Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Magufuli afanya uteuzi mpya

$
0
0
Rais wa Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Siza Donald Tumbo kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College).

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi huo umeanza rasmi leo Mei 13.

Kabla ya uteuzi wa leo Prof Tumbo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (Center for Agriculture Mechanization and Rural Technology - CAMARTEC).

Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mussa Iyombe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma.

Tanzania yaanza maandalizi ya kuridhia mkataba wa silaha za Baolojia na sumu

$
0
0
Serikali imesema ipo haja ya kuridhia mkataba wa kupambana na silaha za baolojia na sumu ili kuweza kutoa fursa kwa wataalamu mbalimbali nchini katika kuwajengea uwezo wa kukabiliana na athari za mashambulizi ya silaha za sumu na kibaoloji.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 11, 2018 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussein Mwinyi Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 28 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Jasson Rweikiza aliyetaka kujua ni kwa nini Tanzania haijajiunga na mkataba wa kupambana na silaha za sumu (Biological Weapons Convention).

"Tanzania ilisaini mkataba wa kupambana na silaha za baolojia na sumu tarehe 1 Agosti, 1972 lakini mpaka sasa haijaridhia mkataba huo, kutoridhiwa kwa mkataba huo kulitokana na kutoonekana athari zake za moja kwa moja kwa wakati huo ambapo matumizi salama ya mkataba ikiwemo utafiti wa magonjwa ya binadamu, wanyama na mimea yameendelea kufanyika nje ya mkataba huo. Changamoto zinazotokana na matishio mbalimbali ikiwemo ugaidi, zimesababisha hitaji la kuridhiwa kwa mkataba huo na kutekelezwa kwa vitendo baada ya kutungiwa sheria", amesema Dkt. Mwinyi.

Pamoja na hayo, Dkt. Mwinyi ameendelea kwa kusema

"Serikali inafahamu madhara yaliyopo hivi sasa ya kutoridhiwa kwa mkataba huo ikiwemo Tanzania kuwa katika kundi dogo la nchi ambazo hazijaridhia mkataba huo kama vile Haiti, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Misri, Somalia na Syria ambapo Tanzania kuwepo katika kundi hilo hakutoi taswira nzuri kwa jamii ya Kimataifa kwani kati ya nchi hizo nyingi zina migogoro ya muda mrefu ya ndani....

"Kuwanyima fursa wataalamu wetu kupata mafunzo mbalimbali yanayotolewa katika kujenga uwezo wa kukabiliana na athari za mashambulizi ya silaha za sumu na kibaolojia na pia kunanyima fursa kwa wataalamu na viongozi wa kitanzania kushiriki kwenye uongozi wa taasisi mbalimbali za kimataifa zinazosimamia sheria za silaha za kibaolojia na sumu".

Kwa upande mwingine, Dkt. Mwinyi amesema teyari waraka umeshaandaliwa na muda si mwingi utapelekwa Bungeni kwa ajili ya kuridhiwa ambapo ameahidi mpaka kufikia Septemba 2018 utakuwa umeshawasilishwa.

Fisi Avamia Wapenzi na Kuua Mmoja......Mwingine Kajeruhiwa Vibaya

$
0
0
Mkazi wa wilayani Igunga, mkoani Tabora ameuawa na fisi na mwingine kujeruhiwa baada ya kushambuliwa na mnyama huyo katika Kata ya Ziba, wakati wakirejea nyumbani kutoka kwenye klabu ya pombe.

Azizi Kombe, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ziba, alimtaja aliyeuawa ni Mwajuma Masanja (37), mkazi wa Kijiji cha Iduguta wilayani Nzega na Shija Maneno (35), mkazi wa Kitongoji cha Ipuli Kijiji cha Igumila Kata ya Ziba ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufani Nkinga na hali yake ni mbaya.

Mtendaji huyo alifafanua watu hao walikuwa ni mtu na mpenzi wake ambao walikuwa wakinywa pombe za kienyeji kwenye klabu iliyopo Kata ya Ziba na kuongeza kuwa baada ya kufika saa 3 usiku waliamua kuondoka kurudi nyumbani.

Hata hivyo, Kombe alibainisha wakati wakiwa njiani kurejea nyumbani walishambuliwa na fisi eneo la vichaka ambapo alimng’ata Mwajuma sehemu za makalio na tumboni, hali iliyomlazimu Shija amsaidie huku akipiga kelele za kuomba msaada.

Mtendaji huyo alisema wakati mwanaume huyo akitoa msaada kwa mpenzi wake, ndipo fisi alimng’ata usoni na ndipo aliposhindwa kutoa msaada na fisi huyo aliendelea kumshambulia mwanamke huyo hadi alipopoteza maisha papo hapo.

Kwa mujibu wa mtendaji huyo, muda mfupi wananchi walifika eneo hilo wakiwa na baadhi ya askari wa kituo kidogo cha polisi Ziba kisha kufanikiwa kumuua fisi huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Willibrod Mutafungwa, alithibitisha kuuawa kwa mwanamke huyo kwa kushambuliwa na fisi na kwamba fisi huyo aliuawa.

Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, majeruhi alikimbizwa Hospitali ya Rufani ya Nkinga ambako alilazwa na kutoa wito kwa wananchi mkoani Tabora kuwa makini na wanyama hatari kwa kutotembea usiku kwenye maeneo hatarishi kwa ajili ya usalama wao.

Raia wa Senegal ateuliwa Kuwa Makamu wa Rais Benki ya Dunia

$
0
0
Makhtar Diop, raia wa Senegal ameteuliwa kuwa makamu wa rais wa Benki ya Dunia (WB) atakayekuwa anasimamia miundombinu.

Diop alitangazwa kushika nafasi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita na hivyo kumfanya kuwa miongoni mwa maofisa wa ngazi za juu wa taasisi hiyo muhimu duniani.

Taarifa iliyotolewa na benki hiyo inasema Diop anayaanza majukumu hayo mapya baada ya kuwa Makamu wa Rais anayesimamia Afrika katika miaka sita iliyopita akifanikisha kutolewa kwa mikopo yenye thamani ya Dola 70 bilioni za Marekani.

Ndani ya miaka hiyo sita, Diop alisimamia miundombinu ya usafiri na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), nishati na madini, fedha na ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi (PPP).

‘Katika majukumu yake mapya, Diop atasimamia ufadhili wa miundombinu ya fedha katika ufanikishaji wa maendeleo endelevu hivyo kupunguza tofauti iliyopo kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Uteuzi wa Diop anayetajwa kuwa miongoni mwa Waafrika 100 wenye ushawishi zaidi duniani utaanza Julai Mosi.

Alipokuwa akiisimamia Afrika, inaelezwa alisimamia upatikanaji wa fedha za kufanikisha miradi ya aina tofauti akihamasisha zaidi ubunifu na uvumbuzi wa kisayansi.

Alihakikisha Afrika inapata umeme wa uhakika na nafuu huku ikiunganishwa kwa barabara zinazopitika wakati wote.

Ndani ya benki hiyo, Diop ameshahudumu kama mkurugenzi wa fedha, sekta binafsi na miundombinu Amerika Kusini na Visiwa vya Caribbean.

Kati ya mwaka 2009 na 2012 alikuwa mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia, Brazil ambako alisimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

Alishawahi kuwa Mkurugenzi Mkazi katika nchi za Kenya, Eritrea na Somalia.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, (TMA) Yatoa Tahadhari ya Mvua Kubwa Hadi May 17

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa kwa siku tano kuanzia jana, ambazo zinaweza kuleta mafuriko katika maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Katika taarifa ya TMA iliyotolewa jana Mei 13, mvua hizo zilizoanza kunyesha  zitaendelea mpaka Mei 17 mwaka huu.

TMA imesema athari zinazinaweza kutokea ikiwemo mafuriko ambayo yanaweza kusababisha kuvurugika kwa usafiri, barabara kubwa kutopitika na maisha ya watu kuwa hatarini  kutokana na maji kujaa au kupita kwa kasi.

Pia imetoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zitakazotolewa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 15

Mama Kanumba: Nimeumia Sana Lulu Kutoka Gerezani, Presha Imepanda na Nimekosa Usingizi

$
0
0
Siku mbili tangu alipoachiwa muigizaji Elizabeth Michael ’Lulu’, mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema ameumia na tangu alipopata taarifa hizo hajalala.

Mama Kanumba amesema, tangu alipopata tetesi za msanii huyo ametoka jela, amejikuta anakosa usingizi na kuumwa presha.

Ameongeza na kusema, kutokana na suala hilo, imemlazimu jana Jumatatu kwenda kwenye maombi kwa ajili ya afya yake hiyo.

Amesema, licha ya kuwa si yeye aliyemuhukumu, Lulu alipaswa kukaa hata mwaka mmoja ili roho yake iridhike lakini ndio hivyo: "Siku zote maskini hana haki."

Hata hivyo,  amewashukuru wote waliohusika kumtoa na kuongeza kuwa yote ni kwa sababu yeye hana pesa na anajua watu wataanza kumtusi mitandaoni kwa sababu hiyo lakini yote anamuachia Mungu.

Jeshi la Magereza kupitia Ofisa Habari wake, Lucas Mboje, limesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

Hamisa Mobetto Awajia Juu Watu Wanaombeza Kisa Amezaa na Wanaume Wenye Hela

$
0
0
Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto amewajia juu watu wanaombeza baada ya kusema kuwa yeye sio Single mothers.

Siku ya juzi ilikuwa ni Mother’s Day/ siku ya Mama duniani na Hamisa aliweka wazi kuwa yeye sio Single mother kwa sababu anasaidiwa kulea watoto wake na Baba watoto wake.

Hamisa ana watoto wawili ambapo mtoto wake wa kwanza Fantansy amezaa na Majizzo na mtoto wake wa pili Dylan amezaaa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Lakini baada ya video hiyo kuingia mtandaoni watu walianza kumsema vibaya kutokana na yeye kuongelea suala lake la kuzaa na wanaume wawili tofauti ambao wote ameweka wazi wana uwezo.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Hamisa altoa povu hili:

“Alafu ngoja niwaambie kitu. Mimi ni mbaya kweli nakubali kabisa, alafu pia ni maskini kweli kwenye maisha bado najikongoja kwahiyo hayo sio matusi bali ni hali halisi. Kwahiyo mkikubali hali kama niliyokubali mie labda mtaacha matusi yasio na faida.”

Aliongeza kuwa “Alafu miaka inaenda siku zinakimbia pia…hamuwezi kuwa mna hasira kila siku kisa nimezaa na wanaume wenye hela..hivi nachanganyikiwa au? maana sababu ningine hamna zaidi ya hao wanaume wawili.”

Aliendelea kuandika hivi, “Mnatakiwa mjua kwamba Fancy na Dee Mungu ndo alipanga wazazi wa hawa watoto wawe nani..hasira zenu please msinimalizie mie mtoto wa marehemu Mzee hassan..Its getting boring now.”



Sethi avuliwa ukurugenzi wa IPTL akiwa mahabusu

$
0
0
Huku akikabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, Harbinder Sing Sethi ameondolewa katika orodha ya wakurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL).

Uamuzi wa kumuondoa Seth katika ukurugenzi umefikiwa na bodi ya wakurugenzi ambayo pia imemvua madaraka ya kuwa mwenyekiti mtendaji wa IPTL, baada ya kushindwa kushiriki na kuhudhuria mikutano ya bodi.

Seth anadaiwa kushindwa kuhudhuria vikao vya bodi bila kuruhusiwa na wakurugenzi wenzake kwa miezi sita mfululizo tangu Juni 19, 2017 alipokamatwa na kushitakiwa. 

Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa IPTL, Ambroce Lugenge wakati akitoa muhtasari wa maazimio yao wakati wa mkutano mkuu wa tatu uliofanyika Aprili 10.

Mkutano huo ulikuwa na ajenda kuu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili kampuni hiyo na uendeshaji wa mambo yanayohusu IPTL.

Sethi anakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola22.198 milioni za Marekani na Sh309.5 bilioni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu. 

“Bodi ilijadili kuhusu kesi namba 27 ya 2017 ya uhujumu uchumi inayomkabili ndugu Harbinder Sing Sethi na athari yake kwa kampuni, muundo wa kiutendaji wa kampuni ikiwemo na uongozi, udhibiti na ushushaji wa gharama pamoja na uwepo wa kesi mbalimbali mahakamani dhidi ya kampuni au ya kufunguliwa na kampuni,” alisema Lugenge.

Taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana ilisema bodi ilimtunuku Sethi ukurugenzi wa heshima kwa msingi kuwa “aliongoza” kampuni hiyo kutoka katika hatari ya kufilisiwa kutokana na kesi iliyokuwa imefunguliwa na kampuni ya VIP Engineering and Marketing kati ya mwaka 2002 hadi 2013.

Kutokana na uamuzi huo, Sethi hataruhusiwa kwa namna yoyote ile kushughulikia masuala yanayohusu kampuni hiyo au kuingia makubaliano yoyote kwa niaba ya kampuni. 

“Bodi imeelekeza uongozi mpya, hasa menejimenti kuwafikia wadau ikiwa ni pamoja na Serikali ili kuangalia namna bora ya kutatua madai yote dhidi ya kampuni, ikiwemo hasara inayodaiwa kusababishwa na ndugu Sethi kwa mamlaka husika, iliyopelekea kukamatwa na kushtakiwa kwake ibebwe na kampuni na kuyatafutia ufumbuzi kwa masilahi ya umma,” alisema Lugenge katika taarifa hiyo.

Pia, alisema bodi imeagiza menejimenti mpya kukaa na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) ili kubaini kodi stahiki na kuweka mazingira bora ya kuzilipa haraka iwezekanavyo baada ya kubaini kiasi kisicho na pingamizi. 

Lugenge katika taarifa hiyo alisema bodi hiyo imemteua Joseph Makandege kuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ili kuongoza uboreshaji kiutendaji, uteuzi ulioanzia Aprili 10.

Alisema katika mkutano, bodi ilijadili na kufikia maazimio katika vipengele vingine 10 vya ajenda, ambavyo vilikuwa vinachangia kwa kiasi kikubwa kuamua mwelekeo na hatima ya kampuni hiyo.

Alikiba Apokea Tuzo ya Nyota wa Michezo.

$
0
0
Ikiwa ni siku tano zimepita tangu Alikiba aachie ngoma yake mpya ‘Mvumo wa Radi’ amepokea tuzo ya heshima ya Plaque inayoitwa Nyota wa Mchezo kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM.

Msanii huyo amepewa tuzo hiyo jana Jumatatu  kutokana na mchango wake kwenye muziki na jitihadi alizipiga kupeperusha bendera ya Tanzania na kuwa inspire wasanii wengine wachanga na kuendelea kuwepo mpaka leo kwenye muziki.

Kiba amekuwa msanii wa tatu kupewa tuzo hiyo baada ya Vanessa Mdee aliyekabidhiwa mwezi January mwaka huu na Diamond aliyepewa mwezi wa tatu.

Kwa sasa video ya ngoma yake mpya ya Mvumo wa Radi ina views milioni 1.1 kwenye mtandao wa YouTube.

Kama Dalili Hizi Unazo Upo Kwenye Hatari Ya Kuishiwa Nguvu Za Kiume Kabisa

$
0
0
Una dalili zifuatazo?
1: Kushindwa kurudia tendo la ndoa
2: Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa
3: Maumivu ya kiuno mgongo
4: Tumbo kuunguruma na kujaa gesi
5: Uume kusinyaa, kuingia ndani na kuwa mdogo au mfupi
6: Korodani moja kuvimba

KAMA DALILI HIZI UNAZO UPO KWENYE HATARI YA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME KABISA

Kwa matibabu tumia OZYMIX POWER-dawa bora ya nguvu za kiume ya miti shamba ambayo haina kemikali ambayo itakuwezesha kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha.
Pia tunatoa huduma hizi:>

1.Dawa ya Kuondoa michirizi
2.Kumrudisha mwanaume aliyekuacha 
 
Tunapatikana KAWE UKWAMANI karibu na kituo cha mabasi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI ; 0716096205 /0756726865 FIKA OFISIN AU PIGA SIMU NA UTALETEWA DAWA POPOTE ULIPO DAR ES SAALAM NA KWA MIKOANI TUNATUMA KWA NJIA YA MABASI.

TEMBELEA KATIKA BLOG YETU HAPA>>>;

Tiba Bora ya Nguvu za Kiume, Kisukari, Ngiri, Miguu Kuvimba

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume yanawaathiri watu wengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wengine. Kawaida mwanaume anatakiwa kuwa na uume kuanzia nchi 6- 8, vinginevyo mtu huwa na matatizo. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo. 

Baadhi ni upungufu wa vichocheo hivi; Homoni za getrogen ambazo mwanaume anapobalehe, vichochea hivi huchochea ukuaji wa uume.

Ngiri; Hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na hufanya tumbo kuunguruma na kujaa gesi. Sababu zingine ni korodani moja kuvimba, kupopata choo vizuri.

Sababu hizi na zingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara kwa mara husababisha kukosa tendo ya kurudia tendo na baadae kushindwa kabisa

SILYA: Ni dawa inayozalisha homoni zxa Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka hadi nchi 6-8
 
WET POWER: Ni dawa bora ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba na matunda ambayo huongeza nguvu za kiume kuanzia miaka 15-95 na hukomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi, ina imariisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara mbili bila hamu kuisha na pia itakuchelewesha kufika kileleni

Pia tunatibu kisukari, presha, ngiri, miguu kuvimba na kuwaka moto

Wasiliana na Sheikh Khatib akutatulie matatizo yako. Namba zake; 0785 234 837  au 0656 551 093  au 0746473974

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume,maumbile Madogo, Mvuto Wa Mapenzi ,magonjwa Sugu

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO 0758840958 / 0785687900

Wema Augua Ghafla Mahakamani

$
0
0
JANA Mrembo Wema Sepetu ameshindwa kujitetea katika kesi yake ya kutumia dawa za kulevya baada ya kuugua ghafla akiwa mahakamani hapo.

Wakili wa Serikali, Costanine Kalula alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo limeitishwa ili Wema na wenzake waanze kujitetea, lakini Wema anaumwa, hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Baada ya kueleza hayo, Mama mzazi wa  Wema Sepetu, Miriam Sepetu aliieleza mahakama kuwa Wema alifika mahakamani hapo lakini wakati anasubiri  kuingia mahakamani alianza kuumwa ambapo alianza kutapika na hivyo kuondoka.

Baada ya maelezo hayo , Hakimu, Thomas Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi May 29 na 30, 2018  washtakiwa watakapoanza kujitetea.

Mbali na Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kuzitumia.

Inadaiwa February 4, 2017 katika makazi ya Wema eneo la Kunduchi Ununio, washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa February mosi 2017 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.

Mwandishi wa Habari asimulia alivyotekwa na wafanyakazi wa Ofisi ya RC Arusha

$
0
0
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha, limesema kuwa linaendelea na uchunguzi kuhusiana na kuwepo kwa tukio la utekaji  wa mwandishi wa mitandao ya Kijamii, lililofanywa na watumishi wawili wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha na kisha kushtakiwa kuwa alifumaniwa na mke wa mtu.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, amesema hayo ofisini kwake leo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuelezea kuwepo kwa tukio hilo .

Akisimulia tukio hilo Lucas Myovela, amesema  alipigiwa simu na Amina Msuya au Ravness anayefanya kazi ofisi RC Arusha upande wa kutunza kumbukumbu, akimuomba wakutane ili amuelezee tatizo kati yake na rafiki yake wa kiume aitwae Swalehe Mwindadi, ambae nae ni mtumishi ofisi ya mkuu wa mkoa, masijala ingawa kwa sasa anasaidia ofisi ya Itifaki.

Anasema  Amina au Ravness, alimsimulia mkasa na kumwambia kuwa hawana maelewano na mwenzake hivyo anaomba suala hilo liandikwe kwenye vyombo vya habari kwa kuwa limeshafikishwa kwa Katibu tawala wa mkoa kwa utatuzi lakini hadi leo hajafanikiwa.

Siku ya Jumamosi, May 12 Amina alimpigia simu Lucas na kumtaka wakutane ndipo Lucas aliposema alikuwa hospital ya rufaa ya KCMC akishughulikia suala la baba yake mzazi kuhamishwa hospital kutoka hospital ya Seriani ya jijini Arusha kwa ajili ya matibabu  na hivyo alimwambia hataweza kufika.

Amesema kuwa ilipofika saa 3 usiku  Amina aliendelea kumpigia simu ya kumsihi waonane ndipo alipomkubalia na kumweleza kuwa yupo wilayani Arumeru na aliambiwa achukue usafiri wa pikipiki hadi Ngurero, jijini Arusha na alipofika eneo aliloagiziwa alimkuta mwenyeji wake akimsubiri akiwa amesimama nje ya gari na mwenyeji wake alimwambia asubiri kidogo amalize kuzungumza na simu.

Amesema muda mfupi alimuona Swalehe na vijana wengine wawili ambao mmoja wapo alivalia Maski usoni na walipofika Swalehe alimshika mikono na kumfunga kwa kamba na kisha wakasaidiana kumuingiza ndani ya gari.

Amesema wakati amefungwa akiwa ndani ya gari alianza kushambuliwa kwa kipigo kutoka kwa Swalehe ambae alisaidiana na vijana wawili huku Amina akiendesha gari na kuelekea Sakina darajani  na kisha kumshusha upande wa pili wa Daraja huku wakiendelea kumshambulia  na damu ilipoaanza kutoka walimvua nguo na kumwagia maji ya baridi yaliyokuwepo darajani hapo huku wakimpiga picha za utupu na kumlazimisha awape shilingi 500 000/.

Amesema walichukua kadi ya ATM na walitumia Sime na Bastola ndogo kumlazimisha  kuwapatia namba za siri na hivyo mmoja alienda kuchua fedha zilizokuwemo kwenye Account yake.

Amesema wakati hayo yakiendelea Swalehe alikuwa akiwasiliana na polisi aliyepo kituo kidogo cha polisi cha Ngarenaro na walipofika walikuta kituo kimefungwa hivyo alipelekwa kituo kikuu cha polisi jijini Arusha, ambapo walitoa maelezo kuwa wamemkamata mwizi akijaribu kufungua milango ya gari lao kwa lengo la kuwaibia madai ambayo aliyapinga na kueleza tukio zima.

Lucas, anasema  wakati alisimulia tukio hilo polisi Swalehe alitoka nje na kuingia ndani ya gari huku akianza mchakato wa picha za utupu za  tukio hilo walizozipiga wakiwa Darajani Sakina ndipo polisi walipomfuata na kuchukua simu hiyo kabla hajafanikiwa kufuta picha hizo

Faiza: Nampenda Sugu Ila Sio Kimapenzi

$
0
0
Muigizaji Faiza Ally ambaye ni mzazi mwenzie na Mbuge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, amedai kuwa bado anampenda Sugu ila hana hisia naye za kimapenzi kutokana na kile kilichotokea kati yao.

Hata hivyo Faiza amesema licha ya yote yaliyotokea kati yao mapenzi yake ya kweli kwa Sugu hayajawahi kuisha.

“Hisia na mapenzi ni tofauti, kwa sababu nampenda mapenzi ya kweli hayajawahi kufutika, i will always love him na kumpenda haina maana kuwa nina hisia naye. Nampenda ni ndugu yangu, baba watoto wangu,” Alifunguka Faiza Jumapili Katika Mahojiano Bongo5

Faiza na Sugu wamejaliwa mtoto kupata mtoto mmoja, Sasha.

Sheria yawabana wanandoa Kenya, Hakuna kugawana 50/50 Mkiachana

$
0
0
Nchini Kenya kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya ugavi wa mali pindi wanafamilia wanapopeana talaka, jambo kubwa likiwa ni iwapo wanandoa wanatakiwa kugawana mali nusu kwa nusu wanapoachana kwa talaka au la?.

Jaji wa mahakama kuu nchini humo John Mativo amepinga wanandoa kugawana mali nusu kwa nusu wanapo achana kwa talaka uamuzi ambao wengi wameuchukulia kama pigo kwa haki za wanawake.

Uamuzi huo umetokana na sheria ya ndoa nchini humo ambayo hata hivyo imekuwa ikipingwa na shirikisho la mawakili wanawake Kenya FIDA wakidai kuwa sheria hiyo inawanyanyasa wanawake.

Ombi la FIDA limekataliwa na mahakama kwa madai kuwa kuruhusu kugawana mali nusu kwa nusu kutatoa mwanya kwa watu kuingia katika ndoa kwa lengo la kujinufaisha.

Mahakama imesema sheria haiwanyanyasi wanawake kwasababu umauzi huu pia utakuwa na manufaa na kuwalinda wale wanaofanya kazi kwa bidii katika familia.

Sadaka Yangu Ya Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani Kwa Watu Wanao Sumbuliwa Na Maradhi Ya Kisukari.

$
0
0
Asalaam  Aleykum ndugu  zanguni.  Ni  matumaini  yangu kuwa  mnaendelea  vyema  na  maandalizi  ya  mwezi  mtukufu  wa  Ramadhani.

Kama ilivyo  ada  kila ufikapo  Mwezi  Mtukufu  wa  Ramadhani  huwa  ninatumia  karama  niliyo  jaaliwa  na  Mwenyezi  Mungu  kuwasaidia  watu wenye  kusumbuliwa na  magonjwa  mbalimbali.

Mwenyezi  Mungu  amenijaalia  karama  ya  uponyaji  kwa  njia  ya  mitishamba  na  tiba  za  asili  kwa  ujumla.

Na  katika  tiba  ambazo  Mwenyezi  Mungu  amenijaalia  kuzifahamu  ni  pamoja  na  tiba  hii  ya  asili  ambayo  inasaidia  kuondosha  kabisa maradhi  ya  kisukari.

Kupitia  karama  hii  ya  uponyaji, Katika  wiki  ya  kwanza  ya  Mwezi  huu  Mtukufu  wa Ramadhani, nitatoa  sadaka  yangu  kwa  watu kumi  na  wawili  wanao  sumbuliwa  na  maradhi  ya  kisukari kwa  kuwatibia  bure  kabisa  bila  kupata  malipo yoyote  yale kutoka  kwao.

Kati  yao,  watu  sita  watakuwa  wanawake  na  watu  sita  watakuwa  wanaume. 

Kwa  wewe unae hitaji  kuwa  miongoni mwa watu  hawa  kumi  na  wawili.  Unatakiwa  kwanza  uwe  na  maradhi  ya  kisukari lakini  pili uwe  hauna  uwezo wa kifedha kugharamia matibabu yako   kwa sababu  sadaka  yangu  hii ninaitoa kwa  wagonjwa  wasio  na  uwezo.   Watu  hawa  kumi  na  wawili  nitawapatia  tiba  hii  bure  kabisa  bila  malipo  yoyote  kama  sehemu  ya  sadaka  yangu kwa  Mwenyezi  Mungu katika  mwezi  Mtukufu  wa  Ramadhani

Kuhusu  tiba  hii, hii  ni  tiba  ya  asili inayo  ondosha  na  kuponyesha   maradhi  ya  kisukari. Tiba  hii  ya  asili  ni  sahihi  kabisa  na  mujarabu  na  inshaalah  watu  hawa  kumi  na  wawili watapata  kupona  maradhi  hayo  ya  Kisukari  kwa  idhini  yake  Mwenyezi  Mungu.

Kwa  wewe  mwenye  maradhi  ya kisukari  ambae  umehangaika  kutumia  tiba  mbalimbali  bila mafanikio yoyote  na  hauna  uwezo  wa  kifedha basi  wasiliana  nami  Dokta. MUNGWA  KABILI  kwa  simu  namba : 0744  000  473 .  Wasiliana  nami  mapema  kwani  sadaka  yangu  hii  nitaitoa  kwa  watu  kumi  na  wawili  tu.

NINAKUTAKIENI  MAANDALIZI MEMA  YA MWEZI  MTUKUFU  WA  RAMADHANI.

Serikali Yaunda Baraza kuchunguza askari wa Tanzania aliyepotea Congo

$
0
0
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi ameziagiza familia za askari waliouawa wakilinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kumaliza haraka taratibu za mirathi.

Pia, amesema Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo amekwisha kuunda Baraza la Uchunguzi, kuchunguza kupotea kwa askari mmoja aliyekuwa akilinda amani DRC.

Waziri Mwinyi ameyasema hayo jana Mei 14 wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya wizara yake ya mwaka 2018/19 ya Sh1.9 trilioni.

Waziri Mwinyi alisema tayari baadhi ya familia za askari hao zimeshakamilisha taratibu za mirathi.

Alisema fedha za mirathi zimetolewa kwa baadhi ya familia lakini zipo baadhi hazijakamilisha taratibu.

 “Familia ambazo hazijakamilisha taratibu za mirathi zikamilishe haraka,” alisema.

Kuhusu askari mmoja aliyepotea siku hiyo ya mapigano Waziri Mwinyi alisema: “Umoja wa Mataifa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, wanaendelea kumtafuta na ikitimia miezi sita kwa Serikali ya Tanzania tutaitisha uchunguzi na Mkuu wa Majeshi ameitisha baraza la uchungizi,” alisema.

Alisema baada ya hapo Mkuu wa Majeshi atatoa taarifa ya kifo. “Lakini huyu kijana amepotea na mpaka sasa anatafutwa, hatuwezi kusema amepotea au yuko hai.” Alisema

Marekani yafungua rasmi ubalozi wake Jerusalem

$
0
0
Marekani imeufungua rasmi ubalozi wake Jerusalem huku Wapalestina zaidi ya 40 wakiuawa na wengine wakijeruhiwa kwenye mapambano na askari wa Israel katika harakati za kuipinga hatua hiyo.

Hatua ya Marekani ya kuuhamishia rasmi ubalozi wake kwenye mji  wa Jerusalem kutoka Tel Aviv imetekelezwa baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Aidha, balozi wa Marekani nchini Israel, David Friedman amesema kuwa baada ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa taifa la Israel wakati muhimu kama huu ni wa kihistoria kwa sababu ya ujasiri wa mtu mmoja tu ambaye ni rais wa Marekani Donald Trump ameweza kuitambua Jerusalem.

Hata hivyo, Trump amesema kuwa Marekani itaendelea kujitolea kikamilifu katika kuuwezesha mpango wa amani wa Mashariki ya Kati.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images