Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Alichokisema Joshua Nassari baada ya kuvuliwa ubunge

$
0
0
Aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amesema ni kweli hakuhudhuria vikao vya mikutano mitatu ya Bunge la Tanzania kama ilivyoelezwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai ,lakini amesema alitoa taarifa

Nassari ametoa kauli hiyo baada ya jana Spika Ndugai kumwandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC,) Jaji Semistocles Kaijage kumtaarifu kuhusu jimbo hilo la Arumeru Mashariki kuwa wazi baada ya mbunge wake kupoteza sifa.

Nassari amesema Januari 29, 2019 alimwandikia barua akimtaarifu kwamba asingeweza kuhudhuria mkutano wa 14 wa Bunge kutokana na kuwa nje ya nchi akimuuguza mke wake aliyekuwa amejifungua.

Askari polisi akutwa amekufa baa

$
0
0
Askari Polisi mkoani Ruvuma, amekutwa amekufa kwenye baa moja inayopatikana katikati ya mji wa Songea mkoani Ruvuma.

Akithibitisha taarifa za kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa amesema askari aliyefariki anajulikana kwa jina la Donald Motoulaya (29), mzaliwa wa Mtwango mkoani Njombe, na alifariki kutokana na maradhi ya presha na si ulevi kama ilivyosemekana.

Kamanda Marwa amesema kwamba Donald alikutwa amelala kwenye kochi la bar hiyo, baada ya kuteleza alipokuwa akiingia na kumueleza kuwa alikuwa akijisikia vibaya.

“Si kweli kuwa alikuwa amelewa, alikuwa  ameenda pale bar, wakati anaingia kateleza akaanguka, hata ukimuangalia shavuni ana mkwaruzo hivi, muhudumu mmoja anaitwa Jovina akamuuliza vipi akasema najisikia kukosa hewa, akamsaidia kumtoa nje, kumbe baadaye akaingia ndani akaa kwenye sofa akalala, alivyolala watu hawakujua kama kuna mtu, asubuhi wanakuja kufanya usafi ndio wakamuona, kumkimbiza hozpitali Daktari akasema ameshafariki, na kilichomuua kwa mujibu wake ni kushuka kwa presha”, amesema Kamanda Marwa.

Kamanda Marwa amesema kwamba mwili wa askari huyo tayari umeshasafirishwa kwenda Mtwango kwa mazishi ambayo yanafanyika mchana wa leo Machi 15.

Kwa mujibu wa Kanda Marwa, askari huyo hakuagiza kinywaji chochote, kutokana na taarifa walizozipata kutoka kwa wahudumu wa bar hiyo, pia wengine hawakujua kama yumo ndani.

Kikao cha mwisho cha Nassari kabla ya Spika Ndugai kumvua ubunge kwa 'utoro'

$
0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akichangia mjadala katika Chuo cha Uhifadhi Wanyamapori - Mweka wakati Kamati ya Bunge ya Maliasili, Utalii na Mazingira ilipotembelea chuo hicho jana Machi 14, 2019. Jana hiyo hiyo, Spika Job Ndugai alitangaza kumvua Nassari ubunge kwa ‘utoro’.

LIVE: MBOWE, MATIKO Waanika Yote ya GEREZANI

$
0
0
LIVE:  MBOWE, MATIKO Waanika Yote ya GEREZANI

Ndege za Boeing 737 Max zapigwa marufuku nchini Rwanda

$
0
0
 Shirika la usafiri wa ndege nchini Rwanda limetoa agizo kwa marubani na kampuni za ndege kutoendesha ndege za Boeing 737 Max 8 na 9 katika anga ya Rwanda.

Rwanda sasa imejiunga na mataifa mengine duniani ambayo yamepiga marufuku usafiri wa ndege hizo za aina ya Boeing 787 Max 8 na Max 9.

Hii inafuata baada ya ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines ilioanguaka Jumapili muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu Addis Ababa na kusababisha vifo vya watu 157.

Taarifa zinaeleza kwamba Rwanda ilikuwa na mipango ya kukodisha ndege mbili za aina hiyo Boeing 737- 800.

Hatahivyo huenda mipango hiyo ikasitishwa kwa muda sasa wakati kukisubiriwa uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoanguka Jumapili nje kidogo ya mji mkuu Addis Ababa.

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kuja Na Mkakati Wa Kuwa Na Mfumo Wa Kielektoniki Wa Kufuatilia Na Kuhifadhi Taarifa (Commodity Tracking System)

$
0
0
Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma
Kutokana na kukua kwa Technolojia kila siku, na matumizi ya techolojia yanaongeza ufanisi, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza na unaendelea na mkakati wa kuhakikisha kunakuwa na mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia na kuhifadhi taarifa za Hifadhi ya Taifa ya Chakula (Commodity Tracking System). 

Lengo la kuwepo kwa mkakati huo ni kuongeza ufanisi kwa kupunguza mianya ya udanyanyifu na wizi na ili kufikia lengo hilo ifikapo mwishini mwa mwaka 2020, Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umekubali kusaidia kupata ufadhili wa fedha na utaalamu ili kufanikisha lengo hilo.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia Zikankuba wakati akizungumza kwa niaba ya watumishi wenzake Kwenye hafla ya kukabidhi mtambo wa kusafisha nafaka uliotolewa na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na kuzinduliwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb).

Alisema kuwa WFP ni mdau muhimu wa NFRA katika kuzungusha akiba ya chakula huku Utekelezaji wa mauzo ya tani 36,000 ukiwa unaendelea.

Zikankuba alisema kuwa mpaka sasa Tani zote zimekwisha andaliwa na WFP wamekwisha kuchukua Tani 20,400 huku Tani 15,600 zikiwa zimekwisha andaliwa na zimehifadhiwa vizuri kwa ajili ya WFP kuchukua.

“Mauzo haya moja kwa maana yake ni kwamba Mkulima hasa mdogo anapata fursa ya soko la kimataifa moja kwa moja kwa kuwa NFRA hununua mazao yake moja kwa moja kutoka kwa wakulima” Alikaririwa

Bi Zikankuba alitumia mkutano huo kuujulisha ujumbe wa WFP kuwa NFRA ipo tayari na ina uwezo wa kuuza tani nyingine zaidi baada ya mkataba unaoendelea wa Tani 36,000 kukamilika.

“Pia tupo tayari kufanya mazungumzo na WFP ili kukusanya na kuwauzia mazao mengine ya nafakai mtama kuanzia msimu ujao wa mavuno” Alisema

Aliongeza kuwa Mikakati na programu mbalimbali zinazoendeshwa na WFP zinasaidia NFRA kupata mazao yenye vigezo kupitia vikundi vya wakulima. Mfano: Katika msimu huu, kati ya vikundi vya wakulima 216 vilivyouza mahindi yao NFRA takribani vikundi 62 vilipata mafunzo ya kutunza na huhifadhi mazao ya nafaka kupitia programu ya Farm to Market Alliance ya WFP.

Watu 49 wauawa kwenye shambulio la misikiti New Zealand

$
0
0
Watu 49 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch nchini New Zealand.

Kamishna wa polisi, Mike Bush amesema wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa wakihusishwa na tukio hilo huku akisisitiza kuwa huenda washukiwa wengine zaidi wakakamatwa.

Duru za habari zinasema washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali.

Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia. Amemtaja mshukiwa wa shambulio hilo kuwa "gaidi mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia".

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wameviambia vyombo vya habari kuwa walilazimika kutoroka kuokoa maisha yao na waliona watu walioanguka chini wanaovuja damu nje ya msikiti wa Al Noor.

Polisi inasisitiza kwamba hali bado haijaimarika na wamethibitisha pia kwamba "vilipuzi kadhaa vilivyofungwa kwenye gari vimeharibiwa".

Mwanamume wa Palestina ambaye alikuwa katika moja ya misikiti hiyo alisema aliona mtu akipigwa risasi kichwani.

Mbowe Asimulia Maisha ya Gerezani

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Hai Freeman Mbowe amesema hali ya magereza nchini siyo ya kuridhisha kutokana na mrundikano wa maabusu pamoja na wafungwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya hali ilivyo katika magereza nchini baada ya kukaa huko zaidi ya miezi mitatu amesema kuwa magereza kuna ugonjwa wa ngozi ambao chanzo chake ni kunguni na chawa ambao chanzo chake ni uchafu uliokithiri.

"Ugonjwa huu wanauita burudani kwa sababu mtu ukilala unajikuna sana mwisho wa siku unaathiri viungo vya mwili mtu anaweza kukaa wiki hajaoga na wanalala godoro futi tatu wanalala wanne, mmoja akiupata ugonjwa hapo ni wote, ugonjwa huu unawatesa sana wafungwa," amesema Mbowe.

Mbowe amewaomba jaji mkuu, jeshi la polisi pamoja na kamishna wa magereza kufanya operesheni ya safisha magereza kwa sababu mkakati huo utasaidia kuondoa nusu ya maabusu wanaongezeka magerezani kutokana na upelelezi na uchunguzi wa kesi zao kutokamilika kwa wakati.

"Maabusu wakifikishwa wanaambiwa upelelezi unaendelea, watu hawa wanalalamika, wanafutiwa mashtaka na kufunguliwa mashtaka, katika operesheni hii ya magereza hawa watu waangaliwe, kama kweli wanahusika na ugaidi wanapelekwa mahakamani kwa ulinzi mkali, basi wahukumiwe, tunawafanya hawa watu wawe magaidi zaidi na wanafundishwa wawe raia wasiojua kuheshimu sheria," amesema Mbowe.

Aidha Mbowe ameviomba vyombo husika kutafakari kuhusu suala hilo kwa sababu wakifanya hivyo watatambua nusu yao hawana kesi. Mbowe ameomba mahakama za mwanzo zimulikwe sana kwa sababu watu hawapati haki zao kwa wakati.

Ziwa Manyara Hatarini Kutoweka Serikali Yaashauriwa Kuweka Mikakati Madhubuti

$
0
0
Na Lulu Mussa-Manyara
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeshauri Serikali kuandaa mpango Mkakati wa haraka wa kunusuru Ziwa Manyara ambalo liko hatarini kutoweka kutokana shughuli za kibadamu.

Akizungungumza kwa niaba ya Kamati yake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Murad Sadick amesema ni wakati muafaka sasa jambo hili kupewe kipaumbele ili kunusuru hali ya sasa inayotishia uhai wa ziwa hilo.
 
Wakiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Manyara, Kamati hiyo imetembelea Ziwa Manyara na kujionea kupungua kwa kina cha maji kwa kiasi kikubwa kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kilimo kisicho endelevu hususan katika vyanzo vya maji kinachopelekea ziwa hilo kujaa tope pamoja na ongezeko la mimea vamizi.
 
“Sote tumejionea hali halisi, hali ni mbaya, mimi na Kamati yangu tunawajibu wa kuishauri Serikali, hatua za haraka na za maksudi kunusuru hali hii, hata kwa maziwa mengine pia kama Ziwa Jipe na Ziwa Chala. Endapo hatua za haraka hazitachukuliwa ndani ya miaka kumi ijayo Ziwa hili litatoweka. Ikumbukwe kuwa ziwa hili ni chanzo kikubwa cha kukuza pato la Taifa kupitia Utalii hapa nchini” Alisisitiza Mhe. Sadick.

Akiwasilisha hatua za zilizochukukuliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kuhusu kunusuru ziwa hilo Naibu Mkurugenzi Bw. William Mwakilime amesema kuwa Ofisi yake imechukua hatua za makusudi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa Umma juu ya namna bora ya kuwa na kilimo endelevu kinachozingatia matumizi bora ya ardhi na kujenga mabwawa maalumu kwa ajili ya kuchuja maji.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba alieambatana na Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge katika ziara hiyo, amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za kukamilisha andiko jumuishi litakalogusa sekta zote kwa kuwa ni suala mtambuka na kuahidi kuwa Serikali inalipa uzito jambo hilo kwa mustakabali wa nchi na ustawi wa wananchi wake.

Katika hatua nyingine Kamati imeipongeza Serikali kwa kupokea ushauri wa Kamati hiyo ya kuunda kikosi kazi cha kupambana na mimea vamizi ambayo imekuwa ikiathiri maeneo mengi hapa nchini ikiwa ni pamoja na maeneo ya Hifadhi. Waziri Makamba ameainisha kuwa Kikosi kazi hicho kilichoundwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais kimekamilisha kazi na taarifa yake iko katika hatua za maamuzi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira iko katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha pia itatembelea miradi ya uchimbaji wa visima Bagamoyo Mkoa wa Pwani, ikiwa ni miongoni mwa miradi inayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais chini ya Mkataba wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Mbowe Asikitika Lowassa Kurudi CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesikitishwa na kitendo cha kuondoka kwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Machi 15, Mbowe amesema walimpokea Lowassa mwaka 2015 kwa nia njema lakini leo kaamua kurudi CCM.

“Nilisikitika, nikisema nafurahi nitakuwa mwongo, lakini  kwenda kwenye chama kingine cha siasa siyo mbaya, basi akaseme kweli na akisaidie chama hicho kisiendelee kuwatesa Watanzania na sisi tutaendelea kuijenga demokrasia.

“Enzi za uhai wake Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema chama cha siasa ni dodoki ukiliweka kwenye maji litanyonya maji na ukiliweka kwenye maziwa litanyonya maziwa kilichobaki ni kujenga chama kwa kuongeza wanachama,” amesema Mbowe.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 16

Msemaji wa Serikali: Utoji wa Taarifa za Miradi ya Maendeleo kwa Wananchi ni Takwa la Kisheria

$
0
0
Na Frank Mvungi- Mwanza
Watendaji Wakuu wa Serikali katika ngazi mbalimbli wametakiwa kutoa taarifa za miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa maslahi ya wananchi wa maeneo husika ili kuendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza ushirikishaji.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalum jana Jijini Mwanza, Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inawataka Viongozi wote kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

 “Kutoa taarifa kwa wananchi ni takwa la Kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria Na 12 ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, hivyo kila Kiongozi ahakikishe kuwa wananchi wanapata taarifa za utekelezaji wa sera na miradi yote inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi” Alisisitiza Dkt. Abbasi.

Akizungumzia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano Dkt. Abbasi amesema kuwa kwa sasa dhamira ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na maisha bora kutokana na dhamira safi ya Serikali ya Awamu ya Tano kulenga kuwakwamua wananchi wanyonge kiuchumi.

Serikali inatekeleza miradi ya kimkakati ya; mradi wa kufua umeme wa mto rufiji, ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa hospitali za Wilaya 67, ununuzi wa ndege sita (06) ambazo tayari zimenunuliwa ili kuhakikisha maendeleo endelevu yanafikiwa kwa maslahi mapana ya Taifa na wananchi wote.

Mkurugenzi Abbasi ameitaja miradi mingine ya ujenzi wa vivuko, meli mpya na za kisasa  ambapo tayari bilioni 20 zimetolewa na Serikali kwa ajili kutekeleza kujenga meli, ujenzi wa uwanja changamani na wa kisasa kwa ajili ya kukuza sekta ya michezo eneo la Nane nane jijini Dodoma.

“Miradi yote inayotekelezwa na Serikali imekuwa chachu ya maendeleo na imekuwa chanzo cha kuzalisha ajira kwa wananchi hasa Vijana lengo ni kuhakikisha kuwa wanaiunga mkono Serikali ili azma yakuwaletea maendeleo itimie kwa wakati”. Alisisitiza Dkt. Abbasi.

Katika Kuboresha sekta ya Elimu Serikali ya Awamu ya Tano inatoa zaidi ya bilioni 23 kila mwezi kugharamia elimu bure ili kusaidia kuongeza kasi ya maendeleo hapa nchini kwa kuzingatia umuhimu wa suala la elimu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Paschal Shelutete amesema kuwa  Maafisa Habari wote  Tanzania wanakutana Jijini Mwanza kwa mkutano mkuu wa Mwaka utaoanza Jumatatu Machi 18 hadi 22, 2019 kwa lengo la kujengewa uwezo Maafisa hao ili kuisemea Serikali katika kuwaeleza wananchi utekelezaji wa miradi inayetekelezwa na Serikali katika maeneo yao.

“Naipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kujali na kuona umuhimu wa Kada ya Mawasiliano Serikalini na kuweka mkazo katika kuimarisha sekta hii kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla” Alisisitiza Shelutete.

Akifafanua hayo, Shelutete amesema kuwa wakati wa mkutano huo Maafisa Habari watajengewa uwezo na kupewa mbinu za kisasa katika kuisemea Serikali katika maeneo yao zikiwemo Wizara,  Mikoa, Wilaya, Majiji, Halmashauri, Taasisi, Wakala, Idara zinazojitegemea kote nchini.

Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano kitafanyika Jijini Mwanza kuanzia machi 18-22, 2019 na kinatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa. Mahojiano na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbasi pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) yamefanyika leo machi 15, 2019 Jijini Mwanza wakati wa ziara yao ya kutembelea vyombo vya habari Jijini humo.

Waziri Aagiza Kuongezwa Dalala 10 Kusaidia Mabasi ya Mwendokasi Dar

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, ameagiza kuongezwa kwa mabasi 10 ya kawaida katika usafiri wa mwendokasi jijini Dar es Salaam ili kupunguza changamoto ya usafiri.

Jafo alitoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara katika kituo cha mwendokasi cha Kivukoni na kuzungumza na abiria kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika usafiri huo wa mabasi ya mwendokasi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Jafo alisema usafiri huo wa mwendokasi umekuwa ukisuasua jambo ambalo halimfurahishi ikizingatiwa kwamba wananchi wengi wamekuwa wakiutegemea.

Alisema tatizo hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara na kusababisha usumbufu kwa wananchi na mpaka sasa hajaona njia stahiki na ya kuridhisha zilizochukuliwa na watoa huduma katika kupata ufumbuzi changamoto hiyo.

“Tatizo hili limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika kituo cha mabasi cha Kimara wakati wa asubuhi na Kivukoni na Gerezani wakati wa jioni. Imeonekana pia kuna wakati mabasi yanaonekana yakisafiri tupu au yakiwa yameegeshwa pembeni mwa vitu, huku abiria wakiwa wamejazana katika vituo vya mabasi,” alisema.

”Kutokana na hali hiyo namwelekeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi ya Mwendokasi Dar es Salaam (Dart), Mhandisi Ronald Lwakatare, ahakikishe angalau mabasi 10 ya Feeder Road maarufu kama Bomberdier yanayobeba abiria kutoka Mbezi kwenda Kimara Mwisho yahamishiwe katika barabara ya mwendokasi. Matano yawe yanabeba abiria wa Kivukoni na matano mengine yabebe abiria wa Gerezani,” aliongeza.

Jafo alisema milango ya mabasi hayo hairuhusu kupakia katika vituo vya mabasi ya mwendokasi ya kawaida, hivyo mabasi hayo yatachukua abiria moja kwa moja kutoka Kimara hadi Kivukoni au Gerezani na wakati wa kurudi Kimara yatachukua abiria wanaoshuka Kimara pekee.

Aidha, Jafo alitoa maelekezo ya Dart kuwasiliana na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ili mabasi ya kawaida yaongezwe kwa eneo la Kimara mpaka Mbezi ili abiria watakaoshuka Kimara wakitokea katikati ya Jiji kwenda Mbezi na wale watakaotoka Mbezi kwenda Kimara wapate usafiri wa haraka.

“Namwelekeza Mtendaji Mkuu wa Dart, Mhandisi Lwakatare, ahakikishe Udart ambayo ndiyo kampuni yenye dhamana ya kusafirisha abiria ihakikishe inafanya matengenezo ya mara kwa mara ya mabasi yake ili kuondoa usumbufu unaojitokeza wa upungufu wa mbasi kutokana na mabasi mengi kuwa mabovu,” alisema.

Jafo alimtaka Lwakatare awasilishe kwa Katibu Mkuu wa Tamisemi majina ya watendaji walio chini yake ambao anahisi hawasaidii ipasavyo kiushauri na kiutendaji ndani ya siku saba ili wafanye marekebisho kwa maslahi mapana ya Taasisi ya Dart.

Auawa Wakati Akijaribu Kupora Pikipiki

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
OMARY Abdallah maarufu Mboweto (50) mkazi wa Kagera ,Dar es salaam aliuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi ,kijiji cha Malale kata ya Vihingo, Mzenga Kisarawe mkoani Pwani,baada ya marehemu akiwa na washirika wenzake wawili kufanya jaribio la kupora pikipiki huko Maneromango.
 
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema, tukio hilo limetokea  usiku wa kuamkia march 15 mwaka huu.
 
Alieleza, marehemu kabla ya kuuawa akiwa na wenzake wawili wakitumia gari namba T. 613 DFG aina ya carrina walifika Maneromango na kufanya tukio hilo.
 
“Baada ya wananchi kuwashtukia ndipo marehemu alikimbiza gari kwa lengo la kukimbia.
 
“Walipofika katika cha Vihingo, gari lao lilipata ajali ya kuingia kwenye korongo ambapo waliacha gari hilo na kukimbia ndipo wananchi waliwakimbiza na kumshambulia marehemu kwa silaha mbalimbali za jadi na mawe na kusababisha kupoteza maisha “alifafanua Wankyo.
 
Wankyo alieleza, mtuhumiwa mwingine mmoja Abdul Zuberi maarufu Mvidunda (35)mkazi wa Chamazi alikamatwa maeneo ya Sumbwi wakati akijaribu kutoroka.
 
Watuhumiwa baada ya kuhojiwa wamekiri kujihusisha na matukio mawili ya uporaji tarehe 14 January mwaka huu huko Kitonga Kisarawe ambapo walipora pikipiki aina ya sanlg namba MC 324 CDL aina ya haoujue mali ya Haruna Goha.
 
Wankyo alisema, tukio jingine walilolifanya ni kupora bajaji eneo la Kibuta mali ya Shukuru Ally february 13 mwaka huu.
 
Aidha jeshi la polisi mkoani hapo, limewakamata Ally Said maarufu kwa jina la Sober (37)Ramadhani Hamza -Mijoke (40)na Said Ramadhani -Ubwabwa (37)wakazi wa Mwendapole wakijihusisha na uhalifu wa kushusha mizigo katika magari,yanayotumia barabara kuu ya Dar es salaam kwenda Morogoro kwa jina maarufu Lumbesa /Shushashusha.

Mwanafunzi akutwa ameuawa shambani

$
0
0
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Yungwe wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita, Alex Pastory amekutwa ameuwawa kwenye eneo la kichaka  huku sababu za kifo hicho zikiwa bado azijajulikana.

Akizungumza na  Waandishi wa  habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema marehemu wakati akiwa shuleni akiendelea na masono aliomba ruhusa ya kwenda Nyumbani kwao ukerewe kwaajili ya matibabu kutokana na hali ya afya yake kutokua nzuri.

Amesema,marehemu alipewa ruhusa na kuondoka kwenda nyumbani na alivyo maliza matibabu February 28   mwaka huu alirejea shuleni na kuendelea na masomo yake.

Aidha,Kamanda Mponjoli amesema tangu Machi mosi mwezi huu mwanafunzi huyo  alitoweka shuleni pia hakuonekana katika maeneo ya nyumbani ambapo alikua amepanga.

Sanjari na hayo, Kamanda amesema ilipofika tarehe 8 mwezi huu mama mmoja ambaye jina lake halikujulikana, wakati akiwa shambani analima aliona fuvu la Binadamu kwenye eneo la shamba lake hali iliyomshitua na kupelekea kuwaita wananchi na walipofika na kuchunguza walibaini kuwa ni mabaki ya nguo za shule kuwepo kwenye eneo hilo.

Coaster lililobeba wanafunzi lagonga treni na Kuua Mmoja

$
0
0
Gari la abiria lenye namba za usajili T930 DML aina ya Toyota Coaster lililobeba wanafunzi wa sekondari limegonga Treni eneo la Kwamichi Jijini Tanga na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi.

Basi hilo lililokuwa limebeba wanafunzi wachezaji pamoja na washangiliaji zaidi ya 30 liliweza kuburuzwa umbali wa mita 50 kutoka eneo ilipotokea ajali .

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe akizungumzia ajali hiyo iliyotokea jana Ijumaa Machi 15, 2019 amemtaja aliyefariki katika ajali hiyo kuwa ni kondakta wa basi hilo ambaye jina lake halijatambulika mara moja.

Majeruhi waliofikishwa hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo ni wanafunzi 30 ambapo 19 kati yao hali zao si nzuri na madaktari wanaendelea na kuwapa matibabu.

Video Mpya : Lyyn - Kama Yote

Video Mpya: Aslay - nyang'anyang'a

$
0
0
Video Mpya: Aslay - nyang'anyang'a

Rais Magufuli Afanya Ziara Ya Kustukiza Kukagua Ujenzi Wa Nyumba Za Askari Magereza Ukonga Na Magomeni Kota Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na baadhi ya wazee waliokuwa wakaazi wa nyumba za Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kuona maendeleo ya ujenzi wa nyumba za ghorofa alizoziwekea jiwe  la msingi Aprili 15, 2017 ambapo mpaka sasa ujenzi wake umesimama kwa sababu ambazo hazikuweza kujulikana mara moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za ghorofa za Magomeni Kota jijini Dar es salaam alizoziwekea mnamo  Aprili 15, 2017 ambapo mpaka sasa ujenzi wake umesimama alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za ghorofa za Magomeni Kota jijini Dar es salaam alizoziwekea jiwe  la msingi Aprili 15, 2017 wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019.Picha na Ikulu

Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa Uganda Ambaye Ni Mjumbe Maalum Kutoka Kwa Rais Wa Uganda Yoweri Museveni Ikulu Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa ambaye pia ni mjumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni iliyowasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa ambaye pia ni mjumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa wapili kutoka kushoto, Balozi wa Uganda hapa nchini Richard Kabonero pamoja na Balozi Zuhura Bundala mara baada ya mazungumzo na mjumbe huyo maalum Ikulu jijini Dar es Salaam.Picha na Ikulu
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images