Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Taarifa kwa Umma:Wagonjwa 45 Kufanyiwa Upasuaji Wa Moyo Wa Kufungua Na Bila Kufungua Kifua

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupitia madaktari wake bingwa wa magonjwa ya moyo kwa kushirikiana na Madaktari Afrika na Shirika la Cardio Start wote kutoka nchini Marekani  wameanza  kambi maalum ya matibabu ya moyo  ya siku 12  kwa watu wazima .

Matibabu yanayofanyika  katika kambi hiyo ni upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua. Upasuaji wa bila kufungua kifua unafanyika kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja kwa wagonjwa kuzibuliwa mishipa ya moyo iliyoziba (Percutaneous Coronary Intervention - PCI) na kuwekewa vifaa  vinavyosaidia kurekebisha mapigo ya moyo ambavyo ni (Permanent Pacemaker na High powered devices CRT-P, CRT –D) .

Wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ambayo ni  valve, mishipa ya moyo iliyoziba, moyo kushindwa kufanya kazi vizuri, matibabu kwa watu wazima waliozaliwa na matatizo ya moyo na wale wenye matatizo ya moyo yaliyotokana  na ugonjwa wa Kisukari

Kambi hii inaenda  sambamba na utoaji wa elimu kwa madaktari na wauguzi pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi kwa wageni na wataalamu wetu. Katika kambi hii tunatarajia kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa  20 na bila kufungua kifua kwa wagonjwa 25. Hadi leo tarehe 8/1/2019 jumla ya wagonjwa nane wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na wagonjwa wanne wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua.

Hii ni kambi ya kwanza ya matibabu ya moyo tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2019 na ni mara ya kwanza kwa shirika Cardio Start  kuja  hapa nchini kufanya kazi na sisi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
08/01/2019

Umoja wa Ulaya washushiwa hadhi ya kidiplomasia Marekani

$
0
0
Utawala wa rais Donald Trump umeishusha hadhi ya kidiplomasia ya ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Marekani. Afisa wa Umoja wa Ulaya amethibitisha taarifa hizo kwa shirika la utangazaji la Ujerumani, DW.

Hatua hiyo ya wizara ya mambo ya ndani ya Marekani ambayo haikutangazwa, na ambayo haijawahi kuripotiwa, iliishusha hadhi ya kidiplomasia ya ujumbe wa Umoja wa Ulaya mjini Washington kutoka nchi mwanachama hadi shirika la kimataifa. 

"Hatufahamu hasa lini walipochukua hatua hiyo, kwa sababu walisahau kutuarifu," afisa mmoja anayeifahamu vizuri kadhia hiyo ameiambia DW katika mahojiano maalumu. 

Ninaweza kuthibitisha uamuzi huu haujapokelewa vyema mjini Brussels," akasema afisa huyo na kuongeza kwamba suala hilo na jibu rasmi la Umoja wa Ulaya bado vinajadiliwa.

Baada ya ujumbe wa Umoja wa Ulaya kutambua kwamba balozi wake mjini Washington hakualikwa kuhudhuria matukio muhimu mwishoni mwa mwaka uliopita, maafisa walioandaa mazishi ya rais wa zamani wa Marekani, George H.W Bush, walitoa thibitisho la mwisho kwa wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya kwamba hadhi ya uwakilishi ilikuwa imeshushwa. 

Wanadiplomasia wanaamini hatua hiyo ilianza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi wa Oktoba au mapema Novemba.

Afisa wa Umoja wa Ulaya amesema, katika tukio hilo la Desemba 5, wakati wanadiplomasia walipokuwa wakikusanyika mjini Washington kutoa heshima zao, balozi wa Umoja wa Ulaya mjini Washington, David O'Sullivan, hakuitwa katika hali ya kawaida ya kufuata orodha ya mabalozi kuanzia waliohudumu kwa muda mrefu hadi wale waliohudumu kwa kipindi kifupi. Badala yake aliitwa kama mtu wa mwisho kabisa katika orodha hiyo.

Kabla ya kushushwa hadhi, O'Sullivan, ambaye amehudumu kama balozi wa Umoja wa Ulaya mjini Washington tangu mwaka 2014, angekuwa miongoni mwa mabalozi 20 au 30 kati ya wajumbe zaidi ya 150 wa kigeni wanaohudumu katika mji mkuu huo wa Marekani.

Chanzo:DW

Zitto Kabwe kwenda Mahakamani sakata la CAG na Spika Ndugai

$
0
0
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameeleza kuwa wamepanga kwenda mahakamani kuhusu sakata la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof.  Prof. Mussa Assad.

"Baada ya kushauriana na Wanasheria na Wabunge tumeona ni muhimu sana kwa maslahi mapana ya nchi yetu kulinda Katiba yetu. Baadhi ya Wabunge kutoka vyama vyote tumeamua kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya KINGA ya CAG kwa mujibu wa Katiba na mamlaka ya Spika kutoa Wito kwa CAG,"ameandsika Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Utakumbuka hapo jana Spika Ndugai alimtaka CAG, Prof. Mussa Assad  kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 21 mwaka huu kujieleza kufuatia kauli za kudhalilisha Bunge

LHRC Wametoa Ufafanuzi wa Kisheria Kuhusu Mamlaka na Mipaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali-CAG

$
0
0
UFAFANUZI WA KISHERIA KUHUSU MAMLAKA NA MIPAKA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CONTORLLER AND AUDITOR GENERAL -CAG)

Ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali ni ofisi ambayo imeundwa kikatiba kupitia Ibara ya 143 na 144 ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa mara kwa mara.

Ibara hiyo kwa ufupi inaeleza ifuatavyo;
143.-(1) Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano.(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa na jukumu juu ya mambo yafuatayo:
 
(a) kuhakikisha kwamba fedha zozote zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali matumizi yake yameidhinishwa na kwamba zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 136 ya Katiba hii, na iwapo atatosheka kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo, basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe;
 
(b) kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi yake yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au fedha ambazo matumizi yake yameidhinishwa na sheria iliyotungwa na Bunge, na ambazo zimetumika, zimetumiwa kwa ajili ya shughuli zilizo husika na matumizi ya fedha hizo na kwamba matumizi hayo yamefanywa kwa kufuata idhini iliyotolewa kuhusu matumizi hayo; na
 
(c) angalau mara moja kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa taarifa juu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano, hesabu zinazosimamiwa na watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na hesabu za Mahakama zote za Jamhuri ya Muungano na hesabu zinazosimamiwa na Katibu wa Bunge.
 
(3) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu na kila mtumishi wa Serikali aliyeruhusiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa na haki ya kuchunguza vitabu, kumbukumbu, hati nyinginezo zote zinazohusika na hesabu za aina yoyote iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii.
 
(4) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atawasilisha kwa Rais kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) ya ibara hii. Baada ya kupokea taarifa hiyo Rais atawaagiza watu wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofanyika baada ya Rais kupokea taarifa hiyo na itabidi iwasilishwe katika kikao hicho kabla ya kupita siku saba tangu siku ile kilipoanza kikao hicho.
 
Iwapo Rais hatachukua hatua za kuwasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge (au Naibu wa Spika ikiwa kiti cha Spika ki wazi wakati huo au ikiwa kwa sababu yoyote Spika hawezi kutekeleza shughuli za kazi yake) ambaye atawasilisha taarifa hiyo kwenye Bunge.
 
(5) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa pia na jukumu la kutekeleza kazi na shughuli nyingine, na atakuwa na madaraka mengine ya namna mbalimbali, kama itakavyoelezwa na sheria kuhusu hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano au hesabu za vyombo vya Umma au hesabu za Mashirika.
 
(6) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2), (3) na (4) ya ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au sivyo.

Uwajibikaji/Kuwajibishwa kwake

1.Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anawajibika kwa Rais sio kwa Bunge. Ibara ya 143 (4). Bungeni huwasilisha taarifa ambayo imetoka kwa Rais.

ii.Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikai halazimiki kufuata Maagizo ya mtu yeyote Ibara ya 143 (6).

iii.Mahakama ina uwezo wa kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii ama sivyo.Ibara ya 143 (6).

iv.Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ataondoka kazinikwa yafuatayo;

a)Kustaafu
b)Kuugua
c)kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. lbaya ya 144

v.Kuondolewa kazini kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ni mchakato mrefu unaoanza na Rais kuteua Turne Maalum ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili.Ibara ya 144 (3).
 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya January 9

Ufafanuzi Toka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kuhusu Usimamizi Kwa Watoa Huduma Ndogo Za Fedha

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania imetoa tangazo kwa umma kupitia tovuti yake (www.bot.go.tz) likiwataka watu na taasisi zote zinazofanya biashara ya huduma ndogo za fedha zilizoko Tanzania Bara (isipokuwa vyama vya ushirika vya akiba na mikopo – SACCOS) kutoa taarifa zitakazotumika katika utayarishaji wa Kanuni za Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha. Taarifa hizo zinatakiwa kutumwa Benki Kuu ya Tanzania hadi tarehe 31 Januari 2019.

Benki Kuu inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao kuhusu tangazo hilo:

Lengo la tangazo hilo siyo kuvifunga au kuvibana vikundi vya kijamii kama VICOBA, watu binafsi na taasisi zinazotoa huduma ndogo za fedha kama ambavyo inapotoshwa na baadhi ya watu na mitandao mbalimbali ya kijamii, bali ni kukusanya taarifa za awali kuhusu huduma hizo. 

Kama ilivyoainishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kupitisha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, lengo la sheria hiyo  ni kuwalinda wadau wote wanaohusika na huduma hizi (watoaji na watumiaji) kwa kuziwekea utaratibu mzuri zaidi wa uwekaji kumbukumbu, uendeshaji na uongozi kwa ujumla. 

Pia kuwalinda wamiliki na watumiaji wa huduma hizi dhidi ya vitendo vinavyoweza kupelekea kupoteza fedha na mali zao, pamoja na kuzuia watu binafsi, taasisi na vikundi vya kijamii kutumika kufanya uhalifu ikiwemo utakasishaji fedha haramu.
 
Benki Kuu inafahamu kuwa baadhi ya watu binafsi, taasisi na vikundi vinavyotoa huduma ndogo za fedha vikiwemo VICOBA, havina usajili rasmi na hivyo havitambuliki kisheria. 

Kwa kutambua hilo, Sheria imeweka kipindi cha mpito cha mwaka mmoja (kuanzia sheria itakapoanza kutumika rasmi) kwa wote wanaojihusisha na utoaji huduma ndogo za fedha, kujipanga ili wawe tayari kusimamiwa pale kanuni zitakapokuwa zimetolewa rasmi. 

Hivyo, katika kipindi hiki cha mpito, siyo kosa kwa watu binafsi, taasisi na vikundi vya kijamii kutokuwa na usajili rasmi.  

Aidha, Wadau wote watashirikishwa kikamilifu katika utayarishaji wa Kanuni hizo, na mara zitakapokuwa tayari na kutolewa na Benki Kuu ya Tanzania, maelezo zaidi kuhusu usajili yatatolewa.

Benki Kuu inawasihi wananchi wote kutokuwa na taharuki na inasisitiza kwamba uamuzi wa kusimamia watoa huduma ndogo za fedha umechukuliwa kwa nia njema na  kwa faida ya watumiaji na watoaji wa huduma hizi.

Aidha, Benki Kuu  inautahadharisha umma kujiepusha na taarifa na miongozo inayotolewa kiholela na watu, kampuni na mashirika ambayo yanajitangaza kufanya shughuli za uandikishaji wa watoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi kwa niaba ya Serikali au Benki Kuu. 

Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu, kampuni au shirika lolote litakalojihusisha na vitendo vya kuwakanganya wananchi kwa lengo la kupotosha au/na kujipatia mapato haramu.

Tunawahamasisha wananchi kufuatilia taarifa zaidi kuhusu tangazo hili zinazoendelea kutolewa na Benki Kuu katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu usimamizi wa watoa huduma ndogo za fedha Tanzania Bara.

Kwa ufafanuzi/maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu   022-2235585/0767503145 au barua pepe:vctarimu@bot.go.tz, nfmongateko@bot.go.tz, dasasya@bot.go.tz, botcommunications@bot.go.tz, au tembelea Benki Kuu Makao Makuu Mtaa wa 2 Mirambo, 11884 Dar es Salaam Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha.

Waziri Mkuu Afungua Jengo La Taasisi Ya Karume Ya Sayansi Na Teknolojia

$
0
0
*Asema kukamilika kwa taasisi hiyo kutakuwa na manufaa makubwa kwa jamii

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa  amefungua Jengo la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), wilaya ya Magharibi ‘B’ lililojengwa kwa ghararama ya sh. bilioni 4.2.

Afungua jengo hilo jana (Jumanne, Januari 8, 2019) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyotokea Januari 12, 1964.

Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa Jengo la taasisi hiyo kuna manufaa makubwa kwa jamii ikiwemo kutoa elimu ya ufundi itakayowasaidia vijana kujiajiri na kuondokana na utegemezi.

“Kusaidia azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 na msukumo katika sekta ya viwanda kwa vijana kujiajiri na kuajiriwa katika sehemu mbalimbali pamoja na Serikalini.”

Amesema manufaa mengine ya KIST ni kutoa mafunzo ya fani mbalimbali zinazokwenda sambamba na mabadiliko ya ulimwengu katika Nyanja za sayansi, teknolojia na ualimu.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa KIST ubuni mbinu mbalimbali na utafute miradi mingine ya ujenzi itakayosaidia kuwa na miundombinu ya kisasa ya kutolea elimu.

Amesema uongozi wa taasisi hiyo hauna budi kuweka mikakati ya kushirikiana na taasisi nyingine zinazotoa mafunzo ya ufundi ndani na nje ya nchi ili kubadilishana uzoefu.

Waziri Mkuu amesema kulingana na maendeleo ya kiteknolojia na mahitaji ya soko uongozi wa KIST ujipange kutoa mafunzi ya biomedical Engineering na kuimarisha mafunzo ya matengenezo ya ndege na urubani katika ngazi ya stashahada.

Awali, Waziri wa Elimu na Mafunzi ya Amali, Riziki Pembe Juma alisema Wizara yake itaendeleza taasisi hiyo ili kuwaendeleza vijana na baadae waweze kujiajiri na kuajiri.

Alisema vijana wanaohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika taasisi hiyo wanapewa mikopo ya masharti nafuu na Serikali baada ya kujiunga kwenye vikundi.

Waziri Huyo, alisema wahitimu hao kabla ya kupewa mikopo wanaandika andiko la miradi ambayo watakwenda kuitekeleza ambapo tayari vikundi zaidi ya 10 vya vijana vimeshawezeshwa.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Naibu Waziri Dk Mabula Akerwa Makusanyo Madogo Ya Kodi Ya Ardhi Katika Halmashauri

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM Geita
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amekerwa na makusanyo madogo ya mapato katika halmashauri mbalimbali nchini kupitia kodi ya ardhi.

Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi wa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita jana mkoani Geita alipofanya ziara ya kushtukiza kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa katika halmashauri hizo, Dk Mabula alisema, mapato ya sekta ya ardhi katika halmashauri nyingi hayaridhishi na kueleza kuwa halmashauri nyingi mapato yake yako chini ya asilimia 30.

Alisema pamoja na halmashauri hizo kuwa na mapato kidogo kupitia sekta ya ardhi lakini watendaji wake hawaoneshi jitihada zozote kuhakikisha wanakusanya mapato ya kutosha kupitia sekta hiyo na hivyo aliwataka watendaji hao kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwa kuwa msisitizo wa serikali ya awamu ya tano ni kukusanya kodi.

‘’Kwa staili hii tutafika kweli? Mna bahati mbaya sasa watendaji wa sekta ya ardhi katika halmshauri mtakuwa chini ya wizara moja kwa moja na rais amepiga kelele kuhuisiana na kodi ninyi mnarelax’’ alisema Dk mabula.

Hata hivyo, Dk Mabula aliisifu halmashauri ya Mji wa Geita kwa kukusanya mapato kwa zaidi ya asilimia sitini. Kwa Mujibu wa taarifa ya Halmshauri ya Mji wa Geita, kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba 2018, halmashauri hiyo imekusanya jumla ya shilingi 389,699,937.28 kati ya milioni 600,000,000 ilizopanga kukusanya.

Kwa upande wake Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupitia, Afisa Ardhi wake Faraja Kaluwa pamoja na halmashauri hiyo kupewa malengo ya kukusanya milioni 150 lakini kufikia desemba 2018 imefanikiwa kukusanya shilingi milioni 12,480,500 tu.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwataka wakuu wa idara za ardhi katika halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita kutoa ahadi ya utekelezaji maagizo aliyoyatoa na hatua gani zichukuliwe kwao iwapo maagizo hayatatekelezwa kwa wakati.

Maagizo aliyoyatoa Dk Mabula ni kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya kodi ya ardhi, uingizaji viwanja na mashamba katika mfumo wa kielektronik, utoaji hati za ardhi pamoja na utoaji hati za Madai (demand notes) kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi.

Aidha, Dk Mabula ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaingiza viwanja na mashamba kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya kielektronik na kutaka kasi ya utoaji hati kuongezeka ili kuwawezesha wananchi kiuchumi na wakati huo kuiingizia serikali mapato kupitia kodi ya ardhi.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha zinatoa leseni za makazi katika maeneo yenye nyumba zilizojengwa nje ya urasimishaji na mipango Miji na kueleza kuwa zoezi hizo linatakiwa kukamilika mwezi machi mwaka huu.

Dk Mabula amezitaka Halmashauri kuanisha maeneo yote ya nyumba hizo na kupatiwa leseni za makazi kwa gharama ya shilingi 5000 sambamba na kuziingiza katika kumbukumbu za halmashauri na kubainisha kuwa leseni hizo ni hatua za kuelekea wamiliki wake kupatiwa hati.

Mfumuko wa Bei kwa Mwaka 2018 Washuka, Wavunja Rekodi Miaka 40

$
0
0
Na: Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma
Wastani wa Mfumuko wa Bei wa Taifa kutoka Januari hadi Desemba Mwaka 2018 umepungua hadi asilimia 3.5 kutoka wastani wa asilimia 5.3 kama ilivyokuwa mwaka 2017.

Hayo yamesemwa jana  jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa mwezi Desemba 2018 pamoja na wastani wa mfumuko huo kwa mwaka mzima.

“Wastani huu wa mfumuko wa bei wa mwaka wa asilimia 3.5 ndiyo wastani mdogo kabisa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 40 iliyopita ambapo tangu mwaka 1970 mfumuko huo ulikuwa 3.6,” ameongeza Kwesigabo.

Aidha, akizungumzia kuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Desemba ,2018, Kwesigabo amesema kuwa mfumuko huo umeongezeka hadi kufikia asilimia 3.3 kutoka asilimia 3.0 kwa mwezi Novemba 2018.

“Kuongezeka kwa Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2018 kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Desemba, 2018 zikilinganishwa na bei za mwezi Desemba, 2017, mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Desemba, 2018 umeongezeka hadi asilimia 1.0 kutoka asilimia 0.4 ilivyokuwa mwezi Novemba, 2018,” amefafanua Kwesigabo.

Aidha amesema kuwa, baadhi ya bidhaa ya chakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na nyama kwa asilimia 4.6, samaki wabichi asilimia 8.2, dagaa asilimia 26.2, matunda kwa asilimia 4.3 na mbogamboga asilimia 8.5 baadhi ya bidhaa zisizo za chakula zilizochangia mfumuko wa bei ni pamoja na vitambaa vya kushonea nguo kwa asilimia 2.1, nguo za kiume na za kike kwa asilimia 6.1, nguo za watoto kwa asilimia 3.0, sare za shule kwa asilimia 3.1, dizeli kwa asilimia 27.6, petroli asilimia 10.8 na huduma za malazi kwa asilimia 6.8.

Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki, mfumuko wa bei kwa mwaka unaoishia mwezi Desemba, 2018 nchini Kenya umeongezeka hadi kufika asilimia 5.71 kutoka asilimia 5.58 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2018 na mfumuko wa bei kwa mwaka unaoishia mwezi Desemba, 2018 nchini Uganda umepungua hadi kufika asilimia 2.2 kutoka asilimia 3.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2018.

Serikali Kusaini Mikataba Ya Ubanguaji Wa Korosho Januari 10

$
0
0
 Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara
Serikali imesema kuwa tarehe 10 Januari 2019 itasaini mikataba na wamiliki wa viwanda vya ubanguaji wa korosho waliojitokeza kwa ajili ya kubangua korosho za serikali za msimu wa mwaka 2018/2019 zilizonunuliwa na serikali kwa bei ya Shilingi 3300 kwa kilo.

Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo jana tarehe 8 Januari 2019 wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara.Alisema kuwa hivi karibuni serikali ilitangaza kuwa korosho ghafi zote zitabanguliwa nchini hivyo utekelezaji wa jambo hilo umeanza, ambapo Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko itaingia mikataba ya ubanguaji.

Pamoja na wamiliki wa viwanda kupewa kazi ya kubangua korosho lakini pia serikali imewakaribisha wananchi kujitokeza kubangua korosho za serikali kupitia vikundi au mtu mmoja mmoja. “Wananchi wenye uwezo wa kubangua tunawaomba waende Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo-SIDO) kwa ajili ya kujiandikisha ambapo mpaka sasa watu 126 kwa ajili ya ubanguaji na Tani 29 zimechukuliwa kwa ajili ya kuanza kubanguliwa” Alisisitiza Mhe Hasunga

Katika mkutano huo Waziri huyo wa kilimo Mhe Japhet Hasunga amempongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kushuhudia utiaji wa saini mkataba wa mauziano ya mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) wa Bilioni 21 zitakazoiwezesha NFRA kunua mahindi kwa wakulima hivyo kuimarisha soko la nafaka nchini.

Mhe Hasunga alisema kuwa pamoja na kuanza ubanguaji kupitia SIDO lakini serikali imeanza mchakato wa kukufua viwanda vya ubanguaji vya serikali na watu binafsi nchini ili kuongeza ajira kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo vya wabanguaji wadogo wadogo.

Akizungumzia kuhusu swala la malipo ya korosho na uhakiki wa wakulima alisema kuwa tayari kiasi cha korosho ambayo imekusanywa kwenye maghala makuu ni Tani 203,938.3 wakati korosho iliyopo kwenye Vyama vikuu vya ushirika ni Tani 29,803.53 inayofanya jumla ya korosho yote iliyopokelewa kwenye vyama vya ushirika na maghala makuu kuwa Tani 233,741.83 sawa na asilimia 84.7 ya lengo lililowekwa la ukusanyaji katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Pwani.

Kuhusu malipo ya wakulima alisema kuwa miamala ya malipo ambayo imefanyika ni 261,458 yenye jumla ya watu 203,569. Aidha, vyama 490 vilimelipwa kati ya vyama 617, Alisema Mkoa wa Mtwara jumla ya vyama 39 bado havijalipwa, Mkoa wa Lindi vyama vitano na Ruvuma viwili hivyo serikali imejipanga ndani ya wiki mbili vyama hivyo kuwa vimelipwa.

Waziri Hasunga amesema kuwa mpaka kufikia jana tarehe 7 Januari 2019 fedha ambazo zimeingizwa kwenye Account za wakulima ni zaidi ya Bilioni 257 huku ambazo tayari zimeingia kwenye Account za wakulima ni Bilioni 226.2 ambapo Zaidi ya Bilioni 30.7 zilizohakikiwa bado hazijaingizwa kwenye Account za wakulima kutokana na taarifa za baadhi ya wakulima hao kutofautiana majina ama vinginevyo. “Tunawaomba sana wananchi kwenda Benki kujiridhisha kama Account zao zinafanya kazi kwani serikali ina fedha za kuwalipa wakulima wote wa korosho” Alisema

“Tena nisisitize kwa wale wanaofanya biashara ya korosho kinyume na utaratibu maarufu kama (Kangomba) wajisalimishe na kuomba radhi wenyewe kuliko kusubiri serikali iwabaini” Alisema.Vilevile, Mhe Hasunga alisema kuwa wizara yake imeweka mikakati mbalimbali ambapo hadi kufikia Januari 31 mwaka huu zoezi la uhakiki wa wakulima wanaostahili kulipwa liwe limekamilika ambapo zaidi ya asilimia 80 ya wakulima wawe wamelipwa.

Pia amewataka wananchi kupuuza taarifa mbalimbali zizotolewa na baadhi ya wananchi wasiolitakia mema Taifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa serikali hailipi wakulima badala yake amesisitiza kuwa serikali ina fedha za kutosha kulipa wakulima wa korosho isipokuwa kangomba wao hawatalipwa.

Jipatie Dawa ya Asili ya Kupunguza Maziwa, Kupunguza Tumbo,Kuongeza Unene, Kuongeza Maumbile ya Kiume na Kuondoa Chunusi

$
0
0
Anza mwaka 2019 na mambo mapya kutoka kampuni ile ile inayofanya vizuri TANZANIA na nchi za NJE ambayo ni @natural_beauty_prod.

           BADO TUNATOA OFFA KAMA IVI👇👇👇
1. SHARK POWER--Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza uume urefu na upana mpaka nchi 7.5 ilikua inapatikana kwa @170,000/= sasa ni @160,000/= tu

2.VIGA 84000---Hii dawa ya kuspray yenye uwezo mkubwa wa kuchelewesha wakati wa tendo la ndoa ilikua ni  @160,000/=. Sasa ni 150,000/= tu

3. HANDSOME UP ORIGINAL-- Hichi ni kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo wewe pamoja na kuimalisha misuli kifaa hichi kilikua kinapatikana kwa @230,000/=. Sasa ni 210,000/= tu

4. MAXMAN CAPSULE--- Hii ni dawa ya vidonge ya kuongeza uume urefu na upana pamoja na kuongeza nguvu za kiume kwa wiki mbili ilikua inapatikana kwa @200,000/=. Sasa ni 180,000/= tu

5. VIG RX---- Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza uume urefu na upana mpaka nchi 10 ilikua inapatikana kwa @190,000/=. Bei ya sasa ni 170,000/=

6. BODY BOOSTER---Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza mwili pamoja na hamu ya kula vizuri ilikua inapatikana kwa @150,000/=. Sasa ni 140,000/=

7. BOTCHO MULT PLUS-- Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza (hips mapaja na makalio) kwa size uipendayo ilikua inapatikana kwa @200,000/=. Sasa ni 180,000/=

8. WHITE COLLECTION---- Ni vidonge vya kuwa mweupe mwili mzima pamoja na kuwa soft ilikua inapatikana kwa @150,000/= Sasa ni @140,000/= tu

9. BOTCHO HOLOGRAM CREAM--- Hii ni dawa ya kuongeza hips na makalio ilikua inapatikana kwa@180,000/= Sasa ni@160,000/=       

N.K

Wasiliana nasi kwa simu
NO:. +255 759029968  AU +255 659618585
Popote ulipo utapata huduma zetu.

Pia hakikisha unapatiwa risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY PROD ununuapo bidhaa kampuni hii.
               WELCOME ALL

Rudisha heshima yako Kwa Mpenzi Wako, Mke Wako...Tumia Tiba Hii ya Asili

$
0
0
Rudisha heshima yako sasa kwa kutumia Dawa hii iitwayo SUPER GAFINA, kwa ajili ya nguvu za kiume na NKOLOMIJE ni kwaajili ya kuongeza maumbile.

Kwa mwanaume aliye kamilika anatakiwa awe na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara mbili ,ila ukiwa unapiga moja tena kwa shida wewe ujue  unamatatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.

TIBA YA TATIZO LAKO NI; Dawa iitwayo SUPER GAFINA, dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge na unga wa asili ambavyo havina madhara kwa mtumiaji ambayo hutibu matatizo matatu kwa pamoja;-

1).itakufanya urudie tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuchoka.

2).ltakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dk.15 hadi 20 kwa tendo la kwanza.

3).lnaimarisha uume uliolegea na uliosinyaa na kuupa nguvu maradufu.

Je unamaumbile madogo pamoja na uume mfupi? NKOLOMIJE ni suluisho la tatizo lako. Na ni dawa inayoboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi kuanzia inch. 5 hadi 8 kwa muda mfupi sana .Dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk.30 ukisha tumia guarantee miaka 50  ikishakutibu.

Pia ninatibu;- KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU, MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE ,BP, NK.

IGULYATI, ni dawa ya mvuto wa biashara, kazi,kupandishwa cheo na humfanya mfanyakazi kupendwa na mwajiri wake. Pia humvuta mke,Mme,hawara ,mchumba unae muitaji utampata kwa dk.30 tu na atatulia na kumfunga asitoke nje ya ndoa, Pia natoa Pete za bahati ambazo zimetajirisha wengi.

Pia ipo dawa ya kupunguza matiti,unene ,tumbo,na kitambi ,hupunguza mafuta ,kuondoa makovu,chunusi,michilizi mwilini na kuongeza hipsi, makalio na mguu wa bia nk. 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na DR,HOSUTWA .Anapatikana Mbagara

Simu no, 0756241666 na 0672186977.

       Huduma hii utaipata popote ulipo

Katibu Mkuu CCM Dk. Bashiru Ally Awapatanisha Anthony Diallo na Said Meck Sadiki

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amemwonya aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Said Meck Sadiki kuacha kuendeleza fitina na badala yake ashirikiane na mshindi halali wa kiti hicho, Anthony Diallo kujenga chama.

Onyo hilo alilitoa jana wakati akizungumza na wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Mkoa wa Mwanza ambacho kiliwahusisha pia watendaji wa serikali ngazi ya mkoa, wilaya na halmashauri kuangalia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi.

Baada ya hotuba yake hiyo, Dk. Bashiru aliwaita Diallo na Sadiki mbele ya wanachama na kuwataka kupeana mikono ya heri na kukumbatiana ikiwa ni ishara ya kuondoa tofauti zao na kuwa kitu kimoja ili mkoa uweze kuwa imara na kushinda uchaguzi ujao. 

Dk Bashiru alisema, Sadick alifikisha malalamiko ya kumpinga Dk Diallo ambapo kila mmoja alisikilizwa na uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM iliamuru aliyeshinda uchaguzi wa mwaka jana awaongoze.

Alisema viongozi hao walielezwa kuwaunganisha wanachama kukiimarisha chama na kukinadi kwa wananchi wazidi kukiunga mkono lakini Meck Sadiki ameendeleza fitina za chini chini, jambao ambalo ni hatari kwa ustawi wa  chama hicho.

Alisema anatambua Meck Sadik na Dk Dialo ni marafiki lakini wanagawanywa na wanachama na makada ambao dhamira yao washindwe kushirikiana na viongozi kusimamia maendeleo ya wananchi, hivyo aliwaonya kwa pamoja kuachana na tofauti hizo.

“Tukiendekeza migogoro na makundi ya watu  hatutafika salama maana tutatoa mwanya kwa watu  kufanya ubinafsi kwa maslahi yao.

“Kwanza kinachoendelea kati ya Dk Diallo na Sadick ni sawa na kukidhalilisha chama na wananchi, hali ambayo husababisha kukichukia na kukiadhibu kwenye baadhi ya maeneo,” alisisitiza katibu mkuu huyo.

Aidha Dk Bashiru aliwataka viongozi wa chama ngazi ya mkoa na wilaya kutowapokea na kuungana nao kwenye ziara zao mawaziri ambao hawapiti na kujitambulisha kwenye ofisi za chama hicho na pengine hata kuelezwa kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Awali Dk Bashiru alitembelea na kukagua shamba la ekari 29.23 la CCM lililopo Kijiji na Kata ya Katunguru Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza ambapo alipendekeza kijengwe chuo cha uongozi cha chama ili kusaidia kuelimisha viongozi wa CCM wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Kwa upande wake, Dk Diallo  alisema kwamba wamepokea kwa mikono miwili ushauri na maelekezo ya katibu mkuu huyo na watayafanyia kazi ili chama kiwe imara.

Naibu Waziri atangaza upungufu wa tani 260,000 za sukari Nchini

$
0
0
Serikali imesema taifa kwa sasa linakabiliwa na upungufu wa sukari, zaidi ya tani 260,000 ambazo zinapaswa kuwa sehemu ya mahitaji ya lazima kama nchi.

Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba amekiri kuwa upo upungufu wa sukari ya viwandani tani 155,000 na kwa sukari ya mezani, upungufu ni zaidi ya tani 105,000.

Mgumba alitoa taarifa kuhusu upungufu huo, wakati alipokwenda kujionea hali halisi ya uzalishaji wa sukari katika Kiwanda cha Sukari cha TPC Moshi.

“Tumeanza ziara ya siku sita mikoani na leo (jana), tumeanzia Kilimanjaro na kisha tutakwenda mikoa yote inayolima miwa ili kusikiliza, kupokea changamoto na kuzitatua kwa pamoja.

“Tutahakikisha tunamaliza upungufu huu wa sukari hapa nchini, wawekezaji tuelezeni sisi serikali changamoto zinazowakabili wakati wa uzalishaji ili tukae na kuona njia bora ya utatuzi wake, kuacha mazingira bora ya uzalishaji.”

Katika ukaguzi huo, Naibu Waziri Mgumba ameongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Profesa Kenneth Bengesi.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, mkurugenzi huyo ameeleza bayana kwamba bado mahitaji ya sukari hapa nchini ni makubwa na kuwataka wawekezaji waliowekeza katika viwanda vya sukari kuitazama fursa hiyo na kuifanyia kazi.

Kutokana na mahitaji hayo, Profesa Bengesi alisema: “Tumeweka mazingira rafiki ya wawekezaji kuwekeza katika sekta ya sukari, tunawakaribisha kwa sasa, serikali imedhamiria kuingia katika uchumi wa kati wa viwanda.”

Awali akitoa taarifa ya uzalishaji wa sukari kwa Naibu Waziri huyo, Ofisa Mtendaji Mkuu na Utawala wa TPC, Jafary Ally, alisema tangu walipowekeza katika kiwanda hicho wameweza kuongeza uzalishaji kutoka 36,000 hadi kufikia tani 110,000 kwa mwaka.

“Mawazo ya serikali ya kututaka kuzalisha sukari ya viwandani, tumeyapokea na tutakaa na bodi yetu kuona kama tunaweza kuwekeza katika sekta hiyo. Hata hivyo, tunaipongeza serikali kwa kuziba mianya yote ya uingizaji kiholela wa sukari kutoka nje, sasa wawekezaji wana uhakika wa soko,”alieleza Jafary.

LIVE: Rais Magufuli akiwaapisha Viongozi Wapya aliowateua jana.

$
0
0
LIVE: Rais Magufuli akiwaapisha Viongozi Wapya aliowateua jana.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Makanga 3 Power, Dawa Bora Za Nguvu Za Kiume

$
0
0

Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.

Tupo dar es salam Buguruni

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348.

CCM Yamtaja Atakayegombea Urais Mwaka 2020

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa alichokifanya Rais Magufuli kwa kipindi hiki kifupi alichokaa madarakani, ni dhahiri kuwa hakuna mwingine atakayepewa ridhaa na chama zaidi yake kugombea 2020.

Polepole ametoa kauli hiyo leo katika kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio ambapo amesema CCM haina sababu ya kupitisha mgombea mwingine ikiwa Rais Magufuli amefanya vitu vikubwa na bado uwezo na nguvu ya kulitumikia taifa bado anao.

"Mwaka 2020 hatuna shaka katika nafasi ya Urais mgombea wetu ni Rais Magufuli hatuna wasiwasi kabisa na kiongozi wetu kwa aliyofanya kwa kipindi hiki njia ni nyeupe, lakini hatujakataza wengine kuchukua fomu wao wachukue tu", amesema Polepole.

Akizungumzia kupunguzwa kwa wanachama wanaotakiwa kupiga kura za maoni amesema kuwa, "Sisi hatuukatai ubaya ambao ulikuwepo zamani, tunakiri na kufuta kwa kufanya mema, CCM tuna kadi za kielektroniki hivyo huwezi kupiga kura ya maoni, kama huna kadi ile na sio kwamba tumewapunguza bali ni mabadiliko ya teknolojia hivyo wahakikishe wanakubaliana na mabadiliko na hakuna aliyefukuzwa".

Aidha Polepole amesema kuwa chama chake, hakipokei tena watu wanaotoka upinzani wao wabaki hukohuko usajili umeshafungwa, na kudai kuwa waliobaki hawana vigezo na wajiandae kuachia majimbo 2020.

Breaking News: Rais Magufuli Afunguka Mambo Mazito Sakata la Dhahabu ya Mamilioni ya Pesa Iliyonaswa Jijini Mwanza

$
0
0
Rais Magufuli amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania-IGP Simon Sirro  kwa kuhakikisha watuhumiwa wote wa Dhahabu ya mamilioni ya pesa iliyokuwa inatoroshwa jijini Mwanza wamekamatwa wakiwemo Askari polisi 8.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo Leo Jumatano January 9, 2019  Ikulu Dar es Salaam wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua jana.

Akisimulia kwa kina kuhusu tukio hilo, Rais Magufuli amesema watuhuhiwa hao walikamatwa January 4 Misungwi, kisha wakarudishwa kituo kikuu cha kati, lakini hawakuwekwa Mahabusu.

"Kwa taarifa nilizonazo, watuhumiwa wale walishikwa Januari 4, wilayani Misungwi, wakarudishwa mjini Mwanza na Kikosi cha Polisi nane, wakawapeleka Central wala hawakuwaingiza ndani, watuhumiwa walikuwa kwenye gari, wakawa wanajadili namna ya kuwapa hela, wakawaambia watawapa Bilioni 1 "  Amesema Rais Magufuli

Amesema, watuhumiwa hao walitoa Rushwa ya milioni 700, ikawa imebaki milioni 300 ambayo polisi hao waliahidiwa kwamba watapewa wakifika Sengerema.

Rais Magufuli ameendelea kusimulia kuwa, usiku huo  watuhumiwa waliondolewa Central  huku wakisindikizwa na Polisi hao kuelekea Sengerema.

“Askari  Polisi hao waliendelea kuzunguka na watuhumiwa hao  kwa kutumia magari na mafuta ya Serikali, wakavuka Kigongo Ferry kuelekea Sengerema. "Amesema Rais Magufuli

Rais amesema taarifa za kiintelijensia zikawa zimemfikia, akatoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwamba watu hao wafuatiliwe haraka na wakamatwe.

"Niliwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema ili wakamatwe, iliwekwa road block na wakakamatwa. Askari wale wakaanza kupiga king’ora eti walikuwa wanawafukuza kumbe walikuwa wanawasindikiza. "Amesimulia Rais Magufuli.

“Nakupongeza sana IGP kwa kuwashughulikia askari hao, tena huyo Superintendent wa Polisi aliyekuwa akisindikiza huo mzigo umemvua cheo, na watapelekwa kwenye mahakama za kijeshi kisha mahakama za kiraia,” Amesema


Spika Ndugai awaombea likizo Mawaziri kwa Rais Magufuli

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Job Ndugai, amewaombea likizo Mawaziri wa Tanzania kwa Rais John Pombe Magufuli.

Spika Ndugai, ametoa ombi hilo kwa Rais Magufuli, leo Januari 9 wakati akiwapongeza viongozi walioapishwa kutumikia nafasi mbalimbali wakiwepo Mawaziri na Makatibu Wakuu.

Mh. Ndugai amesema kwamba Mawaziri wa awamu ya tano wanachapa kazi sana kiasi ambacho hakijawahi kutokea, hivyo ameona bora awaombee likizo japo ya mwezi ili waweze kupumzika.

"Serikali ya awamu ya tano ina kasi ya kipekee sana. Wakati zoezi la kuapishwa linaendelea nikawa naangaliana na waheshimiwa mawaziri wanaonekana wamechoka sana nikajiuliza hivi wanalikizo. Mheshimiwa Rais nawaombea likizo japo ya mwezi kila mmoja mmoja. ", amesema Spika Ndugai.

Hata hivyo, Rais Magufuli amewataka Mawaziri pamoja na watendaji wengine wa Serikali wavumilie tu maana hata yeye hana likizo na hajawah chukua Likizo tangu achaguliwe kuwa Rais
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images