Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Laini za simu kusajiliwa upya nchini kuanzia Mei Mosi mwaka huu

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na watoa huduma za mawasiliano ya simu wanakutangazia kuwa, kuanzia Tarehe 1 MEI, 2019 watumiaji wote wa simu za mkononi ambao hawajasajili laini zao kwa kutumia mfumo wa alama za vidole wanatakiwa kusajili UPYA laini zao.

Viongozi saba wa Vyama vya Upinzani Wanazungumza Muda Huu....Tazama Hapa

$
0
0
Viongozi saba wa Vyama vya Upinzani ambavyo ni CHADEMA, NCCR-Mageuzi, ACT-wazalendo,CHAUMA, DP, CCK na UPDP wanazungumza na waandishi wa habari muda huu

==>>Tazama hapo chini

Msimu Wa Tatu Wa “Smirnoff Ice Black Dj Search” Wamalizika, Washindi Wajizolea Zawadi

$
0
0
Dar es Salaam. Aprili 14, 2019. Hatimaye msimu wa tatu wa wa shindano la ‘Smirnoff Ice Black Dj Search’ kwa mwaka 2019 umemalizika huku DJ KG akiibuka mshindi kwa kuwapiku maDj sita walioshiriki kwenye fainali hizo.
 
DJ KG kutoka Mkoa Dar es Salaam alitangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa shindano hilo ambapo jumla ya maDJ sita walishiriki na kudhaminiwa na kinywaji cha Smirnoff Ice Black kinachozalishwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).
 
Akizungumza wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbu wa Life Park Mwenge, Meneja wa bidhaa wa SBL Ester Raphael alisema lengo ni kuibua vipaji vipya kweye tasnia ya muziki kupitia fani ya uburudishaji ‘DJ’ sanjari na kutoa hamasa kwa wateja wa bidhaa zao.
 
“Tunaamini kwa kupitia shindano hili, SBL itatoa msisimko kwa wateja wake na muziki mzuri na nafasi ya kipekee kuonyesha uwezo wa MaDj wanaochipukia,” alisema
 
Shindano hilo limefanyika katika mikoa mitano ikiwamo Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Mwanza na Arusha ambapo waliweza kuwapata maDj sita waliotinga hatua ya fainali.
 
Alitaja zawadi zinazotolewa kwa washindi ikiwamo vifaa vya Dj “Dj Kit,Laptop pamoja na Conrollers kwa washindi watatu.
 
“Ushindani wa msimu huu ni mkubwa sana na tumeona Madj wakipamana kwa hali na mali na hamasa imekuwa kubwa sana kwao na kwa wateja wa kinywaji chetu cha Smirnoff Ice Black,” alisema
 
Katika fainali hizo, DJ KG kutoka Mkoa wa Dar es Salaam aliibuka mshindi wa kwanza na kuibuka na DJ kits pamoja na Laptop (Mac). Mmoja wa Majaji, Immanuel John ‘DJ Summer Tz’ alisema walizingatia zaidi ujuzi wa DJ pamoja na muitiko kutoka kwa watu wanaowasikiliza.

World Bank Launches Human Capital Plan to Propel Investment in Africa’s People

$
0
0
WASHINGTON, April 11, 2019– The World Bank unveiled a new plan today to help African countries strengthen their human capital. The objective of the plan is to enable Africa’s young people to grow up with optimal health and equipped with the right skills to compete in the digitizing global economy.

Sub-Saharan Africa scores the lowest of all the world’s regions on the World Bank’s Human Capital Index, a measurement of how well countries invest in the next generation of workers.  The score is explained by high mortality and stunting rates in the region, as well as inadequate student learning outcomes – all of which have a direct effect on economic productivity.

In an effort to help countries turn these indicators around, the World Bank’s Africa Human Capital Plan is setting ambitious targets to be achieved in the region by 2023. These include a drastic reduction in child mortality to save 4 million lives, averting stunting among 11 million children, and increasing learning outcomes for girls and boys in school by 20%. These achievements can raise Africa’s Human Capital Index score upwards to increase the productivity of future workers by 13%.

“Preventing a child from fulfilling his or her potential is not only fundamentally unjust, but it also limits the growth potential of economies whose future workers are held back. GDP per worker in Sub-Saharan Africa could be 2.5 times higher if everyone were healthy and enjoyed a good education from pre-school to secondary school,” says World Bank Vice President for Africa Hafez Ghanem at the launch of the Bank’s Plan during the World Bank-IMF Spring Meetings.

The Plan also aims at empowering women to prevent early marriage and pregnancy for adolescent girls.   “The adolescent fertility rate in Sub-Saharan Africa is 102 births per 1,000 girls—three times as high as in South Asia. This not only damaging for girls and their children, but it also hurts economic growth,” noted Ghanem.

The World Bank will increase its investments in human capital in Africa by 50% in the next funding cycle. This includes new World Bank grants and concessional finance for human capital projects in Africa totaling $15 billion in fiscal years 2021-2023.  The World Bank will invest these funds strategically to unblock structural constraints to human capital development. The World Bank will also target game changing interventions that leverage technology and innovation and that prevent and reverse damage to human capital in fragile and conflict-affected settings.

The World Bank is already supporting countries to come up with new strategies to invest more and better in their people. Twenty-three African countries, covering over 60% of the region’s population, have joined a coalition of nearly 60 countries to join the Human Capital Project, committing to a set of accelerated investments in their human capital.

“Human Capital Project countries are breaking away from traditional paradigms to make investment in their people a priority and are working in a more coordinated way across government to ensure that households have the right enabling environment to support human capital formation,” said Annette Dixon, World Bank Vice President for Human Development.

UK Government and UNHCR extend a lifeline to 300,000 refugees in Tanzania

$
0
0
Dar es Salaam, United Republic of Tanzania, 15 April 2019– UNHCR, the UN Refugee Agency, welcomed a generous contribution of £5 million (USD 6,385,696) from the UK Government through its Department for International Development (DFID). This financial contribution will support more than 300,000 refugees and asylum-seekers hosted the Kigoma region in northwestern Tanzania.
 
The donation will help ensure continued access to much-needed services including health, education and water and sanitation for Burundian and Congolese refugees and asylum-seekers. Funds will also be used to provide access to alternative energy sources and to support environmental initiatives in the refugee hosting region.
 
“This additional funding from the UK Government represents part of our ongoing commitment to supporting the Government of Tanzania host refugees seeking refuge due to instability in neighboring countries,” stated Beth Arthy, Head of UK DFID Tanzania. “Alongside this support, we continue to invest significantly in the Kigoma region, supporting host community schools, infrastructure and the development of businesses in the region, as well as supporting refugees reintegrate back into Burundi should they choose to return.”
 
UNHCR’s Representative in Tanzania, Chansa Kapaya, praised UK Government’s collaboration with UNHCR, noting, “The allocated funds will greatly support UNHCR’s effort in responding to protection and basic needs of 300,000 refugee and asylum-seekers in Tanzania in 2019. I wish to express my sincere appreciation to the government of the United Kingdom for its continued support to UNHCR, especially the Tanzania operation.”
 
UNHCR and UK DFID have a long track record of cooperation in support of refugees in Tanzania. Since 2015, the UK Government through DFID has contributed USD 43,394,745 to support refugees, asylum-seekers and host communities in Tanzania through its humanitarian funding, with additional support to the Kigoma region provided through longer term development programmes.
 
Tanzania hosts more than 300,000 refugees and other persons of concern in the three refugee camps in the Kigoma region. 74% of the refugees are from Burundi and 26% are from the Democratic Republic of Congo and other countries.

Aliemteka Mtoto na kumnyonga Mbeya amekamatwa na Jeshi la Polisi

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja [Jina linahifadhiwa] kwa tuhuma za mauaji ya mtoto aitwaye JUNIOR BAKARI @ SIAME [12] Mwanafunzi Shule ya Msingi Hayanga Darasa la III na Mkazi wa Hayanga.

Marehemu alitoweka nyumbani kwao tangu tarehe 09.04.2019 saa 16:00 jioni wakati anatoka masomo ya ziada na ndipo mtuhumiwa hayo alimteka na kuondoka naye kusikojulikana na baadae mtuhumiwa alipiga simu kwa baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye BAKARI SIAME akihitaji kupatiwe fedha Milioni Kumi [Tshs.10,000,000/=] ili aweze kumuachia mtoto huyo ila alimnyonga shingo na kumuua na kukimbilia Mkoa wa Iringa maeneo ya Ipogolo ambapo kikosi kazi cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kilifika na kumkamata na kuja nae Mbeya hadi eneo la tukio.

Ambapo tarehe 13.04.2019 saa 23:00 usiku huko Mtaa wa Shinya, Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jijini na Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa [Jina linahifadhiwa] aliwapeleka Askari hadi eneo la tukio alipomnyongea mtoto JUNIOR BAKARI @ SIAME [12] ambapo mwili wake ulikutwa umetupwa kwenye shamba la mahindi lililopo maeneo ya Mlima Nyoka.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu. Upelelezi unaendelea.

AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.

Mnamo tarehe 14.04.2019 saa 20:30 usiku huko maeneo ya Ituta, Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Barabara kuu ya Mbeya – Tunduma, Jiji la Mbeya. Gari yenye namba za usajili T.775 BYV aina ya Toyota Station Wagon ikiendeshwa na dereva MWAMZI TILA [28] Mkazi wa Uyole ilimgonga mtembea kwa miguu ambaye ni askari G.1008 D/C ANANIA JAMES KIWANGA [36] askari idara ya Upelelezi, Wilaya ya Mbeya mkazi wa FFU Mbeya aliyekuwa kazini kizuizi cha magari Ituta – Iwambi na kumsababishia kifo.

Mtuhumiwa amekamatwa na gari lipo kituoni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Chanzo cha ajali ni mwendokasi. Upelelezi unaendelea.

Makusanyo Ya Kodi Kwa Kipindi Cha Miezi Tisa Ya Mwaka Wa Fedha 2018/19 (Julai 2018 – Machi 2019)

$
0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 11.96 katika kipindi cha Miezi Tisa ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai 2018 hadi Machi 2019.

Katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2018/19 TRA, ilifanikiwa kukusanya Shilingi Trillioni 1.30 kwa mwezi wa Januari, Shilingi Trillioni 1.23 kwa mwezi wa Februari na kiasi cha Shilingi Trillioni 1.43 kwa mwezi wa Machi, 2019.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inawashukuru walipakodi wote waliochangia makusanyo hayo kwa kulipa kodi zao kwa hiari na kwa wakati na kuhimiza wale ambao bado wanasuasua kujitokeza kulipa kodi hizo kwa wakati. TRA inaendelea kuhimiza wananchi wote ambao wana changamoto za kikodi kutembelea ofisi za TRA na kuonana na mameneja wa mikoa na wilaya kwa ufumbuzi wa changamoto hizo.

Aidha, katika kuongeza wigo wa kodi, TRA kwa sasa imeweka utaratibu wa kurahisisha upatikanaji wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambapo TIN inaweza kutolewa katika ofisi zote za TRA katika ngazi ya Mkoa na Wilaya baada ya mwombaji kuwasilisha kitambulisho cha taifa au kwa kupata namba ya kitambulisho wakati kitambulisho kikiendelea kushughulikiwa . Sambamba na hilo TRA inaendelea kuhamasisha, kutoa elimu ya kodi na kusajili walipakodi wapya katika mikoa, wilaya na vitongoji mbalimbali nchini kote.

Wakati huo huo, Mamlaka inapenda kuwakumbusha wamiliki wote wa majengo nchini kujitokeza kulipia kodi za majengo haraka kuepuka usumbufu wa kulipa mwishoni kwani kwa sasa viwango ni rafiki na vinalipika. Viwango hivyo kwa mwaka ni Shilingi 10,000 kwa nyumba ya kawaida, Shilingi 50,000 kwa kila sakafu nyumba ya ghorofa katika majiji, Manispaa na halmashauri za miji na Shilingi 20,000 kwa jengo la ghorofa katika maeneo ya halmashauri za wilaya.

Vile vile, TRA inawaasa wale wote wanaojishughulisha na vitendo vya kughushi risiti za kielektroniki za EFD nchi nzima kuacha mara moja kwa sababu wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani. Kila mwananchi na mfanyabiashara atambue wajibu wake wa kudai risiti kwa kila manunuzi na kutoa risiti kwa kila mauzo.

Tunaendelea kuwakaribisha wakazi wa Dar es Salaam kutembelea kituo cha ushauri kwa walipakodi kilichopo katika makutano ya mitaa ya Samora na Bridge katikati ya jiji, karibu na jengo TTCL. Pia wanaweza kupiga simu bure namba 0800 750075 au 0800 780078 na kwa upande wa barua pepe tafadhali tuandikie huduma@tra.go.tz. Vile vile, wanaweza kutuma ujumbe kupita namba ya Whatsapp 0744 233 333.

Viongozi Vyama 8 vya Upinzani Wamtaka Spika Ndugai Ajiuzulu

$
0
0
Vyama vinane vya kisiasa nchini vimemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai ajiuzulu kutokana na kauli yake ya kumtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) Profesa Musa Assad akamuombe msamaha Rais Dk. John Magufuli au ajiuzulu kwani kufanya hivyo ni kushindwa kazi.

Vyama hivyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP), Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Chama cha ACT-Wazalendo, Chama cha Democratic Party ( DP), Chama cha NCCR MAGEUZI, Chama cha National League for Democracy (NLD) na Chama cha Kijamii (CCK).

Akizungumza katika mkutano wa vyama hivyo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 15, kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP), Fahmi Dovutwa amesema kauli hiyo ya Spika ni kutaka kuichanganya ofisi ya Rais na Bunge.

“Desturi tuliyoachiwa na Hayati Baba wa taida Mwl. Julius Nyerere ni kuwa viongozi wakubali kukosolewa na wasijisie vibaya wanapokosolewa, kauli ya Spika ya kumtaka CAG ajishushe kwa Rais ama kujiuzulu sio nzuri, taaifa haliwezi kwenda namna hii.

“Leo ameanza na CAG, kesho atasema IGP na Mkuu wa Majeshi ya ulinzi wajiuzulu, hii inaonesha Splika ameshindwa kazi hivyo ni bora ajiuzulu yeye,” amesema Dovutwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe amesema kauli ya Spika ni yake binafsi na si msimamo wa Bunge kwasababu kama wabunge hawakukaa bungeni na kujadili wamwambie CAG ajiuzulu.

“Spika ameligeuza Bunge ni chombo chake binafsi, wabunge wanafukuzwa bungeni hovyo, mbunge anapofanya kitu kisichokupendeza wewe usisahau kuwa yule ni muwakilishi wa wananchi, pamoja na udhaifu wake Bunge halijamtuma akamwambie CAG ajiuzulu huo ni mtazamo wake binafsi,” amesema.

Wapinzani Waishitaki Serikali Mahakama ya Afrika Mashariki

$
0
0
Vyama vinane vya kisiasa nchini vimefungua shauri la kupinga Sheria ya Vyama vya Siasa katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) lililopewa namba 03/2019.

Sheria hiyo namba 1 ya mwaka 2019 ilisainiwa na Rais Dk John Magufuli Februari 13, mwaka huu baada ya muswada wa sheria hiyo kupitishwa na Bunge mwaka jana.

Akizungumza katika mkutano wa vyama hivyo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 15, kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia a Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema waliamua kwenda katika mahakama hiyo kwani kuna ukomo wa kupeleka mashauri na shauri lao limepokelewa na wamempa siku 45 Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujibu maombi yao.

“Kupitia maombi tuliyowasilisha mahakamani hapo katika shauri hilo tumeiomba mahakama itamke kwamba vifungu tunavyolalamikia havina hadhi ya kisheria, tumelazimika kuitafuta haki kutokana na kuwa sheria hiyo ni mbaya na ambayo inafanya shughuli za kisiasa nchini kuwa jinai.

Msingi wa madai yetu katika shauri hilo ni kwamba sheria ni mbovu na inakiuka misingi ya mkataba y uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hususani katika ibara ya 6, 7 na 8B ya mbali na hilo pia inakiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na misingi ya utawala bora na mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo nchi imetia saini, “ amesema.

Katika hatua nyingine Mbowe amesema kanuni mpya za chaguzi za Serikali za Mitaa zinawanyima haki wapinzani kwani hawaruhusiwi kwenda kufanya kampeni na mikutano ya kisiasa katika maeneo mbalimbali nchini.

Tunaingiaje katika uchaguzi bila kujijenga miaka minne sasa hatujajijenga kwa mikutano, hatuwezi kufanya uchaguzi kwa kampeni za siku Saba tena karibia na uchaguzi,” amesema.

Aidha vyama hivyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Chama cha wa Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP), Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Chama cha ACT-Wazalendo, Chama cha Democratic Party ( DP), Chama cha NCCR MAGEUZI, Chama cha National League for Democracy (NLD) na Chama cha Kijamii (CCK).

Mkuu wa Mkoa, Wilaya atakae msweka mtu mahabusu bila sababu kuchukuliwa hatua

$
0
0
Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wenye tabia ya kuwasweka mahabusu watu wasiokuwa na hatia watachukuliwa hatua.

Mkuchika amesema kuwa mtu nawekwa ndani kama ana hatarisha amani sio watu wanadaiana madeni huko una muweka ndani, mtu asiwekwe mpaka awe amehatarisha amani.

“Hawatatetewa na  Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ninamshukuru mwanasheria mkuu wa Serikali ametoa waraka kwa wote waliopewa mamlaka ya kuweka mtu ndani na mimi kanipa nakala, ikieleza mazingira ya mtu kuwekwa ndani,” amesema Mkuchika leo Jumatatu Aprili 15, 2019 bungeni jijini Dodoma.

Akiwa anajibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti hiyo mwaka 2019/2020 Mkuchika amesema, “Moja awe ametenda kosa la jinai, na (mkuu wa wilaya, mkoa) uweke kwa maandishi kwa nini umemuweka ndani. Utawala bora unasema kesi ikiwa mahakamani hakuna mkuu wa wilaya, mkoa au waziri anayeweza kuisikiliza.”

“Mahakama ya chini uamuzi wake unaweza kutenguliwa na mahakama ya juu wengine wamejiingiza katika matatizo kwa mambo ambayo tayari yametolewa hukumu mahakamani.”

Mkuchika amesema wakuu wa wilaya na mikoa wanapotumia mamlaka yao kuweka mtu mahabusu kwa saa 24 na 48 wazingatie sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997.

“Sheria hii inawapa mamlaka kuwaweka ndani watu pale inapothibitika anahatarisha amani. Nawaomba wabunge tusikilize sheria na nawaomba na huko walipo (wakuu wa wilaya na mikoa) wanisikilize,” amesema.

“Mtu anawekwa ndani kama amehatarisha amani, si watu wanadaiana madeni hawataki kulipa unawapeleka kwa mkuu wa mkoa, hawa wanadaiana si kuhatarisha amani.”

Alisema viongozi hao wakitekeleza hatua kinyume na utaratibu wanaweza kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kushtakiwa binafsi.

Serikali kufanya mabadiliko kanuni za matumizi ya Nyavu baharini

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Serikali imepanga kufanya mabadiliko ya kanuni za matumizi ya nyavu upande wa bahari ili wavuvi waweze kutumia nyavu za milimita nane badala ya milimita kumi zilizokuwa zikitumika awali.

Hayo yamesemwa jana, Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi lililohoji kuwa ni lini Serikali itakuwa tayari kufanya utafiti katika eneo la Ziwa Victoria kama inavyofanya upande wa Bahari ili kuweza kuruhusu matumizi ya nyavu za chini ya milimita nane.

Ulega alisema kuwa kwa mujibu wa Sheria, nyavu za kuvulia dagaa zenye ukubwa wa macho chini ya milimita nane zimekatazwa kutumika kwa uvuvi wa dagaa katika maji baridi ikiwemo maeneo ya maziwa kwa sababu tafiti zinaonyesha kuwa aina hiyo ya nyavu ikitumika itavua dagaa wachanga hivyo kuathiri uvuvi wa dagaa.

“Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania itafanya utafiti na endapo itaridhika itaruhusu wavuvi wanaovua ziwani wavue kwa kutumia aina hiyo ya nyavu, kwa upande wa bahari  Serikali imeielekeza TAFIRI kufanya utafiti na kujiridhisha kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya kanuni kwa haraka ili ikiwezekana tuweze kutumia nyavu za milimita nane zitakazoweza  kuwanufaisha wavuvi wa upande wa bahari”,  alisema Ulega.

Alifafanua kuwa kwa upande wa bahari, nyavu zilizokuwa zikitumika kuvua dagaa ni milimita kumi lakini maoni ya wadau wengi yanaonesha kuwa milimita kumi zimeshindwa kuvua dagaa ndio maana Serikali imeamua kufanya utafiti huo ili kuona kama inawezekana wavuvi wa bahari kutumia nyavu za milimita nane.

Akizungumzia kuhusu uvuvi wa samaki aina ya Gogogo, Ngele na Mingu waliopo katika Ziwa Victoria, Naibu Waziri Ulega amesema kuwa katika mabadiliko ya Kanuni yanayofanyika hivi sasa Serikali imezingatia kufanya makubaliano ya kupitisha kanuni rasmi itakayoruhusu uvuaji na matumizi ya aina hizo za samaki.

Waziri Ulega alitoa rai kwa wavuvi kuendelea kuzingatia sheria na kanuni zilizopo kwani Sheria na kanuni hizo zinalenga uvuvi unaofanyika nchi uwe endelevu na wenye tija.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya April 16

Rais Magufuli Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Ya Halmashauri Kuu Ya Ccm (NEC) Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Kikao cha Kamati Kuu kimemteua Ngugu, John Danielson Pallangyo kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Arumeru.

Tume ya Uchaguzi ilitangaza uchaguzi wa marudio kuwa ni Mei 19 na Jimbo la Arumeru Mashariki lilikuwa wazi baada ya aliekuwa Mbunge wake Joshua Nassari kuvuliwa ubunge na Spika kutokana na kutohudhuria vikao vitatu.

Chama cha Mapinduzi kimefanya Kikao cha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa NEC jana mchana jijini Dodoma wakiogozwa na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.

Benki ya CRDB na UBA yaidhamini serikali ujenzi wa Stieglers George

$
0
0
Benki ya CRDB kwa kushirikiana na benki ya UBA zimetoa Dola za Kimarekani milioni 737.5 ambazo ni sawa na Sh Trilioni 1.7 kwa ajili ya kuidhamini serikali katika ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji wa Stieglers George.

Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa benki ya UBA, Usman Isiaka alisema fedha hizo ni dhamana ya benki inayotakiwa na mkandarasi katika mradi huo ambao utagharimu Sh trilioni 6.6.

“Kwa mujibu wa masharti ya mkataba huo, umoja huo unahitajika kutoa dhamana za benki za kigeni na za ndani zikiwa ni jumla ya Dola za Kimarekani milioni 737.5 kupitia utekelezaji wa mradi na dhamana ya malipo ya awali kwa mradi huo.

“Kwa kuanzia, Benki ya CRDB na UBA zimeshirikiana na Benki ya Afrika Export-Import (Afrieximbank) na benki nyingine za Misri kutoa dhamana za benki kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambapo sehemu ya dhamana hizo tumezitoa hapa leo (jana),”alisema Isiaka.

Mradi  huo mkubwa unatarajia kuiongezea nguvu Serikali kukabiliana na upungufu wa umeme kwa kuwa uchumi wa nchi na idadi ya watu inaongezeka.

Takukuru Njombe Yachunguza Mradi Wa Mabilioni Ya Pesa

$
0
0
Na Amiri kilagalila, Njombe.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Njombe inaendelea na uchunguzi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi cha Njombe mjini ambacho kimeshindwa kukamilika kwa wakati na kuchukua zaidi ya miaka 6 mpaka sasa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoani Njombe , Bw Charles Mulebya wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake.

"TAKUKURU mwanzoni mwa mwezi Machi mwaka huu (2019) tulianza kufanya uchunguzi juu ya ujenzi wa stendi kuu ya mabasi inayoendelea kujengwa katika halmashauri ya mji wa Njombe, kufuatia taarifa ya ukaguzi uliofanywa na ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali na kuibua ubadhilifu katika ujenzi huo.” Alisema Bw Mulebya.

Aidha, Bw Mulebya alisema kuwa kutokana na uchunguzi wanaoufanya mpaka Sasa wamefikia katika hatua nzuri na  karibuni utakamilika.

“Ujenzi huu utagharimu shilingi Bil 9.7 hadi kukamilika kwake na uchunguzi upo kwenye hatua nzuri za kukamilika, uchunguzi unafanyika kwa umakini mkubwa ili yeyote aliyehusika akutane na mkono wa sheria kwa kusababisha ucheleweshwaji wa kituo hicho pamoja na ubadhilifu wa fedha ulioibuliwa hivi karibuni.” ameongeza Bw Mulebya.

Mbali na hivyo, Kaimu huyo amebainisha kuwa uchunguzi wa majalada ya mwanzo umebaini makosa chini ya manunuzi ya umma na kanuni zake za mwaka 2013 na mara baada ya kukamilika majalada yatapelekwa makao makuu kwa hatua zaidi.

Katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  iliyofanyika kwa siku tatu mkoani Njombe, Rais alimuagiza mkurugenzi na mkandarasi wa kituo hicho cha mabasi mjini Njombe kuhakikisha mpaka mei 5  kimekamilika na kuanza kutumiwa.

Walimu 86,000 Waidai Mabilioni Serikali

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Imeelezwa kuwa kuna jumla ya walimu zaidi ya  86,000 wanaidai Serikali kwa madeni ya Malimbikizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Malimbikizo ya Mishahara na fedha za likizo .
 
Hayo yamesemwa jana  April 15 bungeni jijini Dodoma na Naibu waziri wa nchi ,ofisi ya Rais na Serikali za mitaa ,TAMISEMI Mwita Waitara wakati akijibu swali la Mbunge la Mbunge wa viti Maalum Kiza Husein aliyetaka kujua  namna ya ulipaji fedha za likizo kwa walimu.

Katika majibu yake  Naibu Waziri wa  TAMISEMI, Mwita Waitara alisema Serikali ina nia nzuri kuhakikisha inalipa walimu kwa wakati na kwamba wapo walimu 86,000 ambao wanaidai Serikali zaidi ya Shilingi Bilioni  43 .

Awali, katika swali lake la msingi mbunge huyo alisema Serikali imekuwa ikiwapandisha madaraja walimu lakini haitoi malipo stahiki kwa madaraja hayo mapya kwa kipindi kirefu tangu walipopanda madaraja yao.

 
Akijibu swali hilo, Waitara alifafanua kuwa Serikali ilisitisha kupandisha walimu na watumishi wengine madaraja katika mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 kutokaana na uhakiki wa watumishi.

Waitara alisema kutokana na sababu hiyo ni kweli wapo watumishi ambao walipandishwa madaraja hawajalipwa mishahara mipya, wapo waliopata mishahara mipya na baadaye kuendolewa na wengine hawakupandishwa licha ya kuwa na sifa.

Alisema ili kurekebisha changamoto hizo, Serikali ilitoa maelekezo kuanzia Novemba 2017 kwa waajiri wote wakiwamo wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kuhuisha barua za kuwapandisha madaraja watumishi hao ili waweze kulipwa stahili zao .

Kwa upande wake Naibu waziri wa Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mhe.Mary Mwanjelwa ametoa ufafanuzi  juu ya suala la  muda wa kukaimu kwa watumishi wa umma ambapo ukomo wake ni   miezi sita zaidi ya hapo    mwajiri anatakiwa kuandika barua tena ya ombi la kuendelea kukaimu na sababu zake.

Hii imekuja baada ya  mazoea kwa baadhi ya wakurungezi hapa nchini kuendelea kuwakaimisha  watumishi wao wakiwemo maafisa watendaji wa vijiji na kata kwa muda mrefu.

Serikali Yadhamiria Kukamilisha Skimu Zote Za Umwagiliaji Ambazo Utekelezaji Wake Haujakamilika

$
0
0
 Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali inayo dhamira ya kukamilisha skimu zote za umwagiliaji ambazo utekelezaji wake haujakamilika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma jana tarehe 15 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Azza Hillal Hamad aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji katika Kijiji cha Ishololo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mhe Mgumba amesema kuwa Skimu hiyo ipo miongoni mwa skimu za umwagiliaji zitakazopewa kipaumbele katika kutekeleza Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji (Irrigation Master Plan 2018 - 2025) ambao kwa sasa umeanza kutekelezwa.

Alisema kwa kuzingatia umuhimu wa miradi hiyo ukiwemo mradi wa umwagiliaji Ishololo, tayari Serikali imekwishaanza mazungumzo na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA kwa lengo la kuboresha miradi yote ambayo haijakamilika na ile inayofanya kazi chini ya ufanisi uliokusudiwa.

Naibu Waziri huyo wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) alisema kuwa mradi wa ujenzi wa bwawa wa Ishololo uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini ni moja kati ya miradi iliyokuwa ikitekelezwa kupitia Mradi wa Uwekezaji katika Kilimo katika Wilaya (DASIP) chini ya iliyokuwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Alisema Utekelezaji wa Mradi huo ulifikia ukomo wake mwezi Desemba 2013 ambapo Benki Maendeleo ya Afrika ilisitisha kutoa fedha za utekelezaji wa miradi wakati utekelezaji wake ukiwa haujakamilika.

LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka bungeni Dodoma

$
0
0
LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka bungeni Dodoma

Serikali kuleta mabehewa na vichwa vya treni ya umeme 1,400

$
0
0
Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amebainisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Serikali inatarajia kuleta mabehewa na vichwa vya treni ya umeme 1,400.

Hayo yamebainishwa alipokuwa akizungumzia tukio la uungwaji wa reli ya treni za Umeme, Standard Gauge Railway kuunganishwa kwa vipande vya SGR na kufanya reli hiyo kuwa moja kutoka Morogoro hadi Dar uliofanyika Aprili 14, 2019 katika kijiji cha Soga mkoani Pwani na kuhudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe

Waziri Kamwele alieleza kuwa ifikapo mwezi wa saba mwaka huu, Mkandarasi wa reli hiyo ya Shirika la Reli nchini(TRC) wataleta kichwa cha treni ya umeme kwa ajili ya majaribio kwenye kipande cha reli cha Kilometa 30.

Mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge – unaendelea. Reli hiyo itaanzia bandari ya Dar es Salaam hadi mji mkuu wa Dodoma na baadaye hadi nchi za jirani za Rwanda Burundi na DR Congo.

==>>Tazama hapo chini

Katibu Mkuu CHADEMA Aitwa Kujieleza Mahakamani

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemtaka Katibu Mkuu CHADEMA , Dk Vicent Mashinji kuieleza mahakama kwa nini ameshindwa kuhudhuria kesi yake iliyopo mahakamani hapo.

Dk Mashinji ambaye ni mshtakiwa wa sita katika kesi ya kufanya mikusanyiko isiyo halali, inayowakabili vigogo tisa wa chama hicho, ameshindwa kufika mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa yupo kwenye kesi nyingine iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea mkoani Ruvuma.

Dk Mashinji ametakiwa kufika mahakamani hapo Aprili 17, 2019  na kuieleza mahakama hiyo sababu za yeye kushindwa kufika mahakamani hapo, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.

Dk Mashinji na wenzake wanakabiliwa na makosa 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko la kutawanyika.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images