Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Atiwa Mbaroni Kwa Kumlawiti mtoto wa mwaka mmoja kwa imani za kishirikina

$
0
0
Kadege Thabit (18), mkazi wa Utemini wilaya ya Uyui mkoani Tabora anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa mwaka mmoja na miezi miwili kutokana na imani za kishirikina.

Tukio hilo, limetokea Juni 21 saa tatu asubuhi katika kata ya Ndono. Akizungumzia tukio hilo leo Juni 27, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa, amesema mtuhumiwa alimchukua mtoto huyo na kumwingilia kinyume cha maumbile.

Kamanda Mutafungwa ameeleza kwamba mtuhumiwa alitenda tendo hilo baada ya kumchukua mtoto huyo kutoka kwa mama yake akidai anaenda kumnunulia maandazi.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa baada ya kumnunulia maandazi mtoto huyo alimpeleka chumbani kwake akafunga mlango ndipo akatenda unyama huo.

“Uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la polisi umebaini kuwa sababu za kufanya ukatili huo ni imani za kishirikina, na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unafanyika,” amesema

Kamanda Mutafungwa amefafanua kwamba  mtuhumiwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa alidai kuwa alitenda kosa hilo kutokana na maelekezo ya mganga mmoja wa kienyeji kwamba ataweza kupata mali nyingi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 28

Zainab Katimba: “Serikali ina mkakati gani wa kuwaendeleza vijana?”

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Kakunda imesema kuwa zipo idara nyingi ambazo zinaweza kuwasaidia vijana kujikwamua ili kuendeleza biashara kama kujiunga katika idara ya vijana kwenye Halmashauri.

Kauli hiyo imetolewa na Kakunda jana, Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM)Zainab Katimba, aliyehoji “Kwa kuwa jitihada za kutoa mitaji kwa vijana na wanawake inabidi ziende sambamba na kuwajengea uwezo wa kuanzisha na kuendeleza biashara, Je serikali ina mkakati gani wa kuwatumia hawa maafisa Biashara katika kuwajengea uwezo vijana wanaokuwa katika vikundi ambao wananufaika na asilimia 10 inayotengwa kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri?

“Nataka nikuhakikishie kwamba vijana katika nchi hii wana idara nyingi sana za kuweza kuwasaidia mawazo ya kujikwamua kutoka pale walipo kutoka kwenda mbele, kuna idara ya vijana katika Halmashauri kuna idara katika maendeleo ya jamii, kuna idara ya mipango sasa Maafisa Biashara tunawaongezea sehemu nyingine,” alisema Kakunda.

“Kwahiyo mimi napenda nitumie nafasi hii kuwaomba vijana wa nchi hii kutumia fursa ambazo zipo katika Halmashauri wamekuwa hawazitumii ipasavyo, ukienda katika Halmashauri unaona maombi ya vijana yako asilimia 10 ya maombi yote yaliyowasilishwa naomba tujitahidi sisi Wabunge kuwaelimisha kuwaomba vijana wajitokeze katika vikundi na watumie fursa zilizopo kwaajili ya kujiendeleza na serikali tuko macho kuhakikisha jambo hilo linatekelezwa vizuri.”

Baba mzazi wa Michael Jackson, Joe Jackson afariki dunia

$
0
0
Baba mzazi wa aliyekuwa Mfalme wa muziki wa Pop duniani Michael Jackson, Joe Jackson amefariki dunia  jana  mchana mjini Los Angeles nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 89.
 
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Joe Jackson alilazwa tangu mwezi Machi mwaka huu  na alikuwa na anasumbuliwa na Saratani.

Joe Jackson ni moja Mameneja walioacha historia nchini Marekani kwa kuwameneji watoto wake katika kazi zao za muziki akiwemo marehemu Michael Jackson na Janeth Jackson.

Waziri Mkuu asisitiza wanaume kupima VVU

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi hasa wanaume kupima Virusi vya Ukimwi na wale wenye maambukizi waanze dawa mapema.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana Juni 27 wakati wa uzinduzin wa vituo 51 vinavyojitegemea vya kupima hali ya hewa, Wilayani Bahi, Dodoma.

 “Ugonjwa wa Ukimwi ni hatari na hatari zaidi ni pale wananchi tunapotembea tukiwa hatujiju kama tuna VVU ama hatuna, kwa hiyo mipango ya Serikali ni kila mmoja bora ajijue afya yake kwa kwenda kupima,”alisema.

Pia amewataka viongozi mbalimbali watakapoandaa mikutano yenye zaidi ya watu mia moja kuweka vibanda kwa ajili ya kupima kwani huduma huyo haina gharama.

“Nahamasisha wote kuanzia watumishi na wananchi wote kupima afya zao, tunataka ifikapo mwaka 2020 asilimia 90 ya wananchi wawe wanazijua afya zao hasa wanaume,”alisema na kuongeza:

“Na kwa wale wataokutwa na maambukizi waanze kutumia dawa na uzuri sasa hivi hizi dawa zinaanza kutumiwa mara tu baada ya kugundulika umeathirika.”

Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutenga fedha kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa mradi wa vituo vya hali ya hewa ili wananchi wapate taarifa za hali ya hewa katika maeneo mbalimbali nchini.

Pia amewaagiza wataalamu wa sekta mbalimbali kutumia taarifa za hali ya hewa katika kazi zao ikiwemo kutoa taarifa mbalimbali kwa wakulima na kushauri maeneo gani wanaweza kufanya kilimo.

Mbowe na Vigogo wengine CHADEMA Wapinga Kesi Yao Kusikilizwa

$
0
0
Viongozi 9 wa CHADEMA, akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe jana June 27, 2018 kupitia wakili wao wamewasilisha maombi chini ya hati ya dharura ya kutaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu isitishe usikilizaji wa kesi yao ya kufanya maandamano.

Maombi hayo yanayotarajiwa kusikilizwa June 28, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri yamewasilishwa na wakili utetezi, Peter Kibatala.

Katika maombi hayo namba 15/2018 upande wa utetezi umedai kuwa wanaomba usikilizwaji wa kesi hiyo usitishwe hadi pale Mahakama Kuu itakapoyapitia maamuzi yote yaliyotolewa na Mahakama ya Kisutu kuhusu kesi hiyo.

Naye Wakili wa serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameiambia mahakama kuwa wamepokea nakala ya maombi hayo, hivyo wanaomba kuwasilisha majibu yao ya hati kinzani leo June 28, 2018.

Awali wakili Nchimbi alieeleza mahakama kuwa kesi hiyo imeitishwa ili washtakiwa wasomewe maelezo ya awali (Ph).

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri ameiahirisha kesi ya msingi hadi July 2,2018.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.

Katibu wa chama hicho Dk.  Vicenti  Mashinji, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Tarime mjini Esther  Matiko na  mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Katika kesi hiyo namba 112 ya mwaka 2018 Mbowe na wenzake hao wanaokabiliwa na mashtaka 13 ikiwamo ya kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi wa uasi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai.

Makosa hayo  yanadaiwa kutendeka Februari 16,2018 katika maeneo ya viwanja vya buibui, Mwananyamala na  barabara ya Kawawa kinondoni mkwajuni

Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania Bilioni 780

$
0
0
Benki ya Dunia imeidhinisha mkopo nafuu wa Dola 350 milioni (zaidi ya Sh787.5 bilioni) kwa Serikali ili kuboresha miundombinu ya maji safi na salama.

Taarifa ya benki hiyo iliyotolewa jana , Juni 27 inasema mkopo huo utawanufaisha watu milioni tatu kupata maji safi na wengine milioni nne wakiishi kwenye mazingira safi.

“Jana bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Dunia imeidhinisha mkopo huo utakaoinufaisha mikoa 17 kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama vijijini,” inasomeka taarifa hiyo.

Takwimu zinaonyesha watu 11 katika kila 100 hupata maji safi maeneo ya vijijini ambako ni shule moja kati ya kila mbili ina matundu ya vyoo yanayokidhi mahitaji hivyo juhudi za ziada kuhitajika ili kuboresha miundombinu.

Kutokana n ahali hiyo, watoto ndio wahanga wakubwa kwani takwimu zinaonyesha mmoja katika kila watatu hukosa virutubisho muhimu yakiwamo maji ya kutosha.

 Kutokana na mkopo huo, mkurugenzi mkazi wa benki hiyo, Bella Bird anasema kaya 1,250 na shule 1,500 zitanufaika kutokana na jitihada za Serikali kuboresha huduma za umma.

“Ubora wa rasilimaliwatu ni muhimu sana hasa kipindi hiki Tanzania inapojipanga kuelekea uchumi wa kati. Upo uhusiano wa karibu kati ya maji safi na salama na maendeleo ya afya ya mtoto hasa wa kike ambao uhudhuriaji wao shuleni unalegalega nchini,” amesema Bella.

Ratiba Ya Mechi Zote Kombe La Dunia Hadi Fainali

$
0
0
 Fainali za Kombe la Dunia 2018  zilianza rasmini June 14 nchini Urusi .

Tazama  hapa  ratiba ya mechi zote za michuanpo hiyo kuanzia ile ya ufunguzi hadi fainali yenyewe.

Volkswagen Kuanza kutengenezwa Rwanda

$
0
0
Kampuni ya kutengeneza magari ya Volkswagen imezindua na kutangaza kuanza kuunda magari hayo nchini Rwanda huku ikitarajia kuunda magari mpaka 5000 kwa mwaka ambao mengine yatauzwa nje ya Rwanda.

Uwekezaji huo umetajwa kugharimu  dola milioni 20, ambao utengeneza ajira 1,000.

Katika uzinduzi wa tukio hilo ambalo,Rais Paul Kagame, amesema kuwa ni hatua muhimu kwa nchi hiyo.

Amesema kuwa bila shaka kituo kinawakilisha sura mpya katika safari ya mabadiliko ya kiuchumi Rwanda.

"Najua kwa wengine inaweza kuwa vigumu kuamini kuwa magari ya Ujerumani, kama tulivyozoea  kuwaita, yangeundwa kweli nchini Rwanda." Kagame.

Hata hivyo bado umiliki wa magari  nchini Rwanda bado ni mdogo ambapo kati ya watu milioni 12, laki mbili tu ndiyo wanaotumia magari binafsi hao ni wale waliosajiliwa tangu mwaka 1997 kwa mujibu wa mamlaka ya ukusanyaji wa kodi.

Licha ya kiwango cha chini cha umiliki wa magari nchini Rwanda, Volkswagen inatarajia kuuza magari hayo nchi za jirani za jirani huku mengine yakitarajiwa kutumika katika biashara ya usafiri ya kimataifa  kama vile 'Uber'  ambapo itawezesha watu kuagiza safari kupitia simu za kisasa

Hata hivyo  Makampuni ya ushirikiano wa safari ya kimataifa 'Uber'  bado hawajafika Rwanda hivyo Volkswagen itawasaidia kwa kuanzisha huduma yake nchini humo.

Mbali na hayo imeelezwa kuwa magari mengi ya sasa kwenye barabara za nchi hiyo ni yale yaliyoagizwa kutoka nchi kama Japan.

Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Waingilia Kati Sakata la Korosho

$
0
0
Baraza la uongozi la Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) limetoa tamko kuhusu mjadala wa kisheria juu ya tozo ya ushuru wa korosho ghafi zinazouzwa nje ya nchi.

Katika tamko lililotolewa  jana Juni 27,  TLS imesema mwaka 1996 Bodi ya Korosho na Wadhamini wa Mfuko wa Kuendeleza Korosho waliingia makubaliano na Bodi ilikubali kuulipa mfuko asilimia mbili kati ya tatu ya ushuru wa korosho wanazolipa wauzaji wa korosho kwa mujibu wa Kanuni ya 21(1) ya Tangazo la Serikali namba 369 la mwaka 1996.

Baraza hilo limesema mwaka 1999, Bodi ilikuwa imeulipa mfuko Sh1.73 bilioni zilizokusanywa kutoka ushuru huo.

Kutokana na ukaguzi, mfuko uliishitaki Bodi ya Korosho kwa kushindwa kulipa Sh1.8 bilioni. Hukumu ya Rufaa ya shauri la madai namba 18 ya mwaka 2001 kati ya mfuko na bodi, Mahakama ya Rufaa Iliamua kuwa mfuko haukuwa na haki ya kulipwa asilimia mbili ya ushuru huo kwa sababu (a) bodi haikuwa wakala wa mfuko na (b) Kanuni 21(1) ya Gazeti la Serikali (GN) namba 369 haikuelekeza fedha hizo kupewa mfuko.

Sehemu ya 4 ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2010, Bunge lilirekebisha sheria ya korosho na marekebisho hayo yalielekeza kutozwa kwa ushuru wa korosho unaolipwa na wauzaji kwa asilimia 15 ya thamani ya mazao kabla ya kupakiwa kwenye meli au dola za Marekani 160 kwa tani moja ya korosho inayouzwa, au yoyote itakayokuwa kubwa.

TLS inasema Sheria ya Fedha ya Mwaka 2010 iliitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya kodi hiyo na kukabidhi asilimia 65 kwa mfuko wa kuendeleza zao la korosho.

“Kwa hiyo, Sheria ya Fedha ya Mwaka 2010, inaitaka TRA kuwasilisha kwenye mfuko asilimia 65 ya ushuru wote wa korosho kutoka kwa wauzaji kuanzia Julai 21, 2010 mpaka hapo sheria tajwa itakapokuwa imebadilishwa au kufutwa,” inasema TLS katika taarifa iliyosainiwa na Rais wa chama hicho, Fatma Karume.

TLS inasema fedha iliyokusanywa na kutowasilishwa kwa mfuko ni suala la kisheria na kwamba, mfuko unaweza kufungua madai mahakamani kwa hoja hiyo.

TLS inasema shauri namba 18 la mwaka 2001 liliamuliwa kabla ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2010 na haina maana wala uzito wowote kwa mjadala unaoendelea katika jamii na vyombo vyake.

"Uamuzi wa shauri lile ulihusu tu mahusiano kati ya Bodi ya Korosho na Mfuko wa Korosho na tafsiri ya kanuni ya 21 (1) ya Gazeti la Serikali namba 369 ya mwaka 1996," linasema tamko hilo.

TLS inasema shauri la madai namba 18 la mwaka 2001 halikufuta sehemu ya 4 ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2010.

"Katika kuimarisha utawala wa sheria nchini, tunashauri watu wote walio kwenye mjadala huu kuheshimu sheria zilizopitishwa na Bunge mpaka hapo zitakaporekebishwa na Bunge au kufutwa na Mahakama.

Watu 15 Wakamatwa Kwa Makosa ya Wizi wa Mtandao....."Ni Wale wa Ile pesa nitumie kwa namba hii, Nipo kwa Wakala"

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 15 ambao wamekutwa na vitu mbalimbali, zikiwamo laini za simu 352 walizokuwa wakitumia kufanya utapeli kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kutapeli fedha.

Ukamataji huo umekuja baada ya kuibuka wimbi la walaghai ambao hutuma jumbe mbalimbali kwa watu zinazoshawishi kutuma fedha au kufanya malipo ya kifedha kwa njia ya simu pesa.

Kutokana na wimbi hilo la matapeli kuongezeka, mapema mwezi huu Jeshi la Polisi lilitahadharisha wananchi kuzipuuza jumbe hizo na kuwataka waliotapeliwa kupitia 'SMS' hizo kutoa taarifa kituo cha polisi kilicho karibu yao.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Liberatus Sabas, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa watuhumiwa hao 15 wamekamatwa katika operesheni maalum.

Alisema walikutwa na laini za simu 352 za mitandao mbalimbali zenye usajili usio na utambulisho wa watuhumiwa hao.

Pia, Kamanda Sabas alisema, matapeli hao wamekutwa na vitambulisho mbalimbali 31 vikiwa pamoja na leseni, kadi za benki, kompyuta mpakato tano, kompyuta moja na modemu mbili.

“Watu hawa wamekiri kutumia mfumo wa simu inayoitwa 'Bulk SMS' (SMS za mkupuo), ambayo ina uwezo wa kutuma jumbe fupi zaidi ya 10,000 kwa siku na inazalisha namba nyingine za kupokea ujumbe baada ya kuweka namba ya kwanza,” alisema.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa kwa ushirikiano wa mkoa wake, mikoa ya jirani na Rukwa.

Kamanda Sabas alimtaja mmoja wa watuhumiwa hao kuwa ni Lule Lusale (35), mkazi wa Eden Ng’ambo mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Alisema ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakidai kupokea jumbe hizo.

“Katika kipindi cha kuanzia mwezi Aprili 2018 kumekuwa na jumbe fupi za maneno ambazo zimekuwa zikitumwa kwa watu mbalimbali zenye maneno ‘Nitumie hiyo hela katika namba hii... namba ile ya awali ina matatizo; nitumie sasa hivi,” alisema Sabas.

Kamanda Sabas alitaja baadhi ya namba ambazo matapeli hao walikuwa wakizitumia kutuma jumbe hizo za kitapeli kuwa ni 0758713746, 0764581220, 0744105579.

Alisema uchunguzi zaidi unaendelea na pindi utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.

Jeshi la Zimamoto Kuzindua Kampeni Ya Ufungaji Wa Mifumo Ya Kugundua Na Kung’amua Moto Mashuleni

Taarifa Toka Ofisi ya Rais IKULU

Diamond: Mtoto Wa Hamisa ni Mtoto Wangu Kama Walivyo Watoto Wa Zari

$
0
0
Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemwaga povu zito kwa mashabiki waliokuwa wanamnanga mtoto wake  aliyezaa na Hamisa wakidai sio mtoto wake.

Siku ya jana Diamond aliachia trailer mpya ya shoo yake ya ‘The real Life of Wasafi’ itakayoonyesha maisha halisi ya familia ya Diamond itakayorushwa Kwenye Wasafi Tv.

Kwenye trailer hiyo kuna kipande kinachomuonyesha Diamond akiwa anazungumzia watoto wake lakini watoto wanaoonekana ni wawili tu ambao amezaa na Zari huku mtoto wake aliyezaa na Hamisa hakuonekana.

Kuona hivyo mashabiki wa Zari wakaanza kumnanga mtoto wa Hamisa kuwa sio mtoto wa Diamond ndio maana hajaonekana kwenye trailer ya shoo ile na hapendwi kama watoto wa Zari wanavyopendwa.

Baada ya maneno mengi sana Diamond alishindwa kujizuia na kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa Dylan ni mtoto wake kama walivyo watoto aliozaa na Zari walionekana kwenye trailer ile sababu pekee ambayo ilisababisha mpaka Dyalan hakuonekana ni kwa sababu hakuwa na clip yake:

Casto: Ni Maamuzi Ya Tunda Mwenyewe Kuchora Tatoo Ya Jina Langu....Siwezi Mlazimisha

$
0
0
Mtangazaji wa Kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv, Casto Dickson amefunguka na kuweka wazi kuwa kama Tunda ataamua kumchora na yeye Tatoo ya Jina lake mwili mwake ni uamuzi wake binafsi.

Suala hili limekuja siku chache baada ya Casto kuanika hadharani tattoo yake aliyochora Kwenye mkono wake yenye Jina la mpenzi wake Tunda.
 
Kwenye mahojiano na Bongo 5, Casto aliulizwa endapo ni zamu ya mpenzi wake Tunda na yeye kuchora Tatoo ya Jina lake Casto amesema hadi kufikia hatua hiyo kuna jambo la tofauti baina yao na iwapo Tunda atafanya hivyo watu wataona.

"Utamuona akichora, kama akichora utamuona akichora, ana maamuzi yake, yeah!. Kwa sababu kuchora tattoo si pete sisi tumeanza hivi tuna sababu zetu.

"Tuna maana yetu ambayo itakuja kuwa tofauti kabisa, for the first time in Africa tuseme, mtakuja kuona, yeah”.

Wawili hao waliozama Kwenye penzi zito Miezi michache iliyopita wameweka wazi kuwa wana mipango ya kufunga ndoa

Harmonize Afungukia Ushindani Uliopo WCB

$
0
0
Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize amefunguka na kuelezea ugumu uliopo katika kufanya kazi kama msanii wa label ya WCB kutokana na ushindani.

Harmonize amefunguka na kuweka wazi kuwa ushindani ndani ya Label hiyo kati ya wasanii ambao wapo ndani ya Label ndio ugumu ambao upo humo.

Kwenye mahojiano na Planet Fm, Harmonize amesema ugumu uliopo WCB ni kila msanii ana uwezo mkubwa, hivyo kila mmoja anahakikisha anafanya kazi nzuri.

"Ugumu ni pale ambapo unafanya kazi na wasanii wote ambao ni talented, so way competion katika kurekodi ngoma kila mtu anataka kutoa ngoma yake kali kumshinda mwenzake, so ugumu unaanzia hapo“.

WCB ni Label kubwa kabisa Tanzania na inabeba wasanii wanaofanya vizuri sana, wasanii hao kama vile Diamond Platnumz, Rayvanny, Harmonize, Rich Mavoko, Mbosso na wengineo.

Gigy Money Ajutia Kuanika Listi Ya Wanaume Aliotembea Nao

$
0
0
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kuelezea majuto yake kuhusiana na uamuzi wake wa kutaja orodha ya wanaume aliowahi kubanjuka nao.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Gigy Money amekiri anajutia kutaja orodha hiyo ya wanaume kwani mpaka leo kuna wanaume wanaogopa kumtongoza kwa kuogopa kuanikwa.

“Kuwataja wanaume nilipitaga nao najutiaga sana, inafanya kuna muda nikose vitu vya maana kwa kuogopa kuwa nitaropoka. 

"Kumbe ule ni utoto na ni foolish age kila mtu lazima apitie hata uikimbie ni bora uipitie ukubwani usiirudie. Kwahiyo najutia kuwataja wanaume niliowahi kutembea nao ila sijutii kupitia ile hatua,“amesema Gigy Money.

Mwaka jana Gigy Money alitaja wanaume zaidi ya 10 wengi wakiwa mastaa wa muziki wa Bongo Fleva na watangazaji wa Redio na Tv.

DalaDala Kuondolewa Jijini Mwanza Kupisha Mabasi Makubwa

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra) imepanga kuondoa daladala zote zinazosafirisha abiria katika 'ruti' zote za Jiji la Mwanza, mwakani.

Akizungumza jijini hapa, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe, alisema mamlaka hiyo imeanzisha mfumo mpya wa usafiri ambapo wamiliki wa daladala zitoazo huduma sasa jijini hapa wanatakiwa kuungana ili kutoa huduma hiyo kwa kutumia mabasi makubwa ya usafirishaji kupitia ama kampuni au ushirika.

Ngewe alikuwa akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja ya elimu juu ya utoaji wa huduma ya usafirishaji mijini, kwa kuziondoa daladala na kutumia usafiri wa mabasi makubwa.

"Serikali imechukua hatua madhubuti ya kusimamia wamiliki wa daladala kuhakikisha wanaunganisha mitaji yao na kununua mabasi makubwa ya kutoa huduma katika jiji hili la Mwanza kupitia makampuni (kampuni) au ushirika," alisema Ngewe.

"Tunatarajia kufikia mwakani 2019 (mwakani) daladala zote ziwe zimeondolewa katika jiji hili na kuanza kutumia mabasi makubwa yenye kubeba abiria wengi kwa mara moja."

Ngewe alisema kuanzishwa kwa mfumo huo mpya jijini Mwanza kutaondoa changamoto ya msongamano wa magari unaosababishwa kwa kiasi kikubwa na daladala.

Alisema jiji hili lina wamiliki wa daladala zaidi ya 2,000 na idadi ya magari 3,400 yanayotoa huduma hiyo.

Kama mpango huo utatekelezeka, ndani ya miezi sita ijayo Mwanza litakuwa jiji la pili nchini kuondoa huduma ya usafiri wa daladala baada ya Dar es Salaam iliyozipunguza kwa kiasi kikubwa katika Barabara za Morogoro na Kawawa mwaka 2016.

Katika njia hiyo, jiji hilo limeweka mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Ngewe alisema mfumo mpya huo kwa Mwanza utasaidia pia madereva na makondakta wa daladala za sasa kupata mikataba ya kisheria ya ajira zao na kulipwa mishahara na mafao ya uzeeni pindi wanapostaafu kazi.

Ngewe alisema mabasi makubwa yatakayokuwa yakitoa huduma hizo yatatumia mfumo wa kielektroniki katika utoaji wa tiketi kwa abiria.

Aidha, mfumo wa kielektroniki utaondoa wizi wa fedha za makusanyo ya nauli za wenye magari unaofanywa na madereva na makondakta wasio waaminifu, alisema.

Ngewe alisema mfumo wa kuungana mitaji kwa wamiliki kupitia kampuni au ushirika ili kuendesha biashara ni mzuri kwani utawasaidia kupata mikopo ya kifedha kwa urahisi, kukuza mitaji na uchumi kuliko umiliki wa mtu mmoja mmoja.

Mafunzo hayo yalihusisha viongozi wa usalama barabarani, wamiliki wa daladala za abiria mijini, viongozi wa Chama cha Kutetea Abiria (Chakua) na wadau mbalimbali wa usafirishaji kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Credit: Nipashe

UKAWA Kufungua Kesi Mahakamani Sakata la Korosho

$
0
0
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia, amesema endapo serikali haitatoa fedha za mauzo ya korosho, Umoja huo wa Katiba ya Wananchi utakwenda mahakamani kudai haki hiyo.

Mbatia alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari kwenye Viwanja vya Bunge jijini Dodoma jana akiwa na wabunge wa vyama vinavyounda Ukawa.

Umoja huo unaundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), alisema watazitumia siku mbili zilizobaki za Bunge la Bajeti kudai bungeni malipo hayo ya korosho na endapo serikali haitatoa fedha hizo, watalazimika kuisaka haki hiyo nje ya Bunge kwa kufunga kesi mahakamani.

"Korosho ambayo ilikuwa inatuingizia fedha za kigeni ni wazi sasa uchumi wa taifa letu utazidi kudidimia na ukididimia wote tunaumia," Mbatia alisema na kuongeza:

"Sasa tutaendelea kupinga bungeni wakati wa mjadala wa 'Finance Bill' (Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2018), hiyo sheria inayotaka kupokonya haki za wakulima, ikishindikana tutaidai haki hii mahakamani."

Mbatia alisema serikali inapaswa kuwa makini kwa kuwa taifa linapokuwa limepasuka na watu wake kuwa na hofu, haliwezi kuwa na maendeleo.

"Jambo hili la korosho ni kubwa na tusipolisimamia vizuri hatutafika pazuri. Kwenye Finance Bill, serikali ihakikishe wakulima hawa wa korosho wanapata haki zao za msingi," alisema Mbatia huku akieleza kuwa wanaunga mkono hoja ya Mbunge wa Kilwa Kusini, Seleman Bungara 'Bwege' (CUF) kuitisha maandamano kudai fedha hizo.

Naye Mbunge wa Malindi, Ally Saleh (CUF), alisema kitendo cha serikali kutotoa fedha hizo za wakulima ni kuvunja sheria na wawekezaji wataogopa kuja nchini.

“Serikali inapothubutu kuondosha fedha za wakulima ambazo zipo kisheria, tunapeleka ujumbe mbovu kwa wawekezaji. Sasa hivi tunataka kujenga viwanda na kukaribisha wawekezaji, ina maana kwamba hatuheshimu sheria, hivyo wawekezaji wataogopa kuja kuwekeza," alisemana kuongeza:

“Serikali inashindwa kuwekeza kwenye zao ambalo ni 'the best' (bora zaidi) katika nchi kwa sasa na inasema inashawishi watu waje wawekeze viwanda vya kubangua. Je, utamleta nani aje awekeze ikiwa serikali haiaminiki? Nadhani serikali inapaswa kuwa makini sana katika hili."

Naye Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF), alisema hakubaliani na maelezo yaliyowasilishwa bungeni Jumatatu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, kuwa serikali haitolipa fedha hizo kwa sababu za kisheria na kwamba wanayo nakala ya hukumu ya mahakama inayoonyesha serikali ilishindwa katika kesi dhidi ya Bodi ya Korosho na kutakiwa kulipa fedha hizo.

Katika maelezo yake bungeni, Dk. Kilangi alisema fedha hizo ni za umma na kwamba Bodi ya Korosho inakusanya kwa niaba ya serikali na kupanga matumizi.

“Msimamo huo umetokana na uamuzi wa kesi zilizofunguliwa kwenye Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa na haujawahi kupingwa," alisema na kuongeza kuwa:

“Serikali haiwezi kulipa fedha kwenye mfuko ambao haujaanzishwa kwenye sheria ambayo haijatungwa na Bunge. Endapo serikali ikifanya kinyume cha hapo, itakuwa imevunja sheria."

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images