Duniani hakuna mwanamke mbaya. Wanawake wote ni wazuri. Na uzuri wa mwanamke sio sura wa umbo uzuri wa mwanamke ni tabia yake.
Kama nilivyo sema hapo juu kwamba wanawake woote duniani ni wanawake wazuri, isipokuwa wamegawanyika katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza ni wanawake wenye uzuri wa kawaida na kundi la pili ni wanawake ambao ni wazuri kupita kawaida.
Katika Makala haya nimewalenga wanawake walio katika kundi la pili, yani wanawake wazuri kupita kawaida.
Katika jamii inayo tuzunguka kuna Imani kubwa imejengeka kwamba wanawake wazuri kupita kiasi hawafai kuolewa kwa sababu inaaminika kwamba wanawake wazuri kupita kiasi ni vigumu sana kutulia na mwanaume mmoja kwa sababu wana tama asana na kwamba wengi wao hawana mapenzi ya ukweli. Bila shaka hii ndio sababu inayo wafanya wanaume wengi kuogopa kuwaoa wanawake wazuri kupita kiasi na mwisho wa siku wanawake wazuri kupita kiasi kuishia tu kuwa katika mahusiano ya kimapenzi ya muda mfupi na kuachwa.
Je dhana hiyo ni ukweli au ni uzushi tu wa walimwengu ?
Katika Makala haya utapata kuyajua majibu ya kina kwanini baadhi au kwanini wengi wa wanawake wazuri kupita kiasi huwa hawaolewi na hata ikitokea wakiolewa basi ndoa zao huwa hazidumu .. Nikiwa kama Tabibu wa Jadi, sababu zangu ni sababu za kiroho.
Zipo sababu kadhaa zinazo fanya wengi wa wanawake wazuri kupita kiasi wasiolewe.
Baadhi ya sababu hizo ni kama ifuatavyo :
1. MAJINI MAHABA.
Kuna wanawake ni warembo na wazuri kupita kawaida kiasi kwamba huwavutia mpaka majini mahaba.
Kabla sijaelezea namna majini mahaba wanavyo sababisha wanawake wazuri kupita kiasi wasiolewe ni vyema nikakujulisheni kwa ufupi kuhusu historia ya suala la majini na viumbe wengineo wa kiroho kua katika mahusiano ya kimapenzi na wanawake wa kibinadamu.
Suala la majini na viumbe wengine wa kiroho kuvutiwa kimapenzi na wanawake wa kibinadamu
( wenye uzuri na urembo ambao unapita kawaida )na kuanzisha nao mahusiano ya kimapenzi halijaanza jana wala juzi.
Suala hili lipo duniani toka enzi za mitume na manabii.
Ukiisoma vizuri Taurati utagundua kwamba kuna malaika waliwapenda wanawake wa kibinadamu na kuwaoa kisha kuzaliwa viumbe walio julikana kama wanefili.
Kwa hiyo suala la viumbe wa kiroho kuvutiwa kimapenzi na wanawake wa kibinadamu ni suala la kawaida kabisa katika ulimwengu wa rohoni.
Nirudi kwenye mada yangu. Majini mahaba huwa wanavutiwa sana kimapenzi na wanawake walio jaliwa uzuri wa sura na maumbo ambao si wa kawaida.
KITU GANI HUTOKEA JINI MAHABA AKIMPENDA MWANAMKE
Jini mahaba akimpenda mwanamke huwa anaingia na mwanamke huyo katika agano la kichwa na mwili ( Jinni mahaba huwa kichwa na mwanamke huyo huwa mwili/ katika ulimwengu wa kiroho agano la kichwa na mwili maana ake ni agano la ndoa kati ya mwanamke na mwanaume )
Kwa lugha ya kawaida jinni mahaba huyo huingia na mwanamke huyo katika agano la ndoa ya mke na mume . Jinni mahaba huwa mume na mwanamke huyo huwa mke.
Agano hili hufanyika bila ridhaa ya mwanamke huyo. Kwa lugha nyingine mwanamke huyo anakuwa amelazimishwa kuolewa na jinni mahaba huyo bila yeye mwenyewe kujua au kutaka.
KITU GANI HUTOKEA JINNI MAHABA AKIFUNGA NDOA NA MWANAMKE
Jinni mahaba akifunga ndoa na mwanamke, maana yake ni kwamba katika ulimwengo wa rohoni mwanamke huyo anakuwa mke halali kabisa wa jinni huyo.
Jinni huyo anakuwa anammiliki mwanamke huyo na kumtumia kama mke wake na anakuwa na haki za kiroho za kufanya jambo lolote juu ya mwanamke huyo kama mke wake ikiwa ni pamoja na kutoa adhabu kwa wanaume wanao mzengea mwanamke huyo.
KITU GANI HUTOKEA PINDI MWANAUME ANAPOINGIA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MWANAMKE AMBAE AMEOLEWA NA JINNI MAHABA.
Mwanaume unapoingia katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamke ambae ameolewa na jinni mahaba maana yake katika ulimwengu wa rohoni ni kwamba umeingilia ndoa ya “ mtu “ mwingine.
Umefanya dhambi ya zinaa kwa kuzini na mwanamke ambae tayari anamilikiwa na “ mtu “ mwingine.
Kitakacho fuatia hapo ni wewe kulipa deni la kiroho kwa ‘dhambi’ ya kutembea na mke wa mtu.
Haijalishi kwamba ulikuwa unajua au ulikuwa haujui kama mwanamke huyo anamilikiwa na jinni mahaba, kwa sababu katika ulimwengu wa rohoni kutojua kuhusu jambo sio kinga ya kukuepusha na adhabu ya kufanya jambo ambalo limekatazwa ambalo wewe haulijui.
NI ADHABU GANI ZA KIROHO ANAZO WEZA KUZIPATA MWANAUME AMBAE AMEINGIA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MWANAMKE AMBAE AMEOLEWA NA JINNI MAHABA.
Zipo adhabu nyingi sana ila leo nitazitaja chache hususani zile ambazo zinahusiana moja kwa moja na suala la wanawake wazuri kupita kiasi kutokuolewa.
1. KUHARIBIKIWA MAMBO YAKO KIFEDHA NA KIMAISHA KWA UJUMLA : Jinni mahaba anae mmiliki mwanamke ambae umeingia nae katika mahusiano ya kimapenzi akisha gundua kwamba wewe ‘ umeingilia ndoa yake ‘ atakacho kifanya atatafuta kujua kitu gani ambacho kimemvutia ‘mke wake’ huyo kuja kwako. Atataka kujua ni Kitu gani ambacho kimemfanya ‘mke wake ‘ akupende na kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na wewe.
Akigundua kwamba kitu kilicho mvutia “ mke “ wake kuwa katika mahusiano ya kimapenzi au kuolewa na wewe ni pesa au mali zako, atakacho kifanya ni kuharibu ‘ chanzo cha tatizo’ ( Naposema chanzo cha tatizo namaanisha chanzo cha wewe kuleta matatizo katika ndoa yake kwa kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na mke wake )
Kwa hiyo sasa jinni huyo atakacho kifanya ni kutia giza , utupu na ukiwa kwenye nyota yako.
Kwa lugha rahisi ni kwamba jinni huyo ataharibu na kuua nyota yako. Na kama nilivyo wahi kufundisha kwenye masomo yangu yaliyo pita, nyota ya mtu ndio chanzo cha kila kitu katika maisha ya mwanadamu.
Jinni huyu akiharibu nyota yako basi mambo yako yataanza kuharibika taratibu, kama ni kazini basi itaanza kutokea misuko suko, utashushwa cheo au kufukuzwa kazi kabisa, na maisha yako yataanza kuyumba taratibu na mwisho wa siku utafilisika kabisa.
Kama ni mfanyabiashara basi ataua biashara zako zote na kuziba vyanzo vyote vya pesa katika maisha yako na kukufanya uwe na maisha magumu na hatimaye kufilisika kabisa.
Kwa sababu huyu mdada mzuri alikupenda kwa sababu ya pesa zako na wewe sasa hivi hizo pesa huna tena wala maisha yako hayaonyeshi dalili zozote kwamba utaanza kupata pesa kama hizo tena hivi karibuni, mwanamke huyo ima atakuacha na kuchukuliwa na mwanaume mwingine mwenye pesa na uwezo wa kumtunza au wewe mwenyewe utamkimbia kwa kushindwa kumudu kumuhudumia au kwa kukimbia aibu ya kuadharauliwa na mwanamke huyo kwa sababu utakapo anza kuishiwa pesa za kumuhudumia na atakapo kuwa akikuomba pesa za matumizi na mahitaji ambazo wewe huna atakuwa akipokea pesa za matunzo kutoka kwa wanaume wengine ambao watakuwa wanamtaka.
Mwanaume atakae kupokea kijiti nae mambo yake yatakuwa hivyo hivyo kama ilivyo kuwa kwako. Hali hii itajirudia na kujirudia kwa mwanamke huyo. Na anaweza kwenda nayo hivyo hivyo katika maisha yake yote.
Watu wa nje wataanza kumuogopa na kumnyanyapaa mwanamke huyo kwa kusema ana nukushi ( nuksi ) na mwanaume yoyote mwenye pesa atakae ingia katika mahusiano nae ya kimapenzi basi atafilisika.
Mwisho wa siku sasa wanaume waoaji wataanza kumkwepa mwanamke huyo na kumbuka kuwa muda hausimami.
Mwisho wa siku mwanamke huyo atafikisha miaka 35 bado yupo nyumbani kwa wazazi wake akiwa na mtoto Zaidi ya mmoja na kila mmoja akiwa na baba yake wakati huo uzuri wake unakuwa umeisha chuja na kunakuwa hakuna mwanaume mwingine wa maana ambae ana fikiria kumuoa.
Wakati watu wa nje wakimuona mwanamke huyo kama mwanamke mwenye nuksi ambae kila mwanaume anaeingia nae katika mahusiano huishia kufilisika, hali huwa tofauti kabisa ndani ya nafsi ya mwanamke huyo.
Ndani ya nafsi yake mwanamke huyu hubaki kujilaumu mwenyewe kwa kudhani kuwa suala la yeye kutopata mume wa kumuoa limesababishwa na tabia zake za kutowavumilia wanaume zake pindi wanapo kuwa wamefulia.
Na mara nyingi huanza kujitafakari pindi umri unapokuwa umeanza kusogea.
Katika kipindi hiki mwanamke huyu anakuwa tayari ana miaka thelathini au na Zaidi na anakuwa na mtoto Zaidi ya mmoja huku kila mtoto akiwa na baba yake.
Mara nyingi wanaume ambao aliwaacha baada ya kufilisika wanakuwa tayari wanaendelea na maisha yao na wengi wao wanakuwa wameoa na kutulia na wanawake wengine ambao uzuri wao ni kawaida.
Wanawake hawa hujilaumu sana na hatimae huanza kubadili tabia na mtazamo wao kuhusu wanaume wa kufunga nao ndoa .
Kinapokuwa kimefikia kipindi hiki mwanamke huyu anakuwa yupo tayari kujishusha na kuishi na mwanaume wa aina yoyote ile hata kama hana kitu.
Cha kushangaza ni kwamba hata inapo tokea wakaingia katika mahusiano na mwanaume asie na kitu nayo huishia hewani bila sababu yoyote ya msingi.
Dada huyu anasema “ Kuna mwanaume mmoja alinifuata tukaanzisha nae mahusiano. Baada ya kuzoeana nikaanza kumshawishi nataka tufunge ndoa akasema mambo yake ya kifedha bado hayajakaa sawa nikamwambia nitamkopesha hela afungue biashara. Mipango ya kwenda kujitambulisha nyumbani kwetu ikaanza kufanyika na huwezi kuamini pesa aliyo nitolea mahali mimi ndio nilimpa kwa sababu hakuwa na uwezo. Lakini kitu cha ajabu mipango ile iligeuka ghafla na mimi na yule mwanaume tukabaki kuwa maadui wakubwa “.
Mwisho wa siku wanawake hawa huamua kukubaliana na matokeo na kuishi maisha ya kusononeka kutokuwa na mume katika maisha yao yote. Hubaki kujilaumu kwa usaliti walio wafanyia wapenzi wao wa awali bila kujua kwamba ilisababishwa na jinni mahaba.
2. KUSABABISHIWA MARADHI YA UKHANITHI : Jinni mahaba akigundua kwamba kinacho mfanya mke wake akupende wewe ni uwezo wako mzuri kitandani basi atakacho kifanya ni kukutia ukhanithi jambo litakalo kufanya kutokuwa na uwezo tena wa kumridhisha mwanamke huyo na hali hiyo ikiendelea kwa muda mrefu basi mwanamke huyo atakuacha na kwenda kwa mwanaume mwingine ambae nae atafanyiwa hivyo hivyo.
Mzunguko huo utaendelea na kuendelea na mwisho wa siku mwanamke huyo atawachukia kabisa wanaume na kudharau uwezo wao wa kufanya tendo la ndoa pamoja na kulichukia tendo la ndoa kabisa.
Na hii ndio sababu kwanini baadhi ya wanaume hulalamika kwa kusema “ Nikiwa na mwanamke Fulani nakuwa sina uwezo kabisa wa kufanya tendo la ndoa au nafanya mara moja halafu nachoka sana kiasi ambacho nakuwa siwezi kurudia tena tendon na kama ni usiku basi nitalala fofofo hadi asubuhi na kumuacha mwenzangu akiwa bado ananihitaji lakini nikienda kwa mwanamke mwingine ninakuwa na uwezo mkubwa sana. Mbaya Zaidi mwanamke huyo anaweza kuwa mke wako wa ndoa kabisa ( UNAWEZA KUMUOA KABISA MWANAMKE AMBAE AMEOLEWA NA JINNI MAHABA LAKINI NDOA YENU HAITADUMU NA ITAVUNJIKA KWA SABABU YA MUME KUTOKUWA NA UWEZO WA KUMTIMIZIA UNYUMBA MKE WAKE AU KINYUME CHAKE YANI MUME KUTOKUWA NA HAMU KABISA YA KUFANYA TENDO LA NDOA NA MUME WAKE )
3. KUKUSABABISHIA MARADHI NA MAGONJWA MBALIMBALI : Jinni mahaba anaweza kuamua kukusababishia maradhi mbalimbali ya kisheitwani ili ya kufanye uwe bize kutafuta tiba yake na kuachana na ‘mke wake’
4. KIFO : Baadhi ya majini mahaba hutoa adhabu ya kifo kwa wanaume wanao tembea na wanawake ambao majini hao wamewaoa. Majini hawa wanakuwa hawataki kushea ‘mke’ na wanaadamu na hutoa adhabu ya kifo ili kuwatisha wanaume wengine wasijaribu kumfuata mwanamke huyo.
Hali hii inapotokea wanaume huogopa kumfuata mwanamke huyo na mwanamke huyo husalia kuishi maisha hayo ya upweke ya bila kuwa na mume wala mpenzi katika siku zote za maisha yake. Wapo wanawake wengi tu ambao wamefungwa kwenye kifungo hiki.
Miaka ya tisini alikuwepo dada mmoja huko Chalinze ambae uzuri na urembo wake ulikuwa sio wa kawaida. Dada huyo alitoka katika familia ya kawaida na alifanya biashara ya kuuza chakula. Binti huyu ‘aliua’ madereva wengi sana wa malori yaliyo kuwa yakitoka Dar kwenda mikoani na nchi jirani. Kila mwanaume aliyejaribu kufanya mapenzi na dada huyo alifariki dunia baada ya wiki kadhaa. Hali hii ilizua taharuki sana miongoni mwa madereva hao na mwisho wa siku wote walimuepuka wakidhani amewekewa tego.
MWISHO WA SEHEMU YA KWANZA. KATIKA MAKALA YANGU YA KESHO NITAENDELEA NA SEHEMU YA PILI AMBAPO NITAELEZEA SABABU NYINGINE ZINAZO WAFANYA BAADHI YA WANAWAKE WAZURI KUPITA KIASI WASIOLEWE.
MAKALA HAYA YAMESIMULIWA NA DOKTA. MUNGWA KABILI. ANAPATIKANA KWA SIMU NAMBA 0744 - 000 473.