Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wapinzani waipigia kura ya hapana bajeti Kuu ya Serikali

$
0
0
Wabunge wanane wa CUF wanaomuunga mkono Ibrahim Lipumba wameipiga kura ya ‘ndio’ Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19 ya Sh32.45 trilioni.

Kati ya wabunge hao wawili ni wa majimbo ambao ni Maftaha Nachuma (Mtwara Mjini) na Magdalena Sakaya (Kaliua).

Wangine sita ni wa Viti Maalum ambao ni; Zainab Mndolwa, Alfredina Kahigi, Rukia Kassim, Nuru Bafadhili, Kiza Mayeye, Rehema Migilla.

Kura zao za ‘ndio’ zimeshangiliwa na wabunge wengine wa CCM ambao wengine waligonga meza huku wakisimama kuwashangilia.

Sakaya yeye amepiga kura  huku akisema; “‘ndio kwa maendeleo ya wana Kaliua.”

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Jacqueline Ngonyani ‘Msongozi’ alipoitwa yeye alianza kwa kupiga vigele gele kisha akasema;  ‘ndiooooo’ na kuendelea kupiga vigelegele jambo lililoibua shangwe ndani ya ukumbi huo hasa kutoka upande wa CCM.

Kura za wabunge wa CCM walioshangiliwa mara baada ya kusema ‘ndio’ ni za Hussein Bashe (Nzega Mjini), Nape Nnauye (Mtama), na Abdallah Bulembo (Kuteuliwa).

Jina la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu lilipoitwa wabunge walikaa kimya kwa muda huku  minong’ono ikisikika kwa mbali.

Mawaziri ambao hawakuwapo ni; Dk Augustine Mahiga (Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa) na Profesa Palamagamba Kabudi wa Katiba na Sheria.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe amekuwa miongoni mwa wabunge wa upinzani ambao hawakuwepo bungeni.

BREAKING: Wabunge Wapitisha Bajeti Kuu ya Serikali 2018/ 2019

$
0
0
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameipitisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19 ya Sh32.45 trilioni kwa kura 266 kati ya 348 sawa na asilimia 76.

Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai akitangaza matokeo ya kura leo jioni Juni 26, 2018 amesema jumla ya wabunge waliokuwamo bungeni na kupiga kura walikuwa 348.

“Idadi ya wabunge waliopiga kura 348, wabunge 43 hawakuwepo. Kura za hapana 82 na hakuna kura ambayo haikuamua na kura za ndio ni 266,” amesema Kagaigai

Mara baada ya kauli hiyo, shangwe kutoka kwa wabunge wa CCM ziliibuka huku Spika wa Bunge Job Ndugai akiwashukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema mara baada ya kuondoka Ijumaa, bila shaka mawaziri wataondoka wakiwa wamesheheni maoni ya wabunge na ushauri ambao kimsingi umetoka kwa wananchi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya June 27

Majina ya Wanaodaiwa Na Suma JKT Yaanikwa....Wamo Mawaziri, Wabunge na Makada CCM

$
0
0
Shirika  la Uzalishaji Mali la Suma JKT, limetangaza orodha ya majina ya wadaiwa wake sugu wa matrekta ambamo wako pia mawaziri wa sasa, mawaziri wastaafu, wabunge na wakuu wa mikoa.

Baadhi ya majina ya mawaziri wa sasa yaliopo kwenye orodha hiyo ni Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Luhaga Mpina na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Kangi Lugola.

Pia kwenye orodha hiyo yumo Naibu Waziri wa Wizara ya Uvuvi na Mifugo, Abdalah Ulega, ambaye ni Mbunge wa Mkuranga.

Mawaziri wastaafu waliotajwa kwenye orodha hiyo ni Dk. Juma Ngasongwa ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na waziri wa wizara mbalimbali kwenye serikali zilizopita.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato mkoani Geita naye ametajwa kwenye orodha hiyo.

Mwingine aliyetajwa kwenye orodha hiyo yenye jumla ya majina 1,392 ni aliyekuwa Waziri wa Fedha kwenye utawala wa awamu ya nne, Mustapha Mkulo.

Wakuu wa mikoa wa sasa waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na Mkuu wa Mkoa wa Sindiga, Dk. Rehema Nchimbi.

Wabunge waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Husna Mwilima wa Kigoma Kusini (CCM), Mbunge wa Shinyanga Mjini, Steven Maselle (CCM) na Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (CCM).

Wabunge wengine waliotajwa ni Ignas Malocha wa Jimbo la Kwela (CCM), Mbunge wa Kilolo (CCM), Venance Mwammoto, Mbunge wa Korogwe Mjini (CCM), Mary Chatanda na aliyekuwa Mbunge wa Songea Mjini (CCM), marehemu Laurence Gama.

Kwenye orodha hiyo pia wamo wabunge waliopita akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila na aliyewahi kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini (CCM), Benson Mpesya (2000-2010).

Wabunge wengine waliopita waliotajwa ni aliyekuwa Mbunge wa Manyoni Magharibi (CCM), Paul Lwanji, aliyekuwa Mbunge wa Afrika Mashariki (CCM), Kate Kamba, aliyekuwa Mbunge wa Mbarali (CCM), Modestus Kilufi na aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Manju Msambya.

Mwingine aliyetajwa ni aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM na mwanachama wa Chadema sasa, John Guninita.

Kwenye orodha hiyo pia ametajwa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, marehemu Said Mwambungu.

Katika tangazo la SumaJKT lililotoka jana kwenye moja ya magazeti ya kila siku, wadaiwa walioshindwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kulipa madeni wanayodaiwa kwa wakati, walitangaziwa hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Wakati akizindua Kituo cha Uwekezaji cha Jeshi la Wananchi (JWTZ) kupitia Suma JKT kilichopo Mgulani, jijini Dar es Salaam Mei 17, Rais John Magufuli alitoa mwezi mmoja kwa wadaiwa hao kulipa madeni yao kabla ya msako wa kuwatafuta haujaanza.

Baadaye, Suma JKT iliwatangazia wote wanaodaiwa kupitia tangazo lao la hivi karibuni kwa kuwataka wadaiwa kulipa kabla ya Juni 15, muda ambao tayari umeshaisha.

Tangazo lingine lililotolewa na Makao Makuu ya SumaJKT la Jumanne wiki hii likiwa na kichwa cha habari 'Lipeni madeni kwa wakati' lilisema wale walioshindwa kutekeleza agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria.

Pia tangazo hilo liliwaeleza wale waliopatiwa huduma ya ulinzi na Suma JKT Guard na kushindwa kulipa kuwa huduma hizo zitasitishwa na watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwamo kukamata mali zao kufidia deni wanalodaiwa.

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Usajili Maalumu Wa Vitambulisho Vya Taifa Kwenye Maonesho Ya Sabasaba 2018

Peru Yashinda Mechi Kombe La Dunia Baada Ya Miaka 40

$
0
0
Timu ya taifa ya Peru imemaliza mechi zake za makundi kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Australia na kuvunja rekodi yake ya kutoshinda mchezo kwenye Kombe la Dunia tangu mwaka 1978.

Tangu ishinde mechi yake ya mwisho dhidi ya Iran kwa mabao 4-1, imepita miaka 40 na siku 15. Ushindi wa Peru jana haujaisaidia kusonga mbele ambapo imetoka pomoja na timu ya Australia.

Ufaransa, Argentina, Denmark Na Croatia Zafuzu 16 Bora

$
0
0
Croatia na Argentina zimefuzu kucheza hatua ya mtoano katika 16 za michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi.

Argentina wamemaliza michezo yao kwenye kundi D wakiwa na alama 4 katika nafasi ya pili kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nigeria jana usiku.

Mabao ya Argentina yaliwekwa kimiani na Lionel Messi mapema katika dakika ya 14 huku la pili likifungwa na Marcos Rojo mnamo dakika ya 86 ya kipindi cha pili.

Bao pekee la Nigeria liliwekwa kimiani kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Victor Moses katika dakika ya 51 ya kipindi cha pili.

Wakati huo Ufaransa pamoja na Denmark zimefuzu kuingia mtoano baada ya sare ya kutofungana  jana mchana katika mchezo wa kundi C.

Kutokana na matokeo hayo, Ufaransa sasa itakipiga dhidi ya Argentina katika hatua ya mtoano huku Denmark ikicheza dhidi ya Croatia.

Ajira Mpya 22,150 Kutolewa Wiki Hii

$
0
0
Serikali  imesema itaongeza mishahara ya watumishi wa umma mwaka ujao wa fedha. Pia imesema hadi kufikia Jumamosi itakuwa imetoa ajira mpya 22,150 kwa mwaka huu wa fedha.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jijini Dodoma jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, alipokuwa anachangia mjadala wa mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha na Taarifa ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017.

Alisema serikali ilisimamisha utoaji ajira, ili kuhakikisha uhakiki wa wafanyakazi hewa unafanyika lakini baada ya zoezi hilo kukamilika sasa, ajira zimeshaanza kutolewa.

Mkuchika alisema uhakiki huo ulibaini watumishi hewa 19,708 na wengine 14,409 walio na vyeti feki.

Alisema kuwa hadi Jumamosi ajira 22,150 zitakuwa zimetolewa. Kati yake 7,000 ni za walimu na 8,000 za kada ya afya.

Hata hivyo, lengo la serikali mwaka huu wa fedha lilikuwa kuajiri watumishi wapya 52,000.

"Waheshimiwa wabunge kwa ajira hizo, hakuna zahanati itakamilika halafu ikakosa watumishi," Mkuchika alisema.

Kuhusu watumishi wa umma kutopandishwa mishahara kwa muda mrefu, Mkuchika alisema hoja hiyo si sahihi kwa kuwa serikali imeshatoa nyongeza ya mwaka 2017/18 na katika mwaka ujao wa fedha 2018/19 itatolewa.

Hata hivyo, waziri huyo alibainisha kuwa sasa serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ukiwamo utoaji huduma za afya na maji itakayowezesha kuimarisha uchumi wa nchi.

Alisema kuwa mara uwezo wa kibajeti ukiwa mzuri serikali haitosita kupandisha mishahara kwa watumishi wa umma.

"Kwa watumishi ambao walipaswa kupandishwa madaraja, lakini hawakupata fursa hiyo hadi wakastaafu, wanapaswa kwenda kwa waajiri wao wajaziwe fomu maalum ili walipwe malipo yao," Mkuchika alisema.

Wolper Amwaga Povu Baada Ya Tetesi Za Kutoka na Mr. Nice

$
0
0
Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amemwaga povu baada ya tetesi kusambaa anatoka kimapenzi na msanii mkongwe wa Bongo fleva Mr. Nice.

Siku chache zilizopita Wolper na Mr. Nice walionekana pamoja wakila bata Kwenye club moja Nairobi nchini Kenya huku wakionyesha kuwa na ukaribu fulani.
 
Kwenye video ambayo iliwekwa Mtandaoni na Jacqueline Wolper iliwaonyesha wawili hao wakila bata yaani Wolper akivuta shisha huku Mr. Nice akinywa pombe ambapo watu mbalimbali walidai huenda wanatoka kimapenzi.

Baada ya Tetesi hizo za Mahusiano gazeti la Risasi  lilimtafuta Wolper kwa njia ya simu akiwa nchini Kenya na kumuuliza kuhusu ukaribu wake na Nice ambapo alisema ni wa kawaida tu na wako karibu kwa sababu bosi wao ni mmoja.

"Watu wajue sisi tupo kikazi zaidi kwani kuonekana na mtu ni lazima awe mpenzi wako? Si lazima, huyu ni kaka yangu na bosi wetu ni mmoja, projekti yetu ikiwa tayari tutaitangaza itajulikana tu lakini kwa sasa bado ni mapema kuitangaza”.

Gigy Money: Ningekuwa Mwanaume Kamwe Nisingetembea Na Irene

$
0
0
Bifu kati ya mwanadada Gigy Money na Irene bado linaendelea na wanazidi kutoleana maneno ya kashafa katika mitandao ya kijamii.

Hivi karibuni Gigy Money amefunguka na kumponda vibaya mwanadada Irene na kumwambia kuwa hana uzuri wowote labda ile rangi ndio inayompa kiburi mjini.

Katika Interview yake Gigy Money anasema kuwa Irene sio mtu wa kutamani kukutana nae personally kama watu wengi wanavyomuona alivyo huko Instagram , lakini ni msichana wa kawaida tu na hana uzuri wowote huku akiongezea na kusema kuwa kama angekuwa mwanaume wala asingehangaika kutoka kimapenzi na Irene.

"Sijawahi kufikiria kumpenda hata siku moja na hata siku tunakutana i was too drunk,na nilipokutana nae sikumjua hata mana live na personal ni tofauti kabisa,mimi ni mwanamke lakini ningekuwa mwanaume wala nisingepita."

Huddah Monroe Ataja Kinachowafanya Wanaume Wasibanduke Kwake

$
0
0
Mrembo kutokea nchini Kenya, Huddah Monroe  amefunguka kitu ambacho kinavutia wanaume kutoka kwake.

Mrembo huyo ambaye alikuwa hapa nchini hivi karibuni, katika mahojiano na Wasafi TV amesema tabasamu lake ndilo linavutia wanaume wengi.

“Which part on my body wanaume wengi wapo attractive is….., I think is my smile,” amesema Huddah.

June 17, 2018 katika show ya Harmonize ‘Kusi Night’, Huddah ni miongoni mwa wale waliotoa burudani ya aina yake. Alipanda jukwaani na kucheza ngoma ya Diamond ‘ African Beauty’ kitu kilichoibua shangwe la aina yake.

Infinix Yazindua Infinix Note 5 Yenye Teknolojia ya Android One

$
0
0
Kampuni ya simu ya Infinix imeweka dhamira ya kuzalisha simu zenye teknolojia ya hali ya juu na muonekano mzuri kwajili ya kizazi kipya. Infinix NOTE 5 inaendeshwa na mfumo wa Android wenye kuifanya kuwa simu ya pekee yenye sifa zenye kushawishi ukilinganisha na simu yoyote ya Infinix kwa sasa. Kupitia mfumo wa Android One Infinix NOTE 5 imethibitika kuwa simu yenye ulinzi zaidi wa software na inayopokea updates katika muda mfupi.

Baada ya kuzinduliwa jijini Dubai, Infinix NOTE 5 itazinduliwa katika nchi zaidi ya 30 ikiwemo Nigeria, Egypt, India, Morocco, Kenya, Uganda Cote d’ voire na nyengine nyingi.0

Na katika kuhakikisha kampuni inatimiza ahadi ya kuzalisha simu zenye muonekano mzuri kuendana na wakati Infinix NOTE 5 inamuonekano wa tofauti ikiwa na wigo mpana wa kioo cha 18:9 na nchi 6.0 FHD.

Pamoja ya kuwa na mfumo pendwa hasa kwa wale wenye matumizi makubwa kama ya kiofisi, lakini pia Infinix NOTE 5 imempendelea mpenzi wa kamera pia kwa kupitia pixel 16 low light selfie na pixel 12 nyuma zenye kupiga picha nzuri hata katika mwanga hafifu.

Infinix NOTE 5 inauwezo wa kukaa na chaji kwa siku tatu pasipo kuzima data kutokana na ujazo wake wa chaji kuwa 4500.

Akiongea na vyombo vya habari makamu wa raisi wa TRANSSION HOLDINGS Bwana Arif Chowdhury alisema kwamba, “nikiwa miongoni mwa wazalishaji na wasambazaji wa simu za Infinix katika masoko mbalimbali tunawahakikishia bidhaa zetu zinawafikia idadi kubwa ya watu na kuongeza utandawazi kupitia njia ya mawasiliano”.

Na mkurugenzi wa Android, Bwana Mahir Sahin alisema, “unaponunua simu mpya unategemea kuona sifa mpya katika simu hiyo na hii ndio sababu iliyotufanya tushirikiane na GOOGLE na kuwaletea simu yenye maajabu yanayotokana na Android One kupitia GOOGLE Lens na GOOGLE Assitant”.

About Infinix

Infinix is a premium smartphone brand from TRANSSION Holdings designed for young generations who desire to live a smart lifestyle. Launched in 2013, Infinix is committed to building cutting-edge technology and fashionably designed dynamic mobile devices to create globally-focused intelligent life experiences through a merging of fashion + technology. 
Though daily interactions, these intuitive products become part of a lifestyle that represents trend-setting and intelligent experiences for young people around the world. Infinix currently promotes five product lines: ZERO, NOTE, HOT, S, and SMART in a globally marketplace reaching countries in Africa, Latin America, the Middle East, Southeast Asia and South Asia. With the brand spirit of challenging the norms, Infinix smart devices are designed specifically for young people who want to stand out, reach out and in sync with the world.

Unaweza kuwafata kupitia mitandao yao.

    Infinix Mobile Tz

         @InfinixMobileTz

      @InfinixMobileTZ

Viwanja vya makazi Vinauzwa Bunju na Mapinga Kwa Bei Nzuri

$
0
0
Viwanja vya makazi: Bunju na Mapinga
Viwanja vipo Kimele, ni km 3 kutoka main road.
 
Vipo viwanja size zote kwa bei tofauti: mil 2 for 10/20, mil 4 for 20/20, mil 6 for 20/30, mil 8 for 20/40, mil 12 for 30/40, mil 16 for 40/40 na mil 24 for 40/60. 

Ruksa kulipa kwa awamu. Hakuna dalali, mpigie mhusika: 0757489709

Wanafunzi Shule ya Msingi Wachomana Visu

$
0
0
Mwanafunzi funzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Azimio Wilaya ya Tarime mkoani Mara mwenye miaka 15, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma kisu na kumuua mwanafunzi mwenzake, Rhobi Chacha (14).

Kamanda wa polisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo lilitokea juzi na Rhobi alifariki dunia saa sita mchana wakati akipata matibabu Hospitali ya Mji wa Tarime.

Marehemu alikuwa mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Azimio na mkazi wa Iganana, kata ya Sabasaba, Tarime.

“Baada ya kitendo hicho mtuhumiwa alikimbia na polisi tunamtafuta ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Mwaibambe.

Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Mji Tarime, Dk Innocent Kweka alisema alimpokea Rhobi juzi saa nne asubuhi lakini alifariki dunia akiendelea na matibabu.

“Kwenye uchunguzi ilibainika kuwa alichomwa na kitu chenye incha kali na kilizama kwenye mapafu, hali iliyosababisha marehemu kuvuja damu na kupoteza maisha,” alisema Dk Kweka.

Akizungumzia tukio hilo mwalimu mkuu msaidizi shuleni hapo, Bahati Lucas alisema Rhobi na Charles wanasoma shuleni hapo. “Inasikitisha sana, mtuhumiwa alikuwa anatarajia kufanya mtihani wake wa mwisho wa darasa la saba mwaka huu,” alisema.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Iganana, Edward Thomas alisema mtuhumiwa na Rhobi ni majirani wanaotenganishwa na barabara ya mtaa. 

“Ulizuka ugomvi kati yao wakati wanacheza mpira, mtuhumiwa aliingia nyumbani na kuchukua kisu na kumshambulia mwenzake,” alisema Thomas.

Waziri Mkuu Atoa Mwezi Mmoja Kwa Watumishi Bahi.....Akataza magari ya Serikali kulala nyumbani kwa mtu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wanaoishi nje ya eneo lao la kazi wawe wamehamia ifikapo Julai 30, mwaka huu.

“Tunataka watumishi wa umma wawajibike na waishi katika vituo vyao vya kazi. Nawataka watumishi wote wa wilaya hii wanaoishi Dodoma wawe wamehamia hapa ifikapo Julai 30 mwaka huu na wasiohamia nipewe majina yao,” amesisitiza.

Pia ameagiza magari yote ya Serikali baada ya kuisha muda ya kazi yawe yameegeshwa kwenye ofisi za halmashauri na ni marufuku kwa magari hayo kulala nyumbani kwa mtu.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizinduavituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa, vituo 15 vya haidrolojia, kanzidata ya taarifa za hali ya hewa na kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura wilayani Bahi, Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Serikali inataka watumishi wote wa umma nchini waishi kwenye vituo vyao vya kazi ili waweze kuwahudumia wananchi kwa ukaribu katika maeneo husika.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi, Bibi. Rachel Chuwa aanzishe mradi wa upimaji wa viwanja na viuzwe kwa watumishi na wananchi kwa gharama nafuu.

Waziri Mkuu amesema ni vema wilaya hiyo ikachangamkia fursa ya Serikali kuhamia Dodoma kwa kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo nyumba za kuishi, hoteli na sehemu za burudani ili watumishi waliohamia Dodoma wapate sehemu za kujipumzisha pindi wamalizapo majukumu yao.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu: Wataalamu Tumieni Taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)

$
0
0
WAZIRIMKUU Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa sekta za kilimo, mifugo na maji watumie taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ili waongeze ufanisi katika utendaji kazi wao.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizinduavituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa, vituo 15 vya haidrolojia, kanzidata ya taarifa za hali ya hewa na kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura wilayani Bahi, Dodoma.

Amesemakuwa kuongezeka kwa vituo vipya vya kisasa vya ufuatiliaji wa mwenendo wa hali ya hewa kumeboresha uhakika wa utabiri kutoka asilimia 81 hadi 87 kama inavyoshuhudiwa kwenye taarifa zinazotolewa katika siku za hivi karibuni. “Hivi sasa tukiambiwa kwamba mvua itanyesha katika maeneo fulani tunakuwa na uhakika kwa asilimia 87 ya utabiri huo,”.

“Vituo hivi ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa nchi wa utoaji wa huduma za hali ya hewa na haidrolojia kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuongeza ufanisi katika utoaji wa tahadhari za awali za majanga yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi,”.

Amesema kupitia mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Serikali imeweza kufungua vituo 51 vya kisasa vya hali ya hewa katika maeneo mbalimbali nchini na vituo 15 vya kupima ujazo wa maji kwenye mito iliyopo kwenye mabonde ya Pangani, Ruvuma na Pwani ya Kusini ambavyo vinajiendesha vyenyewe.

“Pia, mradi huu umeiwezesha Serikali kuanzisha kanzidata ya takwimu na taarifa za mafuriko         na ukame na taarifa za hali ya hewa na kuondoa ucheleweshwaji wa kupata takwimu au taarifa kutoka Wizara moja kwenda Wizara nyingine,” amesema.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano zitenge fedha kwenye bajeti zao ili ziweze kufuatilia na kusimamia mradi huo baada ya wafadhili kumaliza muda wao.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo katika kuhakikisha kuwa vituo na mifumo iliyowekwa inafanya kazi ipasavyo kwa usimamizi bora ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.

Wengine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola, Wabunge na Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bibi Natalie Boucly.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Muarobaini wa kumaliza tatizo la mafuta ya kula nchini wapatikana

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini kwa kufanya mageuzi makubwa katika zao la michikichi, alizeti na ufuta.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Balozi Dkt. Ramadhan Dau ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma.

’’Tunataka kufanya mageuzi makubwa ya zao la michikichi, tunataka kuondoa miti ya zamani na kupanda miche mipya. Tutafanya kampeni ya kuhamasisha upandaji wa miche mipya ya michikichi ili tuondoe tatizo la upatikanaji wa mafuta nchini,’’.

Waziri Mkuu amesema licha ya kuwepo kwa michikichi mingi nchini ila uzalishaji wake unafanyika kwa njia kienyeji, hivyo Serikali imedhamiria kuboresha kilimo hicho kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili liweze kuleta manufaa makubwa kwa Taifa na wakulima.

Amesema mbali na zao la michikichi, pia Serikali imedhamiria kuboresha mazao mengine ya mbegu za kukamua mafuta kama alizeti na ufuta, ambayo itayafuatilia kuanzia hatua za awali za uandaaji wa mashamba hadi masoko.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Tanzania bado ipo chini kwenye uzalishaji wa mbegu za kukamulia mafuta na inahitaji wawekezaji katika mazao hayo, hivyo amemuagiza Balozi wa Tanzania nchini Malaysia atafute wawekezaji hao.

’’Inawezekana kujitosheleza kwa mafuta ya kula kwa sababu Tanzania tuna ardhi ya nzuri yenye rutuba na watu ambao kilimo ndiyo shughuli yao kubwa. Na hivi karibuni nitafanya ziara mkoani Kigoma kwenda kuhamasisha kilimo cha michikichi,’’.

Kwa upande wake, Balozi Dkt. Dau amesema Malaysia ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa kilimo cha michikichi na inatengeneza zaidi bidhaa 400 kutokana na zao hilo, yakiwemo mafuta ya kuendeshea magari.

Balozi Dkt. Dau amemhakikishia Waziri Mkuu kwamba atatafuta wawekezaji kutoka nchi za Malaysia na Indonesia ili waje kuwekeza kwenye mashamba na viwanda vya mafuta na sukari.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Ujerumani OUT kombe la dunia nchini Urusi

$
0
0
Timu ya taifa ya Ujerumani imevuliwa rasmi ubingwa wa Kombe la Dunia baada ya kukubali kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa Korea Kusini.

Ujerumani ambayo kabla ya kuanza kwa fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia, ilikuwa ikipigiwa chapuo la kutetea ubingwa wake lakini leo iliingia uwanjani ikiwa na matarajio ya kupata ushindi kirahisi.

Hata hivyo mambo yakawa tofauti na matarajio yao, katika mchezo huo uliopigwa Kazan Arena, mjini Kazan kiasi kwamba kadiri muda ulivyokwenda Ujerumani walikutana na kizingiti kutokana na mfumo uliotumiwa na Kocha wa Korea Kusini, Shin Tae-yong wa 4-4-2 ambao ulikuwa wa kujilinda zaidi.

Hilo liliwafanya kupoteza umakini na kupiga mipira mingi isiyo na malengo jambo lililosababisha timu hizo kwenda mapumziko zikiwa hazifungana.

Mwanzoni mwa kipindi cha pili, Ujerumani walijaribu kusaka bao la kuongoza lakini kukosa umakini kwa washambuliaji wake kukawa kiwazo.

Kocha wa Ujerumani, Joachim Löw aliyetumia mfumo wa 4-2-3-1 na benchi lake la ufundi walikua katika wakati mgumu sana ilipofika dakika ya 60 huku matokeo yakiendelea kuwa bila bila wakati matokeo ya mechi nyingine ya kundi hilo yakionyesha kuwa Sweden ilikua ikiongoza kwa mabao 2-0 dhidi ya waliokua vinara wa kundi hilo kabla ya mechi hizo Mexico.

Kitendo cha Mesut Ozil kushindwa kuuweka mpira wavuni katika dakika ya 62 kuliwakera Low na hata mashabiki wa Ujerumani ambao walianza kuona dalili za kuvuliwa ubingwa wao katika raundi ya kwanza.

Ujerumani walianza kuvuliwa ubingwa baada ya Kim Young-Gwon kufunga bao la kwanza katika dakika ya pili ya muda wa nyongeza, jambo lililowafanya wachezaji wote kupagawa na kipa wa Ujerumani Manuel Neuer aliamua kulicha lango lake na kwenda mbele kusaidia kusaka bao.

Uamuzi huo ukawa kama kaa la moto kwao kwani mpira mrefu ulionaswa na Son Heung-Min ulimfanya mshambuliaji huyo wa Korea Kusini kulikimbilia lango lililokuwa tupu na hivyo kufunga bao rahisi katika dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza.

Kuingia kwa bao hilo kuliangusha kilio kwa wachezaji, viongozi  na mashabiki wa Ujerumani ambao tayari walifahamu fika kuwa wamevuliwa ubingwa katika raundi ya kwanza kwani tayari Sweden walikua wameilaza Mexico mabao 3-0 kuashiria kuwa ndio waliokua vinara wa kundi F na Mexico wanashika nafasi ya pili zote zikiwa na pointi sita, Korea Kusini wamemaliza wa tatu na Ujerumani wameburuza mkia kwenye kundi hilo wakiwa na pointi tatu.

Mahakama Yakaraa Ombi la Mmiliki wa Shule ya Scolastica

$
0
0
Mahakama ya Hakimu mkazi mjini Moshi imelikataa ombi la mmiliki wa Shule ya Scolastica, Edward Shayo anayekabiliwa na shtaka la mauaji ya mwanafunzi wa shule hiyo la kwenda kutibiwa.

Shayo pamoja na mwalimu wa shule hiyo, Labani Nabiswa na mlinzi wa shule hiyo, Hamis Chacha, wanatuhumiwa kumuua mwanafunzi wa kidato cha pili shuleni hapo, Humphrey Makundi (16).

Ombi hilo limewasilishwa leo Juni 27  na wakili Elikunda Kipoko anayemtetea mfanyabiashara huyo, aliyeomba Mahakama itoe kibali kwa mtuhumiwa huyo akatibiwe ingawa hakusema mteja wake anaumwa nini.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Jullieth Mawole amesema ingawa kutibiwa ni haki ya mtuhumiwa, mahakama hiyo haina uwezo wa kutoa kibali hicho kwa vile haina mamlaka kusikiliza kesi za mauaji.

“Mgonjwa ana haki ya msingi ya kupewa matibabu lakini Mahakama hii haiuhusiki kutoa kibali, hivyo Magereza ndiyo inayohusika kumpeleka mtuhumiwa wao hospitali,” alisema na kuongeza:-

“Mimi sina mamlaka ya kumruhusu mtuhumiwa kupelekwa hospitali hiyo ni kazi ya Mahakama Kuu,”

Hayo yalijitokeza baada ya upande wa Jamhuri katika kesi hiyo ukiwakilishwa na wakili wa Serikali, Agatha Pima, kuitaarifu Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika kwa asilimia 100.

Baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo, Hakimu Mawole aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 29 mwaka huu, wakati washtakiwa watakaposomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo vitakavyotumika dhidi yao.

Mwanafunzi huyo anadaiwa kuuawa Novemba mwaka jana na mwili wake kutupwa mita 300 kutoka shuleni hapo na ukazikwa bila kutambuliwa, hadi ulipofukuliwa kwa amri ya Mahakama.

Rais Magufuli Kumpokea Rais Mnangagwa Wa Zimbabwe Kesho

$
0
0
Nchi yetu imepata heshima ya kupokea  ugeni wa Mhe. Emerson Mnangagwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Zimbabwe ambaye anatarajiwa kufika hapa nchini siku ya Alhamis tarehe 28/06/2018 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 28/06/2018 hadi 29/06/2018.
 
Mhe. Mnagangwa atapokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport Terminal I na mwenyeji wake hapa nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli muda wa saa 5.00 asubuhi.
 
Ikumbukwe kuwa hii itakuwa ni ziara ya kwanza kwa Rais Mnagangwa kufika Tanzania kama Rais tokea aingie madarakani mwishoni mwa mwezi Novemba, 2017.
 
Ujio huu wa Rais Mnagangwa hapa nchini una lengo kuu la kuendelea kudumisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya nchi yetu na nchi ya Zimbabwe tangia wakati wa kupigania Uhuru wa Taifa hili la Kusini mwa Afrika.
 
Mgeni wetu anatarajiwa kuondoka hapa nchini tarehe 29/06/2018 saa 8.00 mchana na atasindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
 
Kwa kutambua ugeni huu sisi kama wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa niaba ya wananchi wote wa Tanzania tunawakaribisha wageni wetu na wajisikie kuwa wako nyumbani muda wote watakapokuwa hapa jijini.
 
Asanteni sana.
Paul C. Makonda
MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM
27/06/2018
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images