Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yatangaza ajira 1500 Askari wa Kikosi cha Zima Moto

$
0
0
Serikali inatarajia kutoa ajira 1,500 kwa askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji kwa mwaka wa fedha 2018/19, ili kuondoa tatizo linalolikabili pamoja na kutenga zaidi ya shilingi bilioni 4.5 kwa jeshi hilo ili liweze kutoa huduma zitakazokidhi viwango vya kitaifa na kimatafa.

Akizungumza jana Agosti 29, 2018 katika wiki ya Jeshi la Zimamoto katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola alisema ajira hizo zitaongeza kasi ya kukabiliana na majanga ya moto yanayojitokeza maeneo mbalimbali nchini.

“Tunatambua changamoto ya upungufu wa wafanyakazi katika kikosi hiki hivyo tutaajiri watumishi 1,500 ili kuongeza nguvu iliyopo,” amlisema Lugola.

Katika hatua nyingine, Lugola amewaagiza wakurugenzi wote wa majiji pamoja na miji kutoruhusu ujenzi holela na badala yake wazingatie mipango miji kwa sababu unasababisha vikosi vya zimamoto kushindwa kufika eneo la tukio kwa wakati.

Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye alisema wanakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi ikilinganishwa na ukubwa wa nchi na idadi ya wananchi na kutaja changamoto nyingine kuwa ni upungufu wa magari katika ofisi za mikoa na wilaya na kupendekeza magari 100 yatasaidia kufanya kazi kwa urahisi.

Agosti 19 magari saba ya mizigo yaliteketea kwa moto katika kituo cha forodha Rusumo wilaya ya Ngara, mpakani mwa Tanzania na Rwanda, baada ya gari moja la mafuta ya petroli kuligonga gari jingine hali iliyopelekea Helkopta ya jeshi la Rwanda kusaidia kuzima moto ulioteketeza shehena iliyokuwa imepakiwa na magari hayo baada ya kukosekana kwa magari ya zimamoto wilayani humo.

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Huna Sababu Ya Kuaibikatena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0622344969

Taarifa Muhimu Toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu

Jeshi la Polisi Lasema Mtawa Alijirusha Mwenyewe Ghorofani, Hakusukumwa na Mtu

$
0
0
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema picha za kamera za CCTV walizonazo zinamuonyesha aliyekuwa mfanyakazi wa Hospitali ya Bugando, Mtawa Suzan Batholomeo (48) akipanda kwenda ghorofani na kujirusha.

Hivyo ameitaka jamii kuacha kusambaza uzushi kuwa huenda mtawa huyo aliuawa.

Mtawa huyo alifariki akidaiwa kujirusha gorofani Agosti 28 mwaka huu.

Akizungumza leo Agosti 30,  Shanna amesema: “Tuna vithibitisho kamili ikiwamo kamera za CCTV zikimuonyesha Mtawa huyo akipanda ghorofani na wakati akijirusha, hivyo hayo yanayosemwa kwenye mitandao wasiyaamini sana.”

Ameutaka umma kuacha kuamini tetesi za mitandao ya kijamii kuhusu tukio hilo.

Pia, Shanna amesema wanaendelea kufanya uchunguzi na hivi karibuni  ataita vyombo vya habari ili kujibu maswali ya wananchi waliyokuwa wakijiuliza kuhusu kifo cha Mtawa huyo.

Kuhusu mtawa huyo kugawa mali zake kwa ndugu siku chache kabla ya kifo chake, Shanna amesema hawezi kulizungumzia kwa sasa kwani linaweza kuharibu uchunguzi unaoendelea.

Siku chache kabla ya kifo chake, ofisi ya mtawa huyo aliyekuwa mkurugenzi wa fedha ilikuwa akikabiliwa na upotevu wa zaidi ya milioni  Sh300 .

Jenerali Davis Mwamunyange ateuliwa kwenye tume ya kuchunguza ghasia za baada ya uchaguzi Zimbabwe

$
0
0
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnagangwa amteua Mkuu wa Majeshi wa Tanzania Mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange katika Tume ya Kutathmini athari za ghasia zilizotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Jenerali Mwamunyange ambaye alikuwa mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa miaka 10 toka 2007 mpaka alipostaafu 2017 ndio mtu pekee katika tume hiyo mwenye  ujuzi wa mambo ya kijeshi.

Mwanasheria kutoka Uingereza Rodney Dixon ambaye aliiwakilisha serikali ya Kenya katika kesi ya vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007 katika mahakama ya ICC, The Heague ni moja ya wajumbe wa tume hiyo.

Mjumbe mwengine kutoka nje ya Zimbabwe ni katibu mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Madola Chifu Emeka Anyaoku kutoka Nigeria.

Kutoka ndani ya Zimbabwe wajumbe ni Profesa Charity Manyeruke na Profesa Lovemore Madhuku kutoka Chuo Kikuu cha Zimbabwe pamoja na Vimbai Nyemba ambaye ni rais wa zamani wa chama cha wanasheria wa Zimbabwe.

Ghasia katika uchaguzi uliofanyika Julai 30 zilisababisha vifo vya watu 6 na wengine wakiwa wamejeruhiwa.

Lugola Adai Halijui JESHI LA ZIMAMOTO.....Awatimua Maafande 30 Kikaoni

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewatoa nje Makamanda zaidi ya 30 kwa kosa la kutaja Jeshi la Zimamoto bila kumalizia ‘na Uokoaji’ ambapo amesema  hilo jeshi lao halitambui.

Hali hiyo imejitokeza leo Alhamisi Agozti 30, jijini Dodoma kwenye ufunguzi wa kikao cha mwaka cha Makamanda wa Zimamoto na Uokoaji ambapo amesema makamanda hao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea.

“Mimi nalijua Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wale wote ambao walijitambulisha bila kumalizia na uokoaji watoke nje.

“Nisikilizeni kwa makini makamanda ambao nimewaita majina yenu simameni na ambao hamjasikia nikitaja majina yenu tokeni nje kwani hilo jeshi lenu mlilolitaja silitambui hivyo kikao hiki hakiwahusu.

“Haiwezekani ofisa mzima unasimama unajitambulisha kuwa unatoka Jeshi la Zimamoto, kwa hiyo kazi yenu nyinyi ni kuzima moto tu na siyo pamoja na uokoaji,” amesema.

Waziri Lugola alisema amefanya hivyo kwa kuwa anataka jeshi hilo lijitambue kuwa ni jeshi lenye majukumu hayo kwani lipo na lilianzishwa kwa mujibu wa sheria kuwa ni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Hata hivyo, Lugola baada ya kuwatoa nje makamanda hao aliwaruhusu kuingia kushiriki kikao hicho wakiwa kama wageni waalikwa na si wahusika wa kikao hicho.
Maofisa wa Jeshi la Zimamoto wakitoka nje baada ya kutolewa.

Tume ya Utumishi wa Walimu yaonya waalimu wanaoadhibu wanafunzi kinyume na sheria na kanuni

$
0
0
Katibu Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa ametoa onyo kwa Walimu wanaowaadhibu wanafunzi bila kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu zinazotoa mwongozo wa aina, kiwango na namna  adhabu inavyotakiwa kutolewa kwa wanafunzi.

Amesema kuwa, kutoa adhabu ya viboko kwa wanafunzi bila kuzingatia taratibu zinazohusika sio tu kwamba inaleta athari kwa wanafunzi wanaoadhibiwa bali inaweza kusababisha chuki kati ya wazazi na walimu.

Ameeleza kuwa, Tume ya Utumishi wa Walimu imesikitishwa na tukio la hivi karibuni lililoripotiwa kwenye vyombo vya habari juu ya  Mwalimu Respecious Patrick wa Shule ya Msingi Kibeta, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera anayedaiwa kumwadhibu mwanafuzi  Sperius Eradius, ambapo mwanafunzi huyo amefariki dunia.

“Mwalimu ni mlezi na kwa mujibu wa kuu tano za maadili ya ualimu, mwalimu ana wajibu wa kumlea mwanafunzi kimwili, kiakili na kiroho. Sasa mwalimu anapogeuka na kuwa tishio kwa wanafunzi ni jambo la kusikitisha ambalo hatuwezi kulifumbia macho wala kulivumilia hata kidogo” alisema.

Amefafanua kuwa, Uongozi wa shule una jukumu la kusimamia nidhamu ya Walimu pale shuleni kwani Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu inamtambua Mwalimu Mkuu/Mkuu wa Shule kuwa ni mamlaka ya kwanza ya nidhamu kwa mwalimu.

“kwanza nimejiuliza, hadi huyu mwalimu anafikia huko kuna uwezekano mkubwa amekuwa na tabia ya kuwaadhibu wanafunzi kupita kiasi na alipaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu huko nyuma kabla ya kusababisha madhara makubwa hivi” alisema.

Aliongeza kuwa,“nimeshindwa kuelewa inawezekanaje mwalimu anafanya tukio la kumpiga mwanafunzi kiasi hicho na walimu wengine wapo na hakuna jitihada wanazofanya kumsaidia mwanafunzi”.

Amesema kuwa, amemuagiza  Kaimu Katibu Msaidizi wa Wilaya ya Bukoba kuangalia taratibu za kufuata kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu na. 25 ya mwaka 2015 ili kama yatabainika masuala yanayohitaji kuchukuliwa hatua za kidnidhamu kwa walimu wa shule hiyo sheria ichukue mkondo wake.

Amefafanua kuwa, mwongozo wa kutoa adhabu mashuleni umetoalewa chini ya kifungu cha 61 (1) (v) cha Sheria ya Elimu sura ya 353 marejeo ya mwaka 2002 ambapo kinampa Mamlaka Waziri wa Elimu kutunga kanuni za Masuala mbalimbali zitakazokidhi utekelezaji wa utekelezaji wa masuala ya Sheria hiyo.

Miongoni mwa kanuni zilizotungwa ni The Education (corporal Punishment) Regulation G. N. 294 ya mwaka 2002. Kanuni hizi zinatoa mwongongozo ni wakati gani adhabu ya viboko inatakiwa kutolewa na kwa kiwango gani.

“Kanuni ya 3 (1) inasema adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhamu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo litaishushia shule heshima. Kanuni ndogo ya (2) inasema adhabu ya Viboko itatolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi na isizidi viboko vinne (4) kwa tukio lolote,” alisema.

Sheria inamtaka mwalimu mkuu au mkuu wa shule kutoa adhabu ya viboko au kukasimisha mamlaka yake kwa mwalimu yeyote kutekeleza adhabu hiyo.

Kwa mujibu wa kanuni hiyo, kila adhabu ya viboko inapotolewa kwa mwanafunzi  ni lazima mwalimu aweke kumbukumbu kwenye kitabu ikitaja jina la mwanafunzi, kosa alilolifanya, idadi ya viboko pamoja na jina la mwalimu aliyetoa adhabu na kumbukumbu hizo zinatakiwa kusainiwa na mwalimu mkuu au mkuu wa shule.

Ni wajibu wa walimu kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za utumishi wao ili kuleta ustawi mzuri kwa wanafunzi wanaowafundisha.

Adili Mhina,
Afisa Mawasiliano,
Tume ya Utumishi wa Walimu.
30/08/2018.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yamuengua Mgombea Mmoja wa Udiwani, Saba Wanusurika

$
0
0
Idara ya Habari-NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefanya uamuzi wa rufaa nane za wagombea udiwani wa kata saba zinazoshiriki uchaguzi mdogo na kukubali rufaa ya kumuengua mgombea mmoja wa kata ya Sisimba  katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Akitoa taarifa ya uamuzi wa rufaa hizo jijini Dar es Salaam leo (Agosti, 30) Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Athumani Kihamia amesema mbali na kumuengua mgombea huyo, Tume imeamua kuwa wagombea saba (7) wataendelea na uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Septemba 16.

Mbali na uamuzi wa rufaa hizo, Dkt. Kihamia amevikumbusha vyama vya siasa na wagombea wanaoshiriki katika uchaguzi huo,  kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, wakati wote wa kampeni na hata siku ya uchaguzi.

Dkt. Kihamia alifafanua kuwa uamuzi wa rufaa hizo umezingatia matakwa ya kanuni ya 29(3), (4) na (5) ya Kanuni za Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015.

“Tume, ilipokea, ilijadili na kufanya maamuzi ya Rufaa hizo nane (8) ambazo kati ya hizo rufaa, mbili (2) zilipinga kuondolewa kugombea na kutaka kurejeshwa kugombea na rufaa sita (6) zilikuwa zikipinga wagombea walioteuliwa”, alisema Dkt. Kihamia na kuongeza kuwa:

“Tume imeamua kuwa wagombea saba (7) wataendelea na uchaguzi na mgombea mmoja ameenguliwa na hivyo kutoendelea kuwa mgombea.Taarifa za maamuzi ya rufaa hizo, zimetumwa kwa wahusika kupitia kwa Wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri husika”.

Aliongeza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea rufaa nane (8) kutoka kwa wagombea udiwani wa Kata za Sisimba, Maanga, Nsalaga na Iwambi katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Alisema wagombea wengine walitoka Kata ya Nkuyu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela; Kata ya Kizota katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Kata ya Mwanhuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

Mwisho

DC Jokate Mwegelo, Hamisa Mobeto Wateuliwa Kuwa Mabalozi wa Kampeni ya BE SMART. ya TCRA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo,mwanamitindo Hamisa Mobeto, wanamuziki Barnaba , Shilole na muigizaji wa vichekesho Dullvani wamechaguliwa kuwa mabalozi wa  kampeni maalumu inayohusu elimu kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii iliyopewa jina la BE SMART.

Kampeni hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatarajia kuanza Septemba 3 katika shule za sekondari.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu na Mwanzilishi wa kampeni hiyo, Marry Msuya alisema wasanii hao wamechaguliwa kuwa mabalozi kutokana  na michango yao kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii.

“Wasanii hawa wamekua wakitumia mitandao katika mambo mbalimbali ya kujinufaisha wengine wanatangaza biashara na wengine wanaonyesha vipaji mbalimbali walivyonavyo”. Amesema katibu huyo.

Wizara ya afya Yatuma Mtaalum BINGWA Kuchunguza mwili wa mwanafunzi aliyeuawa Kwa Kichapo na Mwalimu

$
0
0
Na WAMJW
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemwagiza mtaalamu bingwa wa uchunguzi kwenda mkoani Kagera kwa ajili ya kurejea uchunguzi wa chanzo cha kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius (13) wa shule ya Msingi Kibeta iliyopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera na kuwahakikishia wanafamilia na wananchi kuwa uchunguzi utafanyika kwa ufanisi na haki itatendeka. 

Ameyasema hayo mapema leo wakati akizungumzia kuhusu kifo cha mwanafunzi huyo kinachosemekana kilisababishwa na mwalimu wake Respicius Patrick baada ya kumpiga kwa kumtuhumu kumuibia pochi yake.

Waziri Ummy amesema kuwa kitendo hicho ni cha ukatili kwani ni kinyume na Sheria ya Mtoto Namba 21 ya Mwaka 2009 kifungu cha 13 (2) ambayo inasisitiza kutolewa kwa adhabu stahiki kwa mtoto kulingana na umri, hali ya kimwili na kiakili.

Aidha, amelaani vikali Vitendo vya Ukatili dhidi ya watoto vinvyoendelea kufanyika katika jamii na kusema kuwa Serikali itahakikisha inawafuatilia na kuwachukulia hatua watakaofanya vitendo hivyo.

Ameongeza kuwa wa kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi, anaamini pindi uchunguzi utakapokamilika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa.

Amesisitiza kuwa jamii na kila mtu anaowajibu wakuhakikisha mtoto anaishi, kukua na kuendelezwa katika mazingira salama na rafiki kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.

TAMWA Yalaani Vipigo Kwa Wanafunzi

$
0
0
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini (Tamwa), kimelaani vitendo na matukio ya ukatili unaofanywa na baadhi ya walimu kuwapiga wanafunzi bila kufuata sheria na kusababisha baadhi yao kuathirika kisaikolojia na hata kupoteza maisha.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Edda Sanga, imesema miongoni mwa matukio ya kusikitisha ni lile la Agosti 27 mwaka hu ambapo mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kibeta, Bukoba mkoani Kagera, Sperius Eradius (13) alifariki dunia baada ya kupigwa na mwalimu wake kwa kutuhumiwa kuiba pochi ya mwalimu.

Amesema Sheria juu ya viboko mashuleni katika Kifungu cha 61(1)(v) cha Sheria ya Elimu Sura ya 353 marejeo ya mwaka 2002, kinampa mamlaka waziri wa huyo kufanya hivo.

“Tukio jingine ni lile la mwaka 2016 lililotokea kwa msichana wa kidato cha nne (17) aliyekuwa akisoma katika shule moja ya sekondari ya kata mkoani Mbeya ambaye alivuliwa nguo zake za ndani na kucharazwa bakora zisizo na idadi kwa sababu za utoro shuleni, adhabu iliyotolewa na walimu wanne wa shule hiyo akiwemo mkuu wa shule hiyo.

“Sheria inamtaka mwalimu mkuu wa shule husika kutoa adhabu ya viboko au kukasimisha mamlaka yake kwa umakini mkubwa kwa mwalimu yeyote kutoa adhabu hiyo, Mwalimu anayechaguliwa kutoa adhabu atakuwa na mamlaka ya kutoa adhabu pale tu atakapopata idhini ya mwalimu mkuu katika tukio husika.

“Tamwa inalaani kwa nguvu ukatili wa aina hii na ni matarajio yetu kuwa vipigo na mauaji mashuleni havitatokea tena,” amesema.

BREAKING: Rais Magufuli Apigilia Msumari Sakata la Makontena ya Makonda....Asema Ni Lazima Yalipiwe Kodi

$
0
0
Rais John Magufuli amewataka viongozi kujenga mazingira ya kuwatumikia wananchi bila kujali wapo kwenye nafasi gani.

Magufuli ameyasema hayo leo Agosti 30, akizungumza na madiwani, viongozi na watumishi wa Halamshauri ya Wilaya ya Chato, Geita.

Akizungumza katika Mkutano uliofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Magufuli ametolea mfano sakata la makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yanayotarajia kupigwa mnada baada ya kushindwa kulipiwa kodi bandarini.

“Umesikia hili sakata la Dar es Salaam, eti Mkuu wa Mkoa, ameleta makontena, ameambiwa alipe kodi, kwa nini asilipe kodi?” amesema.

 Amesema sheria za nchi zinasema wazi kuwa ni mtu mmoja tu katika nchi mwenye dhamana ya kutolipa kodi kwa mujibu wa sheria ya fedha, sheria ya madeni, sheria ya dhamana na ya misaada.

 Rais Magufuli aliitaja sheria hiyo kuwa ni namba 30 ya 1974, kifungu cha 3, 6, 13 na cha 15 ndicho kinampa mtu huyo dhamana ya kupokea misaada. Rais Magufuli amesisitiza. “Hakuna mtu mwingine.”

 “Sasa ukichukua makontena kule, umezungumza na watu wengine labda na wafanyabiashara, unasema ni makontena yako,  halafu ukasema tena labda ni ya  walimu, wala hata shule hazitajwi,  Maana yake nini?”

“Maana yake si unataka utumie walimu, ulete haya makontena, utapeleka  shule mbili au tatu, ndizo zitapewa mengine unakwenda kuyauza unapeleka kwenye shoping mall. Lakini walimu walikuambia wanahitaji makochi, sofa,” amesema.

Rais Magufuli aliwataka wafanyakazi wasitumike kwa maslahi ya watu fulani.

VIDEO: Msikilize Hapa Rais Magufuli Alivyomkaanga Makonda Sakata la Makontena

$
0
0
Rais John Magufuli amepigilia msumari sakata la makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yanayoshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kumtaka kuyalipia kodi.

Aidha, amewataka viongozi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria sambamba na kuhakikisha wanasimamia ipasavyo matumizi ya rasilimali za umma kwa maslahi ya wananchi.

Rais Magufuli amesema hayo leo Alhamisi Agosti 30, wilayani Chato mkoani Geita, wakati akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa wilaya hiyo.

“Viongozi wote wajenge utaratibu wa kusoma sheria na kujiepusha kutumiwa kwa maslahi ya watu binafsi, kwa mfano mgogoro wa makontena yanayodaiwa kuwa na fenicha za shule yanayoshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Bandari ya Dar es Salaam, nasema makontena hayo yanapaswa kulipiwa kodi kwa mujibu wa sheria.

“Eti Mkuu wa Mkoa ameleta makontena anaambiwa alipe kodi hataki, kwa nini asilipe kodi, kwa sababu ni mtu mmoja tu  katika nchi hii kwa mujibu wa sheria ya Madeni, Dhamana na Misaada Namba 30 ya mwaka 1974 (kama ilivyorekebishwa na sheria namba 9 ya mwaka 2003) kifungu cha 3, 6,13 na 15 Waziri wa Fedha na Mipango ndiye mwenye mamlaka ya kukopa nje na ndani, kutoa dhamana na kupokea misaada kwa niaba ya Serikali hakuna mtu mwingine, hayupo.


“Kwa msingi huo, hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kukopa, kutoa dhamana na kupokea misaada kwa niaba ya Serikali bila mtu huyo kukasimiwa mamlaka hayo na Waziri wa Fedha kwa mujibu wa sheria hiyo.

==>> Msikilize Hapo chini akiongea

Mkuu wa Mkoa Kaituliza Familia ya Mwanafunzi Aliyeuawa kwa Kipgo.......Mkuu wa Shule, Makamu Wake na Afisa Elimu Kata Wasimamishwa Kazi

$
0
0
Kifo cha mwanafunzi wa shule ya msingi Kibeta Siperius Eradius aliyedaiwa kuuawa na mwalimu wake kimeondoka na walimu watatu huku familia ya marehemu ikikubaliana na uchunguzi ambao haujawekwa wazi.

Akizungumza leo Alhamisi Agosti 30, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti baada ya kutembelea shule hiyo, amemuagiza mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba awasimamishe kazi walimu watatu ili wachunguzwe kama walitekeleza majukumu yao.

Waliosimamishwa ni Renatha Izidory aliyekuwa mwalimu mkuu na msaidizi wake Sunday Elisha na ofisa elimu wa Kata ya Kibeta,  Hashimu Mponda.

Mkuu huyo wa mkoa pia amekwenda kwa familia ya marehemu na kubainisha kuwa familia hiyo imekubaliana na matokeo ya uchunguzi wa pili wa kifo cha mwanafunzi huyo uliofanywa na madaktari kutoka nje ya Mkoa wa Kagera.

Awali, familia hiyo ilisusia mwili wa mwanafunzi huyo baada ya uchunguzi uliotolewa na mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa Mkoa wa Kagera, Dk John Mwombeki kueleza kuwa mwili wake ulikutwa na alama zinazoonyesha alipigwa siku kadhaa kabla ya kukutwa na umauti.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Agosti 31

Katibu Mkuu CCM Amtolea Uvivu Waziri Anayemiliki Heka 1000 za Ardhi Morogoro

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema amemuita mmoja wa mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano aeleze alipopata ekari 1,000 za mashamba.

Bila kumtaja jina waziri huyo, Dk Bashiru amesema atamtaka achague jambo moja kati ya kuwa mporaji ama kiongozi wa chama hicho.

Ametoa kauli hiyo jana Alhamisi Agosti 30, 2018 wakati akifungua mkutano wa Baraza la Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa jijini Dodoma.

Amesema mambo yanayozungumzwa katika vyombo vya habari unaweza kudhani ndio hali halisi katika Jamii.

"Viongozi msifanye kazi katika vyombo vya habari nendeni katika maeneo mbalimbali mkatatue kero za wananchi. Nilikwenda eneo moja wananchi wanajiuliza waziri huyo amepataje ardhi hiyo," alisema Dk Bashiru.

Alisema atamuita waziri huyo aeleze amepataje eneo hilo kwa sababu CCM haiwezi kuwa na wanachama ambao ni waporaji wa ardhi.

“Achague kimoja kama ni mporaji ama kuwa kiongozi wa CCM," alisisitiza.

Luka Modric Anyakua Mchezaji Bora, Ronaldo Mshambuliaji Bora

$
0
0
Kiungo wa Klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Croatia, Luka Modric amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya akiwafunika Mo Salah wa Liverpool na Cristiano Ronaldo wa Juventus.

Kipa wa Real Madris, Kyle Navas, ametwaa tuzo ya goli kipa bora wa michuano ya Uefa msimu wa mwaka 2017/18.

Beki kisiki wa Real Madrid, Sergio Ramos, ametwaa tuzo ya beki bora kwenye michuano ya Uefa msimu wa mwaka 2017/18.

Aidha, Cristiano Ronaldo aliyekuwa Real Madrid kabla ya kutimkia Juventus, ametwaa tuzo ya mshambuliaji bora wa michuano ya Uefa msimu wa mwaka 2017/18.

Pia, Legendari, David Bechkam amepewa tuzo ya heshima kutoka uefa kutokana na mchango wake mkubwa katika soka.

Walioshika nafasi kuanzia ya 4 za mchezaji bora ni;

4 Antoine Griezmann (Atlético & France) – 72 alama
5 Lionel Messi (Barcelona & Argentina) – 55 alama
6 Kylian Mbappé (Paris & France) – 43 alama
7 Kevin De Bruyne (Manchester City & Belgium) – 28 alama
8 Raphaël Varane (Real Madrid & France) – 23 alama
9 Eden Hazard (Chelsea & Belgium) – 15 alama
10 Sergio Ramos (Real Madrid & Spain) – 12 alama

Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma Awaasa Wanasheria Kuzingatia Misingi Ya Taaluma

$
0
0
Na. Idara ya Habari-MAELEZO
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amewaasa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma kuzingatia misingi ya taaluma wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.

“Mkiwa maafisa wa Mahakama tunawatazamia kufanya kazi zenu kwa kuzingatia misingi ya taaluma iliyowekwa kwa kuzingatia maadili, weledi, uwazi na usiri” alisisitiza he Profesa Juma.

Profesa Juma pia amewakumbusha wanasheria hao walio kwenye utumishi wa umma kuhakikisha  kuwa sheria wanazosimamia zinalenga kuleta ustawi wa wananchi wanyonge na kuiwezesha serikali kutimiza azma yake ya kifanya Tanzania iweze kufikia hadhi ya  nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Vilevile, wanasheria hao wa serikali wameaswa kuzingatia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kutekeleza majukumu yao ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya karne ya 21.

Aliongeza kuwa, wanasheria wanalo jukumu kubwa la kukidhi matarajio ya wananchi ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025,  amani, usalama, umoja, utawala bora, na kujenga uchumi imara.

Kabla ya Jaji Mkuu Profesa Juma, kuhutubia mkutano huo Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palagamba Kabudi  alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya mabadiliko katika muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao unategemewa kuleta ufanisi. Kwenye mabadiliko hayo yaliyoidhinishwa na Rais Magufuli, yamesababisha kuanzishwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Wakili Mkuu wa Serikali.

Mkutano huo wa siku mbili unawakutanisha wanasheria zaidi ya mia tisa kutoka Wizara, Serikali za mitaa, Mashirika, Wakala na Idara mbalimbali za Serikali.

Dr Kanengo: Bingwa Wa Tiba Asili Hutibu Matatizo Yafuatayo

$
0
0
NKURURU:-ni dawa inayotibu miguu kuwaka moto, kiuno tumbo kupooza kupoteza fahamu 

MALABALA; hutibu kisukari , uti wa mgogo, Change, pumu, busha, kaswende, kifua kikuu, muwasho sehemu ya siri 

NKURUNGU,: Ni dawa kutibu  N, B, G, POWER :-ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume ni vidonge 20 

MPERAMPERA:- ni dawa ya kurudisha Mke, mme, mpenzi,mchumba aliyekuacha /kuteseka, ni kwa mda wa siku 2 tu kusafisha , pia kuna dawa za kupunguza vitambi(nyama uzembe), maziwa makubwa,michirizi, mikovu makubwa, chunusi sugu. 

NR SIX POWER:-inatibu upungufu wa nguvu za kiume kwa wasio weza kumudu tendo la ndoa itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara 4 bila hamu Kuisha, inaboresha maumbile madogo na inaimarisha misuri iliyo legea na kusinyaa una pona kabisa, ndani ya siku 4 tu 

GASELA:-ni dawa ya maajabu (9) yaliyoshindikana. (1)-Kisukari, vidonda vya tumbo, tezi dume,walioshindikanika kupata watoto(ugumba),busha bila oparesheni, (2)zindiko Kali Katika biashara yako (chuma ulete) ndo kiboko yao kumkamata mwizi aliye kuibia vitu vyako pikipiki, gari, n, k( 2)zindiko la nyumba, mashamba, viwanja,.(4)kukutolea sumu uliyo ikanyaga (Mtego) (5)ujiamini kutumia dawa ya maajabu Saba (6)kutoa mikafara mfano ugomvi ndani ya nyumba kufukuzwa kazini bila sababu (7)kutabiri nyota na kung'arisha (8)kurudisha Mali iliyo potea mazingira ya kutatanisha, kushinda kesi uliyo sumbuka nayo mda mrefu. (9)kufukuza majini wachafu ndani ya mji,.

Haya yote yanawezekana kwa DR KANENGO popote ulipo . Muone  DR KANENGO,anatibu nguvu za kiume anarefusha na kunenepesha uume kwa saizi uipendayo kwa muda mfupi sana, pamoja na kuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa mara 4 bila hamu kuisha Na utachelewa kufika kileleni kwa muda wa dakika 40 bila kuchoka .

Angalizo usitume meseji wala kubipu..
 
You can get it in all East African countries,,our service is fast and easy... contact Whatsapp 0784,47,59,46.Dar es salaam Tanzania. ,..Dr. KANENGO 0744,92,29,82...You are welcome. Yuko pia Khahama Mjini, Bunda kwa sasa
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images