Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wema Sepetu Amwanika Mume Wake Mtarajiwa

$
0
0
Msanii wa Bongo Movie na aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu ameamua kumwanika hadharani  mume wake mtarajiwa kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Wema ameposti picha hiyo na mwanaume mmoja ambaye hakuweza kutambulika kwa haraka ingawa sura yake inaonekana,picha hiyo inaonekana kabisa Wema na mwanaume huyo wako kitandani wamelala ingawa mpiga picha ni Wema mwenyewe akipiga Selfie.

Wema Sepetu amefanikiwa kuwa kwenye mahusiano tofauti tofauti lakini hakuweza kudumu nao licha ya wengi kuonekana kama walikuwa na mahusiano ya kweli


Vigogo ACACIA Wafikishwa Mahakamani Wakikabiliwa na Mashitaka 39

$
0
0
Aliyekuwa makamu wa rais wa kampuni ya Acacia, Deo Mwanyika na Alex Lugendo ambaye ni mshauri wa Serikali ndani ya kampuni hiyo, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji fedha, kughushi na kula njama.

Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao leo mbele ya Hakimu  Mkazi  Mfawidhi,  Kevin Mhina na Jopo la mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili  wa  serikali  Mkuu,  Faraja  Nchimbi  akisaidiana na Wakili wa serikali Mwandamizi,  Shadrack  Kimaro na Jackilline Nyantori.

Mbali na Mwanyika na Lugendo, washtakiwa wengine ni kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama 3, mashtaka yakughushi 7. Utakatishaji wa fedha 17, Kuwasilisha nyaraka  za uongo  kwa  Mamlaka ya Mapato Tanzanian (TRA), shtaka moja, kuongoza uhalifu wa kupangwa shtaka moja, kukwepa kodi, mashtaka 8 na shtaka moja la kutoa Rushwa.
 
Akisoma hati ya mashtaka wakili Nchimbi amedai washtakiwa hao pamoja na watu wengine ambao bado hawajakamatwa, walitenda makosa hayo kati ya Aprili 11.2008 na June 30.2007 katika sehemu tofauti za jiji la dar es Salaam, Kahama Mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini  Uingereza.

Imedaiwa katika kipindi hicho na mahali huko washtakiwa hao kwa pamoja wakiwa na watu wengine ambao bado hawajakamatwa walikula njama ya ya kutenda makosa ya kughushi na ukwepaji wa Kodi.

Pia mshtakiwa Mwanyika (56), na Lugendo (46), wanadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.

 Aidha washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Mei 16.2008 na Desemba 31,2008 huko Kahama na Biaramulo, walitoa tamko la uongo kwa kamishna Generali wa TRA kwa nia ya kukwepa kodi kulipa USD 9,309,600 ambayo ilikuwa ni kodi iliyopaswa kulipwa kwa TRA.

Katika mashtaka ya utakatishaji, washtakiwa Mwanyika na Lugendo wanadaiwa kati ya Desemba 2009 na Desemba 31 2018 katika maeneo tofauti ndani na nje ya nchi ya Tanzania kwa pamoja na wengine ambao hawapo mahakamani, walisaidia mgodi wa North Mara kuhamisha fedha kiasi cha USD 374,243,943,45 huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la makosa ya kughushi na kukwepa kodi.

Pia washtakiwa wanadaiwa kati ya Novemba 2. 2012 na Novemba 27. 2015 huko Shinyanga walitoa Rushwa ya sh. 718,520,001.76 kwa Hussein Kashindye ambaye  ni mkuu wa upelelezi makosa ya jinai wa Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kumshawishi ili aweze kuachana na uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyokuwa yametendwa na Mgodi wa Bulyanhulu.

Katika shtaka la kughushi washtakiwa hao wakiwa na nia ya ulaghai waligushi mkataba wa mkopo wakitaka kuonyesha kwamba Aprili 30.2014 Kampuni ya Pangea limited ilikubali kukopa USD 90,000,000 ikiwa na riba Kutoka benki ya kimataifa ya barrick huku wakijua kuwa siyo kweli.

Katika shtaka la kutoa nyaraka ya uongo, mshtakiwa Mwanyika anadaiwa Aprili 30.2018 huko BOT iliyopo wilaya ya ilala, kwa makusudi aliwasilisha  nyaraka ya uongo ya mkopo baina ya kampuni mgodi wa Bulyanhulu na Barrick international bank Corp kwa madhumuni ya kuonesha kuwa, kati ya June 2001 na Desemba 13.2007 Bulyanhulu walijipatia mkopo usio na faida wa USD 416,100,000 kutoka Barrick.

 Hata hivyo wa washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Na kesi itatajwa tena Oktoba 31, mwaka huu.

Hatima ya Kubenea na Komu Baada ya Kikao Cha Kamati Kuu CHADEMA Kumalizika

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kesho Alhamisi kinatarajia kutoa hatma ya wabunge wake wawili Saed Kubenea wa jimbo la Ubungo pamoja na Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini, Antony Komu kufuatia wabunge hao kudaiwa kupanga njama za kumdhuru moja ya mwanachama mwenzao.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya nje wa CHADEMA, John Mrema hatma ya wabunge hao inatarajia kujulikana kesho kufuatia kikao cha dharura cha wajumbe wa kamati kuu wa chama hicho walioketi hii leo wakiongozwa na Mwenyekiti wake wa taifa, Freeman Mbowe.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, John Mrema amesema ;“kamati kuu imeitishwa na tukawaita wabunge hao wawili, tumeshamaliza kumhoji mheshimiwa, Antony Komu na sasa tunaendelea na mahojiano na mheshimiwa Kubenea”

 “Kwa kuzingatia  mamlaka ya nidhamu ya kamati kuu kwenye chama chetu, tutapata wasaa wa kuwaita waandishi wa habari ili kuzungumza na kwa mwenendo unavyokwenda maamuzi hayo yatatolewa kesho kwa maana kikao kinaweza kumalizika usiku”, ameongeza John Mrema

 Hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, ilisambaa sauti fupi ikimuhusisha mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea pamoja na Mbunge wa Moshi Vijijini Antony Komu  wakipanga njama ya kumzuru Meya wa Manispaa ya Ubungo, Borniface Jakob.

LHRC Wapinga Matumizi ya neno "HUO NI UMAMA" Kwa Madai Kwamba Linawadhalilisha Wanawake

$
0
0
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimepinga vikali matumizi ya neno 'umama' katika mitandao ya kijamii kwa kile kilichodaiwa kuwa ni ubaguzi na udhalilishaji.

Tamko lililotolewa na kituo hicho limesema kuwa kwa kufanya hivyo neno hilo linahalalisha kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu, kwani mambo yanayofanywa na wanaume hata wanawake wanaweza kufanya pia.

"Mfano kuna hii sentensi, 'mwanaume kulea mtoto ni umama, mwanaume ni kubebesha mimba' kitu ambacho kinalenga ni udhalilishaji hivyo basi, kwa pamoja tuwajibike kupinga udhalilishaji kwa wanawake", imesema taarifa hiyo.

Neno 'umama' limeibuka siku za hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, likijikita katika kuelezea namna ambavyo mwanaume anatakiwa kufanya vitu tofauti na wanawake kwa kutaja baadhi ya vitu ambavyo wanawake hawapaswi kuvifanya, jambo ambalo halina ukweli wowote.

Mbali na LHRC, mwingine ambaye amepingana na matumizi ya neno hilo ni Wakili msomi, Albert Msando ambaye alionesha kukerwa na msemo huo na kuandika maneno haya katika ukurasa wake wa Instagram,

"Aliyeanzisha huu utani (meme) wa ‘umama’ na wanaondelea nao nadhani wanasahau kwamba kama sio mama zetu basi tusingekuwa hapa tulipo. Ni upuuzi ni sentensi ambayo inamdhalilisha mwanamke. Kabla hujatunga sentensi na kutaka iwe ‘meme’ basi jiulize kama unaona aibu mama yako kuwa mama, utani huu unaonyesha ni jinsi gani bado ‘wanaume’ wanajiona wao ni bora kuliko wanawake".

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe na Wenzake Kortini Kwa Matumizi Mabaya Madaraka...Mgawe Kakosa Dhamana

$
0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe na wenzake watatu, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu kesi ya uhujumu uchumi.

Mgawe na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh.984.8 Milioni .

Pamoja na Mgawe, washtakiwa wengine ni Wajumbe wa Bodi ya Manunuzi ya TPA, Happiness Senkoro, Apolonia Mosha na Theophil Kimaro ambao kwa pamoja wamesomewa mashtaka yao, mbele ya Hakimu Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Akiwasomea hati ya mashtaka leo Jumatano Oktoba 17, 2018, wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita amedai Septemba 28, 2010 katika ofisi za TPA zilizopo Ilala, Dar es Salaam, Mgawe akiwa mtumishi wa umma kama Mkurugenzi Mkuu na ofisa masulufu, alitumia madaraka yake vibaya.

Amesema alishuhudia mikataba kati ya mamlaka hiyo na Kampuni ya Leighton Offshore Pte Ltd 19800397 na kupata faida ya Sh984,828,000 baada ya kuvunja sheria ya manunuzi kwa kuiwezesha kampuni hiyo kupata upendeleo.

Mwita amedai katika shtaka la pili la matumizi mabaya ya madaraka linalowakabili mshtakiwa wa pili, tatu na wa nne,  alidai kuwa Julai 13, 2010 katika ofisi ya TPA washtakiwa wakiwa watumishi wa umma na wajumbe wa bodi ya manunuzi, walitumia vibaya madaraka kwa kuidhinisha zabuni na kuvunja sheria ya manunuzi ya umma kwa kuiwezesha Kampuni ya Leighton Offshore Pte Ltd kupata faida ya Sh984,828,000.

Katika shtaka la tatu linalowakabili washtakiwa wote, inadaiwa kati ya Julai 13, 2010 na Juni 30, 2016 katika ofisi za mamlaka hiyo, washtakiwa wote wanne waliisababishia TPA  hasara ya Sh984,828,000.

Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili, walikana  mashtaka hayo.

Upande wa Jamhuri umedai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo uliomba tarehe ya kutajwa kwa ajili ya kupanga tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali.

Mwita amedai upande wa mashtaka hauna pingamizi la dhamana.

Hakimu Mashauri amewataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminiwa wenye barua na nakala za vitambulisho vya uraia watakaotia saini hati ya dhamana ya Sh15milioni.

Pia,  amewataka washtakiwa wawasilishe Sh100milioni taslimu au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo ya fedha.

Hata hivyo, mshtakiwa wa pili na wa tatu walitimiza masharti ya dhamana huku Mgawe na mshitakiwa wanne wakipelekwa mahabusu hadi Oktoba 31, 2018 kesi itakapokuja kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao.

Video Mpya: Chin Bees - Inogire

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Chin Bees anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya uitwao Inogire. Itazame hapa.

Amber Lulu Awatolea Povu Zito Wanaodai Ana Sura Mbaya!

$
0
0
Amber Lulu ameamua kuwatolewa uvivu wale wote wanaomsema vibaya kuhusiana na muonekano wake.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa ingawa anasemwa kuwa ana muonekano mbaya ila akijiremba basi anapendeza. Kupitia ukurasa wake Instagram ameandika;

"Raha kujivunia ulicho nacho ???? sura langu bayaa lakin make up inakaa nalipenda sura langu unanita sura mbaya wakati me ndo Mamakoo.
 
"Rafiki mzuri ni yule anaye kuface private na kukwambia ukweli pasipo kutaka sifa or kusema pembeni kama kweli anania ya kukushauli au kukuelewesha lakini life goes on tunashaish nao." ameeeleza  Amber Lulu.

Kwa sasa Amber Lulu ambaye alijizolea umaarufu mkubwa alipokuwa video vixen, anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Vuruga.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya October 18


Alichoandika Nay wa Mitego baada ya Kuitwa Tena BASATA

$
0
0
Hapo jana October 17, 2018 msanii Nay wa Mitego alifika kuchukua barua Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).

Bado  Nay hajaweka wazi kile kilichopo ndani ya barua ile ametumia ukurasa wake wa Instagram kueleza hisia zake mara baada ya kutoka Basata, Nay ameandika;

"Unaweza fungwa kila kitu, mikono, mdomo, miguu, kazi na kila kitu but huwezi funga mitazamo na akili za mtu. Itafungwa kwasasa ila muda ukitimia hakuna kitacho shindikana," ameeleza.

Kwa sasa Nay wa Mitego anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Alisema ambao ndio unatajwa kupelekea msanii huyo kuitwa Basata mara mbili ndani ya wiki mbili.

Kwanini Wanawaume Wenye Pesa Za Kichawi Huwa Wanatumia Pesa Nyingi Sana Kuwahonga Wanawake Zao?

$
0
0
DOKTA  MUNGWA  KABILI  : 0744  000  473.
Je  Mwanaume  Mwenye  Pesa  Za  Kichawi  Anaweza  Kutumia  Uchawi  Huo  Huo  Kumroga  Mwanamke  Kimapenzi  ? 
Kama  Jibu  Ni  Ndio  Kwanini  Basi  Wanawaume  Wenye  Pesa  Za Kichawi  Huwa  Wanatumia  Pesa  Nyingi  Sana  Kuwahonga  Wanawake  Zao ?, Kwanini  Wasitumie  Tu  Uchawi  Wa Mapenzi Ili  Kujiepusha  Na  Gharama  Za  Kutumia Pesa  Nyingi  Kwa  Kitu  Ambacho  Uchawi  Unaweza  Kufanya.?

Hili  ni  swali  nililo  ulizwa  na   kijana  mmoja  ambae  amejitambulisha  kama  msomaji  mzuri  wa  makala  zangu.

YAFUATAYO  NDIO  MAJIBU  YANGU :
Kwanza  kabla  ya yote  unatakiwa  ujue  mwanaume  huyo  ambae  unasema  ana  pesa  za  kichawi  amezipata  kwa  kutumia  tambiko  la  aina  gani.

Na  hii  ni  kwa sababu  matambiko  ya  biashara  na  mali yamegawanyika  katika  aina  kuu  mbili.

Aina  ya  kwanza  ni  matambiko  yanayo  julikana  kama  MATAMBIKO  BARIDI  na  aina  ya  pili  ni  matambiko  yanayo julikana  kama  MATAMBIKO  YA  MOTO.

Linapokuja  suala  la  matumizi  ya  pesa  kwa  wanawake, ni  vigumu  sana  kwa  mtu  asie  na  jicho la  tatu  kutofautisha  baina  ya  mwanaume  anae  tumia   matambiko  baridi  katika  biashara  zake na  mwanaume  anae tumia  matambiko  ya  moto  katika  biashara  zake  kwa  sababu  wote  huwa  wanatoa  pesa  nyingi  sana  kwa  wanawake.

TOFAUTI  NI  HII  HAPA CHINI
MWANAUME   ANAE  FANYA  BIASHARA  ZAKE  KWA  KUTUMIA  MATAMBIKO  BARIDI.

Mwanaume  ambae  anafanya  biashara  zake  kwa  kutumia  matambiko  baridi  hutoa  pesa  nyingi  kwa  mwanamke  kwa  lengo  la  kuitumia  nyota  ya  mwanamke  huyo  katika  biashara na  shughuli  zake  zote  za  kumuingizia  riziki na kipato.

Ni  hivi  katika  ulimwengu  usio  onekana, ukitaka  kuchukua  nyota  ya mtu  kwa  njia  rahisi  kabisa, ni  kumfanya  mtu  huyo  akutegemee  wewe  kwa  kila  kitu  hususani  katika  masuala  yote  yanayo  husu  pesa  na rizki kwa  ujumla.

 Ukifanikiwa  kumfanya  mtu  yoyote  Yule  akutegemee  wewe  kwa  kila  kitu, kuanzia  kula  chakula, kuvaa,  na  mambo  yote  muhimu katika  maisha  hasa  hasa  yale  yanayo  husu  rizki  basi  unakuwa  umeichukua  nyota  yake  na  matokeo  yake  milango  yake  yote  ya kuingiza  rizki  inahamia  kwako.

Riziki  yake  inakuwa  inapitia  kwako. Mlango wake  wa  kuingizia  riziki  unahamia  kwako.  Mtu huyo  anakuwa  hawezi  kupata  pesa yoyote  ile  bila  pesa  hiyo kupitia  kwenye  mikono  yako.

 Ili  mtu  huyo  apate  rizki  yoyote  ni  lazima  rizki  hiyo  ipitie  kwanza  kwako.

 Kwa hiyo  mwanaume  huyu  anapokuwa  anakupa  wewe  mwanamke  pesa  nyingi  maana  yake  ni  kwamba  anakupa  pesa  zako  mwenyewe.

Kama  nilivyo dokeza  hapo  juu  kwamba  njia  hii  ni  njia  ya  halali  kabisa   kwa  sababu  wote  mnafaidika .

Anaeitumia  nyota  yako  anafaidika  na  wewe  ambae  nyota  yako  inatumika  unafaidika  pia.

 Kwa  lugha  nyepesi  mwanaume huyo  anakuwa  anasafiria  nyota  yako.

Ndio  maana  sharti  kuu  la  kutumia  njia  hii  ni lazima  umtunze  vizuri  mtu  ambae  anakutegemea  wewe  kwa  kila  kitu.

Kadri  unavyo  mtunza  vizuri  na  kumpa mahitaji  yake  muhimu  ndivyo  mambo  yako  katika  biashara  na  shughuli  zako  yatakavyo  kuwa  yanakunyookea.

Hii  ni  njia  ya  asili  na  ya  halali  kabisa, hata  wewe  unaesoma  makala  haya  unaweza  kuwa  unasafiria  nyota  za  watu  wengine  bila  wewe  mwenyewe  kujua  wala  bila  wao  wenyewe  kujua.

Kwa  mfano  kama  una  watu  wanao  kutegemea  wewe  kwa  kila  kitu  kama  vile  mke, watoto, au  wazazi  na  wewe  unajitahidi  kuwatunza  na  kuwapa  mahitaji  yao  ya  muhimu  basi milango  yao  ya  rizki  inahmia  kwako  na  rizki  yako  inakuwa  kubwa  na  wala  unakuwa  hauwezi  kuishiwa  kabisa.

Ni rahisi  kwa mwanaume  ambae  hana kabisa  watu  wanao  mtegemea  kuishiwa  na  kukosa  hata  hela  ya  kula  lakini  mwanaume  mwenye  wategemezi  kama  vile  watoto.   Ndio  maana  hata  kwenye  mabar  na  sehemu  za  starehe  wanaume  walio  kwenye  ndoa  ndio  wanao  ongoza  kwa  kutoa  ofa  za  pombe  kuliko  ambao  hawana  wategemezi.

Kama  una  nafasi  unashauriwa  usiishie  kuwatunza  watoto, mke  na  wazazi  wako  tu , jaribu  kutafuta  na  watu  wengine  ambao  unaamini  wana  mahitaji  maalumu  katika  maisha  lakini  hawana  watu  wa  kuwasaidia.

 Kwa   mfano  watoto  yatima.  Unaweza  kwenda  kwenye  kituo  cha  watoto  yatima  ukachukua mtoto  mmoja au  wawili  kwa kadri   Mwenyezi  Mungu  alivyo  kujaalia  na  kwenda  kuishi  nao  nyumbani  kwako  au  kama  nyumbani  kwako  hauna  nafasi  ya  kuwaweka  basi  uwe  unawapelekea  mahitaji  yao  hapo  hapo  kituoni  kwao.

Hii  ni  njia  rahisi  sana  na  ya  uhakika  ya  kufungua  na  kuongeza  milango  ya rizki.

 Ni  njia  mujarab  sana  na  watu  walio  tumia  njia  hii  wamepata  mafanikio  makubwa  sana  katika  shughuli  zao  zinazo  husisha  vipato  vyao.

MWANAUME  ANAE  FANYA  BIASHARA  ZAKE  KWA  KUTUMIA  MATAMBIKO  YA  MOTO

Mwanaume huyu  anakupa  pesa  nyingi  sana  wewe  mwanamke  kwa  sababu  pesa  zake  ni pesa  za  kichawi  ambazo hazina  thamani.Chenye  thamani  ni  nyota  yako.

Kwanza  kabla  ya  kuanza  kukupa  pesa  zake, anaanza  kwanza  kwa  kuimiliki  nyota  yako  kichawi.

Na  anapata  uhalali  wa  kiroho  wa  kumiliki  nyota  yako  baada  ya  kutoa sadaka  maalumu  kwa  ajili  ya  kumiliki  nyota  yako.

Mwanaume  huyu  anakuwa  anaitumia  nyota  yako  katika  shughuli  zake  na anakuwa  anapata  pesa  nyingi  sana  kupitia  nyota  yako.

Pesa  anazo  kupa  wewe  ni  pesa za kichawi  ambazo  anakuwa  amezipata  kwa  kufanya  matambiko  ya  moto.

Ni  pesa  ambazo  zina  thamani  tu  katika  ulimwengu  wa  rohoni  lakini  hazina  thamani  katika  ulimwengu  wa  nyama.

Ili  pesa  hizo  ziwe na  thamani  ni  lazima atafute  mtu   mwenye  pesa  zenye  thamani  katika  ulimwengu  wa  nyama kwa  ajili  ya  kubadilishana  nae.

Mtu  huyo  ni  wewe  kwa  sababu  nyota  yako  ina  utajiri  mkubwa.

Kwa  hiyo  anacho  kifanya  hapo  anakuwa  anakupa  pesa  zake  za  kichawi  ambazo  hazina  thamani kwa  kubadilishana  na  nyota  yako  ambayo  thamani  yake  ni mara  elfu   zaidi  ya  pesa  anazo  kupa.

Hii  haina  tofauti  na  uchawi  wa  chuma  ulete. Wachawi  wanao  chukua  pesa  za  watu  kwa  chuma  ulete  huwa  wanakuwaga  na  pesa  za  kichawi  pia  ambazo  hazina  thamani  katika  ulimwengu  wa  nyama.

Ili  pesa ziwe  na thamani  ni   lazima  wazibadilishe  na  mtu  mwenye  pesa  zenye  thamani  katika  ulimwengu  wa  nyama.

 Ndio  maana   mtu  wa  chuma  ulete  akikupa  pesa  yake  ukamrudishia  chenji. Hiyo  chenji  uliyo  mrudishia  ndio  yenye  thamani  na  sio  ile  aliyo  kupa.

KUHUSU   WANAUME  WENYE  PESA  ZA  KICHAWI  KUWAROGA  KIMAPENZI   WANAWAKE.

Kwa  kawaida  mwanaume  mwenye  pesa  haitaji  kutumia  uchawi  kumroga   mapenzi  mwanamke.Uchawi  wanao  weza  kuutumia  wanaume  hawa  ni  kumfunga  mwanamke  asiende  kwa  mtu  mwingine  kwa  sababu  za  kinyota.

 Hataki  nyota  ya  mwanamke  wake ichafuliwe  kwa  sababu tendo la  kujamiiana ni  moja  kati  ya  mambo  makuu  yanayo  chafua  nyota  za  watu  kwa  kiasi  kikubwa  sana.

Kwa  hivyo  mwanaume  huyu  hatumii  uchawi  wa  jamii  ya  limbwata  katika  kumroga  mapenzi  mwanamke  isipikuwa  atamfunga  tu  kichawi  mwanamke  huyo  asiwe  na  mwanaume  mwingine  kwa  sababu  za  kinyota.

Hata  hivyo  yapo  mazingira  yanayo  walazimisha  wanaume  hawa  kuwaroga  mapenzi  wanawake  wanao  wataka  .Hasa  hasa  pale  anapo  gundua  mwanamke  Fulani  ana  nyota  kali  ya  biashara, mali  na  utajiri.

Mwanaume  anae  fanya  biashara  zake  kwa kutumia  uchawi  akigundua  kuna  mwanamke  ana  nyota  kali  ya  biashara, mali na utajiri  basi  atafanya  juu  chini  kumpata  mwanamke  huyo  hata  kama  ni  mke  wa  mtu.

Hata  kama  mwanamke  huyo  yupo  kwenye  ndoa  na  mumewe  na  wana  watoto  zaidi  ya  mmoja, mwanaume   mwenye    kutafuta  pesa  kichawi  atafanya  juu  chini  ampate  mwanamke  huyo.

Na  hii  ni  moja  kati  ya  sababu  ya  ndoa  nyingi  sana  kuvunjika  siku hizi  licha  ya  kuwa  wanandoa  mmepata  watoto  na  watoto  wenyewe  bado  wadogo.

Kinacho  tokea  mwanaume  huyu  akigundua  kuwa  mwanamke  Fulani  ana  nyota  kubwa  ataanza  kwa  kutumia  njia  zake  zote  za  kawaida  ili  kumnasa  kimapenzi  mwanamke  huyo  kama  vile  kutoa  pesa, zawadi  kubwa  kubwa  na  kadhalika.

Mwanamke  huyu  akiweka  ngumu  licha  ya  jamaa  kutumia  njia  zake  zote ikiwemo  pesa  kushindikana, basi  ndipo  mwanaume  huyu  huamua  kutumia  uchawi  sasa.

Hii ni njia  inayo  fanywa  hata  na  wachawi  katika  shughuli  zao  za  kichawi.

 Wachawi   wakitaka  kufanya  misheni  yao  ya  kichawi  huwa  wanaanza  kwanza  kwa  kutumia  njia  za  kawaida.  Njia  za  kawaida  zikishindwa  ndipo  sasa  hutumia  uchawi.

Kwa  mfano  A  na  B ni  mke  na  mume  wanao  pendana  sana  na  wanafanya  shughuli zao  na  zinawaendea  vizuri.  Wachawi   hawapendi  kuwaona  A  na  B  wakiwa pamoja  kwa  upendo .

Watakacho  kifanya  wachawi  hao  ni  kuanza  kupeleka  maneno  ya  umbea  kwa  A  na  B  ili  kuwagombanisha.

Maneno ya  umbea yakigonga  mwamba  sasa  ndio  wachawi  hao  huamua  KUPELEKA  MAJESHI.  Kupeleka  majeshi  maana  yake  ni kufanya  uamuzi  wa  kutumia  silaha  za  kichawi  kukamilisha  misheni  yao  na  uamuzi  huu  ukishafikiwaga  huwa  haubatilishwi.

Vivyo  hivyo  mwanaume  huyu  anapokutana  na  mwanamke  mwenye  nyota  ya  mali  huanza  kumtongoza  kwa  kutumia  njia  za  kawaida  na  njia  za  kawaida  zikishindikana  basi  ndio  hutumia  uchawi.

Wakati  mwingine  mwanamke  huyu  kwa  sababu  anakua  anampenda  mume  wake  na  ndoa yake  na  hataki  kuwasumbua  watoto  wake  anaweza  kumkubalia  mwanaume  huyo  kama  mchepuko, lakini  lengo  la  mwanaume huwa  ni  mwanamke  huyo  awe  wake  peke  yake.

Kwa  hiyo  hata  baada  ya  kuwa  katika  mahusiano  na  mwanamke  huyo, mwanaume  huyo  ataendelea  kumshawishi  mwanamke  huyo  aachane  na  mume  wake.

Juhudi  za  kumshawishi  mwanamke  huyo kwa  njia  ya  kawaida  zikishindikana  basi  ndipo  mwanaume  huyo  huamua  kutumia  uchawi  wa  kuwatenganisha  mwanamke  huyo  na  mume  wake  na  yeye  mwanaume  kumchukua  mke na kwenda  kuishi nae.

Mwanaume  aliye  kimbiwa  na  mkewe  katika  mazingira  haya  anaweza  kujiona  hana  thamani  na  kwa  kudhani  labda  ana  kasoro  kumbe  kilicho tokea  ni  kitu  kingine  kabisa  ambacho hata  mke  wake  akijui.

Ushauri  wangu  ukiwa  na  mkeo  hakikisha  unamtunza  na  kumuhudumia  kwa  kila  kitu  bila  kujali  na  yeye  ana  kazi  au  lah.

Wazee  wetu  walikuwaga  na  msemo  wao  mzuri  sana  ambao vijana  wa  siku hizi  wanautumia  vibaya.   Wazee walikuwa  na  msemo  usemao  “ Mwanamke  ni  kama  mtoto “  sasa bahati  mbaya  vijana  wa  siku  hizi  msemo  huu  wanauchukulia  kumaanisha  kwamba  mwanamke  ana  akili  kama  za  mtoto.

Watu  wenye  mtazamo  huu  wanakosea  sana . Wazee  waliposema  wanawake  ni  kama  watoto  walimaanisha  kitu  kimoja tu, nacho  ni  MATUNZO.

Mtoto  wako  hatakiwi  kuwaza  atakula  nini  au  atavaa  nini,  mtoto  wako  akiumwa  atakacho  kiwaza  ni  uchungu  wa   dawa  au  maumivu  ya  sindano  na  sio  kwamba  atapata  dawa  au  la.

Vivyo  hivyo  mke  wako  au  mwanamke  wako  hatakiwi  kuwaza  atakula  nini  au  atavaa  nini nakadhalika.

 Wewe  unatakiwa  kuwaza  kwa  ajili  yake  na  ni  lazima  uwaze  kwa  ajili  yake  kwa  sababu  usipo  waza  kwa  ajili  yake  watatokea  wanaume  wengine  ambao  watawaza  kwa  ajili  yake na kuchukua  nafasi yako.

Asili  ya  wanawake  ni  kuishi  kwenye  utajiri  kwa  sababu  nyota  zao  ni  nyota  za  utajiri. Hivyo  ndivyo Mwenyezi  Mungu  alivyo  waumba. Hakuwaumba  wateseke.

Ndio  maana  HAWA  alimkuta  ADAMU  akiwa tayari   kwenye  bustani  ya  Edeni  ambayo  ndani  yake  kulikuwa  na  kila  kitu.  Katika  ulimwengu  usio  onekana  EDEN maana  yake  ni  utajiri.

Simaanishi  kwamba  kama  wewe  sio  tajiri  usioe  au  usiwe  na  mwanamke, hapana  namaanisha  unapokuwa  na  mwanamke  au  mke  jitume  fanya  kazi  kwa  bidii  na  umtunze  mkeo  kwa  kila  kitu, ukifanya  hivyo  basi   utachukua  nyota  yake na  wewe  pamoja  na  yeye  mtapata  mafanikio  makubwa  sana  kwa  sababu  wanawake  karibu  wote  wana  nyota  za  mali na  utajiri  na  wasio  kuwa  na  nyota  za  mali  na utajiri  ni  wale  ambao  nyota  zao  zimechafuliwa.  Katika  ulimwengu  usio  onekana, hapa  ndipo unapokuja  ule  msemo  “nyuma  ya  mafanikio  ya  kila mwanaume  kuna  mwanamke”.

Sura  ya  saba  ya   kitabu  changu  “ MAMBO  TISA  YANAYO  UNDA  NYOTA  YA  MWANADAMU:  UHUSIANO  KATI  YA  NYOTA   YA  MTU  NA  MAFANIKIO  YAKE  KATIKA  MAISHA   ina itwa  “ NAFASI  YA  NYOTA  YA  MWANAMKE  KATIKA  MAFANIKIO  YA  MUME  WAKE “.

Watu wengi  walio  pata  bahati  ya  kusoma  kitabu  changu  hicho  wameniomba sura  hiyo  niitolee  kitabu  chake yenyewe  na  nina  wa ahidi  kuyafanyia  kazi  maombi  yenu.

Nitakapo  kamilisha  kuandika  kitabu  hicho  basi  nitawatangazia ili  mpate  kujifunza  zaidi.

Kwa  ambao  hawakubahatika  kupata  nakala  za  kitabu  changu  mnaweza  walau  kusoma  maelezo  kuhusu  kitabu  hicho  kupitia  : http://mungwakabhili.blogspot.com/2018/06/mambo-tisa-yanayo-unda-nyota-ya.html

MAKALA  HAYA  YAMESIMULIWA  NA  DOKTA  MUNGWA  KABILI. DOKTA  MUNGWA  KABILI  ANAPATIKANA  KUPITIA  SIMU  NAMBA : 0744  000  473.

Baada ya Wema Sepetu Kumwanika Mume Wake Mtarajiwa.... Diamond , Idriss Wajibu Mapigo

$
0
0
Baada ya Mrembo Wema sepetu kumuanika hadharani mume wake mtarajiwa, Msanii Diamond Platnumz ambaye amewahi kutoka kimapenzi na Wema ameamua kujibu mapigo kwa kuposti picha yake na kujitangaza na yeye ni mume mtarajiwa, japo hajamtaja  mkewe mtarajiwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameandika; "Your Future Husband!!!!🙏🏻...au sifai?😋" .

Wema Sepetu  amewahi kuwa kwenye mahusiano na watu maarufu Bongo kama Diamond Platnumz, Idris Sultan, TID, Mr. Blue na wengineo.

Idriss Sultan yeye kaamua kumjibu Wema Kwa Kupost Mafuta ya kupaka ya Girl Friend akidai ndo "Future Wife Wake"

Maiti za Watoto Watatu Zakutwa Katika Gari Bovu Dar

$
0
0
Watoto  watatu wa familia moja wamekutwa wamefariki dunia ndani ya  gari bovu la Toyota Mark X.

Walitoweka tangu Oktoba 15, mwaka huu  katika Mtaa wa Njaro wilayani Temeke,  Dar es Salaam.

Miili ya watoto hao, Jamila Mohamed (9), Amina Kunambi (7) na Yusuph Selemani (2) ilipatikana jana saa 4.00 asubuhi,   ndani ya gari hiyo iliyokuwa imeegeshwa kwenye gereji ya Inshallah inayomilikiwa na raia   mwenye asili ya Asia.

Miili hiyo ilipatikana  baada ya babu yao anayefanya kazi katika gereji hiyo kuhisi harufu ya mzoga hali iliyomlazimu kufanya upekuzi.

Taarifa za tukio hilo zilianza kusambaa katika mitandao ya jamii jana asubuhi ikieleza kuwa watoto hao wa familia moja walionekana wakiwa wamefariki dunia baada ya kupotea kwa siku tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari, baba mdogo wa watoto wawili kati ya watoto hao, Kagoda Issa, alisema tukio hilo ni la kutatanisha kutokana na mazingira ya watoto hao kupotea na kupatikana kwao kughubikwa na utata.

Issa alihoji watoto hao waliwezaje kuingia katika gari hilo na kujifungia mlango kiasi cha kushindwa kutoka wakati gari hilo limeharibika kwa muda mrefu.

“Tunashindwa kuelewa waliingia vipi wakajifungia wakati hata mfumo wa milango ya gari umekufa na baadhi ya vifaa vimetolewa.

“Tunashindwa kujua kama ni kweli waliingia kucheza wenyewe au ni mtu kafanya mambo yake halafu kawatupia humu,” alisema Kagoda.

Baba mzazi wa Amina, aliyekuwa akiishi na watoto hao, Omary Thomas, alisema   watoto hao waliondoka nyumbani kwao Mtaa wa Njaro Wilaya ya Temeke saa 10:00 jioni Oktoba 15, mwaka huu kwenda kucheza.

Alisema watoto hao  hawakurejea nyumbani hadi miili yao ilipokutwa kwenye gari hilo jana asubuhi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alidai kuwa watoto hao walikwenda lindoni kwa babu yao ambako waliingia ndani ya gari na kujifungia hivyo wakashindwa kutoka baada ya milango kujifunga.

“Nikiri kupokea taarifa ya vifo vya watoto watatu wa familia moja.

“Siku ya Jumatatu mama yake na mmoja wa watoto waliofariki dunia yaani mama yake Amina Kimambi, alifika na kutoa taarifa polisi, tulipokea hiyo taarifa na tukawashauri warudi wajiridhishe ili baada ya saa 24 waje waandikshe maelezo.

“Kwa hiyo ufuatiliaji wa tukio hilo ulianza na leo saa tano kasoro tulipokea taarifa kuwa mlinzi wa ile gereji alipokuwa akikagua lindo lake alipofungua mlango wa moja ya gari lilizokuwa katika gereji hiyo alithibitisha kuwapo miili ya watoto hao,” alisema Mambosasa.

Kamanda alisema jeshi hilo linaendelea na upelelezi wa tukio hilo kubaini kama ni kweli watoto hao walifariki dunia baada ya kujifungia katika gari hilo.

Wizara Zakutana kujadili Kamera za kudhibiti Uhalifu

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, zimekutana kujadili ufungaji kamera maalumu za kudhibiti na kuzuia uhalifu.

Akizungumza wakati wa kikao hicho jana mjini hapa, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alisema serikali inatambua umuhimu wa ulinzi na usalama kwa raia wake na iko katika mpango wa kufunga kamera hizo katika miji yote mikuu nchini.

Masauni alisema lengo la kufunga kamera hizo ni kuiwezesha serikali kupambana na matukio ya uhalifu ya utekaji, makosa ya barabarani, uporaji wa fedha katika taasisi za fedha.

“Tumekuja kuchukua uzoefu kwa wenzetu wa Zanzibar ambao tayari wameshafunga kamera hizi katika maeneo mbalimbali na nimeona jinsi zinavyofanya kazi za kubaini wahalifu.

“Teknolojia haiepukiki katika kudhibiti, serikali tumejipanga na hivi karibuni tutaanza kufunga kamera za CCTV katika miji mikuu na maeneo ya mikoa iliyoko mipakani ili kudhibiti wahalifu kutoka nje ya Tanzania,” alisema.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub alisema tayari washafunga kamera hizo zilizozinduliwa Oktoba 3, mwaka huu.

Alisema uzinduzi wa kamera hizo ulifanywa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein. “Mfumo huo ni muhimu na tumehakikisha unaimarisha usalama katika mji wa Zanzibar ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa amani na salama na tayari ushaanza kufanya kazi katika maeneo mbalimbali hapa Zanzibar,” alisema.

Leo Ni Siku 7 Tangu Mo Dewji Atekwe...Hii Ni Kauli Mpya ya Haji Manara

$
0
0
Ikiwa zimetimia siku saba hii leo tangu mfanyabiashara maarufu barani Africa na mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ alipotekwa na watu wasiojulikana .

Afisa Habari wa klabu ya Simba ambaye alikamatwa siku ya pili baada ya tukio kutokea na kuachiwa siku chache baadaye baada ya kuhojiwa, ameendelea kumkumbuka Mo Dewji kwa kuandika mfululizo wa kauli mbalimbali zenye kuwafariji mashabiki na wanachama wake wa Simba.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram hii leo, Manara ameandika;” Wiki moja kamili imetimia toka tukio la kutekwa kwa kiongozi wetu litokee, MO kwangu mimi binafsi ni tukio baya sana toka nimeanza kazi Simba na moyo wangu bado umesinyaa, tuendelee kumuomba Mola apatikane akiwa mzima na salama.

“Naamini Dua na Sala zetu zitasikika na Insha'Allah kwa jitihada za vyombo vyetu na matakwa yake Mwenyezi, mambo yatakaa sawa." Ameandika Haji Manara

Katika jitihada za kumpata Mo Dewji, familia yake imetoa ofa ya kiasi cha Shilingi billioni 1 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa za ukweli za kupatikana kwake huku Jeshi la Polisi likiwashikilia watu saba mpaka sasa kwa mahojiano zaidi, baada ya kuwaachia kwa dhamana watu 19 mapema wiki hii akiwemo Haji Manara.

Bibi kizee wa miaka 85 abakwa na kijana wa miaka 21

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia     Charles Colner (21) kwa tuhuma za kumbaka ajuza   wa miaka 85  wilayani Rombo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita, alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 15   jioni katika Kijiji cha Kingachi, Kata ya Kingachi wilayani humo.

Alisema mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, alibakwa na kijana huyo baada ya kumvamia na kuvunja mlango wa nyumba yake.

Alisema baada ya kuvunja mlango  kijana huyo alimvuta nje mwanamke huyo na   kumfanyia kitendo hicho.

“Baada ya kuingia ndani alimvuta nje na baadaye alimlaza kando ya nyumba hiyo na  kumfanyia kitendo hicho,”  alisema.

Alisema baada ya kijana huyo kufanya kitendo hicho, alikimbia na raia wema walitoa taarifa polisi.

Baada ya msako mkali polisi waliweza kumkamata na kumfikisha katika Kituo cha Polisi Moshi, alisema.

“Kwa sasa tumemhifadhi na baada ya uchunguzi kukamilika tutamfikisha mahakamani  kujibu shitaka linalomkabili,”alisema Kamanda.

BREAKING: Komu, kubenea wavuliwa nafasi za uongozi Chadema

$
0
0
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imewavua nafasi zote za uongozi na kuwaweka chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu baada ya kukiri kuwa sauti zilisombaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita ni za kwao.

Sauti hizo ni zile ambazo wabunge hao wanasikika wakipanga namna ya kumshughulikia Meya wa Ubungo, Boniface Jacob huku Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, akitajwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamini Oktoba 18, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, amesema hatua hizo zimechukuliwa baada ya wabunge hao kuhojiwa na kamati kuu na kukiri sauti hizo ambazo zilihusisha mazungumzo ya kuashiria utovu wa nidhamu ndani ya chama hicho ni za kwao.

“Tumewapa adhabu mbalimbali kwa mujibu wa kanuni 6.5 (d) za chama na kamati kuu iliwaita wabunge hao kuja kujibu tuhuma na walifika na kuhojiwa na walikiri mbele ya kamati kuu ya chama kuwa sauti zilizosikika ni zao.

“Tukafikia maamuzi ya kuwapa adhabu mbalimbali pamoja na kuwavua uongozi tuliwapa onyo kali na kuwataka waandike barua ya kuomba radhi kwa chama na kwa watu waliotajwa katika sauti hizo,” amesema Mnyika.

Tiba Bora ya Nguvu za Kiume, Kisukari, Ngiri, Miguu Kuvimba

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume yanawaathiri watu wengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wengine. Kawaida mwanaume anatakiwa kuwa na uume kuanzia nchi 6- 8, vinginevyo mtu huwa na matatizo. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo. 

Baadhi ni upungufu wa vichocheo hivi; Homoni za getrogen ambazo mwanaume anapobalehe, vichochea hivi huchochea ukuaji wa uume.

Ngiri; Hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na hufanya tumbo kuunguruma na kujaa gesi. Sababu zingine ni korodani moja kuvimba, kupopata choo vizuri.

Sababu hizi na zingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara kwa mara husababisha kukosa tendo ya kurudia tendo na baadae kushindwa kabisa

MWIFU: Ni dawa inayozalisha homoni zxa Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka hadi nchi 6-8
 
WET POWER: Ni dawa bora ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba na matunda ambayo huongeza nguvu za kiume kuanzia miaka 15-95 na hukomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi, ina imariisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara mbili bila hamu kuisha na pia itakuchelewesha kufika kileleni

Pia tunatibu kisukari, presha, ngiri, miguu kuvimba na kuwaka moto

Wasiliana na Sheikh Khatib akutatulie matatizo yako. Namba zake; 0782682648  au 0656 551 093  au 0746473974

Okoa Ndoa Yako Mke,Mume Na Afya Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Za Asili

$
0
0
Asilimia kubwa ya binadamu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wengi wamejaribu kutumia tiba sehemu tofauti bila mafanikio na  kukata tamaa hasa kina baba ambao ndoa zao au mahusiano yao na wapenzi wao yapo hatarini kuvunjika kwa sababu Mume hana uwezo wa kumridhisha mpenzi wake 

KWA NINI UJIONE MPWEKE PALE UKUTANAPO NA MKE AU MPENZI WAKO SABABU ETI UNAUPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME AU UUME MDOGO: tumia dawa ya NSENWA POWER ;dawa hii hutibu na kuponesha tatizo la  nguvu za kiume .

1 itakupa uwezo wa kurudia tendo zaidi ya Mara tatu 
2 itakupa uwezo kuchelewa kukojoa mda wa dakika 15-20 na kumfanya mpenzi wako naye aridhike 
3 huimalisha misuri iliyo legea na kusinyaa 

JE UNA UUME MFUPI NA MWEMBAMBA : tumia dawa ya MASHESHE NO 2; hii huboresha uume saizi upendayo kuazia urefu wa inch 5,6,7,8 na unene  wa sentumita 2,3,4,5, dawa hizi hazina madhara yeyote kwa mtumiaji hata wazee hutumia na kupona 

MASANZA ni dawa ya vidonda vya tumbo zipo dawa za mvuto wa biashara ,mpenzi,uzazi ngiri,korodani kuvimba miguu. mgongo,kiuno kuuma nk 

MAHALI ILIPO OFISI UNAWEZA UKASHUKIA BUGURUNI MALAPA AU BUGURUNI ROZANA na MWANZA YUPO WAKALA pia unaweza ukaletewa popote ulipo wasiliana nami 0783185060  0752348593 DR AGU

Tahadhari Ya Mvua Kubwa toka TMA

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya vipindi  vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili 2019 katika kanda za magharibi, kati na nyanda za juu kusini.

Maeneo yatakayoathirika na mvua hizo za juu ya wastani hadi wastani ni Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Kusini mwa Morogoro, Lindi na Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Oktoba 18, 2018 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi amesema  utabiri huo ni kwa mikoa inayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.

"Katika kipindi cha mvua za msimu hali ya unyevunyevu wa udongo kwa ustawi wa mazao na upatikanaji wa chakula cha samaki vinatarajiwa kuimarika katika maeneo mengi,” amesema.

"Hata hivyo, mazao yasiyohitaji maji mengi kama vile mahindi, maharage na mtama yanaweza kuathiriwa na hali ya unyevunyevu wa kupitiliza na maji kutuama.”

Kutokana na mvua hizo, Kijazi amewatahadharisha pia wachimbaji wa madini hasa wadogo kuwa makini na ongezeko la maji linaloweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi au maji kujaa kwenye mashimo.

Pia, amezishauri mamlaka za miji na majiji kuchukua tafadhali kwa kuhakikisha mifumo ya kupitisha maji inafanya kazi ili kuepusha maji kutuama na kusababisha mafuriko yanayogharimu maisha ya watu na uharibifu wa miundombinu.

Wema Sepetu akana kuchepuka na mume wa Irene Uwoya

$
0
0
Wema Sepetu amekanusha vikali tetezi ambazo ziliibuliwa na mwanadada wa mitandaoni Mange Kimambi kwamba kuna siku alichepuka na Dogo Janja ambaye ni mume wa ndoa wa Irene Uwoya.

Mange ambaye amekuwa akilumbana kwenye mitandao ya kijamii na Wema Sepetu, siku ya jana alipost chart mtandaoni akionyesha kuzungumza na Dogo Janja kuhusiana na tetesi hizo.

Hata hivyo aliufuta ujumbe huo muda mchache huku watu wengi mtandaoni wakidai kwamba taarifa hizo hazikuwa na ukweli wowote.

Baada ya kuibua tetesi hizo, Wema ambaye siku ya jana alimtangaza mpenzi wake mpya, amedai sio kweli kwamba anatoka kimapenzi na mpenzi huyo wa Irene Umoya.

“Pale unapoona mtu anakuongelea vitu visivyo make sense ili mradi tu… Mi Arusha nimeenda Lini…??? Na Huyo Dogo nimekaa nae WAPI…???? Hata mazoea nae sina…!!!Ila Dada anakuwaga na stress za ajabu sometimes… Kimambi… Utaniacha lini nipumue in Peace…!??? You are Obsessed wallahy,” aliandika Wema Sepetu.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images