Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

JWTZ Yatangaza Ajira kwa Vijana

$
0
0
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kuandikishwa jeshini madaktari wa binadamu na fani nyingine za tiba.

Taarifa hiyo imetolewa jana tarehe 31, 2018 na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano JWTZ, Kanali Ramadhan Dogoli wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

“Nafasi hizo zinatolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika hospitali zetu, vituo vya afya na Zahanati kulingana na mahitaji ya sasa na siku zijazo,” alisema Kanali Dogoli.

Alisema watakao andikishwa Jeshini ni wale wenye taaluma za Doctor of Medicine, Doctor of dental sugery, bachelor of pharmacy, bachelor in laboratory science, bachelor of science in nursing, bachelor of science in physiotherapy na bachelor of science in prosthetics and orthotics.

Kanali Dogoli ametaja sifa za watu wanaohitajika kuandikishwa ikiwemo, mhusika awe na umri kati ya miaka 18 hadi 28 na mzaliwa wa Tanzania, awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa jela, awe na cheti halisi cha kuziliwa.

Pia, kama ni daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo na kutunukiwa vyeti pamoja na kusajiliwa na Bodi. Awe hajawahi kutumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.

Kanali Dogoli amesema   wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na JWTZ waripoti katika kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo, Mgulani Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2018 kuanzia saa moja asubuhi.

“Watakaochaguliwa na kuandikishwa jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya jeshi na yatakayo waendeleza katika taaluma zao. Wakiwa Jeshini majukumu watakayopatiwa ni yale yatakayowapachangamoto na fursa nzuri za kutumia taaluma zao,” alisema Kanali Dogoli.

Lugola Ampa Miezi Minne Lugumi....Akishindwa Atamtupa Mahakama ya Mafisadi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ametoa onyo kwa mfanyabiashara  Said Lugumi baada ya kumpa miezi minne ya kukamilisha makubaliano  ya mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, jijini Dar es Salaam jana Jumanne Julai 31, 2018 Waziri Lugola alisema kuwa mahakama  ya  kushughulikia kesi za rushwa iliyoanzishwa na Rais Dkt.Magufuli  bado haijapata wateja wakati ni wengi wanaoiba fedha za serikali.

“Mahakama ya kushughulikia kesi za rushwa inakosa wateja,na wanaoibia serikali wapo wengi mtaani,na kutokana hili  Saidi Lugumi nimempa miezi minne kukamilisha makubaliano ya mkataba na akishindwa atakuwa mteja wa mahakama hiyo” amasema Lugola.

Aidha Waziri Lugola aliongeza kuwa  mkataba unaomhusu mfanyabiahashara Said Lugumi  bado unafanyiwa uchunguzi na taasisi ya  kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) na baada ya uchunguzi hatua sitahiki zitachukuliwa.

Ikumbukwe kuwa mfanyabishara huyo aliingia katika msuguano na serikali mwaka 2016, ambapo kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) ilibaini ubadhilifu katika mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi chini ya Mkuu wa jeshi la polisi wakati huo Ernest Mangu.

Mkataba huo  ulisainiwa kwa ajili ya  kufungwa  kwa mashine za utambuzi wa alama za vidole (AFIS) kwenye vituo 108 kwa gharama  ya shilingi bilioni 37 ambapo kampuni hiyo ilifunga  mashine hizo kwenye vituo 14 tu.

Mfuko wa Pensheni wa PSSSF Kuanza leo.....Kabla ya PSSSF kuzaliwa kulikuwa na LAPF, GEPF, PPF na PSPF Ambayo Imeunganishwa

$
0
0
Serikali imetangaza rasmi kuanza kutumika kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumsihi wa Umma, PSSSF, kuanzia leo Agosti 1, mwaka huu huku sekta binafsi watasajiliwa katika mfuko wa NSSF, ambayo itatoa mafao na pensheni kwa wastaafu .

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, alisema, Serikali imekamilisha maandalizi yote muhimu ya utekelezaji wa Sheria ya matumizi ya mfuko wa PSSSF na imeridhika kwamba Mfuko huo unaweza kuanza kutekeleza majukumu yake.

"Napenda kutangaza rasmi kwamba, kwa mamlaka niliyonayo chini ya kifungu cha 1(1) cha Sheria ya PSSSF nimeteua tarehe 1 Agosti, 2018 kuwa ndiyo tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya PSSSF", alisema Mhagama.

Waziri Mhagama amesema kuwa Wanachama wote ikiwa ni pamoja na wastaafu na warithi waliopo katika mifuko inayounganishwa watahamishiwa katika mfuko wa PSSSF na haki na stahili zao zitaendelea kutolewa na mfuko huo bila kuathiriwa kwa namna yeyote ile.

Akizungumzia rasilimali, vitega uchumi, madeni, mifuko ya hiari na mikataba iliyokuwa chini ya mifuko inayounganishwa  Waziri Mhagama amesema itahamishiwa katika Mfuko mpya wa PSSSF. 


Pia Waziri Mhagama amewatoa hofu ya kupoteza ajira watumishi wote wa mifuko iliyounganishwa  kwa kuwa watahamishiwa katika mfuko mpya ambako uongozi wa mfuko huo utawapangia majukumu yao kwa kuzingatia muundo wa taasisi.

Kabla ya PSSSF kuzaliwa kulikuwa na mifuko mitano ya aina hiyo ambayo ni NSSF, LAPF, GEPF, PPF na PSPF lakini serikali kwa kutumia sheria mpya imeipunguza mifuko hiyo na kuweka utaratibu wa mifuko miwili ambayo sasa ni NSSF unaoshughulikia watumishi wa sekta binafsi na PSSSF ambao wanachama wake ni watumishi wa sekta za umma.

Uundwaji wa PSSSF kama chombo kipya kwa watumishi wa umma ulitokana na kitendo cha Rais John Magufuli kusaini sheria namba 5 ya Mifuko ya hifadhi ya jamii mwaka 2018, iliyosainiwa mwezi Februari iliyotaka mifuko yote kuwa na mwangalizi mmoja ili kuboresha maslahi ya wastaafu.

TLS Wamvaa RC Mnyeti Wakimtuhumu kwa Matumizi Mabaya ya Madaraka

$
0
0
Chama cha Wanasheria Tanganyika Law Society, kimelaani vikali kitendo kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti aliyetoa amri ya kukamatwa kwa mmoja ya wakili wao Menrad De Souza kitu ambacho ni kinyume cha Sheria ukizingatia hana mamlaka hiyo.
 
Akizungumza na Waandishi wa habari jana  jijini Dar- esa Salaam Rais wa chama hicho Bi Fatma Karume alisema juzi  mchana mkuu huyo wa mkoa alimkamata mwanasheria wa chama hicho pamoja na wateja wake waliokwenda ofisini ili kuingia mkataba baina ya wateja na wakulima ndipo mkuu wa mkoa alipotoa amri kwa polisi mwanasheria huyo na wateja wake wakamatwe na kuwekwa ndani kwa masaa 48 kwa amri ya mkuu huyo wa mkoa.

Alisema chama hicho kimelazimika kutoa taarifa hiyo kwani siyo mara ya kwanza kwa wakuu wa mikoa na wilaya kutoa amri watu kuwekwa ndani na polisi kwa masaa 48, hivyo chama hicho kinapinga matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi hao dhidi ya wananchi.

Fatma alisema hapa nchini hakuna mtu anayetoa hukumu ya mtu kukaa ndani isipokuwa Mahakama na hiyo ni baada ya kusikiliza pande zote mbili, hivyo wakuu wa wilaya na mikoa kutoa matamko ya kuwakamata watu ni sawa na kutoa hukumu jambo ambalo hawapaswi kufanya.

Alitumia fursa hiyo kueleza utofauti wa kisheria uliopo baina ya Zanzibar na Tanzania bara kwa kusema kuwa; "Zanzibar huwezi kukaa ndani kwa miezi 9 bila kuhukumiwa hapo utapata dhamana moja kwa moja, hapa bara watu wanakaa miaka 9 mpaka 10 na hii ndio tofauti ya Sheria za Tanzania Bara na Zanzibar".

Aliongeza kuwa ...." Kuna changamoto kubwa sana kwa mawakili wetu kukaa ndani kwa muda mrefu, tatizo ni Tanzania Bara na sio Visiwani, bunge la huku Tanzania bara likipitisha Sheria siyo kwamba kesi hii hakuna kupata dhamana basi ndo imepita hapanaa hii ni sheria ovu".

Kwa upande wake wakili msomi Jebra Kambole alisema wakili huyo amekamatwa akiwa anatimiza majukumu yake ya kikazi, na kwamba Wakuu wa mikoa wamekuwa wakitumia sheria vibaya kuwaumiza wananchi na watu wengine kinyume na sheria.

"Kuna sheria na matumizi mabaya ya sheria, kwahiyo Wakuu wa mikoa wamekuwa wakitumia vibaya sheria na matokeo yake wanawaumiza wananchi, waandishi wa habari na wengine" aliongeza wakili Kambole.

Zari: “Mimi Sio Level Zenu, Msiniringanishe na Vinuka Mkojo”

$
0
0
Baby mama wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amekuja juu na kumwaga povu zito siku ya jana na kuomba asilinganishwe na vinuka mkojo.

Povu hili la Zari limekuja siku chache baada ya kupishana Kauli na wasanii mbali mbali kutoka Bongo Movie ambao walitakiwa kwenda nchini South Africa kwa ajili ya birthday ya mtoto wa Diamond, Tiffah.
 
Zari aliwaambia wasanii kama Wema Sepetu, Aunty Ezekiel, Maimatha na kamati nzima ya Zamaradi kuwa hataki waende South Africa kwenye birthday ya Mtoto wake kwani watachafua nyumba yake.

Siku ya jana pia Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Zari aliwamwagia povu hili watu ambao hakuwataja majina lakini hakutaka kulinganishwa nao.

"Ati sijui A or B, mimi sio level zenu I worked hard for my name, Am not a social climber. Hatuuzi sura tu, tunapambana na  msiniringanishe na vinuka mkojo vwenu, mxiuuu.”.

Maofisa wa Marekani Wadai Korea Kaskazini Bado Inaendelea Kuunda Makombora Mapya

$
0
0
Korea kaskazini inaonekana kuwa inaunda makombora mapya licha ya kuidhinisha uhusiano mwema na utawala wa Trump, vyombo vya habari vinaripoti.

Satelaiti za kijasusi zimegundua shughuli zinazoendelea katika eneo ambako kumetengezwa makombora ya masafa marefu, maafisa wa Marekani wameliambia Washington Post.

Shirika la habari la Reuters linamnukuu afisa huyo akisema kuwa haijulikani wazi ni kwa kiwango gani shughuli hiyo imeendelea.

Rais Donald Trump amekutana na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un mnamo Juni. Baada ya mkutano wa kwanza, viongozi hao wawili waliahidi kushughulika kuhakikisha wanasitisha matumizi ya silaha za nyuklia. Trump alisema Korea kaskazini, 'sio tishio tena la nyuklia'.

Lakini Trump alishutumiwa nyumbani kwa 'kuafikiana kwa mdomo' pasi kufikia makubalino madhubuti kutoka kwa Kim ya kusitisha mipango na matumizi ya nyuklia.
 
Siku ya Jumatatu gazeti la Washington Post limewanukuu maafisa wanaosema Korea kaskazini inaeonekana kuunda kombora moja au amawili ya masafa marefu katika kiwanda cha Sanumdong karibu na mji mkuu Pyongyang.

Kiwanda hicho kiliunda kombora la kwanza la masafa marefu la nchi hiyo lililo na uwezo wa kufika Marekani, gazeti hilo linaongeza.

Kwa mujibu wa Reuters, picha za satelaiti, zinaonyesha magari yakiingia na kutoka kwenye kiwanda hicho , lakini sio kiwango cha ujenzi huo wa makombora.

Hizi sio taarifa za kwanza kuwa Korea kaskazini huenda inaendelea na uundaji wa mpango wake wa silaha, na kutilia shaka athari halisi ya mkutano wa Singapore.

Mwishoni mwa mwezi Juni vyombo vya habari Marekani viliangazia taarifa zinazotokana na uvujaji wa taarifa za ujasusi zinazoashiria kuwa kaskazini ingali inaendeleza shuguli zake za kurutubisha nyuklia katika viwanda vyake miongoni mwa shughuli nyingine.

Wiki iliyopita Mike Pompeo amewaambia Maseneta kuwa viwanda vya Korea kaskazini "vinaendelea kurutubisha kemikali za nyuklia" zinazotumika kuunda silaha.

Chanzo: BBC

Mradi Wa Kusambaza Gesi Asilia Majumbani Wafikia Asilimia 76

$
0
0
Meneja Mradi wa usambazaji wa gesi majumbani  Dar es Saaalam, Denice Byarushengo, amesema kazi ya kusambaza mabomba ya gesi asilia kwa wananchi imekamilika kwa asilimia 76.8.

Byarushengo alisema hayo jana wakati akimueleza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC), Kapuulya Musomba kuhusu hatua ambazo mradi huo umefikia.

Byarushengo alisema mradi huo unalenga kuunganisha kiwanda cha Coca Cola Kwanza Ltd. na Kiwanda cha Mafuta cha BIDCO   na wateja   takribani 1000 wa majumbani.

Alisema kazi hiyo pia imekwenda sambamba na kusimika  mtambo wa kupunguza mgandamizo ambao nao  umekamilika kwa asilimia 97.

“Uunganishaji wa mabomba umekamilika kwa asilimia 88.6, ulazaji na ufukiaji wa mabomba umekamilika kwa asilimia 56.9.

“Viainisho sita  vya bomba linapopita vimeshawekwa na ujenzi wa daraja  la waenda kwa miguu umekamilika kwa asilimia 90,”alisema Byarushengo .

Alisema  mradi huo utahusisha kuvuka mto Ubungo   na  barabara ya Ubungo Maziwa na ya Mandela, kazi  ambayo hadi sasa imekwisha kukamilika.

Alisema kwa   barabara ya Ubungo Maziwa kazi  imekamilika kwa asilimia 50, huku kwa barabara  ya Mandela kazi iko mbioni kuanza.

Alisema mradi huo utawezesha upatikanaji wa gesi asilia ya kutosha katika bomba linalotoka  Ubungo kwenda Mikocheni kupitia barabara ya Sam Nujoma  na kusambaza gesi kwa wateja wa majumbani katika maeneo ya Ubungo, Shekilango, Mlalakuwa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza na Mikocheni.

Musomba alieleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao utaunganisha bomba kubwa la gesi asilia la urefu wa kilomita 7.8  na lile la Ubungo kwenda Mikocheni   na uwezo wa kusafirisha  gesi ya  futi za ujazo milioni 7.5    kwa siku.

Naibu Meya Manispaa ya Ilala Ajiuzulu

$
0
0
Diwani wa Kata ya Vingunguti (CUF), Omary Kumbilamoto ambaye pia ni naibu meya wa manispaa ya Ilala amejizulu uanachama wa chama hicho.

Amechukua uamuzi huo jana Julai 31, 2018 huku akieleza kuchoshwa na mgogoro wa uongozi unaoendelea ndani ya CUF.

CUF kimekumbwa na mgogoro tangu mwaka 2016 baada ya kurejea kwa Profesa Ibrahim Lipumba ambaye mwaka 2015 alijiuzulu uenyekiti wa chama hicho kutokana na kutofautiana na viongozi wenzake.

Kumbilamoto  ameufananisha mgogoro huo wa CUF na mvutano wa mataifa ya Palestina na Israel, akieleza kuwa hauna suluhu na unamfanya ashindwe kuwatumikia ipasavyo wananchi wa Vingunguti.

Amesema amekuwa akipewa vitisho vya kufukuzwa uanachama kwa sababu ya hatua yake ya kuwa karibu na viongozi wa Serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Amesema wakati kata ya Vingunguti ikikumbwa na mafuriko,  hakuna kiongozi yoyote  wa CUF aliyekwenda kutoa msaada isipokuwa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam.

“Sikuletewa hata kijiko na viongozi wangu wa chama  lakini viongozi wa Serikali walinisaidia. Hata hivyo, upande chama kinadai mimi ni msaliti kutokana na ushirikiano ninaoupata,” amesema Kumbilamoto.

Amesema wakati wowote atafanya mkutano wa hadhara wa kueleza wa wananchi wa kata hiyo wapi atakapoelekea kwa ajili ya kufanya shughuli za kisiasa.

Credit: Mwananchi

Mpina Aja Na Mikakati 15 Ya Mapinduzi Makubwa Kwenye Sekta Ya Mifugo Na Uvuvi

$
0
0
Na John Mapepele
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua mikakati 15 itakayotumika kama nyenzo ya kusimamia utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo na kuleta mageuzi makubwa na ya muda mfupi kwenye sekta za mifugo na uvuvi kabla ya kumalizika awamu ya kwanza ya utawala wa Serikali ya awamu ya tano mwaka 2020.

Mikakati hiyo ni pamoja nakudhibiti magonjwa ya mifugo chanjo na viatilifu, mpango kazi wa kudhibiti upotevu wa mapato yatokanayo na biashara ya mifugo na mazao yake, mkakati wa usimamizi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi nchini, mkakati wa upatikanaji wa uhakika wa malisho na maji kwa ajili ya mifugo pamoja na mkakati wa kuboresha na kuzalisha kwa wingi ng’ombe wa nyama na maziwa kwa njia ya uhimilishaji.

Mwingine ni mkakati wa kudhibiti na kuondoa migogoro baina ya wakulima, wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi, mkakati wa kuboresha uzalishaji wa kuku,mkakati wa kuanzisha na kuwezesha ushirika wa wafugaji, mkakati wa kuendeleza ukuzaji wa viumbe kwenye maji pamoja mkakati wa kufufua Shirika la Uvuvi nchini TAFICO

Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kuzindua mikakati hiyo, Waziri Mpina ameiagiza wizara hiyo kuunda kikosi kazi kitakachosimamia utekelezaji wake na kwamba kila baada ya miezi mitatu kufanyike tathmini na kwa watumishi wataoshindwa au kukwamisha utekelezaji wa mikakati hiyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria,Kanuni na taratibu.

Alisema mikakati hiyo ikikamilika Serikali itaweza kukusanya zaidi ya sh bilioni 100 kwa mwaka zitokanazo na sekta za mifugo na uvuvi tofauti na sh bilioni 30 zilizokusanywa katika kipindi cha mwaka 2016/2017 ambapo kwa mwaka 2017/2018 Serikali imeweza kukusanya sh bilioni 46 baada kufanyika Operesheni Sangara na Nzagamba.

Hivyo Waziri Mpina alisisitiza kuwa utoroshaji wa mazao ya mifugo nje ya nchi, uvuvi haramu,mifugo kufa kwa kukosa tiba sahihi za magonjwa kwa wakati havitapata tena nafasi chini ya uongozi wake huku ulinzi wa rasilimali za mifugo na uvuvi ukiimarishwa kwa kuweka vizuizi katika njia zote zilizobainika kuhusika na utoroshwaji huo.

Alisema udhibiti wa magonjwa ya mifugo utawezesha kuongeza uzalishaji kuanzia ndege wafugwao, mbuzi, kondoo,ng’ombe na kuchochea uwekezaji katika viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo hapa nchini na kuwezesha upatikanaji wa ajira,kodi na upatikanaji wa bidhaa za mifugo kwa gharama nafuu.

Waziri Mpina alisema ni aibu kwa Taifa ambalo asilimia 37 ya nchi yake ni maji na yenye uoto wa asili mzuri lakini tunashuhudia mifugo ikidhoofika na mingine hata kufa kwa kukosa maji na malisho hivyo mkakati huo utatoa majawabu ya changamoto hiyo.

Pia alishangazwa na kitendo cha baadhi ya watu wakihodhi mashamba ya mifugo ya Serikali waliobinafsishiwa na kubadilishiwa matumizi na kwamba kwa miaka mingi wameshindwa kuendeleza mashamba hayo hivyo Serikali itayataifisha yote na kurejeshwa serikalini ili yatumike kulishia mifugo.

Pia mikakati hiyo itamaliza kabisa tatizo la wafugaji kukosa haki ya kupata malisho kutokana na migogoro ya ardhi huku akitolea mfano mnada wa Pugu wenye ukubwa wa ekari 1,900 lakini sasa zimebaki ekari 108 tu baada ya wananchi wengi kuvamia eneo la mnada na kugeuza makazi.

Waziri Mpina alisema mikakati hiyo ndio itakuwa mwarobaini wa matatizo yote yaliyokuwa yanakabili sekta ya mifugo na uvuvi , na kuziagiza halmashauri zote nchini nazo zishiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mikakati ili kuiwezesha sekta ya mifugo na uvuvi kutoa mchango unaostahili katika pato la taifa.



Hivyo Wizara itaandaa mafunzo kwa maofisa Mifugo na Uvuvi kutoka katika halmashauri zote nchini mwezi Agosti ili kuwawezesha kuufahamu mkakati huo na kuutekeleza kwa umakini na kwa wakati.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu-Mifugo, Celina Lyimo alisema kuandaliwa kwa mikakati hiyo ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mpina alilolitoa Julai 6 mwaka huu la kutaka kuandaliwa mikakati ya kuwezesha kuwepo mageuzi katika sekta hizo na kuwataka watumishi wa wizara hiyo kuifanyia kazi kwa wakati weledi na uadilifu ili kupata matokeo chanya katika kipindi kifupi.

Naye Kaimu Katibu Mkuu-Uvuvi, Julius Mairi alisema mikakati hiyo itawezesha sekta za mifugo na uvuvi kuwezesha kuongeza pato la Taifa na mtu mmoja mmoja na kumshukuru Waziri Mpina kwa uongozi wake thabiti uliolenga kuona kunakuwepo mageuzi ya haraka kwenye sekta hizo.

Makamu wa Rais Akerwa na Wakurugenzi Wanaotumia Vibaya Pesa za Serikali

$
0
0
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amesema anashangazwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali na wasaidizi wao kuendelea kufuja fedha za halmashauri zao licha ya maneno mengi ya kukemea hali hiyo.

Akizungumza baada ya kuapishwa viongozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatano Agosti Mosi, Mama Samia pia amewataka wakuu wa mikoa, makatibu tawala na makatibu wakuu kufanya kazi kwa kusimamia kiapo walichoapa na kuendeleza uhusiano mzuri kwa watakaowakuta maofisini mwao.

“Mnapokwenda huko mfanye kazi sambamba na ilani ya chama (Chama Cha Mapinduzi), hatutegemei tukizunguka hukio tukute mivutano.

“Halmashauri huko chini kuna mapato mengi ya kukusanywa lakini hayakusanywi ipasavyo na mengine yanakusanywa kinyume cha sheria.

“Mimi nashangazwa katika halmasahuri wakurugenzi na wasaidizi wao wanafuja fedha pamoja na yote tunayozungumza lakini bado huku chini kuna wanaume wanafuja fedha,” amesema Mama Samia.

Pamoja na mambo mengine, Mama Samia amewataka wakuu wa mikoa kusimamia na kutekeleza ilani ya CCM katika kutekeleza majukumu yao.

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Kusinyaa Na Kudumaa Kwa Maumbile Ya Kiume

$
0
0
Wanaume  wanao  jihusisha  na  upigaji  wa  punyeto  kwa  muda  mrefu  husalia  kuwa  na  maumbile  ya  kiume  yaliyo  sinyaa  na  kudumaa.

Kwa mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, kufanya  punyeto  kwa  muda  mrefu  huathiri  na  kuharibu  mishipa  na  misuli  ya  uume na  hivyo kusababisha  kujengeka  kwa  mafuta na  tishu  zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri na  hivyo  kuzuia  mishipa ya  ateri  kupanuka na  kuongezeka  pamoja  na  damu  kutiririka  kwenda  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili yanapotokea  huathiri  uzalishaji  wa homoni muhimu  zinazo  husika  na ukuaji wa misuli ya  uume, na hatimaye  hufanya  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa, kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama wa  mtoto.

 Homoni  hizo hujulikana   kitaalamu kama  HGH  na  huzalishwa  kwenye  ini.

Sababu nyingine   inayo  tajwa  na  wataalamu  ni kwamba, mtu  anaye fanya punyeto   hutumia  akili,  nguvu na  nishati  nyingi sana, jambo ambalo  huathiri utendaji  wa  ogani  nyingine  muhimu  katika  mwili , likiwemo  ini.

Na kwamba  ini  linapo kosa  nishati   ya kutosha  hushindwa  kufanya kazi  zake  vizuri  na  moja  kati  ya  kazi kubwa  za  ini  ni  pamoja  na  uzalishaji  wa  homoni  zijulikanazo  kitaalamu kama  HGH  ambazo  kama  ilivyo andikwa  hapo juu, zinahusika na  kuchochea  ukuaji  wa  sehemu mbalimbali  katika  mwili  wa  mwanadamu  ikiwemo   misuli  ya  uume.

Mbali na  kuathiri  utendaji  wa  ogani  nyingine  mwilini, upigaji  punyeto  husababisha  athari nyingine  kwenye  mwili wa  mwanadamu  kama  vile uchovu  sugu  wa mwili  pamoja na kunyonyoka kwa  nywele.

Athari nyingine  za  upigaji punyeto  ni  pamoja  na  kupoteza  kumbukumbu, kuwahi  kufika  kileleni  ambako  husababishwa  na  kulegea  kwa  mishipa  ya  ateri, kushindwa  kurudia  tendo  la  ndoa, kukosa  hamu  ya  tendo  la  ndoa, uume  kusimama  katika  hali  ya  ulegelege,   maumivu  wakati  wa  tendo  la  ndoa  husuani  wakati  wa  kurudia  tendo  la pili na    mara  baada  ya  tendo  la  ndoa  la  kwanza.

KWANINI   WATU WENGI  WANAO  JIHUSISHA  NA  UPIGAJI  PUNYETO  WANA  MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME YALIYO  DUMAA, SINYAA  NA  KURUDI NDANI.

Uzeofu  unaonyesha  kuwa,  asilimia  kubwa  ya  wanaume  ambao  wamewahi  kufanya  punyeto  kwa  muda  mrefu, wanakabiliwa  na  tatizo  la kuwa  na  maumbile  ya  kiume yaliyo dumaa, sinyaa  na  kurudi ndani.

SABABU  KUBWA   NI  HII  HAPA
Sababu  kubwa  ni kwamba   vijana wengi  wa  kiume, huanza  kujihusisha  na  punyeto   wakiwa  na  miaka  kumi  na sita , kumi na  saba  au  chini  ya  hapo.

Hiki ni  kipindi  ambacho  vijana  hawa  ndio  wanakuwa  wamebalehe.

Na kwa mujibu  wa  tafiti  za kisayansi, katika  kipindi  hiki cha  balehe  ndio  kipindi  ambacho  homoni za  HGH  ambazo huhusika  na  ukuaji  wa  sehemu  mbalimbali  za  mwili  ikiwemo  maumbile ya  kiume, huzalishwa  kwa wingi.

Kama  tulivyo ona  hapo  juu, upigaji  punyeto  huathiri  uzalishwaji  wa   homoni  hizo.

Mwisho wa  siku  maumbile  ya  kiume  ya  wahusika, hushindwa  kukua  na  kuishia  kudumaa na  kusinyaa.

Na  hii ndio  sababu  kubwa  wanaume  wanao  kabiliwa  na  tatizo  hili  husalia  kuwa  na  maumbile yenye  ukubwa  ule  ule  walio kuwa  nao wakati wa  kubalehe

NINI  TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  LA  KUDUMAA, KUSINYAA  NA  KURUDI NDANI KWA  MAUMBILE  YA  KIUME.
Kama uume wako  umedumaa, sinyaa, legea, nywea  na  kurudi ndani  kwa  sababu  ulifanya  punyeto  kwa  muda  mrefu  na  unataka  kuondokana  na  hali  hiyo. HII  NI HABARI NJEMA  SANA  KWAKO! 
 
Ipo dawa  ya ASILI   ambayo  HUTIBU  na  KUPONYESHA  KABISA  tatizo la  KUDUMAA, KUSINYAA, KUNYWEA  NA  KURUDI NDANI  KWA MAUMBILE  YA  KIUME kunako  tokana  na  ufanyaji  punyeto  wa  muda  mrefu.
 
Ni  dawa  ya  asili  kabisa ambayo  hutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la kudumaa  na  kusinyaa  kwa  uume  ndani ya siku thelathini.

JINSI YA  KUPATA  TIBA  HII : Kupata  tiba  hii  fika  ka6ika  duka  la  kuuza  dawa  za  aslili  la  NEEMA  HERBALIST.  Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa wateja  waliopo  jijini  Dar  Es  Salaam  ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu  watapelekewa  dawa  mahali  walipo  ( HOME & OFFICE  DELIVERY )  na kwa  wateja  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabus  au  boti  kwa  waliopo  Zanzibar.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  :    0693  005 189.

Jeshi la Polisi Lasema Mbwa Aliyedaiwa Kupotea Alikuwa Kwenye Mafunzo

$
0
0
Mbwa wa kazi maalum za Bandari ya Dar es Salaam anayedaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha, alikuwa kwenye mafunzo bwalo la Polisi.

 Hayo yameelezwa leo Agosti Mosi na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa katika mkutano na wanahabari. Amezungumza hayo huku ukumbini hapo kukiwa na mbwa wawili wa polisi, akiwamo anayedaiwa kutoweka.

Amesema kulikuwa na mkanganyiko na hakuna mbwa aliyepotea.

“Tunataka kuwaambia kuwa mbwa huyo alikuwa kwenye mafunzo ya bwalo la Polisi na mbwa aliyekuwa hayupo siyo hobi,” amesema Mwakalukwa na kuongeza:

“Mbwa wote wapo hakuna hata mmoja aliyetoweka huwa wanaenda kwenye kazi na kurudi.”

 Julai mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alimpa saa saba Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) Simon Sirro kuhakikisha mbwa huyo anarudi bandarini baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Rais Magufuli Awaapisha Viongozi Aliowateua......Asema Ilimlazimu Kukaa na Majina yao Miezi Minne Akiwachuja

$
0
0
Rais John Magufuli, amewaambia Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Makatibu Wakuu alikaa na majina yao kwa muda wa miezi mine kabla ya kuwateua kushika nafasi hizo.

Akizungumza baada ya kuwaapisha viongozi hao leo Jumatano Agosti Mosi, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewataka viongozi hao kutambua ni Mungu ndiye amewachagua.

“Nimekaa na majina yenu zaidi ya miezi minne, wengine wamepungua wengine wameongezeka.

“Tanzania ni kubwa mno, mimi sikufaa kuwa rais, ni Mungu alitaka na ndiyo sababu siwezi nikasimamam nikajisifu, ni Mungu alitaka vile vile Makamu wa Rais.

“Hata Waziri Mkuu… kwanza hata sijui nilimchaguaje, kwa sababu kuna watu walikwenda Dodoma na suti wameshona ili wawe Waziri Mkuu, lakini Majaliwa (Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa) ni Mungu aliamua awe Waziri Mkuu, vivyo hivyo katika nafasi zenu,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli pia amesema nafasi hizo kwa viongozi hao, zimepangwa na Mungu ambaye alitaka wazipate ambapo wakiamini hivyo kila mmoja katika nafasi yake atatenda haki kwa wakati wake.

“Wengine wanasema nimechagua wapinzani, nani mpinzani Tanzania hii, Kafulila (David Kafulila, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe) mtasema ni mpinzani.

“Alipokuwa huko alipigania suala la IPTL, akaitwa tumbili leo umteue useme umeteua mpinzani, huyu si mpinzani ni mpiganaji wa serikali yake,” amesema.

Mizizi 29 Power ,ndio Dawa Bora Na Imara Kwa Sasa Kwa Kutibu Na Kuponesha Tataizo La Nguvu Za Kiume Kwa Dakika 30 Tu

$
0
0
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume limekuwa ni janga kubwa sana kwa sasa sio vijana au wazee wanalalamiki kukimbiwa na wa wapenzi wao au ndoa kuvunjika kutokana na mwanaume kulala na mwanamke kitanda kimoja hata wiki mbili bila kushiriki tendo la ndoa na hii ndio inachangia wanawake wengi kutoka nje ya ndoa kwa nini huteseke na wakati dawa zipo ambazo zitarudisha heshima yako ya ndoa 

MIZIZI 29 POWER; ni ambayo hutibu na kurudisha virutubisho mwilini ambavyo humfanya mwanaume awe na matatizo yafatayo 1 kuwahi kukojoa kabla mke au mpenzi wake

 2. kushindwa kurudia tendo dawa, hii itakufanya kurudia tendo zaidi ya Mara tatu 

3... dawa hii inatibu uume uliolegea na kusinyaa 

4. dawa hii inatoa miungurumo ya tumbo na uchovu wakati wa kumaliza tendo 

NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupiga punyeto kwa mda mrefu 
2 upungufu wa vichochoe mwilini 
3 magonjwa ya moyo, kisukari, presha, vidonda vya tumbo kiuno na mgongo 
4 utumiaji ovyo wa madawa ya kizungu 
4 usongo wa mawazo, hasira, tumbo kujaa gesi na kutopata choo.

 PATA TIBA YANGU NA NI TOFAUTI NA ULIZO WAHI KUTUMIA: 

Je una uume mfupi na mwembamba? MASHESHA MIX ni dawa ya kuboresha uume saiz upendayo asa kwa wale waliofanyiwa tohara wakiwa wadogo.. chagua saizi upendayo inch 5,6,7, adi 8 iyo ni kwa urefu na unene sentimita 2,3,4, adi 5 .dawa hizi zipo za kupaka na kunywa na hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ,

Tunatibu kisukari,vidonda vya tumbo,ngiri, korodani iliyovimba, kupnguza kitambi, maziwa makubwa NK 

KWA TIBA NA USHAULI FIKA OFISINI KWANGU DARE S SALAAMU MBAGALA ZAKHEMU NA MIKOA YA KANDA YA ZIWA YUPO WAKALA WETU HAPO MWANZA NA KWA AMBAO HAWANA NAFASI YA KUJA OFISINI HUDUMA YETU UTALETEWA POPOTE ULIPO PIGA SIMU 0783185060 DR MAKOYE

Watetezi Haki Za Binadamu Walaani Mnyeti Kumtupa Selo Wakili

$
0
0
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umelaani kitendo cha kushikiliwa kwa Wakili Menrad D’Souza na wateja wake kwa amri ya Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti juzi Julai 30, mwaka huu.

Mratibu wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa amesema kitendo hicho ni ukandamizaji wa haki na uvunjwaji wa katiba ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Agosti Mosi, Jijini Dar es Salaam Olengurumwa amesema kuwa hawakufurahishwa na kitendo hicho hivyo wanalaani kwa nguvu zote na kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kufanya kazi kwa mujibu wa katiba.

“Wakili huyo alifungiwa katika chumba kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa Manyara juzi, kutokana na madai ya kushinikiza wakili na wateja wake waweze kuwasiliana na wakurugenzi wa wateja hao ili wakubali kuongeza kiasi cha fidia kwa wakulima katika mgogoro wa mbegu kati yao na wateja wa wakili D’Souza.

“THRDC kama mwavuli wa watetezi wa haki za binadamu inatambua kuwa mawakili ni watetezi wa haki za binadamu na wanafanya kazi zao za utetezi kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na nchi,” amesema.

Kutokana na hilo, ameshauri kwamba ikitokea kuna wakili viongozi anadhani amekiuka maadili ya kazi yake basi atoe taarifa kwa chama cha mawakili au mahakama.

Pia kwa mawakili amewasihi  kupitia vyama vyao wasimame kwa umoja na kulinda Uhuru wa kazi ya mawakili na utawala wa sheria hapa nchini.

Sambamba na hilo, Mratibu huyo amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuacha kutumia madaraka yao chini ya kifungu cha 15 na 17 cha sheria ya Tawala za Mkkoa ya mwaka 1996 kwa kutoa amri ya kuwakamata watu na kuwaweka vizuizini bila sababu za msingi za kisheria kwani vitendo hivyo vimekuwa vokijirudia mara kwa mara.

Stiggler’s Gorge Kuendesha Treni Ya Umeme

$
0
0
Waziri wa Nishati,  Dk. Medard Kalemani, amesema umeme wa mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge ndiyo utatumika kuendeshea treni mpya ya umeme.

Dk. Kalemani ameyasema hayo leo Mjini Morogoro, kwenye kikao cha mawaziri na makatibu wakuu ambao wizara zao zinatekeleza mradi huo.

“Mradi huu  utazalisha Megawati 2,100 na ndiyo utakaotumika kuendeshea treni ya kisasa ya umeme ya  Standard Gauge.

“Hivyo tumekutana hapa kujadili taarifa ya wataalamu kuhusu mradi, kutafakari changamoto na kuzifanyia kazi pamoja na kutembelea eneo la mradi,” amesema Dk. Kalemani.

Pia Waziri huyo wa Nishati, amesema Serikali itachukua hatua za kisheria kwa yeyote atakayekwamisha uwekezaji wa mradi huo ambao unahusisha wizara 11.

Kikao hicho kimewakutanisha watalaamu na viongozi wengine mbalimbali wakiwamo  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba.

ACT-Wazalendo Wamvaa Kangi Lugola

$
0
0
Chama cha ACT-Wazalendo kimemtaka kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe kuendelea na majukumu yake kama kawaida kwa kuwa agizo lililotolewa na Waziri wa mambo ya Ndani Kangi Lugola halina nguvu kisheria.

Jana Lugola alimtaka Zitto kujisalimisha kwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi kwa kile kilichoelezwa alitoa maneno ya kichochezi wakati wa mkutano wa hadhara kati yake na Mbunge wa Kilwa Kusini(CUF), Seluiman Bungara 'bwege'.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho,Ado Shaibu ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti Mosi 2018 wakati akizungumza na wanahabari.

Amesema wanasheria wa chama wamelipitia kwa undani tamko hilo la Lugola na kujiridhisha kuwa lina makosa na halina nguvu kisheria.

"Wanasheria wa chama wamejiridhisha pasipo shaka na kugundua kuwa Lugola amekurupuka kutoa tamko lile.Lugola katumia siasa kutoa tamko lile na siyo kufuata sheria.

“Zitto akiitwa kisheria ataenda kuripoti polisi na hatuna sababu ya kuogopa.Zitto ni kiongozi mbunge akiitikia wito huu wa Lugola atakuwa hajiheshimu, "amesema Shaibu.

Shaibu amesema hakuna kosa lolote ambalo Zitto amelitenda katika mkutano ule, lakini Lugola amekuwa na makeke katika kutoa matamko yake.

“Yaani tumetesti mitambo mara moja tu, pale Kilwa kwa kumpandisha jukwaani Zitto imekuwa nongwa watu wanalipuka? Hatuwezi kuvumilia hali hii,"amesema.

Viwanja Vianuzwa......Surveyed plots for sale: Mapinga (Baobab Sec, km 5 kutoka Bunju-DSM)

$
0
0
Surveyed plots for sale: Mapinga (Baobab Sec, km 5 kutoka Bunju-DSM)...
Viwanja ni vikubwa sana (Low density & Medium densiy plots). Viwanja viko umbali wa km 2.5 kutoka main road (Bagamoyo Road).
Ziko plots za sqm 3000, sqm 2400, sqm 1500, sqm 1400, sqm 1200, sqm 900, na sqm 800
 
Bei ya kila sqm ni sh 13,000 (negotiable)
Huduma za kijamii (maji, umeme) zipo na miundombinu yote iko vizuri (mradi wa kusogeza lami mpaka nyumbani umeanza). Ramani zote (Town plan & Deed plan) zipo tayari. Hati ya miaka 99 itapatikana ndani ya mwezi mmoja tu.
 
hakuna dalali, contact mhusika: call 0758603077, whatsap 0757489709

Rais Magufuli Awataka Viongozi wa Jiji la Dar es Salaam Wajitafakari

$
0
0
Rais John Magufuli, amewataka viongozi wa Jiji la Dar es salaam,  kujitafakari katika utendaji kazi wao kwani imeonekana kukwama katika sekta mbalimbali ikilinganishwa na majiji mengine.

Kauli hiyo ameitoa leo katika hafla ya uapishwaji wa viongozi walioteuliwa wakiwamo Wakatibu wa Wakuu wa wizara mbalimbali, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala iliyofanyika Ikulu jijini.

Rais Magufuli amesema kumekuwa na ‘upigaji’ mkubwa huku viongozi wakiangalia bila kuchukua hatua zozote.

“Juzi nilikuwa naongea na mabalozi, nikawaambia Dodoma ndiyo inaongoza katika majiji, manispaa, wilaya Tanzania nzima hivyo unaweza ukajiuliza kuna nini unaweza ukajua hapa Dar es salaam kuna upigaji na viongozi wapo,” amesema Magufuli.

Amesema viongozi wa Dar es salaam wakikutana kwenye vikao wanakaa siku mbili lakini zitajazwa ni siku nne hivyo kwa namna hiyo hawawezi kupata mapato kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

“Utakuta hata wamachinga wanasimama barabarani hawana mahali pa kufanyia biashara, wakina mama wamedhulumiwa lakini viongozi wapo hivyo nataka niwaambie viongozi mlioteuliwa hakuna mwenye garantii ya kazi,” amesema Rais Magufuli.

Pacha walioungana tumbo Jijini Mwanza Wafariki Dunia

$
0
0
Watoto pacha walioungana tumboni na kifuani waliolazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza wamefariki dunia leo Agosti Mosi.

Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Abel Makubi amesema watoto hao wamefariki kwa tatizo la upumuaji.

Pacha hao walizaliwa Julai 25 katika Hospitali ya Sekotoure na baadaye wakapelekwa Hospitali ya Bugando, walikolazwa ICU.

Akizungumzia hali za pacha hao wiki iliyopita Dk Makubi alisema watoto hao Angelina Ramadhani (34) mkazi wa Nyakato jijini Mwanza, wameungana sehemu ya kifua na tumbo.

 “Baada ya jopo la madaktari kuwafanyia uchunguzi, limebaini kwamba wanachangia moyo mmoja, mshipa mmoja unaorudisha damu kwenye moyo (inferior venacava), ini moja na kwamba viungo vilivyobaki kama mapafu, figo, tumbo kila mtoto ana vyake.”amesema Dk Makubi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>