbunga hiki kitakapoingia nchi kavu kikiwa na nguvu inayotarajiwa kitakuwa na madhara makubwa kwa maisha ya watu na mali zao. 

Madhara yanayotarajiwa ni pamoja na mtawanyiko mkubwa wa mafuriko, uharibifu wa mali na makazi, kuezuliwa mapaa kutokana na upepo mkali, uharibifu wa mazao mashambani, miundombinu kutokana na mafuriko na upepo mkali, kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari katika kipindi kifupi (storm surge), kuathirika kwa shughuli za usafirishaji kwa njia ya anga, kwenye maji na nchi kavu inaweza kuathirika hasa katika mkoa wa Mtwara na maeneo jirani (umbali wa kilometa 500).

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania inaendelea kufuatilia mwenendo wa kujengeka kwa kimbunga hicho kusini magharibi mwa bahari ya Hindi pamoja na mwenendo wa mifumo mingine ya hali ya hewa kwa ujumla na itaendelea kutoa taarifa za mrejeo kila itakapobidi.

USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kuzingatia tahadhari zilizotolewa na mirejeo yake pamoja na kupata na kuzingatia ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Imetolewa na:
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Wizara ya Mambo ya Ndani Yaliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya Sh. Bilioni 921.2

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Ndani imeliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya Sh 921.2 bilioni mwaka wa fedha 2019/2020.

Kati ya fedha hizo, Sh889.3 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida,Sh372.2 bilioni kwa ajili ya matumizi mengineyo na ShSh517 bilioni za mishahara.

Fedha za miradi ya maendeleo ni Sh 31bilioni na kati ya fedha hizo za maendeleo, Sh21.5 bilioni ni fedha za ndani na Sh10.4 bilioni ni fedha za nje.

Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni leo Jumatano Aprili 24, Waziri wa Wizara ya Mmabo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema vipaumbele vya bajeti hiyo ni kudumisha usalama wa raia na mali zao kwa kufanya doria, misako na operesheni mbalimbali.

Vingine ni kuboresha mazingira ya ofisi na makazi ya askari na watumishi raia na kuwaongezea ujuzi watumishi raia na askari kwa kuwapa mafunzo ya ndani na nje ya nchi.

Lugola amesema vipaumbele vingine ni kuendelea kutekeleza mkakati wa jeshi la magereza wa kujitosheleza kwa chakula, kuendelea kupunguza msongamano wa wafungwa na mahabusu kwa kuimarisha utendaji wa shirika la uzalishaji mali la jeshi hilo

Serikali Yawajaza Mapesa Bilioni 688 Wakandarasi Wa Mradi Wa Umeme Wa Rufiji

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Ni tukio la kihistoria ambapo leo, Aprili 24, 2019,  Serikali ya Tanzania, imetoa  dola za Marekani milioni 309.65, sawa na takriban shilingi bilioni 688.65, fedha zake za ndani,  kama malipo ya awali kwa Mkandarasi - Arab Contractors ya Misri, wanaojenga mradi wa kuzalisha umeme unaotokana na maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, mkoani Pwani.

"Haijapata kutokea katika historia ya nchi hii Serikali kutoa fedha nyingi za malipo ya awali ya kiasi kama hiki cha shilingi bilioni 688.65 katika mradi wa aina yoyote uliowahi kutekelezwa hapa nchini isipokuwa huu" alisema Bw. Doto James, Katibu Mkuu  Wizara ya Fedha na Mipango.

Bw, Doto James, ambaye pia ndiye Mlipaji Mkuu wa Serikali, alimkabidhi  hundi kifani ya dola za Marekani milioni 309.65, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, ambaye alimkabidhi hundi hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ugavi wa Umeme nchini-TANESCO, Dkt. Alexender Kyaruzi, ambaye pia alimkabidhi hundi hiyo  Naibu Mkurugenzi wa Ujenzi wa mradi huo Mhandisi Mohamed Hassan, kwa niaba ya kampuni za Arab Contractors (Osman A. Osman & Co na Elsewedy Electric S.A.E (AC-EE JV).

Alisema kuwa kiasi kilichotolewa cha shilingi bilioni 688.65 ni sawa na asilimia 70 ya zaidi ya shilingi trilioni 1 ya malipo ya awali yanayotakiwa kutolewa ya asilimia 15  ya mradi huo ambao hadi kukamilika kwake ndani ya miaka mitatu ijayo, unakadiriwa utagharimu zaidi ya shilingi trilioni 6.6.

Bw. James amezitaja baadhi ya faida za mradi huo utakapo kamilika na kuzalisha megawati 2,115 za umeme kuwa ni pamoja na nchi kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika, kuongezeka kwa uwekezaji katika sekta ya viwanda vitakavyo chochea uzalishaji wa bidhaa,  ajira pamoja na upatikanaji wa maji ya uhakika katika maeneo yanayozunguka mradi na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

"Ninamtaka Mkandarasi akamilishe mradi huu kwa wakati na kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba ili mradi utakapo kamilika uwe kichocheo muhimu cha kuiwezesha Tanzania kufikia azma yake ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025" alisisitiza Bw. Doto James

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamisi Mwinyimvua,  alifafanua kuwa kwa mujibu wa kifungu Na. 14.2 cha Mkataba, malipo ya awali ya Mkandarasi ni asilimia 15 ambazo zimegawanywa katika sehemu mbili ambapo asilimia 70 zinalipwa kwa kutumia sarafu ya kigeni (dola za Marekani 309.645m) na asilimia 30 zitalipwa kwa fedha za ndani ambazo zitalipwa baada ya Mkandarasi kukamilisha taratibu za kimkataba zinazohusu malipo hayo.

"Ninao uhakika kwamba malipo haya ya awali yatamwezesha Mkandarasi kukamilisha taratibu za kupeleka vifaa katika eneo la mradi na kuanza ujenzi mara moja kwa mujibu wa Mkataba.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Dkt. Alexender Kyaruzi, alisema uzalishaji wa umeme hapa nchini umefikia megawati 1600 na kwamba kuongezeka kwa megawati nyingine 2,115 ni hatua kubwa na ya furaha na amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kutekeleza mradi huo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi huo Mhandisi Mohamed Hassan ameishukuru Serikali na wananchi kwa ushirikiano mkubwa wanaoupata na amewahakikishia watanzania kwamba mradi huo utatekelezwa kwa haraka na kwa viwango ili kutimiza matarajio ya nchi ambayo ni maendeleo.

Kikosi Kazi Cha CARD Tanzania Chaagizwa Kukamilisha Mpango Kazi Wa Kuendeleza Zao La Mpunga Kabla Ya Juni 2019

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro
Kikosi Kazi cha CARD kwa kushirikiana na Mshauri wa CARD, kimeagizwa kuandaa rasimu ya awali ya mkakati wa kuendeleza zao la mpunga nchini mapema kabla ya June, 2019.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe leo tarehe 24 Aprili 2019 wakati wa kikao cha kazi cha maandalizi ya uandaaji wa Mpango mkakati wa pili wa kuendeleza uzalishaji wa zao la Mpunga nchini (National Rice Development Stratergy II - NRDS II) kilichofanyika katika Hoteli ya Edema Mkoani Morogoro.

Alisema kuwa ili kikamilishe hiyo kazi lazima kuwe na takwimu sahihi zinazoonyesha hali halisi ya uzalishaji wa mpunga nchini. ” Ni lazima kutoa takwimu zenye uhakika zitakazowezesha mpango wa pili wa kuendeleza zao la mpunga kukamilika ipasavyo, Timizeni wajibu wenu mliopewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais wetu mpendwa, Mhe Dr. John Pombe Joseph Magufuli” Alikaririwa Mhandisi Mtigumwe

Alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa takwimu hizo kikosi kazi hicho kitaanza kuandika rasimu ya mpango mkakati wa kuendeleza zao la mpunga, awamu ya pili kwa kuzingatia kuwa CARD wameazimia kuongeza uzalishaji mara mbili zaidi hivyo Tanzania inapaswa kuzalisha mara mbili zaidi ya mwaka jana.

Alilitaja lengo kuu la Mpango Mkakati wa Tanzania katika uzalishaji wa zao la Mpunga nchini, kuwa litakuwa ni kuzalisha kutoka tani 2,219,628 za sasa na kufikia tani 4,500,000 ifikapo mwaka 2030.

Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Mpango mkakati wa kuendeleza zao la Mpunga unaandaliwa kwa kushirikiana na "Coallition for African Rice Development" (CARD), ambapo makao makuu yake yako Nairobi, nchini KENYA. Tanzania ni moja kati ya chi 32 ambazo ni wanachama.

Pamoja na CARD kumaliza kipindi cha awamu ya kwanza, mwaka 2018, nchi wanachama pamoja na wafadhili walikutana Octoba 2018 huko Tokyo, Japan ambapo walifanya tathmini ya awamu ya kwanza na ilionyesha kuwa lengo lilifikiwa.

Aidha, walikubaliana kuanzisha awamu ya pili ya CARD, kuanzia 2018 hadi 2030. Awamu hii inatarajiwa kuzinduliwa nchini Japan, mwezi wa Agosti, 2019. Moja ya jambo muhimu na linalozingatiwa ili kila nchi ipate nafasi ya kupata miradi itakayonufaika na CARD, ni kuwa na Mpango Mkakati wa Kuendeleza zao la Mpunga Awamu ya Pili (2018-2030). Lengo kuu la CARD, awamu ya pili ni kuongeza uzalishaji wa mpunga kutoka tani 28 milioni (zilizofikiwa katika awamu ya kwanza mwaka 2018) hadi tani 56 milioni mwaka 2030 kwa nchi zote wanachama.

Mtigumwe alisema kuwa kama ilivyofanyika kwa nchi nyingine, na kwa kuzingatia kwamba zao la mpunga ni mojawapo ya zao muhimu la chakula na biashara linalozalishwa takribani mikoa yote hapa nchini, mwaka 2008 Wizara ya Kilimo iliandaa pia Mpango Mkakati wa Kuendeleza zao la Mpunga (NRDS I). Mpango huo ulikuwa ni wa miaka 10 na ulikamilika mwaka 2018 ambapo ulitoa matokeo chanya ikiwemo kuongezeka kwa uzalishaji wa mpunga kutoka tani 899,000 mwaka 2008 hadi tani 2,219,628 mwaka 2018.
 
CARD ni Muungano wa Wabia ambao hupokea maandiko mbalimbali ya miradi ya uzalishaji na usindikaji wa mpunga  na kuyatafutia fedha  kwa ajili ya utekelezaji, na huongozwa na Sekretariati ya CARD, iliyoundwa na Wabia wanachama. Hadi sasa kuna Wabia 23. Miongoni mwa Wabia hao, kama alivyokwishawataja Mkurugenzi ni JICA, Benki Kuu ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika na wengineo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images