Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mshtakiwa adai Waziri Lukuvi Alimkaba na kumpora Begi la Pesa

$
0
0
Mkurugenzi wa Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa amedai mahakamani kwamba Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alimkaba akiwa ofisini kwake akimlazimisha kutoa hela alizo nazo kwenye mkoba na alipogoma waziri mwenyewe akafungua zipu akazitoa akaweka mezani na kisha akatoka nje na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakaingia.

Kiluwa amedai hayo leo saa tatu asubuhi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mbele ya Hakimu Mkazi Samweli Obas, akiongozwa na Wakili wake Imani Madega ambapo katika utetezi wake amedai alikuwa kwenye manunuzi ya vitu vya ofisi, walikuwa wanakarabati ofisi, alipanga kuanza kununua kwanza ndiyo aende ofisini kwa waziri lakini Waziri alimpigia simu mara tatu akimuharakisha aende ofisini kwake anamchelewesha ndipo alipokatiza kazi yake akaenda.

Amedai waziri alitaka afike ofisini kwake akiwa na hati zake 57 lakini hakwenda nazo kwa madai kwamba mwenzake anayetunza alisafiri.

“Nilipofika aliniuliza nimebeba nini, nikamjibu nimebeba hela… akasema nipe… nikamwangalia… waziri akainuka ananinyang’anya begi, akanikaba akafungua zipu, akatoa hela akazimwaga mezani, ofisini tulikuwa wawili.

“Sikumpa hela kwa hiari yangu, nataka hela zangu zirudishwe, kusema ukweli waziri anatumika na watu wanaotoka mimi niharibikiwe wao waendelee.

“Waziri anamkwamisha Rais John Magufuli katika azma yake ya kuiingiza Tanzania katika uchumi wa viwanda kwa kujiangalia yeye binafsi,” amedai Kiluwa ambaye anashtakiwa kwa kumpa rushwa ya Sh milioni 90 Waziri Lukuvi.

Saudi Arabia yalaani Seneti ya Marekani kwa 'kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake'

$
0
0
Saudi Arabia imepuuzilia mbali maazimio ya Bunge la Seneti la Marekani ya kutaka kusitishwa kwa msaada wa kijeshi wa Marekani katika vita vinavyoongozwa na Saudi Arabia nchini yemen.

Bunge la Seneti limemlaumu mwanamfalme wa Saudia kwa mauaji ya mwanahabari wa nchi hiyo Jamal Khashoggi nchini Uturuki.

Wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia, imeelezea hatua hiyo kama kuingilia masuala ya ndani ya taifa na kutoa "madai yasiyo ya kweli''.

Maamuzi hiyo ya Marekani Alhamisi ya wiki iliyopita, kwa kiasi kikubwa ni ishara tu na hakuna uwezekano mkubwa wa kufanywa kuwa sheria inayoweza kutekelezwa karibuni.
 
Lakini wametuma ujumbe wakimuonya Rais Donald Trump kuhusiana na hasira ya wanasiasa wa Marekani dhidi ya sera za Saudi Arabia.
 
Kwa njia ya taarifa rasmi iliyochapishwa na chombo kikuu cha habari cha nchi hiyo- Saudi Press Agency, Wizara ya nchi za kigeni inasema kwamba: "Utawala wa kifalme unalaani msimamo huo wa Bunge la Seneti la Marekani. "

Inasema kuwa, msimamo kama huo "umejengwa juu ya madai ya uongo". Saudi Arabia inaongeza pia kuwa, inakataa katu "kuingiliwa kwa aina yoyote kwa maswala yake ya ndani".

"Awali utawala huo ulikanusha kabisa na kusema mauaji ya raia wake, mwaandishi habari Jamal Khashoggi, ni uhalifu mbaya mno ambao hauwezi kuhusishwa na sera za utawala huo wa kifalme au hata taasisi zake" na kurejelea tena kuwa, inakataa "jaribio la kuchukua suala hilo nje ya namna ilivyo sheria na haki ya utawala wa nchi hiyo."

Marekani bado haijajibu taarifa hiyo ya Saudia.

-BBC

Shirika la Ndege Air Tanzania (ATCL) lajibu tuhuma Za Msanii Diamond Kuachwa na Ndege Mwanza

$
0
0
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeeleza masikitiko yake kutokana na tuhuma zilizotolewa na mteja na mteja wao ambaye pia ni msanii maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz mkoani Mwanza kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao wa kijamii akidai kuwepo kwa huduma mbovu kwa baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo.

Akizungumza na wanahabri leo, Msemaji wa ATCL, Josephat Kagirwa amesema tuhuma zilizotolewa na Diamond kuwa limeuza tiketi yake baada ya kubaini kuwa alichelewa kufika uwanjani siyo za kweli, na kwamba mteja huyo ameomba kusafiri tarehe inayofuata (leo).

“Diamond alishindwa kusafiri na ndege ya shirika yetu kutoka Mwanza kwenda Dar jana, kwa sababu alichelewa kufika uwanja wa ndege na tiketi yake haikuuzwa kwa mtu mwingine, bali ataitumia leo jioni. Hivi sasa tumezidi kujiimarisha, tunaruka katika viwanja 11 hapa nchini , na tunaruka viwanja vingine 3 vya nje ya nchi,” amesema Kagirwa.

Jana, Diamond aliwatolea uvivu wafanyakazi wa Air Tanzania Tawi la Mwanza akidai kuwa amekuta  tiketi zake alizokuwa amezifanyia Booking zimeuzwa kwa watu wengine na kuelezwa kuwa hawezi kuondoka na ndege kwa kuwa alikuwa amechelewa, lakini muda mfupi baada ya yeye kuzuwiliwa kuingia eneo la watu wanaosafiri Diamond alisikika akisema “kwanini huyo ameruhusiwa kuingia kwani yeye hajachelewa?”

Wasikilize ATCL  Wakiongea hapo chini

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Disemba 18

PICHA: Mwenyekiti Wa CCM Rais Magufuli Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Jijini Dar Es Salaa

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM kilichokutana jijini Dar es salaam jana Desemba 17, 2018.PICHA NA IKULU

Serikali Yapokea Maombi 594,300 Ya Waombaji Wa Kazi Katika Utumishi Wa Umma

$
0
0
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imepokea jumla ya maombi 594,300 kutoka kwa waombaji wa nafasi za kazi katika Utumishi wa Umma zilizotangazwa katika Wizara, Idara, Wakala, Sekretarieti za Mikoa, Manispaa, Halmashauri na Taasisi za Umma kuanzia Mwezi Novemba 2015 hadi Desemba 2018.

Akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka mitatu ya Taasisi hiyo (2015-2018) jana Desemba 17, 2018 Jijini Dar es Salaam, Katibu wa Sektretarieti ya Ajira, Xavier Daudi alisema tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, Serikali imetangaza nafasi zilizo wazi 6,554 ambapo jumla ya waombaji 140,000 waliitwa katika usaili.

Daudi aliongeza kuwa hadi kufikia Desemba 15 mwaka huu jumla ya nafasi wazi za kazi 6,099 zilikwishajazwa, ambazo nafasi 455 zilizotangazwa kati ya mwezi Novemba na Desemba mwaka huu mchakato wake unaendelea na kukamilika hivi karibuni.

Aidha Xavier alisema mbali mchakato huo unaoendeshwa na Ofisi yake, pia wapo watumishi walioajiriwa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika kada za Afya na Walimu, ambapo katika kipindi cha miaka mitatu jumla ya watumishi wa kada za afya 24,728 wameajiriwa wakati kwa upande wa kada ya ualimu jumla ya walimu 40,086 waliajiriwa Serikalini.

“Idadi hii inaweza kuongezeka katika mwaka huu wa fedha 2018/19 kwa watumishi watakaoajiriwa kwa kada za walimu, afya pamoja na watumishi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama ambao utaratibu wake wa ajira unataratibiwa na mamlaka husika” alisema Xavier.

Akizungumzia kuhusu udhibiti wa waombaji wasio na sifa ikiwemo wenye vyeti feki vya kughushi, Xavier alisema Ofisi yake imeendelea kukagua  nyaraka za waombaji mbalimbali ikiwemno vyeti vyao ili kuhakikisha kuwa wanaoajiriwa Serikalini ni wale wenye sifa na vyeti vinavyostahili kwa mujibu wa sheria.

Akifafanua zaidi, Xavier aliongeza kuwa katika yam waka 2015-2018 jumla ya nyaraka za vyeti vya waombaji kazi 18,817 viliwasilishwa kwenye mamlaka zinazohusika na utoaji wav yeti hivyo kwa ajili ya uhakiki, ambapo jumla ya vyeti halali vilikuwa 18,112 na vyeti 706 vilibainika kuwa ni vyeti vya kughushi.

Kuhusu uimarishaji wa mfumo wa matumizi ya Tehama katika mchakato wa ajira, Xavier alisema Serikali ya Awamu ya Tano imewekeza katika matumiZi ya TEHAMA ili kurahisisha utoaji hudumazake kwa kupitia TEHAMA na kuanzisha mfumo wa kielectroniki kwa watumiaji wa maombi ya kazi ujulikanao kama ‘Rectruitment Portal’ unaopatikana katika anuani ya portal.ajira.go.tz.

“Mfumo huu ulianza kutumika mwaka 2014/15 hadi kufikia tarehe 15 Desemba mwaka huu zaidi ya watu 300,500 wamejiandikisha na maombi ya kazi yaliyowasilishwa kupitia mfumo huu ni zaidi ya 594,200” alisema Xavier.

Kwa mujibu wa Xavier alisema tangu kuanzishwa kwake, Mfumo huo umekuwa na mafanikio makubwa kwani umesaidia kupunguza mchakato wa ajira kutoka siku 90 hadi kufikia siku 52 na hivyo kupunguza malalamiko ya waombaji kazi kuhusu upotevu wa barua zao za maombi ya kazi pamoja na kupunguza ufinyu wa nafasi ya kutunza nyaraka za maombi ya kazi.

Rais Magufuli Awataka Waislamu Wadume Amani, Umoja na Mshikamano

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 17 Desemba, 2018 ameungana na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kuadhimisha miaka 50 ya tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Waheshimiwa Mabalozi wa Iran na Misri, viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Vuai Mwinyi Mohamed, Wajumbe wa Baraza la Ulamaa na Masheikh wa Mikoa na Wilaya zote 26 za Tanzania pamoja na Makatibu wao.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza BAKWATA na Waislamu wote nchini kwa kuendelea kudumisha amani, umoja, mshikamano na kuyashika vizuri mafunzo ya dini, na amebainisha kuwa mambo hayo yana faida kubwa kwa jamii nzima ya Waislamu na Madhehebu mengine.

Mhe. Rais Magufuli amesema katika kipindi cha miaka 50 taasisi mbalimbali zilizo chini ya BAKWATA na Uislamu kwa ujumla zimeendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma za elimu, afya, maji na nyingine na kwamba Serikali inatambua mchango huo mkubwa.

Ameahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano wake mzuri na BAKWATA na Madhehebu mengine ya Dini, na ametoa wito kwa Waislamu na Waumini wa Madhahebu mengine ya Dini kuendeleza utamaduni mzuri wa kushirikiana, kuvumiliana, kusameheana na kutunza amani, mambo ambayo yanasaidia kuepusha migogoro.

“Naomba niwahakikishie ndugu zangu, Serikali inawapenda Waislamu na inayapenda Madhehebu yote ya Dini, tutaendelea kuhakikisha tunashirikiana kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo la Taifa letu, kwa pamoja tunaweza” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe Rais Magufuli ameelezea juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuharakisha maendeleo ikiwemo ununuzi wa ndege, kuanza mradi wa uzalishaji wa umeme katika mto Rufiji, kujenga viwanda, kujenga reli ya kati na kufufua reli ya kaskazini, kujenga meli mpya na kukarabati za zamani, kujenga barabara, kuongeza kasi ya usambazaji umeme vijijini, kujenga hospitali na vituo vya afya na kuongeza ukusanyaji wa kodi.

Amempongeza Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally kwa uongozi wake mzuri wa BAKWATA, ushirikiano mzuri na taasisi nyingine ikiwemo Serikali na kutojikweza kwake, na pia ametoa mchango wa shilingi Milioni 30 kwa BAKWATA.

Mapema Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuungana nao katika maadhimisho hayo, amemshukuru kwa kusaidia kujengwa kwa Msikiti mkubwa wa BAKWATA Jijini Dar es Salaam ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua Waumini 9,000 kwa mara moja, na pia kwa juhudi alizoanza kufuatilia na kurejesha mali za Waislamu zilizoporwa.

“Mhe. Rais kwa niaba ya BAKWATA tunakushukuru sana na Waislamu wameridhika sana kwa kuhakikisha Msikiti huu unajengwa na ujenzi wake unaendelea vizuri” amesema Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally.

Katika Maadhimisho hayo Mhe. Rais Magufuli pia amekabidhi tuzo kwa Waislamu waliotoa mchango mkubwa katika BAKWATA.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
17 Desemba, 2018

Lowassa, Maalim Seif, Zitto Kabwe Wajichimbia Zanzibar

$
0
0
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa vya upinzani  nchini wamejichimbia visiwani Zanzibar kwa ajili ya kupatiana mafunzo mbalimbali juu ya mwenendo wa siasa na demokrasia.
 
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi, pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa na Kiongozi wa ACT - Wazalendo Zitto Kabwe.

Mbali na hao, viongozi wengine walionekana na Rais wa Chama Cha Mawakili Tanzania, (TLS) Fatma Karume pamoja viongozi wengine mashuhuri nchini ambapo imeelezwa walijadili juu ya mwenendo wa hali ya kisiasa nchini.

Kaimu Msemaji wa chama cha CUF, Mbarara Mahagande amesema kikao hicho kimeandaliwa na taasisi ya marekani IRI kupitia kwa Katibu wa CUF, Maalim Seif.

"Ni kweli kuna semina inafanyika ya viongozi wa vyama inafanyika Zanzibar ambayo inafanyika kwa siku tatu, na aliyewaalika ni Katibu Mkuu wetu Maalim Seif na imeandaliwa na taasisi ya IRSA, watu wa democratic ya America," amesema Maharagande.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Maalim Seif aliandika; "Ni heshima kubwa kwangu na kwa CUF kuandaa na kuwa mwenyeji wa kikao cha kutathmini demokrasia yetu na kujitathmini sisi wenyewe kama vyama vya upinzani na mwelekeo wetu."

PICHA: Ndege Mpya Airbus A220-300 Ikiwa Tayari Kuletwa Tanzania Kutoka Canada

$
0
0
Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi ikiwa imebatizwa jina la Ngorongoro
 Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi
 Mmoja wa wajumbe wa Tanzania akipata maelezo ya Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi
 Ujumbe wa Tanzania ukiwa na Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi
Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi

Wanaofanya biashara mitandaoni kuanza kutozwa kodi

$
0
0
Wafanyabiashara wanaofanya biashara kupitia mitandao mbalimbali wametakiwa kufika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili wajiandikishe waanze kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kama wafanyabiashara wengine wote.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere jana asubuhi alipokuwa akizungumza kupitia Clouds FM kuhusu mbinu mbalimbali wanazokusudia kuzitumia ili kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya walipa kodi na kuongeza mapato.

Kamishna Kichere alilazimika kutoa maelezo hayo baada ya kuhojiwa na mtangazaji kuhusu uwepo wa watanzania wachache wanaolipa kodi (zaidi ya milioni 2) wakati jumla ya Watanzania wapo takribani milioni 55.

Akizungumzia mkakati wa TRA kuongeza idadi ya walipakodi, kamishna huyo alisema wameanza kuwafikia watu wanaofanya biashara mitandaoni ambao wamekidhi vigezo vya kutakiwa kulipa kodi, wawe wanalipa kodi kama wafanyabiashara wengine.

Alieleza kuwa, wafanyabishara ambao thamani ya biashara zao ni zaidi ya shilingi milioni nne wanatakiwa kufika TRA wajiandikishe ili wapate Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) waanze kulipa kodi.

“Wapo watu wanafanya biashara za bidhaa mbalimbali kwa njia ya mtandao na wanapata wateja ambao huwasambazia bidhaa husika, sasa tunawataka walipe kodi kama wengine,” Kayombo alisema.

“Hizo ni biashara za kawaida kama nyingine zinafanyika kwa njia ya mtandaoni tu.”

Alisema wafanyabiashara hao ni kama wa 'Uber' (magari yanayobeba abiria walioyaita kwa njia ya mtandao) ambao awali walikuwa hawalipi kodi lakini kwa sasa wanalipa na ni biashara ambayo inafanyika mtandaoni.

Alipoulizwa juu ya namna ya kuwadhibiti na kuwapata walipakodi hao, Kayombo alisema TRA itawafuatilia kwenye mitandao wanapotangazia biashara zao na kuwataka walipe kodi kwa mujibu wa sheria kabla ya kufuatwa.

Ujenzi Wa Mahakama Kuu Kanda Ya Musoma Waendelea Kwa Kasi

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Musoma
WAKAZI wa mkoa wa Mara wanatarajia kuondokana na adha ya kufuata huduma za Mahakama Kuu mkoani Mwanza, umbali wa zaidi ya kilometa 200 kutoka mjini Musoma, baada ya ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma kukaribia kukamilika mapema mwakani.

Wakizungumza na timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, baadhi ya wakazi wa mji wa Musoma Mary Mohamed na Happy Mjito, wamesema kuwa hivi sasa wanatumia fedha nyingi kufuatilia haki zao Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza hali inayowafanya wengi wao kukata tamaa kufuatilia kesi zao hivyo kupoteze haki zao

"Ukikata rufaa ya kesi unaambiwa uende Mwanza wakati hata Mahakama Kuu yenyewe ya Kanda ya Mwanza hatuijui mahali ilipo, sasa tunafurahi kwamba tutakuwa tumiendesha kesi zetu hapa hapa Musoma" alisema Bi. Happy Mjito

Akielezea hatua ya ujenzi wa Mahakama hiyo Kuu Kanda ya Musoma ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 6 nukta 2, Wakala wa Mkandarasi anaye jenga Mahakama hiyo, Kampuni ya DF Mistry, Mhandisi Uday Dadrawalla, ameiambia timu hiyo ya Wizara ya Fedha na Mipango inayofuatilia utekelezaji wa miradi ya Maendeleo mkoani Mara kwamba ujenzi huo umefikia asilimia 80.

"Mkataba wetu unaonesha kuwa tunatakiwa kukabidhi jengo ifikapo tarehe 21 mwezi Mei, 2019 lakini kwa kasi tunayokwenda nayo tutakabidhi jengo hili mapema zaidi Mwezi April, 2019" alisema Mhandisi Dadrawalla.

Mradi huu unaotekelezwa na Mahakama Kuu Nchini ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele iliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/18 hivyo utekelezaji wake ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2021, hususani katika eneo la Utawala Bora.

Mwisho

Jipatie Dawa ya Asili ya Kupunguza Maziwa, Kupunguza Tumbo,Kuongeza Unene, Kuongeza Maumbile ya Kiume na Kuondoa Chunusi

$
0
0
NATURAL BEAUTY PROD.
🍋🥑🍒OFFER ya X MAS na MWAKA MPYA🍉🍇

 Ofa hii itaisha tareh. 22/12/2018 wahi sasa jipatie bidhaa original kwa punguzo la bei.

 %%Bidhaa hizi zimetengenezwa kwa mimea na matunda hazina chemical wala madhara yoyote kwa mtumiaji.             Ukinunua bidhaa kuanzia mbili utapatiwa offer ya bidhaaa nyingine yoyote uipendayo wewe bureeee.

1. SHARK POWER--Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza maumbile ya kiume urefu na upana mpaka nchi 7.5 ilikua inapatikana kwa @170,000/= sasa ni @160,000/= tu

2. VIGA 84000---Hii dawa ya kuspray yenye uwezo mkubwa wa kuchelewesha wakati wa tendo la ndoa ilikua ni  @160,000/=. Sasa ni 150,000/= tu

3. HANDSOME UP ORIGINAL-- Hichi ni kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo wewe pamoja na kuimalisha misuli kifaa hichi kilikua kinapatikana kwa @230,000/=. Sasa ni 210,000/= tu

4. MAXMAN CAPSULE--- Hii ni dawa ya vidonge ya kuongeza maumbile ya kiume urefu na upana pamoja na kuongeza nguvu za kiume kwa wiki mbili ilikua inapatikana kwa @200,000/=. Sasa ni 180,000/= tu

5. VIG RX---- Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza uume urefu na upana mpaka nchi 10 ilikua inapatikana kwa @190,000/=. Bei ya sasa ni 170,000/=

6. BODY BOOSTER---Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza mwili pamoja na hamu ya kula vizuri ilikua inapatikana kwa @150,000/=. Sasa ni 140,000/=

7. BOTCHO MULT PLUS-- Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza (hips mapaja na makalio) kwa size uipendayo ilikua inapatikana kwa @200,000/=. Sasa ni 180,000/=

8. WHITE COLLECTION---- Ni vidonge vya kuwa mweupe mwili mzima pamoja na kuwa soft ilikua inapatikana kwa @150,000/= Sasa ni @140,000/= tu

9. BOTCHO HOLOGRAM CREAM--- Hii ni dawa ya kuongeza hips na makalio ilikua inapatikana kwa@180,000/= Sasa ni@160,000/=       

N.K

Wasiliana nasi kwa simu

NO:. +255 759029968  AU +255 659618585

Popote ulipo utapata huduma zetu.

Pia hakikisha unapatiwa risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY PROD ununuapo bidhaa kampuni hii.

WELCOME ALL

Makanga 3 Power, Dawa Bora Za Nguvu Za Kiume

$
0
0

Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.

Tupo dar es salam Buguruni

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348.

Walimu Watiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumchapa Mwanafunzi Hadi Kuzirai

$
0
0
Walimu watatu wa Shule ya Sekondari Kasamwa, Wilaya ya Geita, mkoani Geita, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumshambulia mwanafunzi wa kike kidato cha tano hadi kuzirai kwa madai ya kutoga masikio.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mpojoli Mwaburambo, alithibitisha jana kuwapo kwa tukio hilo. Alisema mwanafunzi huyo Anneth Kulwa (19), baada ya kushambuliwa alikimbizwa katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa ambako alitibiwa na kupatiwa fomu Na. 3 ya Jeshi la Polisi (PF3).

Kamanda Mwaburambo alisema tukio hilo lilitokea Desemba 12, majira ya saa 5 asubuhi na chanzo kinadaiwa kuwa walimu hao kumtuhumu mwanafunzi huyo na wenzake saba kutoga masikio na kuchukua jukumu la kuwaadhibu.

Alisema baada ya tukio hilo kubainika, polisi ilifuatilia kwa kuchukua maelezo ya wanafunzi na kufunguliwa jalada la uchunguzi. Aidha, Kamanda alisema polisi walifika eneo la tukio na kuwakamata watuhumiwa na kuahidi kuwa uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Akizungumzia tukio hilo akiwa wodini, mwanafunzi huyo alisema anakumbuka kabla ya kupoteza fahamu yeye na wanafunzi wenzake saba walikuwa wakishambuliwa na walimu kwa kipigo cha viboko, makofi na mateke.

Alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Kasamwa, Happy Magati, alikiri kutokea tukio hilo, lakini akadai asingeweza kulizungumzia kwa kina kwa sababu tayari lilikuwa mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi.

Kutana Na Dr Chikago Bingwa Na Mwokozi Kwa Waliosumbuka Na Magonjwa Bila Mafanikio

$
0
0
Ninauwezo wa kumrudisha mume, mke ,mchumba, hawara, mtu unaempenda ndani ya masaa mawili tu (2) na kumfunga asiwe na mtu mwingine zaidi yako na kumfanya akutimizie kilakitu unachokihitaji kutoka kwake hata km yupo mbali na atatulia kabisa

GALIMBO 3 MIX;  nidawa ya mitishamba iliyitengenezwa kwa kwa utabibu wa hali ya juu kwakuchanganya miti na matundatiba , Huogeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15 -85 ) , inakomaza zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakat wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaid ya Mara tatu bila ham kuisha wara kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-40.

YOLANI :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inch (6-8) na unene wa sm (3-4)

Matatizo haya husababishwa na mambo mbalimbali km upigaji wa punyeto, kisukali,  vidonda vya tumbo, tumbo kuunguluma na kujaa gesi, ngili, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani, maumivu ya mgongo ama kiuno, namengineyo mengi  (nk )

SUPER MBUKE :- nidawa inayotatua tatizo la kisukali na kupona kabisa Kwa mda mfupi sana na utakuwa na uwezo wakula chakula chochote chenye sukali baada ya kupona,

vilevile ninadawa ya uzazi kwa akina Mama na akina Baba, kurudisha mali iliyopotea kwamda mfupi sana, vidonda vya tumbo, kaswende,presha,chango la uzazi, gono,nyama uzembe, kusafisha nyota, kuzuia majini wachafu, kinga ya mwili, kuuza vitu bila kununuliwa, dawa za biashara, pesa nyingi (utajili)  mambo ya kes nk

Kwa huduma n msaada wasiliana na Dr CHIKAGO atakusaidia hatakama ulikata tamaa utarudisha furaha yako

Napatikana Dar es salaam  sm no 0743543944   /0620510598

Nb :km huna nafasi ya kufika ofisin huduma hii itakufikia popote ulipo kwawatu wa mkoani tunatuma kwanjia ya mabasi.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala- Dar

Sumaye ataja maadui wanaoiua CHADEMA

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amewataja maadaui ambao watapelekea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukosa ushindi katika chaguzi mbili zijazo.
 
Akifungua mkutano wa ndani wa Baraza la uongozi la CHADEMA Kanda ya Pwani, Sumaye amesema kuwa, maadui wa chama hicho ni baadhi ya wanachama wanaoweka maslahi binafsi mbele kuliko ya Chama na ya wananchi waofifisha jitihada za kukijenga.

"Umefika wakati kwa wanachama wetu kufikiria masilahi mapana ya wananchi na chama la sivyo itakuwa vigumu kushika dola, na kama wanachama watajikita kutetea masilahi binafsi kama ilivyotokea kwa baadhi, ni dhahiri lengo la kuongoza nchi halitafikiwa", amesema Sumaye.

Sunaye ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho baadhi ya wabunge, madiwani, wenyeviti wa halmashauri na wanachama wakijiuzulu nafasi zao na kutimkia CCM ambako baadhi yao walipitishwa na kurudi kwenye nyadhifa hizo.

Uchaguzi wa serikali za mitaa nchini unatarajiwa kufanyika mwakani kabla ya uchaguzi mkuu 2020.

Waziri Mkuu Majaliwa ampongeza Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakary Zuberi

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakary Zuberi migogoro ya misikiti imepungua.

Licha ya kupungua huko Waziri Majaliwa amemtaka Sheikh huyo aongeze bidii, ubunifu na kasi kubwa ili afanikishekumaliza migogoro yote inayokabili misikiti nchini.

Akizungumzia umuhimu wa dini Waziri Majaliwa amesema uwepo wa dini mbalimbali nchini ni muhimu  kwa kuwa umesaidia kuunga mkono jitihada mbalimbali za serikali katika kuhakikisha nchi inasonga mbele.

Waziri Mkuu amesema hayo jana Desemba 17, jijii Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuaanzishwa kwa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata).

Alisema kila dini kwa imani zao wanasaidia kutekeleza mambo ambayo kikawaida yangetakiwa kufanywa na serikali.

Akizungumzia sekta ya Afya alisema vituo vya kutoa huduma za afya nchini vimejengwa na taasisi za dini.

“Katika elimu taasisi za dini zikiwamo za waislamu zimejenga vyuo na shule ambazo zinafundisha kuanzia elimu yachekechea. Zimejenga watu wengi wamekuwa na maadili mema ya kujua umuhimu wa uzalendo na mshikamano tangu walipokuwa wadogo,” Alisema na kuongeza.

“Hata utulivu uliopo nchini ni kutokana na dini kuhamasisha amani nchini  kupitia kamati za amani zilizoundwa katika maeneo yote nchini, kupitia makongamano na mikutano yahadhara ya kidini ndio maana hadi leo nchi yetu ina amani kubwa,“ alieleza Majaliwa.

Hukumu Ya Tido Muhando Kusomwa January 25

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Januari 25, 2019 kutoa hukumu ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili  aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando.

Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa leo Jumanne Desemba 18, 2018 lakini Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi amesema hajakamilisha kuandaa hukumu kwa sababu kuna vitu bado anavifanyia utafiti kabla ya kutoa hukumu hiyo.

"Hukumu yako Tido bado haijakamilika, kuna vitu bado navifanyia utafiti. Januari 25 nitatoa hukumu, utaendelea kuwa nje kwa dhamana hadi siku hiyo,” amesema Hakimu Shaidi.

Tido anakabiliwa na mashtaka matano, mashtaka manne ni ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.

Mtoto Mchanga wa Siku 3 Atupwa Jijini Mwanza

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kutumia kikosi chake kabambe na jasiri, tumefanikiwa kumuokoa mtoto mchanga mwenye jinsia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja hadi tatu aliyekua ametupwa na kuachwa bila msaada na mwanamke/mtu asiyefahamika  huko mtaa wa Mwambani Wilayani Ilemela, kitendo ambacho ni kosa la Jinai.

Tukio hilo la kikatili limetokea tarehe 17.12.2018 majira ya saa 20:30hrs usiku, hii ni baada ya mtoto huyo kufungwa nguo mwilini mwake kisha kutupwa bila msaada wa aina yoyote. 

Ndipo kikosi chetu cha askari kilichokuwa doria chenye umakini wa hali ya juu kilipata taarifa na kufanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kumkuta mtoto huyo akiwa hai akilia sana akiwa ametupwa uwanjani hapo na mwanamke/mtu asiyefahamika.

Baada ya Mtoto huyo kuokolewa amepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu na uhifadhi, hali yake inaendelea vizuri. 

Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza, tunaendelea na upelelezi pamoja na msako mkali wa kumtafuta mwanamke/mtu aliyehusika katika kutenda ukatili huu ili aweze kukamatwa na kufikishwa  katika vyombo vya sheria, ili baadae iwe fundisho kwa wengine.

Sambamba na hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunatoa onyo kwa baadhi ya wanawake wenye tabia kama hizi za kinyama kuwa waache kwani ni kosa la jinai lakini pia ni kinyume na haki za binadamu. Hivyo endapo mtu atabainika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Vilevile tunawaomba wananchi pindi wanapomwona jirani yake ni mjamzito alafu baada ya muda ghafla ujauzito wake unapotea na mtoto haonekani watoe taarifa polisi ili tuweze kujiridhisha juu ya usalama wa mtoto.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images