Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Awatimua TBA na Askari Magereza katika Mradi....Aukabidhi kwa Wanajeshi wa JWTZ

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 16 Machi, 2019 amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Magereza wa gereza la Ukonga Jijini Dar es Salaam na kuagiza mradi huo ukabidhiwe kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo baada ya kubaini kuwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imeshindwa kutekeleza mradi huo kwa wakati, licha ya Serikali kutoa shilingi Bilioni 10 za ujenzi.

Ametaka wataalamu wa TBA waliokuwa wakisimamia mradi huo pamoja na Askari Magereza waondoke na kuwapisha JWTZ.

“Kwa hiyo hapa nisimuone mtu wa TBA, nisimuone mtu wa Magereza kuja kusimamia, muwaache Jeshi la Wananchi wafanye kazi zao, siku watakapokuja kunikabidhi na mimi nitawakabidhi Magereza, kwa hiyo watu wa TBA kuanzia leo nimewafukuza hapa” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli ameelezea kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA katika mradio huo ambao ulianza zaidi ya miaka 2 iliyopita kwa kushirikisha Jeshi la Magereza ambalo lilikuwa linaisadia TBA katika kazi za ujenzi, na ametaka TBA na Jeshi la Magereza wabadilike katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Nataka kila mlipo watu wa Magereza mfanye kazi, msimamie watu, kama ni ng’ombe muwafuge vizuri wazalishe vizuri hadi muuze mazao nje, kama ni kilimo mlime kwelikweli, muwe ni jeshi la kuzalisha, hii ni aibu kuleta jeshi jingine la wananchi kuja kuwajengea nyumba nyinyi, wakati nyumba mnakaa nyinyi, mlitakiwa muwe mmeshapanga mkakati kwamba TBA wamesuasua, ngoja tufyatue matofari, tuanze kujenga” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Charles Mbuge amesema JKT itakamilisha ujenzi huo ndani ya kipindi cha miezi 2 na nusu kuanzia kesho na kwamba kazi zitafanywa usiku na mchana.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameitaka TBA kutoa maelezo ya namna fedha zilizotolewa na Serikali kiasi cha shilingi Bilioni 10 zilivyotumika, na ameonya kuwa endapo itabainika matumizi ya fedha hizo hayaendani na kazi zilizofanyika hatua kali zitachukuliwa.

Katika mradi huo, ujenzi wa majengo 12 ya makazi ya Askari Magereza yaliyopangwa kuwa na ghorofa 4 kila moja ulioanza Desemba 2016 umefikia asilimia 45 tu na unaendelea kwa kusuasua.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa majengo ya makazi wa Magomeni Kota Jijini Dar es Salaam na kuelezea kusikitishwa na hali ya kusuasua kwa ujenzi huo ulioanza Aprili 2017.

Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia ujenzi wa majengo yenye ghorofa 3 ukiwa umefikia asilimia 36 na kazi za ujenzi zikiwa zimesimama kwa muda usiojulikana.

Mmoja wa wananchi wanaosubiri kukamilika kwa ujenzi wa nyumba hizo Mzee Omary Mpimbila amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa wamekuwa wakifanya juhudi za kufuatilia hatma ya majengo hayo kutoka TBA na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano lakini mpaka sasa hawajapatiwa majibu ya sababu za kutelekezwa kwake.

Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuchukua hatua za haraka kuhakikisha ujenzi huo unaendelea na wakazi wa Magomeni Kota wanapatiwa makazi kama walivyoahidiwa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
16 Machi, 2019

Je wewe ni Mmiliki wa Gari? Ni Fundi Magari au Muuza Spea? ...Hapa Tunahabari Njema Inayokuhusu

$
0
0
Habari njema kwa wamiliki wa Magari, mafundi na Wauza Spea za Magari. EDRIVE PRO wamekeletea mfumo ambao unawaunganisha pamoja na pindi gari lako likiharibika popote ulipo hutapata tena tabu ya kuhangaika kutafuta fundi au maduka ya spea.

www.edrivepro.co.tz ni mfumo wa kufanya na kusimamia utengenezaji wa magari online.

1. Katika mfumo huu wamiliki wa magari, maduka ya spare, na mafundi wanajisajiri ama wanaweza kusajiliwa kwa kuwasiliana na mtoa huduma wetu kwa e-mail edriveprotz@gmail.com

2. Baada ya kujisali kulingana nafasi yako [ mmiliki wa gari, muuza spare, fundi ama mwandika makala juu ya magari] msimamizi wa mfumo atakuthibitisha katika mfumo na utatumiwa e-mail na mfumo.

Baada ya kudhibitishwa utaweza kupata huduma za uuzaji wa spare, matengenezo ya magari kwa wamiliki wa magari na mafundi kupata fursa za mateja wapya mtandaoni nchi nzima.

3. Kutokana na wahusika wote katika mfumo huu kuwa wamesajiliwa, huduma katika mfumo huu ni nafuu na za uhakika.

Karibuni mjisajili katika www.edrivepro.co.tz

CHADEMA Arusha wacharuka Joshua Nassari kung’olewa ubunge

$
0
0
Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Arusha, kimemtaka Mbunge Joshua Nassari, aliyevuliwa ubunge na Spika wa Bunge, Job Ndugai, kukusanya vielelezo vyote ili shauri hilo lipelekwe kwenye mikono ya sheria.

Agizo hilo lilitolewa mjini hapa jana na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha ambaye pia ndiye Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa.

Akizungumza kwa njia ya simu juu ya sakata hilo la kuvuliwa ubunge Nassari, Golugwa, alisema watapeleka vielelezo hivyo ili mikono ya sheria itafsiri uamuzi uliofanywa na Spika Ndugai.

 “Chama na Nassari tupo naye imara kuhakikisha tunachukua hatua za haki. Ndio maana tumemwambia akusanye vielelezo vyote vya taarifa alizoandika kwetu na kwa Spika,” alisema Golugwa na kuongeza:

“Sisi hatuoni utoro hapo wa kutohudhuria vikao vya Bunge kama taarifa inavyojieleza, kwani alikuwa anatoa taarifa za kuhudhuria masomo nje ya nchi pamoja na matibabu ya mke wake.

“Kwenye mikono ya sheria tunaamini hakuna wanasheria wala majaji watakaovumilia jambo hili.

“Lakini alikuwa akihudhuria vikao vya Kamati za Bunge, uthibitisho upo posho alizokuwa analipwa kwenye vikao vya Kamati ushahidi upo, pengine kesho Nassari atazungumza na wanahabari,” alisema.

Golugwa aliendelea kufafanua kwamba, kati ya wabunge vijana waliofanya vizuri kwenye majimbo yao ni pamoja na Nassari kwani amekuwa na kumbukumbu nzito kwa masuala ya kuhudumia jamii.

“Nassari si mtafuta sifa, ni kijana amekuwa karibu na wananchi, anajituma kutafuta wadau wa maendeleo watakaoleta miradi ya macho, maji, madarasa kwenye eneo lake.

 “Hapa hatutetei ubunge tu, tunaangalia kwa upana mzima kwamba unawaondolea wananchi mwakilishi wao kwa utaratibu gani, ili tu uchaguzi uitishwe tena kwa mamilioni ya fedha,” alisema Golugwa.

Nassari alivuliwa ubunge juzi kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo, huku mwenyewe akisema amepokea taarifa hiyo akiwa kwenye kazi za kibunge mkoani Kilimanjaro na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

CUF Lipumba Wamtema Maalim Seif

$
0
0
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemtangaza Khalifa Suleiman Khalifa kuwa katibu mkuu wa chama hicho.

Mbali na Khalifa, Profesa Lipumba pia amemtangaza mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya kuwa naibu katibu mkuu Bara na Fakhi Suleiman Khatibu kuwa naibu katibu mkuu Zanzibar.

Profesa Lipumba amemtangaza Khalifa ambaye ni mbunge wa zamani wa Gando kuchukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad leo Jumamosi Machi 16, 2019 makao makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam.

Katibu mkuu huyo mpya, amepatikana baada ya kuchaguliwa na Baraza Kuu la Uongozi lililokutana jana Ijumaa.

Hata hivyo, hatima ya viongozi hao wapya wa CUF akiwamo Profesa Lipumba aliyechaguliwa na mkutano mkuu Jumatano iliyopita Machi 14, 2019, itajulikana baada ya hukumu itakayotolewa Jumatatu ya Machi 18, 2019 na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.

Hukumu hiyo ni ya kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachana wa chama hicho upande wa Maalim Seif wakipinga uhalali wa Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti wa CUF.

Habari Zilizopo Katka Magazeti Ya Leo Jumapili ya March 17

Waziri Mkuu: Wakandarasi Acheni Kulipua Kazi Zingatieni Viwango

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakandarasi wanaojenga majengo mbalimbali nchini yakiwemo na ya Serikali wahakikishe wanazingatia viwango na waache kulipua kazi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wakandarasi wawafundishe kazi mafundi wasaidizi wanaowatumia katika ujenzi wa miradi malimbali ili waweze kunufaika kwa kuongeza ujuzi.

Ametoa wito huo  jana mchana (Jumamosi, Machi 16, 2019), alipotembelea miradi mbalimbali ya ujenzi wilayani Ruangwa mkoani Lindi, ukiwemo wa Hospitali ya wilaya.

Amesema Serikali inatoa pesa kulingana na kazi inayotakiwa kufanyika, hivyo amewataka wakandarasi wafanyekazi wanazopewa kwa kufauata taratibu za kiufundi na si ‘kulipua lipua’.

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza wakandarasi hao kuwatumia mafundi wasaidizi waliopo kwenye maeneo ya karibu na miradi husika ili nao waweze kupata ajira.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka mafundi wasaidizi wahakikishe wanafanyakazi kwa bidii na uadilifu ili wawe mabalozi wazuri, jambo litalalowawezesha wengine kupata kazi.

"Nataka niwaambie mkifanya kazi kwa uaminifu wakandarasi watawachukua na kuwapeleka katika maeneo mengine wanayopata mradi. Jitumeni acheni uvivu mtafika mbali."

Amesema Serikali inatengeneza ajira kwa vijana kupitia wakandarasi wanaotekeleza miradi, hivyo wakandarasi wanatakiwa wawatumie mafundi wasaidizi walioko kwenye maeneo ya miradi.

Waziri Mkuu amesema amefarijika sana kuona vijana wanapata ajira na amewataka  watumie nafasi hizo kujifunza ufundi ili nao waje kuwa mafundi wakubwa na kuajiri wenzao.

Naye,  fundi msaidizi wa jengo la utawala katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa,Hamisi Ali amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwapelekea miradi mkubwa ambayo inawapatia ajira.

Ali ametoa wito kwa vijana wengine waache kukaa mitaani na badala yake wajitokeze na wachangamkie fursa za ajira zilizopo kwenye maeneo yao na wafanye kazi hizo kwa bidii.

Waziri Mkuu ametembelea ujenzi wa hospitali ya wilaya, ghala, Ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Shule ya Seondari ya  Wasichana Lucas Maria.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Kamati ya Kudumu ya Bunge Yaipongeza Wizara ya Madini

$
0
0
Na Issa Mtuwa Songea
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri amesema kamati yake inaipongeza na itaendelea kuiunga mkono Wizara ya Madini kwa kazi nzuri wanayoifanya.
 
Akiongea na waandishi wa habari mbele ya kamati yake Machi 13, 2019 mjini songea baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha umahiri (Centre of excellence) kwa mkoa wa ruvuma, Mzuzuri amesema kamati yake inaridhishwa na kazi za Wizara ya Madini na wataendelea kuiunga mkono (support) hasa swala la wachimbaji wadogo.
 
“Tunawapongeza sana Wizara ya Madini, mnafanya kazi nzuri na sisi kama kamati niseme tutaendelea kuwaunga mkono (support) hasa hili la wachimbaji wadogo” alisema Mzuzuri.
 
Naibu Wziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo ameiambia kamati kuwa wizara yake imejipanga katika kukamilisha ujenzi wa vituo vyote vya umairi kikiwemo cha Songea kwa kuzingatia ubora. Amesema ujenzi wa vituo vyote unakwenda vizuri, hata hivyo kituo cha songea kilichelewa ujenzi wake tofauti na vituo vingine kwa sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa kokoto tatizo ambalo lilisha tatuliwa na kwa sasa ujenzi unaendelea kwa kasi.
 
“Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imekusudia kukamilisha ujenzi wa kituo hiki na vingine kwa wakati na kama nilivyo tangulia kusema zile changamoto zimesha tatuliwa na tuaendelea vizuri. Naishukuru kamati yako kwa kutuunga mkono na ushauri wote uliotolewa tutauzingatia.” Alisema Nyongo.

Nae Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma Prof. Riziki Shemdoe akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo amewambia wajumbe wa kamati kuwa ni kweli kuna kipindi mkoa wa Ruvuma ulikumbwa na changamoto za upatikanaji wa kokoto na miradi mingi ya serikali ilisimama kutokana na kuwa na kampuni moja tu ya uzalishaji wa kokoto mkoa nzima, mara baada ya mitambo yake kuharibika na uzalishaji kusimama upatikanaji wa kokoto ulikuwa ni tatiizo.
 
Kituo cha Umahiri Songea ni miongoni mwa vituo mbalimbali vinavyo jengwa hapa nchini katika maeneo mbalimbali kama vile, kituo cha Bukoba, Simiyu, Tanga, Chuya kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo kujifunza na kupata uelewa wa masuala mbalimbali madini.

Wagonjwa watano wapandikizwa Figo Benjamin Mkapa

$
0
0
Na WAMJW – DOM
Hospitali ya  Benjamin Mkapa imefanikiwa kupandikiza Figo jumla ya Wagonjwa saba tangu ilipoanza kufanya huduma hiyo kwa kushirikiana na Madaktari kutoka shirika la afya la Tokushukai lilopo nchi ya Japan.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto   wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za kibingwa za magonjwa ya Figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Dkt.  Ndugulile amesema kuwa Idadi ya wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 43, ambapo 38 wamepatiwa huduma hiyo kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili na wagonjwa watano(5) hospitali ya Benjamin Mkapa

“Hivi navyoongea tayari mgonjwa mmoja amekwishapandikizwa figo na ameshatoka salama, yupo anaendelea kuangaliwa, lakini wana mpango wa kuwafanyia wengine wawili tutapokuwa tumekamilisha hili tutakuwa na wagonjwa saba ambao wamefanyiwa hospitali hii” alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa, Serikali imelenga kuhakikisha kwamba inawajengea uwezo Wataalamu wa ndani kufanya upasuaji  wa kibingwa ili waweze kuwahudumia Watanzania bila msaada kutoka Wataalamu wa nje.

“lengo na kusudio ni kuhakikisha kwamba tunajenga uwezo wa ndani wa kuweza kufanya upasuaji huu” Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka  wagonjwa nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya wagonjwa.  80 mpaka 100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.” alisema Dkt. Ndugulile

Aidha, Dkt. Ndugulile amewashukuru Wataalamu kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan kwa kujitoa na kuja kuwajengea uwezo Wataalamu wa ndani hali iliyosaidia kupunguza kiasi kikubwa cha fedha ambacho hutumika kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania nimepita kuwashukuru na kuwapongeza,  kwa sababu badala ya kutusaidia sisi samaki, wenzetu wa Japan wameamua kutupatia sisi mishipi na kutufundisha jinsi ya kujua naamini ujuzi huu utatusaidia sana ” alisema Dkt. Ndugulile.

Video: Kayumba - Wasi Wasi

Viwanja Vikubwa Vinauzwa: Bunju na Mapinga (Baobab Sec)

$
0
0
Viwanja Vikubwa Vinauzwa: Bunju na Mapinga (Baobab Sec)
Viwanja vipo mtaa wa Kimele, Kata Mapinga, km 2 tu kutoka Shule ya secondary Baobab (main road ya Dar to Bagamoyo).
Viwanja vimepangwa vizuri, vina miundombinu ya maji na umeme. 


Viwanja viko vya size na bei tofauti kuanzia mita 20/25 kwa bei ya tsh 6 milion, mita 20/30 kwa bei ya tsh 8 milion, mita 20/40 kwa bei ya tsh 10 milion, mita 30/50 kwa bei ya tsh 18 milion, mita 40/50 kwa bei ya tsh 24 milion, mita 40/60 kwa bei ya tsh 30 milion,

Pia ipo nyumba pagala (haijapauliwa) na ina vyumba 3, kimoja master, sebure, dining, public toilet, kitchen etc na bei yake ni tsh 23,000 (kiwanja chake ni sqm 400 au 20/20 mita)

Na pia, kwa Bunju sokoni, kipo kiwanja cha sqm 1800 kinauzwa tsh 54 milion.

Luksa kulipa kwa awamu (anza na 75%, maliza na 25%)
Ukipata ujumbe huu mjulishe ndugu/jamaa/rafiki yako.
Biashara hii haina dalali, mpigie mhusika: 0758603077, whatsap 0757489709

Ufugaji wa nguruwe : Gharama na Faida Zake

$
0
0
 Utangulizi
Nguruwe ni mnyama amabaye hutumika kama chakula / mboga na pia ni zao la biashara kwa mfugaji, mjasirimali na mfanyabiashara.
 
NGURUWE HUTEGEMEA SANA MAMBO YAFATAYO
1 . Banda imara na rafiki kwake
2. Usafi ni muhimu sana katika banda la Nguruwe
3 Mchaganyo bora wa chakula
4. Tiba bora na kinga
5. Maji na Lishe ( access ya vyakula Muhimu kwake )
 
CHANGAMOTO
KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE KUNACHAGAMOTO ZAKE LAKINI ZAWEZA KUTATULIWA KWA KUFATA MAMBO KADHAA.
Katika ufugaji wa nguruwe kunachagamoto ya vifo vya nguruwe wachanga ambao hupunguza faida ya biashara ya nguruwe kwa kupunguza idadi ya nguruwe wazima wa kuuzwa lakini utunzaji mzuri wa nguruwe wachanga huepusha vifo vinavyotokana na shida kama:
 
Matatizo ya kupumua
Ni kifo kinachosababishwa na mama anapomlalia nguruwe mchanga.chagamoto hii inaweza kutatuliwa kwa kuwatenga au kuwa na mabanda makubwa ya kulelea watoto.
 
Baridi
Nguruwe wachanga huathiriwa na baridi haswa katika majuma mawili au matatu ya mwanzo. Hii ni kwa kuwa wana kiwango kidogo cha utando wa mafuta wa kuwakinga.
 
Unashuriwa kuwaweka katika hali ya joto, wape matandiko na utumie vipasha joto kama vile kuwasha globu za joto kama utakuwa umewaweka kwenye mabanda ya kuta au nyumba yenye sakafu baridi.
 
Namna bora utunzaji wa nguruwe wachanga
Nguruwe moja wa kike ana uwezo wa kuzaa watoto 12. Namna ifuatayo itasaidia kupunguza idadi ya vifo vya nguruwe wachanga:
1.Pale nguruwe awapo na kidonda nyunyizia dawa ya ayodini 5% kwenye kovu ili kuzuia kuambukizwa kwa magonjwa.
2.Wawekee matandiko (nyasi kavu au maganda ya miti) mahali pa mapumziko ili wapate joto au utumie globu za joto.
3Wadunge sindano ya madini ya chuma (iron) siku ya tatu baada ya kuzaliwa ili kuzuia upungufu wa damu.
3. Yalainishe meno ya vichaga kabla ya masaa 24 ili kuzuia uharibifu wa matiti wakati wanaponyonya.
4. Watie vibandiko au utoboe masikio ili uwatambue na uhifadhi rekodi zao kama kuna umuhimu kama vile wafanyavyo wafugaji wa ng’ombe.
5. Wapime uzani wanapozaliwa na uhifadhi rekodi hiyo itakusaidia kujua ukuaji wao na maendeleo yao
6. Wahasi wale wa kiume juma la tatu, wale ambao hawafai katika kuendeleza kizazi kwa kutumia mtindo wazi (open method) kama unaona inafaa.
7. Wapatie dawa ya kuzuia minyoo pia zipo dawa za asili kama unga wa mkaa na majivu pia zipo za kitaalamu, wasiliana na wataalamu wa mifugo
8.Waachishe kunyonya katika juma la nane au wafikapo kilo 14 hadi 20 hii itasaidia kujitegemea na kukua kwa haraka.
 
Nguruwe Walioachishwa Kunyonya
1.Walioachishwa kunyonya wawekwe makundi ya 10 hadi 12 kulingana na uzito au ukubwa wao kwenye eneo ambalo watajitosheleza.
2.Watenganishe wakubwa kwa wadogo ili kuzuia kupigana.
3.Wakati wa kuwaachisha kunyonya mwondoe mama yao kutoka kwa watoto ili kupunguza usumbufu.
4Watoto wa nguruwe wa mama tofauti wasiwekwe pamoja maana hii husababisha mapigano kati yao na
5.Unapowachanganya watoto wa mama tofauti wapake mafuta ya gari yaliyotumika kwenye ngozi yao au mafuta ya kula ili kuiondoa harufu ya kutambulika ili wasipigane
 
FAIDA YA UFUGAJI WA NGURUWE
Faida kuu ya nguruwe ni zao la chakula lakini pia ni zao la kukuongezea kipato ukiwa kama mjasirimali / mfanyabiashara.
Lengo langu nikueleza namna unavyoweza kufuga na kutupa faida, Steps zifatazo ni muhimu kuzigatia.
 
JIPE MTAJI WA MILLION 4 / 3.5 KWA NGURUWE 50
UANDAAJI WA BADA WEKA MAKADILIO YA LAKI TANO (800,000/=) .
Hapo nazugumzia banda lenye heru U yenye mstatili ikiwa na kitako kirefu
Eneo lenye ukubwa wa mita 50 kwa 50 litafaa zaidi ili kuhakikisha usalama wa nguruwe wako na ukuaji bora.
1. Tafuta mabati used kwa bei ya 5000 mfano mabati 20 ya futi 10 /10 = 100,000/=
2. Tafuta mabazi ya futi 10 kwa 2000 kila moja utapata mabazi pic 100 = 200,000/=
3. Tafuta miti ya nguzo na kechi ya 1000 na 2000 miti ya 1000*70 na 2000*3 = 120,000/=
4. Tafuta chagalawe / moramu trip 10*3000 =30000/=
5. Cement mifuko kwa ajiri ya sakafu na mashimo ya kulishia 5 *18000 = 90,000/=
6. Misumari ya aina 4, nch 6 kg5,nch 3 kg5 nch 5 kg10 na nch4 kg10, Bawaba na komeo =100,000/=
7. Malipo ya fundi 75000 fundi uashi na 75000 fundi seremala =150,000
JUMLA HAPO INAKUWA 790,000/= MAKADILIO INAKUWA 800,000/=
 
UNUNUZI WA NGURUWE WA KUANZIA .
Nguruwe wadogo wadogo ni vinzuri zaidi kuanza nao kwa sababu watakuzalia watoto wengi na kwa muda mrefu . Chukua mfano MILLION 2.5 . Nguruwe wadogo wa dogo wanauzwa 50000 au 40000 inategemeana na mahala na maelewano . Milioni 2.5 inakupa vitoto 50 au 55 . Hivyo unawexa kuwa na vitoto jike 50 na vidume 5. baadaye ukaongeza madume matano ya kuazima au kukondi kwa ajiri ya kupandishia
 
MAANDALIZI YA CHAKULA
Mchaganyiko wa chakula cha nguruwe na gharama zake tunaweza ukadilia kujitosheleza kwa laki tatu kwa mwenzi mmoja kwa nguruwe hao 50, kwa 300,000/= , ambapo itajumuisha tiba / kinga, lishe, vyakula vya nguruwe vinaweza kuwa pumba ya mpunga ile laini,pumba ya mahindi, mashundu, mabaki ya magada ya vianzi amba mabaki ya chakula yaliyosalama
 
MALIPO YA MSIMAMIZI NA ENEO LA KUWEKEZA
Katika kipengele hiki makadilio ya juu ama ya chini kwa msimamizi wa kazi yako waweza mlipa 100,000/= ama chini yake pia kwa mwenye eneo huwa nimaelewano tu aunaweza pata kwa fair au kukakodi kwa laki tatu, 300,000/= kwa mika miwili.
 
HIVYO JUMLA YOTE YA GHARAMA ZA UAZISHAJI UWEKEZAJI WA NGURUWE 50 ZITAKUGHARIMU MILLION 4 AMA MILLION 3.5 KWA MAANA KUWA HAPO JUU NIMETUMIA MAKADILIO YA JUU NA UKIINGIA KWENYE UHALISIA KAMA MJASIRIMALI LAZIMA IPUNGUE NA KUFIKIA 3.5

KIPATO AU FAIDA YA UFUGAJI NGURUWE
Nguruwe wanafaida ya haraka na nimradi wa uhakika kabisa, ukipitiia mchanganuo hapo juu wa nguruwe 50 utatupa faida kama ifatavyo
 
Nguruwe huzaa Mara mbili kwa mwaka na huzaa watoto zaidi ya watanoyaani huzaa watoto 12 ama nane .
Basi chukua nguruwe 50 * vitoto 5 yaani ufanye kuwa nguruwe wako 50 wakupatie vitoto vitano vya uhakika
Nguruwe 50*5 = 250 ukijumlisha na wale 50 wa mtaji umakuwa nao 300 . Chukua zao la nguruwe la 250 na uza kwa 200000 kwa kila nguruwe yaan bei ya kawaida kabisa. Utapata Million 50.

Hivyo zao la kwanza ndani ya robo tatu ya mwaka inakutegenezea million 50 pia na mienzi sita ijayo inakupa tena 50 na zaidi ili kukamilisha uzao wa pili hii inkupa uhakika wa kutegeneza million 100 za uakakika ndani ya mwaka mmoja na nusu ama miaka miwili ukijipa timeframe work lakini kumbuka hapo tumefanya kwa hesabu ya uzao wa chini kabisa ambapo tumeangalia na hasara ya vifo kama vifo visipotokea na uzao ukawa mkubwa utakuwa na uhakika wa kutegeneza million 150 kwa miaka miwili.

Kwenye hesabu ya kuwale unaweza kuwaza sana kuwa itaongezeka na kukughalimu sana jibu ni hapana mpka kufikia kuuza hawatokugharimu zaidi ya million 7 je million 7 kwenye million 150 ni kitu kisicho nafaida ?
 
NB . jambo lolote linahitaji umakini naa dhamira ya dhati pia kushirikisha wataalamu na wenye uzoefu ili kufikia leng Ewe ndugu kila kitu kinawezekana UTAYARI WAKO / UTHUBUTU WAKO, UAMINIFU .NA MAAMZI YAKO.
 

Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 2 na Nusu tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji. Tazama Hapa

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, yawezekana umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini.  Kulalamika tu vyuma vimekaza haitakusaidia kitu kama hutaki kujiongeza ili uongeze kipato chako.

Yako mambo mengi ya kufanya ili kujikwamua kiuchumi. Usitegemee mshahara wako tu. Mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.
 
Somo  ni dogo tu lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana.
 
Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo.

==>>Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4.

Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na

vifaranga 20 x 10 = 200Watunze vizuri.

Wale vifaranga tunakadiria kuwa majike watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga.

Utakuwa na kuku 200 + 25( ulioanza nao) =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700.

Ndugu msomaji, hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000. 

Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku baadhi  ili upate fedha ya kuwalisha ????

Ukiuza kuku 1000, utabaki na kuku 1000, kati yao tuseme majike ni 750. Ndani ya Miaka 2 maanake ni  750(majike) x 10 = kuku 7500 (uza wengine upate pesa ya kutumia kuwalisha) . 

Tuseme sasa utabakiwa na kuku jike  3000 x 10( jike moja ni mayai 10) = kuku 30,000. 

Hao kuku 30,000  ukiwauza wote utapata; 30,000x 13000( bei ya kawaida kbsa)= 390,000,000. Je, bado utakuwa masikini? Bado vyuma vitakuwa vimekaza?

Nina uhakika, mpaka mwisho wa mwaka huo wa pili utakuwa umefanikiwa sana kuukimbia UMASIKINI.

Kwenye hayo mamilioni, hata ukitoa milioni 100 kwamba  tuseme ndo zimetuka kuendeshea mradi wako, bado utakuwa ni milionea tu. Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi.

NB: Ukiyapata hayo mamilioni ya pesa, kumbuka kutoa Zaka, sadaka na kusaidia masikini wasiojiweza ili ubarikiwe zaidi 


Waziri wa Kilimo: Machi 31 malipo ya wakulima wa Korosho yatakuwa yamekamilika

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Lindi
Serikali imewahakikishia wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuwa kufikia tarehe 31 Machi 2019 wakulima wote watakuwa wamelipwa fedha zao kwani uhakiki umekamilika kwa kiasi kikubwa.

Hakikisho hilo mbele ya kamati hiyo limetolewa leo Tarehe 16 Machi 2019 na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) katika ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati akitoa ufafanuzi katika mkutano uliowakutanisha wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wake Dkt Christine Ishengoma, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Naibu Katibu Mkuu wizara ya Kilimo, wataalamu serikalini sambamba na wakulima.

"Kumekuwa na urasimu mkubwa tangu kuanza kwa zoezi hili la uhakiki lakini sasa tumeamua kama serikali kabla ya mwisho wa mwezi huu wa tatu wakulima wote wawe wamelipwa malipo yao ili kuondoa adha wanazokumbana nazo" alikaririwa Mhe Hasunga

Alisema pamoja na kwamba malipo ni mchakato unaohitaji kupitia katika hatua nyingi za mchakato ikiwemo uhakiki lakini kila jambo lenye mwanzo ni lazima kuwa na ukomo.

Alisema mpaka sasa Tani 222,684 zimekwisha kusanywa huku hadi kufikia tarehe 14 Machi 2019 tayari jumla ya Shilingi Bilioni 596.9 zimekwishalipwa kwa wakulima kati ya Shilingi Bilioni 723

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amewahakikishia wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuwa pamoja na mchakato huo wa malipo ya Korosho kuendelea lakini pia Wizara imepitia katika michakato mbalimbali ya kumpata Mkurugenzi mpya wa Bodi ya Korosho ili kuendelea na majukumu ya Bodi hiyo.

Kuhusu wanaofanya biashara ya zao hilo kinyume na sheria maarufu kama Kangomba Waziri Hasunga alisema kuwa tayari serikali imewabaini na wote watachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumzia Pembejeo feki Mhe Hasunga alisema kuwa tayari hatua zimeanza kuchukuliwa kwa wafanyabiashara wote waliofanya hujuma kwa kuwauzia wakulima Mbegu na mbolea feki ambapo hatua kali zimeanza kuchukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kutolipwa fedha wanazodai kwa kusambaza Pembejeo hizo.

Katika hatua nyingine Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameuagiza uongozi wa Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu Vya Tropiki (TPRI) kutuma wataalamu Mkoani Lindi ili kuchukua sampuli za viuatilifu kwa wakulima na kuvipima ili kubaini kadhia ya usambazaji wa viuatilifu feki kwa wakulima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Dkt Christine Ishengoma (Mb) amemuagiza Waziri wa Kilimo kuhakikisha kuwa taarifa ya malipo ya wakulima wote wa Korosho inafika bungeni tarehe 2 Aprili 2019.

Joshua Nassari Kumshitaki Mahakamani Spika Ndugai

$
0
0
Aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema atakwenda mahakamani kutafuta haki ya uwakilishi wa wananchi wa Arumeru baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kutangaza kwamba hana sifa za kuendelea na ubunge.
 
Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumapili Machi 17, 2019, Nassari amesema mara ya mwisho alihudhuria mkutano wa Bunge wa Septemba lakini hakuhudhuria mkutano wa Novemba na Januari kwa sababu alikuwa anamuuguza mke wake huko Marekani.

"Nilifanya jitihada za kuwasiliana na Spika, nikamtumia ‘email’ (barua pepe) nikiwa Marekani kumjulisha hali ya mke wangu. Nasikitika kwa uamuzi alioufanya, nawapa pole wananchi wangu wa Arumeru, haki yao tutaitafuta kwenye vyombo vya sheria," amesema Nassari.

Akizungumza kwa huzuni, Nassari amesimulia jinsi alivyokuwa akimuuguza mke wake kutokana na matatizo aliyokuwa nayo na kusema alijaaliwa kupata mtoto wa kike Januari 27, siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano wa Bunge la Januari.

Amesema alikuwa njia panda kuamua kati ya kuhudhuria vikao vya Bunge au kukaa na mke wake ambaye alikuwa mgonjwa.

Amesema hajutii uamuzi wake wa kusimamia kiapo chake cha ndoa kwa kuamua kumuuguza mke wake.

"Pamoja na huzuni ya kuvuliwa ubunge, bado nina furaha ya kupata mtoto. Kuwa mbunge hakuondoi majukumu mengine ya kifamilia. Spika alihudhuria harusi yangu mwaka 2014, alikuwa anajua sina mtoto na nilimjulisha juu ya matatizo ya mke wangu. Alitakiwa kujiridhisha kwa kuniita na kunihoji badala ya uamuzi alioufanya," amesema Nassari.

Katika mkutano huo na wanahabari, Nassari hakuruhusu kupokea maswali kwa madai kwamba alikuwa amevurugwa (devastated), hivyo akaomba asipokee maswali.

Waziri Mkuu Majaliwa azindua rasmi soko la dhahabu Geita......Atoa Onyo Kwa Wadau wa Madini

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa tahadhari kwa wadau wote wa madini kuwa atakayekamatwa anatorosha madini, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo utaifishaji wa madini atakayokuwa akiyatorosha.

Pia amewataka viongozi na watendaji wote wa Serikali wasimamie kwa weledi, uaminifu na uadilifu, sheria, kanuni na miongozo kuhusu sekta ya madini kwa lengo la kudhibiti utoroshwaji wa madini hususan dhahabu kwenda nje ya nchi.

Waziri Mkuu ametoa tahadhari hiyo leo (Jumapili, Machi 17, 2019) wakati akifungua soko la madini la Mkoa wa Geita. Ufunguzi wa soko hilo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilotoa tarehe 22.01.2019 la kuitaka mikoa yote ianzishe masoko ya madini.

Waziri Mkuu ameitakaWizara ya Madini, Tume ya Madini, Serikali ya Mkoa, Idara na Taasisi nyingine za Serikali zinazohusika na maendeleo ya sekta ya madini waheshimu mipaka ya majukumu yao ili waweze kulisimamia vizuri soko hilo na kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

“Wizara ya Madini ishirikiane na vyama na mashirikisho ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuandaa mpango kazi mahsusi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya soko hili ili lisigeuke kuwa kikwazo kipya kwa wachimbaji na wafanyabishara wa madini”

Waziri Mkuu ameviagizaVyombo vya Ulinzi na Usalama vihakishe soko hilo linapata ulinzi wa kutosha muda wote ili watendaji, mali zitakazokuwemo, vitendea kazi na miundombinu yote iwe salama muda wote. “Mkuu wa mkoa na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, nawaagiza hakikisheni Suala hili mnaliandalia utaratibu haraka iwezekanavyo”.

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuielekeza mikoa mingine yenye kiwango kikubwa cha uzalishaji wa madini hususan ya metali na vito iharakishe uanzishwaji wa masoko ya madini sanjari na miundombinu yote muhimu ili masoko hayo yaanze kufanya kazi kabla ya kwisha kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019.

Amesema anaamini kwamba, usimamizi mzuri wa soko hilo na masoko mengine ya madini yanayoendelea kuanzishwa nchini utaimarisha makusanyo ya kodi za Serikali na kuongeza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la Taifa.

Vilevile, amesema wafanyabiashara wa madini, hususan kutoka nje ya nchi wataongezeka kwa sababu tutakuwa tumewaepusha na matapeli na vikwazo vingine vya kibiashara. “Uimara wa soko hili pia, utaboresha uhusiano kati ya wadau wa biashara ya madini na Serikali”.

Waziri Mkuu amesema Serikali imefuta baadhi ya tozo na kodi ambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara wa madini hususan wachimbaji wadogo. Miongoni mwa tozo zilizofutwa ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Zuio ya asilimia tano ya mwisho (final withholding tax) inayotozwa kwenye bei ya kuuzia madini ya aina zote.

Amesema baada ya kufutwa kwa kodi na tozo hizo Serikali inatarajia kuwa utoroshwaji wa madini utapungua, pia kutasaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa kupitia uanzishwaji wa masoko ya madini; kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato kwa nchi.

“Nitoe wito kwa wachimbaji wote wadogo kwamba endeleeni kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yenu kwa kufuata taratibu, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali”. 

AmesemaSerikali inachukua hatua zote hizo si kwa lengo jingine bali kuziba mianya ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi, na hivyo, kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katika maeneo mengi ya nchi yetu.

Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga vema katika kuhakikisha vikwazo vyote vilivyomo katika mnyororo wa biashara ya madini vinaondolewa kwa lengo la kukuza sekta hiyo na kuwanufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla.

Amesema Serikali imeamua kutoa mwelekeo mpya katika usimamizi na maendeleo ya sekta ya madini. “Utekelezaji wa dhamira hii unakwenda sambamba na kuweka mazingira mazuri na miundombinu itakayowezesha kuimarika kwa sekta ya madini nchini”.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema wachimbaji wadogo wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa masoko ya uhakika ya madini ambao umekuwa sababu ya utoroshwaji madini, hivyo kuanzishwa kwa soko hili kunawahakikishia wachimbaji wadogo masoko na kukua kwa kipato kutokana na shughuli za madini.

Waziri Mkuu amesema kwa muda mrefu sasa, kumekuwepo na malalamiko ya kudhulumiwa au kupunjwa kutoka kwa baadhi ya wachimbaji wadogo, vitendo hivyo vimekuwa vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu.

“Ndugu wachimbaji wadogo, soko hili linakwenda kuwa mwarobaini wa tatizo hilo kwani litasheheni vifaa vya kupimia uzito na ubora wa madini kabla hayajauzwa. Naielekeza Tume ya Madini, isimamie ipasavyo vifaa na taratibu za vipimo kwenye soko hili na kuhakikisha hakuna manung’uniko juu ya utendaji kazi wa vifaa hivyo”.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa soko hilo  pia litaondoa uwezekano wa wanunuzi wa madini kuibiwa na wajanja wachache wanaojifanya kuwa na madini wakati hawana. “Nawasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko hili kikamilifu ili kuepuka udanganyifu na matapeli”.

Pia ameiagiza Tume ya Madini kuratibu bei za madini ndani ya soko hilo na ihakikishe mchimbaji anapata stahiki zake, Serikali inapata mapato yake na mfanyabiashara naye ananufaika. “Tunaimani kabisa tatizo la kudhulumiana na kupunjana linaenda kwisha kabisa. Na kwa kweli ikitokea mtu amepunjwa, atakuwa amejitakia mwenyewe”.

“Ndani ya soko hili kutakuwa na huduma zote muhimu kwa mfanyabiashara ikiwemo huduma za Tume ya Madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mabenki na nyinginezo, hivyo kuokoa muda na gharama nyingine katika kuendesha biashara hii ya madini.

Amesema soko hilo litasaidia sana katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na takwimu za biashara ya madini. Hivyo, niwasihi wachimbaji wa madini kulitumia soko hili na kuacha vitendo vya utoroshaji wa madini. Serikali kwa upande wake, haitomvumilia mtu yeyote yule atakaye jihusisha na utoroshaji wa madini.

Ufunguzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Wabunge wa mkoa wa Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robertt Gabriel, wakuu wa mikoa jirani na maafisa wa Serikali.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya March 18

Polisi Tanga Waua Jambazi Mmoja

$
0
0
Jeshi la Polisi wilayani Muheza mkoani Tanga limemuua kwa kumpiga risasi Mkazi wa Dar es Salaam, Mwinyiheri Nuhu, likidai alikuwa anajihusisha na ujambazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, alidai jana kuwa Nuhu alikuwa miongoni mwa watuhumiwa wanne wa ujambazi waliovamia nyumba ya mfanyabiashara Ally Nassoro wilayani Muheza wakiwa na bunduki juzi usiku.

Alisema tukio la kuuawa kwa mtuhumiwa huyo wa ujambazi lilitokea juzi usiku saa nne usiku katika Kijiji cha Songa wilayani humo ambako mfanyabiashara huyo anaishi.

Kamanda Bukombe alidai watuhumiwa hao wa ujambazi walivamia nyumbani kwa mfanyabiashara huyo wakitumia gari ndogo na kupora Sh. milioni moja zilizokuwako.

Alidai kuwa wakati watuhumiwa hao wakiendelea kufanya uhalifu, askari polisi kutoka vituo vya Wilaya ya Muheza na Hale wilayani Korogwe, walifika kwenye nyumba hiyo na kuanza kupambana nao kwa kurushiana risasi.

Kamanda Bukombe alidai kuwa wakati wakirushiana risasi, polisi walimuua Nuhu, lakini wenzake walitoroka na wanaendelea kusakwa na jeshi hilo.

Alidai walinasa bunduki mbili, kitambulisho cha Nuhu na Sh. milioni moja zilizokuwa zimeporwa kutoka kwa mfanyabiashara huyo.

Lugola Akagua Na Kupima Ulevi Madereva Wa Mabasi, Malori Mjini Morogoro

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA, Morogoro.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amefanya operesheni kubwa ya kukagua na kupima ulevi wa pombe kwa madeveva wa mabasi na malori mjini Morogoro, jana.

Lugola pia alizungumza na abiria wa mabasi hayo, pamoja na viongozi wa madereva waliopo stendi kuu ya mabasi Msamvu, mjini humo, ambapo walimwelezea kero mbalimbali zinazowakabili.

Ukaguzi wa mabasi na malori hayo ulifanyika barabara kuu itokayo Dodoma kuja Morogoro-Dar es Salaam ambapo Waziri huyo akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa huo (RPC), Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa huo (RTO), alisimamisha vyombo hivyo vya moto vilivyokuwa vinaingia Mizani iliyopo eneo la Kihonda, nje kidogo ya Mji wa Morogoro.

Akizungumza na madereva, kondakta, wapiga debe na abiria mara baada ya kufanya ukaguzi huo, Lugola alisema ni wajibu wake kufanya hivyo katika hatua ya kupunguza kwa kasi ajali mbalimbali zinatokana kwa uzembe wa madereva nchini.

“Mimi ni Waziri wa vitendo, nikiagiza nataka nitekelezwe, na pia nikiahidi lazima nilifuatilie, niliwaambia nitakua nakuja kufanya ukaguzi muda wowote ambao hamuujui, na ninafanya hivi kwa lengo moja tu, kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinafuatwa ikiwa ni hatua ya kumaliza kupunguza au kumaliza kabisa ajali za barabarani hapa nchini,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa, kwasasa ajali zimepungua nchini, hasa Mkoa wa Morogoro, kwasababu ya askari wa usalama barabarani kufanya kazi zao kiweledi, na pia madereva kufuata sheria za usalama barabarani.

Lugola aliwataka madereva nchini, kuacha uendeshaji wa mashindano, kuwa na leseni na pia kuhakikisha wanapokuwa barabarani wanakua makini kwasababu ya kuwabeba abiria au mizigo mbalimbali wanayoisafirisha sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi.

“Madereva wa mabasi na malori ambao nimefanikiwa kuwapima kilevi leo, ambao wasiopungua sita, sijawakuta na kilevi, wapo makini na hii inaleta nguvu na imani kuwa madereva wanaelewa na kuzingatia sheria za usalama barabarani, na pia ndani ya mabasi niliyokuwa nayakagua nimezungumza na abiria wakaniambia madereva wanaendesha vizuri na pia niliwakuta wamevaa mikanda, naamini safari yetu ya kuondoa ajali za barabarani tunazidi kufanikiwa,” alisema Lugola.

Wakizungumza kwa wakati tofauti katika stendi kuu ya mabasi, madereva walilipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, kwa usimamizi mzuri ambao umewaunganisha na kuwafanya waifurahie kazi wanayoifanya.

Dereva Juma Rashidi wa basi linalosafiri kutoka Ifakara kuja Morogoro, alisema wanajisikia furaha kubwa kwa uongozi mpya wa Jeshi la Polisi ulioletwa Mkoani Morogoro hivi karibuni. 

“Naomba niseme ukweli, RPC na RTO hakika wanatuongoza vizuri, hakuna kero za ajabu kama zamani, tupo huru kufanya kazi zetu, hii inaonyesha viongozi hawa wanataka tufanye kazi ili tuweze kupata riziki zetu kwa njia halali bila usumbufu wa kusumbuana kama ulivyokuwa siku za nyuma,” alisema Rashidi.

Lugola alifanya ziara katika kituo hicho, na baadaye kutoka nje ya kituo hicho kuyakagua mabasi na malori, mara baada ya kumaliza ziara yake aliyoifanya Wilayani Kilosa ya kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa Tarafa ya Kimamba wilayani humo, juzi.

VIDEO: Moni Centrozone Ft Nikki wa Pili - Chuchu Dede

$
0
0
VIDEO: Moni Centrozone Ft Nikki wa Pili - Chuchu Dede

Waziri Mhagama Afungua Mkutano Wa Baraza La Wafanyakazi Ofisi Ya Waziri Mkuu

$
0
0
NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amefungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi yake upande wa Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu uliofanyika mapema mwishoni mwa wiki hii.

Akifungua mkutano huo uliofanyiaka Machi 16, 2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Magadu mkoani Morogoro waziri aliwataka watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na ubunifu ili kuendelea kuleta tija na utendaji wenye kuleta maendeleo nchini.

“Naamini mkutano huu unalenga kugusa maeneo yote ya utendaji kazi ikiwemo kubainisha changamoto, fursa na jinsi ya kujipanga ili kuongeza tija na ufanisi katika maeneo yetu ya kazi,”alisema Mhagama

Waziri aliwaeleza watumishi kuutumia mkutano huo kama chombo muhimu cha kuendelea kujadili na kuweka maazimio yanayotekelezeka kwa kuzingatia umuhimu wa chombo hicho kilichopo kisheria katika kusaidia watumishi wa umma.

“Tumieni mabaraza haya kama eneo muhimu la kujadili na kutoa mapendekezo juu ya kuboresha mazingira ya kazi ili kuendelea kuwa na weledi katika kutekeleza majukumu ya ujenzi wa Taifa,”alieleza Mhagama

Waziri aliongezea kuwa, matumizi sahihi ya mkutano huo ni kuona namna  utavyosaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili Idara, Vitengo pamoja na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo na kuwa na  maoni, ushauri na mapendekezo yanayotekelezeka ili kufikia malengo waliojiwekea kwa mwaka wa fedha ujao 2019/2020

Pamoja na hayo Waziri alipongeza utendaji wa watumishi wa ofisi yake hususan Idara ya Kazi, inayoshughulikia masuala ya vibali vya kazi na kuendelea  kuboresha mifumo na mazingira wezeshi ili kuendelea ,kulinda mazingira ya kazi na ajira nchini.

“Pamoja na idara zote kuendelea kufanya vyema, kipekee naipongeza Idara ya kazi kwa mabadiliko mapya ya kiutendaji kwa kuzingatia ilikuwa Idara inayotupa shida hususani upande wa vibali vya ajira, tunashukuru kwa mageuzi makubwa yaliyofanyika katika Idara hiyo kwa kuwa na usimamizi mzuri na kulinda mazingira ya ajira na kuleta manufaa nchini,”alieleza Mhagama

Sambamba na hilo waziri aliwapongeza watendaji wa Ofisi kwa ujumla kwa nafasi zao kwa kuwepo na mafanikio makubwa ya kiutendaji pamoja na mchango wa kila mtumishi katika utoaji wa huduma bora bila upendeleo kwa wananchi wote kwa haki na usawa.

“Sina budi kuwapongeza kwani kila mmoja wetu ametimiza majukumu na kuwa na mchango mkubwa katika kutimiza majukumu ya serikali yetu kwa kuendelea  kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020,”alisisitiza Waziri Mhagama.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe aliahidi kuendelea kusimamia maagizo na ushauri wa waziri kwa watumishi wa ofisi yake ili kuleta matokeo chanya yanayotarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika kuboresha mazingira ya utendaji kwa watumishi ikiwemo kuendelea kupambana na rushwa mahali pa kazi na kuzingatia haki na usawa kwa watumishi wote.

Aidha Katibu Mkuu aliongezea kuwa, uwepo wa mabaraza hayo ni kwa mujibu wa sheria na  agizo Na. 1 la mwaka 1970 ambalo linaelekeza utaratibu wa kuundwa kwa mabaraza katika Taasisi na Ofisi za Umma kwa kuzingatia sheria mbalimbali za Kimataifa ikiwemo zile za Shirika la Kazi Dunia (ILO)

“Kwa kuzingatia lengo la kuanzishwa kwa mabaraza haya ni pamoja na kuona utekelezaji wa Bajeti za Ofisi zetu pamoja na kutoa mapendekezo katika kuboresha utekelezaji wa bajeti zetu za kila mwaka,”alisisitiza Massawe
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images