Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Japan Kuipiga Jeki Tanzaniashilingi Bilioni 794 Kutekeleza Miradi Ya Maendeleo

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Washington D.C
Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa-JICA inakusudia kuipatia Tanzania mkopo nafuu pamoja na ruzuku wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 345 za Marekani, sawa na takriban shilingi bilioni 794, kwa ajili ya kutekeleza miradi mitatu ya maendeleo ikiwemo ukarabati wa barabara ya Arusha hadi Holili, ukarabati wa Bandari ya Kigoma na Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Visiwani Zanzibar.

Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la JICA anayesimamia Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. Hiroshi Kato, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Mjini Washington D.C nchini Marekani.

Ameitaja miradi hiyo iliyoko mezani kwao inayosubiri kupatiwa fedha wakati wowote kuanzia sasa kuwa ni mradi wa ukarabati wa barabara ya Arusha-Holili utakaopatiwa mkopo wa dola milioni 221, Mradi wa maji safi na usafi wa mazingira Zanzibar utakaopatiwa fedha kupitia mkopo wa dola milioni 99 na mradi wa upanuzi wa Bandari ya Kigoma ambao Japan itatoa ruzuku ya dola za Marekani milioni 25.

Bw. Kato amesema kuwa Japan inajivunia ushrikiano wa muda mrefu kati yake na Tanzania na kwamba iko tayari kusaidia juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuwaletea wananchi wake maendeleo na kuitaka Serikali kuwasilisha miradi yake ya kimkakati ambayo Japan itafadhili kupitia mikopo yenye riba nafuu pamoja na ruzuku.

Akizungumza na Mwakilishi huyo wa Japan katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Japan kwa uhusiano wake mzuri na Tanzania na namna inavyo isaidia nchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo akitaja mmoja wa miradi hiyo kuwa ni barabara ya juu ya kwanza nchini Tanzania  katika makutano ya Tazara Jijini Dar es Salaam, maarufu kama Daraja la Mfugale.

Dkt. Mpango ameiomba Japan kupitia Shirika lake la JICA kutoa ruzuku na mikopo nafuu ili kutekeleza miradi ya kimkakati ya ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha kimataifa - SGR, Mradi wa kufua umeme wa Rufiji, Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato mkoani Dodoma, ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dodoma, ujenzi wa mtandao wa barabara, upanuzi wa bandari na miradi mingine ya kijamii.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mikutano ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, inayofanyika mjini Washington DC nchini Marekani, ambapo ametumia fursa hiyo kukutana na wadau wa maendeleo kupenyeza ajenda za maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania.

Video: Ommy Dimpoz x Alikiba x Cheed - ROCKSTAR

$
0
0
Video: Ommy Dimpoz x Alikiba x Cheed - ROCKSTAR

Ofisi Ya Bunge Yakanusha Uzushi Unaosambaa Mitandaoni Kuhusu CAG

Wimbo Mpya: Lady JayDee - I Don't Care

$
0
0
Wimbo Mpya: Lady JayDee - I Don't Care

CUF Wamshitaki Zitto Kabwe na Maalim Seif Mahakamani.....Wanadai Fidia ya Milioni 900

$
0
0
Chama cha Wananchi CUF  kumemfungulia kesi mbili katibu wake mkuu wa zamani, Maalim Seif Sharif Hamad na wenzake, kikiwadai fidia ya jumla ya Sh900 milioni.

Kesi hizo zimefunguliwa na Bodi ya Wadhamini CUF katika Mahakama Kuu Zanzibar na Mahakama Kuu ya Tanzania dhidi ya Maalim Seif na wenzake akiwamo Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kikiwadai fidia hiyo kutokana na uharibifu uliofanywa katika ofisi zake.

Katika kesi hizo, chama hicho kinadai kuwa uharibifu huo ulifanywa na mawakala au wawakilishi wa Maalim Seif na wenzake muda mfupi tu baada ya kutangaza kujiunga na ACT-Wazalendo.

Maalim Seif alijiunga ACT-Wazalendo Machi 18 muda mfupi baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliomhalalisha Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa CUF) na siku chache baada ya Baraza Kuu la Uongozi la CUF kutangaza kumvua uanachama yeye na wenzake.

CUF inadai kuwa kufuatia uamuzi huo, Maalim Seif, Zitto na wenzao kwa msaada wa mawakala na au wawakilishi wao, walipaka rangi ya chama cha ACT-Wazalendo katika majengo mbalimbali ya ofisi za CUF, ngazi ya matawi na wilaya Zanzibar na Bara.

Kwa mujibu wa hati za madai, chama hicho kinadai kuwa mawakala na wawakilishi hao wa Maalim Seif na wenzake walifanya uharibifu huo kwa ushauri wa mmoja wa wadaiwa katika kesi hizo, Daimu Halfan, huku wakijua kuwa ni kinyume cha sheria

Uharibifu mwingine unaodaiwa ni kushusha na kuchoma bendera zake na kisha kupandisha za ACT- Wazalendo katika ofisi zake, kuondoa na kuharibu samani na nyaraka za ofisini.

Chama hicho kinapinga madai ya baadhi ya wadaiwa (Mazrui, Faki na Juma) kwamba majengo hayo yalikuwa ni ya watu binafsi waliokuwa wameyatoa kwa chama hicho kumuunga mkono Maalim.

Badala yake, CUF inadai kuwa tangu mwaka 1992, kimekuwa kikimiliki majengo kilipoanzisha ofisi zake katika ngazi za matawi na vijiwe, ambayo kiliyanunua maeneo ya Mabibo na Magomeni Dar es Salaam, Tanga mjini na maeneo mengine Tanzania Bara.

Katika kesi namba 60 iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wadaiwa ni Zitto (mdaiwa wa kwanza), Maalim Seif (mdaiwa wa pili) na wenzao saba.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 17

Jeshi lA Sudani Lepwa Siku 15 Kuondoka Ikulu

$
0
0
Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, limelitaka Jeshi la Sudan kuhakikisha linaachia madaraka kwa utawala wa kiraia vinginevyo litatengwa.

Baraza hilo limetoa siku 15 kwa Baraza la Kijeshi la Sudan kutekeleza maelekezo hayo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Waziri Mkuu anasimikwa na anatokana na matakwa ya wananchi.

Lieutenant General Jalal al-Deen al-Sheikh, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Kijeshi la Sudan amekutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia jijini Addis Ababa yalipo makao makuu ya Umoja wa Afrika, na amemueleza kuwa wanaendelea na mchakato wa kuweka utawala wa kiraia.

“Tayari tuko kwenye mchakato wa kumchagua Waziri Mkuu kwa ajili ya kuweka Serikali ya kiraia,” Shirika la Habari la Sudani (SUNA) limemkariri.

“Kwahiyo tumeanzisha mchakato huu kabla hatujakutana na Umoja wa Afrika. Huo ndio msimamo wetu na ndio njia ya kuelekea kwenye amani, lakini pia tunaheshimu na tunafuata maamuzi ya Baraza la Amani na Usalama,” aliongeza.

Wananchi wameendelea kuandamana katika mitaa ya jiji la Khartoum wakishinikiza kuwepo kwa utawala wa kiraia, baada ya kufanikiwa kushinikiza kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 30, Omar Al-Bashir.

Al-Bashir aliondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo baada ya kuongezeka kwa maandamano makubwa, anashikiliwa na chombo hicho cha ulinzi ambacho kimeeleza kuwa kitamfikisha kwenye mahakama za ndani ya nchi hiyo na sio Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC).
 
Al-Bashir anakabiliwa na mashtaka ya jinai kwenye mahakama ya ICC, na amekuwa akitafutwa kwa miaka kadhaa ili akajibu mashtaka dhidi yake.

Bunge la Iran latangaza vikosi vya jeshi la Marekani katika Mashariki ya Kati kuwa la kigaidi

$
0
0
Wabunge wa Iran kwa kauli moja wamevitangaza vikosi vya jeshi la Marekani katika mashariki ya kati kuwa ni vya kigaidi siku moja baada ya uamuzi wa Marekani kuliweka jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya Iran kuwa la kigaidi kuanza kufanyakazi rasmi. 

Waziri wa Ulinzi Jenerali Amir Hatami amewasilisha mswada huo unaoidhinisha serikali kuchukua hatua kali katika kujibu hatua za kigaidi za jeshi la Marekani. 

Mswada huo unataka maafisa kutumia hatua za kisheria, kisiasa na kidiplomasia kuzuwia hatua za Marekani, lakini hakutoa maelezo zaidi. 

Hatami amewaambia wabunge kwamba hatua ya Marekani inayo lenga kuzuwia ushawishi wa Iran, inaonesha kwamba vikwazo vya muda mrefu vya Marekani dhidi ya Iran havijaleta athari. 

Katika mjadala huo baadhi ya wabunge wenye msimamo mkali walitaka kuliorodhesha jeshi zima la Marekani na majeshi ya usalama kuwa ni ya kigaidi.

Waziri Jafo Katimiza Agizo la Rais Magufuli Kuhamia Kwenye Jengo Lisilokamilika "Pagala"

$
0
0
Agizo la Rais John Magufuli limesababisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, na wasaidizi wake kuhamia kwenye ofisi za mabati mjini Dodoma.

Jaffo na manaibu waziri wake wawili, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu pamoja na watumishi wengine wamelazimika kuhamia kwenye ofisi za muda za mabati hayo kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Magufuli mwishoni mwa wiki.

Jengo la ghorofa mbili la wizara hiyo lililopo kwenye mji wa serikali uliopo Mtumba jijini hapo halijakamilika, hali iliyomkera Rais Magufuli ambaye aliwataka wahamie hivyo hivyo.

Mbali na mawaziri hao, pia baadhi ya Idara muhimu za wizara hiyo zimehamia kwenye ofisi hizo za mabati, huku mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo ambalo walipaswa kuwamo.

Rais Magufuli mwishoni mwa wiki alizindua mji huo ambapo aliagiza wizara zote 23 kuhakikisha zinahamia eneo hilo zikiwamo tatu ambazo hazijakamilisha majengo yake.

Jafo amesema walihamia tangu Jumatatu yeye pamoja na manaibu wake, Katibu Mkuu na baadhi ya idara muhimu.

Amesema wanaendelea kutekeleza majukumu yao katika ofisi yao hiyo mpya, huku mafundi wakiendelea na ujenzi ambao unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu.

“Nilipokuwa nakuja hapa, kuna watu walikuwa wananishangaa wakiwamo mafundi wetu ambao waliniambia ofisini kuna joto, mimi najiona nipo sawa,” alisema.

Jafo alisema yeye anashinda vijijini kukagua miradi ya maendeleo hivyo katika mazingira hayo ya sasa ya mabati anaona ni jambo la kawaida tu.

Hata hivyo, Jaffo alisema jengo lake ni kubwa la ghorofa mbili na ni miongoni mwa majengo ya kisasa ambayo baada ya kukamilika litakuwa linavutia.

Jafo alisema litakuwa na uwezo wa kuchukua watumishi 88, kutakuwa na kumbi mbili za mikutano ambao mmoja utachukua watu 25 na ukumbi mkubwa utakuwa na uwezo wa kuhudumia watu 60.

PICHA: Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana CHADEMA Ajiunga Rasmi CCM

$
0
0
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu  wa Baraza la Vijana CHADEMA Tanzania Bara,Getrud Ndibalema na baadae kujiuzuru nafasi hiyo mwezi Machi mwa mwaka jana (2018), jana  amejiunga na chama cha Mapinduzi CCM akipokelewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ndg Mussa Mwakitinya makao makuu ya chama hicho Dodoma

LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka bungeni Dodoma

$
0
0
LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka bungeni Dodoma

Jela Miaka Miwili Kwa kosa la kughushi na kutumia vyeti bandia.

$
0
0
Mahakama  ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani imemuhukumu kwenda jela miaka miwili Anna Kasanda kwa kosa la kughushi na kutumia vyeti bandia.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Rose Kangwa, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa utetezi kuwa mtuhumiwa alikuwa anatumia vyeti bandia.

“Mtuhumiwa anahukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kwanza la kughushi leseni ya uuguzi na ukunga kinyume cha kifungu cha sheria namba 355(a) na 337 cha mwaka 2002,” alisema Rose.

Alisema kwa kosa la kujaribu kuihuisha (renew) leseni hiyo, mtuhumiwa atatumikia miaka miwili mingine. 

Rose alisema japokuwa hakuna sehemu katika ushahidi inaonesha mtuhumiwa anamiliki mashine ya kuchapa nyaraka hizo, lakini kwa mujibu wa shahidi wa pili inaonesha kuwa mtuhumiwa alitaka kuendelea kutumia vyeti hivyo.

Bunge Lakubali mikutano ya Hadhara isiendelee kufanyika hadi wakati wa kampeni za uchaguzi.

$
0
0
Bunge limekubaliana mikutano ya kisiasa isiendelee kufanyika hadi wakati wa kampeni za uchaguzi.

Hatua hiyo ilifikiwa jana baada ya wabunge kuhojiwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, kutokana na swali na Mbunge wa Moshi Mjini, Jafary Michael (Chadema), aliyetaka kujua ni kwanini Serikali imezuia mikutano ya kisiasa nchini.

Michael aliuliza swali hilo juzi usiku wakati Bunge lilipokuwa limekaa kama kamati, kujadili bajeti ya Wizara ya Tamisemi, iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita na Waziri wa Wizara hiyo, Seleman Jafo.

Katika hoja yake, Michael alianza kwa kutaka Serikali imweleze ni kifungu gani cha sheria kinachozuia mikutano ya siasa huku akitaka iruhusiwe kwa kuwa taifa linakabiliwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baadaye mwaka huu.

“Uchaguzi ni ‘process’ kwani unaanzia wakati wa kuchagua wagombea hadi kwenye kufanya kampeni na kupiga kura.

“Kwa kuwa kwa sasa wanasiasa hatufanyi mikutano ya siasa kwa sababu mheshimiwa rais ameizuia, naomba mniambie ni kifungu gani cha sheria kinachozuia mikutano hiyo kwa kuwa mikutano ya siasa ni haki ya wanasiasa,” alisema Michael.

Baada ya hoja hiyo kuungwa mkono na wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mjadala wa hoja hiyo ulianza kwa kuhusisha wabunge wa Chadema, Aida Kenani na Lucy Magereri.

Wengine waliochangia hoja hiyo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na Waziri wa Zamani wa Wizara hiyo, Mwigulu Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi (Chadema).

Katika michango yao, Kenani na Magereri walitaka mikutano ya kisiasa iruhusiwe kwa sababu inatambuliwa kikatiba huku Mwigulu na Kangi wakisema hakuna sababu ya mikutano hiyo kuruhusiwa hadi uchaguzi utakapofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa upande wake, Kangi alisema hakuna mikutano ya siasa iliyozuiwa bali inaruhusiwa kwa kupata kibali kutoka kwa Jeshi la Polisi ambalo ndilo lenye jukumu la kulinda raia na mali zao.

Baada ya michango hiyo, Naibu Spika alilazimika kuwahoji wabunge kuona kama wanakubaliana na hoja ya Michael ya kutaka mikutano ya siasa iruhusiwe, lakini wabunge wengi walitaka mikutano hiyo isiruhusiwe.

Umoja wa Mataifa walaani matumizi ya silaha nzito Libya

$
0
0
Ujumbe wa usaidizi wa Umoja wa Mataifa Libya umelaani ongezeko la matumizi ya silaha nzito na mashambulizi holela dhidi ya makazi ya watu, shule na miundombinu na kutaka huduma za dharura kuwafikia raia waliokwama

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, idadi ya watu wasio na makazi ndani na nje ya mji wa Tripoli hivi sasa inakaribia 20,000. Zaidi ya watu 2,400 walikimbia makazi yao katika kipindi cha masaa 24 pekee.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujaric, amewaambia waandishi wa habari jijini New York kwamba familia nyingi zinazokimbia maeneo yaliyo na machafuko zinaelekea katikati mwa Tripoli na maeneo ya karibu, lakini takribani watu 14,000 wasio na makazi wametafuta hifadhi nje ya mji huo mkuu katika maeneo ya Tajoura, Al Maya, Ain Zara na Tarhouna.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana lilianza kujadili azimio lililoandaliwa na Uingereza la kutaka kusitishwa mapigano nchini Libya, baada ya majeshi tiifu ya kamanda Khalifa Haftar kuanzisha mashambulizi mjini Tripoli.

Mapigano mapya nchini Libya yalizuka kiasi wiki mbili zilizopita wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutteres, baada ya kiongozi wa vikosi vya mashariki Jenerali Khalifa Haftar kuanzisha operesheni ya kuchukua udhibiti wa mji mkuu Tripoli na kukabiliana na upinzani wa vikosi vya serikali inayotambuliwa kimataifa

Kupiga Punyeto Kwa Muda Mrefu Husababisha Maumbile ya Kiume Kusinyaa na Kupungukiwa Nguvu za Kiume

$
0
0
Wanaume  wengi  waliofanya  mchezo wa  kujichua  kwa  muda  mrefu hupatwa  na  madhara  ya kuwa  na  kusinyaa  na  kudumaa  kwa  maumbile  yao  ya  kiume  ambayo  huenda  pamoja  na  tatizo  a  Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume.

Tendo  la  kujichua  kwa  mwanaume  linapofanyika  kwa  kipindi  kirefu huathiri na  kuharibu mishipa  na  misuli  ya uume  na  hivyo  kusababisha  kujengeka  kwa mafuta na tishu zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri.  Jambo  hili  husababisha  makuu mawili; 1. Huzuia  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  kuongezeka jambo  linalotajwa  na  wanasayansi  kama jambo  muhimu  sana  katika  kukua  kwa  uume. 2. Huzuika  kutirika  kwa  damu  kuingia  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili  huathiri  sana  ukuaji  wa  maumbile ya kiume  kwa  sababu  yanapo tokea huathiri uzalishaji  wa  homoni  muhimu  zinazo  husika  na  ukuaji  wa  misuli  ya  uume na matokeo  yake husababisha  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa,kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama uume  wa  mtoto.
 
Hii ndio  sababu  kwanini watu  wengi  walio athirika  na  punyeto  hulalamika  kwamba  maumbile  yao  ya  kiume  hayajaongezeka  tangu  walipo anza  kujihusisha  na  punyeto  wakiwa  na  umri mdogo. 

Maumbile  yao  huonekana  kama  ya  watoto  kwa  sababu hayakupata  nafasi  ya  kupokea  vichochea  vya  kuyafanya  yakue  na  kuongezeka  tangu  walipo  anza  kujihusisha  na  punyeto.

Suluhisho  La  Tatizo La Maumbile  Ya  Kiume  Yaliyo  Sinyaa  Kwa  Sababu  Ya  Punyeto.
Kama  bado  unaendelea  kujihusisha  na punyeto  basi  jitahidi  uache  tabia  hiyo  mara  moja  kwani  inakuharibu. Inaweza  isiwe  rahisi  sana  kuacha  mara  moja  lakini  ukiweka  nia  thabiti  basi  unaweza  kuacha  kabisa  kama  walivyofanikiwa  kuacha  wengine  ambao  walikuwa  wametopea  kwenye  tabia  hiyo  lakini  wakajitahidi  kujilazimisha  na  hatimaye  wakafanikiwa  kuachana  kabisa  na  tabia  hiyo.

==>> Acha kuangalia video chafu za ngono.
Video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie  punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako.. 


Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.

==>>Epuka kukaa nyumbani peke yako;
Mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine. 


Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata kama vile misuli ya uume kulegea, kushindwa kurudia tendo uwapo na mwenzi wako, kuishiwa nguvu za kiume, maumbile kusinyaa, kurudi ndani na kuwa kama ya mtoto mdogo.

Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema hivyohivo, kama unaacha acha mara moja ili utunze heshima yako mbele ya mwenzi au mke wako.

Kama utaona  kuna  ugumu  wa  kuacha  tabia  hiyo  na tayari ushaapata madhara ya maumbile kusinyaa na kupungiwa nguvu za kiume, basi  wasiliana nasi kwa ushauri zaidi; Simu  0744040721

Waziri Angellah Kairuki azungumza na Mabalozi wa Nchi 3 Kuhusu Mambo ya Uwekezaji Nchini

$
0
0
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki atakutana na wawekezaji kutoka nchi mbalimbali waliowekeza Tanzania ili kujua changamoto zao na kuzifanyia kazi kwa haraka na kuimarisha mahusiano ya nchi hizo na Tanzania katika sekta ya Uwekezaji.

Akizungumza katika mazungumzo mafupi aliyoyafanya jana kwa wakati tafaouti Mabalozi kutoka nchi za Ufaransa, Uholonzi, Norway pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Marekani USAID, Waziri Kairuki alisema kuwa mazungumzo hayo ni chachu ya ushirikiano katika sekta ya uwekezaji nchini.

Katika mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini, Frederic Clavier, Waziri Kairuki alisema kuwa nchi ya ufaransa na Tanzania zina ushirikiano wa muda mrefu katika sekta mbalimbali ikiwemo ya uwekezaji pamoja na biashara.

“Tulikuwa na mazungumzo na Balozi wa Ufaransa ambaye tumejadili mambo mbalimbali katika ushirikiano wetu ili kuwaita wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Ufaransa waje nchi kama ilivyokuwa mwaka jana, ambapo kulikuwa na ugeni wa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka huko na walifanya majadiliano na TPSF, kwa hiyo na mwaka huu tumekubaliana watawaalika tena TPSF na TIC ili kuweza kujadili mambo ya uwekezaji”, Waziri Kairuki.

Waziri Kairuki alisema kuwa katika kukutana na wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kutafungua fursa na namna ya kufuatilia changamoto ili uwekezaji mkubwa uweze kufanyika nchini, pia Waziri Kairuki alieleza kuwa wamekubaliana na Balozi wa Ufaransa kuwa na ugeni mkubwa wa wawekezaji kati ya mwezi Mei na Septemba ambao watakuja kuwekeza katika sekta ya kilimo.
 
Aidha Waziri Kairuki alimhakikishia Balozi wa Ufaransa nchi kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji kutoka Ufaransa ili kuongeza uwekezaji nchini kutoka wawekezaji 40 na kuongezeka ili kuweka namba kubwa ya wawekezaji kutoka Ufaransa.

“Uwekezaji unaongeza pato letu, unaongeza fedha za kigeni, ajira pamoja na masuala mengine katika uchumi, katika hili Ufaransa wamesema wako tayari kuanzisha jukwaa la biashara kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania na Ufaransa ili kuweza kuvutia zaidi wawekezaji”, Waziri Kairuki.

Waziri Kairuki aliongeza kuwa Serikali iko pamoja na wawekezaji na amewahakikishia kuwa iko tayari kutatua changamoto zao katika masuala ya uwekezaji ili kuweza kuvutia wakezaji na kuwa mabalozi wa uwekezaji nchini.

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier amesema kuwa Serikali ya Ufaransa iko pamoja na itashirikaina na Tanzania katika kitimiza adhima ya Rais Magufuli ya kuifikisha Tanzania uchumi wa kati mwaka 2025.

“Tulikuwa na Mazungumzo ya kubadilishana mawazo kuona namna gani ya kuipeleka Tanzania mbele katika sekta ya uwekezaji, Serikali ya Ufaransa inamuunga mkono Rais, Dkt.John Pombe Magufuli kwa nia yake ya kuipeleka Tanzania mbele kimaendeleo na kuwa nchi ya Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025”, Frederic Clavier, Balozi wa Ufaransa Tanzania.

Aidha Balozi Clavier aliongeza kuwa Serikali ya Ufaransa inawekeza Euro milioni 50 kwa mwaka na itaongeza mpaka kufika Euro milioni 100 ambazo zitatrumika katika uwekezaji mbalimbali hapa nchini ikiwemo Sekta ya mafuta, Viwanda vya Dawa na kilimo.

Katika mazungumzo mengine na Mabalozi wa Uholanzi, Jeroen Verheul, Norway, Elisabeth Jacobsen pamoja na Mkurugenzi Mkazi USAID, Andy Karas, Waziri Kairuki amewahakikishia kuwa atakutana na wawekezaji kutoka nchi hizo, kuwasikiliza changamoto zao na kuzitatua ili kuimarisha sekta ya uwekezaji nchini.

Urusi Kuunda INTERNET Yake ya Pekee....."Marekani ina uwezo wa kutizimia INTERNET wakati wowote ikitaka ndio maana na sisi tunajiandaa"

$
0
0
Bunge la Urusi limepitisha muswada ambao ukiwa sheria basi Taifa hilo lenye Watu zaidi ya M.140 litaunda INTERNET yake peke yake na kuachana na inayotumika duniani

Muswada huo uliopitishwa kwa kura nyingi za wabunge 307 huku 68 wakiupinga, utawasilishwa katika Bunge Kuu la Urusi ili kuidhinishwa na kisha kuwasilishwa kwa Rais Vladmir Putin kutia sahihi ili kuufanya sheria kamili na kuanza kutekelezwa Novemba, mosi.

Sheria hiyo itawezesha Serikali ya Urusi kubuni miundombinu yake binafsi ya Intaneti na kuweza kusalia mtandaoni hata kukitokea dharura ya taifa lolote kujaribu kuuzima.

Mmoja wa waandishi wa muswada huo, Andrei Klishas aliliambia Shirika la Habari la Ujerumani (DW) kuwa hawana shaka Marekani ina uwezo wa kiufundi wa kuizimia Urusi huduma za intaneti wakati wowote wakipenda, hivyo wanajiandaa kiufundi kuhakikisha wanajilinda dhidi ya mashambulizi kama hayo.

Hadi sasa maswala ya kiufundi ya namna miundombinu hiyo itakuwa hayajakuwa bayana, lakini taasisi kuu ya mawasiliano ya Urusi – Roskomnadzor ndiyo itakuwa kituo kikuu cha kufuatilia na itasimamia intaneti hiyo kukitokea mashambulizi.

Kangi Lugola Atoa ONYO Kwa Wahalifu Nchini.....“Waelewe kwamba watakapofanya uhalifu, wataenda kwenye magereza yenye msongamano,”

$
0
0
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola amewaonya Watanzania kuachana na matukio ya kiuhalifu kutokana na hali ya magereza ya sasa kuwa yana msongamano wa wafungwa wengi.
 
Kangi Lugola ametoa kauli hiyo bungeni Dodoma baada ya Mbunge kuhoji juu ya hali ya msongamano ndani ya Magereza ya Tanzania.

"Nitumie fursa hii kuwataka watanzania popote pale walipo wasijihusishe na matukio ya uhalifu utaowafanya kuwa wafungwa au wawe mahabusu, waelewe kwamba watakapofanya uhalifu utawafanya waende kwenye magereza yenye msongamano", amesema Kangi Lugola

Aidha maswali na majibu Mbunge Khatibu Haji alihoji juu ya wanawake kupata ujauzito wakiwa ndani ya Gereza wakati walinzi wao ni wanawake wenzao.

Akijibu swali hilo, Kangi lugola amesema; "hakuna mimba zinazotokea gerezani, mimba tunazozungumzia ni ambazo mfungwa aliingia nazo akiwa gerezani, ndiyo maana kulitokea jaribio kwa Wabunge tupitishe sheria wenza wa wabunge waende gerezani ili kufanya mapenzi lakini hatutakubali jaribio hilo." Amesema Lugola na kuongeza;

"Na tumekuwa na utaratibu,watoto ambao wamezaliwa magerezani kwanza wanapofikia umri wa kuanza elimu ya awali, wamekuwa wakisoma katika shule za awali za magereza yetu" 

Naibu Waziri Omary Mgumba: Biashara Ya Zao La Kahawa Na Mazao Mengine Itaendelea Kupitia Vyama Vya Ushirika

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo – Dodoma
Serikali imeelekeza biashara ya zao la kahawa na mazao mengine kufanyika kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) badala ya wanunuzi kwenda kwa wakulima moja kwa moja.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma jana tarehe 16 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini Mhe Martin Msuha aliyetaka kufahamu kwanini Serikali ilibadilisha mfumo wa ununuzi na uuzaji kahawa kwamba ni lazima kupitia Vyama vya Ushirika vya Msingi pia ni vyama vingapi vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vimeundwa Wilayani Mbinga kufuatia kubadilishwa kwa mfumo huo.

Alisema kuwa utaratibu huo utamuwezesha mkulima kunufaika na kilimo cha kahawa kwa kuzalisha kahawa yenye ubora na kuuzwa kupitia minada ambapo wanunuzi watashindanishwa na hivyo kupelekea mkulima kupata bei nzuri na yenye tija.

Mhe Mgumba alisema kuwa Vyama vya Ushirika huanzishwa na wananchi kutokana na mahitaji yao hivyo, kupelekea kuwepo kwa aina mbalimbali za Vyama vya Ushirika kama vile Vyama vya Ushirika wa kilimo na masoko, mifugo, uvuvi, viwanda, nyumba, fedha na madini. Kwa mujibu wa Sheria ya Ushirika Na.6 ya Mwaka 2013.

Kadhalika, alisema hadi sasa mkoa wa Ruvuma una jumla ya Vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) vya kahawa 67 na chama Kikuu cha Ushirika kimoja (MBIFACU) ambavyo vimeanzishwa na wakulima wa kahawa katika Mkoa wa Ruvuma. Aidha, Wilaya ya Mbinga ina jumla ya Vyama vya Ushirika vya msingi vya kahawa 58 ambavyo ndio vitasimamia na kuendesha biashara ya kahawa katika Wilaya ya Mbinga.

Akijibu swali la Mhe Conchesta Rwamilaza ambaye ni Mbunge wa Viti maalumu kuhusu mradi wa kujenga masoko eneo la Nkwenda na Murongo katika Wilaya ya Kyerwa, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba alisema kuwa Masoko ya Nkwenda na Murongo katika Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa ni kati ya masoko matano (5) ya kimkakati yaliyopangwa kujengwa kupitia mradi wa Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo Wilayani (District Agricultural Sector Investment Project – DASIP) na ujenzi ulioanza kutekelezwa mwaka 2006/07 hadi mwaka 2014.

Alisema masoko mengine yapo katika Halmashauri za; Busoka (Kahama), Kabanga (Ngara) na Sirari (Tarime). Mradi huo uligharamiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Tanzania.

Mhe Mgumba alisema kuwa lengo la ujenzi wa masoko hayo ya kimkakati ilikuwa ni kuanzisha mfumo thabiti wa masoko utakaongeza tija na pato kwa wakulima ndani ya Wilaya.

Alisema kuwa mfumo huo utajenga mazingira wezeshi kibiashara katika maeneo ya mpakani ili kurahisisha biashara na nchi jirani na kuinua hali za kiuchumi za wananchi wa maeneo hayo na uchumi wa Taifa kwa ujumla. 

Alisema hadi sasa mradi wa DASIP unafungwa Disemba 2013/14 kazi ya ujenzi wa masoko hayo ilikuwa haijakamilika na yalikuwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Kwa kuzingatia umuhimu wa masoko hayo ya kimkakati katika Halmashauri husika, Serikali imepanga kukamilisha ujenzi wa masoko hayo na mengine nchini kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ambapo katika bajeti ya mwaka 2019/2020 Serikali imetenga Shilingi bilioni 2.9 kuendelea na ujenzi wa masoko hayo.

Naibu Waziri wa Kilimo: Serikali Imejipanga Kuendeleza Kilimo Cha Umwagiliaji

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Katika mpango kabambe wa Tanzania wa kufanya kilimo cha umwagiliaji kuwa kipaombele kikuu yaani ASDP II kauli ya kuwa kilimo ni maji inajipambanua zaidi kwani inazingatia matumizi bora ya ardhi na maji.

Katika kuongeza ufanisi na tija katika kilimo kupitia umwagiliaji Serikali imejipanga vyema kuimarisha sekta ya kilimo kupitia mbinu bora za kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Rehema Juma Migila aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kuendeleza Kilimo cha Umwagiliaji katika Manispaa ya Tabora, kwa kutumia maji kutoka Bwawa la Igombe baada ya ujio wa maji kutoka Ziwa Victoria kufika Tabora.

Mhe Mgumba alisema kuwa wakati wa kupanga matumizi ya maji kutoka katika chanzo, utunzaji wa mazingira na matumizi ya jamii hupewa umuhimu zaidi kabla ya matumizi mengine.

Ujenzi wa miundombinu ya kutoa maji kutoka Ziwa Victoria umelenga zaidi katika kupunguza upungufu wa maji uliopo kwenye Manispaa ya Tabora ambayo kwa sasa inahudumiwa na Bwawa la Igombe. Maji hayo ni kwa ajili ya matumizi ya kijamii tu kwani hayatatosha kwa kilimo cha umwagiliaji.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa tija na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Wizara ya kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ina Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji unaotekelezwa kuanzia 2018/2019 hadi 2035/2036 ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo katika Manispaa ya Tabora, mpango huo umejumuisha uboreshaji na ujenzi wa skimu za umwagiliaji za Imalamihayo, Inala, Magoweko na Bonde la Kakulungu.

Aliongeza kuwa rasilimali maji ni muhimu katika jamii na kama itawekwa vizuri matumizi yake katika kila hatua huleta manufaa makubwa kwa kilimo  kupitia umwagiliaji  na kupata nishati ya umeme kwenye maporomoko.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images