Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yawapa Matumaini Mapya Wenye Virusi Vya UKIMWI

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu amesema Serikali itaanza kutoa dawa mpya za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARVs) itakayokuwa na ufanisi zaidi kuliko inayotumika hivi sasa nchini.

Ummy ameyasema hayo leo Juni 19 2018 katika uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu, Pima, Jitambue, Ishi, inayolenga kuhamasisha watu hasa wanaume kupima VVU kwa hiari na kuanza matumizi ya dawa za kufubaza makali ya ugonjwa Ukimwi (ARVs)

“Tutaanza kutoa dawa mpya za ARVs kwa watu wanaoishi na VVU ambazo zina ufanisi mkubwa na zinapunguza maudhi kwa watumiaji,”amesema.

Ummy pia amesema wameanza majaribio ya kutoa dawa za ARVs kwa miezi mitatu kwa watu ambao mwenendo wao wa matumizi ya dawa hizo unaridhisha badala ya mwezi mmoja.

Amesema mpango huo wa kutoa dawa kwa miezi mitatu hautawahusu wajawazito, watoto na wale ambao mwenendo wao wa utumiaji ARVs hauridhishi.

Ummy amesema pia wamepanga kuongeza vituo vya kutoa huduma kwa watu wanaoishi na VVU ambapo hadi kufikia Desemba mwaka huu vitafikia 4,050 kutoka 1,866 vilivyopo sasa.

Kuhusu upatikanaji dawa za kutibu magonjwa nyemelezi, Ummy amesema kuwa katika bajeti ya mwaka 2018/19 wametenga Sh 5.3 bilioni kwa ajili ya kununua dawa za kutibu magonjwa nyemelezi nchini kati ya Sh 266bilioni zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa nchini

Japani Yapeleka Kilio Colombia Kwa Bao 2-1

$
0
0
Na Magdalena Kasahindye.
Timu ya taifa ya Japan imeibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Colombia.

Katika mchezo huo wa kundi H uliochezwa saa 9:00 mchana Japan ilikuwa ya kwanza kupata goli mapema dakika ya 5 kwa njia ya penati kupitia kwa Shinji Kagawa kufuatia mchezaji wa Colombia Carlos Sanchez kushika mpira ndani ya eneo la 18 katika harakati za kuokoa na alitolewa nje kwa kadi nyekundu na ni kadi nyekundu ya kwanza kutoka kwa mwaka huu tangu kombe la dunia kufunguliwa .

Colombia walisawazisha dakika ya 39 kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Juan Quintero na kuzama nyavuni, dakika 73 Yuya Osako aliiandikia Japan goli la pili na la ushindi.

Mtibwa Yaivua Ubingwa Simba .....Yatinga Fainal Na Stend.

$
0
0
Na, magdalena kashindye
Timu ya Mtibwa sugar ya Morogoro imeingia hatua ya fainali ya michuano ya vijana chini ya miaka 20 kwa kufunga bingwa mtetezi Simba kwa goli 1-0.

Goli pekee la Mtibwa lilifungwa na Abuu Yohana, timu nyingine iliyotinga fainali ni stend ya Shinyanga aliyomtoa Azam kwa goli 1_0 goli lililofungwa na Morice Mahela.

Mtibwa na stend zitacheza juni 21 katika viwanja vya chuo kikuu Dodoma kumtafuta bingwa wa Uhai Cup huku simba wakimenyana na Azam kusaka mshindi wa tatu.

Senegal Yaanza Vizuri Kombe La Dunia, Yaichapa Poland 2-1

$
0
0
Na Magdalena Kashindye
Senegal imekuwa timu ya kwanza toka Afrika  kushinda katika mchezo wake wa kwanza  kombe la dunia dhidi ya Poland kwa goli 2-1

Senegal ilikuwa ya kwanza kupata goli dakika ya 37 ya mchezo kupitia kwa Thiago Cionek na dakika ya 60 Mbaye Niang aliifungia Senegal goli la pili lililodumu hadi dakika ya 86 ambapo poland waliandika goli la kufutia machozi lililofungwa na Grzegorz Krychowiak.

Senegal inakuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kushinda mchezo wake wa ufunguzi baada ya wawakilishi wengine kufungwa katika mchezo yao .Tunisi alifungwa na England 2-1,Nigeria akafungwa na Croatia 2-0,  na Morroco alifungwa na Iran 1-0.

BASATA imefungia wimbo wa Mbunge Sugu

$
0
0
Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa #219 ulioimbwa na Mbunge Joseph Mbilinyi 'Sugu' kwa madai kwamba una maneno ya uchochezi na kuhatarisha amani na utengano miongono kwa jamii.

Taarifa kutoka BASATA inasema kwamba wamekuwa wakipokea simu za malalamikp kadhaa kutoka kwa wadau ambao wamechukizwa na wimbo huo ambao si tu kutokana na umaneno ya kichochezi bali pia kutofuata taratibu za utoaji wa wimbo kwa umma hali inayopelekea kuhoji weledi na hadhi ya msanii.

Katibu Mtendaji wa BASATA, Ngereza amesema kuwa wasanii wengi wanafanya sanaa kuburudisha na kuelimisha lakini hawapo tayari kuvumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza sekta ya sanaa kama kichaka cha kusambaza sumu kwa lengo la kuigawa jamii na kuharibu amani na utulivu.

Mbali na kuufungia wimbo huo, BASATA imemuonya Sugu kuacha mara moja kujihusisha kwa namna yoyote ya kuutangaza au kuusambaza wimbo huo.

Misri Yatandikwa Tena Bao 3-1 na Urusi....Kwa Matokeo Haya, Misri ndo Basi Tena!!

$
0
0
Timu ya taifa ya Misri huenda ikawa timu ya kwanza kuaga Fainali za Kombe la Dunia, baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo pamoja na kuwa kimahesabu inaweza kuwa bado, lakini kiuhalisia ni ngumu.

Misri ambayo ilifungwa bao 1-0 na Uruguay kwenye mechi yake ya kwanza, leo tena imekubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa wenyeji Urusi hivyo kuwa na hali mbaya katika Kundi A.

Msimamo wa Kundi A lenye timu za Urusi, Saudi Arabia, Misri na Uruguay unaongozwa na wenyeji Urusi wenye alama 6 kwenye mechi mbili wakifuatiwa na Uruguay yenye alama 3 kwenye mechi 1.

Saudi Arabia zinavutana na Misri mkiani ambapo Saudi Arabia imepoteza mechi moja dhidi ya Urusi ilipofungwa mabao 5-0 kwenye mechi ya ufunguzi.

Misri ili isonge mbele inahitaji kushinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Saudi Arabia kwa kuanzia mabao angalau 5 kwenda juu huku ikiomba Uruguay ipoteze dhidi ya Saudi Arabia kwa idadi ndogo ya mabao. Kiujumla Misri imeaga michuano.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya June 20

Tamko la Brazil baada ya Neymar kutofanya mazoezi

$
0
0
Shirikisho la soka nchini Brazil CBF limeweka wazi kuwa nyota wa timu Neymar Jr hajafanya mazoezi ya Jumatatu na wenzake kutokana na kuwa na programu maalum na daktari wa timu hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya nyota huyo pamoja na wenzake wawili Paulinho na Thiago Silva, kukosa mazoezi ya Jumatatu na badala yake kukaa na watalaam wa afya kwaajili ya uchunguzi iwapo wamepata amajeraha.

CFB imesema kwa mujibu wa daktari wa timu Rodrigo Lasmar, Neymar na wenzake hawana shida yoyote na ni kawaida kwa wachezaji kuangaliwa hali yao na watalaam wa maabara ili kuepusha kuwaweka kwenye hatari iwapo wana maumivu.

Neymar alifanyiwa faulo mara 10, katika mchezo dhidi ya Switzerland uliopigwa Jumapili na kumalizika kwa sare ya 1-1. Ikumbukwe kuwa Neymar Jr aliumia mguu wa kulia kwenye klabu yake ya PSG mwezi Februari hali iliyopelekea kukosa raundi ya pili.

Brazil itarejea uwanjani tena leo  Jumatano kucheza na Serbia kwenye mechi yake ya pili katika kundi E. Mpaka sasa Serbia wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 3 baada ya kuanza kwa ushindi dhidi ya Costa Rica.

Hukumu ya Wema Sepetu ni July 16

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu  inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Msanii Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili July 16,2018.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya mawakili wa upande wa utetezi kufunga ushahidi wao wa mashahidi watatu akiwemo Wema.

Mbali ya Wema, katika kesi hiyo washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abas.

Hakimu Simba amesema mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu hiyo July 16,2018 baada ya kufungwa kwa ushahidi wa utetezi uliokuwa na mashahidi 3 akiwemo Wema.

Awali kabla ya kupangwa kwa tarehe ya hukumu Wema na wafanyakazi wake walijitetea, ambapo Wema amedai kuwa ni kweli nyumbani kwake kulikutwa msokoto unaodhaniwa kuwa ni bangi na vipisi.

Katika hoja zake, Wema amedai kuwa hajui vitu hivyo ni vya nani kwa sababu yeye ni msanii wa Filamu na nyumbani kwake wanaingia watu tofauti tofauti pia huwa anafanya Party na kualika watu katika nyama choma na chakula cha mchana.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Februari4,2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Tiba Bora ya Nguvu za Kiume, Kisukari, Ngiri, Miguu Kuvimba

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume yanawaathiri watu wengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wengine. Kawaida mwanaume anatakiwa kuwa na uume kuanzia nchi 6- 8, vinginevyo mtu huwa na matatizo. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo. 

Baadhi ni upungufu wa vichocheo hivi; Homoni za getrogen ambazo mwanaume anapobalehe, vichochea hivi huchochea ukuaji wa uume.

Ngiri; Hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na hufanya tumbo kuunguruma na kujaa gesi. Sababu zingine ni korodani moja kuvimba, kupopata choo vizuri.

Sababu hizi na zingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara kwa mara husababisha kukosa tendo ya kurudia tendo na baadae kushindwa kabisa

SILYA: Ni dawa inayozalisha homoni zxa Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka hadi nchi 6-8
 
WET POWER: Ni dawa bora ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba na matunda ambayo huongeza nguvu za kiume kuanzia miaka 15-95 na hukomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi, ina imariisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara mbili bila hamu kuisha na pia itakuchelewesha kufika kileleni

Pia tunatibu kisukari, presha, ngiri, miguu kuvimba na kuwaka moto

Wasiliana na Sheikh Khatib akutatulie matatizo yako. Namba zake; 0785 234 837  au 0656 551 093  au 0746473974

Mwanaume amuua mkewe kwa kumchoma Kisu kisha na yeye mwenyewe kujichoma kisu tumboni na kufariki dunia

$
0
0
Kwamba tarehe 19.06.2018 majira ya saaa 05:00hrs alfajiri katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Angel Guest House iliyopo kijiji cha Kanyara kilichopo kata ya Buliyaheke wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza, mwanamume mmoja aliyefahamika kwa jina la Michael Daud @mwanzamila, miaka 31, mkulima na mkazi wa kijiji cha Bukokwa, anatuhumiwa kumuua mkewe aitwaye Tecla Kamuli @ rutha miaka 30, mkazi wa Bukokwa.

Hii ni baada ya kuzuka ugomvi kati ya wawili hao wakati wakiwa wamelala katika nyumba ya kulala wageni ndipo inasemekana mwanaume aliamka kisha alimchoma mkewe na kitu chenye ncha kali katika sehemu mbalimbali za mwili wake hadi akafariki dunia ndipo baada ya kuona hali hiyo na yeye mwenyewe alijichoma kisu  tumboni na baadae alifariki dunia, kitendo ambacho ni kosa la jinai.

Awali inadaiwa kuwa wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu katika familia yao, hali iliyopelekea mwanamke kuondoka nyumbani kwao kijiji cha Bukokwa kisha kwenda kupumzika kwa wakwe zake kijiji cha Kanyara.

Inasemekana kuwa  tarehe 18.06.2018 mwanaume alimfuata mkewe kijijini kwao Kanyara lakini hakufika nyumbani kwa wazazi wake bali alifikia kwenye nyumba ya kulala wageni kisha alimuita mkewe wakakutania hapo, ndipo majira tajwa hapo juu inadaiwa ulizuka ugomvi kati yao uliopelekea mwanaume kumchoma mkewe na kitu chenye ncha kali kisha baadae na yeye aliamua kujichoma kisu tumboni na baadae wote wawili walifariki dunia.

Inadaiwa kuwa wahudumu wa Geust hiyo walisikia kelele za mtu akiomba msaada ndipo walifuatilia  kelele hizo zinapotokea ndipo baadae waliona tukio hilo kisha walitoa taarifa polisi. 

Askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kukuta marehemu wote wawili wakiwa tayari wamefariki dunia. 

Miili ya marehemu wote wawili tayari imefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza Naibu Kamishina wa Polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi wa jiji na mkoa wa mwanza hususani wanandoa akiwataka kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi wanapokuwa kwenye migogoro ya ndoa kwani ni kosa kisheria, bali ni vyema wawaeleze wazee, viongozi wa dini au vyombo vya dola ili wayasuluhishe matatizo yao kisha waendelea kuishi kwa amani.

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Ufaransa Kuipatia Tanzania Mkopo Nafuu Wa Sh. Trilioni 1.3 Kusaidia Sekta Za Maji, Nishati Na Usafirishaji

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
SERIKALI ya Ufaransa kupitia Shirika lake la  Maendeleo (AFD), itaipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa Euro milioni  500, sawa na takriban Shilingi trilioni 1.3, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maji, Nishati na Usafirishaji, kupitia Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo (2017-2021).

Hayo yamesemwa Jijini Dodoma, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bw. Remy Rioux, ambapo ujumbe wa Tanzania na Ufaransa umejadili namna ya kuendeleza ushirikiano mzuri kati ya nchi hizo mbili uliodumu kwa zaidi ya miaka 58.

"Kupitia makubaliano hayo, AFD itakuwa inatoa Euro milioni 100 kila mwaka, sawa na karibu shilingi bilioni 267 kwa kipindi cha miaka mitano, kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu" Alisema Bw. James.

Bw. James amesema kuwa fedha hizo ni tofauti na  Euro milioni 600 ambazo shirika hilo limeipatia Tanzania kama msaada na mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa hapa nchini ukiwemo Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Ziwa Victoria unaohusisha mikoa ya Mwanza, Bukoba na Musoma ambapo Serikali hiyo ilitoa Euro milioni 45.

Miradi mingine inayofadhiliwa na Shirika hilo ni pamoja na Mradi wa Kuendeleza Sekta ya Maji Awamu ya Pili (WSDP II), Mradi wa Vituo vya kupoza umeme kupitia TANESCO, na Ujenzi wa njia ya Umeme kutoka Geita hadi Nyakanazi na mingine mingi ambayo kwa pamoja  imefikia thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 1.055.

Bw. James ameishukuru Serikali ya Ufaransa kupitia AFD kwa namna inavyoshiriki katika kuleta maendeleo ya nchi na watu wake kupitia ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuiomba iendelee kuangalia maeneo mengine ya vipaumbele vya taifa ikiwemo kilimo, elimu na miundombinu mingine.

Akizungumza katika kikao hicho kilichowashirikisha pia viongozi waandamizi wa pande zote mbili, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bw. Remy Rioux, amesema kuwa Shirika lake litaangalia namna ya kutoa fedha zingine kwa ajili ya miradi mipya ya kipaumbele iliyoainishwa na Katibu Mkuu-Hazina, Bw. Doto James, ukiwemo mradi mkubwa wa Bwawa la Maji wa Farkwa utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha lita za ujazo 37,000 kwa siku kwa ajili ya wakazi wa Jiji la Dodoma, uliopangwa kugharimu Dola la Marekani milioni 420.

"Tuko tayari pia kufadhili ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme jua katika mkoa wa Shinyanga na tutakamilisha majadiliano yetu na Wizara ya Nishati ili kufadhili mradi wa kuunganisha umeme kati ya Tanzania na Zambia pamoja na kushiriki kwa kutoa fedha katika Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza" aliongeza Bw. Rioux.

Alisema pia kuwa Shirika lake liko tayari kuelekeza nguvu zake katika kukuza sekta zingine ikiwemo Sekta ya utalii kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa-TANAPA, Shirika la Simu Tanzania-TTCL, na Taasisi nyingine ambazo serikali itaona zina umuhimu wa kupata rasilimali fedha kutoka AFD kwa ajili ya kusukuma haraka gurudumu la maendeleo ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema kuwa Shirika lake ambalo juzi limesherehekea miaka kumi tangu lianze kufanya shughuli zake hapa nchini, limeamua kuanzisha Ofisi yake ya Kudumu nchini Tanzania badala ya kutegemea Ofisi yake iliyopo Nairobi Kenya, baada ya kuridhika na kutambua jitihada kubwa za Serikali ya Awamu ya Tano za kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi.

"Tumeamua kufanya hivyo ili tuweze kushirikiana kwa karibu zaidi na Serikali katika azma hiyo ya kuifanya Tanzania nchi yenye uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025" alisisitiza Bw. Rioux.

Uhusiano wa Tanzania na Ufaransa ulianza tangu miaka ya 1960 na ukaimarishwa zaidi mwaka 1979, ambapo kwa mara ya kwanza, Serikali ya nchi hiyo iliipatia Tanzania mkopo wa kiasi cha fedha za Ufaransa, faranga milioni 361, kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (Julius Nyerere).

Mwisho

TECNO Spark 2, Angaza Nyakati Za Maisha Yako

$
0
0
 TECNO inafanya vizuri kwenye soko la ‘smartphone’ Tanzania.

 Hii inajidhihirisha kutokana na jinsi simu ya Spark ilivyofanya vyema mwaka jana. Mwaka huu TECNO wamekuja na Spark 2 ambayo imeboreshwa zaidi maalum kabisa kwa ajili yako wewe.

Imekuja na umbo jembamba pia ni nyepesi yenye nchi 6.0 HD+ na wigo mpana wa kioo chenye uwiano wa 18:9 kwa kuweza kuona vizuri zaidi na kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja kwenye skrini yako.

Kamera ya Spark 2 ni ‘megapixel’ 13 nyuma ikisindikizwa na flash tatu zilizokaa pamoja sehemu moja na ‘megapixel’ 8 mbele yenye flash mbili zilizokaa pamoja. Hivi vionjo vyote vinafanya kazi kwa pamoja ikiwa ni kung’aza picha na kupiga picha yenye uhalisia hata katika mwanga hafifu.

Uwezo wa ‘Portrait mode’ umeongezwa kwenye kamera ya mbele ili pale unapopiga selfie yako, sura yako inakua inaonekana vizuri kabisa. Pia kwa mfumo wa mixed flash 2.0, mwanga wa flash ya mbele umeongezwa kwa 40% na ule wa flash ya nyuma kwa 70%.

Spark 2 ina aina mpya ya ‘security’ yenye ulinzi madhubutu ambayo ni ‘face id’. Kupitia ‘face id’ una uwezo wa kufungua simu yako haraka zaidi kwa kuitazamanisha sambamba na paji la uso. Lakini pia ina ‘fingerprint’ yenye kufungua simu yako kupitia alama za vidole.

Pamoja ya kua kifaa hiki kinaendeshwa na Android 8.1 pamoja na processor ya 1.3Ghz quad core yenye kuipa simu kasi ya kufanya kazi kwa haraka zaidi na kupunguza uishaji wa chaji kwa haraka, lakini bado Spark 2 ina betri lenye ujazo wa 3500mAh. Kupitia Spark 2 unapata uhuru wa kusikiliza mziki, kupiga picha na kufanya kazi mbalimbali pasipo kikomo.

Kwa wale wapenzi wa simu nzuri, hakika hiki ni kifaa kwa ajili yako.

Kwa maelezo zaidi tembelea ; http://bbs.tecno-mobile.com

Wabunge Waibua UFISADI Mradi wa Stempu za Kielekroniki

$
0
0
Bunge limeitaka serikali kujiridhisha kuhusu gharama za mfumo wa stempu za kodi za kielektroniki huenda ukamnufaisha zaidi mwekezaji wa kigeni, huku ukiongeza gharama kwa watumiaji wa vinywaji nchini.

Limesema limebaini udhaifu katika makubaliano ya utekelezaji wa mradi huo kwa kuwa linaona gharama zitabebwa na watumiaji wa bidhaa (soda, juisi, maji na bia).

Udhaifu katika makubaliano hayo uliibuliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia, alipowasilisha bungeni jijini Dodoma jana taarifa ya kamati yake kuhusu mapendekezo ya bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha na Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2017.

Vilevile, baadhi ya wabunge waliochangia bungeni jana kuhusu mapendekezo hayo ya serikali, walishauri kupitiwa upya kwa gharama za utekelezaji wa mradi huo, wakidai zimekuwa mara 10 ya nchi nyingine zinazoutumia.

Katika taarifa yake, Ghasia alisema katika mwaka ujao wa fedha, serikali imedhamiria kuanzisha mfumo wa stempu za kodi za kielektroniki ili kudhibiti udanganyifu wa wazalishaji wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa.

Alisema kampuni ya SCIPA kutoka Uswisi ndiyo iliyoshinda zabuni hiyo na ina mkataba wa miaka mitano na serikali kwa mfumo wa 'Self Financing'.

Alisema mfumo huo unamtaka mwekezaji kurudisha gharama zake za uwekezaji kwa kutoza stempu ya kielektroniki kwa kila bidhaa itakayozalishwa na kwamba kiasi cha fedha kinachotarajiwa kuwekezwa na SCIPA ni Dola za Marekeni 21,533,827 (Sh. bilioni 48.473).

"Kamati haina pingamizi na uanzishwaji wa mfumo huu, jambo la msingi ambalo linahitaji lifanyike kwa umakini ni kujiridhisha na gharama za mfumo huo, ambazo zitabebwa na watumiaji wa bidhaa pamoja na mapato atakayoyapata mwekezaji kutokana na stempu," Ghasia alisema.

"Kamati ina maoni kuwa hatua ya serikali kutoongeza ushuru wa bidhaa zisizo za petroli itakuwa haina maana kama gharama ya stempu itabaki kama ilivyopangwa na serikali. Hatua hii itasababisha kuongezeka kwa bei kwenye vinywaji kama maji, soda, bia na juisi ambazo sasa hazitozwi stempu.

"Tathmini ya kamati inaonyesha kuwa pale serikali itakapokuwa inaongeza ushuru wa bidhaa kwa asilimia ya mfumuko wa bei kama Sheria ya Ushuru wa Bidhaa inavyotaka, kiwango cha stempu kitakuwa kinaongezwa juu yake kulingana na mkataba kwa miaka

mitano," alisema.

Ghasia ambaye pia ni Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM), alisema kamati yake imefanya uchambuzi ili kubaini kiwango cha fedha ambacho kampuni ya SCIPA itakipata katika mkataba huo kwa mwaka mmoja.

Alisema uchambuzi wao ulihusisha takwimu za bidhaa tatu za maji, soda na sigara bila spiriti kwa kuangalia viwango vya uzalishaji wa bidhaa hizo kwa mwaka.

Alisema uzalishaji huo unaonyesha kiwango cha maji kinachozalishwa nchini kwa mwaka ni lita za ujazo 268,702,209, soda lita 732,315,008, bia lita 409,274,746 na sigara ni pakti 429,310,400.

"Mheshimiwa Spika, ukikadiria kwamba stempu itatozwa kwa idadi (unit) na si kwa ujazo (lita), hivyo chupa moja ya bia mls 500 itatozwa Sh. 22.73; soda 500 mls itatozwa Sh. 13.5, spiriti mils 1,000 itatozwa Sh. 29.57," alisema.

"Hivyo, ukijumlisha na ushuru wa bidhaa kwa kila bidhaa iliyoainishwa hapo juu, inaonekana kuwa gharama itakwenda kwa mlaji wa mwisho.

"Kwa mantiki hii, ukokotoaji unaonyesha kwa mwaka mmoja SCIPA atakusanya jumla ya Sh. bilioni 66.69 bila ya kuhusisha takwimu za bidhaa ya spiriti. Kiasi hiki ni kikubwa kuliko alichowekeza katika kipindi cha mwaka mmoja tu wa mkataba.

"Kamati imekuwa ikifuatilia hatua mbalimbali za serikali zenye lengo la kukusanya mapato yake yenyewe na sio kutumia mawakala kukusanya mapato.

"Mfano; kuhamisha fedha zake kutoka Benki Binafsi kupeleka Benki Kuu, mfumo wa manunuzi ya Luku kutoka Kampuni ya MaxMalipo na Mitandao ya simu kwenda GePGS (Government Electronic Payment Gateway System), ukusanyaji wa mapato katika mabasi ya mwendo kasi na matumizi ya mashine za EFD.

"Kamati inaona kuwa serikali kuamua kumpa SCIPA mkataba wa miaka mitano wa kuhakiki uzalishaji kupitia stempu za kielektroniki ilhali uhakiki huu ungeweza kufanywa na serikali yenyewe.

"Hata hivyo, kamati imeona kuwa kiwango cha mapato kinachotarajiwa kukusanywa katika kipindi cha mwaka mmoja (Sh. bilioni 66.69) kwa bidhaa nne zilizoainishwa hapo juu ni kikubwa kuliko kiwango cha uwekezaji cha Sh. bilioni 48.473 ambacho kimewekezwa na Kampuni ya SCIPA."

Ghasia alisema baada ya kamati kufanya uchambuzi huo, inaishauri serikali iwekeze yenyewe mfumo huo wenye mtaji wa kiasi cha Sh. bilioni 48.473, ili kiasi cha fedha kitakachopatikana kiwe ni sehemu ya mapato ya serikali badala ya mapato yatokanayo na stempu kuchukuliwa na kampuni binafsi kama ilivyofanya kwenye Mfumo wa TANCIS.

Vilevile, alisema wanaishauri serikali ianze kutumia mfumo huo kwenye vinywaji vikali ambavyo mara kwa mara mbele ya kamati hiyo serikali imekuwa ikithibitisha kuna udanganyifu mkubwa.

"Ni bora serikali kuongeza ushuru wa bidhaa kwa asilimia tano ya mfumuko wa bei kama ilivyokuwa ikifanya hapo awali kuliko inavyopendekeza sasa kutumia mfumo wa stempu kwa bidhaa hizo kwa kuwa gharama za stempu ni kubwa kuliko ushuru wa bidhaa wa asilimia tano," Ghasia alisema na kufafanua zaidi:

"Mathalani ukichukua bidhaa ya soda (Mils 250) inatozwa ushuru wa bidhaa kiasi cha Sh. 15 na wa stempu utatozwa kiasi cha Sh. 13.5. Hivyo, gharama ya jumla (gharama ya ushuru wa bidhaa na wa stempu) itakuwa kiasi cha 28.5 na hivyo itaongeza gharama kwa uzalishaji na kwa mlaji."

Akichangia mjadala huo jana, Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (CCM), alidai kampuni iliyopewa tenda ya mfumo huo ina matatizo makubwa na imeziangusha serikali zingine kutokana na mfumo wake wa rushwa.

“Hili la stempu za kielektroniki ni jambo zuri, lakini tumechelewa," Zungu alisema, "nilitaka kujiridhisha serikali imejiridhisha na huyu aliyepewa kazi hii kwa sababu ukitazama taarifa mbalimbali ina matatizo makubwa, ina kesi Morocco wamefanya ‘price offering’ mara 10 zaidi ya nchi zingine walizofanya kazi hii.

“Kampuni hii inachunguzwa na Bunge la Kenya na imeziangusha serikali zingine kutokana na mfumo wake wa rushwa. Napenda waitwe hawa mabalozi waliopitisha hii kampuni kwamba taarifa zao walizipata wapi.

“Nakumbuka tulifanya semina na TRA (Mamlaka ya Mapato) na walishindwa kuzijibu hoja za wabunge kwa kuwa zilikuwa za msingi na za kizalendo.

“TTCL ni chombo cha umma kwa gharama za mradi huu wa Sh. bilioni 48, binafsi nashauri serikali ibadilishe mpango wake wa kuajiri watu wa nje kusimamia makusanyo ya kodi hapa nchini.

“'Unapo-surrender' kwa kampuni ambayo ina matatizo makubwa duniani, naiomba serikali hii shughuli ifanywe na TTCL ambacho kina uwezo na ni chombo cha umma.

“Mwaka 2008, tulishauri serikali kuhusu wizi wa mtandao wa simu, serikali ikang’oa mtambo, wakatuambia walinunua kumbe hawakununua, walimweka mwekezaji ambaye kaja na mtambo wake kwa gharama kubwa ya Sh. bilioni 50, wakaingia mkataba wa miaka 15, kitu ambacho si sahihi.

“Masuala ya mtandao wa fedha kama ni mali ya 'vendor' utapigwa tu na tumepigwa na tutaendelea kupigwa. Mimi hoja yangu, tulihoji hata gharama za mtambo wenyewe.

Kwenye semina tumeambiwa mkataba wake ni miaka mitano.“Kuna nchi nyingi wameweka hii 'system' (mfumo), kuna kitu kinaitwa 'new generation' hoja kubwa ni makusanyo. Naomba Waziri wa Fedha alitazame hili ili tupunguze gharama za uendeshaji. Chombo hiki kiendeshwe na mamlaka ya umma ya Tanzania."

Hoja hiyo ya Zungu iliungwa mkono na Mbunge wa Mvomero, Sadiq Murad, ambaye alisema makubaliano ya serikali na kampuni hiyo kutekeleza mradi huo yanakwenda kuongeza gharama za bidhaa husika.


Wabunge kupima UKIMWI June 21

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge wa masuala ya Ukimwi, Rwegasira Oscar,  amesema wabunge wanatarajia kupima Ukimwi kwa hiyari Alhamisi Juni 21 shughuli itakayoenda sambamba na mjadala wa wazi juu ya ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari  jana Juni 19, 2018, jijini Dodoma, Oscar amesema mjadala huo utahudhuriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wabunge.

Oscar ambaye ni Mbunge wa Biharamulo Magharibi (CCM) alisema baada ya majadala huo unaoshirikisha taasisi zisizo za kiserikali na asasi za kiraia, zinazoratibiwa na Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU  (Nacopha) kufanyika  Alhamis Juni 21, 2018, kutafanyika shughuli ya upimaji wa VVU/Ukimwi.

“Zitatolewa huduma za upimaji na matibabu ya VVU kwa waheshimiwa wabunge, ambao   watapima kwa hiyari,” alisema Oscar

Alisema kauli mbiu ya mjadala huo itakuwa ni ‘Ushiriki wa viongozi katika kufikia malengo ya 90 tatu.”

Mkapa Ataka Wataalam Wote, Taasisi Zinazohusika Na Umeme wa Jua Kupanua Wigo wa Matumizi Ya Nishati Hiyo

$
0
0
RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa amewataka watalaam wote na taasisi zinazohusika na nishati ya umeme-jua kuangalia namna ya kupanua wigo wa matumizi ya nishati hiyo ya jua ambayo ipo kwa wingi katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwamo Tanzania.

Amefafanua katika kiwango cha Gigawatt 400 za umeme jua zinazotumika duniani kwa sasa bado ni Gigawatt moja tu ndio zimefungwa na kutumika katika nchi za Afrika ,Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa namna mbili.

Mkapa amesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati anazindua Kitabu cha Mafunzo ya Umeme wa Jua ambacho mtunzi na mwandishi wake ni Godwin Msigwa.Kitabu hicho ambacho kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili kitasaidia kusambaza taaluma na maarifa katika eneo la nishati ya umeme wa jua nchini.

Akizungumza kabla ya kuzindua kitabu hicho ambacho ameomba kisambazwe kwa watalaamu wa nishati ya umeme jua na mafundi mitambo wa umeme jua, amesema pamoja na duniani kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme unaotokana na jua bado nchi za Afrika zipo chini kwenye matumizi.

Mkapa amefafanua kwa mujibu wa taarifa za Mtandao wa jarida la kimataifa la nishati Jadidifu linaloitwa REN 21 ya 2018 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2017 jumla ya zaidi ya Gigawatt 400 za umeme jua zimefungwa duniani kote kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme ambayo sote tunaifahamu kuwa ni nishati muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Aidha amesema ongezeko la uzalishaji wa umeme duniani kote linatokana na  uzalishaji kwa kutumia umeme-jua lilifikia Gigawatt 380 katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2017. "Ongezeko hilo ni la kasi sana, jambo ambalo linaashiria kuwa kuna mwelekezo mkubwa duniani wa matumizi ya nishati ya umeme unaozalishwa kwa kutumia nishati ya jua.

"Kutokana na ukweli huu ni faraja kubwa kuona hata sisi Watanzania tuko pamoja na wenzetu wa nchi nyingine katika kukuza matumizi na teknolojia ya umeme-jua kupitia njia mbalimbali ikiwemo mafunzo kwa vijana wetu. 

"Uzinduzi wa kitabu hiki tunaoufanya hapa ni ushahidi tosha wa jitihada zetu kama nchi kuelekea matumizi makubwa ya umeme wa nishati ya jua,"alisema.

Mkapa amlisema pamoja na ongezeko hilo nchi zote za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara .Ukweli huo unakinzana na hali halisi ya eneo hilo kwa maana mbili;kwanza nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ndizo zenye maeneo mengi ambayo hayajafikiwa na umeme.

Pili nchi hizo zipo ukanda wa Tropiki ambao una jua jingi muda wote wa mwaka ambalo linaweza kutumika kuzalisha nishati hiyo ya jua. 

"Nichukue fursa hii kuwataka watalaam wote na taasisi husika zinazoshughulikia masuala ya nishati kuangalia jinsi ya kupanua wigo wa matumizi ya nishati hii ya jua ambayo tunayo kwa wingi katika eneo la Kusini mwa Jagwa la Sahara ikiwemo Tanzania ili kuzalisha umeme wa uhakika na gharama nafuu kwa wananchi wetu.

"Hii itasaidia kuharakisha upatikanaji wa umeme jambo ambalo litaharakisha ukuaji wa uchumi wa viwanda na kuongeza ajira kwa vijana.Wenzetu wa nchi za Ulaya,China ,Marekani ,Japan na India licha ya kuwa na vyanzo vingine na vikubwa vya uzalishaji umeme kama vinu makaa ya mawe na nyukilia bado wanaendeleza uzalishaji umeme kwa kutumia teknolojia ya umeme jua,"alisema.

Mkapa ametoa mfano nchi ya Ujeruman pekee tayari imefunga zaidi ya Gigawatt 400 za umeme-jua zilizounganishwa kwenye mtandao (grid) wao wa umeme , nchi ya China zaidi ya Gigawatt za umeme-jua.Hiyo inaonesha teknolojia ya umeme huo imekuwa , imekomaa na sasa inaweza kutumika bila mashaka yoyote katika kukidhi mahitaji.

Alifafanua kinachohitajika kwa sasa ni kuweka mipango madhubuti na kuitekeleza lakini ili kufanikisha hilo wanahitaji taasisi muhimu za Serikali kama COSTECH kusimamia mipango hiyo kwa kushirikisha wabia wa maendeleo na watalaam mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi.

Alisema ushirikishwaji wa tasnia za mafunzo na uandishi wa vitabu kama alivyofanya mtunzi wa kitabu hicho Godwin Msigwa ni muhimu maana mafunzo na vitabu vya teknolojia hiyo vitasaidia kwa kiwango kikubwa katika kufikia malengo ya nchi.

Aliongeza maendeleo endelevu yanategemea mazingira endelevu;mazingira endelevu yanategemea jinsi wanadamu wanavyotumia mazingira hayo katika shughuli za kawaida na uzalishaji mali ikiwa pamoja na rasilimali za uzalishaji umeme. 

Kinana Awaaga Wabunge wa CCM Kwa Maneno Mazito

$
0
0
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amewaaga wabunge wa chama hicho akiwahusia wanachopaswa kufanya ili kuendelea kujenga imani kwa wananchi.

Kinana amesema hayo Juni 19, 2018 katika halfa iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga na kumkaribisha Katibu Mkuu, Dk Bashiru Ally iliyofanyika katika hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Alisema chama hicho kimekuwa na makatibu wakuu kadhaa na kila mmoja aliondoka kama yeye.

"Nilijitahidi kujitolea, kufanya kazi, kujituma kwa maarifa yangu yote na ninyi ndio mtakaonihukumu kama nilifanya kazi ipasavyo," alisema.

Kinana alisema kama kuna upungufu uliojitokeza anakiri kwamba ni wake binafsi na kama kuna mafanikio hayakuwa na maarifa na juhudi zake bali ni matokeo ya juhudi za wana CCM na wabunge wote.

“CCM si chama cha viongozi ni chama cha wanachama wote, chama chetu bado ni imara na kinakubalika na kuheshimika ndani na nje ya nchi, chama ambacho ni bora kwa muundo wake,” alisema Kinana.

Alisema chama hicho kimekamilisha chaguzi za jumuiya na kazi iliyo mbele ni kuhakikisha inatekeleza mambo matatu.

Ameyataja kuwa ni kutimiza ahadi kwa Watanzania kama zilivyo katika ilani; kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani; na kujiandaa na uchaguzi mkuu ujao.

Kinana alisema, “Serikali ikitimiza ahadi zake kwa wananchi, itaendelea kuaminika na serikali ikipokea matatizo ya wananchi na kutimiza yale wanayoyataka, watafarijika na mtaendelea kuchaguliwa kwa idadi kubwa na mwisho wa siku CCM itapata ridhaa ya kuendelea kuongoza.”

Alisema ili kuendelea kupata ushindi inapaswa kuendeleza sera kwa kuwasikiliza wananchi, kuwa karibu nao na kuchukua hatua kutatua matatizo yanayowakabili, yanayowasumbua na yanayowaudhi ili wasipoteze mapenzi kwa chama chao na viongozi wao.

“Kuna wakati wa kuchukua dhamana na kukubali kuondoka, kuna wakati wa kukubali kazi moja na kwenda kufanya nyingine, kuna wakati wa kufanya kazi na kuna wakati wa kupumzika. Nimeamua kwenda kupumzika,” alisema.

“Nampongeza Bashiru Ally kwa kuteuliwa na ninamtakia kila la kheri katika dhamana hii, sina shaka hata kidogo ndugu Bashiru atapata ushirikiano mkubwa,” alisema.

Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema alichozungumza Kinana ni funzo."Katika uongozi wa kisiasa, hakuna heshima kubwa kama itafika mahali wewe mwenyewe, tena katika wakati uko juu unafanya vizuri kabisa unasema inatosha, hili ni funzo zuri ambalo Komredi Kinana amelifanya na sisi viongozi tujifunze hilo,” alisema.

“Wabunge wengi tunaondoka kinyemela, tunasubiri hadi mageziti yaandike Ndugai chali, sasa hayo yasitufike, tufanye kama ndugu yetu Kinana. Hii ni historia kubwa na utaingia katika vitabu vya kihistoria,” alisema.

Mtazamo Wa Wadau Kuhusiana Na Infinix Hot 6.

$
0
0
Baada ya ujio wa Infinix HOT 6 na kufanya vizuri sokoni kutoka na muonekano na uwezo wake lakini pia wadau wameweza kuongelea upande wake wa pili na kuweza kuyawasilisha kama ifuatavyo. 
 
Infinix HOT 6 ni simu iliyoboreshwa zaidi katika vionjo vya muziki kama vile spika mbili ikiwa na maana imemlenga zaidi mpenzi wa muziki hivyo basi tulitegemea Infinix HOT 6 kuja ikiwa na headphone kama ilivyo kwa TECNO BOOM J8 na si vi earphone.
 
Na kulingana na teknolojia kuendelea kukuwa tulitegemea Infinix HOT 6 yenye kasi ya 4G lakini hapa tumeona kampuni ya simu ya Infinix wameturudisha kwenye mfumo wa 3G tunategemea mabadiliko ya mtandao katika matoleo yanayokuja.
 
Sifa nyengine ambayo ni kijivunia ni uwezo wa kamera simu inakamera nzuri sana ya megapixel 13 nyumba ikiwa na flashi mbili na megapixel 5 mbele ikiwa na flashi. Infinix HOT 6 inakupa uhakika wa picha nzuri wakati wowote ule hata katika mwanga hafifu. Lakini pia muonekano wake unavutia sana ikiwa na wigo mpana wa kioo cha 18:9 kwa nchi 6.0.
 
Katika upande wa Android ipo vizuri sana Infinix HOT 6 imekuja na Android 8.1 yenye kuzuiya uishaji wa chaji katika simu kwa haraka lakini pia imesaidia simu kuwa na ‘application’ mpya kama vile face id lakini pia imeongeza ufanisi katika simu.

Kuhusiana na uwezo wa processor sio kama vile tulivyotegemea tumeona simu nyingi zikija na Qualcomm spandragon kama ilivyo kwa toleo la  awali la Infinix HOT S3 lakini kampuni imeturudisha nyuma na MTK6580 processor ya 1.3 ghz quard core.
 
 Na uhakika wa kudumu na chaji ni mkubwa inabetri ya ujazo wa 4000mAh inaweza kuhimili matumizi ndani ya siku mbili pasipo kuzima.

Dawa Lishe Ya Kuongeza Na Kunenepesha Mwili

$
0
0
Je  umekonda  na  kudhoofu  mwili  wako  kwa  sababu  ya  kuugua  maradhi  mbalimbali  au  kwa  sababu  ya  msongo  wa mawazo  ?

Unataka  kurejesha   mwili  na  afya  yako  katika  hali  yake  ya  awali ?  Kama  jibu  lako  ni  NDIO  basi  HII  NI HABARI  NJEMA  SANA  KWAKO.

Tunayo  DAWA  LISHE  YA  ASILI  ambayo  inasaidia  kurejesha   afya  na  mwili  wa  mtu  alie  dhoofu    kwa sababu  ya kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali  au  kwa  sababu  ya  msongo  wa  mawazo.

Dawa  hii  ya  asili  itarejesha  afya  na  mwili  wako  ndani  ya  muda  wa  siku  thelathini.

Na  kama  wewe  ni   MWEMBAMBA   na  unataka   KUONGEZA  MWILI  na  KUNENEPA  basi  DAWA  LISHE  hii ndio  JAWABU  LAKO.  Dawa  hii  itafanya  mwili  wako  uongezeke  na  kunenepa  ndani  ya  siku  thelathini.

Ni  dawa  ya  asili  kabisa ( pure  herbal ) isiyo  na  kemikali  yoyote  ya  viwandani  na  inapatikana  kwa  gharama  utakayo weza  kuimudu.

Kupata  dawa  hii  fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST  linalo patikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA  jirani na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL   HOUSING.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba    0766  53  83  84    au  0693 00 51 89

Kwa  wateja  wasio  na  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu, tunayo  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  popote  walipo ndani  ya  jiji  la  DAR  ES  SALAAM.

Na kwa  taarifa  zaidi kuhusu  dawa  mbalimbali za  asili  pamoja   na huduma  zetu  kwa ujumla  , tutembelee  kupitia  blogu yetu:

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>