Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Lugola Ataka Magereza Kuanza Kujenga Viwanda Vya Samani Vya Kisasa Nchini.....Asema Vilivyopo Haviwezi Kutupeleka Uchumi Wa Viwanda

$
0
0
Na Felix Mwagara (MOHA), Arusha
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelitaka Jeshi la Magereza lianze maandalizi ya ujenzi wa viwanda vya samani vya kisasa kwa kuwa vilivyopo havina hadhi ya kwenda na kasi ya uchumi wa viwanda nchini.

Alisema Viwanda vya Samani cha Ukonga, jijini Dar es Salaam, cha Arusha pamoja na cha Uyui Mkoani Tabora, havina hadhi ya kuitwa viwanda vya kisasa kutokana na uzalishaji wake kuwa mdogo na pia ukubwa wa viwanda hivyo ni mdogo.

Akizungumza leo akiwa katika Kiwanda cha Samani cha Magereza kilichoungua moto mwezi uliopita eneo la Unga Limited, jijini humo, Lugola alisema kiwanda hicho kilichoungua hakuna haja ya kukijenga kingine katika eneo hilo kwa kuwa kiwanda hicho ni kidogo, hivyo maandalizi ya ujenzi wa kiwanda kipya cha kisasa uanze kuanzia sasa.

Alielekeza kuwa, kwa kuwa eneo hilo ni dogo, linatakiwa liboreshwe kwa ajili ya kuhifadhiwa samani ambavyo zitakua zimetengenewa katika kiwanda cha kisasa kitakachojengwa jijini humo.

“Kamishna Jenerali wa Magereza, aanzeni maandalizi ya ujenzi wa kiwanda kingine ambacho kitakua cha kisasa, hili eneo ni dogo mno, na pia hata cha kule Ukonga Dar es Salaam, eneo lake ni dogo, tafadhali anzeni kufikiria kwa upana zaidi kuanza maandalizi ya kutengeneza viwanda hivyo vya kisasa,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, Jeshi la Magereza lina maeneo mengi nchini ya kuweza kujenga viwanda hivyo ambavyo vitaenda kuongeza kasi ya uchumi wa viwanda nchini ambao aliutangaza Rais Dk. John Magufuli katika mipango ya maendeleo ya nchi.

“Tuongeze kasi kwa kuanza kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kisasa, nyie mmeshakua wazoefu, eneo hili litatufanya tuwe na ufinyu wa mawazo kwasababu hata nusu eka halifiki, hili eneo ni dogo mno, na pia mkijenga kiwanda kikubwa mtaweza kutenganisha pia fenicha za chuma na fenicha za mbao katika kiwanda hicho, mnauwezo sana Magereza wa kutengeneza fenicha za kisasa zaidi na kwa wingi,” alisema Lugola.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP), Phaustine Kasike, alisema amepokea maelekezo hayo na atakaa na viongozi wenzake kuyafanyia kazi kwa kuwa Jeshi lake lina maeneo ya kujenga viwanda nchini.

“Tumepokea maelekezo yako mheshimiwa Waziri, tunaahidi tutayafanyia kazi ipasavyo na pia tunakushukuru kwa kuja kututembelea na umefanikiwa kukiona kiwanda hiki kilichoungua na kutusababishia hasara ya mamilioni ya fedha” alisema CGP Kasike.

Kiwanda hicho kiliteketea moto usiku wa kuamkia Novemba 17, 2018 na kusababisha hasara ya zaidi ya milioni nane kutokana na mashine mbalimbali, mbao pamoja na nyaraka zilizopo katika kiwanda hicho ziliteketea moto.

Rais Magufuli Awachana TRA.... "Mnakera sana, sijawatuma mkadhulumu"

$
0
0
 Rais John Magufuli amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatakiwa kujitathmini kwanini watu wanakwepa kulipa kodi na kuamua kutumia wamachinga na wafanyabiashara wadogo kuwauzia bidhaa zao.

Ameyasema hayo leo Jumapili Desemba 2, 2018 wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi wa uboreshaji wa huduma za maji safi na maji taka katika kijiji cha Kimnyaki mkoani Arusha.

Amesema baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wamekuwa na tabia ya kutumia wamachinga kuuza bidhaa zao ili wasilipe kodi.

"Mnaweka viwango vikubwa ambavyo havilipiki jambo ambalo linafanya wafanyabiashara kukwepa, hivyo ni bora kuweka viwango vidogo vinavyolipika na wengi kuliko kiwango kikubwa kinacholipwa na watu wachache," amesema.

Amesema baadhi ya kodi zinazokusanywa na TRA ni za kuudhi kwani licha ya kuwa aliwaagiza kukusanya kodi kila sehemu ila sio za dhulma.

Mbali na hilo aliwataka wamachinga kutumia vizuri fursa ya kufanya biashara kila sehemu waliyopewa ila sio katika kukwepa kodi.

"Serikali isiyokusanya mapato ni Serikali mfilisi, niwaombe sana wafichueni watu wenye tabia hiyo ili wasiwaharibie na muwe mnatoa elimu na sio kupeleka polisi kuwakamata wananchi wanaposhindwa kulipa kodi," amesema.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Aendelea Kushikiliwa na Jeshi la Polisi

$
0
0
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita jana Jumamosi Desemba Mosi, 2018 alikamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na hadi leo saa 9:25 alasiri alkuwa bado anaendelea kushikiliwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema leo kuwa sababu ya Mwita kukamatwa ni kitendo chake cha kuongoza maandamano bila kuwa na kibali. Manadamano hayo yalifanyika jana katika kata ya Vijibweni wilayani Kigamboni kuelekea daraja la Mwalimu Nyerere.

Mwita pia ni diwani wa kata ya Vijibweni Kigamboni kwa tiketi ya Chadema.

“Tulipomkamata akaeleza alikuwa anakwenda kuzindua kisima cha maji ambacho hakukijenga yeye kilijengwa na Serikali kupitia kwa mheshimiwa DC aliyehamia Ruangwa,” amesema Mambosasa.

“Sasa yeye alikuwa anataka kupora ili kutafuta sifa kwamba alijenga yeye wakati mradi ni wa Serikali, aliokuwa amewaalika walikimbia wote.”

Amesema polisi wanaendelea kumshikilia hadi upelelezi utakapokamilika, baadaye atafikishwa mahakamani.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema meya huyo jana alikuwa na mkutano na baadhi ya wananchi wa kata ya Vijibweni kabla ya kuzindua matawi mapya.

Amesema walipokuwa wakielekea katika uzinduzi wa matawi hayo polisi waliwavamia na kuwakamata.

Jinsi ya Kubadili Picha yako na Kuwa Cartoon

$
0
0
Kama wewe ni mpenzi wa picha, utakuwa umeshasikia au kutumia baadhi ya programu za kuedit picha au hata kuzibadili kabisa na kuzifanya kuwa katuni. 

Katika makala hii fupi, tutaangalia programu mbadala za kubadili picha ukiacha ile maaarufu iliyozoeleka miongoni mwetu ya Adobe Photoshop.

Kwa muda mrefu uliopita kama ungemuuliza mtu ni ipi programu nzuri kwa kubadili picha sikuzote angesema Photoshop. Sawa nikweli Photoshop itaendelea kuwa programu kubwa na imara ila ni tabu kidogo kuitumia  maana ina mambo mengi na inahitaji ujuzi wa hali ya juu.

Hapo chini tumekuwekea Program mbadala ambazo zitakufanya u edit picha zako kwa wepesi zaid na pia zitakusaidia kujibadili na kuwa Katuni. 

#1. Be Funky
#2.Cartoonize
#3.Toonyphotos
#4.Cartoon photo 

Maelezo ya jinsi ya kuzipata au kuzitumia Progamu hizo yanapatikana hapa<<HAPA>>

Endelea kuwa nasi, tutaendelea kukuletea makala fupifupi kama hizi

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya Disemba 3

Video Mpya: Kusah ft. Ruby - Chelewa

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Kusah ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Chelewa ambao amemshirikisha Ruby. Itazame hapa.

Je Wewe ni Mwanasiasa, Mfanyabiashara.?...... Tunazo dawa na PETE za bahati Zenye Uwezo wa Kubadili Maisha Yako

$
0
0

Je Wewe ni Mwanasiasa, Mfanyabiashara, Msanii wa Maigizo, Mwanamziki, ama mwanafunzi tunazo Dawa na PETE za Bahati zenye uwezo mkubwa wa kuyabadilisha maisha yako nakukupatia mafanikio makubwa ndani ya mda mfupi tu.

Kutana na Sheikh Jumaa Bilal. Yeye ni mtaalam na mtabibu wa nyota za binadam na bingwa wa tiba za asili Afrika mashariki. 

Wasiliana na mtaalam huyu kwani yeye ufaulu pale wote waliko shindwa na pia humaliza kazi zilizo shindikana ama zilizo achwa ndani ya siku1 tu. Sheikh Jumaa Bilal ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOASHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA-  Sheikh Sasa amezianza ziara zake za mikoani na atayatembelea maeneo mbali mbali ndani na Nje ya nchi.

Anatibu magonjwa sugu yanaojulikana nayasiojulikana kwakutumia QUR_AN MAJI , KIOO MAJINI NA MITISHAMBA.

Anazo dawa za mapenzi( Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu LIMBWATA) kumrudishaa alipote, kutoa Mikosi, Kutatuwa shida za chumaulete, mvuto wa biashara na sehem za kazi, kusafisha nyota, kurudisha mali zilizo ibiwa, zilizpotea, ama zilizodhulumiwa, kushika wezi na wachawi, Kutoa kinga ya mwili, nyumba, Biashara, kufukuza majini wabaya, KUUZA kwa haraka (shamba, NYUMBA, GARI..), Kuweka Zindiko ya mwili, nyumba, shamba, Gari, kupata Kazi na kupandishwa cheo, mali na UTAJIRI bila masharti na mengine mengi ya Siri. (Anazo Pia Pochi zisizo kwisha Hela MAGIC WALLET)

*{لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أيْمَانِكُمْ وَلَٰكِنْ يُؤَاخِذُكُمْ بِمَا عَقَّدْتُمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِمَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ }* ﴿٨٩﴾

✨Wabillahhi Tawfiq Asallam  Alaikum

Kwa tiba na ushauri wasiliana na ofisi kwa
nambari ya simu

+255 688 745 790
+255 672 861 042
Whatsapp :  0762 252 102

Video Mpya: Mkaliwenu – Tumbo La Pombe

$
0
0
Mchekeshaji Mkaliwenu ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Tumbo la Pombe. Itazame hapo chini

Wimbo Mpya: Bright – Shotoa

Dr.Mjukuu wa kushosha : Pata Tiba Asili ya Tatizo la Uzazi, Kutopata Hedhi kwa Mpangilio, Nguvu za Kiume, UTI Sugu

$
0
0
SIX(6) power; Ni dawa ya Nguvu za kiume inayofanya kuchelewa kufika kileleni dkk 30 Hadi 46 unaweza kurudia tendo utakavyo,pia inarutubisha mbegu za kiume kwa wasio na sifa ya kupata mtoto,dozi Ni siku sita mabadiliko masaa manne.Tumia six(6) power ndio kiboko wa yote usisubiri kuhadithiwa.

SHOOLA 4 POWER; Wenye maumbile madogo (KIBAMIA) inanenepesha na kurefusha uume,kama tatizo Ni la kuzaliwa siku 12 Kama Ni la ukubwani siku 6.

MBUKE; Dawa ya Uzazi kwa aliyefungwa na kutofanikiwa kupata mtoto,kwa asie pata hedhi kwa mpangilio mzuri tatizo huisha kabisaa..Ni ya unga.

LYONGO;dawa ya mvuto wa mapenzi Kama umeachwa yote yatakwisha aliembali atakuhudumia mwenza wako atarejea ndani ya SAA 12 hata Kama yupo mbali.

HOLAZA; Ni dawa ya kumaliza matatizo mengi mengi Kama kesi,dhuluma,kushindwa kuuza eneo nyumba na Kama biashara haziendi.

TALIGULA;dawa ya kufungua kitu kilichofungwa kuchawi,kimizimu,majini wabaya mashuleni,kutokupata ajira,kuoa au kuolewa na Safari zilizofungwa
 
KASELA;Ni kiboko ya kusafirisha mizigo na kufika salama..iwe majini,migodini pia katika kilimo na ufugaji.

DR.Mjukuu wa kushosha asema kwanini usumbuke na maradhi mwilini wakati tiba zipo?? ,Amini tiba asilia Sasa maradhi yako yatakwisha .

Je,wewe una maradhi gani mwilini mwako??

(1)Sukari ya kupanda na kushuka(TUNDWA)Ni ya unga inayochemshwa ,dozi Ni siku 20.

(2)Presha ya kupanda na kushuka(NGADA) ni dawa ya unga dozi siku 14

(3)maleria sugu(NINJIWE) dozi siku 8 unapona kabisa

(4)U.T.I sugu(GUMO)Dozi siku 4 habari kwisha kabisa.

(5)Typhoid sugu(IKWATA) Dozi siku 3

(6)Kifua kubana,moyo,Figo(LUGALA)dozi siku 7

(7)Tezi dume(Dozi siku 8 - unga),ngiri,busha bila operation (SALIUNGU)dozi siku 14

(8)Miguu kuwaka moto (JIMYA) dozi siku 6

(9) kilungulia,kwikwi(INJACHI)dozi masaa 6.

(10)msongo wa mawazo.

(11) vidonda vya tumbo (MPALALA) Dozi siku 7.

Hizo Ndizo Huduma Zitolewazo Na Nyingine Nyingi,usitume Meseji Wala Kubip,nahudumia Duniani Pote Ulipo.

Ofisi Zipo Katika Mikoa Miwili Shinyanga Wilaya Ya Kahama Na Dar Es Salaam Wilaya Ya Ilala..Sehemu Zingine Nasafirisha..niulize Kwa Mawasiliano Yafuatayo...

     0744 922 982
     0716 608 959
     0784 475 946.

Lijualikali Ataja Sababu Zitazomfanya Aihame CHADEMA na Kutimkia CCM

$
0
0
Mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali, ameibuka na kutaja sababu inayoweza kumshawishi kujiunga na chama tawala hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, muda mfupi baada ya kukagua mradi wa reli ya kisasa (SGR), kipande cha Dar es Salaam-Kilosa, akiwa miongoni wa wabunge wa kundi la maendeleo endelevu bungeni walioutembelea, Lijualikali alisema anaweza kuihama Chadema na kujiunga na CCM ikiwa serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa kama huo.

“Wanaosema nitahamia CCM ni jambo jema kuwa wanapenda nihamie CCM, ila nitahamia CCM kama tu nitaona kuna sababu za msingi na mengine ya msingi yanafanyika," alisema.

Lijualikali alisema kuwa kama serikali itaendelea kutekeleza miradi mingine mikubwa nchini, hatakuwa na sababu za kukataa kukihama chama chake.

Hata hivyo, mbunge huyo alisema anakwazwa na kitendo cha kutishwa na kukamatwa kamatwa kwa viongozi wa upinzani nchini.

"Nitahamia CCM kama nitaona sababu za msingi sana na mengine ya msingi, lakini si huku kutishana na kufungwa fungwa na kufia jela," alisema Lijualikali.

Alisema hayuko Chadema kwa bahati mbaya na anaamini kwa sasa ni sehemu sahihi kuwapo.

Akizungumzia mradi huio, Lijualikali alisema: "Mradi huu ni kitu endelevu, kitu ambacho tunaamini hata Chadema tukichukua nchi, hatutaing'oa reli, itabaki."

Alisema mafanikio ya mradi huo yataonekana mara utakapokamilika nchi nzima na mizigo kuanza kusafirishwa kwenda nchi mbalimbali.

“Baada ya mizigo kuanza kusafirishwa, nchi itapiga hatua kubwa kiuchumi na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja utakua," alisema Lijualikali.

Alishauri serikali kujenga barabara za kiwango cha lami kuunganisha na stesheni za reli mpya ya kisasa.“Mradi huu utapendeza kama zitajengwa na barabara za kiwango cha lami kwa ajili ya kuunganika na stesheni za reli, hivyo kurahisisha maisha ya watu," alisema.

AU yaionya Burundi kutaka kumkamata Pierre Buyoya

$
0
0
Muungano wa Afrika (AU) umeionya Burundi dhidi ya hatua zinazoweza kuhujumu mchakato wa amani baada ya kutolewa waraka wa kimataifa kumkamata rais wa zamani Pierre Buyoya na maafisa wengine 16.

Wanatuhumiwa kwa mauaji ya mwaka 1993 ya rais wa kwanza aliyechaguliwa nchini humo ambaye alitoka kabila la Hutu, ambapo kuuliwa kwa, Melchior Ndadaye kulisababisha kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Aidha, kuna hofu kuwa kumlenga Buyoya ambaye ni kutoka kabila la Tutsi anayeishi nchini Mali kunaweza kuchangia kuzuka misukosuko ya kikabila.

Zaidi ya watu 300,000 waliuawa kwenye vita ya miaka 12 vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi lenye watutsi walio wachache na waasi wa Hutu.

Hata hivyo, Buyoya 69, alihusika kwenye mchakato wa amani uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuongoza kuchaguliwa kiongozi wa zamani wa waasi wa Hutu, Pierre Nkurunziza kuwa rais mwaka 2005.

Mchungaji Apigwa Mawe Na Waumini Wake Wakimtuhumu ni Mchawi

$
0
0
Waumini wa Kanisa la Sauti ya Uzima  wamevamia na kushambulia kwa mawe  nyumba ya Mchungaji wa   Kanisa hilo, Nabii Elia (36) wakimtuhumu kuwa ni mshirikina.

Jina  kamili la Nabii Elia limeelezwa kuwa ni Elia Zabron Balashika raia wa Burundi ambaye amekuwa akitoa huduma ya roho zaidi ya miaka sita eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema tukio  hilo   lilitokea Mtaa wa Kazima Ringini Manispaa ya Mpanda, baada ya waumini kuvamia nyumbani kwa kiongozi huyo.

Alisema waumini  watano wametiwa mbaroni na watu kadhaa  kutokana na kujichukulia sheria mkononi.

Aliwataja waumini  waliokamatwa  kuwa ni William  Kaluzi (19) mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa , Steven Alfred (31) mkazi wa Mtaa Kazima, Nicholaus Shadrack (33)  mkazi wa Mtaa wa Kazima  na Tekla Didas (17) mkazi wa Kijiji cha Rungwa

Wengine ambao  siyo waumini wa kanisa hilo   ni  Mashaka Moshi (23) mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa na Faraja Hussein (22) mkazi wa Mtaa wa Kazima.

Kamanda Nyanda  alisema chanzo  ni imani za ushirikina baada ya taarifa kuzagaa kuwa  Nabia Elia alikuwa ameweka ‘misukule’ watano nyumbani kwake  ambao waumini   wa kanisa hilo walimtaka awatoe  hadharani.

Alisema siku ya tukio saa 11:30 jioni,  Nabii Elia alifika  Kituo cha Polisi mjini Mpanda ambako alitoa taarifa kuwa nyumba yake ilikuwa  imevamiwa na wananchi ambao walikuwa wanaharibu mali zake .

“Ndipo timu ya  polisi wakiongozwa na SSP Focus Malengo, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa  ya Jinai Mkoa wa Katavi, Abdallah Hussein  na Kaimu  Ofisa Upelelezi  Wilaya ya Mpanda, Mkaguzi Ngagala, walifika eneo la tukio na  kukuta kundi  la wananachi     wakiendelea kurusha mawe,“ alieleza.

Alisema walianza  kutuliza ghasia kwa kufyatua mabomu ya kishindo   kuwatawanya wananchi hao, huku  waumini wawili wa kanisa hilo wakijeruhiwa  kwa  kupigwa  mawe kichwani .

Waliojeruhiwa ni Mchungaji wa Kanisa hilo,  Mussa Elia (24) na mkazi wa Mtaa wa Kazima, Joseph Elia (29) ambao wanadaiwa kuwa ni ndugu zake na Nabii Elia .

Alisema mali za Nabii Elia zilizoharibiwa  ni  pamoja na vioo vinne vya madirisha ya nyumba yake, kioo cha nyuma cha gari lake  la Spacio,  huku thamani kamili  ikiwa bado haijafamika.

China, Marekani Waanza Mazungumzo Kumaliza Vita ya Kibiashara

$
0
0
Nchi mbili zenye uchumi mkubwa zaidi duniani wamekubaliana kufikia masikilizano madogo katika vita iliyokuwa inaongezeka ya kibiashara baada ya kukutana kwa marais Donald Trump na Xi Jinping katika mkutano wa nchi tajiri zenye viwanda G20.

Trump akiongea na waandishi wa habari katika ndege ya rais Air Force One baada ya ndege kuondoka Argentina, amesema makubaliano yaliofikiwa wakati wa chakula cha usiku na Xi, yatakuwa katika historia “kama moja ya makubaliano makubwa yaliyowahi kufikiwa…Na yatakuwa na athari kubwa chanya katika kilimo, bidhaa za viwandani na kompyuta – kila aina ya bidhaa.”

Trump amekubali kuwa ushuru wa bidhaa za China zenye thamani ya dola za Marekani milioni 200 kuendelea kuwa asilimia 10, na hatoongeza ushuru huo hadi asilimia 25, kwa hivi sasa, kama alivyokuwa ametishia kutekeleza hilo ongezeko ifikapo Januari 1, kwa mujibu wa tamko la White House.

Trump na Xi pia “ wamekubaliana mara moja kuanza mazungumzo ya mabadiliko ya miundo ya kuhamisha teknolojia, kulinda haki miliki za kitaaluma, mazungumzo juu ya bidhaa zisizo kuwa na vikwazo vya ushuru, udukuzi wa mitandao na wizi wa kimitandao, huduma na kilimo, kwa mujibu wa tamko la White House.

“Pande zote zimekubaliana kuwa wataendelea kufanya juhudi za kukamilisha majadiliano haya katika kipindi cha siku 90. Na iwapo muda huu utamalizika na pande hizi mbili hazijafikia makubaliano, ushuru huu wa asilimia 10 utaongezeka hadi asilimia 25.

Baadhi ya maelezo hayo yalifafanuliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye alithibitisha kuwa nchi zote mbili zitaanza mazungumzo.

Habari hizi bila shaka zitaleta furaha Jumatatu katika masoko ya fedha ya kimataifa, ambazo zimekuwa na wasiwasi juu ya kuongezeka kwa vita ya kibiashara kati ya China na Marekani.

Credit:VOA

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Aachiwa Kwa Dhamana

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuachia kwa dhamana Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita baada ya kumshikilia kwa zaidi ya saa 24.

Mwita ambaye ni diwani wa Vijibweni (Chadema) alikamatwa na polisi juzi Desemba Mosi, 2018 saa 11 jioni baada ya kumaliza kikao cha kutunisha mfuko wa vijana na kuachiwa jana saa 2 usiku akituhumiwa kufanya maandamano bila kuwa na kibali.

Wakili wa Meya huyo, Alex Massaba amesema baada ya polisi kuchukua maelezo walimuachia kwa dhamana na kumtaka aripoti leo kwa mkuu wa upelelezi Wilaya ya Kigamboni.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Mwalimu Jela Miaka Mitatu Kwa Kupokea Mishahara Miwili

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na kurejesha Sh milioni 10.3, Mwalimu Josiah Mkome baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili.

Mwalimu Mkome alikuwa akifundisha Shule ya Sekondari Kandawe wilayani Magu, mkoani Mwanza alishtakiwa kwa kosa la kupokea mishahara miwili kutoka katika Wilaya ya Magu na Maswa kinyume cha sheria.

Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa, amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Fredrick Lukuna, mshtakiwa alipokea mishahara hiyo miwili tangu Februari mwaka 2012 hadi Mei mwaka 2015.

Godbless Lema Ataka Naibu Spika Tulia Ackson Ashughulikiwe Kwa Kuimba Wimbo wa Nyegezi Mwanza Uliofungiwa

$
0
0
Video inayosambaa mtandaoni ikimuonyesha Naibu Spika wa Bunge, Dr. Tulia Ackson Mwansasu akiwa na Wabunge wanzake wakiimba wimbo ‘Mwanza’ wa muimbaji Rayvanny ambao umefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), imezua gumzo mtandaoni.

Wabunge hao walikuwa nchini Burundi kwenye michuano ya wabunge na baada ya kuibuka na ushindi wakaanza kushangilia kwa style ya kuimba wimbo huo ambao upo kifungoni.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka kwa kudai kwamba, Mhe Spika Tulia anatakiwa kuhojiwa na kamati ya maadili ya Bunge kuhusiana na tukio hilo.

“Nina muomba Mh Spika Ndugai aitishe kamati ya maadili ya Bunge juu ya kitendo cha Naibu Spika Mh Tulia kuimba na kucheza wimbo uliopigwa marufuku na Basata unaoitwa Nyege,Nyege ,Nyegezi /Mwanza akiwa Nchini Burundi.Mimi na Mke wangu tume huzunika sana".
Video hiyo ipo kwenye mtandao wa Instagram wa meneja wa Diamond, Babu Tale.

Katibu Mkuu CCM Azidi Kumkomalia Benard Membe...Amtaka Ajifunze Toka Kwa Lowassa

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amemsifia Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akisema kuwa ni mtu muungwana na hana unafiki na kumtaka Bernard Membe kuiga tabia hiyo.
 
Akizungumza jana usiku Desemba 2, 2018 mjini Geita Bashiru amesema Lowassa ambaye kwa sasa ni mwanachama wa CHADEMA, hajawahi kuzusha wala kutoa kauli mbaya dhidi ya Rais John Magufuli.

"Mtu kubaki ndani ya CCM kinafiki na kuendelea kugawa chama kwa makundi hawezi kumvumiliwa na nitahakikisha ninamaliza makundi kwenye chama", amesema Dkt Bashiru.

Kauli hiyo ya Dk. Bashiru ni mwendelezo wa mjadala kati yake na Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimtaka afike ofisini kwake kujieleza, ambapo alitoa kauli hiyo kwa mara ya kwanza akiwa mkoani Geita, akijibu ujumbe uliotumwa kwenye akaunti ya mtandaoni ya mtu mwenye jina la Bernard Membe kujibu tuhuma zilizotolewa na Dkt. Bashiru akiwa Geita.

Dkt. Bashiru alimtuhumu Membe kuandaa mpango wa kumkwamisha Rais John Magufuli katika uchaguzi wa Rais na kwamba tangu ateuliwe hajawahi kuonana na mbunge huyo wa zamani wa Mtama.

Dkt. Bashiru amesema anamheshimu Lowassa kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM baada ya kutopewa ridhaa ya kugombea Urais na kwenda chama kingine badala ya kubaki ndani ya chama tawala kinafiki na kuwagawa wanachama

Amesema hayupo tayari kuona migogoro iliyowakumba makatibu wakuu waliomtangulia wakati wa uchaguzi akutane nayo sasa na kwamba mkakati wake mkuu ni kuua makundi.

Wakili Medium Mwale Ahukumiwa Kwenda Jela Miaka 5 Au Kulipa Faini Ya Milioni 200

$
0
0
Jaji Issa Maige wa Mahakama Kuu Arusha, amemuhukumu wakili Medium Mwale kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya Sh 200 milioni kutokana na kosa la utakatishaji fedha

Pia amemuhukumu kifungo cha miaka saba ambacho ameshakitumikia kutokana na makosa mengine.

Wakili Mwale na wenzake, Boniface Mwimbwa aliyekuwa meneja wa Benki ya CRDB tawi la Meru na Elias Ndejembi wanatuhumiwa kwa makosa 41 ikiwemo kughushi na utakatishaji fedha.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images