Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Maandalizi Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa Yaanza

$
0
0
Na.Alex Sonna/ Fullshangwe
Wakati  uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, ukitarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) leo imekutana na wadau wa vyama vya siasa kwa ajili ya kupitia rasimu za kanuni za uchaguzi huo.

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo wakati wa kufungua kikao cha kupitia rasimu ambapo ametaja  rasimu tatu ambazo wadau hao watazijadili kuwa ni pamoja na Rasimu ya kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za mwaka 2019.

Waziri Jafo ametaja rasimu zingine kuwa ni ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka za Miji za mwaka 2019 na Rasimu ya Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji midogo za mwaka 2019.

Aidha Jafo amewaomba wadau hao kutoa maoni na mapendekezo yatakayokuza demokrasia na utawala bora huku akiahidi kuwa serikali itazingatia maoni yao ili kanuni hizo ziweze kuleta tija na ufanisi kwenye uchaguzi.

Hata hivyo Jafo amesema utii wa Sheria za Nchi, Kanuni na Taratibu za Uchaguzi ndio msingi wa uchaguzi ulio wa haki na wenye kuzingatia ushiriki wa makundi yote ya jamii.

“Vyama vya siasa vinaowajibu wa kuwaelimisha na kuwaelekeza wagombea, wafuasi na wanachama wao kuzingatia matakwa ya Sheria za Nchi na kanuni hizi za uchaguzi wa serikali za mitaa,”amesema Jafo

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa John Shibuda  ametoa neno la shukrani kwa niaba ya wajumbe ameshukuru kwa fursa hiyo waliyoipata na kuwataka wajumbe kuvumiliana na kutumia vizuri nafasi waliyoipata kwa maslahi mapana ya wananchi.

Rais Magufuli Atoa Pole Kwa Mbunge Wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa Aliyefiwa Na Dada Yake Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wametoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu na kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mbunge wa Iringa Mjini Mch Peter Msigwa ambaye amefiwa na Dada yake Tryphosa Simon Sanga aliyefariki dunia tarehe 30 Machi, 2019 kwa ajali ya gari Jijini Dar es Salaam.

Wakiwa nyumbani kwa Marehemu Kimara Stopover, Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli wameungana na wanafamilia kumuombea Marehemu apumzike mahali pema peponi, Amina.

PICHA: Rais Magufuli Alivyokutana na Godbless Lema Katika Msiba wa Dada yake Mchungaji Msigwa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wakati akitoka kutoa heshma za mwisho kwenye msiba  wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.

Waziri Biteko Awasimamisha Kazi Maafisa Madini Ofisi Ya Madini Chunya

$
0
0
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko, ameagiza kusimamishwa kazi kwa wafanyakazi wote ofisi ya madini Wilayani Chunya na kuagiza  kuwafunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi na kwa tuhuma za kushirikiana na wachenjuaji wa madini.

Waziri Biteko ametoa kauli hiyo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya , wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika ukumbi wa halmashauri ya Chunya.

Amesema, baada ya serikali kupitia Wizara husika kuhakikisha inadhibiti mapato yake, utafiti umebaini kwamba Wilaya ya Chunya inashika namba moja kwa wizi na utoroshaji wa madini aina ya dhahabu ikifuatiwa na Kahama.

“Baada ya kufanya utafiti tumeabaini kunawizi mkubwa na usio na aibu ambapo unakuta mtu amepata kilo 1 na gramu 1620 lakini serikali inapata  gramu 208, lakini kuna mahali mtu anapata kilo nne anawasilisha taarifa za gramu 155,sasa wizi namna hii tukiendelea kunyamaza nchi haiwezi kuwa na afya.,”alisema.

Kutokana na hali hiyo Waziri Biteko  amewataka watendaji na viongozi husika kubadilika na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

“Ukiangalia sasa, wazalishaji wengi wanakimbilia Chunya na hii ni kwa sababu ya utaratibu wa eneo husika kushindwa kubaini wizi huu unaofanyika kupitia taarifa za kiwango cha uzalishaji ambacho ndicho kinachohalalisha mapato kwa serikali kupitia mrahaba wa Madini “Amesema Waziri Biteko

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, alimueleza Biteko kuwa Wilaya ya Chunya inahitaji msaada hasa wa kielimu na utaalamu wa madini na kuomba watendaji wasafi wapatikane kwenye sekta hiyo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa sasa wanataka kuzungumza na uongozi wa Mkoa  wa Songwe  ili kuunda nguvu ya pamoja itakayosaidia kuimalisha Ulinzi katika maeneo hayo ili kuepusha wizi wa Madini.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne April 2

Taarifa kuhusu kuanza kwa Mkutano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma Leo tarehe 2 Aprili

$
0
0
Leo Jumanne tarehe 2 Aprili 2019 Bunge la Tanzania linatarajia kuanza Mkutano wa Kumi na Tano utakaomalizika tarehe 28 Juni 2019 Mjini Dodoma.

Mkutano huu utakuwa ni mahsusi kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.

Katika Mkutano huo, wastani wa maswali 515 ya Kawaida yanatarajiwa kuulizwa na  kujibiwa na Serikali Bungeni.

Aidha, wastani wa Maswali 88 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa kwa siku za Alhamisi.

Pia, Bunge litajadili Hotuba ya Hali ya Uchumi wa Taifa na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 itakayowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango.

Katika hatua nyingine Bunge pia linatarajia kujadili na kupitisha Miswada Miwili  (2) ya Sheria ambayo itasomwa kwa hatua zake zote ambayo ni Muswada wa Sheria ya Fedha za Matumizi wa mwaka 2019 (The Appropriation Bill, 2019), na Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2019 (The Finance Bill, 2019.

Vyama vya Ushirika Vyashauriwa kukopa fedha kwenye Mabenki kwa ajili ya wanachama wao

$
0
0
Bashiri Salum,Wizara ya Kilimo Arusha
Vyama vya Ushirika vimeshauriwa kukopa fedha kwenye Mabenki kwa ajili ya  wanachama wao kwa kuwa waliowengi hawakopesheki hivyo kufanya shughuli za kilimo kuwa ngumu.

Akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha Maafisa Ushirika, umwagiliaji na afisa kilimo  Mkoani Arusha Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari Mgumba amesema miundombinu mingi ya umwagiliaji inahitaji marekebisho makubwa  ili kuweza kutumiwa na wakulima.

Aidha miundombinu hiyo imekosa ukarabati kutokana na wakulima kutokuwa na mitaji ya kutosha na kutoaminiwa na taasisi za fedha kusaidia ukarabati huo.

Ameshauri tume ya Ushirika kuvisimia vyama vya ushirika ili viweze kukopa fedha Benki Kwa ajili ya wanachama lengo likiwa ni kufanya ukarabati Wa miundombinu ya umwagiliaji ambapo kila mwanachama atawajibika kuchangia huduma hiyo.

Hatuwezi kufanya Kilimo cha kibiashara Kwa kutegemea mvua ambazo Nazo zimekuwa haziyabiriki nawashauri tume ya Ushirika na tume umwagiliaji kusimamia vyama hivyo kwenye skimu mbalimbali za umwagiliaji kukopa fedha ambazo zitatumika kurekebisha miundombinu ya umwagiliaji badala ya kutegemea serikali .alisema Mhe. Naibu Waziri

Naibu Waziri aliwataka maafisa ugani kuwafikia wakulima na kuelimisha namna ya kutumia na kutoa elimu juu ya matumizi bora ya viuatilifu vya mimea ili kupambana na visumbufu vya mazao ambavyo vimekuwa vikimsababishia mkulima hasara kubwa.

Naye afisa Umwagiliaji wa kanda mhandisi Juma Mdete amesema katika ukanda huo eneo ambalo linafaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta elfu 40 kati ya hilo linalotumika ni  hekta elifu 24 tu

Amesisitiza kwamba pamoja na matumizi kidogo ya eneo la umwagiliaji lakini maeneo yanayomwagiliwa yanasaidia upatikanaji wa chakula wakati wa ukame.

Akichangia wakati wa mjadala huo Afisa Kilimo Mkoa wa Arusha Bwana Daniel Loiruck amethibitisha kwamba ukiondoa Magonjwa ya mlipuko na uvamizi wa visumbufu vya mimea  maafisa kilimo wamekuwa wakijitahidi kuwafikia wakulima ili kutatua changamoto zinazowakabili.

Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoani Arusha bwana Loata Erasto Sanare  akamueleza Mhe. Naibu waziri kwamba hali ya ukame mkoani humo ni kubwa hivyo kuishauri serikali kuanza kufikiri njia mbadala ya kupambana na hali hiyo.

‘Msimu wa kilimo upo katikati lakini mpaka sasa hakuna mvua na tumezunguka sehemu mbalimbali hapa arusha mahindi yamekauka hata mvua ikinyesha  haiwezi kuleta mabadiliko tunaishauri serikali kufikiri mbinu za kukabiliana na hali hiyo’. Alisisitiza bwana Loata  Sanare

TAKUKURU Dodoma Yaokoa Milioni 152....Milioni 900 Zinachunguzwa

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dodoma imesema inachunguza ufisadi wa shilingi Milioni 900  baada ya kuwa na viashiria vya rushwa katika miradi mbalimbali.

Pia taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa kiasi cha Sh152.3 milioni ambazo zingelipwa kwa wakandarasi ambao ufuatiliaji wa ukaguzi wa miradi ya maji umebaini hawakutimiza majukumu yao ipasavyo.

Hayo yamebainishwa jana  mkoani Dodoma na kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, mkoa wa Dodoma Sosteth kibwengo wakati akitoa taarifa ya robo ya mwaka kwa wanahabari.

Ambapo alisema kwa robo ya mwaka taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi  milioni 152.3, zilizokuwa zilipwe kwa wakandarasi ambao hawakutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Taasisi hiyo  pia imemtaka mkurugenzi wa kampuni ya Global Space East Africa Limited, inayojenga kituo cha afya Mima kilichopo Wilayani Mpwapwa mkoani hapa kulipoti katika ofisi ya zake zilizopo wilayani humo kwa mahojiano.

Vile vile alibainisha kuwa katika kipindi husika, TAKUKURU ilipokea jumla ya taarifa 96 za rushwa na makosa yahusianayo ambapo sekta  ziliongoza kwa tuhuma ni;

Serikali za mitaa (25%), Ardhi (17%), Elimu (16%), Afya (8%), Maji, Ujenzi na Mahakama (kila moja asilimia 7), na Polisi (6%), taarifa hizo zilifanyiwa kazi kwa njia mbalimbali na majalada nane (8) ya uchunguzi yalikamilika ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.5 ya majalada yaliyokamilika kwa kipindi hicho mwaka 2018.


Watu 28 wakamatwa na polisi kwa kupiga askari wakiwa kazini

$
0
0
Watu 28 wamekamatwa na polisi wilayani Nyang'hwale, Geita kwa tuhuma za kuwajeruhi askari polisi watatu kwa silaha za jadi wakati askari hao wakizuia wananchi wenye hasira kumshambuliwa mtu aliyedhaniwa ni mwizi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatatu Aprili mosi 2019 kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjoli  Mwabulambo amethibitisha askari wake kujeruhiwa na kuwataja waliojeruhiwa kuwa ni Omari ambaye ni mkaguzi wa Polisi tarafa ya Nyangwale.

Mwingine ni askari H16 D/C Yusuph aliyejeruhiwa mguu wa kulia na H4311 D/C Joseph aliyelazwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

Akielezea tukio hilo, Mponjoli amesema Jumamosi Machi 30, 2019 kundi la majambazi wakiwa na silaha za jadi walivamia nyumba za wakazi wawili kijiji cha Nyijundu na kumuua mkazi mmoja na kujeruhi wengine watatu kisha kupora fedha.

Amesema kufuatia hali hiyo, wananchi walipiga yowe na kuanza msako kwa kushirikiana na polisi na walipomkamata mmoja waliyedhani ni mtuhumiwa na kumhoji kisha kukiri walitaka kumuua na walipozuiwa na polisi wakawageuzia kibao. 


==>>Msikilize hapo chini

LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka bungeni Jijini Dodoma.

$
0
0
LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka bungeni Jijini Dodoma.

Vituo 41 Vya Boda Boda Mkoani Njombe Vyapewa Askari Wa Usalama Barabarani Kwa Ajili Usimamizi

$
0
0
Na Amiri kilagalila
Jeshi la Polisi Kupitia Kitengo Cha Usalama Barabarani Limepeleka Askari Polisi Katika Vituo 41 Vya Boda boda Mkoani Njombe Ambao Watakuwa Wakifanya Kazi ya Ulezi Kwa Madereva Hao Kwa Lengo la Kuwasaidia Kufanyakazi Hiyo Kwa Weledi na Nidhamu.

Hii Itasaidia Kupunguza Ajali za Barabarani Kwa Kuwa Elimu Itakuwa Ikitolewa Mara Kwa Mara Kwa Madereva Pikipiki Wawapo Katika Vituo Vyao Ikiwa ni Pamoja na Kuwa na Kofia Ngumu Yaani Helmet Kwa Dereva na Abiria Wake na Usafi Kwa Ujumla.

Mkuu wa Kikosi Cha Usalama  Barabarani Mkoa wa Njombe Kelvin Ndimbo Amezungumza na mtandao huu juu ya Hatua Hiyo huku Akisema kuwa huu ni Kwa Mujibu wa Sheria na Kwamba Tayari Tangu Askari Hao Wapelekwe Kwenye Vituo Mafanikio Yameanza Kuonekana Huku Akitoa Wito Kwa Abiria Hususani Wanawake Ambao Wanagoma Kuvaa Kofia Ngumu Kwa Kisingizio Cha Kuchafuka  Nywele.

"Natoa wito na rai kwa abiria wote wanaopakizwa kwenye hizi piki piki wahakikishe wanavaa kofia kwasababu wanapanda kwenye pikipiki ambazo waendeshaji wote wamevaa hizi kofia kwa kuwa sio sale ni usalama,niwaombe abiria wavae kofia la sivyo kwa maana sheria haitasita kuwachukilia sheria wote wanaokiuka sheria"alisema Ndimbo
  
Madereva Bodaboda Mjini Njombe Akiwemo Kenedy Mligo na Kenedy  Mkonga Wanakiri Kuwapo Kwa Mabadiliko Makubwa Tangu Askari Walezi Kuwepo Katika Vituo Vyao na Kwamba Hata Usafi Umeimarika Kwani Sasa Wanavaa Reflector Pamoja na Kuwa na Kofia Ngumu Kwa ajili Yao na Abiria Wao Licha ya Baadhi ya Akina Dada Kugoma Kuvaa Kofia Hizo.

"Askari walezi wananvyokuwepo wanafanya kweli madereva wajitambue ikiwamo kuwa na leseni,kuvaa vikinga upepo pamoja nakofia kwa kweli hii inasaidia na sisi kila wakati tunatoa elimu kwa hawa abiria wetu kwa kuwa wakati mwingine wamekuwa hata wakigoma kuvaa hizi kofia ngumu"alisema Kenedy mligo mmoja wa dereva boda boda.

Baadhi ya wanawake Akiwemo Honey Mnenuka  Licha ya Kukiri Kuhofia Usafi Hasa Katika Nywele Zao Pamoja na Suala Zima la Urembo Wengine Wanashauri Sheria Kuchukua Mkondo Wake.

"Uvaaji wa kofia uwepo maana ni usalama wetu kwa hiyo ni lazima abiria kwa anayegoma lazima sheria zichukuliwe na alipe yeye na sio dereva,ila tatizo kwenye usalama unakuwa mdogo zile kofia zikiwa chafu tungeomba ziwe zinafanyiwa usafi"alisema Honey mnenuka

Neema ni Miongoni Mwa Abiria Aliyekutwa na mtandao huu Akipanda Bodaboda Ambaye Baada ya Kuvalishwa Kofia Alianza Kwa Kusita.

"Mimi siendi mbali jamani nitavaaje naenda jirani tu hapo"alisikia mmoja wa abiria wa kike akigoma kuvaa kofia ngumu.

Mtandao huu umezungumza na Baadhi ya Wanaume Mjini Njombe Akiwemo Reginald Danda na Obeid Ngailo Juu ya Suala la Kofia Ngumu Kwa Abiria Ambao Wanaeleza Umuhimu wa Kuvaa Kofia Hizo Huku Wakiwataka Akina Dada Kutumbua Thamani ya Uhai Wao Badala ya Urembo.

"Mimi nimewahi kupata ajali ya boda boda nikiwa nimevaa kofia ngumu na kofia ngumu ilipasuka huku mimi nikiwa nimepoteza fahamu siku mbili kwa hiyo kama ningekuwa sikuvaa kofia na maisha yangu yangekuwa yamekwisha,kofia hizi ni muhimu sana na watu kwa kweli waache kisingizio cha nywele ukiona nywele ni muhimu basi bora utumie gari" alisema Reginald Danda  

Suala la Usalama Katika Maisha Ni Muhimu Kuliko Urembo.

DC Wa Ruangwa Awataka Tamwa Kurudisha Watoto Shule...Apiga Marufuku Unyago.

$
0
0
Na Bakari Chijumba,Lindi.
katika kuendeleza kusaidia watoto wa kike, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandiliwa  amewaomba Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA) kuchukua jukumu la kuwasaidia kuwaendeleza kimasomo watoto walioacha shule na wana nia ya kuendelea na masomo.

Amesema hayo 30 Machi 2019, wakati wa muendelezo wa  kikao cha kujadili jinsi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kilichofanyika ukumbi wa Rutesco mjini Ruangwa.

"TAMWA bebeni hawa watoto wenye nia  ya kurudi shuleni hawajachelewa wanaweza kusaidiwa na wakafikia malengo yako kama watoto wengine waliopata bahati ya kusoma kwa wakati" amesema Mgandilwa.

Pia amewataka TAMWA kuhakikisha katika kila mikutano yao wanayofanya wanahamasisha wazazi kufanya shughuli za unyago wakati wa likizo ili kutomnyima haki ya mtoto kupata elimu.

"Serikali haipingi unyago mimi pia sipingi unyago hizo ni mila na desturi zipo katika kila kabila nchini, ila mfanye jambo hilo kwa kufuata maelekezo yanayotolewa, narudia serikali haina tatizo na mila na desturi " DC Mgandilwa na kuongeza kuwa;

"Hakuna ujanja zaidi ya elimu Elimu ndiyo kila kitu hata mie kuwa hapa ni kwasababu ya elimu sasa mkitoka hapa nyie wanafunzi mliopata mafunzo haya mkawe mabalozi kwa wenzenu muwaeleze umuhimu na faida ya elimu"

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TAMWA Bi Rose Reuben, amewataka watoto wakike kuamka na kutambua thamani yao na kuacha tabia za kuiga mambo yasiyo na maana katika maisha yao.

"Mkianza kujitambua nyie hata watu wengine wataanza kuwatambua jisimamieni katika vitu vyenye manufaa umeshindwa kumaliza masomo kwa ajili ya ujauzito basi msimamie mtoto uliyenaye aje kuwa kiongozi mkubwa baadae" Amesema Bi Rose

Aidha kwa niaba ya wenzake, Mwanafunzi Amina Omari Makota, ameuomba uongozi kuwachukulia hatua za kisheria wazazi ambao hawawapi ushirikiano watoto wanaoitaji kusoma  na wanapopeleka malalamiko sehemu husika basi mzazi huyo achukuliwe hatua kwa haraka.

Amina amesema siyo watoto wote wanaoacha masomo ni kwasababu hawataki kusoma, wapo wanaoacha kusoma kwasababu wazazi wao hawawatimizi mahitaji muhimu yanayoitajika shuleni .

LIVE Video:Rais Magufuli Akiweka Jiwe la Msingi Upanuzi wa Uwanja

$
0
0
Rais Dkt. Magufuli amewasili Mtwara leo April 2, 2019 ambapo ataweka jiwe la msingi la upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara.

Bunge Lapitisha Azimio la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

$
0
0
Kamati ya Maadili imemtia hatiani kwa kulidhalilisha Bunge,Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali CAG,Prof.Mussa Assad,kwa kusema kuwa "Bunge ni dhaifu".

Kufuatia hatua hiyo Kamati imetoa mapendekezo ya Bunge kutofanya kazi na CAG,Prof.Asaad.

Akisoma ripoti ya kamati hiyo bungeni leo Aprili 2 mwaka 2019, mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka amesema kamati yake imemtia hatia kwa kuvunja kifungu cha 26 E cha Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.

Amesema Profesa Assad wakati wa mahojiano na kamati hiyo alionyesha dharau na hakuonyesha kujutia maneno yake 

 "Prof. Assad alikiri mbele ya kamati kuliita Bunge dhaifu lakini alipingana na tafsiri ya neno 'dhaifu' iliyopo kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu inayosema 'goigoi, hafifu, isiyo imara' akisitiza kiuhasibu udhaifu ni 'upungufu'.

"Tuliangalia maana ya neno upungufu kwenye kamusi tukabaini ni 'isiyo kamili, isiyo imara', hivyo alidhamiria kulidhalilisha Bunge.
 
 "Tulimuuliza CAG Assad kama ataacha kulitumia neno udhaifu akasisitiza ataendelea kulitumia na hakujutia kulitumia dhidi ya Bunge.CAG hakuomba msamaha wala kujutia na akasisitiza ataendelea kulitumia neno hilo".Amesema Mwakasaka

Baada ya ripoti hiyo ya kamati, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alitoa nafasi kwa wabunge kujadili jambo hilo huku wabunge wakipishana maoni yao,   kukubaliana na uamuzi huo na wengine kupinga .

Baada ya wabunge kutoa maoni yao,  Dk Tulia amelihoji Bunge kuhusu hoja hiyo, akiwakata wanaokubaliana na jambo hilo kusema ndio na wasiokubaliana na suala hilo kusema sio,  "waliosema ndio wameshinda. "

Godbless Lema Atakiwa Kuripoti Kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge.....Wabunge wa CHADEMA Wasusa na Kutoka Nje ya Bunge

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Dr Tlia Ackson amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuripoti kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutokana na kauli yake kuwa "Bunge ni dhaifu". 

Lema ametoa kauli hiyo leo Aprili 2, 2019  Bungeni wakati akichangia hoja ya kamati hiyo na kudai Halima Mdee hajatendewa haki kutokana na kamati hiyo kupendekeza Bunge kumsimamisha kuhudhuria vikao viwili vya Bunge kutokana na kuunga mkono kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuwa Bunge ni dhaifu

"Alichokisema Mdee naungana naye na ni kweli kuwa Bunge ni dhaifu," amesema Lema. 


Baada ya kauli hiyo, Naibu Spika  Dk Tulia ameagiza Lema akahojiwe  na kamati hiyo ya Maadili  kwa kuliita Bunge ni Dhaifu.

Kutokana na Maamuzi hayo ya Naibu Spika, Wabunge wote wa CHADEMA na Baadhi ya Wabunge wa CUF wametoka nje ya ukumbi wa Bunge

Wizara ya Maliasili na Utalii Kutangaza Utalii kupitia AFCON U17

$
0
0
Na Anitha Jonas – WHUSM- Dodoma.
Serikali ya dhamiria kutumia jukwaa wa Mashindano ya AFCON U17 yatakayofanyika hivi karibuni kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kunufaika na wageni mbalimbali watakao kuja kushiriki michuano hiyo ya Kimataifa.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda wakati wa kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa lengo la kuhakiki mikakati itakayotumika kutangaza vivutio hivyo ambavyo ni tunu ya Taifa.

“Sisi Wizara ya Maliasili na Utalii tutahakikisha tunatumia jukwaa hili la michezo kuongeza idadi ya watalii katika vivutio vya utalii nchini na tumejipanga vizuri kwa matangazo mbalimbali ambayo yanamvuto wa ushawishi kwa watalii hawa wamichezo kuvutiwa kufika katika maeneo hayo tunafukwe nzuri,Mbuga za wanyama,majengo ya kale yenye hishoria mbalimbali,maporomoko ya maji na Mlima Kilimanjaro,”alisema Prof.Mkenda.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Prof.Mkenda alisisitiza kuwa ujio wa mashindano hayo ya AFCON U17 nchini ni jambo lenye manufaa makubwa kwa taifa kwani kwa kujipanga vizuri huu ndiyo wakati wa kunufaika kwa watanzania wote kupitia wageni hao, wajasiriamali mbalimbali watanufaika kwa namna moja kwani wageni hao watahitaji huduma mbalimbali kwa kipindi chote watakapo kuwa hapa nchini hivyo ni vyema watanzania watumie fursa hii.

Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi alitoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni Moja kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo tunashukuru sana kwani fedha hizo zitasaidia kukamilisha uendeshaji wa shughuli mbalimbali katika kipindi cha mashindano.

 “Wizara yangu kama mlezi wa Sekta ya Michezo Nchi  mpaka sasa tumesha kamilisha mambo muhimu yote tuliyoagizwa CAF na vimebaki vitu vidogo sana ambavyo vitakamilika ndani ya muda mfupi hivyo naweza kusema tupo tayari kwa mashindano,”alisema Bibi.Mlawi.

Pamoja na hayo nae Bibi.Mlawi alieleza  kuwa mashindano hayo yanataanza Aprili 14, Mwaka huu na Mechi ya ufunguzi inatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo ni vyema wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na kujipanga kwa ugeni huu na watanzania nivyema kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hili la kihistoria kwa taifa letu kuandaa mashindano haya ya Kimataifa.

Halikadhalika nae Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidao alieleza kuwa katika mashindano hayo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni Infantino atakuja hivyo ujio wake katika mashindano hayo utakuwa ni fursa ya kutangaza nchi yetu, vilevile uongozi wote washirikisho la mpira wa Miguu Afrika  (CAF) nao utahamia Tanzania katika kipindi chote cha mashindano.

“Katika mashindano hayo ndipo wadau wa soka duniani wanakuja kusaka vijana wenye vipaji kwa ajili ya kuwaunga katika timu zao kubwa za kimataifa mfano mchezaji kama Neymar ni mmoja ya wachezaji waliyoibuliwa katika mashindano ya mpira kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 hivyo wapo wadau mbalimbali duniani watakuja kwa ajili ya hilo,”alisema Kidao.

Wito kwa watanzania ni kuwa tayari kwa ujio huu wa kimataifa na kujipanga vyema kunufaika na wageni hawa kwa kuhakikisha wanakuwa watulivu na wakarimu kwa ajili ya kuiletea nchini mafanikio katika uchumi.

Wankyo: Baba Amnyonga Mwanae Hadi Kufariki Dunia, Akidai Sio Mtoto Wake

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
JESHI la polisi mkoani Pwani linamshikilia Robison Enerst (33) fundi ujenzi kwa kosa la kumnyonga shingo,  mwanae Modesta Robison mwezi umri wa miezi sita, akidai sio mtoto wake. 

Kamanda wa polisi mkoani hapo, ACP Wankyo Nyigesa, alieleza kwamba,tukio hilo limetokea April mosi, mwaka huu  huko mtaa wa Vitendo kata ya Misugusugu ,Kibaha. 

“Kabla ya kuolewa na mtuhumiwa, mama wa mtoto (marehemu)  alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine ambae mtuhumiwa anamtuhumu ndio baba halali wa mtoto “

“Hali hiyo ilisababisha migogoro ya mara kwa mara kati ya wazazi hao “alifafanua Wankyo. 

Wankyo alibainisha, wamemkamata mtuhumiwa ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria na mwili wa marehemu umehifadhiwa hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi, kabla ya kukabidhiwa ndugu kwa mazishi. 

Kamanda huyo alitoa rai kwa wananchi, kuwa wanapokuwa na mashaka na jambo fulani la kihalifu watoe taarifa mapema katika vituo vya polisi ili yaweze kushughulikiwa mara moja kabla ya kuleta madhara yeyote kwa lengo la kudhibiti watuhumiwa.

Hata hivyo, baada ya kumhoji mama wa marehemu yeye alidai mtuhumiwa alishafanya majaribio ya mtuhumiwa kumuua marehemu mwanae mara mbili. 

Anaeleza, mara ya kwanza alitaka kumpa sumu ya vidonge lakini mama huyo aliwahi kumuokoa .

“Mara ya pili mtuhumiwa alinoa panga ili amkate mtoto lakini hakufanikiwa pia kufikia april 1, ambapo alimuua mtoto kwa kumnyonga shingo hadi kufariki dunia “

Rais Magufuli awashukia wakulima wa korosho wanaodai hawajalipwa

$
0
0
Rais John Magufuli amewajia juu wakulima wa korosho mkoani Mtwara wanaodanganya kuwa hawajalipwa fedha zao na serikali jambo ambalo si kweli na kumuamuru Mkuu wa Wilaya kuwachukulia hatua wadanganyifu wote.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 2, wakati akihutubia wananchi mkoani humo katika ziara ya siku tatu aliyoianza ambapo pia ameweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege na kuwataka wakulima wa korosho kuacha kutoa kisingizio cha kutolipwa fedha za korosho katika kila jambo.

“Wakulima 17,616 hawajalipwa wenye kilo 1,500 kwa sababu nyingi tu, wapo waliowekewa fedha kwenye benki unakuta akaunti aliyoitaja jina ni tofauti na lake wapo waliokuwa hawana akaunti wakazungumza ilipiwe kwenye akaunti ya shangazi sasa fedha ya serikali haiendi hivyo.

“Waliotoa maelezo na wakabadilisha wakafungua akaunti na kadhalika sasa ni karibu asilimia 98 hadi 99 na ninataka niwaambie orodha yao ninayo, kila wilaya, mkoa, kijiji, akaunti na jina alilolipwa na nitamuachia Mkuu wa Mkoa ili mshirikiane na Mkuu wa Wilaya ili muangalie hao waliolipwa,” amesema.

Aidha, amewataa wafanyabiashara wadogo wadogo kutumia vitambulisho walivyopewa ili wasisumbuliwe wakati wanafanya biashara.

“Itafika mahali wale ambao hawatakuwa na vitambulisho hawataruhusiwa kufanya biashara katika baadhi ya maeneo kwa hiyo tumieni fursa hiyo na mnapokuwa na vitambulisho hivyo hakuna kudaiwa na mtu yeyote,” amesema

Gari La Mafundi Umeme Lapata Ajali, Watatu Wafariki

$
0
0
Watu watatu wanasadikiwa kupoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa katika ajali ya basi dogo lililokuwa limebeba mafundi wa mradi wa kuzalisha umeme Mto Kagera eneo la Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera, leo Jumanne, Aprili 2, 2019, majira ya asubuhi.

Majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa katika Hospitali ya Murugwanza na Nyamiaga kwa matibabu zaidi.

Umeme huo a umeme unaojengwa na wakandarasi kutoka nchini China, utatumika nchini Tanzania, Rwanda na Burundi.

Rais Magufuli Awasamehe Kangomba.....Aagiza Walipwe Fedha zao za Korosho

$
0
0
Rais wa Tanzania John Magufuli ameagiza zipelekwe Sh50 bilioni kwa ajili ya kulipia wakulima wenye kilo zaidi ya 1,500 wapatao 18,103 huku akiwasamehe walionunua korosho kwa mfumo wa kangomba.

Magufuli amesema hayo leo Jumanne Aprili 2, 2019 mkoani Mtwara ambako yupo kwenye ziara ya kikazi.

Amesema watakaokiri kuwa walikuwa kangomba na wamefanya hivyo kimakosa tuwaangalie kuwalipa kwa sababu ni wengi akiwamo mwenyekiti wangu wa CCM wa mkoa.

“Kufanya kosa si kosa, ila kurudia kosa ndiyo kosa, lakini nataka wakiri nilinunua korosho sina shamba nilinunua kwa fulani wa namna hiyo walipeni nafikiri watakuwa ni hawa 780 ila wasirudie kwenye msimu unaokuja,”amesema Magufuli na kusisitiza kuwa amewasamehe lakini waandike kuwa walinunua na wana kilo ngapi.

Amesema kwenye uhakiki wa wananchi waliokuwa na kilo zaidi ya 1,500, walikuwa 18, 103 hawajalipwa, waliolipwa ni wachache na uchambuzi wake umekamilika isingekuwa rahisi kutoa fedha bila uchambuzi.

Amesema kati yao yamepatikana majina 780 hawana mashamba wala hawana mkorosho lakini walikuwa wanadai nao wana kilo zaidi ya 1,500.

Amefafanua hao wenye kilo 1,500 ziletwe Sh50 bilioni kuanzia kesho, keshokutwa hawa nao waanze kulipwa, zikiisha zinaletwa nyingine.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images