Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mwakyembe: Vazi la kitenge liruhusiwe bungeni

$
0
0
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (pichani) amepeleka rasmi katika Kamati ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, maombi ya kutaka Bunge kuruhusu wabunge wanaume kuvaa mashati ya vitenge, batiki na nyinginezo za asili ndani ya Bunge.

Hatua hiyo itaondoa sheria ya wabunge wanaume kuvaa suti, jambo linalowafanya kupata shida pale vipoza upepo vinaposhindwa kufanya kazi. 

Mwakyembe alisema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya sanaa na utamaduni iliyoadhimishwa ndani ya uwanja wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa suala hilo likipitishwa na Bunge, litachochea kuongeza utengenezaji wa mavazi hayo pamoja na wajasiriamali kuwa wabunifu zaidi.

Alisema hatua hiyo itakwenda sambamba na uvaaji wa mavazi yenye rangi za taifa, hivyo maombi yakipelekwa na kukubalika yatachochea sanaa nchini. 

Dk Mwakyembe alisema kazi za sanaa na utamaduni katika maonesho ni fursa ya wanasanaa kuonesha ubunifu na vipaji walivyonavyo huku akibainisha siku kama hiyo mwakani wataitangaza zaidi ili kupata washiriki kutoka nchi nzima.

Alisema tamasha kubwa la sanaa katika nchi za Afrika Mashariki linalotarajiwa kufanyika Septemba au Oktoba mwakani, litafanyika katika viwanja hivyo, wataanza kujipanga ili kuangalia namna watakavyofanya kutokana na ukubwa wa uwanja huo.

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya alisema maonesho ya mwaka huu yamefana katika sanaa kwani zamani watu walikuwa wanakusanya vya nje ya nchi na kuuza lakini sasa nyingi zimetengenezwa na watanzania wenyewe. 

Awali Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Edwin Rutageruka alisema wameamua kuwa na siku hiyo kwa ajili ya kutangaza sanaa za Tanzania huku akitaka wanautamaduni na wadau wa sanaa kutumia uwanja huo kwa shughuli mbalimbali.

Mke akatwa kiganja, mume akiporwa fedha za vicoba mil 4/-

$
0
0
WAKAZI wa Kijiji cha Korotambe wilayani Tarime mkoani Mara, ambao ni mtu na mkewe wamejeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, ambao pia wamewapora Sh milioni nne, walizokuwa wanatunza kwa ajili ya kikundi chao. 

Joseph Makonyo (81) na mke wake, Robhi Makonyo (54), walikumbwa na mkasa huyo mjini hapa juzi baada ya kuvamiwa na majambazi hao majira ya saa moja usiku waliokuwa na silaha zikiwemo za jadi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Korotambe, Anthony Mwita, katika tukio hilo, Rhobi alikatwa kiganja cha mkono na majambazi hao. Alisema majambazi hao walivamia nyumba ya Makonyo na kumkuta akiwa na mkewe wakiwa jikoni, ambapo ghafla walianza kushambuliwa huku wakilazimishwa watoe fedha zote walizonazo za kikundi.

Mume ndiye aliyekuwa na fedha hizo. Mwita alisema majambazi hao walichukua fedha hizo, lakini tayari walikuwa wameshawajeruhi vibaya wanandoa hao, kwa kuwakata mapanga katika miili yao na Rhobi alikatwa kiganja chake cha mkono. 

Alisema wawili hao walipiga kelele za kuomba msaada, ndipo wananchi walijitokeza, lakini tayari majambazi hao walishakimbia na fedha hizo.

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa baada ya kuwasili eneo la tukio, Rhobi ambaye kiganja chake kilikuwa sakafuni, alikimbizwa katika Hospitali ya wilaya Tarime na mumewe na kupatiwa huduma za matibabu na baadaye walihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza baada ya hali zao kuwa mbaya.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime Rorya, Henry Mwaibambe alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa polisi inaendelea na uchnguzi, ikiwa ni pamoja na kuwasaka watuhumiwa. 

Aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kuwakamata watuhumiwa hao waliohusika katika uhalifu huo wa unyang’anyi na kuwajeruhi vibaya wakazi hao.

Madereva Dar Watakiwa Kuzisalimisha Leseni Zao

$
0
0
KAIMU Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Liberatus Sabas amewataka madereva wote kupeleka leseni zao kwenye vituo vikubwa vya Polisi au Polisi Usalama Barabarani Kanda Maalumu kwa ajili ya ukaguzi.

Agizo hilo lilitolewa na kamanda huyo jana wakati akizindua operesheni ya ukaguzi wa magari, madereva, leseni na vyeti vya udereva katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi, Ubungo. 

Sabas alisema lengo la operesheni hiyo ni kukagua leseni ili kubaini leseni za kughushi zilizopatikana kwa njia isiyo halali, kubaini vyeti vya udereva ambavyo ni halali ama vya kughushi, kubaini magari mabovu na yasiyofaa kuwepo barabarani kwa kuzingatia ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Alisema katika operesheni hiyo waliyoifanya wapo madereva waliokutwa wana leseni feki, yapo magari ambayo yamekutwa hayana ubora wa kusafirisha abiria, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za usalama barabarani. 

“Wapo waliokutwa na matatizo ikiwemo kutokuwa na leseni, magari hayana ubora, ni muhimu wakaelewa operesheni hii itaendelea nchi nzima, ninavyozungumza hivi popote walipo madereva na magari yao wajue kwamba watakutana na operesheni hii Mwanza, iwe Kigoma, iwe Mtwara, iwe Lindi, iwe Ruvuma,” alisema.

Alisema matarajio yao baada ya operesheni hiyo ni kuwafanya madereva kuacha tabia ya kughushi leseni, kuwahimiza madereva wajiunge na mafunzo ya udereva katika vyuo vinavyotambulika na serikali. 

Pia kujenga mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi, wamiliki, madereva na mawakala wa usafirishaji na wamiliki wapate elimu ya ukaguzi wa magari ambao bora ni ule unaozingatia ubora wa tairi.

Pamoja na kuwajengea utaratibu wa kukagua vifaa vyote vilivyo mbele ya gari, vinavyoongoza mfumo wa injini, mfumo wa breki, usukani na mfumo wa umeme na kuhakikisha madereva wote wenye leseni za kughushi au waliozipata kwa njia zisizo halali wanaacha kuendesha. 

Sabas aliwataka madereva wasio na leseni halali, madereva walevi, wamiliki wa magari walio na magari mabovu, kutoyaruhusu magari hayo kuingia barabarani hadi yatakapotengenezwa na kukaguliwa.

Pia aliwataka wamiliki wote wa magari, madereva na watumiaji wengine wote wa barabara, kuchukua tahadhari za kiusalama kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani wakati wote ili kupambana na ajali zinazoweza kuzuilika. 

“Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wamiliki, madereva na kampuni za usafirishaji zitakazokwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani,” alisema Sabas.

Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dar es Salaam, Marison Mwakyoma alisema kuwa operesheni hiyo imekuja baada ya kugundua kuwa baadhi ya madereva, wana leseni feki pamoja na ukosefu wa elimu kwa madereva ambapo wengi wao wanaogopa askari wa usalama barabarani badala ya kuogopa sheria. 

“Tunataka watu waogope sheria wasiogope trafiki, asilimia kubwa ya madereva wanaogopa askari wa usalama barabarani na ndio maana akifika njiani anamuuliza mwenzake ‘huko vipi?’ akishamwambia kupo salama anapita anaendesha mwendo,” alisema Mwakyoma.

VETA yabuni teknolojia kuwabana bodaboda Wasiovaa Kofia

$
0
0
MAMLAKA ya Elimu ya Ufundi (VETA) katika chuo chake cha Kipawa Dar es Salaam, imevumbua mfumo kwa waendeshaji bodaboda kulazimika kuvaa kofi a unaofanya bila kuvaa kofi a pikipiki isiwake.

Kutokana na uvumbuzi huo, imeomba serikali katika kukabiliana na athari vichwani kwa waendesha bodaboda, kuweka sheria ya pikipiki zote kwenda VETA kufungiwa mfumo huo kabla ya kuendelea na matumizi kama walivyofanya kwa sare za madereva. 

Pikipiki hiyo iliyopo katika viwanja ya Maonesho ya 42 ya Biashara, imewekwa kifaa maalumu na kwenye kofia za pikipiki ‘helmet’ ambayo ndiyo inaendesha mfumo mzima.

Akizungumzia mfumo huo, mwanafunzi Rentius Pesha alisema kofia hizo ni kwa dereva wa bodaboda pamoja na abiria wake, na lazima kofia iwekwe kichwani ili iwake na siyo sehemu nyingine. 

Alisema lengo la kubuni mfumo huo ni kubainisha teknolojia siyo lazima itoke nje ya nchi, bali mamlaka hiyo ina uwezo wa kuvumbua teknolojia mbalimbali ikiwemo kusaidia kuokoa nguvukazi ya taifa kwa kuanzia na kuokoa wanaopata matatizo vichwani. 

Mwalimu katika chuo hicho cha Kipawa, Anneth Mganga aliomba serikali kutunga sheria katika kutumia mfumo huo.

Tunatibu Na Kuponesha Kabisa Upungufu Wa Nguvu Za Kiume, Maumbile Mdogo, Busha Bila Kupasua

$
0
0
TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO BUSHA BILA KUPASUA PRESHA VIDONDA VYA TUMBO : Asilimia kubwa ya wanadamu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wapo waliohangaika sehemu mbalimbali bila mafanikio.

Mabula Clinic ni kituo cha tiba asilia kilichopo mbagara zakhemu njia kuu ya jeshini. Je unaupungufu wa nguvu za kiume au uume wako mdogo na mwembamba? 

Mapro pawer no 2 ndio tiba, kwa sasa hutibu matatizo matatu kwa pamoja 1. itakufanya uchelewe kufika kileleni dikika 15-20 kwa tendo la kwanza 2. Huimalisha misuli iliyolegea na kusinyaa hasa kwa wale walio athirika na upigaji punyeto 3. itakufanya upate hamu ya kurudia tendo zaidi ya mara tatu :Kwa nini ujione mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kisa unawai kukojoa au unakomea bao moja tu na huku dawa zipo 

Makakanua mix ni dawa iliyochanganywa na miti shamba 9 na kuwa na uwezo wa kuongeza uume saizi upendayo inchi 5-8 kwa urefu na unene sentimita 1-5, dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ata wazee wenye umri mkubwa wanapona

 Zipo dawa za mvuto wa mpenzi mme au mke kwa masaa matatu tu ,mvuto wa biashara, kutengeneza mwonekano mzuri wa mwili kwa wanawake yani shepu.

Tunatibu ngiri, miguu, mgongo na kiuno kuumwa, kupunguza kitambi minyama uzembe matiti na mwili mkubwa 

Tiba na ushauli muone Dr Mabula au piga simu no 0743362017.Huduma zangu utazipata popote ulipo kama uwezi kufika ofisini

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Waziri Mwijage Amteua Dkt.ludovick Manega Kuwa Afisa Mtendaji Mkuu Wa Wma

Tanzania Yasisitiza Ushirikiano Kutekeleza SDGs

$
0
0
SERIKALI ya Tanzania imeomba wadau wa maendeleo na taasisi mbalimbali zikiwemo za Umoja wa Mataifa kuendelea kufanyakazi nayo kuhakikisha kwamba ajenda ya kimataifa ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030 inaendelea kutekelezwa nchini.

Hayo yalisemwa katika kikao cha kupewa taarifa ya utekelezaji wa malengo hayo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk Augustine Mahiga.

Aidha alisema serikali imetengeneza mikakati kadhaa ya kuwezesha kutekelezwa kwa malengo hayo ya dunia.

Alisema wakati Tanzania imekaza nia ya kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda suala linalosisitizwa katika SDG 9 ni muhimu na kwamba serikali ya Tanzania inataka kuendeleza ushirikiano huo ili malengo ya dunia yafikiwe pia nchini Tanzania.

Alisema Tanzania chini ya uongozi wa Rais John Magufuli inaendelea kutekeleza mpango wa maendeleo endelevu wa Umoja wa Mataifa (SDGs) wenye lengo la kufikia ustawi kwa kila mkazi wa dunia hii.

Ili kutekeleza malengo hayo, mpango wa maendeleo wa miaka mitano umeingiza malengo ya SDGs.

“Kama nchi tangu tumeanza kutekeleza SDG kwenye  mwaka 2016, tumechambua na kuingiza vipengele vya SDGs kwenye mipango mbalimbali ya kitaifa ikiwamo mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano 2016/17-2020/21 (FYDP II) na mpango wa tatu wa kukuza uchumi wa Zanzibar na kupunguza umaskini (MKUZA III)” alisema.

Aidha alisema hatua kadhaa zimechukuliwa kuhakikisha kwamba malengo hayo yanatekelezwa ikiwamo uboreshaji wa vyanzo vya mapato ya ndani.

“ Tumeingia katika mifumo ya kisasa ya ukusanyaji  wa mapato, kutanua wigo wa kodi, kukabiliana na rushwa na kukabiliana na tabia zote zinazochochea upotevu wa mapato” alisema Dk Mahiga na kuongeza kuwa juhudi zilizofanyika zimefanya kuwepo na utekelezaji mzuri wa malengo hayo.

Pia alisema wameweka mikakati ya kuhakikisha kwamba malengo hayo yanapatiwa fedha na pia kushawishi ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma ili kufikia malengo hayo ambayo yametamkwa katika mpango wa maendeleo wa kitaifa.

Pamoja na kuhimiza uwekezaji, serikali pia imekuwa ikifanya juhudi na kuwa na soko la fedha lenye uhakika ambalo litachangia kupatikana kwa mitaji kwa ajili ya uwekezaji.

Waziri Mahiga alisema pamoja na kuhakikisha mambo yanaenda vyema nchini, serikali pia imekuwa ikishirikiana na taasisi za kimataifa na mataifa mengine ili mitaji ya utekelezaji wa malengo hayo ya dunia ikiwamo ajenda 17 unafanikiwa.

Hata hivyo katika mkutano huo Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema kwamba  kumekuwa na uchelewefu wa utekelezaji wa makubaliano ya misaada yenye lengo la kujazia utekelezaji wa SDGs.

Katika mazungumzo hayo alitaka wadau wa maendeleo kutekeleza ahadi zao kwa kuwa mpango wa maendeleo wa miaka mitano unatekeleza makubaliano ya malengo ya dunia ya SDGs.

Alisema mafanikio ya mpango hayo yanategemea sana utekelezaji wa msingi katika siku 1000 za utekelezaji wa malengo hayo ya dunia.

Katika siku hizo imeelezwa ni lazima kuwepo na utashi wa kisiasa,uwajibikaji na ushirikiano.

Alisema yapo makubaliano miongoni mwa nchi za Afrika namna ya kutekeleza kwa kasi wa Agenda hiyo ya maendeleo.

Alisema pamoja na serikali kufanikiwa kutoa elimu kwa watunga sera na sheria na wananchi kwa ujumla kuhusu SDGs na kuingiza ajenga hizo katika mipango ya kitaifa.

Alisema pamoja na mafanikio mengi yanaonekana kuhusu utekelezaji wa malengo hayo, Tanzania imekuwa na matatizo katika utekelezaji wake.

Miongoni mwa matatizo hayo ni ya kifedha, uwezo wa kiufundi, mawasiliano na uragibishi na changamoto zinazotokana na takwimu.

Aidha wadau wa maendeleo wamepunguza misaada yao na pia wakati mwingine wamekuwa wakichelewesha.

“Ukiangalia utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2017/18 inaonesha kuwa mikopo na ruzuku iliyopatikana kutoka kwa wadau wa maendeleo (DPs) inafikia Shilingi trilioni 1.87 sawa na asilimia 47 lengo la Shilingi trilioni 3.97 . “ alisema Dk Mpango na kusema hali hiyo inaathiri utekelezaji wa SDGs.

Wakati huo huo Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amesema umoja huo utaendelea kufanyakazi na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba malengo ya maendeleo endelevu yanafanikiwa.

Mratibu huyo amesema inafurahisha namna ambavyo serikali ya Tanzania inatekeleza malengo hayo kuanzia uhamasishaji na hadi sasa kuwekewa mikakati pamoja na kutumbikizwa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano.

Rodriguez amesema Serikali ya Tanzania inapaswa kuungwa mkono na kupongezwa kwa kufanya juhudi za kuwekeza katika miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha zake.

Pia Mratibu huyoa amesema kwamba yapo mambo ambayo yanastahili kuzingatiwa hasa namna ya kuangalia utekelezaji na uratibu wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Rais Magufuli Awatunuku Kamisheni Maafisa Wa Jeshi

$
0
0
Na. Immaculate Makilika – MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi  Mkuu Dkt. John  Pombe Magufuli  amewatunuku Kamisheni  Maafisa  wapya 123 wa Jeshi la Ulinzi na Wananchi wa Tanzania  (JWTZ) katika cheo ha Luteni UsO.

Rais Magufuli amewatunuku Kamisheni Maafisa hao wapya wa Jeshi la Ulinzi na Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu  ambao walikuwa wanafunzi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi, kilichopo Monduli Arusha leo  [Jumamosi Julai 7, 2018] katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo hicho, Luteni Generali Paul Massao  Maafisa waliohitimu kozi ya 63 mwaka 2017 jumla yao ni 123 kati yao 118 ni watanzania,  na wahitimu 5 kutoka nchi za Uganda,  eSwatini, na Rwanda.

“Kati ya Maafisa  watanzania 118  wanawake ni 3 na wanaume 115, ambapo Maafisa 121 walipata mafunzo yao katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Mondulu  na Maafisa wa 2 walipata mafunzo yao nchini India” alifafanua Luteni Generali Massao.

Sambamba na kuwatunuku Kamisheni Maafisa hao kwa cheo cha Luteni Usu, Rais Magufuli ametoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri ambao ni Emmanuel Kakuba Afisa aliyefanya vizuri zaidi darasani, Danie Meshack aliyefanya vizuri zaidi kwenye mafunzo, na katika medani ni Ramadhan Kakombe.

Wengine, ni Amstrong Mwamwesige kutoka Uganda aliyefanya vizuri kutoka nchi rafiki pamoja na Beatrice Kipinge ambaye ni mwanamke aliyefanya vizuri zaidi.

Aidha, wahitimu 87 waliachishwa mafunzo kwa sababu mbalimbali ikiwemo magonjwa, utovu wa nidhamu ama mtu kuomba kwa hiari yake.

Hafla hiyo ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wa ilipambwa na burudani kutoka vikundi mbalimbali ikiwemo kikundi cha ngoma za asili pamoja na kikundi cha mziki wa dansi cha Jeshi cha Mondulu jijini Arusha.

Aidha, tangu kuingia kwake madarakani mwaka 2015  hii ni mara ya 6 ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwatunuku Kamisheni Maafisa wa Jeshi la Ulinzi na Wananchi Tanzania (JWTZ).

ACT-Wazalendo kushiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Buyungu na Kata 79 ........ Watangaza ushirikiano na wapinzani

$
0
0
Chama cha ACT- Wazalendo kimetangaza kushiriki kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Buyungu na Kata 79 huku kikibainisha kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya upinzani.

Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara), Shaaban Mambo amesema uamuzi huo umefikiwa na kikao cha Kamati Kuu baada ya kufanya tathmini.

Akizungumza leo Julai 7, 2018 Mambo amesema kamati imeona umuhimu wa chama hicho kushiriki katika uchaguzi huo kwa lengo la kujijenga zaidi.

Amesema ACT wapo tayari kushirikiana na vyama vingine vya upinzani kwa kusimamisha mgombea mmoja ili kushindana na CCM.

"Tunaamini kuwa watu watatumia uchaguzi huu kuonyesha hasira yao dhidi ya serikali ya CCM, ndiyo sababu tupo tayari kushirikiana na vyama vya upinzani,"

"Ushirikiano wetu ni kwenye kuachiana wagombea katika maeneo ambayo tunaona chama fulani kinafanya vizuri,” amesema

Amesema katika kata 79, ACT ina uhakika wa kufanya vizuri katika kata 30 lakini itakuwa tayari kuachia chama chochote cha upinzani endapo itathibitika kuwa mgombea wake ni mzuri kuliko wao.

Rais Magufuli kuwaongoza watanzania kupokea ndege Mpya KESHO Jumapili

$
0
0
Rais Dkt. John Magufuli kesho Jumapili Julai 08, 2018 atawaongoza watanzania katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa alasiri ya leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ya Rais, Gerson Msigwa na kusema ndege hiyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa 8:00 mchana ikiwa inatokeaa Seattle nchini Marekani.

Hii ni ndege ya nne kuwasili nchini kati ya ndege 7 zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuimarisha huduma zake.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 8

Waziri Mkuu: Serikali Haitanunua Madeni

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haina mpango wa kununua madeni yaliyosababishwa na mikopo ya kibenki kwenye vyama vikuu vya ushirika nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Julai 7, 2018) wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.

“Serikali ya awamu ya tano hatuna biashara ya kununua madeni ya vyama vikuu, kulikuwa na tabia ya watu wa ushirika kukopa na hali ikiwa mbaya wanakimbilia Serikalini. Serikali hii hatuna biashara hiyo,” alisema.

Waziri Mkuu amesema anazo taarifa kwamba Chama Kikuu cha mkoa wa Kagera (KCU) kimekopa fedha Benki ili kiweze kulipa deni la mwaka 2014. “Nimeambiwa KCU wamekopa fedha benki ili kulipa deni la mwaka 2014, hii inaingia akilini kweli? Mnakopa fedha kulipa deni la zamani, ni kwa nini msiwatafute waliosababisha deni na kuwachukulia hatua?,” alihoji.

“Ninyi mlikuwa watu sita ambao mlikubaliana kama viongozi, mlienda kukopa kuzidi uwezo mlionao. Leo hii ni kwa nini serikali ije kulipa wakati mmetumia ninyi?,” aliuliza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya tatno inasisitiza masuala ya ushirika kwa sababu imeamua kuwahudumia wananchi kuanzia ngazi ya chini kuanzia pembejeo, dawa hadi masoko.

“Tunataka tuondoe utaratibu wa chama kikuu kukopa fedha benki ili kikanunue mazao. Vyama vingi vimetengeneza hasara, leo hii vyama vikuu vina madeni. Hii ni kwa sababu mlikopa fedha benki wakati hata hamjui mna kilo ngapi ambazo zimevunwa.

“Fedha mnachukua nyingi na hata ikibaki hamrudishi benki. Riba anadaiwa mkulima kupitia kilo anazouza, deni anapelekewa mkulima na kuanza kukatwa kwa kila kilo. Hatutaki tena utaratibu huu. Kuanzia sasa, AMCO ndiyo itaratibu na kukusanya mazao ya kila mwanachama kwa sababu yenyewe inajua ina wanachama wangapi, wana ekari ngapi na wanatarajia kuvuna kilo ngapi,” amesema.

Amesema ili kuondokana na utaratibu wa vyama vikuu kukopa benki, Serikali imepiga marufuku utaratibu huo na badala yake wanunuzi wataenda kununua mazao kwenye vyama vya msingi kupitia minada na watatakiwa kuwa wameingiza fedha kwenye vyama vya msingi (AMCOS) ndani ya siku tatu.

“Tulishasema mwisho uwe ni msimu huu, yasijirudie tena haya mambo ya kukopa benki.  Mnunuzi akipata mnada, ndani ya siku tatu, anatakiwa awe amehamisha fedha kwenda kwenye akaunti ya AMCOS husika,” alisema.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema mfumo wa ushirika bado unakabiliwa na changamoto ya upotoshaji na maewagiza maafisa ushirika wakasimamie suala hilo kwa kutoa taarifa sahihi kwa wakulima.

“Leo hii tunakabiliwa na changamoto kubwa kupitia uuzaji wa mazao kwa mfumo wa stakabadhi za Mazao Ghalani, Kuna watu wanapita wakipotosha kwamba serikali inawakopa wakulima mazao yao.”

“Nendeni mkawaelimishe wakulima kwamba mtu akipeleka mazao yake ghalani siyo kwamba anakuwa tayari ameuza, bali anayaweka pale na kujua ana kilo ngapi, amapewa risiti na kusubiri bei iwe nzuri wakati wanunuzi wakibishana. Hela ikilipwa, anapewa hela yote kulingana na mzigo wake,” alisema.

Siku ya Ushirika Duniani huadhimishwa Jumamosi ya kwanza ya Julai kila mwaka. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni: “Ushirika kwa ulaji wa uzalishaji endelevu wa bidhaa na huduma.”

England Yaipiga Sweden 2-0 Na Kutinga Nusu Fainali Kombe La Dunia

$
0
0
Timu ya taifa ya England imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia Urusi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sweden.

Mabao ya England yamefungwa na Harry Maguire (30') pamoja na Dele Alli aliyefunga katika dakika ya 58 ya kipindi cha pili.

Ushindi huo unawafanya England kuingia hatua hiyo ya nusu ikiwa ni baada ya miaka 24 ambapo mara ya mwisho ilikuwa 1990.

Wenyeji Urusi Waaga Mashindano Ya Kombe La Dunia kwa kichapo cha mabao 4-3 kwa njia ya matuta

$
0
0
Wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia Urusi wameyaaga rasmi mashindano hayo kwa kichapo cha mabao 4-3 kwa njia ya matuta dhidi ya Croatia.

Mchezo huo ulifikia hatua hiyo baada ya dakika 120 kwenda sare ya mabao 2-2 na changamoto ya mikwaju ya penati ikaamuliwa kupigwa.

Mabao ya yaliyopatikana ndani ya dakika 90 kwa upande wa Urusi yaliwekwa kimiani na Denis pamoja na Fernandez.

Wakati huo Croatia walijipatia mabao yao kupitia kwa Andrej na Vida.

Baada ya michezo hatua ya robo fainali kukamilika jana, Croatia walioingia nusu fainali watacheza dhidi ya England huku Ufaransa wakikipiga na Ubelgiji.

Gavana Wa Benki Kuu Aipongeza TRA Kwa Kukusanya Kodi Ya Majengo Kielektroniki

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Prof. Florens Luoga ameipongeza TRA kwa kukusanya kodi za majengo kwa kutumia Mfumo wa Kielektroniki.

Akizungumza wakati alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba, Prof. Luoga amesema kuwa, mfumo huo umesaidia kupunguza adha kwa wananchi ambao sasa wengi wao wanatumia simu za mkononi kulipia Kodi ya Majengo badala ya kwenda kupanga foleni benki.

“Nimefurahishwa sana na uboreshaji wa mifumo ya malipo hususani katika kulipia Kodi ya Majengo ambapo watu wengi wanatumia simu zao za mkononi kulipia kodi hiyo badala ya kwenda benki kukaa kwenye foleni. Hii ni moja ya maboresho makubwa yaliyofanywa na TRA hivyo nawapongeza sana,” alisema Gavana.

Gavana Luoga ameongeza kuwa, mifumo ya malipo inapoboreshwa husaidia walipakodi kulipa kodi zao kwa urahisi na kwa wakati na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla.

Aidha, Prof. Luoga ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa wakati kwa sababu maendeleo yaliyopo nchini yanatokana na kodi mbalimbali zinazolipwa na wananchi hao.

“Wito wangu kwa walipakodi na wananchi wote ni kuwasihi kuendelea kulipa kodi kwa wakati kwani faida zote wanazozipata kutokana na mfumo wa utawala waelewe kwamba umetokana na kodi mbalimbali wanazozilipa. Wanachi wanatakiwa kuelewa kwamba, upatikanaji wa elimu, maji, barabara, umeme na mambo mengine kama hayo yote yametokana na kodi,” alieleza Prof. Luoga.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inashiriki maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo inatoa huduma mbalimbali kama vile kusajili walipakodi, kuelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi, kutoa bili na kulipa Kodi ya Majengo.

Huduma nyingine ni pamoja na kuelezea haki na wajibu wa Mlipakodi kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma na Mlipakodi, kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya Mashine za Kielektroniki za kutolea Risti (EFDs), kuelezea mwenendo wa makusanyo ya mapato ya Serikali, na kupokea maoni, malalamiko, mrejesho pamoja na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wananchi.

Waziri wa Kilimo Akabidhiwa Tuzo Ya Heshima Kwa Kuimarisha Sekta Ya Ushirika Nchini

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Mwanza
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim M. Majaliwa (Mb) amemkabidhi tuzo ya heshima Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwa kazi kubwa aliyoifanya na anayoendelea kuifanya katika kuimarisha sekta ya ushirika nchini katika kipindi cha muda mfupi tangu alipoteuliwa kuhudumu katika nafasi hiyo.

Tuzo hiyo imetolewa jana 7 Julai 2018 wakati wa kilele cha siku ya ushirika Duniani na Mhe. Waziri Mkuu kwa niaba ya wanaushirika ambao ndio wameandaa Tuzo hizo ikiwa ni heshima na Utumishi mkubwa kwa Waziri Tizeba katika kipindi kifupi kwa kurudisha imani ya ushirika kwa wananchi waliokuwa wamepoteza matumaini kutokana na baadhi ya viongozi wabadhilifu kujinufaisha na Ushirika kinyume na utaratibu.

Tuzo hiyo kwa Dkt Tizeba inatolewa wakati ambapo ni siku moja pekee imepita tangu Waziri huyo wa kilimo kutangaza Kiama kwa viongozi na baadhi ya watendaji wa vyama vya ushirika wanaofanya ubadhilifu wa Mali za wanaushirika kwa manufaa yao pekee pasina kuwanufaisha wanachama wote.

Kwa msisitizo mkubwa hapo  Julai 6, 2018 Mhe. Dkt Tizeba alieleza kwa ukali kuhusu ubadhilifu wa rasilimali za ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika kwenye hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika kwa siku mbili katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Kongamano hilo liliambatana na maonesho ya bidhaa na shughuli zinazofanywa na vyama hivyo vya ushirika kote nchini ambapo wanachama wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu, na kujadili mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo katika uendeshaji wa sekta ya ushirika nchini na kutoa maoni yao kwa serikali.

Dkt Tizeba amesisitiza kuwa serikali inafanya juhudi mahususi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanahamasishwa na hatimae kujiunga kwenye vyama vya ushirika kulingana na shughuli zao za kiuchumi ili kuondoa dhana kuwa vyama vya ushirika ni kwa ajili ya Kilimo cha Mazao ya biashara ya nchi za nje.

Pia, alisema kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kupitia serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango wa ushirika wa Taifa katika kuyafikia malengo ya milenia na malengo mbalimbali ya nchi kama uimarishwaji wa sekta ya viwanda, Kilimo, Mifugo, uvuvi na biashara na kuchangia katika ongezeko la kipato kwa wananchi na hatimaye kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa.

Tuzo hiyo ya kuimarisha sekta ya ushirika nchini pia imetolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli sambamba na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb).

CUF Ya Lipumba Yasema Itashiriki Uchaguzi Mdogo Uliotangazwa

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya ambaye ytuko upande wa Profesa Lipumba  amesema chama hicho kitashiriki uchaguzi wa ubunge katika majimbo ya Buyungu, Jangombe na kwenye Kata 79.

Akizungumza jana Sakaya alisema chama hicho kimepokea barua kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kikielezwa kuwa majimbo na kata hizo, yapo wazi.

Alisema kutokana na mabadiliko yaliyofanyika NEC na katika vyombo vya Dola ni wazi kuwa wataibuka na ushindi katika chaguzi hizo

“Naomba ifahamike kuwa CUF ipo moja na uamuzi wa chama ni kushiriki uchaguzi,  wanachama wasisikilize maneno ya watu ambao hawahusiki na chama," alisema Sakaya.

Alisema wapo wanaojitambulisha kuwa viongozi wa CUF wanasema hawatoshiriki, si kweli wamachama  na wenye nia ya kutaka kugombea ubunge na udiwani wajitokeze.

"Uchaguzi wa ubunge jimbo la Kinondoni tulilalamikia utaratibu ulivyokuwa na namna NEC walivyokiuka. Ila kw amabadiliko yaliyofanyika sasa, naamini hali itakuwa nzuri,” alisema Sakaya.
 
Pia nae Profesa Ibrahim Lipumba amewataka wanachama kuzipuuza habari kuwa wamesusia kushiriki chaguzi hizo.

Taarifa Muhimu Kwa Umma Kutoka Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji

Mwigulu Nchemba Kasema Hawezi Kujiuzulu Ubunge....Adai Uongozi ni kupokezana kijiti

$
0
0
Mbunge wa Iramba Magharibi, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wakazi wa jimbo hilo kutosikiliza maneno ya watu wanaosema kuwa anaweza jiuzulu nafasi ya ubunge baada ya kuondolewa katika baraza la mawaziri.

Dk Mwigulu alitoa kauli jana wakati akiwa kwenye mkutano na wakazi Kata ya Ulemo kijiji cha Misigiri wilayani Iramba mkoani Singida.

Alisema uongozi ni kupokezana kijiti na kwamba si kweli kwamba analengo la kuacha nafasi hiyo na kwamba ataendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwa mda wote tofauti na mwanzo alivyokuwa kwenye majukumu ya kitaifa.

Alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais John Magufuli kwa kumwamini na kumpa na nafasi katika serikali yake hadi alipombadilisha na hana kinyongo chochote, ataendelea kufanya kazi chini ya mwenyekiti wa CCM na serikali pale itakapoitajika huduma yake.

Alifafanua kuwa uliona wapi mchezaji akasajiliwa kwenye klabu yake, kisha akaitwa timu ya taifa na siku akiondoka timu ya taifa anasema klabu yenu siichezei.

“Hao wanaosema nataka kujiuzulu ubunge, wanataka kutengeneza jambo la ugomvi. lakini kwangu sioni kama ni ugomvi wala tatizo nimerudi kuwatumikia wananchi wa jimbo kwa kazi mlionituma"
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images