Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

CHADEMA Walaan Dereva wa Freeman Mbowe Kushikiliwa Polisi

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelalamikia hatua ya  Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumshikilia kwa siku mbili  mtumishi wao Williard Urassa.

Urassa ambaye ni dereva wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikamatwa jana nje ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Novemba 24, 2018 na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imeeleza tangu Urassa alipokamatwa na polisi, jeshi hilo limekataa kumpatia dhamana huku likizuia mtu yeyote kuonana naye.

Makene amesema zuio hilo limewakumba hadi wanasheria waliofika kwa ajili ya kumpatia msaada wa kisheria.

“Hali ambayo inaibua maswali mengi na sintofahamu kubwa kuhusu hali yake baada ya kukamatwa.

"Tunalaani na kukemea vikali kitendo hicho cha Jeshi la Polisi ambacho ni mwendelezo wa tabia inayopaswa kuachwa mara moja ya jeshi hilo kujipatia mamlaka lisilokuwa nayo, hasa kuwakamata na kuwashikilia chini ya ulinzi kinyume cha sheria,”imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesisitiza ni vyema jeshi hilo likatambua kuwa halina mamlaka ya kumshikilia mtu yeyote kwa namna hiyo.

Kulingana na taarifa hiyo Chadema imelitaka jeshi la polisi kueleza sababu za  kumshikilia dereva huyo.

Albert Msando Afunguka Baada ya Tamasha la Tigo Fiesta Kusitishwa

$
0
0
Mwanasheria maarufu nchini Tanzania, Alberto Msando amefunguka baada ya kamati ya maandalizi ya Tigo Fiesta mwaka 2018 kutangaza kusitisha tamasaha hilo lililopaswa kufanyika leo Novemba 24, mwaka 2018 katika viwanja vywa Leaders Kinondoni Dar es salaam.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram wakili huyo msomi ameandika kuwa maamuzi ya kutoa kibali wakati mtu anajua kuna wagonjwa wa moyo ni ya kipuuzi huku akiongeza kuwa maamuzi ya kufuta kibali cha Tigo Fiesta siku moja kabla ya tukio ni ya hovyo.

”Hatuwezi na hatupaswi kuwa nchi au mkoa ambao mfanyabiashara au mwananchi hana uhakika au hajui maamuzi gani yatatolewa kuhusu maisha yake au jambo lake lolote. Maamuzi ya kutoa kibali wakati mtu anajua kuna wagonjwa wa moyo ni ya KIPUUZI,” ameandika wakili Alberto Msando.

Wakili huyo msomi, Msando ameongeza; ”Maamuzi ya kufuta kibali cha Tigo Fiesta siku moja kabla ya tukio ni ya HOVYO. We must be consistent. Huwezi kusema na ukaeleweka kwamba ‘baada ya malalamiko ya wagonjwa’ ndio umegundua Leaders hapafai kwa tamasha! Uongozi wenye kuacha alama una sifa zifuatazo 1. USAWA 2. UKWELI 3. HAKI 4. BUSARA 5. USHIRIKISHAJI. All said, kila mmoja atajifunza. Jambo ambalo liko wazi sana ni kwamba kila mmoja wetu anayo NAFSI. HUWEZI KUIDANGANYA NAFSI YAKO.”

Mapema asubuhi ya leo uongozi wa Clouds Media kupitia kamati ya maandalizi ya Tigo Fiesta mwaka 2018 imetangaza kusitisha tukio la kilele cha msimu wa Tigo Fiesta 2018 lililopaswa kufanyika leo Novemba 24, mwaka 2018 katika viwanja vywa Leaders Kinondoni Dar es salaam.



A post shared by Msando Alberto (@albertomsando) on

Jinsi ya Kubadili Picha yako na Kuwa Cartoon

$
0
0
Kama wewe ni mpenzi wa picha, utakuwa umeshasikia au kutumia baadhi ya programu za kuedit picha au hata kuzibadili kabisa na kuzifanya kuwa katuni. 

Katika makala hii fupi, tutaangalia programu mbadala za kubadili picha ukiacha ile maaarufu iliyozoeleka miongoni mwetu ya Adobe Photoshop.

Kwa muda mrefu uliopita kama ungemuuliza mtu ni ipi programu nzuri kwa kubadili picha sikuzote angesema Photoshop. Sawa nikweli Photoshop itaendelea kuwa programu kubwa na imara ila ni tabu kidogo kuitumia  maana ina mambo mengi na inahitaji ujuzi wa hali ya juu.

Hapo chini tumekuwekea Program mbadala ambazo zitakufanya u edit picha zako kwa wepesi zaid na pia zitakusaidia kujibadili na kuwa Katuni. 

#1. Be Funky
#2.Cartoonize
#3.Toonyphotos
#4.Cartoon photo 

Maelezo ya jinsi ya kuzipata au kuzitumia Progamu hizo yanapatikana hapa<<HAPA>>

Endelea kuwa nasi, tutaendelea kukuletea makala fupifupi kama hizi

Benki Kuu Tanzania yataja maeneo ya kubadilishia fedha Arusha

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania imewataka wakazi wa Jiji la Arusha kuanza kutumia huduma za kubadilisha fedha za kigeni kwenye maeneo ambayo yanatambulika kisheria ambayo yameainishwa kwenye taratibu za benki kuu.
 
Taarifa ya BOT iliyotolewa leo imesema kuwa “huduma za kubadilisha fedha za kigeni jijini Arusha zinapatikana kwenye hoteli za kitalii na benki za biashara kwa mujibu wa sheria na kanuni  za Benki Kuu ya Tanzania”

Aidha, huduma hiyo pia inapatikana nchini kote katika benki za biashara, maduka ya kubadilisha fedha na hoteli za kitalii.

Benki Kuu ya Tanzania ilifanya ukaguzi wa ghafla katika maduka ya kubadilisha fedha jijini Arusha tarehe 19 Novemba 2018 na kuamua Kuyafunga maduka yasiyozingatia taratibu na sheria za biashara hiyo.

Aidha BOT imewataka wakazi wa Jiji la Arusha kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho huduma za kubadilishia fedha zikiwa zimesitishwa kwenye maduka maalum.

“Benki Kuu inawashukuru wananchi wa jiji la Arusha kwa ushirikiano na kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za kisheria zikiendelea.” imeeleza taarifa hiyo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Septemba 24

Serikali Yafafanua Utolewaji Wa Vibali Kwa Ajili Ya Uchimbaji Visima Nchini

$
0
0
Serikali imewatoa hofu wananchi kuhusu utaratibu ulioanzishwa kwa wenye visima kuanza kuvilipia na kueleza kuwa haina nia ya kuwakomoa wananchi bali sheria inawataka kufanya hivyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa, Kitilia Mkumbo, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akitoa ufafanuzi wa masuala ya maji pamoja na visima.

Prof. Mkumbo alikuwa anatoa ufafanuzi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliyetaka kujua ni visima gani hasa ambavyo vinalengwa na serikali.

"Mkoa wangu una visima vingi moja wapo ni hivi ambavyo wananchi wangu wamejichimbia maji nyumbani mita 12 na wengine kwa sababu hatujawafikishia maji asilimia 100 waliona wana uwezo wa kuchimba visima na kuwasambazia wenzao," alisema na kuongeza:

"Sasa juzi nimesikia kauli ambayo kidogo imeleta taharuki na kuna visima zaidi ya 3,000 naomba na hili utupe kauli yako na Sheria inasema nini maana wanaona kama serikali inawatisha," alisema Makonda.

Mkumbo alisema visima hivyo vimegawanywa katika makundi matatu, la kwanza ni la visima ambavyo havihitaji kibali wala mhusika halipii chochote, la pili vinavyohitaji kibali na kulipa wakati cha tatu ni kile cha kiwango cha kufanya biashara kama viwanda.

Alisema wenye viwanda wote wanafahamu taratibu za kumiliki visima, namna ya kutumia maji na wakulima wakubwa kwa kuwa kila mwaka wanaomba vibali lakini changamoto inakuwa katika kundi la kwanza na pili.

Alisema kwa kundi la kwanza kwa mujibu wa sheria, kama mtu anachimba maji nyumbani chini ya mita 15 kwa ajili ya kwa matumizi ya nyumbani na hajaweka miundombinu yoyote, hahitaji kibali wala kulipia.

"Lakini kama utatengeneza mita 15 au zaidi, ukaweka miundombinu kama mashine za kusukuma maji, hapa utahitaji kibali na ukifuata maji zaidi ya mita 15 utalipia ada fulani kutokana na kiwango cha maji. Hizi ndizo taratibu za msingi," alisema.

Mkumbo alisema suala hilo limewekwa hivyo kwa makusudi ili mhusika atumie maji katika hali ambayo haitaathiri watu wengine, atumie katika hali isiyoathiri mazingira na atumie maji hayo katika hali ambayo itawezesha kutumika na vizazi vijavyo.

"Lengo la kufanya hivyo si kumkomoa mwananchi hata kidogo. Serikali inatambua ni lazima upate maji na imeweka utaratibu wa kawaida wa kurahisisha kupata maji," alisema.

Katibu Mkuu alisema kwa bahati mbaya sheria hizo zilikuwa hazifuatwi na kwa sasa wameanza kufuatilia visima ingawa kumekuwa na changamoto.

Alisema wanatoa elimu kwa wananchi ili waelewe hizo taratibu na kuzizingatia na anaamini kwamba watanzania ni watu wanaofuata taratibu baada ya kuzielewa sheria.

"Katika mchakato huu wa kutekeleza sheria hiyo kama kutajitokeza changamoto za kisheria ndio maana kuna Bunge, wananchi watatoa malalamiko yao na Bunge letu watalichukua na kulifanyia kazi lakini kwa sasa utaratibu ndio huo," alisema.

Aidha, Mkumbo alisema maji ni rasilima ya nchi hivyo mtu binafsi hawezi kusema anamiliki maji yake.

Alisema kwa sababu maji ni rasilimia ya taifa ni lazima kuwepo na utaratibu wa kuipata na Rais ndiye aliyekabidhiwa kuisimamia.

"Wapo wananchi na wafanyabiashara wamechimba visima kwa bahati mbaya bado hatujavitambua vyote kwa sababu hatujapata taarifa kutoka kwa wananchi. Tumeagiza maofisa wetu katika mikoa yote kuanza kufanya kazi ya kuvitambua," alisema

Mkumbo alisema Sheria ya mwaka 2009 na 2011 ya rasilimali za maji imeweka taratibu zake kuhusu namna wananchi wanavyoweza kujishughulisha katika kupata maji.

Aidha, alisema wanaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji na ifikapo 2020 wana uhakika wa kupunguza tatizo la maji kwa asilimia kubwa.

Treni Ya Serikali Ilivyotumika Kusafirisha Mizigo ya Magendo

$
0
0
Shehena ya mbao imekamatwa katika stesheni ya Shinyanga ikisafirishwa kimagendo katika treni ya mizigo kutoka mkoani Tabora kuelekea Mwanza.

Shehena hiyo imekamatwa baada ya kuwekwa mtego na wakala wa huduma za misitu wakishirikiana na Jeshi la Polisi.

Akizungumza jana Ijumaa Novemba 23, 2018 ofisa misitu Wilaya ya Kahama mkoani humo, Mohamed Dossa alisema mbao hizo zimekamatwa wakati mabehewa hayo yakiwa katika kituo cha bandari kavu cha Isaka.

Alisema baada ya kupata wasiwasi waliwasiliana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) mkoani humo  pamoja na polisi na kufanikiwa kukamata mabehewa mawili yakiwa na mbao hizo.

Treni hiyo ya mizigo baada ya kukaguliwa  mabehewa mawili yalibainika kuwa na  shehena ya mazao ya misitu ikiwemo mbao, asali na milango.

Alisema vitu hivyo huenda vimevunwa na kusafirishwa kinyume cha sheria,  bila kulipiwa ushuru   wa Serikali.

Alisema kukamatwa kwa mabehewa hayo kulitokana na taarifa zilizotolewa na wasamaria wema wa wakala wa misitu mkoani Tabora na hivyo treni hiyo kuzuiwa baada ya kufika mjini Shinyanga.

“Treni hiyo ya mizigo ilikuwa ikitoka mkoa wa Tabora, walianza kuishtukia katika kituo cha bandari kavu cha Isaka na askari wa TFS aliyejulikana kwa jina la Leonard Maguta alipopanda katika treni hiyo kufuatilia alipigwa na askari waliokuwemo ndani na kushushwa njiani,” alisema Dossa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule akizungumza na waandishi wa habari alisema katika tukio hilo wanawashikilia watu wanne ambao majina yao yamehifadhiwa hadi uchunguzi utakapokamilika.

Alisema mbao zilizokamatwa ni zile ambazo haziruhusiwi kuvunwa mpaka kwa kibali maalumu na zilikuwa zikisafirishwa bila kuwa na kibali.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amewataka watumishi kuwa waadilifu na kuacha kusafirisha vitu haramu ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo ya nchi na kuwataka kufuata taratibu na sheria.

“Usafirishaji wa magendo kwa njia ya reli umekithiri sana na mizigo mingi ya aina hiyo imebainika na kukamatwa ambapo amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa wanapoona hali kama hiyo ili kuchukua hatua kabla ya tukio kumalizika kutendeka” alisema mkuu wa wilaya .

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Leo Novemba 25


RPC Pwani Apewa Vitisho Na Watu Wasiojulikana,

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,pwani
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa anadaiwa kutishiwa na watu wasiofahamika kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS) kuwa watamhamisha kwenye mkoa huo kutokana na kuzuia kuingiza bidhaa za magendo kwenye bandari bubu .

Licha ya kitisho hicho amesema,hawezi kulegeza uzi kwani shughuli hizo zinasababisha nchi kukosa mapato kwa kukwepa ushuru.

Akizungumza kwenye kituo cha polisi wilaya ya Bagamoyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo baada ya kufanikiwa kukamata bidhaa mbalimbali ikiwemo madumu ya mafuta ya kula 4,311 ya lita 20 kila moja na mafuta ya dizeli madumu 52 kwenye oparesheni zinazoendelea mkoani humo.

“Kwa siku za hivi karibuni mimi pamoja na watendaji wenzangu akiwemo ofisa upelelezi wa mkoa tumekuwa tukitumiwa jumbe za vitisho kupitia simu”

“Nitafanya kazi kwa maelekezo ya mkuu wa mkoa, IGP na Rais hivyo siko tayari kufanya kazi kwa maelekezo ya watu wengine ambayo ni kwa maslahi ya mtu binafsi bali kwa maslahi ya nchi”

“Sitishwi na mtu wala sms eti watatuhamisha ama watatupeleka Mlingotini waambieni meseji zao tunazo ,tunazifanyia kazi na tumechukua namba za hawa tuliowakamata kutokana na operesheni hizi kama ni miongoni mwao tutawachukulia hatua kali “alieleza Nyigesa.

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alisema lazima vyombo vinavyohusika vifuatilie jambo hili ikiwa ni pamoja na mamlaka ya chakula na dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Mapato (TRA).

”Kila mamlaka hapo inapaswa kuhakiki bidhaa hizo ili kujiridhisha kuwa  bidhaa hizi zimeingizwa nchini kwa kufuata taratibu ??na ile ya chakula na dawa kuangalia kama mafuta hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu”alisema Ndikilo.

Katika msako huo pia vifaa vya ujenzi marumaru katoni 200, friji 16, pikipiki moja isiyokuwa na namba bangi kete 512 na pombe ya moshi lita 16 vilikamatwa na watuhumiwa 17 wanaotuhumiwa kuhusika na matukio hayo wanashikiliwa.

Kuwa Makini: App Hizi Zina Uwezo Wa Kuiba Taarifa zako za Benki, Email na Password Zako

$
0
0
Kama ukiangalia katika simu yako  nina uhakika Application nyingi ulizopakua ni za bure.Wote tunapenda App za bure. 

Mara nyingi App za bure zina gharama ya faragha (privacy) wakati wa kuziingiza katika kifaa chako. 

Je unasomaga vigezo na masharti kabla ya kuipakua hiyo Application na kuiweka kwenye simu yako? Ninauhakika jibu na HAPANA.

Wengi huwa tunabonyeza tuu ‘Agree’ katika vigezo na masharti, kitu ambacho ni kosa kubwa.

Lazima usome kuwatambua waliotengeneza na ujue  ni vitu gani unawaachia mikononi mwao kama vile namba za simu, meseji zako, maeneo (locations) na vitu vingine kibao.

Tuende moja kwa moja kwenye mada ya leo.Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wataalam waliobobea wa kituo cha ESET umebaini uwepo wa Application 29 zilizopo Google Play Store ambazo ni VIRUS aina ya TROJAN

Kwa mujibu wa utaifiti huo, virusi hao ambao hutumia majina tofauti tofauti wanauwezo wa kuingilia application zingine zilizopo katika simu yako na kutuma taarifa zote kwa Hackers(Wadukuzi).

App hizo ambazo zina virus ndani yake, pia zinauwezo wa kutengeneza Fake Logins Page ( Phishing)  ambapo ukijichanganya tu basi taarifa zako za siri kama bank details,email, password zako za mitandao ya kijamii huchukuliwa na kutumwa kwa Hackers.

==>Baadhi ya App hizo ni:   
Daily Horoscope – Astrological Forecast
Master Cleaner – CPU Booster     

Speed Cleaner – CPU Cooler
Master Clean – Power Booster    

Horoscope 2018
Super Fast Cleaner 


Ni imani yangu makala hii imekufungua macho na utakuwa makini zaidi ili kujikinga na wadukuzi wa mitandaoni.

<<INGIA HAPA>> Kuzijua App zote 29 ambazo zina virusi ndani yake. Kama ulizipakua basi zifute kabisa kwenye simu yako.

Je wewe ni mmoja kati ya wale wanaokubali vigezo na masharti bila kusoma maelezo ya Application  husika? Funguka apo chini kwenye comments. 

Usisahau Kuinstall App yetu kwa habari motomoto. Ingia playstore, search Mpekuzi, utaipata

Lugola Asema Ili Upate Kitambulisho Cha Taifa Lazima Upitie Katika Mchujo Mkali

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema vitambulisho vya taifa vitatolewa kwa watanzania wenye sifa ambao watapita katika mchujo ili kuepusha kutoa kwa wahamiaji haramu.

Amesema mchujo huo unaofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) upo makini ili kuhakikisha hakuna makosa yatakayofanywa wakati wa utoaji wa vitambulisho, hivyo wananchi wawe na uvumilivu wakati mchujo huo ukiendelea.

Waziri Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara aliyasema hayo jana, wakati alipokua anazungumza na mamia ya wananchi wa jimbo lake katika Kijiji cha Mwisenyi, Kata ya Butimba, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara na kuwataka wapiga kura wake na Watanzania kwa ujumla wawe na subira wakati hatua za utambuzi na usajili zikiendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.

“Hakuna Mtanzania mwenye sifa atakayekosa kitambulisho cha taifa, lakini lazima muwe na subira wakati zoezi la utambuzi wa watu gani wanaweza kupata vitambulisho hivi, na pia katika utambuzi tunapaswa kuwa makini sana kwasababu tusije tukapenyeza wahamiaji haramu wasiostahili na wao wakaweza kupata vitambulisho na baadaye tukaja kupata shida,” alisema Lugola.

Lugola alisema baada ya hatua ya utambuzi, inafuata hatua ya usajili ambayo pia hatua hiyo nayo inahitaji umakini mkubwa zaidi na ikimalizika hatua hiyo majina yaliyosajiliwa yanarudishwa tena kwa wananchi kuulizwa kama waliosajiliwa wanatambuliwa katika sehemu wanazoishi, hatua hiyo ikiwa na lengo la kupata taarifa sahihi ya waliosajiliwa wanatambuliwa au hawatambuliwi na wazawa katika eneo husika.

“Endapo majina tulioyasajili na kuyaleta kwenu, nanyi mtayakataa basi hatutaweza kutoa vitambulisho kwa huyo au hao mliowakataa, na endapo mtayaridhia majina tuliyowaletea, basi tutaweza kuwatengenezea vitambulisho bila shaka yoyote, na endapo kuna mwananchi amekataliwa na Kijiji kuwa hatambuliwi, anayohaki ya kukata rufaa na kutueleza kwanini apewe kitambulisho,” alisema Lugola.

Lugola ambaye alikua anaulizwa maswali mbalimbali na wananchi hao kuhusu Nida na idara zake nyingine zilizopo ndani ya Wizara yake, aliwahakikishia wapiga kura wake kuwa, hakuna Mtanzania atakayekosa kitambulisho cha taifa, kila mwananchi ana haki ya kupewa akiwa ana sifa ya kupewa.

Aidha, Waziri Lugola aliwataka wananchi wa jimbo lake waanze maandalizi ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara ili kuepuka janga la njaa lisije liwakumba endapo hawata lima. Hata hivyo, kijiji hicho alichokitembelea, kwa mujibu wa taarifa ya mipango yao ya kilimo walisema kuwa wana upungufu mkubwa wa mbegu za mazao mbalimbali hasa zao la pamba.

“Nimeagiza maafisa ugani waje kuangalia upungufu wa mbegu za pamba na kutatua kero hii kutokana na taarifa yenu ya mpango wa kilimo ya mwaka 2018/2019, na pia nasisitiza zaidi mulime mazao ya chakula kwa wingi,” alisema Lugola.

Pia Waziri Lugola alitoa shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho ambao ulisimama kwa zaidi ya miaka sita kutokana na ukosefu wa fedha, na pia aliendesha harambee kwa madiwani na maafisa alioambatana nao katika mkutano huo, na kufanikiwa kuchangisha shilingi milioni moja na elfu ishirini.

Lugola ameanza ziara jimboni kwake akisikiliza kero za wananchi pamoja na kuhamasisha kilimo cha mazao ya pamba, mahindi, mpunga, viazi na mengineyo ambayo wakazi wa jimbo lake wanalima mazao hayo kwa wingi.

Rais Magufuli Na Mkewe Mama Janeth Magufuli Wamesali Ibada Ya Misa Takatifu Dominika 34 Katika Kanisa La Mtakatifu Petro Dar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa sadaka yake wakati wa Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakipeana mkono wa Amani na Masista na  waumini walipojumuika na waumini wengine wakati wa Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikomunika Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoka kanisani mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.

PICHA NA IKULU

TFF yapitisha majina ya wagombea Uongozi Yanga....Yatazame Hapa

$
0
0
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imepitisha majina ya wagombea nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya klabu ya Yanga.

Nafasi hizo ni zile za Uenyekiti, Umakamu na zile za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Zoezi linalosubiriwa hivi sasa ni la mapingamizi pekee kabla ya kuelekea kwenye kampeni na baadaye uchaguzi ambao utafanyika Januari 13 2019.

Kalulumila:Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0
 BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO KALULUMILA.
----------------------------------------
Ni dawa pekee iliyojipatia umaarufu nchini na nje ya nchi kwa kufanya kazi mara 3, kwa wakati mmoja 1, kurefusha uume na kunenepesha saizi uipendayo kuongeza nguvu za kiume na inatibu matatizo na gerentii miaka 30. Na kuendelea haina madhara, inaimarisha mishipa ya uume iliyoregea na udhalishaji wa mbegu za kiume. 


---------NINI HUCHANGIA MATATIZO HAYA--Ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya ili kujua kwamba una ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya, ili kujua kama unangiri dalili zake ni kufika haraka kileleni wakati wa tendo la ndoa, 2)kushindwa kurudia tendo la ndoa. 3)kutoa choo kama cha mbuzi. 4)tumbo kujaa gesi na kuunguruma. 5)kukosa choo kabisa. 6)maumbile kuingia ndani na kuwa mafupi. 7) korodani moja kuvimba 8)kutosikia hamu ya tendo la ndoa na maumivu ya kiuno wakati wa tendo la ndoa. 9)maumivu ya kiuno na mgongo pia tunatibu kisukari kwa siku7, presha, busha, bila kupasuliwa na magonjwa mbalimbali. 

---------------------------------------
TUPO TEGETA KWA NDEVU KARIBU NA MACHINJIO YA NGOMBE UTAONA OFSI IMEANDIKWA KALULUMILA HERBALIST CLINIC HOSPITAL SIMU .
----------------------------------------
-0655-557-182.
-0755-557182.
-0784-557-182.
PIA UTAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO.
---------------------------------------
KARIBUNI SANA.
----------------------------------------

Je Wewe ni Mwanasiasa, Mfanyabiashara.?...... Tunazo dawa na PETE za bahati Zenye Uwezo wa Kubadili Maisha Yako

$
0
0

Je Wewe ni Mwanasiasa, Mfanyabiashara, Msanii wa Maigizo, Mwanamziki, ama mwanafunzi tunazo Dawa na PETE za Bahati zenye uwezo mkubwa wa kuyabadilisha maisha yako nakukupatia mafanikio makubwa ndani ya mda mfupi tu.

Kutana na Sheikh Jumaa Bilal. Yeye ni mtaalam na mtabibu wa nyota za binadam na bingwa wa tiba za asili Afrika mashariki. 

Wasiliana na mtaalam huyu kwani yeye ufaulu pale wote waliko shindwa na pia humaliza kazi zilizo shindikana ama zilizo achwa ndani ya siku1 tu. Sheikh Jumaa Bilal ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOASHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA-  Sheikh Sasa amezianza ziara zake za mikoani na atayatembelea maeneo mbali mbali ndani na Nje ya nchi.

Anatibu magonjwa sugu yanaojulikana nayasiojulikana kwakutumia QUR_AN MAJI , KIOO MAJINI NA MITISHAMBA.

Anazo dawa za mapenzi( Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu LIMBWATA) kumrudishaa alipote, kutoa Mikosi, Kutatuwa shida za chumaulete, mvuto wa biashara na sehem za kazi, kusafisha nyota, kurudisha mali zilizo ibiwa, zilizpotea, ama zilizodhulumiwa, kushika wezi na wachawi, Kutoa kinga ya mwili, nyumba, Biashara, kufukuza majini wabaya, KUUZA kwa haraka (shamba, NYUMBA, GARI..), Kuweka Zindiko ya mwili, nyumba, shamba, Gari, kupata Kazi na kupandishwa cheo, mali na UTAJIRI bila masharti na mengine mengi ya Siri. (Anazo Pia Pochi zisizo kwisha Hela MAGIC WALLET)

*{لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أيْمَانِكُمْ وَلَٰكِنْ يُؤَاخِذُكُمْ بِمَا عَقَّدْتُمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِمَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ }* ﴿٨٩﴾

✨Wabillahhi Tawfiq Asallam  Alaikum

Kwa tiba na ushauri wasiliana na ofisi kwa
nambari ya simu

+255 688 745 790
+255 672 861 042
Whatsapp :  0762 252 102

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala- Dar

Video: Alikiba Alivyoisimamisha Kahama Kwa Show Kali

$
0
0
Usiku wa kuamkia leo msanii Alikiba na wasanii wa lebo yake ya Kings Music walifanya show ya nguvu wilayani Kahama. Tazama hapo chini

Full Video: Tazama Hapa Wasafi Festival Walivyoitikisa Mtwara

$
0
0
Usiku wa kuamkia leo ndipo kumefanyika tamasha la Wasafi Festival mkoani Mtwara. Tazama wasanii wote wakali waliopanda kwenye jukwaa hilo na kutoa burudani ya aina yake.

Ajali ya Mashua yaua Watu 30 Ziwa Victoria Uganda

$
0
0
Watu 30 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 40 wameokolewa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama jana Jumamosi Novemba 24, 2018 katika Ziwa Victoria nchini Uganda.

Hata hivyo, polisi nchini Uganda wamesema kuna uwezekano idadi hiyo ikaongezeka hasa kutokana na idadi ya abiria waliokuwemo kwenye boti hiyo kutojulikana.

Msemaji wa polisi nchini humo, Emilian Kayima amesema kikosi cha uokoaji kinaendelea na operesheni ya uokoaji

Amesema hadi sasa haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa boti hiyo.

Boti hiyo iliyokuwa na watu waliokuwa wanakwenda kwenye sherehe ilipata ajali katika kaunti ndogo ya Mpatta wilaya ya Mukono.

Dar yaburuzwa Tena na Dodoma Makusanyo ya Kodi

$
0
0
Katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/19, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeongoza katika ukusanyaji mapato ya ndani, ikiendelea kuliacha mbali Jiji la Dar es salaam na baadhi ya majiji mengine ya mwanzo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo alipokuwa akitoa ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa robo ya kwanza ya mwaka, ambapo amesema Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeongoza kwa kukusanya mapato ghafi ya Sh bilioni 14.49 kati ya makisiso ya kukusanya Sh bilioni 68.6 ambayo ni sawa na asilimia 21.

Aidha, Arusha inaongoza kwa kukusanya vizuri kiasilimia na imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 4.1 kwa asilimia 26 ya malengo waliyojiwekea ya kukusanya Sh bilioni 15.6.

“Ieleweke wazi kuwa Jiji la Arusha ndio lililofanya vizuri kimakusanyo kwa mujibu wa asilimia lakini Jiji la Dodoma ndio lililokusanya fedha nyingi zaidi kuliko halmashauri zote Tanzania,” amesema.

Kwa mwaka wa fedha 2018/19, halmashauri zilipangiwa kukusanya Sh bilioni 735.6 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani na hadi kufikia Septemba 30, mwaka huu, halmashauri zimekusanya jumla ya Sh bilioni 143.6 sawa na asilimia 20 ya makisio ya mwaka.

Jafo alisema mwaka wa fedha 2017/18, halmashuri zilipangiwa kukusanya Sh bilioni 687.3 na hadi Septemba 30, mwaka 2017, ziliweza kukusanya Sh bilioni 126.8 sawa asilimia 18 ya makisio ya mwaka.

"Kutokana na takwimu hizo, inaonyesha Halmashuri zimeongeza wingi wa mapato kwa Sh bilioni 16.7 na ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani umeongezeka kwa asilimia mbili, uchambuzi wa mapato ya ndani ya robo mwaka ya mwaka wa fedha 2018/2019, unaonesha kuwa halmashauri 76 zimefanya vizuri kwa kukusanya zaidi ya asilimia 20 ya makisio yake ya mwaka," ameongeza.

“Kati ya halmashauri hizo Majiji ni manne, zikiongozwa na Arusha, manispaa saba zikiongozwa na ya Musoma, miji 12 ikiongozwa na mji wa Mbinga na Wilaya 53 zikiongozwa na wilaya ya Kisarawe.”
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images