Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mwenyekiti Wa CCM Rais Magufuli Aendesha Kikao Cha Halmashauri Kuu Ya CCM Dar Es Salaam Leo

0
0
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam leo Desemba 18, 2018
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally akiongea kabla ya ufunguzi wa  kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam leo Desemba 18, 2018.

 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiendesha  kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam leo Desemba 18, 2018

PICHA NA IKULU

Waziri wa Viwanda Atoa Siku 14 Brela Warekebishe Mifumo yao

0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda, ametoa siku 14 kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kurekebisha mifumo ya kielektroniki ya utoaji huduma za wakala huo.

Akizungumza baada ya kutembelea wakala huo leo Desemba 18, Kakunda amesema mifumo ya kielektroniki imekuwa ikilalamikiwa na watu wengi hasa katika siku za karibuni.

“Ndani ya wiki mbili nimekuja tena hapa kwa sababu kuna sababu maalumu, udhaifu mkubwa uko kwenye mifumo kuliko uhalisia.

“Kila nikipokea simu 10 za wafanyabiashara nane zinalalamikia Brela hili ni tatizo,” amesema Kakunda.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Emmanuel Kakwezi, amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama za upungufu wa watumishi 51 na mfumo kutokuwa imara.

“Kuna changamoto ya mtandao wa ORS katikati yakazi unaweza kuzimika. Mteja anatuma maombi lakini haionekani na sisi tunaweza kumjibu lakini haoni,” amesema Kakwezi.

Manchester United Yamfukuza Kazi Mourinho

0
0
Klabu ya Manchester United imetangaza kuachana na kocha wake mkuu, Jose Mourinho,  kuanzia leo Desemba 18, 2018 ikiwa ni siku mbili tangu alipopokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa mahasimu wao, Liverpool, Jumapili iliyopita.

Taarifa ya klabu hiyo iliyochapishwa kwenye tovuti yake imesomeka kuwa, “Manchester United inatangaza kuwa imevunja mkataba na kocha Jose Mourinho”.

“Klabu ingependa kumshukuru Jose kwa kazi yake nzuri katika kipindi chote alichokuwa na Manchester United na tunamtakia maisha mema huko aendako.”

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 katika kikosi cha Manchester United amefanikiwa kutwaa taji la Kombe la Ligi na Ligi ya Europa katika miaka miwili na nusu aliyokaa ndani ya timu hiyo.

Lakini kwa sasa Man United iko katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa nyuma kwa pointi 19 dhidi ya vinara Liverpool ambao waliwafunga mashetani hao wekundu kwa mabao 3-1.

"Kocha atakayechukua jukumu hilo kwa muda anategemewa kutangazwa hivi karibuni, huku tukiendelea na utaratibu wa kusaka kocha mpya," imesema taarifa ya Man United.

Habari Njema Kwa Wenye Matatizo Ya Nguvu za Kiume, vitambi, nyama uzembe

0
0
HABARI NJEMA KWA MLIOATHIRIKA NA MAGONJWA YA MWILI NA AKILI.
Sasa dokta MBALU ana uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa yaliyoshindikana,Kama umehangaika kwa muda mrefu bila mafanikio DK.MBALU Ni kiboko kabisaa.

TIBA ATOAZO NI:- (a)Vidonga vya tumbo,kilungulia,Tumbo kujaa gesi.
 (b)Kifua kikuu(TB),Pumu(ATHMA) na Rovu
(c)Miguu kuwaka moto,nyama za magoti kuuma,kiuno na mgongo.
(d)Uzazi na chango.
 (e)Nguvu za kiume,kurefusha na kunenepesha uume,busha,mshipa wa ngiri na tezi dume.
(f)Elimu mwanafunzi kuwa na uwezo mkubwa darasani na kufanya vizuri katika mitihani yake, kupandishwa cheo kazini, kulipwa madeni au mafao yako.
(g) kutoa ushauri nasaha kwa wenye matatizo ya kisaikolojia.

      AINA ZA DAWA.
NINJIWE:-,Hutibu vidonda vya tumbo,tumbo kujaa gesi,na kilungulia,vidonge 16 kwa muda wa siku nne na ya unga.
MPALAMA:-,Hutibu Kifua kikuu (TB), Pumu (ATHMA),na wenye tatizo la uvimbe katika koromeo yaani (ROVU),Huisha na kutorudi Tena.,dozi siku 6.

NKOLA:-,Hutibu miguu kuwaka moto,nyama za goti kuuma,kiuno na mgongo dozi siku 10.
MWATYA:-,Hutibu Uzazi au chango,dozi siku 30,na tatizo kupona kabisa.

LYONGO POWER:-,Hii ni dawa ya heshima kwa akina baba yenye uwezo wa kurefusha na kunenepesha uume kwa wale wenye maumbile madogo yaani (KIBAMIA).

NENGONENGO(4)POWER:-,Hutibu Nguvu za kiume na kuleta hamu ya tendo hivyo kuchelewa kufika kileleni na kuweza kurudia tendo zaidi ya mara (4),ina Nguvu mno Kama Ni muhanga wa tatizo hili   tumia NENGONENGO (4)POWER Ipo aina ya vidonge na unga dozi Ni siku 5 unapona kabisaa wahi Sasa.

NTUNDWA:-,Hutibu busha,mshipa wa ngiri na tezi dume,Busha dozi Ni siku (30),bila kufanyiwa operation,Mshipa wa ngiri dozi siku (4) na tezi dume dozi siku (10).

GWATA:-,kuuwa kesi na shauri kupangiwa tarehe za karibu zaidi na baadae kesi kufutiliwa mbali kabisaa.
NUGWANO:-, Humfanya mtu kuheshimika na kupandishwa cheo kazini pia kulipwa madeni au mafao kwa wakati muafaka.

NKOMA:-, Hurudisha mke,mme,hawara, mchumba ndani ya siku mbili atatimiza mahitaji yote hata Kama yupo mbali na kumfunga asiwe na mtu mwingine..

  Huduma zinatolewa ndani ya masaa 12,Saa moja asubuhi Hadi kumi na mbili jioni,DAR ES SALAAM NA KAHAMA wa mikoani unapata huduma kwa njia ya kusafirisha..na huduma yetu inakufikia ukiwa ofisini au nyumbani kwako..,CONTACTS 0767,  171  ,773
0716, 608  ,959


 OUR SERVICES ARE EASY.

Okoa Ndoa Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Hii Iitwayo Simpo Power

0
0
Okoa Ndoa Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Hii Iitwayo Simpo Power Kwaajili Ya Nguvu Za Kiuume Na Promix Kwaajili Ya Kuongeza Maumbile;
Kwa mwanaume aliyekamilika na mwenye Afya njema ili kumridhisha mke au mpenzi anatakiwa awe na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya Mara mbili hapo utamridhisha mpenzi wako ila ukiwa unapiga moja au mbili hapo ujue umejilidhisha wewe 

Tiba Ya Tatizo Lako Ni Dawa Hiitwayo Simpo Power No, 1; dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge vya miti shamba na unga ambayo hutibu matatizo matatu kwa pamoja :-1 itakufanya urudie tendo zaidi ya mara tatu 
2 itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika 15-20 kwa tendo la Kwanza 
3 huimarisha uume uliolegea na kusinyaa 

Je Una Mke Au Mpenzi Aliyebalikiwa Kuwa Na Kario Kubwa Au Mwili Mnene Na Wewe Mume Wake Una   Maumbile Mafupu?; tumia sasa dawa ya PROMIX dawa itakufanya umfikishe shemu nyeti maana inaboresha maumbile saizi upendayo.

Dawa zangu haziina madhara yoyote kwa mtumiaji 

MARKSU; ni dawa ya kisukari dozi siku 21 
MWARU; ni dawa ya uzazi,hufungua milija ya uzazi ata kwa Wale waliofungiwa uzazi  
MTUNDUU; ni dawa ya busha bila kupasua 
MAZANZA; ni dawa ya kisukar zipo dawa za miguu Kuuma,tumbo,kupunguza Matiti,kutoa minyama uzembe ngiri,vidondo vya tumbo  

FIKA OFISINI KWANGU BUGURUNI MALAPA KARIBU NA KOTA ZA POLISI AU PIGA  SIMU ULETEWE MAHALI ULIPO SIMU NO 0783185060,  0752348593  -DR AGU

Mkuu wa Majeshi: Maghala Yote Mtwara Yamejaa Korosho

0
0
Jeshi la Wananchi  Tanzania limesema liko tayari kutumia meli yake yenye uwezo wa kubeba tani 500 kusafirisha korosho hadi jijini Dar es Salaam baada ya maghala yaliyopo mkoani Mtwara kujaa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Wananchi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo katika kikao chake na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mtwara.

Amesema katika ziara yake aliyoifanya kwenye maghala makuu ameshuhudia korosho kujaa kwenye maghala hayo na kusema iwapo zitaendelea kukusanywa kwa wananchi jeshi litalazimika kutumia meli yake kupunguza sehemu ya zao hilo ili  kuhifadhiwa Dar es Salaam.

Hata hivyo,  amesema kuhusu upatikanaji wa maghala jijini Dar es Salaam jeshi litalazimika kufanya mazungumzo na wizara ya kilimo ili kuona namna ya kuandaa maghala hayo kwa ajili ya kutunzia korosho.

Kuhusu ubanguaji wake, Jenerali Mabeyo amesema vikundi vya wabanguaji wadogo watatumika kuzibangua na kwamba kitu kikubwa kinachohitajika ni kuongezea nguvu-kazi ya watu ili kazi hiyo iweze kufanyika haraka na kwa tija.

CCM Yawasamehe Na Kuwarejeshea Uanachama Ramadhani Madabida Na Wenzake Watatu

0
0
Kwa kauli moja Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea maombi na kukubali kusamehewa adhabu ya kufukuzwa uanachama kutoka kwa waliokuwa wana CCM wanne ambao walitenda makosa hayo wakiwa Wenyeviti wa CCM ngazi ya Mikoa na Wilaya.

Waliosamehewa na kurejeshewa uanachama ni;
1.   Ndg. Ramadhani Rashid Madabida (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam).

2.   Ndg. Erasto Izengo Kwirasa (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga).

3.   Ndg. Christopher Mwita Sanya (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara).

4. Ndg. Salum Kondo Madenge (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni).

Breaking News: Diamond Platnumz, Rayvanyy Wafungiwa Kwa Muda Usiojulikana.....Tamasha la Wasafi Festival Lafutwa

0
0
Baraza la Sanaa nchini (Basata) limewafungia  wanamuziki  Diamond Platnumz na Rayvanny  kutojihusisha shughuli za sanaa kwa muda usiojulikana.

Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa leo Desemba 18, imesema limefikia uamuzi huo baada ya wasanii hao kuonyesha dharau kwa mamlaka zinazosimamia shughuli za sanaa nchini, kwa kufanya vitendo vinavyokiuka maadili.

Mbali na kuwafungia wanamuziki hao, Baraza limetangaza kukifuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival linaloendelea nchini.

Wimbo wa Mwanza ambao uliowaingiza matatani ulifungiwa Novemba 12.


Juzi, Basata iliahidi kutoa taarifa rasmi baada ya wasanii hao kuonekana jukwaani katika Tamasha la Wasafi jijini Mwanza wakitumbuiza wimbo huo.
 

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha makamu mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Prof. Egid Beatus Mubofu

0
0
Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi  kwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Benjamin Mkapa kufuatia kifo cha Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Egid Mubofu.

Profesa Mubofu amefariki dunia leo Jumanne Desemba 18, 2018 Pretoria, Afrika Kusini alikopelekwa kwa ajili ya matibabu zaidi akitokea taasisi ya tiba ya mifupa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (Moi) alikokuwa akipatiwa matibabu ya kiharusi.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inasema Rais Magufuli amemuomba Mkapa kufikisha salamu zake za pole kwa familia ya marehemu, wahadhiri, wanafunzi na wafanyakazi wa Udom na kwenye  jumuiya na taasisi zote ambazo marehemu alifanya kazi.

“Nimesikitishwa  sana na kifo cha Profesa Mubofu, nitamkumbuka kwa uchapakazi wake, ubinifu, uadilifu na uaminifu mkubwa aliouonesha katika utumishi wake kwa Taifa ikiwemo kazi nzuri aliyoifanya katika Shirika la Viwango la Taifa (TBS) akiwa mkurugenzi mkuu kabla ya kuteuliwa kuwa makamu mkuu wa Udom,” amesema Rais Magufuli.

BREAKING: Vyama vya Upinzani Vyatoa Tamko Ziko Kuhusu Domokrasia Nchini

0
0
Vyama sita vya upinzani vilivyokaa kikao chao Zanzibar vimesema mwaka wa 2019 ni mwaka ambao  watapambana kwa hali zote katika kudai haki zao wanazonyimwa kinyume na sheria za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Shariff Hamad wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao hicho cha siku tatu kilichofanyika Zanzibar kwa niaba ya vyama hivyo.

"Kama vyama vya siasa  vyenye uhalali na uratibu wa  uliowekwa rasmin kikatiba, tunatangaza rasimi namna ya kufanya mikutano yetu ya hadhara katika kila kona ya nchi yetu’’ alieleza Maalim Seif.

Alieleza hawatoruhusu katazo haramu ambalo alisema linakwenda kinyume na sheria za nchi na kudai haliwezi kuzuia kazi zao.

 Aliwataka wanachi pamoja wanachama wote wa vyama sita, wakati ni sasa wa kuondoa hofu na kuunga mkono vyama vyao ili kulinda Demokrasia.

"Hatupaswi kuwa waoga hata kidogo na hatupaswi kujisalimisha katika kudai haki zetu kama mtu mmoja au kikundi, lazima tupeleke ujumbe huu wa uhuru na Demokrasia kwa viongozi wenzetu wote’’ alieleza.

 Sambamba na hilo waliwatangaza viongozi wa vyama vya siasa Freeman Mbowe na  Esther Matiko ambao hadi sasa wako mahubusu kuwa ni Wafungwa wa kisiasa na kueleza kuwa tangazo hilo halitofutwa mpaka pale watakapoachiwa.

 "Tutapambana kwa nguvu zote  kuhakikisha wafungwa wote wa Kisiasa, nchi nzima  wanapewa nafasi ya kupata haki katika mfumo ulio huru mbele ya mahakama na macho ya watu’’ alieleza Maalim Seif.

 Mwenyekiti wa Chama cha UMMA Hashim Rungwe alisema hawawezi kumruhusu mkandamizaji wa siasa aendelea kuwakandamiza wanachi na demokrasi na kueleza sasa basi.

"Lazima tuwaeleze wananchi wakatae utawala huu wa kibabe kwani ndio uliopomorosha maisha yao’’ alifafanua Rungwe.

Alieleza kuwa Demokrasia ina gharama na wakati ukifika watawaeleza nini watafanya katika kupiga viota uvunjwaji wa Demokrasia.

 Akizungumza katika mkutano huo ambao ulitoka na tamko la Azimio la Zanzibar mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alisema hali iliyopo sasa ni kutokana na ubinafsi ya utawala uliopo.

Alieleza kuwa ubinafsi huu ndio uliopelekea maisha ya watu kubadilika na kuwaona wengine ndio walio na haki hapa nchini.

Kwa upande Wa Zanzibar vyama hivyo vilieleza kuwa hawaitambui Serikali ya Mapinduzi inayo Ongozwa Dr. Ali Muhammed Shein na kuita ni serikali haramu kutokana kile walichodai kupora ushindi wa CUF mwaka 2015.

Akizungumzia baadhi ya wabunge na Madiwani waliohama vyama na kujiunga CCM  Waziri Mkuu wa zamani Fredric Sumaye alieleza kuwa viongozi hao hawakuhama bure na wameenda kufanya biashara ya kisiasa.

 "Unapoona wabunge na viongozi wa upinzani wanahamia chama tawala ujue chama tawala kimefika mwisho kutawala katika nchi, na hapa ni dhahiri CCM wamefikia mwisho kutawala Tanzania’’ alieleza Sumaye

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Disemba 19

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kufungwa Kwa Muda Barabara Ya Morogoro Sehemu Ya Kimara Stop Over

0
0
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuutarifa umma kuwa leo  tarehe  19/12/2018, itafunga kwa muda barabara ya Morogoro sehemu ya Kimara Stop Over hadi Temboni Wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana.

Kufungwa kwa muda barabara hii kunatokana na kuwepo kwa sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 19.2   kutoka Kimara hadi Kibaha kuwa njia nane (8) itakayofanyika eneo la Kimara Stop Over.

Wizara inashauri watumiaji wa barabara hiyo kutumia barabara mbadala kwa muda wote ambao barabara hiyo itakuwa imefungwa kwa muda.

Aidha, Wizara inawaomba radhi watumiaji wote wa barabara hiyo kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Jipatie Dawa ya Asili ya Kupunguza Maziwa, Kupunguza Tumbo,Kuongeza Unene, Kuongeza Maumbile ya Kiume na Kuondoa Chunusi

0
0
NATURAL BEAUTY PROD.
🍋🥑🍒OFFER ya X MAS na MWAKA MPYA🍉🍇

 Ofa hii itaisha tareh. 22/12/2018 wahi sasa jipatie bidhaa original kwa punguzo la bei.

 %%Bidhaa hizi zimetengenezwa kwa mimea na matunda hazina chemical wala madhara yoyote kwa mtumiaji.             Ukinunua bidhaa kuanzia mbili utapatiwa offer ya bidhaaa nyingine yoyote uipendayo wewe bureeee.

1. SHARK POWER--Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza maumbile ya kiume urefu na upana mpaka nchi 7.5 ilikua inapatikana kwa @170,000/= sasa ni @160,000/= tu

2. VIGA 84000---Hii dawa ya kuspray yenye uwezo mkubwa wa kuchelewesha wakati wa tendo la ndoa ilikua ni  @160,000/=. Sasa ni 150,000/= tu

3. HANDSOME UP ORIGINAL-- Hichi ni kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo wewe pamoja na kuimalisha misuli kifaa hichi kilikua kinapatikana kwa @230,000/=. Sasa ni 210,000/= tu

4. MAXMAN CAPSULE--- Hii ni dawa ya vidonge ya kuongeza maumbile ya kiume urefu na upana pamoja na kuongeza nguvu za kiume kwa wiki mbili ilikua inapatikana kwa @200,000/=. Sasa ni 180,000/= tu

5. VIG RX---- Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza uume urefu na upana mpaka nchi 10 ilikua inapatikana kwa @190,000/=. Bei ya sasa ni 170,000/=

6. BODY BOOSTER---Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza mwili pamoja na hamu ya kula vizuri ilikua inapatikana kwa @150,000/=. Sasa ni 140,000/=

7. BOTCHO MULT PLUS-- Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza (hips mapaja na makalio) kwa size uipendayo ilikua inapatikana kwa @200,000/=. Sasa ni 180,000/=

8. WHITE COLLECTION---- Ni vidonge vya kuwa mweupe mwili mzima pamoja na kuwa soft ilikua inapatikana kwa @150,000/= Sasa ni @140,000/= tu

9. BOTCHO HOLOGRAM CREAM--- Hii ni dawa ya kuongeza hips na makalio ilikua inapatikana kwa@180,000/= Sasa ni@160,000/=       

N.K

Wasiliana nasi kwa simu

NO:. +255 759029968  AU +255 659618585

Popote ulipo utapata huduma zetu.

Pia hakikisha unapatiwa risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY PROD ununuapo bidhaa kampuni hii.

WELCOME ALL

Mwalimu Amuua mpenzi wake kisha na yeye kujinyonga kisa usaliti

0
0
Watu wawili wanaodaiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi, Karoli Domisian  (36) na Regina Temu (29) wamefariki katika mtaa wa Mafumbo, manispaa ya Bukoba mkoani Kagera baada ya mwanaume kumuua mpenzi wake kisha yeye mwenyewe kujinyonga, kisa usaliti wa mapenzi.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba mauaji hayo yamegundulika Desemba 17 saa 11 jioni katika mtaa huo.

Amesema kuwa Regina Temu (29) ambaye ni mkazi wa Kahororo katika manispaa hiyo na mfanyakazi wa kiwanda cha kusindika kahawa cha Tanica alikutwa amenyongwa kwa tai nyumbani kwa Karoli Domisian (36), Mwalimu wa  shule ya sekondari Nyanshenye iliyoko katika Manispaa ya Bukoba, ambapo baada tu ya kutekeleza mauaji hayo, Karoli alijinyonga palepale kwa kutumia kamba ya manila ndani ya chumba chake.

"Ndani ya chumba chake kulikutwa karatasi yenye ujumbe wa maandishi iliyoonekana kuandikwa na mwanaume, kwamba amejinyonga mwenyewe baada ya kumuua mpenzi wake, kutokana na kumsaliti"Kamanda Malimi.

Malimi ameeleza kwamba Regina alikuwa akiishi na dada yake eneo la Kahororo na kuwa aliondoka Desemba 16 mwaka huu saa kumi jioni na kuaga kuwa anakwenda sokoni lakini hakurudi nyumbani.

"Baada ya dada yake kuona hakurudi, kesho yake ambayo ni Desemba 17, 2018 alianza kumtafuta hadi polisi bila mafanikio, lakini ilipofika saa 11:30 jioni aliamua kuongozana na mtu mwingine kwenda kwa hawara wa mdogo wake na baada ya kufika huko ndipo aligundua kuwa mdogo wake ameuawa na kutoa taarifa polisi ambao waliwahi kufika katika eneo la tukio na kukuta marehemu hao na karatasi yenye maandishi hayo".

Kwa mujibu wa kamanda huyo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha vifo hivyo.

Video Mpya: Lava Lava - Niuwe

0
0
Video Mpya: Lava Lava - Niuwe

Okoa Ndoa Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Hii Iitwayo Simpo Power

0
0
Okoa Ndoa Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Hii Iitwayo Simpo Power Kwaajili Ya Nguvu Za Kiuume Na Promix Kwaajili Ya Kuongeza Maumbile;
Kwa mwanaume aliyekamilika na mwenye Afya njema ili kumridhisha mke au mpenzi anatakiwa awe na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya Mara mbili hapo utamridhisha mpenzi wako ila ukiwa unapiga moja au mbili hapo ujue umejilidhisha wewe 

Tiba Ya Tatizo Lako Ni Dawa Hiitwayo Simpo Power No, 1; dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge vya miti shamba na unga ambayo hutibu matatizo matatu kwa pamoja :-1 itakufanya urudie tendo zaidi ya mara tatu 
2 itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika 15-20 kwa tendo la Kwanza 
3 huimarisha uume uliolegea na kusinyaa 

Je Una Mke Au Mpenzi Aliyebalikiwa Kuwa Na Kario Kubwa Au Mwili Mnene Na Wewe Mume Wake Una   Maumbile Mafupu?; tumia sasa dawa ya PROMIX dawa itakufanya umfikishe shemu nyeti maana inaboresha maumbile saizi upendayo.

Dawa zangu haziina madhara yoyote kwa mtumiaji 

MARKSU; ni dawa ya kisukari dozi siku 21 
MWARU; ni dawa ya uzazi,hufungua milija ya uzazi ata kwa Wale waliofungiwa uzazi  
MTUNDUU; ni dawa ya busha bila kupasua 
MAZANZA; ni dawa ya kisukar zipo dawa za miguu Kuuma,tumbo,kupunguza Matiti,kutoa minyama uzembe ngiri,vidondo vya tumbo  

FIKA OFISINI KWANGU BUGURUNI MALAPA KARIBU NA KOTA ZA POLISI AU PIGA  SIMU ULETEWE MAHALI ULIPO SIMU NO 0783185060,  0752348593  -DR AGU

Video Mpya: Mo Music – Naiona Kesho

0
0
Video Mpya: Mo Music – Naiona Kesho

Vanessa Mdee azindua viatu kwa wanafunzi wa kike

0
0
Msanii wa Bongo Fleva nchini, Vanessa Mdee amezindua bidhaa zake za viatu maalum kwa wanafunzi hasa wasichana alizozipa jina la ‘Bora Star by Vanessa Mdee’.

Kupitia ukurasa wake wa twitter, jana Jumanne Desemba 18, alituma ujumbe na picha akionyesha viatu hivyo huku akisema imekuwa ni ndoto yake kwa muda mrefu.

“Ilikuwa ndoto yangu kutengeneza bidhaa itakayonufaisha na kuboresha maisha ya msichanawa kitanzania ama  kiafrika na leo nimetimiza ndoto yangu, nasema asante Mungu,” ameandika Vanessa.

Kesi ya Malinzi kusikilizwa siku tatu mfululizo

0
0
Kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake wanne ya kutakatisha Dola za Marekani 173,335 imepangwa kuendelea kusikilizwa shahidi wa 10 wa Jamhuri, Januari 16, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Jana kesi hiyo ilipangwa kuendelea kusikilizwa shahidi wa 10 wa upande wa Jamhuri, lakini imeshindwa kuendelea baada ya shahidi huyo kuwa na matatizo ya kifamilia.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Leonard Swai, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi, lakini shahidi waliyemwandaa amepata matatizo ya kifamilia.

Wakili wa utetezi, Richard Rweyongeza, alidai kuwa Jamhuri walitakiwa kuandaa mashahidi wawili tofauti ili mmoja anapopata tatizo au udhuru, mwingine aendelee kutoa ushahidi.

"Mheshimiwa tunaomba hili lisijirudie siku nyingine utetezi tunaomba mahakama ipange siku mbili au tatu mfululizo za kusikiliza ushahidi," alidai Rweyongeza.

Hakimu Mashauri alisema kesi hiyo itatajwa Januari 2 na kusikilizwa kwa mfululizo Januari 16, 17 na 21, 2019 na kuutaka upande wa Jamhuri uandae mashahidi wa kutosha.

Mbali na Malinzi washtakiwa wengine ni, Katibu wa zamani wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu Nsiande Mwanga, ambao wanakabiliwa na mashtaka 28 ya utakatishaji fedha.

Wengine ni Meneja, Miriam Zayumba na Karani Flora Rauya, wote wa TFF, wanakabiliwa na mashtaka 30 yakiwamo ya kula njama na kughushi.

Katika kesi ya msingi ilidaiwa kuwa Malinzi, Mwesigwa na Nsiande walitakatisha Dola za Marekani 173,335 na wako mahabusu kwa sababu mashtaka yao hayana dhamana kisheria.

LIVE: Rais Magufuli Akizindua Barabara Kimara

0
0
LIVE: Rais Magufuli Akizindua Barabara Kimara
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images