Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mke wa Kafulila apata ajali ya gari

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Jesca Kishoa amelazwa hospitali ya Bunge jijini Dodoma baada ya kupata ajali ya gari leo asubuhi Mei 11, 2018 wakati akienda bungeni.

“Hapa nimelazwa hospitali ya Bunge, nasikia maumivu katika mguu wa kulia lakini naendelea vizuri.

“Nimechomwa sindano ya kutuliza maumivu na ninaendelea vyema,” amesema Kishoa mke wa mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, David kafulila

Kuhusu mazingira ya ajali, Kishoa amesema;  “katika mataa ya pale Area D, taa zilivyoruhusu, yule wa mbele yangu hakuwa ameonyesha kama atakata kona, sasa alivyokata kwa ghafla, mimi kufunga breki kwa nguvu ikafeli, nikaigonga kwa nyuma.

Mkurugenzi CDA Afikishwa Mahakamani Kwa Matumizi Mabaya ya Madaraka

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dodoma, jana ilimpandisha kizimbani aliyekuwa Mkurugenzi wa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Paschal Muragili kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka.

Muragili alikuwa Mkurugenzi wa CDA hadi Mei mwaka jana ambapo Rais John Magufuli aliamua kuivunja mamlaka hiyo na shughuli zake kurudishwa Manispaa ambayo kwa  sasa ni Jiji.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengu amesema Muragili anatuhumiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya mamlaka, kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa  cha mwaka 2007.

Mbali na mkurugenzi huyo wa zamani,Takukuru imempeleka pia aliyekuwa fundi sanifu Lemanya Benjamini ambao kwa pamoja walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Emanuel Fovo   wa mahakama ya Hakimu Mkazi.

Akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha mashtaka wa Takukuru  Biswalo Biswalo ameieleza mahakama kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Septemba, 2016.

Hakimu Fovo alitoa dhamana kwa washtakiwa wote baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni pamoja na kila mtu kuweka fedha taslimu Sh 23 milioni au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Nyingine ni kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika pamoja na kuwasilisha hati zao za kusafiria na kuwa washtakiwa hao hawaruhusiwi kusafiri nje ya nchi bila kibali cha Mahakama. Kesi itaskilizwa tena Juni 4 mwaka huu.

Jacqueline Wolper akubali yaishe kwa Harmonize

$
0
0
Malkia wa filamu, Jacqueline Wolper ameamua kunyamaza na kusitisha malumbano yaliyoanza kwenye mitandao kati yake na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Harmonize.

Malumbano hao yasiokuwa ya kawaida yameanza Jumanne hii baada ya Harmonize kupost list ya wanaume aliodai wamewahi kutembea na mpenzi wake huyo wazamani, Jacqueline Wolper.

Hatua hiyo ilimfanya Wolper kuibuka na kuanza kuandika mambo mbalimbali mabaya akimtuhumu muimbaji huyo wa wimbo, DM Chick, huku akidai ndiye aliyesababisha alumbane na Sarah.

Alhamisi hii Wolper aameamua kuwa mpole kwa kufunga malumbano hayo baada ya Harmonize kudai ataandaa list C ya wanaume aliotembea na mrembo huyo kutoka katika kiwanda cha filamu.

“Mungu nifundishe kunyamaza, we ndio unaujua ukweli 🙏#Najifunzakuheshimkilangaziiliyonifikishanilipo  #NdiomaanataupambanesiwezkushukaatanishushaMungupekee #jifunzekuheshimkilangaziiliyokufishaulipokamweutoteterekakwajarbulolote  #MunguwanguwaushindiwewenijbuToshaNimekukabidhiwewekilaktu🙌🙏,”

Baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii wanadai Harmonize anamchokoza Wolper ili apate kiki za project yake mpya.

Muimbaji huyo siku ya leo ameachia kolabo yake ya wimbo ‘Pull Up’ akiwa ameshirikiana na Eddy Kenzo

Mambosasa: Mange Kimambi Ni Mwenzetu Sasa Hivi,amerudi Kundini Na Anatupongeza

$
0
0
Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ametoa wito kwa vijana kuacha ushabiki bila kuchunguza madhara yake.

Kamanda Mambosasa ameyasema hayo mapema leo wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam ambapo amesema mnamo Aprili 26, 2018 Jeshi la Polisi liliwakamata vijana ambao walikuwa kwenye maandalizi ya maandamano ambayo yalihamasishwa kwa njia ya mtandao na mwanadada Mange Kimambi lakini baada ya muda mfupi alianza kuipongeza serikali.

"Nawasihi vijana mnaotumia mitandao ya kijamii mnaposhabikia vitu angalieni madhara, yani faida na hasara zake kwani mnamo Aprili 26 tuliwakamata vijana waliokuwa wakijiandaa kwa maandamano ambapo mhamasishaji Mange Kimambi baadae akaanza kuipongeza Serikali. Mange ameendelea kuipongeza serikali nasi tunampongeza kwa kuwa amerudi kundini", amesema Mambosasa na kuongeza;

"Mange alikuwa anapotosha ila watanzania walipompuuza sasa ametambua ni afadhali naye arudi kuipongeza serikali. Watu tuliowakamata kwa ajili ya kufanya maandamano tuliwahoji na kisha kuwapa dhamana".

Sanjari na hayo Mambosasa amesema kuwa hali ya usalama Jijini Dar es Salaam imezidi kuimarika siku hadi siku

Serikali yatoa kanusha Taarifa za UONGO Kuhusu Bodi ya Mikopo

$
0
0
Serikali ya kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefunguka na kukanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa wanafunzi ambao wazazi wao wana leseni za biashara hawataruhusiwa kupata mkopo wa elimu kuwa sio za kweli na kuutaka uuma kuzipuuza taarifa hizo.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 11, 2018 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. William Ole-Nasha wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kufuatia taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na hoja za baadhi ya Wabunge walizotoa bungeni kuwa leseni ya biashara inatumika kama kigezo cha kutowapa wanafunzi mikopo hiyo.

"Hizo habari ni za uongo zenye lengo la kupotosha jamii, kimsingi tuna taka umma wa watanzania wazipuuzie hizo taarifa kwasababu sio za kweli. Mikopo inatolewa kwa kuzingatiwa uwezo wa mzazi au mlezi wa mwanafunzi, kwa hiyo kinachoangaliwa ni kipato chake", amesema Ole-Nasha.

Pamoja na hayo, Naibu Waziri Ole-Nasha ameendelea kwa kusema "vigezo vinavyotumika vinabadilika kila mwaka kulingana na maboresho yanayofanywa ili kuendana na wakati ambapo kwa mwaka huu mabadiliko hayo yamesaidia kuongeza wanufaika wa mikopo elfu 10,000 zaidi kulinganisha na mwaka jana.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri iza, Mh. William Ole-Nasha amesema mwaka huu matarajio ni kutoa mkopo kwa wanafunzi laki moja na elfu ishirini na mbili (122,000) na kati yao elfu 30 ni wa mwaka wa kwanza na elfu 80 ni wanafunzi wanaoendelea na masomo yao.

Serikali yafuta leseni zote za kuhodhi maeneo ya madini na kuwataka wamiliki kuomba upya wakizingatia Sheria na Kanuni mpya za Madini

$
0
0
Serikali imefuta leseni zote za kuhodhi maeneo ya madini na wamiliki wake wametakiwa kuomba upya wakizingatia Sheria ya Madini na kanuni zake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Mei 11, 2018 Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini, Profesa Idris Kikula amesema tangazo la Serikali namba moja la mwaka 2018 limesema maeneo yote yaliyopewa leseni yanarejeshwa serikalini bila hakikisho la kupewa tena.

Amesema uamuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ikisomwa na marekebisho yake ya mwaka 2017 na kanuni ya 21 ya kanuni za Madini (Haki Madini za mwaka huu).

Amesema leseni zilizofutwa na wamiliki wake wanatakiwa kuomba tena zinazihusu kampuni 11, kwamba leseni hizo zinajumuisha migodi ya kati na mikubwa.

Migodi hiyo ni pamoja na Kabanga Nickel Company Limited, National Mineral Development Corporation Limited, Bafex Tanzania Limited ambayo inamiliki leseni za maeneo matatu.

Nyingine ni Mabangu Mining Limited, Resolute (Tanzania) Limited, Wigu Hill Mining Company Limited, Nachingwea Nickel Limited na Precious Metals Refinery Company Limited.

Profesa Jay amtabiria Sugu kuwa Rais wa Tanzania

$
0
0
Mbunge wa Mikumi (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa J’ amempongeza mbunge mwenzake wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kwa kuhitimisha mafunzo ya kisiasa na kusema sasa Sugu, anasubiri kuwa Rais wa Tanzania.

Profesa J ametoa utabiri huo leo Mei 11, 2018 bungeni kabla ya kuanza kuchangia kwa bajeti ya wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji ya 2018/19, ameanza kwa kusema;

“Natoa pongezi kubwa sana kwa pacha wangu aka Sugu kwa kuhitimu mafunzo huko ndani ambayo yameongeza ujasiri na CV yake ya kisiasa na natumaini sasa hivi hatakuwa rais wa Mbeya bali anakwenda katika mchakato wa kuwa Rais wa Tanzania huko mbeleni.”

Pongezi kama hizo, zimetolewa pia na mbunge wa viti maalum (Chadema), Devotha Minja ambaye amesema kilichompata Sugu ni harakati za ukombozi wa taifa hili.

Profesa J akichangia bajeti hiyo ya viwanda amesema mkoa wa Morogoro ulikuwa na viwanda vingi lakini vingi vimeshindwa kujiendesha na kushauri uchunguzi ufanyike, ili kuona wapi tumejikwaa.

Kauli ya Alikiba kuhusu kesi ya matunzo ya mtoto wake

$
0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Alikiba amezungumzia sakata la mzazi mwenzie Hadija Hassan kufungua kesi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto, akidai matunzo ya mtoto wao.

Akizungumza katika kipindi cha 360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds, Alikiba amesema kesi hiyo imefunguliwa kwa nia ya kumkomoa.
 
“Simuelewi kwa nini amefungua kesi kwa sababu kama ni mtoto namtunza. Ila ugomvi unakuja pale familia yetu inapotaka kumchukua mtoto. Inapotaka kukaa naye japo kwa siku chache, hataki,” amesema.

“Jambo hilo kwa kweli linatutia wasiwasi sana, tunajiuliza kwanini anafanya hivyo.”

Amesema mpaka sasa hajapata barua ya wito huo mahakamani na kuahidi kuendelea kumtunza mtoto huyo ambaye katika siku za karibuni alimuhamishia ‘shule za bei mbaya’.
 
Kuhusu idadi ya watoto wake, Alikiba amesema anao watatu; wawili wa kike na mmoja wa kiume.

Mke wa Ali Kiba Azungumzia Kiba Kuoa Mke wa Pili

$
0
0
 Amina Khalef mke wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba amesema suala la mumewe kuoa mke wa pili anamuachia Mungu.
 
Akizungumza leo Ijumaa Mei 11, 2018 katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa Redio Clouds, Amina ambaye alionekana kuwa mzito kutoa majibu mpaka alipobanwa na watangazaji waliokuwa wakimhoji, amesema suala hilo anamuachia Mungu.

Kwa upande wake Ali Kiba alipotakiwa kuzungumzia jambo hilo amesema ataoa kama mkewe ataridhia kufanya hivyo na kuongeza kuwa kwa sasa angependa kuwa na Amina pekee.
 
Leo asubuhi wakati akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds, Ali Kiba amesema wanawake wanaopenda awaoe wasubiri kwa kuwa ana nafasi tatu za kuoa, kama ambavyo dini inamruhusu.

Alipochomekewa swali kama miongoni mwa wanawake hao ni mrembo, Jokate Mwegelo ambaye inatajwa kuwa aliwahi kuwa na uhusiano naye, Ali Kiba alikwepa swali hilo na kubainisha kuwa kwa sasa ni mume wa mtu.
 
Ali Kiba alifunga ndoa na Amina Aprili 19, 2018 mjini Mombasa, na kisha kufanya sherehe nyingine kubwa nchini iliyohudhuriwa na mstaa kibao.

Amina pia alieleza jinsi alivyokutana na msanii huyo na kubainisha kuwa mara ya kwanza ilikuwa kwenye ndege, kwamba wakati huo hakuwa akimjua.
 
Amesema mara ya pili binamu yake alimkutanisha na Ali Kiba na hapo ndipo walipoanza uhusiano.

Amesema siku Ali Kiba alipomtamkia kuwa anataka kumuoa, alimtaka aende kwa wazazi wake akajitambulishe, jambo ambalo msanii huyo aliliridhia.

“Nyimbo yake inayonivutia ni Aje aliyoitoa mwaka mmoja uliopita,” amesema Amina.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya May 12

Makomando wa Marekani wawakamata Al-Shabaab

$
0
0
Vyombo vya dola nchini Somalia vimeeleza kuwa makomando wa Marekani pamoja na Makomando wa nchi hiyo wamefanikiwa kuwakamata watu watatu wanaoaminika kuwa ni makamanda wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab baada ya kufanya oparesheni kali katika kijiji kimoja.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa watu watano ambao ni wakulima wa ndizi walipoteza maisha katika oparesheni hiyo.

Afisa wa kitengo cha Intelijensia ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema kuwa makomando hao walilenga kituo maalum cha Al-Shabaab ambacho kinatumika kama kiungo cha mawasiliano.

Kiongozi wa kimila wa kijiji hicho, Moalim Ahmed amesema kuwa makombando hao pia waliwakamata baadhi ya wanakijiji.

Kamandi ya Marekani barani Afrika haijatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo.

Kundi la Alshabaab ambalo ni mshirika wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda linaendesha oparesheni dhidi ya Serikali ya Somalia, likitaka kusimika utawala wa  sheria kali za kidini.

Marekani ni moja kati ya nchi zilizotoa msaada wa kijeshi nchini humo kupambana na wanamgambo wa Al-Shabaab.

Sugu Kurudi Bungeni Baada ya Afya ya Mama Yake Kuimarika

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi  maarufu Sugu ambaye tangu juzi yupo uraiani baada ya kutoka gerezani kwa msamaha wa Rais John Magufuli, amesema ataanza kushiriki vikao vya Bunge la bajeti mjini Dodoma baada ya kujua maendeleo ya afya ya mama yake mzazi.

“Nasubiri ripoti ya daktari kuhusu hali ya mama ndipo niweze kwenda bungeni.  Ripoti hiyo huenda ikatolewa Jumapili (kesho),” amesema Sugu ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano jela pamoja na na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga

Bunge la bajeti lilianza Aprili 3, 2018 na linatarajiwa kumalizika Juni 30,

Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.

Ofisa Mauzo Kizimbani Kwa Kuchapisha Taarifa za Uchochezi Telegram

$
0
0
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Aggrey&Clifford, Razack Hamad (26) amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kuchapisha taarifa za uchochezi kupitia mtandao wake wa Telegram.

Wakili wa serikali, Patrick Mwita amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Martha Mpazi kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kuchapisha taarifa ya uchochezi kinyume na kifungu cha 53(1)(c) na 52(1)(a) cha Sheria ya Habari Namba 12, ya mwaka 2016.

Inadaiwa mshtakiwa ametenda kosa hilo, Machi 9, mwaka huu akiwa jijini Dar es Salaam ambapo alitumia mfumo wa kompyuta katika simu yake kupitia mtandao wake wa Telegram kwa kuandika; “Nimepata wazo kwa group jingine huko tunaweza kukwepa gharama pia kuandika hata kwenye kuta za wazi #April 26 Magufuli Out, Pinga Dictator” Maneno ambayo yangeibua chuki kwa Watanzania.

Mshtakiwa amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosani bondi ya Sh milioni tano. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 24, mwaka huu.

Bulembo Ahoji Kigugumizi Cha Mwijage Kwa Wamiliki Wa Viwanda

$
0
0
Mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo (CCM), amemtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuweka kando kigugumizi alichonacho katika kuwanyang’anya wamiliki wa viwanda walioshindwa kuviendeleza.

Bulembo ametoa kauli hiyo jana  Mei 11, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2018/19, na kuongeza kuwa inashangaza kuona Mwijage anashindwa kuwachukulia hatua wamiliki hao ilihali tayari Rais John Magufuli alimwagiza kutekeleza agizo hilo mara kadhaa.

“Viwanda vingi vilibinafsishwa na wamiliki wengi wameshindwa kuviendesha, serikali na Rais magufuli amekuambia wanyang’anye… kuna watu wamepewa vina mashine lakini hakuna kitu.

“Baadhi ya viwanda kule Dar es Salaam, Mara , Lindi na Bukoba, wamiliki wamevichukua na kuvigeuza kuwa maghala, sasa unaogopa nini kuwanyang’anya ilihali tayari wamekiuka masharti ya mkataba,” alisema Bulembo.

Bulembo alisema watendaji walioko chini ya waziri wanamhujumu Mwijage kwa kuwa wanaamini nafasi ya uwaziri ni ya kisiasa kwa kuwa baada ya miaka mitano atakuja kiongozi mwingine.

“Ukipanga nyumba ya mtu ukakuta ina nondo kesho ukiweka mbao mwenye nyumba akikufukuza utampeleka mahakamani? wengine wana viwanda wanachechemea afadhali hao kuliko ambao wamebadilisha matumizi,” amesema.

Mwijage: Niko Tayari Kutolewa Kafara au Kupigwa Risasi

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema yuko tayari kutolewa kafara au kupigwa risasi kwa kuhubiri viwanda kwa kuwa tayari amefanikiwa kufufua viwanda 18 kati ya 56.

Pia amesema hana mamlaka ya kufuta baadhi ya viwanda vilivyobinafsishwa kwa wamiliki walioshindwa kuviendelea hadi hapo atakapopata baraka za Baraza la Mawaziri.

Mwijage ametoa kauli hiyo jana Mei 11 bungeni wakati akihitimisha bajeti ya wizara yake kwa kujibu hoja za baadhi ya wabunge.

Alisema kazi aliyopewa kuhusu viwanda vilivyobinafsishwa ni kuhakikisha viwanda vyote bila kujali mmiliki binafsi au serikali, vinafanya kazi vizuri ndiyo maana serikali inatambua mazingira wezeshi.

Amekiri kuwa ni kweli Tanzania katika takwimu za Benki ya Dunia haiko vizuri katika muktasari wa mazingira wezeshi ila ipo katika juu ya wastani wa asilimia 50.

“Sisi ni wa 137 kati ya nchi 190, lakini tupo juu ya asilimia 50. Sitaki kujivuna na hiyo nitafuata maelekezo yenu, ndio maana tunakuja bodi maalumu ambayo hizi taasisi mnazozilalamikia zitaanza kufanya kazi.

“Nimshukuru shangazi yangu Riziki Lulida (CUF), alisema nisiwe kondoo wa kafara, lakini hili la viwanda niko tayari kuwa kafara, nitahubiri viwanda anayetaka kunipiga risasi anipige risasi.

“Lulida unajua mtoto hakui kwa shangazi yake, nilipoelekezwa suala la viwanda, vilivyobinasishwa vilikuwa 156, nilifanya tathmini baada ya Rais kule Tanga aliponiambia namkwaza. Vilivyokuwa vinafanya kazi vizuri vilikuwa 62, vilivyokuwa havifanyi vizuri 56, vilivyokuwa vinasuasua 28, vilivyouzwa kwa vipuri mfano injini peke yake vilikuwa 10,” alisema.

Alisema baada ya kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja kati ya viwanda 56, viwanda 18 vimekarabatiwa na vimeanza kazi.

“Na 35 vilivyobaki nitawasilisha kwa Spika haya ni mambo ya kitaalamu, vingine havina sifa ya kuitwa viwanda ila kwa mamlaka niliyonayo siwezi kuvifuta.

“Kwa mfano eneo la kiwanda cha kuunga trekta hapo Dar es Salaam nimeenda kufanya kukagua nikakuta wamejenga shopping mall nzuri kabisa inaajiri watu, inaitwa Quality Center, mimi mall naipenda kwa sababu inazalisha ajira, mnanishauri nikabomoe shopping mall?.

“Kulikuwa na viwanda vya kupasua mbao lakini sasa misitu imekwisha, sasa huyu mtu nimfanyeje nimuue huyo mtu? Vingine mali ya serikali mfano kiwanda cha maziwa mali ya NHIF (Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya), kiwanda cha serikali  siwezi kukichukua.

“Nimemwambia ajenge kiwanda cha dawa. Yupo kwenye mchakato na suala dawa hivi namaliza kablda ya asubihi, wengine mnasema Mwijage you are not serious (hauko makini) siwezi kujiua,” alisema.

Bodi Ya Mikopo Yasema Umiliki Wa Leseni Za Biashara Kwa Wazazi Sio Kigezo Watoto Wao Kukosa Mikopo

$
0
0
Tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zisizo za kweli zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa waombaji wa mikopo ambao wazazi wao wanamiliki leseni za biashara hawatapata mikopo ya elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2018/2019. Taarifa hizo sio sahihi na zinapotosha waombaji mikopo na umma kwa ujumla.

Ufafanuzi wa kina ni kama ifuatavyo:
a)   Mikopo inayotolewa na Serikali kupitia HESLB inaongozwa na Sheria ya HESLB (SURA 178) pamoja na Mwongozo unaotaja sifa, vigezo na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mikopo. Mwongozo huu unapatikana katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) na hautaji kigezo cha umiliki wa leseni kama sifa ya kukosa mkopo;

b)   Pamoja na mwongozo huu, HESLB pia imeandaa kitabu kwa lugha nyepesi ya kiswahili chenye Maswali na Majibu 21 ili kuwawezesha waombaji mikopo kufahamu sifa na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mikopo kwa ukamilifu na usahihi. Kitabu hiki pia hakijataja umiliki wa leseni kwa mzazi au mlezi kama sifa ya mwanafunzi kukosa mkopo;

c)    HESLB inaamini umiliki wa leseni ya biashara kwa wazazi ni jambo jema na linapaswa kupongezwa kwa kuwa linaimarisha mifumo ya utambuzi kwa wafanyabiashara.
 
Bodi ya Mikopo inapenda kuwakumbusha wadau wote, wakiwemo wazazi, walezi na wanafunzi waombaji wa mikopo kusoma kitabu cha mwongozo wa utoaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 na kitabu chenye maswali 21 ambavyo vinapatikana katika tovuti (www.heslb.go.tz).

Vitabu hivi ndiyo nyaraka rasmi za HESLB zinazotoa mwongozo kuhusu maombi ya mikopo kwa mwaka 2018/2019. 

Aidha, HESLB inapenda kuwakumbusha wadau wote, wakiwemo wanahabari, kusoma nyaraka hizo na kutumia kalamu na kamera kuwaelimisha waombaji mikopo kwa usahihi.

Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM

Mwijage Adai Uhaba Wa Sukari Ilikuwa Ni Propaganda

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kuadimika kwa bidhaa muhimu ya sukari ilikuwa ni propaganda kwa sababu ipo ya kutosha.

Pia amesema masuala ya propaganda anayafahamu vya kutosha kwa sababu amesomea kutoka China na kufunzwa na mwanasiasa mkongwe marehemu Kingunge Ngombale Mwiru.

Mwijage ametoa kauli hiyo jana  Mei 11 wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala kuhusu bajeti yake kwa mwaka 2018/19 na kuongeza kuwa suala la uhaba wa sukari, yeye ni  mcha Mungu pia aliyekuwa mama yake na bibi walikuwa waislamu hivyo hawezi kuwahujumu Waislamu katika kipindi hiki cha kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Watanzania niwaambie tunayo sukari ya kutosha, kuna tani 45,000 kwenye stoo, Tanzania tunatumia 40,000 kwa mwezi, lakini bandarini nimemwagiza TBS (Shirika la Viwango)  na TFDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa) sukari iliyopo bandarini itoke. Mbunge wa kwanza ameniambia nimpe tani 1,000. Wabunge njooni mchukue sukari tunayo ya kutosha bandarini tani 22,000 zipo tayari.

“Mbali na sukari hiyo, viwanda vyote vya sukari vimebakisha wiki tatu hadi hadi vianze kuzalisha kwa hiyo suala la uadimikaji wa sukari lilikuwa propaganda na katika propaganda mimi nimesomea mpaka China. Ilikuwa propaganda, sukari ipo, kama ni propaganda, propagandist mwenyewe ni mimi. Kama Mzee Kingunge Ngombale Mwiru mngemuuliza kwa sababu alinifundisha yeye.

“Kwa hiyo hakuna tatizo la sukari, niko hapa na tunafunga kwenye mwezi Mtukufu wa Ramadhani atakayekuwa na tatizo aje aniulize. Tunasambaza sukari kwenda mikoani,” alisema.

Polisi Kanda Maalum Dar Yawashikilia Watu 10 Kwa Tuhuma Za Wizi Wa Kutumia Silaha

$
0
0
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa  amesema hali ya usalama ya Jiji hilo ni shwari  huku akielezea matukio kadhaa ambayo yametokea katika kukabiliana na matukio ya uhalifu.

Mambosasa amezungumza jana jijini Dar es Salaam ambapo ameelezea pia kukamatwa kwa watu 10 wanaotuhumiwa kwa ujambazi wa kutumia silaha.

Amewataja watuhumiwa hao ni Bushiri Ally (29) mkazi wa Tandika, Mohamed Ismaili (18) mkazi wa Tandika, Issa Saidi (19) mkazi wa Yombo, Mlekwa Ally (18) mkazi wa Tandika, Shabani Nassoro (17) mkazi wa Tandika, na watano wengine ambao majina yao wameyahifadhi kwa sababu za kiupelelezi.

Mambosasa amesema Aprili 29 mwaka huu, saa sita usiku katika maeneo ya Tandika Foma askari wakiwa doria waliitilia shaka gari namba T 401 CLF aina ya Toyota Alteza rangi ya fedha na kuanza kulifuatilia kisha kulikamata na kukuta watu watano wakiwa ndani ya gari hilo.

Amefafanua askari waliwaweka chini ya ulinzi watu hao na kufanya upekuzi ndani ya gari hilo na kufanikiwa kukamata  Bastola aina ya Browning yenye namba N635BRE ikiwa na risasi mbili ndani ya Magazine ikiwa na Watuhumiwa waliokamatwa kwenye gari hiyo ni Bushiri Ally (29) mkazi wa Tandika, Mohamed Isimaili (18) mkazi wa Tandika, Issa  Saidi (19) mkazi wa Yombo, Mlekwa Ally (18) mkazi wa Tandika na Shabani Nassoro (17) mkazi wa Tandika.

"Watuhumiwa hao walihojiwa na mtumiwa mmoja Bushiri Ally alikiri bastola hiyo ni ya kwake na aliiokota Tandika mtaa wa Mteja mwaka 2014 na huwa anaitumia kufanyia vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji,"amesema.

Katika tukio lingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kukutwa na Bastola 2 na risasi 16, nyundo moja na bisisi  tatu ambavyo walikuwa wakivitumia katika matukio mbalimbali ya uhalifu wa wizi wa magari hapa Jijini.
 
Amesema watuhumiwa hao walikamatwa kutokana na operesheni kali inayoendelea kufanyika dhidi ya wezi wa magari na wahalifu wanaotumia silaha.

Aidha ameeleza Mei 5 mwaka huu, saa tano usiku maeneo ya Mbezi Makondeko Remmy Wilbard (41) mkazi wa maeneo hayo akiwa anatoka kwenye biashara zake na gari Toyota Noah namba T681 DJM rangi ya fedha.

Amesema na alipofika nyumbani kwake alishuka kwenye gari lake kwaajili ya kwenda kufungua geti, ghafla alivamiwa na watu watatu wakiwa na bastola moja na silaha za jadi na kumpora gari hilo.
 
"Mlalamikaji alifungua kesi katika kituo cha Polisi Kimara na upelelezi ulianza mara moja ambapo Mei  7 mwaka 2018, saa 12 jioni Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam lilipata taarifa kutoka msiri wake kuwa huko Sinza Kumekucha kuna watu wanataka kuuza gari la wizi.

Amesema ulifanyika ufuatiliaji na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili, na baada ya kufanya mahojiano ya kina na watuhumiwa hao yalipelekea kuwakamata watuhumiwa wengine watatu.
 
Baada ya kukamilisha mahojiano na watuhumiwa hao watano Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam liliongozana na watuhumiwa hao hadi kwenye makazi yao  na kufanya upekuzi.

Hivyo Mei 8 mwaka huu maeneo ya Kimara King’ong’o Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilienda mpaka kwenye nyumba ya mtuhumiwa wa kwanza na kufanya upekuzi na kufanikiwa kupata silaha bastola ambayo haijatambulika aina yake yenye namba AK-0383 TZCAR 71414 iliyokuwa imefichwa ndani ya kabati la nguo ndani ya nyumba ya mtuhumiwa.

Ameongeza kuwa Mei 10 mwaka huu , saa tano usiku maeneo ya Mbagala rangi tatu alikamatwa mtuhumiwa mwingine  baada ya kufanyiwa Upekuzi katika nyumba anayoishi alikutwa na silaha bastola aina ya Beretta U.S.A CORP. ACOOKEEK.MD ikiwa imefutwa namba na risasi sita ndani ya magazine.

"Watuhumiwa hao walikiri kujihusisha na wizi wa magari na uhalifu wa kutumia silaha katika maeneo ya Jiji.Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao hivi,"amesema. 
 
Kuhusu hali ya usalama barabarani Mambosasa amesema kuanzia Aprili 14 mwaka hadi Mei 10 mwaka huu kikosi cha usalama barabarani kinaendelea na juhudi za kupunguza ajali za barabarani kwa kufanya ukaguzi na ukamataji magari na pikipiki mbovu.

Amesema katika kipindi hicho jumla ya magari yaliyokamatwa ni 44,879 idadi ya pikipiki zilizokamatwa 1,466, idadi ya daladala zilizokamatwa ni 17,199, idadi ya magari mengine (binafsi na malori) ni 27,680 na bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa kofia ngumu na kupakia mshikaki ni 103,hivyo jumla ya makosa yaliyokamatwa ni 125,456. Fedha zilizopatikana kutokana na makosa ya usalama barabarani ni jumla ya Sh.1, 563,082,500.

IGP Sirro Awaaga Makamishna Wawili Wastaafu Jijini Dar

$
0
0
Jeshi la Polisi nchini limewaaga makamishna wa Polisi wawili ambao wamefikia umri wa kustaafu  kwa mujibu wa sheria.

Makamishna hao ni aliyekuwa Kamishna wa Polisi wa Fedha na Lojistiki, Clodwin Mtweve  ambaye baadaye aliteuliwa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Katibu  Tawala wa Mkoa wa Mwanza nafasi ambayo ameitumikia hadi kustaafu kwake.

Mwingine ni aliyekuwa Kamishna wa  Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi wa Makosa ya Jinai, Alice Mapunda ambaye ndiye polisi wa kike wa kwanza kupandishwa cheo hadi kufikia cheo cha Kamishna kwa Jeshi la Polisi tangu uhuru.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro amesema kuwa  katika utumishi wao ndani na nje ya Jeshi la Polisi Makamishna hao walishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo kushiriki kikamilifu katika operesheni mbalimbali za Kitaifa, Kikanda na Kimataifa na kuliletea sifa Jeshi la Polisi Tanzania ndani na nje ya nchi.

Kutokana na mchango wao kwa taifa, makamishna hao wametakiwa kuendelea kuwa msaada kwa Jeshi la Polisi wakati wowote watakapohitajika kwa kutoa ushirikiano na ushauri wa kitaalam utakaosaidia kupunguza uhalifu hapa nchini.

Hafla ya kuwaaga makamishna hao imefanyika jana katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kilichopo Kurasini kuanzia saa moja na nusu na palipambwa na gwaride na mayonesho mbalimbali ya kazi za Polisi.
Wastaafu hao Clodwin Mtweve na Alice Mapunda.

Wizara Ya Afya Yamwaga Ajira 8,000 Sekta Ya Afya Nchini

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata kibali cha Ajira kwa sekta ya afya nchini cha kuwaajiri wataalam wa kada mbalimbali za Afya wapatao 8,000.

Hayo yamesemwa  na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.

Dkt. Mpoki amesema wamepata kibali hicho kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kuongeza kwamba Wizara yake inalo jukumu la kuwapangia vituo vya kazi waombaji wenye sifa kwa mujibu wa waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Umma Namba 1 wa mwaka 2009 kuhusu miundo ya utumishi wa kada za afya chini ya Wizara ya Afya.

Aidha, alisema kibali hicho chenye aina mbili za mwajiri ikiwepo nafasi 6,180 ambazo zimeenda Hospitali zilizo katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenye hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati. 

Nafasi 1,820 zimeenda Hospitali zilizo chini ya Wizara ya Afya, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Wizara zingine na Taasisi za Umma pamoja na Hospitali ya Mlongazila na Benjamini Mkapa.

Alitaja sifa za waombaji wa nafasi hizo kuwa, awe raia wa Tanzania, umri usiozidi miaka 45, asiwe mwajiri wa Serikali au mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali na asiwe ameshawahi kufanya kazi Serikalini na kuacha kazi.

Hata hivyo, Dkt. Mpoki amewakumbusha wataalam hasa wale wanaosajiliwa na mabaraza ya kitaaluma kuambatanisha nakala za usajili au leseni ya kufanya kazi ya taaluma husika wakati wa maombi hayo.

Katibu Mkuu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na kueleza kuwa nafasi hizi 8,000 ni juhudi za Serikali za kupunguza uhaba wa rasilimali watu katika sekta ya afya.

Imetolewa na :
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya
11/5/2018
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images