Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Polisi Dodoma imemkamata mtuhumiwa wa mauaji ya mhadhiri UDOM

0
0
Jeshi la polisi mkoani Dodoma linamshikilia mkazi wa Swaswa jijini Dodoma kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma visu mkewe Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Rose Mndenye kwa kisa kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo  lilitokea mnamo Mei 25, 2018 maeneo ya Swaswa mtaa wa Sulungai jijini Dodoma ambapo mtuhumiwa huyo alimchoma kisu mkewe na kumsababishia kifo na yeye kutoroka.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Giles Muruto jana Juni 18 amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo akiwa mafichoni kijiji cha Chiwachiwa kilichopo kata ya Mbingu, Ifakara Mkoani Morogoro.

Aidha Muroto amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Sweden Yapelekea Kilio Korea Kusini kwa Ushindi wa Bao 1-0

0
0
Sweden imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Korea Kusini katika mechi ya Kundi H hatua ya makundi katika Kombe la Dunia.

Sweden ilipata bao lake kwa mkwaju wa penalti baada ya  beki wa Korea Kusini kufanya madhambi eneo la hatari na kumlazimisha mwamuzi kutumia mfumo wa VAR kupata uhakika.

Mlinzi na nahodha wa Sweden Andreas Granqvist ndiye aliyechukua jukumu la kupiga mkwaju huo na kuukwamisha wavuni.

Ubelgiji Yaanza Vizuri Kombe la Dunia kwa Kuitandika Panama 3-0

0
0
Ubelgiji  jana imeshinda kwa mabao 3-0 huku mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku akipiga bao mbili.

Ubelgiji iliitwanga Panama kwa mabao hayo 3-0 katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia hatua ya makund.

Lukaku alifunga bao la pili kwa kichwa akipokea pasi ya Kevin De Bruyne kabla ya kuongeza la tatu katika dakika ya 75 kwa pasi nzuri ya nahodha wake, Eden Hazard.
 
Awali,  Mertens alifunga bao safi katika dakika ya 47, akipiga shuti safi la kutoka pembeni mwaka uwanja na kuifanya Ubelgiji kuongoza mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Uingereza Yawaliza Tena Waafrika.....Ni Baada ya Kuitandika Tunisia Bao 2-1

0
0
Na Magdalena Kashindye
Timu ya taifa ya  Uingereza imeibuka na udhindi wa goli 2-1 dhidi ya Tunisia.

Harry Kane wa Uingereza ndiye aliyepeleka kilio Tunisia kwa kufunga magoli yote mawili goli la kwanza dakika ya 11 na la pili dakika ya 90 kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona.

Goli la Tunisia lilifungwa na Ferjani Sassi kwa penati na ndiyo goli pekee la timu za Afrika kufungwa tangu pazia la kombe la dunia kufunguliwa mwaka huu.

Timu nne za Afrika zimecheza na hamna hata moja iliyoshinda . Senegal atacheza   Leo Juni 19 na Japani.

Aliyesababisha Ofisi Ya Ridhiwani Kuteketea Kwa Moto Akamatwa

0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
JESHI la polisi mkoani Pwani, lina mshikilia Mariam Joakim mwenye miaka (52),kwa kosa la kudaiwa kusababisha kuteketeza kwa moto ofisi ya mbunge wa jimbo la Chalinze ,Bagamoyo Ridhiwani Kikwete .
 
Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna ,alithibitisha juu ya taarifa hiyo .
 
Alisema tukio hilo limetokea June 17 majira ya saa ya 18:00 ambapo jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa raia mwema kwa njia ya simu ,kuwa jengo la ofisi ya mbunge huyo linawaka moto.
 
“Katika tukio hilo ofisi yote imeteketea kwa moto na kuokolewa vitu vichache” alisema kamanda Shanna.
 
Kwa mujibu wa kamanda hiyo chanzo cha moto kimesababishwa na mtuhumiwa Mariam,ambae anaeleza aliwasha moto eneo la nyuma ya jengo hilo kwa lengo la kuchoma majani kisha moto ukamzidi na kushika majani na mabomba yaliyokuwa kando ya jengo hilo.
 
Anasema hatimaye moto uliunguza jengo lote.Thamani ya uharibifu na vitu vilivyoungua haijajulikana na mtuhumiwa yupo mbaroni kwa mahojiano zaidi. 
 
Nae mbunge wa jimbo hilo ,Ridhiwani aliwashukuru wote walioguswa na mtihani alioupata.
 
“Mtihani unapita, asubuhi saa tano june 19 ,mungu akipenda nitakwenda angalia athari ya moto, na kueleza kwa ujumla tukio hili na hasara iliyotokea” alielezea Ridhiwani.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume,maumbile Madogo, Mvuto Wa Mapenzi ,magonjwa Sugu

0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0785687900

Hamisa Mobetto...."Watanzania Wataishije Bila Mimi?"

0
0
Mwanadada Hamisa Mobetto amerudi tena kwenye headlines  June 18,2018 baada ya kuandika caption ambayo imeacha wengi midomo wazi hasahasa mashabiki baada ya  kudai kuwa kila wakati akiwaza kuondoka Tanzania ni lazima awakumbuke Watanzania wenzake maana bila yeye anahisi hawawezi kuishi.

Hamisa Mobetto ameandika; “Sometimes …. Natamani Kuondoka Tanzania nafika hadi airport ila najiuliza Watanzania Wenzangu Wataishije Bila Mimi🤣🤣🏃🏽‍♀️💘”

Hamisa Mobetto amekuwa hakauki kwenye vyombo vya habari hasa mitandaoni hasa pale alipoweka wazi kuwa baba wa mtoto wake wa pili ni Diamond Platnumz.

Si mtu wa kusafiri sana nje ya Tanzania, mara ya mwisho kuweka wazi kuwa yupo nje ya nchi ni pale alipoenda nchini Uganda kwa ajili ya party yake, Gal Power iliyofanyika December 21, 2017.

Mbunge wa CUF aipongeza serikali kwa kukuza uchumi

0
0
Mbunge wa Viti Maalum, Chama cha Wananchi(CUF), Rukia Kassim amepongeza juhudi za Serikali katika kukuza uchumi ikiwemo kuongezeka kwa pato la Taifa.

Mhe. Rukia ameyasema hayo  jana Bungeni, Jijini Dodoma wakati akichangia mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2018/19.

“Naipongeza Serikali kwa hatua za kukuza uchumi hasa ukuaji wa Pato la Taifa unaotarajiwa kuwa asilimia 7.2”, alisema Rukia.

Naye Mbunge wa Urambo,Magreth Sitta ameipongeza Serikali kwa kupendekeza kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye taulo za kike.

“Mheshimiwa Spika hatua hii ya kusamehe kodi hiyo itapunguza bei ya taulo hizo ambayo itawafanya wanafunzi wa kike kuzipata kwa bei nafuu na kuwawezesha kuhudhuria masomo kwa muda wote wa masomo ikilinganishwa walivyokuwa wakishindwa kufanya hivyo wakiwa katika siku zao kwa kukosa taulo”,alisema Mama Sitta.

Akichangia kwenye bajeti kuu ya Serikali, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba alisema kuwa anampongeza saa Rais John Pombe Magufuli kwa kujenga miradi mikubwa miwili ya Standard Gauge naye Umeme wa Stiegler’s Gorge.

“Historia itamwandika Rais Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya hasa kwa ujenzi wa miradi mikubwa nchini, ule wa reli ya Kisasa (Standard Gauge) na ule umeme wa Stiegler’s Gorge”, alisema Serukamba.

Wabunge wanaendelea kuchangia bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 ambayo iliwasilishwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.

Basi la SABCO Lapata Ajali na Kuua Mtu Mmoja

0
0
Mnamo tarehe 18/06/2018 majira ya saa 13:15hrs mchana katika barabara ya Usagara   – Kigongo Ferry maeneo ya Kingongo Ferry kijiji cha kigongo Ferry kata ya Bukumbi  tarafa ya usagara wilaya ya misungwi mkoa wa mwanza, gari no. T.581 ARL  aina ya scania bus kampuni ya SABCO  iliyokuwa inatokea Mwanza kuelekea Msalala wilaya ya Nyan’gwale mkoa wa Geita likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Idd Omary miaka 40, Mnyamwezi, mkazi wa Mkuyuni- Mwanza, liiligonga ofisi ya Ferry na kusababisja kifo kwa Zabroni Malando, miaka 37, Msukuma, mfanyabiashara na mkazi wa Sengerema, aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya bukumbi.

 Aidha pia ajali hiyo ilisababisha majeruhi kwa watu kumi (10), wanaume sita (6) na wanawake wa nne (4), wote wapo katika hospitali ya Bukumbi wakiendelea kupatiwa matibabu.

Aidha kati ya hao majeruhi mahututi wapo watatu ambao ni Idd Omary, miaka 40, dereva wa gari lililopata ajali, Ibula  Raphael, miaka 34, msukuma, mkulima na mkazi wa Busolwa na Sophia Lugihila miaka 45, msukuma, mkulima na mkazi wa msalala na wote wamepelekwa hospitali ya Sekouture iliyoko Mwanza kwa matibabu zaidi.

Chanzo cha ajali ni kuferi kwa breki za gari hali iliyopelekea gari hilo kugonga ofisi za ferry na kusababisha kifo na majeruhi. 

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Bukumbi kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Kamishina msaidizi wa polisi Mkadamu Khamisi Mkadamu anatoa pole kwa wote hususani kwa  ndugu na jamaa wa marehemu wa ajali hiyo, tunawaombea kwa mwenyezi mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. Aidha pia tunawaombea majeruhi wapone haraka ili waweze kuendelea na kazi.

Kilimo Cha Pamba Kunogesha Mapinduzi Ya Viwanda ......Ni Kutokana Na Juhudi Za Serikali Za Kuhamasisha Kilimo Cha Pamba

0
0
 ZAO la pamba ni miongoni mwa mazao makubwa ya biashara yaliyokuwa yakiliingizia Taifa fedha nyingi za kigeni na kuchangia kukuza uchumi wa wananchi miaka ya 1970.

Kwenye miaka ya 1970 kulisheheni vyama vingi vya ushirika wa zao la Pamba na viwanda vya kuchambua nyuzi na kukamua mafuta, ambavyo vilibadili  hali halisi ya kipato cha wananchi wa eneo linalolimwa zao hilo na kulifanya kujulikana kama dhahabu nyeupe.

Kilimo hicho kilianza kudorora miaka ya hivi karibuni kutokana na kulegalega kwa vyama vya ushirika na matokeo yake pamba iliuzwa ikiwa chafu bila kuzingatia ubora  na madaraja yaliyopo.

Kutokana na sababu hizo Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, iliamua kufufua zao hilo ili kuhakikisha upatikanaji wa malighafi ya viwanda vya nguo na mafuta yatokanayo na mbegu za pamba zinapatikana pamoja na kuinua uchumi wa wakulima nchini.

Katika kufanikisha suala hilo Serikali ilianza kwa kuwaagiza viongozi wa mikoa yote inayolima pamba kuhakikisha wanawahamasisha wakulima kufufua mashamba yao na ilihakikisha inafuatilia jambo hilo kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba, ugawaji wa pembejeo hadi utafutaji wa masoko.

Baada ya kutoa agizo hilo ambalo lilifanyiwa kazi na tayari mafanikio yameanza kuonekana katika msimu wa mwaka huu, kwa wakulima  kuanza kuvuna na kuuza kwa mafanikio.

Akizungumzia kuhusu hali ya zao hilo mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella, anasema msimu wa mwaka huu umekuwa na mafanikio makubwa kutokana na hamasa iliyotolewa na viongozi wakuu wa Serikali.

Bw. Mongella anasema kutokana na hamasa hiyo, mwaka huu wanatarajia kupata mavuno makubwa kutoka katika kilimo  hicho kwa sababu wakulima wengi wamelima na baadhi yao tayari wameshaanza kuvuna.

Anasema Rais Dk. Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, walitoa maelekezo mahususi na walifanya ufuatiliaji wa karibu wa kilimo cha mazao makuu matano ya biashara nchini, likiwamo na zao la pamba.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya zao hilo jijini Mwanza hivi karibuni, Bw. Mongella amesema zao la pamba litasaidia kufufua viwanda vya mafuta ya kula, nguo pamoja na kuongeza ajira.

Amesema baada ya Rais Dkt. Magufuli kuhamasisha kilimo cha zao hilo, ambacho kilianza kusuasua nchini, viongozi waliitikia na kuwahimiza wakulima wachangamkie fursa hiyo, ambao walikubali.

“Tunashukuru kwa hamasa na miongozo iliyotolewa na viongozi wetu kwa sababu iliongeza ari kwa wakulima kulima zao la pamba kwa wingi na mwamko kwa wananchi kulima mazao mengine, likiwamo la mpunga,” anasema.

Hata hivyo, kiongozi huyo ameishukuru Serikali kwa kuagiza pamba itakayovunwa iuzwe kupitia minada itakayosimamiwa na Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) katika kila eneo, jambo ambalo limesaidia  kufufuka kwa vyama hivyo.

“Tunashukuru kwa maelekezo na miongozo iliyokuwa inatolewa na viongozi wetu wakuu. Sasa AMCOS zetu zimefufuka na huu ni mwanzo tu mapinduzi makubwa katika biashara ya zao la pamba na yajayo yanafurahisha zaidi,” anasisitiza Bw. Mongella.

Bw. Mongella anatarajia kuwahamasisha wakulima wote wa mkoa huo pamoja na wafugaji na wavuvi wajiunge katika AMCOS zilizoko katika maeneo yao, ili kuweza kuirahisishia Serikali kufanyanao kazi.

Mkuu huyo wa mkoa pia anatumia fursa hiyo kuwapongeza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maofisa Kilimo kuanzia ngazi ya wilaya hadi kijiji na wakulima kwa kuhakikisha kilimo cha zao la pamba kinapata mafanikio.

Bw.Mongella anaamini ushirikiano wao kupitia vikosi kazi mbalimbali vilivyoundwa kuanzia ngazi ya mkoa ambapo alikuwa Mwenyekiti watendaji hao walitoa ushirikiano mkubwa ulichangia mafanikio ya zao hilo.

Hata hivyo, Bw. Mongella amewashauri wakulima watumie taasisi za kifedha kuhifadhi fedha zao na wajijengee nidhamu ya matumizi, ambayo itawapa fursa ya kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo, ikiwa pamoja kujenga nyumba bora.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza, Bw. Juma Sweda anasema anaishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kulifufua zao hilo pamoja na kuwahamasisha wananchi kulima na kutoa maelekezo ya uuzwaji wake.

“Naishukuru Serikali kwani baada ya kuwahamasisha ufufuaji wa kilimo cha zao la pamba nasi tuliungana na wananchi kuhakikisha maelekezo hayo tunayatekeleza kwa vitendo, lengo letu kubwa ni kuona zao hili linarudi kama zamani.

‘’Mbali na kuwahamasisha wananchi kulima zao la pamba, pia Watumishi wa Halmashauri  nao wamelima jumla ya ekari 306 za zao la pamba kwenye kijiji cha Ikoma katika Kata ya Kijima. Mashamba yaliongeza hamasa kwa wananchi,’’ anasema Sweda.

Bw. Sweda anasema kabla ya wakulima kuanza kuanda mashamba ya kilimo cha pamba, Wilaya ya Misungwi yenye vjjiji 113 ilitoa mafunzo kwa wakulima wawili kila kijiji, ambao wameshirikiana na vikosi kazi vya vijiji husika na Maafisa Ugani kusimamia kilimo cha zao hilo.

Anasema kwa sasa wapo katika hatua ya uvunaji na uuzaji, ambapo wamejipanga kukagua kikamilifu ili kuona zoezi hilo linaenda vizuri na pamba yote inayopokelewa na vyama vya ushirika ni ile iliyo katika ubora unaohitajika.

Anasema baada ya Serikali kuhamasisha kilimo cha zao la pamba kwa mikoa yote inayolima zao hilo, pia iliagiza kuanzishwa kwa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) katika maeneo yote, ambapo AMCOS 50 zilianzishwa wilayani Misungwi.

Bw. Sweda anasema AMCOS zimesaidia kuimarisha ubora wa pamba, ambapo viongozi wake hukagua pamba kabla ya kuipokea na iwapo mkulima atabainika kupeleka pamba chafu hulazimika kuisafisha kwanza kwa kutenga safi pembeni kabla ya kupima na kulipwa.

Mkuu huyo wa Wilaya anaongeza kuwa, mbali na kukagua usafi na ubora wa pamba ili kuhakikisha hakuna pamba chafu inayouzwa, pia wanasimamia zoezi la malipo kwa wakulima na kwamba wanaouza wote wanalipwa hapo hapo na ni marufuku mnunuzi kumkopa mkulima.

Pia, anasema wilaya yao imeanzisha mikakati mbalimbali ya kutoa motisha kwa Maafisa Kilimo na wakulima waliofanya vizuri, ambapo hutoa zawadi za pikipiki kwa mkulima na afisa aliyeongoza katika kata yake.

Anaongeza kuwa Maafisa Kilimo Wasaidizi wapo nchini Brazil kwa mafunzo ya miezi mitatu, ambapo wanajifunza namna ya kilimo bora cha zao la pamba. Viongozi hao ambao ni John Choto, Haika Kimambo na Bahati Mchele walichaguliwa kuhudhuria mafunzo hayo baada ya kuonyesha jitihada kubwa katika kusimamia zao hilo.

Mkuu huyo wa wilaya anasema wilaya ina Maafisa Ugani 90 ambao wamesambazwa kuanzia wilayani hadi vijiji, lengo likiwa ni kupata nafasi ya kusimamia vizuri na kwa ukaribu zao la pamba.

Anasema wilaya ina jumla ya kata 27 ambapo Maafisa Kilimo wake wote walipatiwa pikipiki ili ziwawezeshe kuwafikia wakulima kwa urahisi na kuwahudumia kwa wakati lakini atakayeshindwa kuwajibika atanyang’wanywa pikipiki.

Sambamba na hayo, Bw. Sweda aliwashauri wakulima kutumia vizuri fedha wanazozipata baada ya kuuza mazao yao. Anasema ni vema wakatumia fedha hizo kujiletea maendeleo katika familia zao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba bora za kisasa na kuwaendeleza watoto wao kielimu.

Anasema kwa sasa wapo katika hatua ya uvunaji na uuzaji, ambapo wamejipanga kukagua kikamilifu ili kuona zoezi hilo linaenda vizuri na pamba yote inayopokelewa na vyama vya Ushirika ni ile iliyo katika ubora unaohitajika.

Anasema viongozi wa Vyama vya Msingi vya AMCOS, hukagua pamba kabla ya kuipokea na iwapo mkulima atabainika kupeleka pamba chafu hulazimika kuisafisha kwanza kwa kutenga safi na chafu ndipo hupima na kulipwa.

Mkuu huyo wa wilaya anaongeza kuwa zao la pamba mbali ya kuwapatia wakulima kipato, pia litaimarisha hali ya usalama wa chakula kwa sababu fedha watakayoipata baada ya kuuza pamba itawawezesha kumudu ununuzi wa mahitaji mengine katika familia na hawatouza vyakula walivyonavyo.

Hata hivyo, Bw. Sweda aliwaomba wadau wa sekta binafsi wasaidie katika kuliongezea thamani zao hilo kwa kufanya uwekezaji mkubwa wa viwanda vya nyuzi, nguo na vya kukamua mafuta ya pamba badala ya kuuza malighafi.

Kwa upande wake, Afisa Kilimo wa Kata ya Mondo, Bw. Sebastian Mbandi anasema mafanikio ya zao hilo kwa mwaka huu ni makubwa ukilinganisha na miaka iliyopita, hata hivyo wameshindwa kufika lengo walilojiwekea kutokana na mazao mengi kushambuliwa na wadudu aina ya thrips.

Bw. Mbandi anasema walitarajia kuvuna wastani wa tani 1.5 kwa ekari moja lakini kutokana na changamoto ya ugonjwa iliyosababishwa na mdudu huyo wanatarajia kuvuna wastani wa kilo 800 kwa ekari hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia wakulima kwa kuwatafutia dawa itakayowawezesha kupambana na thrips msimu ujao.

Kwa upande wao, wakulima wakizungumza kwa nyakati tofauti, walitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dk. Magufuli kwa kuhamasisha wananchi walime zao la pamba, ambapo nao waliitikia wito huo na sasa wameanza kuona mafanikio.

Miongoni mwa wakulima hao ni pamoja na Bw. Hoja Ngole mkazi wa Kijiji cha Mondo ambaye amelima ekari sita na tayari ameshavuna na ameenda kuuza na anatarajia kutumia fedha atakazozipata kwa kujenga nyumba ya kisasa.

Bw. Ngole na mkewe Bibi Sara waliahidi kuongeza ukubwa wa shamba katika msimu ujao na wamewaomba wananchi wengine kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo kwa kuwa ni mkombozi wa maisha yao.   ’’Tumehamasika kuongeza ukubwa wa shamba baada ya Waziri Mkuu kututembelea na tunataka akija tena akute tumebadilika, tuwe na nyumba bora,’’ anasema.

Mkulima mwingine,mkazi wa kijiji cha Mondo Bw. Michael Masalamunda ambaye alikuwa amepeleka pamba yake katika kituo cha mauzo cha Mwanimo AMCOS amesema anatarajia kutumia fedha atakazozipata baada ya mauzo hayo kwa kuongeza mtaji wa biashara ya ng’ombe.

Bw. Masalamunda naye amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kuwahamasisha walime zao la pamba pamoja na na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye naye aliwahamasisha na kufuatilia maendeleo ya zao hilo.

Mkulima huyo anaishukuru Serikali kwa kuagiza mauzo ya zao hilo yasimamiwe na vyama vya ushirika kwa sababu vimewezesha wakulima kuwa na soko la uhakika la pamba yao na wakiuza tu wanalipwa fedha zao hakuna anayekopwa. “Mimi leo nakuja kuuza kwa awamu ya pili na fedha zote nimelipwa.”

Naye mkulima mwingine, mkazi wa kijiji cha Maganzo Bw. Swalala Nteminyanda anaiomba Serikali kuwatafutia dawa nzuri itakayoweza kuwaangamiza wadudu aina ya thrips ambao wameonyesha usugu baada ya kupuliziwa dawa mbalimbali bila ya kufa.

Nteminyanda pia anawashauri wakulima wenzie wafuate maelekezo yanayotolewa na Maafisa ugani wanaowatembelea katika mashamba yao ili waweze kupata mavuno mengi na yenye viwango vya ubora vinavyotakiwa. Mkulima huyo amelima ekari saba na anatarajia kujenga nyumba bora kwa fedha atakazozipata.

Kwa upande waowanunuzi wa zao hilo wanaishukuru  Serikari kwa kuweka mfumo mzuri wa ununuzi wa zao hilo, ambalo kwa mwaka huu linauzwa kupitia katika minada inayosimamiwa na AMCOS.

Miongoni mwa wanunuzi hao ni pamoja Meneja Mkuu wa Kampuni ya NGS Investment LTD, Bw. Emmanuel Dandu alipokuwa akizungumzia kuhusu kuanza kwa uchambuaji wa pamba kwa msimu wa mwaka huu.

Bw. Dandu ambaye kampuni yao ya NGS Investment LTD, licha ya kujishughulisha na biashara nyingine, pia inamiliki kiwanda cha kuchambua pamba cha Majahida kilichopo wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, ambayo tayari imeshaanza zoezi ya uchambuaji pamba.

Anasema pamba inayochambuliwa katika kiwanda hicho wanainunua kupitia AMCOS walizopangiwa, ambapo alipongeza mfumo huo kwa sababu unawawezesha kupata malighafi kwa urahisi na kwa wakati.

“Wanunuzi wote tunanunua pamba kupitia AMCOS. Serikali imeweka mfumo mzuri unaotuwezesha wote kununua pamba kadiri ya uwezo wetu. AMCOS zimeagizwa kuuza pamba kwa wanunuzi wote bila ya ubaguzi, tofauti na miaka ya nyuma” anasema Bw. Dandu.

Anasema awali kabla pamba haijaanza kuuzwa kupitia AMCOS suala la ubora lilikuwa halizingatiwi sana na wakulima kwani  pamba yake ikikataliwa na kampuni moja alikuwa na uhuru wa kuipeleka kwenye kampuni nyingine jambo ambalo lilichangia kuishusha thamani.

Hata hivyo, wanunuzi hao wanaiomba Serikali kuziwezesha AMCOS kuwa na maghala makubwa na ya kisasa ya kuhifadhia pamba, lengo likiwa ni kuhakikisha pamba inahifadhiwa kwenye maeneo salama na kuifanya isipoteze ubora.

Mbali na maombi hayo, pia wameiomba Serikali kuwajengea uwezo viongozi wa Ushirika ili waweze kutekeleza majuku yao kikamilifu na pia isaidie kutoa elimu kwa wanachama juu ya umuhimu na faida za AMCOS ili wakulima wengi waweze kujiunga.

Akizungumzia kuhusu uwezo wa kiwanda hicho, anasema kina uwezo wa kuchambua tani 40,000 za pamba kwa mwaka, lakini wanalazimika kuchambua wastani wa tani tano  hadi 12 kutokana na changamoto ya upatikanaji wa pamba ya kutosha pamoja na changamoto ya umeme wa uhakika.

Pia anaiomba Serikali iwasaidie wakulima kwa kuwapatia pembejeo kwa wakati pamoja na kuwapa elimu ya mara kwa mara juu ya kulima kwa kufuata kanuni bora za kilimo cha zao la pamba, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa wakati ili waweze kujiongezea tija.

Anasema kwa sasa kiwanda hicho kina jumla ya wafanyakazi 300, ambao kati yao 62 ni waajiriwa wa kudumu na waliosalia ni vibarua.

Bw. Dandu anasema marobota yanayotengenezwa kiwandani hapo yanakuwa na uzito wa kilo 200 hadi 220, huku wateja wao wakubwa ni Cotton Distributors Inc (CDI) ya nchini Uswisi, Saurashtra Cotton and Agro Product PVT LTD ya nchini India.

Wengine ni Awatac Impex PTE LTD ya nchini Singapore pamoja na viwanda vya nguo vya ndani ya nchi kikiwemo cha Mwatex cha jijini Mwanza. Alisema matarajio ya kampuni hiyo ni kuanzisha kiwanda cha kutengeza nyuzi ili kuongezea thamani ya pamba kabla ya kuiuza.

Aidha, Meneja huyo anasema mbegu zinazopatikana baada ya pamba hiyo kuchambuliwa zinapelekwa moja kwa moja katika kiwanda cha kukamua mafuta ya kula na mashudu huuzwa kama chakula cha mifugo na mabaki yanayopatikana baada ya mafuta kuchujwa, anasema yanatumika kwa kutengeneza sabuni za kufulia, ambazo wanaziuza kwa wananchi.

TFF Yaingia mkataba na LaLiga

0
0
Katika jitihada za uongozi wa TFF ulioingia madarakani Agosti, 2017 kuhakikisha unaboresha soka nchini, umepiga hatua nyingine baada ya Rais Karia kutua nchini Hispania na kusaini makubalinao ya ushirikiano na Ligi Kuu ya huko maarufu La Liga.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), pande hizo mbili yaani TFF na La Liga zimesaini makubaliano ya miaka mitatu kushirikiana kwa pamoja kuendeleza soka la Tanzania.

Pande hizo mbili zimesaini makubaliano hayo, jana Juni 18,2018 kwenye makao makuu ya La Liga yaliyopo jijini Madrid nchini Hispania. Hata hivyo haijawekwa wazi pande hizo zitashirikiana kwenye maeneo gani zaidi.

Rais Wallace Karia wa TFF amekutana na Rais Javier Tebas wa La Liga baada ya kutoka nchini Urusi ambapo alihudhuria ufunguzi wa fainali za Kombe la Dunia zilizoanza Alhamisi iliyopita Juni 14.

Daktari ashtakiwa kwa wizi wa viungo vya marehemu

0
0
Daktari mstaafu nchini Kenya Dkt. Moses Njue ameshtakiwa katika Mahakama ya Meru kwa kosa la kuiba viungo vya maiti za binadamu wakati wa utumishi wake.

Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo Claire Murithi ameiambia Mahakama kuwa  Dkt. Njue aliiba moyo wa Polisi wa zamani wa nchi hiyo Benedict Karau huku akimtuhumu pia kupoteza ushahidi wa kesi hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa Mahakamani March 12, 2015 yalieleza kuwa Dkt. Njue ambaye ndiye aliekuwa kiongozi mkuu wa uchunguzi wa maiti katika hospitali ya Consolatha aliiba moyo wa Polisi huyo kabla haujapelekwa katika shule kwa ajili ya wanafunzi kufundishiwa.

Katika kesi hiyo ambayo imeendelea kusikilizwa , Dkt. Njue amekana mashtaka hayo huku mahakama ikimtaka kuweka dhamana ya zaidi ya shilingi milioni 45 za kitanzania.

Hata hivyo Wakili wa Dkt. Njue aliiomba Mahakama kupunguza dhamana hiyo kwa kile alichokidai kuwa mteja wake ni mtumishi wa umma ambapo baadae Mahakama ilimtaka kutoa zaidi ya milioni 11 za kitanzania kama dhamana.

Freeman Mbowe Aruhusiwa Kutoka Muhimbili

0
0
Afya ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili imeimarika na ameruhusiwa kutoka hospitali huku akieleza kuwa kilichokuwa kikimsumbua ni msongo wa mawazo na uchovu kupita kiasi.

Mbowe ambaye ni Munge wa Hai na Kiongozi Mkuu wa CHADEMA ameweka hayo wazi wakati akizungumza na baadhi ya wanahabari waliofika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo Jijini Dar es salaam.

Mbowe amesema afya yake ni nzima hadi sasa, baada ya kumaliza msiba ataendelea kufanya vipimo  maalumu vya kiafya kwa kadiri ambavyo atatakiwa na madaktari wake kama itakuwa ndani au nje ya nchi.

Mbowe pia amewashukuru viongozi wa vyama mbalimbali pamoja na watanzania ambao walimtembelea na hata waliokuwa wakimuombea kwa njia mbalimbali katika kipindi hiki yeye na familia yake ikiwa na wale ambao walizuiwa kumuona kutokana na sheria za kitabibu.

Mmiliki mgahawa wa Bunge Apigwa Faini ya Laki 3 Baada ya Kunaswa na Samaki Haramu

0
0
Wizara  ya Mifugo na Uvuvi, imekamata samaki aina ya sato (wasiofikia kiwango cha kuvuliwa) kiasi cha kilo mbili kati ya 100 waliokuwa wakiuzwa kinyume cha sheria katika mgahawa wa ofisi ya Bunge jijini Dodoma leo JUmanne, Juni 19, 2018.

Kufuatia tukio hilo, mmiliki wa mgahawa huo, Daniel Lamba, amepigwa faini ya Sh. 300,000 baada ya kukiri kosa la kukutwa na samaki hao wachanga.

Kaimu Meneja wa Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu wa wizara hiyo, John Komakoma amesema samaki hao ni ambao hawapaswi kuvuliwa kwa mujibu wa kisheria.

“Hawa samaki tumewakamata kwa kuvuliwa kinyume cha sheria, mmiliki wa mgahawa huu amekiri kosa mwenyewe hivyo tumemtoza TSh. 300,000 ambayo atakwenda kulipia benki,” alisema Komakoma.

John Mpepele ambaye ni Msemaji wa wizara hiyo amesema aliyewapa taarifa za kuwepo samaki hao ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina aliyekuja kwenye mgahawa huo jana asubuhi. “Waziri Mpina alipowaona samaki hawa, aliwatilia shaka na kutuagiza kuja kufuatilia,” alisema.

Aidha, mmiliki wa mgahawa huo, Bwana Daniel Labiaramba akikiri kosa kosa amesema; “Nakiri kosa ni weli, lakini katika kilo 100 nilizouziwa, ni ngumu sana kujua iwapo umewekewa samaki hawa, sikufanya hivi makusudi, kwani sikujua,” alisema.

Mwenyekiti CHADEMA Ashambuliwa kwa Mapanga na Mishale

0
0
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwikatsi wilayani Babati mkoani Manyara, Simon Lala (CHADEMA) ameshambuliwa na watu wasiojulikana waliomjeruhi kwa mishale na mapanga kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga amesema  kuwa shambulio hilo limetokea Juni 18, 2018 katika kitongoji cha Waloa wakati mwenyekiti huyo kwa tiketi ya CHADEMA akiwa kazini pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji.

Kamanda Senga amesema kuwa mwenyekiti huyo ameshambuliwa akitekeleza majukumu yake ambapo alikuwa akisimamia kesi ya ndugu wakigombea ardhi na ndipo upande wa walioshindwa hawakuridhishwa na matokeo ya baraza la kata.

“Tukio lilitokea mida ya saa 5:00 asubuhi wakati mwenyekiti akiwa shambani akimuonesha mipaka ndugu wa watuhumiwa hao waliokimbia baada ya kutekeleza shambulio hilo, ambao walishindwa katika kesi ya kugombea ardhi lakini hawakuridhishwa na matokeo na kudai mwenyekiti kafanya upendeleo”, amesema Kamanda.

Kwa upande wake Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema mwenyekiti huyo atahamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu zaidi baada ya kupewa rufaa katika Hospital ya Mkoa wa Manyara.


StarTimes yazindua Wasafi TV kwenye king’amuzi chake.

0
0
Wapenzi wa burudani kote nchini ni wakati wao kufurahia baada ya Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes kutangaza rasmi kwamba chaneli ya Wasafi TV imeanza kuonekana kupitia king’amuzi chake. 

Uzinduzi wa chaneli ya Wasafi TV kwenye king’amuzi cha StarTimes umefanyika Jumatatu tar 18 katika Hotel ya Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam.

Sasa chaneli hii mpya ya Burudani itaweza kutazamwa na watu wengi zaidi Tanzania kwa sababu StarTimes ndicho king’amuzi chenye watumiaji wengi zaidi hapa nchini kuliko kingine chochote.

“Kuanzia sasa Wasafi TV itapatikana katika ving’amuzi vyetu vya Antenna, kwa hiyo watumiaji wa Antenna wanaweza kutazama chaneli hii mpya ikiwa na vipindi vipya ambavyo vitatangazwa baadaye. 

"Pia wateja wanaweza kulipia kifurushi chochote cha Antenna kuipata Wasafi TV, unaweza kulipia NYOTA kwa 7000 tu mwezi mzima, MAMBO Tsh 13,000 tu kwa mwezi na UHURU kwa 24,000 tu. 

"Wasafi TV kwa sasa inapatikana kwenye Antenna pekee, na muda wowote kuanzia sasa itakuwa tayari kwa watumiaji wa ving’amuzi vya dish pia”, Ndg David Malisa, Meneja Masoko wa StarTimes.

Ratiba Ya Mechi Zote Kombe La Dunia Hadi Fainali

0
0
 Fainali za Kombe la Dunia 2018  zilianza rasmini June 14 nchini Urusi .

Tazama  hapa  ratiba ya mechi zote za michuanpo hiyo kuanzia ile ya ufunguzi hadi fainali yenyewe.

Wabunge Watakiwa kuwasilisha taarifa za mali zao Kabla ya Tarehe 25 Mwezi Huu

0
0
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imewataka wabunge wote kuwasilisha taarifa za mali wanazomiliki kabla ya Juni 25, 2018.

Taarifa ya hiyo ya Sekretarieti imetolewa bungeni leo Juni 19, 2018 na Naibu Spika Dk Tulia Ackson.

Dk Tulia amesema Sekretarieti ilitoa muda kwa wabunge kuwasilisha taarifa za umiliki wa mali zao kwa kuwa wabunge wengi hawakutekeleza agizo hilo.

“Sekretarieti iliwataka kuwasilisha nyaraka kabla ya Juni 25, 2018 zinazohusu fedha zilizoko benki au taasisi zingine za fedha, hisa, majengo, nyumba, madeni, mashine, viwanda, mitambo, magari na aina nyingine za usafiri, madeni na mikopo kwa mali zote zilipo nje,” amesema.

Amesema mwakilishi wa kamishnaa atafika ofisini kwa Katibu wa Bunge kuchukua taarifa.

Mbunge wa Misungwe, (CCM) Charles Kitwanga amesimama akitumia kanuni ya 68(7) kuhusu tangazo hilo akihoji kuhusu wabunge ambao hawajapata barua.

 “Kwa wale ambao tulikuwa hatujapata barua, vithibitisho vyetu viko nyumbani, Juni 25 ni karibu sana na Juni 26 tunatakiwa kuwapo bungeni kupitisha bajeti, haiwezi kutolewa nafasi zaidi ili kupeleka viambatanisho baadaye?”Alihoji

Akitoa majibu ya mwongozo huo, Dk Tulia amesema kuna  makundi mawili; wale wanaotakiwa kuwasilisha vielelezo vya mali zao wafanye hivyo na kwa kundi la pili ni ambao hawakuwa na taarifa.

“Tutaangalia jinsi ya kuwasiliana nao ili kuona vitawasilishwa lini mara baada ya kurudi majimboni kwenu.” Amesema

Waziri Mkuu: Anzisheni Kampeni Za Kuhamasisha Upimaji Wa Vvu

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote nchini washirikiane na wadau wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kuanzisha kampeni ya kuhamasisha wananchi hususani wanaume kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema.

Kadhalika, amewaagiza Wakuu hao wa Mikoa na Wilaya kwa kusaidiana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wasimamie kwa uzito unaostahili kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa muda wa miezi sita mfululizo.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumanne, Juni 19, 2018) wakati akizindua kampeni ya Kitaifa ya kuhamasisha wananchi hususani wanaume kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema, iliyofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri, jijini Dodoma.

“Kwa vile tunazindua kampeni ya kupima na kuanza ARV mara moja (Test and Treat) natoa rai kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, mhakikishe vitendanishi na dawa za ARV zipo za kutosheleza katika kila kituo kinachotoa huduma katika kila Mkoa na Wilaya,” amesema.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watu wote watakaogundulika na maambukizo ya VVU waelewe kuwa utaratibu wa sasa ni kuanza dawa mara moja pasipo kujali kiwango cha kinga mwilini, yaani CD4.

Amesema huo ni utaratibu ambao nchi imeuridhia kwa kuwa una manufaa kwa mtumiaji wa dawa na jamii kwa ujumla. “Mtu yeyote asisite kuanza dawa mara tu anapogundulika kuwa na maambukizo ya VVU bila hata kusubiri CD4 kushuka sana,”.

Katia hatua nyingine, Waziri Mkuu ametaja baadhi ya njia zitakazosaidia kuwafikia wanaume kwa ajili ya kupima VVU na kuanza dawa mara wanapogundulika kuwa na maambukizi kuwa ni pamoja na kupanua wigo wa kuwatumia wanaogundulika na maambukizi ya VVU kuwaleta wenza wao sehemu za kupata huduma.

“Kuimarisha fursa ya wahudumu wa afya kwa magonjwa mengine, kuwashawishi watumiaji wa huduma hizo kupimwa VVU, hususan wanaume na kupanua huduma za upimaji na ushauri nasaha hasa katika Mikoa na Wilaya zenye maambukizo makubwa ya VVU lakini ikiwa na watu wachache wanaojua hali zao za maambukizo,” amesema.

Pia kuainisha na kutumia maeneo ya shughuli za kiuchumi, kijamii, kidini, kimila na starehe yanayowaleta wanaume pamoja ili kuwahamasisha wanaume (wazee na vijana) kuziendea huduma za upimaji wa VVU na magonjwa mengine sugu.

Waziri Mkuu amesema anaamini utaratibu huo utaleta matokeo chanya hasa kwa kuwatumia wanaume ambao ni viongozi na wanaoheshimika katika maeneo husika pamoja na kuziunganisha huduma za upimaji wa VVU katika upimaji na huduma za magonjwa mengine kama magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ili kuimarisha upatikanaji wa huduma katika sehemu mmoja.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wadau wote wa mapambano ya VVU na UKIMWI kwamba Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais chini ya uongozi Dkt. John Magufuli, itaendelea kufanyanao kazi kwa karibu ili kwa pamoja wafikie lengo ya kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu na Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Bw. Suleiman Jafo.

Wengine ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Stella Ikupa, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kuhusu Masuala ya UKIMWI, Bw. Oscar Mukasa.

Makatibu Wakuu wa Wizara, Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Dkt. Leonard Maboko, Wadau wa Maendeleo, Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA), Bw. Justin Mwinuka, Viongozi wa Dini na Asasi za Kiraia, Wakuu wa Mikoa na Wilaya.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Changamoto 6 Kwa Watu Wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI

0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Justine Mwinuka ametaja changamoto sita zinazowakumba watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).

Mwinuka ameyasema hayo leo Juni 19 2018 katika uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu inayolenga kuhamasisha upimaji wa VVU kwa hiari hasa kwa wanaume na kuanza matumizi ya dawa za kufubaza makali ya ugonjwa wa Ukimwi (ARVs).

Mwinuka amesema iwapo changamoto hizo hazitafanyiwa kazi mipango mingi ya kuwasaidia wanaoishi na VVU haitafanikiwa.

Amezitaja changamoto hizo kuwa ni umbali wa vituo vya afya, upatikanaji hafifu wa dawa za kutibu magonjwa nyemelevu na wanaoishi na VVU kutumia muda mwingi katika kupata huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma hasa katika maeneo yenye maambukizi makubwa.

“Changamoto nyingine ni lugha na unyanyapaa katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma, kuchelewa kupata huduma za matibabu. Zisipotatuliwa zitarudisha nyuma lengo kubwa la kampeni hii,”amesema.

Kampeni hiyo imezinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na inashirikisha taasisi za kiserikali, za kimataifa na zisizo za kiserikali.

Wakazi wa Dodoma walijitokeza mapema asubuhi kwa ajili ya kushiriki katika uzinduzi wa kampeni hizo na baadhi walipata nafasi ya kupima VVU kwa hiari ndani ya Viwanja vya Jamhuri.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images