Katika uganga na uchawi miti na mimea imegawanyika katika makundi makuu matatu.
Kundi la kwanza linahusisha miti na mimea inayo kaliwa na majini na malaika watukufu pekee.
Kundi la pili ni miti na mimea inayo kaliwa na majini wa kisheitwani pekee.
Na kundi la tatu ni miti ambayo ina kaliwa na majini wa kisheitwani pamoja na majini watukufu kwa wakati mmoja.
Katika lugha yakitabibu miti na mimea inayo kaliwa na majini wa kisheitwani na majini watukufu kwa pamoja, hujulikana kama miti au mimea mseto.
Hii ni miti ambayo ndani yake wanaishi majini wa kisheitwani na majini watukufu kwa pamoja.
Miti hii ina sifa moja kubwa na ya kipekee nayo ni kutumika katika uganga na uchawi .
Uchawi kwa maana ya ufisadi na uharibifu na uganga kwa maana ya kujenga, kutengeneza pamoja na kupambana na uharibifu unao sababishwa na wachawi.
Miti inayo kaliwa na majini mseto ( Yaani majini wa kisheitwani na majini watukufu ) ipo mingi sana.
Miongoni mwa miti hiyo ni pamoja na mti wa Tumbaku au Mtumbaku.
MAJINI WA KISHEITWANI NA MAJINI WATUKUFU WANAWEZA VIPI KUKAA NDANI YA MTI MMOJA KWA WAKATI MMOJA.
Majini wa kisheitwani na majini watukufu wanaweza kukaa ndani ya mti au mmea mmoja katika namna inayo fanana kwa kiasi kikubwa sana na namna ambavyo matangazo ya vituo mbalimbali vya redio yanavyo weza kupatikana ndani ya redio moja.
Mfano wewe una redio yako aina ya Panasonic. Ukiweka masafa ya 100 utanasa matangazo ya kituo kimoja cha redio, lakini katika redio yako hiyo hiyo ukihamisha masafa na kwenda masafa ya 200 utanasa matangazo ya kituo kingine cha redio. Ukihamisha masafa na kupeleka masafa ya 300, utapata matangazo ya kituo kingine cha redio.
Redio ni moja lakini ndani ya redio hiyo hiyo moja unaweza kupata matangazo ya vituo tofauti vya redio lakini katika masafa tofauti.
Vivyo hivyo kwa majini mseto. Majini hawa wanaishi ndani ya mti au mmea mmoja lakini wanapatikana katika masafa tofauti. Unacho takiwa kufahamu ni kujua jinni yupi anapatikana kwenye masafa yepi.
Kuhusu masafa hapo namaanisha muda , saa na siku wanazo tawala majini hao. Kwa hiyo unatakiwa kuwa makini sana unapoenda kuchuma dawa kwenye mti Fulani kwa ajili ya matumizi yako. Unatakiwa uwe uujue mti huo ndani nje. Unatakiwa kujua mti huo je unakaliwa na majini watukufu pekee au majini wa kisheitwani pekee au majini mseto yaani majini wa kisheitwani na watukufu kwa wakati mmoja.
Kwa bahati nzuri sana taratibu za kuwatumia majini wanao kaa kwenye miti inayokaliwa na majina wa aina moja yaani majini watukufu pekee au majini wa kisheitwani pekee zinajulikana vizuri.
Tatizo linakuja kwenye miti inayo kaliwa na majini mseto. Watu wengi sana hawana ufahamu kuhusu jambo hili . Ndio maana wengi wao huishia kupata matatizo au kupata matokeo tofauti na kile wanacho kitaka.
Kabla ya kwenda kuchuma dawa kwa ajili ya matumizi yako unatakiwa kuujua mti husika juu chini. Unatakiwa kuitambua miti yote inayo kaliwa na majini mseto. Na ukisha ijua unatakiwa ujue masafa ya majini wanao kaa ndani ya miti hiyo.
Katika masafa hapa namaanisha siku, saa na wakati . ( Wakati namaanisha usiku na mchana )
Kwa mfano mti wa tumbaku. Mti huu unakaliwa na majini Zaidi ya thelathini wazuri kwa wabaya.
Majini hawa wameganyika katika makundi makuu mawili, kundi la kwanza ni majini wa kisheitwani na kundi la pili ni majini watukufu. Kundi moja lina utawala mchana na kundi jingine linautawala usiku.
Hivyo basi unatakiwa kuwa makini sana unapoenda kuchuma mmea wa tumbaku kwa ajili ya tiba. Nimesema hivyo kwa sababu najua watu wengi wanaujua mmea wa tumbaku kama mmea unao tumika katika kusafisha na kupandisha nyota lakini ukienda kuuchuma mmea huu katika muda ambao mmea huu unakuwa chini ya utawala wa kisheitwani basi utaambulia kupata nuksi, mabalaa na mikosi.
Unatakiwa ujue saa, siku na wakati ambao mmea wa tumbaku unakuwa chini ya utawala wa majini watukufu, bila kusahau maneno ya kuzungumza unapoenda kuchuma tumbaku kwa ajili ya kusafisha na kupandisha nyota.
Na hii ndio sababu kwanini mmea wa tumbaku ni moja kati ya mimea yenye matumizi mengi sana katika uganga na uchawi yakiwemo mazuri kwa mabaya.
Majini ( wabaya kwa wazuri ) wanaoishi ndani ya mmea wa tumbaku wana tumika kufanya mambo mengi sana mazuri kwa mabaya. Baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo :
1. Kutengeneza na kusababisha maradhi ya kichawi yasiyo weza kutibiwa kwa dawa za hospitalini
2. Kuua nyota ya mtu
3. Kuua biashara ya mtu
4. Kuua nguvu za kiume
5. Kusababisha maradhi ya upofu na uziwi feki ( Upofu na uziwi wa kichawi )
6. Kuua mtu kichawi
7. Kuzika vitu mbalimbali
8. Kumtia mtu nuksi, balaa na mikosi
9. Kumletea mtu uchimvi au uchuro
10. Kuleta uhasama na uadui mkubwa kati ya wanandugu
11. Kusababisha ndugu wa tumbo moja kuchukiana na hata kuuana
12. Kumtia mtu mikosi ya kukamatwa na polisi na kwenda jela mara kwa mara
13. Kulinda mali, mke, familia, uhusiano, ndoa nakadhalika
14. Kulinda pesa na utajiri ( Ulinzi kwa ujumla ) Kwa mfano, mti huu wa tumbaku hutumiwa sana na watu wanao fanya kazi ya ulinzi wa mali za watu
15.Mafanikio katika elimu hususani kwa watu wenye ndoto za kuwa watalaamu katika fani tatu ambazo utazijua ni fani zipi na kivipi mmea wa tumbaku unawasaidia watu wenye ndoto za kuwa wana fani hizo kupitia kitabu changu MAMBO TISA MUHIMU YANAYO UNDA NYOTA YA MWANADAMU : UHUSIANO KATI YA NYOTA YA MTU NA MAFANIKIO YAKE KATIKA MAISHA ambacho kitakuwa mitaani kuanzia kati kati ya mwezi wa Julai
16.Kazi na ajira hususani kwa watu wenye ndoto za kufanya kazi aina tano ambazo utazijua ni zipi ndani ya kitabu changu : MAMBO TISA MUHIMU YANAYO UNDA NYOTA YA MWANADAMU : UHUSIANO KATI YA NYOTA YA MTU NA MAFANIKIO YAKE KATIKA MAISHA ambacho kitakuwa mitaani kuanzia kati kati ya mwezi wa Julai.
17. Humsaidia mtu aliedhulumiwa mali au pesa au anae taka kulipwa fidia
18. Kumtia mtu umasikini
19. Ni dawa nzuri sana ya biashara hususani kwa wanao fanya biashara ya kuuza vikorokocho vya kula wanafunzi mashuleni kama vile visheti, ice cream nakadhalika. Kama unafanya biashara ya kuuza vikorokocho vya kula wanafunzi mashuleni basi nakushauri utumie mvuto wa tumbaku..Inshalaah utapata matokeo mazuri san.
20.Kuleta na kulinda mali, pesa na utajiri
21. Kumloga mtu ukichaa wa kumtembeza
22. Kuleta heshima na kukubalika mbele za watu
23. Kuleta na kuharakisha ndoa
24. Kuleta watoto na furaha katika maisha
25. Pamoja na mambo mengine mengi sana. Kuyajua yote haya kwa kina pamoja na jinsi unavyo weza kutumia mmea wa tumbaku katika mambo yako pamoja na miti mingine muhimu inayo kaliwa na majini mseto pamoja na masharti na taratibu zake, jiandae kusoma kitabu changu MAMBO TISA MUHIMU YANAYO UNDA NYOTA YA MWANADAMU : UHUSIANO KATI YA NYOTA YA MTU NA MAFANIKIO YAKE KATIKA MAISHA ambacho kitakuwa mitaani kuanzia kati kati ya mwezi wa Julai.
Pamoja na mambo mengine mengi, ndani ya kitabu hiki utafahamu kwa kina kuhusu mti wa tumbaku na jinsi ya kuutumia katika mambo yako, majini wanao utawala mmea wa tumbaku na jinsi ya kuwaita na kuwatumia. Utapata kufahamu kuhusu maneno yanayo tumika kutamka wakati unakwenda kuchuma mti wa tumbaku. Na habari njema ni kwamba, maneno hayo yameandikwa kwa maandishi ya kawaida kwa hiyo hata wewe ambae haujui kiarabu unaweza kusoma na kuelewa.
Mbali na mmea wa tumbaku, utapata kufahamu kwa kina kuhusu mimea mingine inayo kaliwa na majini mseto , bila kusahau kuhusu miti na mimea inayo kaliwa na majini wa kisheitwani pamoja na ile inayo kaliwa na majini watukufu pekee.
Kufahamu kuhusu mambo mengine yaliyomo ndani ya kitabu hiki, tembelea :
MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA DOKTA MUNGWA KABILI. ANAPATIKANA KUPITIA NAMBA
0744 000 473.