Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

RC Makonda Arejesha Nyumba Zilizopigwa Mnada Na Bank Ikiwemo Ya Mama Mjane

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana amekabidhi hati ya nyumba kwa familia ya Bi. Zainabu Kaswaka iliyoteseka na kusababisha ugonjwa wa Kupooza kwa Mume wake baada ya nyumba na ardhi yao kuuzwa baada ya Matapeli kutumia hati ya nyumba yao kuchukuwa mkopo Bank ya FNB pasipo familia kujua.

Upatikanaji wa hati hiyo umekuja baada ya majadiliano ya kina baina ya RC Makonda, Wanasheria na Bank ya FNB iliyotoa Mkopo ambapo baada ya Mkuu wa mkoa kuagiza kufanyika uchunguzi Bank ilibaini uzembe wa baadhi ya watumishi wao Bank hiyo uliopelekea kasoro hiyo.

RC Makonda pia amefanikiwa kumuhakikishia makazi ya kudumu Mama Mjane Bi. Benadetha Rwendera alietakiwa kuondoka kwenye nyumba yake na kujikuta akilala nje baada ya kununua eneo na kujenga Nyumba pasipokujua kuwa aliemuuzia eneo tayari alikuwa amechukuwa Mkopo Bank ya KCB jambo lililopelekea nyumba kuvunjwa na kuuzwa ambapo baada ya majadiliano baina ya RC Makonda na Bank ya KCB waliafiki kwa pamoja kumuachia mjane aendelee kuishi wakati kesi ikiendelea mahakamani na pindi hukumu itakapotoka utafanyika mgawanyo wa ardhi.

Aidha RC Makonda amesema hadi sasa Mkoa umefanikiwa kusikiliza kesi za Wananchi zaidi ya 1,028,000 ambapo Kesi zilizotatuliwa ofisini kwake ni 628,000 na kesi zilizokwenda mahakamani ni 60 ambapo Kati ya hizo kesi 17 zemeshatolewa hukumu na watu kupata haki zao chini ya usimamizi wa Ofisi ya RC Makonda kupitia msaada wa Mawakili waliowasimamia bila malipo.

Itakumbukwa RC Makonda aliahidi kuwasaidia wananchi wasiokuwa na uwezo wa kulipa mawakili Bure na haya Ndio matunda yake.

Wabunge CCM Wapigwa Onyo Kali

$
0
0
Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde amewapiga marufuku wabunge wa CCM kukikosoa chama hicho  ndani ya Bunge kwa kuwatahadharisha wao si wasemaji wa chama na wapo watu waliochaguliwa kufanya hivyo na amesema hayo kama 'bosi' wao.

Lusinde ametoa kauli hiyo jana  bungeni katika mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2018/19, baada ya baadhi ya wabunge kutoka majimbo ya mikoa ya kusini kuonyesha hofu ya CCM kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na serikali kuamua kubadili sheria ya korosho ili kuwezesha mapato yote yatokanayo na ushuru wa korosho inayosafirishwa nje kuingizwa mfuko mkuu wa serikali bila kugawanya.

Lusinde amewataka wabunge kama hawatakuwa na lugha sahihi ya kukosoa au kusifia  ni vyema wakatulia kuliko kufanya shughuli zinazopaswa kufanywa na watu wengine.

“Humu ndani tunapochangia tujiepushe na kazi za wengine. Eti tukifanya hivi tutashindwa sisi si wasemaji wa chama. Sisi wabunge wa CCM kazi yetu ni kuisimamia Serikali, kukosoa na kuitetea na nasema kama bosi wenu humu ndani ni marufuku kwa mbunge wa CCM kukizungumzia chama humu,” alisema.

“Hiki ni chama chenye Serikali na tupo hapa kuisimamia si kuikosoa CCM. Kauli za kuiweka chama kwenye hatari ya kushinda au kushindwa si sehemu yake hapa. Tunavyo vikao vya kukosoana tuataambiana huko. Kama wabunge wangu hamna lugha ya kuisifia na kuikosoa nyamazeni kimya, ”

Lusinde amedai kwamba ametoa onyo hilo siyo kama Mbunge tu bali kama mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho.

Pamoja na hayo akichangia kuhusu mjadala wa korosho uliokuwa  unaendelea ndani ya bunge Lusinde amewataka wabunge kama ni kusimamia ukweli wote wanapaswa kusimamia ukweli na kama ni mabadiliko basi yafanywe kwa kuzingatia sheria.

Kazi Sasa Imeanza: Ureno Kuvaana na Uruguay Huku Hispania Akikipiga na Urusi

$
0
0
Baada ya mechi nne za jana za kufunga makundi ya A na B kwenye Fainali za Kombe la Dunia kumalizika, hatimaye mechi mbili za raundi ya 16 bora zimefahamika ambapo Ureno itacheza na Uruguay huku wenyeji Urusi wakikabiliana na Hispania

Katika mechi mbili za Kundi B zilizomalizika  jana usiku, zilishuhudiwa zikimalizika kwa sare ambapo Hispania ilitoka sare ya 2-2 na Morocco huku Ureno ikitoka sare ya 1-1 na Iran. Hispania itacheza na mshindi wa pili wa Kundi A ambaye ni mwenyeji Urusi na Ureno itacheza na mshindi wa kwanza Uruguay.

Katika mechi ya Ureno dhidi ya Iran zilishuhudiwa penati mbili ambapo Cristiano Ronaldo alikosa huku Karim Ansarifard akipata kwa upande wa Iran. 

Penati hizo zimefanya michuano hii kufikisha penati 20 hadi sasa ambayo ni idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Fainali za Kombe la Dunia.

Ureno pia wamefanikiwa kusonga mbele kutoka hatua ya makundi kwa mara ya nne katika historia yao ya kucheza Kombe la Dunia. Wamefanya hivyo katika miaka ya 1966, 2006, 2010 na 2018.

Naye mshambuliaji wa Hispania Iago Aspas ambaye alifunga bao la kusawazisha la Hispania, sasa amehusika katika mabao 8 kwenye mechi 8 za Hispania hivi karibuni. Amefunga matano na kusaidia matatu. Hispania pia wamefanikiwa kumaliza hatua ya makundi bila kupoteza mechi tangu wafanye hivyo mwaka 2006.

Mbunge Hawa Ghasia:Sakata la gesi nilichomewa nyumba yangu moto, nilimpoteza baba lakini kwa hili sitakubali

$
0
0
Mbunge  wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia, amesema yuko tayari kupoteza maisha na mali zake, ili kupigania haki ya wakulima wa korosho kama ilivyokuwa wakati wa kupigania gesi asilia kuwanufaisha watu wa mikoa ya kusini.

Ghasia aliyekuwa waziri wa iliyokuwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), alitoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma jana, alipokuwa anachangia mjadala wa mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha na Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2017.

Alisema wakati wananchi wa mikoa ya kusini wakiandamana kupinga kujengwa kwa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, alikuwa serikalini na aliamini usambazaji wa gesi hiyo utanufaisha wananchi wote lakini imekuwa kinyume.

“Kwanza nianze kwa masikitiko makubwa sana ambayo yanasambazwa kwa makusudi dhidi ya Wabunge wanaotetea kupelekewa pembejeo Kwenye maeneo yao.Tuna taarifa jana watu wamekaa vikao waje humu kutudhalilisha Wabunge tunaowatetea wananchi wetu wapate pembejeo.

“Wabunge wote humu ndani tuna haki sawa za kutetea wananchi wetu. Anayetoka Kwenye pamba ataitetea pamba, anayetoka Kwenye madini atatetea madini yake, anayetoka Kwenye korosho ana haki ya kuitetea korosho yake.Mimi napenda niwahakikishie wananchi wanaolima korosho; Wabunge wao tupo imara, tutapambana kuhakikisha haki hii inapatikana. Hata kama haitapatikana, wajibu wetu tutautimiza kama wawakilishi kuja kuwatetea wananchi,” ameongeza

“Mimi nilikaa upande wa serikali wakati wa gesi. Niliitetea Serikali kupeleka gesi kokote Tanzania kwa sababu nilijua serikali inafanya haki. Nilichomewa nyumba yangu moto. Mabomba ya kupeleka maji Kijijini kwetu yaling’olewa. Mikorosho ya Baba yangu ilikatwa. Minazi ya Baba yangu ilikatwa. Katika process hiyo nilipoteza Baba yangu. Bado nilimshukuru Mwenyezi Mungu nilisema Alhamdulilah Alhamdullilah Alhamdulillah! Kwa sababu niliona serikali inachokifanya iko sahihi,” alisisitiza Ghasia.

“Ninachosema kama kuna mtu amefanya ubadhilifu, hata kama ni Hawa Ghasia Kwenye mfuko wa korosho, nipelekeni Mahakamani.Hao wananchi tunaowambia wabunge wa Kusini wabinafsi wanataka kuigawa nchi wana akili na wanajiongeza.”

Mawaziri Wasiopokea Simu Kushughulikiwa

$
0
0
Serikali imesema iko tayari kupokea malalamiko kutoka kwa Watanzania ambao wanaona hawakutendewa haki na Mawaziri ikiwemo kutopokelewa simu zao.

Hayo yameelezwa leo Juni 26 bungeni, na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika. Mkuchika amesema simu ni sehemu ya mawasiliano.

Mkuchika ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Jaku Hashim Ayub ambaye amewashitaki mawaziri akisema kuna mawaziri wamekuwa ni tatizo kwa kutopokea simu za wabunge hivyo akasema hali inaweza kuwa mbaya kwa wananchi kama watawapigia.

Katika swali lake mbunge huyo amesema mawaziri wote wamekuwa ni tatizo kubwa katika kupokea simu za wabunge wanapowapigia na akataka namba za mawaziri ziwekwe hadharani kama ilivyo kwa namba za makamanda wa polisi wa mikoa.

“Hii ni kwa Mtanzania yeyote akiona hakutendewa haki ikiwemo simu yake kutokupokewa, aje kutoa taarifa za malalamiko na sisi tutazifanyia kazi na kama litakuwa gumu kwangu nitapeleka kwa ngazi ya juu,” amesema Mkuchika.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume,maumbile Madogo, Mvuto Wa Mapenzi ,magonjwa Sugu

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0785687900

Mama Atiwa Mbaroni Kwa Kumtupa Mtoto Wake Chooni

$
0
0
Rhobina Andrew (40) mkazi wa Kitongoji cha Nyatiti kijiji cha Buriba, kata ya Sirari wilayani hapa mkoani Mara, anashikiliwa na polisi akidaiwa kujifungua na kutupa kichanga kwenye choo cha shimo.

Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Henry Mwaibambe, amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Amesema jeshi hilo lilimkamata Rhobina jana Juni 25 baada ya kupewa taarifa na wananchi ambako alifikishwa kituo cha polisi Sirari.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Buriba, Alex Chacha alisema alipigiwa simu Juni 25 na mkazi wa kitongoji hicho na kuelezwa kuwa mtoto huyo ameokotwa kwenye tundu la choo akiwa hai.

“Tulfanikiwa kubomoa choo na kutoa mtoto akiwa hai, tukamwosha kwa kuwa hakuwa amefunikwa chochote mwilini lakini wakati tunampeleka kituo cha afya akafariki dunia," amesema Chacha.

Familia Yakanusha Taarifa za Kifo Cha Mzee Majuto Zinazosambazwa Mitandaoni

$
0
0
Baada ya kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha Muigizaji Mkongwe nchini, Mzee Amri Majuto, familia yake imeiomba serikali na vyombo husika ikiwemo mamlaka ya mawasiliano, kuwachukulia hatua watu wanaozusha taarifa za kifo kwa madai kuwa sasa ni mara ya 10.

Akikanusha taarifa za kifo cha muigizaji huyo, mtoto wa Mzee Majuto, Hamza Majuto amesema kuwa kama familia wameziona taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii na wala hawafahamu nia ya watu hao wanaozusha taarifa za kifo cha baba yake mara kwa mara.

Aidha mtoto huyo wa Mzee Majuto amesema kwamba baba yake kwa sasa anaendelea vizuri tangu aliporudi kutoka nje ya nchi na sasa (Majuto) yupo kwenye mapumziko kama jinsi ambayo inatakiwa.

"Tangu jana nimepokea simu na sms zaidi ya 500 zikitaka nithibitishe kuhusu kifo cha mzee. Kiukweli hii ni mara ya 10 kwa mzee kuzushiwa taarifa ya kifo. Natambua kwamba kuna vyombo vya usalama pamoja na mamlaka inayohusika na makosa ya mitandao hivyo hili la kuzusha kifo ni kosa la jinai naiomba basi TCRA ifuatilie ili kujua dhamira ya huyu mtu ambaye amekuwa akizusha taarifa za kifo" amesema Hamza.

Hata hivyo, Kijana huyo amesema kwamba kwa sasa wapo mapumzikoni lakini hawawezi kusema ni wapi kwa ajili ya kuepusha usumbufu ili kumsaidia mzee Majuto apate mapumziko mazuri.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Atoa Maagizo Mazito Hospitali ya Ocean Road

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeitaka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kuhakikisha mashine za utoaji wa huduma za mionzi ziwe zinafanya kazi haraka iwezekanavyo ili kuweza kurudisha huduma hiyo kwa wagonjwa ambao wengi wao ni wanawake wenye tatizo la saratani ya mlango wa kizazi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara yake ya kikazi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ili kukagua utoaji wa huduma za matibabu katika hospitali hiyo na kupata fursa ya kuzungumza na wagonjwa mbalimbali waliokuwa wakipata huduma za tiba ya mionzi hospitalini hapo, huku baadhi yao wakilalamika kwamba wamekuwa wakitumia muda mrefu kusubiri kupata huduma hususani za mionzi ya nje.

Vile vile, Waziri Ummy alitembelea kitengo cha utoaji wa huduma za mionzi ya ndani na kujionea changamoto ya kutokufanya kazi kwa mashine hizo za utoaji wa mionzi ya ndani kutokana na kukosekana kwa vifaa vya 'transfer tubes' na 'gyn applicators'.

"Natoa maelekezo kwa uongozi wa Hospitali mhakikishe mnaweka utaratibu mzuri ambao utapunguza muda kwa wagonjwa kusubiri huduma za mionzi ikiwemo kuwepo na ratiba ambayo kila mgonjwa atajua anafika saa ngapi kupata tiba hiyo pia fanyeni utaratibu wa kupata kifaa kilichoharibika mapema iwezekanavyo", amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage amemhakikishia Waziri Ummy kuwa atajitahidi ili vifaa vilivyoharibika vinapatikana ndani ya siku mbili kutoka Hospitali Bugando na pia wameagiza vifaa hivyo kutoka kiwandani nje ya nchi kwa gharama ya Euro 43,200.

Meneja wa Diamond Aitibua Mahakama.

$
0
0
Meneja wa msanii Diamond Platnumz anaejulikana kama Babu Tale ameitibua  mahakama baada ya kutakiwa kufika mahakamani jana  lakini hakufika  kufika kwa madai ya kuwa nje ya nchi huku akiwa alishakatazwa  kutoka nje ya nchi ikiwa kesi yake ikiendelea mahakamani.

Meneja huyo anakabiliwa na kesi ya madai baada ya kampuni yake kufanya matangazo na baishara ya  kanda za dini za shekhe mmoja jijini Dar es salam bila ridhaa yake na kuamuliwa kulipa fidia lakini alishindwa kulipa fidia hiyo.

Babu Tale alitakiwa kufika mahakamani jana kusikiliza uamuzi wa shauri lake kuhusiana na uhalali wa amri ya mahakama hiyo kumkamata na kumfunga jela kama mfungwa wa madai baada ya kushindwa kulipa fidia.

Hata hivyo hakutokea, badala yake alifika kaka yake Idd Shaban Taletale. Wakili wao, Issa Chondo aliieleza mahakama kuwa Babu Tale hayupo mahakamani kwa kuwa amesafiri nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Kitendo cha kusafiri nje ya nchi bila kutoa taarifa na hivyo kushindwa kufika mahakamani kilimfanya Jaji Mkasimongwa aseme kuwa alichokifanya Babu Tale si cha kiungwana, kauli aliyoirudia mara tatu kuonyesha kuwa kilimuudhi.

Awali Wakili Chondo alidai kuwa mteja wake amekwenda kutibiwa nchini Afrika Kusini, lakini alipobanwa maswali na jaji alijikuta akibadili kauli yake na kusema hajui amekwenda nchi gani, huku akiiomba Mahakama imruhusu awasiliane naye kumuuliza.

Maelezo ya wakili huyo yalimshangaza jaji na kumhoji wakili huyo kuwa inawezekanaje mteja wake ambaye yuko kwenye amri ya kukamatwa asafiri nje ya nchi bila kumuaga wakati anajua kuwa anatakiwa mahakamani.

“Lakini si anajua yuko under arrest? (chini ya amri ya kukamatwa?) Inawezekanaje amekwenda nje ya nchi bila taarifa, sasa huu si uchokozi?” alihoji Jaji Mkasimongwa baada ya Wakili Chondo kutoa taarifa kuwa mteja wake amesafiri nje.

Casto Dickson Ataja Sababu Za Kuchora Tattoo Ya Tunda

$
0
0
Mtangazaji wa kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv, Casto Dickson amefunguka na kutaja sababu zilizomsukuma mpaka kufikia uamuzi wa kuchora tattoo ya jina la Tunda mkononi mwake.

Siku ya jana Casto alianika tattoo yake mpya Kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuonyesha jinsi gani amekolea kwa mpenzi wake huyo mpaka kuamua kuchora Jina lake.

Casto amesema kuwa  alitumia dakika 10 kuamua achore tatoo hiyo na hawezi juta kwa kuwa ameutendea haki moyo wake.

"Mimi nimechora ile tattoo kwa sababu kiukweli nampenda yule mwanamke na siko naye kwa ajili ya kumpitia, Hapana ila tuna malengo na kila mtu amepanga atabadilika na tumeamua kufanya maisha.

"Tunda ndio mwanamke pekee ambaye nimechora jina lake mwilini mwangu kwahiyo watu watambue kuwa ana maana sana kwangu halafu kuna wanaosema kuwa ni mapema sana kwa mimi kuchora Tattoo ....ninachotaka watu wajue ni kuwa tumekuwa pamoja kwa muda, mrefu mapenzi yetu hayajaanza jana wala juzi”.

Lakini pia Casto amesisitiza kuwa hata kama wakiachana yeye na Tunda hawezi kufuta ile tattoo lakini amesema anajua kuwa hawawezi kuachana, watakuwa wote milele.

Waziri Mkuu Kuzindua Vituo 51 Vya Hali Ya Hewa Vinavyo Jiendesha Vyenyewe,

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Vituo 51 vya Hali ya Hewa vinavyojiendesha vyenyewe, Vituo 15 vya Kupima wingi wa maji Mtoni, Kanzidata ya Taarifa za Hali ya Hewa pamoja na Kituo cha Operesheni na Mawasilino ya Dharura.   
 
Uzinduzi huo utafanyika Jumatano, tarehe 27 Juni, 2018 katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma. Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1) litaonesha shughuli hiyo mubashara kuanzia saa sita mchana.

Akizungumza wakati wa maandalizi ya Uzinduzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na kuwakaribisha wananchi wote kushiriki katika uzinduzi huo, amebainisha kuwa Kuzinduliwa kwa vituo hivyo , kanzidata na kituo cha Operesheni na Mawasiliano nchini ni  baadhi ya jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo  katika kuhakikisha menejimenti ya maafa inaimarika nchini.

 “Vituo hivyo vitawasaidia Watanzania ambao ni wadau wakubwa wanaotumia Taarifa za Hali ya Hewa katika kupata taarifa za awali za utabiri wa uwepo wa majanga au kutokuwepo ili kujiandaa, kuyakabili endapo majanga yatatokea pamoja na kusaidia katika maandalizi ya shughuli za maendeleao ikiwemo upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa kusaidia kupanga aina za mazao yanayofaa kulimwa kulingana na mabadiliko ya tabia nchi”, amesema Mhagama

Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Mabadiliko ya Tabianchi na Uboreshaji wa Mifumo ya Tahadhari za Awali, imeweza kuimarisha miundombinu na mazingira ya kufuatilia taarifa za mabadiliko ya tabianchi na kutengeneza mifumo imara ya kutoa tahadhari za awali, usimamizi wa maafa na kuchangia katika mipango ya maendeleo endelevu.

Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Mabadiliko ya Tabianchi na Uboreshaji wa Mifumo ya Tahadhari za Awali,  Uliandaliwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kufadhiliwa kupitia Mfuko  wa Uboreshaji wa  Mazingira Duniani (GEF). Mradi umetekelezwa na Wizara na Taasisi za Serikali ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Hali ya Hali ya Hewa Tanzania,  tangu mwaka 2014 hadi  Juni mwaka 2018.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILINO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU

Tangazo La Kusitisha Maombi Ya Kazi Jeshi la Polisi

$
0
0
Jeshi la polisi Tanzania linawatangazia vijana wote wa JKT waliopita oparesheni Kikwete kusitishwa kwa maombi ya ajira mpya zilizokuwa zimetangazwa hivi karibuni kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Hivyo hakutokuwa na upokeaji wa maombi mapya kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali. 

Aidha iwapo kuna waombaji wa ajira mpya ambao walikwisha tuma maombi yao ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, mnajulishwa kusitishwa kwa zoezi hilo.

Sting Achi

[Mussa A. Taibu – ACP]
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya.

Mume na Mke Wateketea kwa Moto.....Ni Baada ya Mwanaume Kufunga Mlango na Kisha Kuwasha Moto

$
0
0
Mume na mke, wamefariki dunia leo Juni 26 baada ya mwanaume huyo, kufunga mlango wa nyumba kwa ndani, kisha kutia moto nyumba hiyo.

Imeelezwa kuwa, tukio hilo limetokea, usiku wa saa saba, mnano Juni 25 katika eneo la Kilimahewa, Mailimoja, Kibaha.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa, chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Jonathan Shanna amemtaja mwanaume huyo kuwa ni Hussein Zaid (58) na mwanamke ambaye amefariki katika tukio hilo ni mke wake mdogo, Zainabu Juma (42).

“Siku ya tukio hilo Hussein alijaribu kujiua akiwa amejifungia ndani ya nyumba yake pamoja na mkewe huyo kwa kuzikusanya nguo zilizokuwa humo na kuziwasha moto kwa kutumia kiberiti,” alisema Kamanda Shanna na kuongeza:

"Kabla ya kutekeleza tukio hilo kwanza alijaribu kumchoma mke wake huyo kwa kisu na alipoona hajafanikiwa ndipo alipoamua kuichoma moto nyumba wote wawili wakiwa ndani.”

Ameongeza kuwa baadhi ya majirani walifika kutoa msaada na kuwajulisha Polisi ambao walifika eneo hilo.

“Hata hivyo, licha ya kuwaokoa wote wawili wakiwa hai, kisha kuwapeleka Hospitali ya Tumbi, lakini  walihamishwa Hospitali ya Muhimbili ambako walifariki dunia wakipata matibabu hospitali,” alisema

Magazeti Yanayoandika Habari za Uchochezi wa Kidini, Kikabila Kushitakiwa

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema wanaochukizwa na magazeti yanayoandika kuhusu ukabila na udini waende mahakamani na wizara itakuwa shahidi namba moja.

Akijibu hoja zilizojitokeza bungeni wakati wa mjadala wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19 ya Sh32.45 trilioni leo Juni 26, 2018 amesema jana kulijitokeza suala la ukabila ambalo haliwezi kubaki katika taarifa rasmi za Bunge bila kujibiwa.

Dk Mwakyembe amesema suala hilo lilizungumzwa na mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia.

“Mbunge ninayemuheshimu sana na mdogo wangu Mbatia, pamoja na maudhi yote tunayoweza kuyapata, sisi viongozi tusikubali kwa njia yoyote kuwa katika basi la ukabila na udini na tukifanya hivyo tutasahau mafanikio makubwa tuliyoyapata hasa kujenga umoja,” amesema Dk Mwakyembe.

Amesema mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini aligusia magazeti ya Tanzanite na Jamvi la Habari, kwamba yana ubaguzi wa Wachanga.

“Haya magazeti yanaweza kushitakiwa na sheria ya habari kifungu cha 41 na unaweza kuyapeleka mahakamani,” amesema waziri Mwakyembe.

Amesema, “Kama umetukanwa wewe nenda mahakamani na sisi tukakuwa shahidi. Hivi leo Mchaga ni nani, nani anaweza kushika jiwe na asimguse mkewe au mjomba wake.”

Waziri Mwakyembe amesema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipigania uhuru wa nchi na wenye kuwaweka Watanzania katika umoja bila ukabila na udini.

Amesisitiza wananchi kudumisha amani na umoja na kuepuka ukabila na udini.

Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza baada ya majibu ya Dk Mwakyembe amesema, “Hili jambo la ukabila si la kuliendekeza kusema hapa, tunaweza kusema tunadhani tunajenga kumbe tunafanya makosa makubwa.”

Ndugai amesema, “Unaweza kujikuta unalalamika jambo fulani kumbe jamii hiyo iko serikalini na kama kuna shida katika jambo hilo, tunong’one pembeni.”

Spika Ndugai amesema, “Makundi ya kisiasa na kijamii, tuendelee kuwa Watanzania wamoja na dalili za ukabila ni mbaya. Hatuwezi kufika popote kama tunaendekeza ukabila.”

Kagere aitosa rasmi Yanga

$
0
0
Na, magdalena kashindye
Mshambiliaji wa timu ya Gor mahia ya Kenya na raia wa Rwanda meddie kagere amesaini mkataba wa kuitumikia simba kwa miaka miwili.

Nyota huyo anayejua kucheka na nyavu amemalizana na wekundu wa msimbazi simba kuitumikia timu hiyo kwa kandarasi ya miaka miwili kwa thamani ya shilingi milioni 110 za kitanzania.

Mshambiliaji huyo aliyekuwa akiwindwa na timu ya yanga atakuwa ameitosa rasmi  timu hiyo iliyokuwa inamuwinda kuongeza nguvu katika mchuano ya kimataifa .

Timu ya Gor mahia tayari imeziba pengo la kagere kwa kumchukua Mshambiliaji wa kimataifa wa Uganda anayechezea vipers FC Eris Ssekisamba.

Spika Ndugai: Wabunge Mkiikataa Bajieti Hii Rais Atalivunja Bunge

$
0
0
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kama wabunge wataipigia kura ya hapana Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19, Rais atalivunja Bunge.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo asubuhi bungeni Juni 26, 2018 wakati akitoa maelezo ya kile kitakachofanyika leo saa 11 jioni ya kuipitisha bajeti.

“Endapo mlio wengi mtaikataa Bajeti ya Serikali, Bunge hili Rais atalivunja haraka,” amesema Spika Ndugai.

Baada ya kauli hiyo, minong’ono ya kutoka pande zote za wabunge ilisikika. Spika Ndugai hakuishi hapo, akasema tena:

 “Na baadhi yenu, mkirudishwa majimboni hamrudi kwa hiyo akili za kuambiwa changanya na zako.”

Amewaomba wabunge wote kuwapo bungeni ifikapo saa 11 jioni huku akisisitiza kwamba mbunge hapigi kura kwa jambo moja, bali ni kwa mfuko wote wa bajeti, kwa hiyo ni vizuri wananchi wakaelewa.

Katika hatua nyingine, Spika Ndugai amesema kuanzia sasa bendi ya muziki ya polisi, (Brass Band) itaingia bungeni kuongoza wimbo wa Taifa kabla na baada ya kikao cha Bunge kuanza.

Waziri Mpango Asema Ataitembelea Mikoa ya Kusini....Hakuna Wa Kumzuia na Yupo Tayari Hata Kufa

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema atatembelea mikoa ya Lindi na Mtwara licha ya vitisho vilivyopo na yuko tayari kufa, na kamwe hawezi kuihujumu mikoa hiyo kiuchumi na hakuna anayeweza kumzuia kuitembelea katika kutekeleza majukumu yake.

Dkt. Mpango ametoa kauli hiyo leo, Bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha hoja yake ya Bajeti ya Serikali aliyoiwasilisha Juni 14 mwaka huu, ambapo amesisitiza kuwa hakuna mtu wa kumzuia na iwapo kuna mwenye chuki binafsi anamwombea msamaha kwa Mungu..

“Kama yupo mtu ana chuki binafsi na Philip Mpango namwombea msahama kwa Mwenyezi Mungu, na niwatahadharishe wanaokula fedha za umma wanakula sumu,” amesema Dkt. Mpango.

Waziri Mpango Ameongeza, “Mimi Philip Mpango siwezi kamwe kuwahujumu wakulima wa mkoa wa Lindi na niwahakikishe watanzania kuwa Mtwara na Lindi nitakwenda iwe kutimiza wajibu wangu na ni uhuru wangu na hata ikibidi kufa katika kulitumia taifa” ameongeza Waziri Mpango.

Amesema amewatumikia Watanzania wote bila ubaguzi, amefundisha wanafunzi wote wakiwamo wanaotoka mikoa ya Kusini bila upendeleo na amewahi kuwa mshauri wa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete na hakuwahi kuwa na upendeleo.

Tayari baadhi ya wabunge wametishia kufanya maandamano iwapo Serikali haitatoa asilimia 65 za ushuru wa mauzo ya korosho nje kwa ajili ya maendeleo ya zao hilo, huku wakipinga mabadiliko ya Sheria ya Korosho yanayokusudiwa kufanywa na Serikali ili ushuru huo upelekwe katika Mfuko Mkuu wa Hazina.

Waziri Mkuu:Vigogo Wa Dawa Za Kulevya Waanza Kukimbia Nchi

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kumewezesha kukamatwa kwa wafanyabiashara wakubwa waliokuwa wakitamba kwamba hawawezi kuguswa.

“Sasa hivi dawa zinakamatwa kwelikweli na wale wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya waliokuwa wakijiita vigogo na kutamba kuwa hawakamatwi na hata wakikamatwa wanaachiwa, wameanza kuikimbia nchi,” amesema.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Juni 26, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika uwanja wa Gangilonga, mkoani Iringa. 
 
Waziri Mkuu amesema Serikali baada ya kuanzisha Mamlaka hiyo, iliiwezesha kwa kuipatia rasilimali fedha, watendaji na vitendea kazi na tayari mafanikio yameanza kuonekana.

Amesema kila mmoja anapaswa kuliona suala hilo la dawa za kulevya kama jambo hatari kwa mustakabali wa Taifa letu na akasisitiza kuwa watu wasioneane haya katika vita hiyo kwa kuwataja wahusika kwa sababu huuzwa katika mitaa yao na wauzaji wanawafahamu.

“Nawasihi viongozi wa siasa, dini pamoja na vyombo vya habari, tuendelee kukemea kwa nguvu zote matumizi na biashara ya dawa za kulevya,” amesema.

Waziri Mkuu amesema matumizi ya dawa za kulevya yapo zaidi kwenye miji mikubwa hasa ya Dar es Salaam, Arusha, Tanga na Mwanza, pia kasi ya kuenea kwa matumizi hayo kwenye miji midogo nayo ni kubwa hasa katika mikoa ya Iringa, Dodoma na Mbeya na Morogoro.

Wakati huohuo,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama amesema tatizo la dawa za kulevya limeiathiri duniia na watu wengi wameathirika na janga hilo ikiwemo jinsia na rika zote.

Amesemabiashara ya dawa za kulevya imesababisha madhara makubwa mbalimbali nchini yakiwemo ya kiafya, kijamii, kiuchumi, kimazingira, kisiasa na kiusalama. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni“tujenge maisha yetu, jamii yetu na utu wetu bila dawa za kulevya”

“Zipo dalili kwamba, endapo biashara hii itaachwa iendelee, athari zaidi zitajitokeza ikiwemo kuingiliwa kwa misingi ya kiutawala na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kwa manufaa  yao  binafsi,” amesisitiza.

Awali,  mmoja wa waathirika wa dawa hizo Bi. Reja Chawe ambaye alitumia dawa hizo kwa muda wa miaka 15 na alianza kutumia akiwa kidato cha pili, alisema alianza akiwa kidato cha pili baada ya kushawishiwa na rafiki yake wa kiume na alianza kwa kutumia bangi.

Bi Reja alisema kwa sasa ameacha ila anaumia sana akiona vijana wenzake wanaitumia dawa hizo kwa sababu yeye alipata matatizo makubwa wakati akitumia dawa hizo ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ambazo ni za kujidhalilisha.

“Nilikuwa naitwa majina mabaya, nililala makaburini na nilifanya kazi ya kuchimba makaburi ya watoto wachanga na kuwazika. Mimi nilikuwa napitisha hata mwezi bila ya kuoga, pia nilikuwa naiba. Sikupenda, ila mkumbo tu, nawaomba vijana wenzangu waachane na dawa za kulevya,” amesema.

Muathirika mwingine, Bi. Christine Mponzi ambaye bado anatumia dawa ameiomba Serikali imsaidie ili aweze kuachana na dawa hizo ambazo alianza kutumia miaka 25 iliyopita na sasa anasikia maumivu ila anashindwa kuacha kutumia dawa hizo.

Alisema dawa hizo zimesababisha atengane na familia yake, ambapo watoto wake wawili nao wamemkataa kutokana na hali aliyokuwa nayo.” Dawa za kulevya ni hatari mimi nilikuwa mzuri na nilikuwa na mume wangu na watoto wamenikataa kwa sababu mama yao wananiona sina hadhi. Nilianza kufanya biashara kabla ya kutumia,”.

Tayari Serikali imesikia kilio chake, baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista kumkabidhi kwa muendeshaji wa nyumba za upataji nafuu (sober house) ili aanze kupatiwa matibabu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Mkuu Asifu Juhudi Za Aga Khan

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Mtandao wa Aga Khan (AKDN ) una lengo la kuleta maendeleo ya Taifa.

Ameyasema hayo jana usiku (Jumatatu, Juni 25, 2018) jijini Dodoma wakati akizungumza na viongozi na wananchi waliohudhuria hafla ya siku ya IMAMAT pamoja na kuhitimisha maadhimisho ya mtukufu Aga Khan kuwa kiongozi wa mtandao huo kwa miaka 60.

Waziri Mkuu alisema maadhimisho hayo yanaonesha kujitolea kwa hali ya juu na kwa moyo wa dhati ya maisha ya Mtukufu Aga Khan katika kuwahudumia na kuwalinda watu hususan wanyonge.

"Leo hii jamii zetu zinanufaika na juhudi hizi za kujitolea kwa hali ya juu alikokufanya Mtukufu Aga Khan kupitia utoaji wa misaada hasa katika kuboresha maeneo ya huduma muhimu kama elimu na afya,” alisema.

Alisema rafiki huyo mkubwa wa Tanzania amechangia kwa kiasi kikubwa kuinua jamii kiuchumi hususan kwa kupigania kuboreshwa kwa huduma za afya na elimu kupitia uwekezaji unaofanywa na Mtandao huo wa AKDN.

Waziri Mkuu aliongeza kuwa maadhimisho hayo yanatoa somo muhimu kuhusu haja ya kujitolea, na kufanya juhudi za kutosha katika kila jambo sambamba na kuwahusisha watu wengine.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema lengo hilo halina budi kuongozwa na nia ya kuboresha maisha ya watu kwa namna yenye staha.

Awali, Mwakilishi Mkaazi wa Mtandao wa Aga Khan, Bw. Amin Kurji aliipongeza Serikali kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.

Alisema Mtandao wa AKDN umeenea katika mataifa 35 ambako wanatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kwa Tanzania wanatekeleza miradi tisa ikiwemo ya kilimo, afya, maendeleo ya jamii na elimu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images