Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kesi Ya Kutoa Lugha Chafu Dhidi ya Rais Magufuli Inayomkabili Halima Mdee Yapigwa Kalenda Hadi February 7

$
0
0
Kesi inayomkabili, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee anayekabiliwa na shtaka la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kusikilizwa Februari 7, 2019.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita ameeleza hayo leo Jumatano Januari 9, 2019 mbele ya hakimu mkazi mkuu Salum Ally kuwa kesi hiyo ilipaswa kuendelea na ushahidi lakini hakimu husika yuko likizo.

"Kesi imekuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini kutokana na hakimu husika kuwa likizo, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na ushahidi," amedai Wakili Mwita.

Baada ya kueleza hayo Hakimu Ally aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 7, 2019 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kuendelea na hatua ya ushahidi. Tayari mashahidi wawili wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi katika kesi hiyo.

Katika kesi hiyo,  Halima anadaiwa kutenda kosa hilo, Julai 4, 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni.

Mdee anadaiwa kumtukana Rais John Magufuli kwa kusema “anaongea hovyo hovyo , anatakiwa afungwe breki” kitendo hicho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Huna Sababu ya Kuabika Tena, Jipatie Dawa Bora ya Nguvu za Kiume, Maumbile Madogo na Mvuto wa Mapenzi

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiathiri watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine ....kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapungufu katika mwili wake.

Kuna sababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huathiri misuli ya uume, 


Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0620510598  / 0743543944

Wizara Ya Ya Kilimo Ipo Katika Mapitio Ya Sifa Za Viongozi Wa Vyama Vya Ushirika

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Rukwa
Wizara ya Kilimo ipo katika mapitio ya sifa za viongozi wa Vyama vya Ushirika nchini ili kupata viongozi watakao ongoza kwa weledi sekta ya Ushirika.

Dhana ya kuchagua viongozi wa ushirika wenye sifa ya kujua kusoma na kuandika imepitwa na wakati hivyo kuna kila sababu ya kuchagua viongozi wenye weledi na utashi katika utendaji.

Hayo yameelezwa jana tarehe 8 Januari 2019 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakati akizungumza kwenye kikao kazi na maafisa wa Kilimo wa Wilaya za Mkoa wa Rukwa, Wadau mbalimbali wa Kilimo wakiwemo mawakala wa pembejeo, wasindikaji, wawakilishi wa vyama vya msingi vya ushirika na wakulima, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Alisema kuwa mfumo wa ushirika  ni nyenzo muhimu ambayo ukitumika vizuri itasaidia kuondoa  umaskini wa wakulima hapa nchini na utaimarisha uanzishwaji wa viwanda kuleta tija katika kilimo hivyo ni lazima kuwa na juhudi za makusudi kuwa na viongozi wenye weledi.

Katibu Mkuu huyo katika ziara yake mkoani Rukwa alitembelea maduka na maghala ya mbolea yanayomilikiwa na kampuni za ETG, YARA na PREMIER na kujionea hali halisi ya upatikanaji wa mbolea ambapo amepongeza utoshelevu wa mbolea uliopo mkoani humo.

Akizungumzia swala la masoko ya mazao ya wakulima Mhandisi Mtigumwe alisisitiza kuwa ubora wa mazao ya wakulima ni suala la msingi kulizingatia ili kuweza kusaidia wakulima kupata masoko ya uhakika na kujiongezea kipato, kwani mazao bora yana ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Kuhusu Milipuko ya visumbufu vya mimea, Mhandisi Mtigumwe alisisitiza kuwa ili kunusuru mazao ya wakulima nchini, hatua madhubuti zinaendelea kuchukuliwa ili kuweza kudhibiti wadudu wanaothiri mazao akiwemo Kiwavijeshi Vamizi (FAW).

Hivyo, alitoa rai kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa na Makatibu Tawala wote nchini, kuwaagiza Maafisa Kilimo kufanya tathmini ya awali na kubaini maeneo ambayo kiwavijeshi vamizi ameanza kuonekana ili Wizara kwa kushirikiana na halmashauri ziweze kuchukua hatua za kudhibiti milipuko ya kiwavijeshi vamizi kabla hajasambaa zaidi na kuleta athari kubwa.

Kuwa Wakwanza Kupokea Habari Zetu....Download App Yetu Kwa Kubonyeza Hapa, Huhitaji tena kuwa na Computer

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Yaomba Radhi Kivuko cha MV. MAGOGONI Kuharibika

$
0
0
Leo tarehe 09/01/2019 mnamo saa 1:30 asubuhi kivuko cha MV. MAGOGONI kinachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam kilipigwa na upepo mkali wakati kikikaribia upande wa Kigamboni. 

Hivyo, katika hali ya kupambana na upepo mitambo ya kuendeshea kivuko hicho iliingiliwa na takataka ambazo zilisababisha injini kupata moto na kupata hitilafu. 

Mafundi wetu wamefanikiwa kutatua hitilafu hiyo na huduma za kivuko hicho zimerejea katika hali ya kawaida mnamo saa 6:30 mchana. 

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) unawaomba radhi abiria wote kwa usumbufu walioupata.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
TEMESA
09/01/2019

Maandamano ya BAVICHA Kumpongeza Ester Bulaya Yapigwa Marufuku

$
0
0
JESHI la Polisi wilayani Serengeti mkoani Mara imepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanywa na Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha).

Maandamano hayo yalikuwa yafanyike leo Jumatano Januari 9, 2019 ili kumpongeza mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya kwa jitihada zake za kuwatetea wastaafu kwenye suala la kikokotoo cha asilimia 25.

Barua ya kuzuia maandamano hayo imeandikwa na mkuu wa polisi wa wilaya hiyo, Mathew Mgema akisema suala la kusitisha kikokotoo cha asilimia 25 lilifanywa na Rais John Magufuli wakati alipozungumza na watumishi Desemba 28, 2018 na wala si Bulaya.

Polisi wamesema badala ya kufanya maandamano, wameshauri anaweza kuwasiliana na wananchi wake wa Bunda Mjini na kupanga namna ya kumpongeza Bulaya kwani ndio eneo lake la uwakilishi lakini si kufanya maandamano.

Mkuu huyo wa Polisi amesema hawatasita kuchukua hatua pale ambapo kuna ukiukwaji na dalili za uvunjifu wa amani.

Rais Magufuli: Sitaacha kubadilisha Viongozi na hata Wewe Biteko ukifanya vibaya nitakutoa tu

$
0
0
Rais  Magufuli amesema hatochoka kufanya mabadiliko kwenye safu yake ya uongozi endapo ataona mambo hayaendi sawa kama anavyotaka.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumatano Januari 9, 2019 katika hafla fupi ya kuwaapisha viongozi aliowateua jana, akiwemo Waziri wa Madini, Dotto Biteko na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki.

Biteko amechukua nafasi ya Kairuki ambaye amedumu kwenye wizara hiyo kwa miezi 14 tangu ateuliwe Oktoba 2017.

Rais Magufuli amesema licha ya mabadiliko ambayo tayari ameyafanya kwenye Wizara ya Madini lakini sekta hiyo bado inaonekana kuwa na changamoto.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli changamoto hizo zinatokana na uongozi wa wizara hiyo kushindwa kuwajibika ipasavyo hali inayosababisha nchi kukosa fedha nyingi zinazotokana na madini.

“Sekta ya madini bado ina changamoto kubwa sana, ripoti inaonyesha nchi inayoongoza kwa kuuza dhahabu Afrika Mashariki si Tanzania wakati nchi yetu ndiyo inaongoza kuwa na dhahabu nyingi lazima tujiulize ni wapi tunakosea,” amesema Magufuli.

“Kuna udhaifu ambao Wizara ya Madini haiwezi kuukwepa. Kama tuna sheria nzuri, maeneo mengi ya kuchimba dhahabu,  je tumeshawahi kujiuliza wanapochimba wanauza wapi na wanapouza tunapata mapato asilimia ngapi?

“Kwenye  sheria kuna maelekezo ya kuanzishwa vituo vya madini je viko vingapi? Hivi vingesaidia kujua kiwango cha madini kinachopatikana na kinauzwa wapi?” Inauma unapoona kilo zaidi ya  300 zenye thamani ya zaidi ya bilioni 30 zinakamatwa zikisafirishwa. Wameshaiona Tanzania ni nchi ambayo unaweza kufanya lolote.” Amesema Rais Magufuli na kusisitriza;

“Nitaendelea kufanya mabadiliko kila mahali nitakapoona sijaridhishwa mhusika ataondoka, hata Biteko nimekuteua nikiona mambo hayaendi ninavyotaka utaondoka.”

TRA Yakusanya Trilioni 7.9 Katika Kipindi Cha Miezi 6 Ya Mwaka Wa Fedha 2018/19

$
0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 7.9 kwa kipindi cha miezi sita ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai hadi Desemba, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 7.8 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo amesema makusanyo ya mwezi Desemba, 2018 yaliongezeka kuzidi makusanyo ya miezi yote iliyopita kwa mwaka huu ambapo TRA ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.63.

“Mbali na makusanyo hayo ya mwezi Desemba, katika mwezi Novemba, 2018 TRA ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.21 na mwezi Oktoba, 2018, zilikusanywa jumla ya shillingi trillioni 1.29. Nachukua fursa hii kuwashukuru walipakodi wote kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati”, alisema Kayombo.

Kayombo aliongeza kuwa, katika kutatua kero na malalamiko mbalimbali ya walipakodi, uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania umeamua kwamba, kila siku ya Alhamisi itakuwa ni siku maalum kwa ajili ya Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa TRA kote nchini kuwasikiliza na kutatua changamoto za walipakodi.

“Pamoja na kutenga siku hiyo maalum, tumeanzisha Kituo cha Ushauri kwa Walipakodi kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambacho kipo katika Jengo la NHC kwenye makutano ya Mtaa wa Samora na Bridge kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuwa karibu na walipakodi.  Tumeanza kwa Dar es Salaam lakini vituo hivi vitaendelea kufunguliwa katika mikoa mingine nchini”, alieleza Mkurugenzi Kayombo.

Aidha, Kayombo amewakumbusha wamiliki wa majengo kote nchini kulipia Kodi ya Majengo ambayo viwango vyake ni shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida, shilingi 50,000/= kwa kila sakafu ya ghorofa na shilingi 20,000 kwa ghorofa za wilayani na vijijini.
 
“Sambamba na kuwakumbusha wamiliki wa majengo kulipia kodi ya majengo, napenda kuchukua fursa hii kuwasisitiza wafanyabiashara wadogo wadogo kuchangamkia vitambulisho vya wamachinga ambavyo vinapatikana nchi nzima katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa shilingi 20,000/=. Vitambulisho hivyo ni maalum kwa wale tu ambao mauzo yao ghafi hayazidi shilingi 4,000,000/= kwa mwaka”, alisisitiza Kayombo.

Mkurugenzi huyo wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati na kusema kuwa, TRA imeanza kampeni rasmi ya usajili wa walipakodi wapya kote nchini kwa kuwapatia Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) bure katika maeneo wanayofanyia biashara.

MWISHO.

Mahakama Kuu Yaitupilia Mbal Kesi Ya Kupinga Kanuni za Maudhui ya Sheria Mpya Ya Mtandaoni

$
0
0
Mahakama Kuu kanda ya Mtwara leo imetupilia mbali kesi ya kutaka mapitio (Judicial Review) ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao iliyofunguliwa na MCT, LHRC na Muungano wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC)

Katika kesi hiyo washtakiwa ni Waziri wa Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mwanasheria Mkuu.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Januari 9, 2019 na Jaji Wilfread Ndyansobera.

Katika maamuzi yake Jaji Ndyansobera amesema kwamba maombi ya wapeleka maombi hayana uzito.

Amesema walalamikaji wameshindwa kuthibitisha  jinsi gani Kanuni hizo zitakavyo athiri haki za msingi za Walalamikaji katika masuala ya uhuru wa habari na mawasiliano ya mitandaoni.

Hivyo, amesema Mahakama imekubaliana na hoja za  Mawakili wa Serikali kuwa Kanuni za Maudhui Mtandaoni zimetungwa kwa mujibu wa sheria na kupelekea Mahakama hiyo kutupilia mbali shauri hilo.

Shauri hilo liliendeshwa na mawakili kutoka Ofisi Mpya ya Wakili Mkuu wa Serikali ambao ni Bibi Alesia Mbuya, Bw. Ladislaus Komanya, Bw. Sylvester Mwakitalu, Bw. Johanes Kalungura, Bw. Killey Mwitasi, Bw. Abubakar Mrisha na Bibi Neisha Shao ambapo upande wa walalamikaji waliwakilishwa na mawakili Fulgence Masawe, James Marenga na Jeremia Mtobyesa.

Kwa hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Septemba 4, 2018, sasa ni rasmi madai ya kwamba Kanuni hizo zinabana uhuru wa habari na kwamba zilitungwa kimakosa yaaanguka rasmi.

Kwa kawaida kanuni hizo zilipaswa kuanza kutumika rasmi Mei 5, 2018 lakini Mei 4, 2018 mwaka huu, Mahakama hiyo iliweka zuio la muda baada ya kuwasilishwa kwa shauri la kupinga.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya January 10

Waziri Mkuu Akutana Na Mwalimu Wake Wa Shule Ya Msingi

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwalimu wake, Bibi Notburga Ivo Mbepera wakati walipokutana na kuzungumza mjini Songea hivi karibuni. Mwalimu huyo alimfundisha Waziri Mkuu katika Shule ya Msingi ya Mnacho wilayani Ruangwa 1973 - 1980.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tamko la Taasisi ya WAJIBU kuhusu sakata la Spika Ndugai, na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

$
0
0
Taasisi ya Wajibu ambayo mkurugenzi wake ni Ludovick Utouh aliyewahi kuwa CAGimesema busara inahitajika kutumika ili kumaliza sintofahamu iliyopo kati ya Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

==>>Hapo chini kuna Tamko la Taasisi hiyo.
 
MAONI YA WAJIBU - INSTITUTE OF PUBLIC ACCOUNTABILITY JUU YA WITO WA SPIKA WA BUNGE KUMTAKA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KUKUTANA NA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE 21/01/2019

WAJIBU - Institute of Public Accountability (WAJIBU), ni Taasisi inayojihusisha na masuala ya uwajibikaji hapa nchini. lmeendelea kufuatilia kupitia vyombo vya habari Tamko la Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyoitoa kwenye mahojiano ya ldhaa ya Kiswahili ya Redio ya Umoja wa Mataifa (UN Redio).

Kwa kuwa suala hili limeleta sintofahamu kwa jamii,WAJIBU ikiwa ni miongoni mwa taasisi fikra za uwajibikaji nchini imeona ni vizuri itoe maoni huru kwa kuzingatia maslahi mapana katika uwajibikaji na utawala bora nchini. lfamike kuwa Bunge na CAG ni vyombo vinavyotambulika na kulindwa kikatiba.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), pamoja na Sheria ya Kinga, Haki na Mamlaka ya Bunge ya mwaka 1988, Bunge ni mhimili unaoishauri na kuisimamia Serikali katika matumizi bora ya rasilimali za umma. Kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge ya mwaka 1988 kinasema (tafsiri isiyo rasmi):

"Bunge, Kamati za Kudumu au Kamati za Muda za Bunge kulingana na matakwa ya kifungu cha 18 na kifungu cha 20 cha Sheria hii, zinaweza kuagiza mtu yeyote kuhudhuria mbele ya Bunge au Kamati husika kutoa ushahidi au kuwasilisha nyaraka alizonazo au zilizo chini ya usimamizi wake ".

Katiba hiyo hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 143 (1-5) pamoja na Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008 zimeainisha majukumu ya CAG. Aidha, Ibara ya 143(6) inampa CAG kinga na uhuru wa kutoingiliwa na mtu au taasisi yeyote ya Serikalikama inavyonukuliwa hapa chini:

"Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2), (3) na (4) ya ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au sivyo".


Kwa kuzingatia umuhimu wa taasisi hizi mbili katika kusimamia rasilimaliza umma na kukuza uwajibikaji na utawala bora, ni vyema busara ya hali ya juu itumike baina ya pande hizi mbili katika kutatua mgogoro huu kwa sababu dhana ya uwajibikaji na utawala bora nchini itaimarika iwapo tuu kutakuwepo na uhusiano mzuri kati ya taasisi zote za uwajibikaji na usimamizi nchini.

Kutokana na umuhimu wa Taasisi hizi mbili ambazo zinatakiwa kushirikiana kwa karibu sana katika kuimarisha uwajibikaji na utawala bora hapa nchini, wananchi wanashauriwa kutoa maoni yatakayoboresha na kuimarisha uhusiano wa taasisi hizi.

Kwa muktadha huo, WAJIBU inaamini kwamba sintofahamu iliyojitokeza kati ya CAG na Bunge nivyema ikashughulikiwa kwa busara kati ya pande zote mbili bila kuathiri uhuru wa kikatiba uliotolewa kwa Mhimili wa Bunge na kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

lmetolewa na:
Bodi ya Wakurugenzi
WAJIBU - Institute of Public Accountability

Tume ya Taifa ya Uchaguzi DRC Yamtangaza Mshindi wa Kiti cha Urais...Tazama Hapa

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Congo (Ceni) imetangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo yanayoonesha mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi ameshinda kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Desemba 30 mwaka uliopita.
 
Tshisekedi amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali ya Rais anayemaliza muda wake, Emmanuel Shadary.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa, mapema leo Alhamisi amesema kwamba kwamba Bw Tshisekedi amepata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na kumtangaza rasmi kuwa Rais mteule wa nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini na mafuta.

Tshisekedi anatokea katika muungano wa kisiasa na aliyekuwa mgombea wa chama cha UNC (Union for the Congolese Nation), Vital Kamerhe ambaye atakuwa ni Waziri Mkuu wa serikali yao kwa mujibu wa makubaliano yao.

Ripoti zinaeleza kuwa mshindi wa kwanza (Felix Tshisekedi) amepata kura takriban milioni 7, huku mshindi wa pili (Martin Fayulu akipata kura takriban milioni 6.4 milioni na mgombea wa tatu ambaye anaungwa mkono na Rais Joseph Kabila (Emmanuel Ramazani Shadary) akipata takriban kura millioni 4.4.

Mzee wa Miaka 80 Auawa na Kunyofolewa Sehemu zake za Siri

$
0
0
Watu wawili wamefariki  dunia mkoani Kagera katika matukio mawili tofauti, likiwamo la mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la Laurian Kakoto (80), mkazi wa kijiji cha Ihunga kata Kishanda wilayani Muleba, kukatwa sehemu zake za siri na wahusika kuondoka nazo.

Akizungumza na waandishi wa habari, kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema kuwa baba huyo aliondoka nyumbani Januari 7 mwaka huu kwenda kuhemea lakini hakurudi hadi maiti yake ilipogunduliwa na wananchi ikiwa imezikwa huku nyayo za miguu zikiwa zinaonekana juu ya kaburi, Januari 08 saa moja asubuhi.

Kamanda Malimi amesema kuwa baada ya wananchi kugundua tukio hilo walitoa taarifa polisi, ambapo walifika na kufukua mwili huo uliokuwa umezikwa kwa kutanguliza kichwa chini, na kukuta amekatwa kwa kitu chenye ncha kali shingoni na sehemu za siri.

Aidha kamanda huyo amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwasaka wananchi waliojichukuliwa sheria mkononi kwa kuchoma moto nyumba 16 na kufyeka migomba, mali za watu waliowatuhumu kumuua mwendesha bodaboda mmoja Albert Antipas, aliyetoweka tangu Januari 02 mwaka huu na maiti yake kupatikana ikiwa katika bwawa la kufugia samaki, Januari 07.

Amesema kuwa maiti ya mwendesha bodaboda huyo ilikutwa ikiwa imefungwa kwa kamba mikononi na miguuni, na kisha kufungwa katika jiwe na kuzamishwa katika bwawa hilo. 

Baada ya wananchi wa kijiji cha Kibingo tarafa ya Murongo wilayani Kyerwa kusikia kuwa watuhumiwa wamekamatwa na polisi, ndipo walipokwenda kuchoma moto nyumba zao.

Lori Laigonga Treni Jijini Dodoma.....Watu Wawili Wajeruhiwa

$
0
0
Na.Alex Sonna,Dodoma
Watu wawili wamenusurika kifo baada ya lori aina ya scania walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kwenda Iringa kuigonga treni ya mizigo katika makutano ya reli na barabara eneo la hazina jijini Dodoma.

Tukio hilo lilitokea jana mchana mara baada ya lori hilo lenye namba za usajili T463 ADW likiwa na tela lenye usajili T483 BLP kuiigonga treni hiyo iliyokuwa ikitoka jijini Dar es salaam kuelekea mikoa ya kanda ya ziwa.

Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa ajali hiyo imechangiwa na mvua zilizokuwa zikinyesha na kumfanya dereva wa lori kutoona kizuizi cha treni mbele yake.

Mmoja wa mashuhuda hao Ramadhani Rashid Mkazi wa Majengo amesema kuwa ajali hiyo ilichangiwa na dereva wa lori kutaka kukatiza kwa mwendo mkali lakini alikuwa kacheleWa hali iliyosababisha kugongwa na treni hiyo ya
mizigo.

“Dereva wa lori alikuwa katika mwendo mkali wakati akikatiza kivuko cha reli hivyo alishindwa kusimama na treni likawa limekaribia na kumgonga tumetoa watu wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya mwingine mmoja utumbo ukiwa nje”alisema

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Dodoma ACP William Mkonda, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo ni uzembe wa dereva wa lori ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi na majeruhi wamelazwa katika hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma

Rais Magufuli amtaka Waziri Mpya wa Madini Dotto Biteko kuanzisha vituo vya madini mikoa inayofanya shughuli za uchimbaji

$
0
0
Rais John Magufuli amemwagiza Waziri wa Madini, Dotto Biteko kuanzisha vituo vya madini kwenye maeneo yanayozalisha migodi nchini.

Alitoa maagizo hayo baada ya kuwaapisha viongozi wapya wa serikali jana  Jumatano, Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Rais Magufuli alieleza kuwa maagizo hayo yanalenga kudhibiti madini yanayoibwa na kupelekwa nje huku nchi kushindwa kunufaika ipasavyo.

“Ripoti mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki zinaonyesha Tanzania kuwa nyuma katika uuzaji wa dhahabu wakati sisi ndio tunaongoza katika uchimbaji, kwa ripoti hii ni lazima tujiulize tunakwama wapi? Dhahabu tunazochimba zinauzwa wapi? Soko lipo wapi na tunalijua? Tunapouza tunapata fedha kiasi gani? Wizara ipo na wataalamu wake na hapo ndio changamoto inapoonekana” Alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli aliagiza pia Waziri Biteko kushirikiana na Benki Kuu (BOT) kuweka mkakati utakaowezesha nchi kuanza kununua dhahabu na kuitunza. 

“Tanzania lazima isimame, hatuwezi kuendelea kuibiwa dhahabu, lazima tutunze dhahabu yetu, itatufaa hata shilingi yetu ikishuka,” aliongeza.

Rais Magufuli Akerwa na Viongozi Anaowateua Kuanza Kugombana Badala ya Kufanya Kazi

$
0
0
Rais John Magufuli ameweka wazi kwamba hafurahishwi na migogoro kati ya viongozi anaowateua na kusema kuwa amewaweka kiporo Mkuu wa Wilaya  na Mkurugenzi wake kutokana na matendo yao ya kugombana badala ya kufanya kazi hivyo wasifikiri kwamba hafahamu.
 
Rais Magufuli ameyasema hayo jana baada ya kumaliza kuapisha viongozi wapya aliowateua baada ya kufanya mabadiliko katika Wizara mbalimbali pamoja na Makatibu wa Wizara.

Rais alisema kwamba anafahamu changamoto ni nyingi katika utendaji wa kazi ingawa yapo mengine mazuri wanayofanya na kuwataka wahakikishe wanajitoa kwa maslahi ya wananchi.

"Nafahamu hizi kazi zina changamoto nyingi sana mfano kuna DC Gairo na Mbunge hawaelewani mpaka Mbunge anapost kumtukana DC tena mke wa mtu, hajui kama anaweza upoteza Ubunge, "I hope' siku moja ataomba msamaha kwenye Bunge", alisema Mh Rais Magufuli na kuongeza;

"Halmashauri ya Nyasa wanagombana sana DC na Mkurugenzi, nimewaangalia tu! nimewaachia kiporo chao. Pale Dodoma Mkurugenzi wa Jiji na DC walikuwa wanagombana nika-send meseji nikawaambia endeleeni kugombana siku moja mtagombania Vijijini, wamenyamaza naona yameisha".

Jipatie Dawa ya Asili ya Kupunguza Maziwa, Kupunguza Tumbo,Kuongeza Unene, Kuongeza Maumbile ya Kiume na Kuondoa Chunusi

$
0
0
Anza mwaka 2019 na mambo mapya kutoka kampuni ile ile inayofanya vizuri TANZANIA na nchi za NJE ambayo ni @natural_beauty_prod.

           BADO TUNATOA OFFA KAMA IVI👇👇👇
1. SHARK POWER--Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza uume urefu na upana mpaka nchi 7.5 ilikua inapatikana kwa @170,000/= sasa ni @160,000/= tu

2.VIGA 84000---Hii dawa ya kuspray yenye uwezo mkubwa wa kuchelewesha wakati wa tendo la ndoa ilikua ni  @160,000/=. Sasa ni 150,000/= tu

3. HANDSOME UP ORIGINAL-- Hichi ni kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo wewe pamoja na kuimalisha misuli kifaa hichi kilikua kinapatikana kwa @230,000/=. Sasa ni 210,000/= tu

4. MAXMAN CAPSULE--- Hii ni dawa ya vidonge ya kuongeza uume urefu na upana pamoja na kuongeza nguvu za kiume kwa wiki mbili ilikua inapatikana kwa @200,000/=. Sasa ni 180,000/= tu

5. VIG RX---- Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza uume urefu na upana mpaka nchi 10 ilikua inapatikana kwa @190,000/=. Bei ya sasa ni 170,000/=

6. BODY BOOSTER---Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza mwili pamoja na hamu ya kula vizuri ilikua inapatikana kwa @150,000/=. Sasa ni 140,000/=

7. BOTCHO MULT PLUS-- Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza (hips mapaja na makalio) kwa size uipendayo ilikua inapatikana kwa @200,000/=. Sasa ni 180,000/=

8. WHITE COLLECTION---- Ni vidonge vya kuwa mweupe mwili mzima pamoja na kuwa soft ilikua inapatikana kwa @150,000/= Sasa ni @140,000/= tu

9. BOTCHO HOLOGRAM CREAM--- Hii ni dawa ya kuongeza hips na makalio ilikua inapatikana kwa@180,000/= Sasa ni@160,000/=       

N.K

Wasiliana nasi kwa simu
NO:. +255 759029968  AU +255 659618585
Popote ulipo utapata huduma zetu.

Pia hakikisha unapatiwa risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY PROD ununuapo bidhaa kampuni hii.
               WELCOME ALL

Rudisha heshima yako Kwa Mpenzi Wako, Mke Wako...Tumia Tiba Hii ya Asili

$
0
0
Rudisha heshima yako sasa kwa kutumia Dawa hii iitwayo SUPER GAFINA, kwa ajili ya nguvu za kiume na NKOLOMIJE ni kwaajili ya kuongeza maumbile.

Kwa mwanaume aliye kamilika anatakiwa awe na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara mbili ,ila ukiwa unapiga moja tena kwa shida wewe ujue  unamatatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.

TIBA YA TATIZO LAKO NI; Dawa iitwayo SUPER GAFINA, dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge na unga wa asili ambavyo havina madhara kwa mtumiaji ambayo hutibu matatizo matatu kwa pamoja;-

1).itakufanya urudie tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuchoka.

2).ltakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dk.15 hadi 20 kwa tendo la kwanza.

3).lnaimarisha uume uliolegea na uliosinyaa na kuupa nguvu maradufu.

Je unamaumbile madogo pamoja na uume mfupi? NKOLOMIJE ni suluisho la tatizo lako. Na ni dawa inayoboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi kuanzia inch. 5 hadi 8 kwa muda mfupi sana .Dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk.30 ukisha tumia guarantee miaka 50  ikishakutibu.

Pia ninatibu;- KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU, MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE ,BP, NK.

IGULYATI, ni dawa ya mvuto wa biashara, kazi,kupandishwa cheo na humfanya mfanyakazi kupendwa na mwajiri wake. Pia humvuta mke,Mme,hawara ,mchumba unae muitaji utampata kwa dk.30 tu na atatulia na kumfunga asitoke nje ya ndoa, Pia natoa Pete za bahati ambazo zimetajirisha wengi.

Pia ipo dawa ya kupunguza matiti,unene ,tumbo,na kitambi ,hupunguza mafuta ,kuondoa makovu,chunusi,michilizi mwilini na kuongeza hipsi, makalio na mguu wa bia nk. 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na DR,HOSUTWA .Anapatikana Mbagara

Simu no, 0756241666 na 0672186977.

       Huduma hii utaipata popote ulipo

Makanga 3 Power, Dawa Bora Za Nguvu Za Kiume

$
0
0

Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.

Tupo dar es salam Buguruni

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images