Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali yapiga marufuku uuzaji wa mazao yakiwa bado shambani

$
0
0
Serikali imewapiga marufuku wafanyabiashara, walanguzi na wakulima kuuza mazao yakiwa bado shambani na kusema pindi atakaebainika kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Hayo yamebainishwa leo Mei 07, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 23 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa na kusema kuwa ili kutatua tatizo hilo serikali inaanda mfumo maalumu ambao utatumika katika kuuza mazao kwa soko huria ili kuepusha hasara kwa wakulima.

"Uimarishwaji wa vyama vya msingi vya ushirika na vyama vikuu vya ushirika ili kupitia vyama hivyo wakulima waweze kuuza mazao yao na kujihakikisha soko la mavuno yao. Serikali itasimamia uzwaji wa mazao ya wakulima kwa njia ya minada ili kuweka kuweka ushindani wa bei na kumuwezesha mkulima kupata bei kubwa kama ilivyo katika zao la korosho", amesema Dkt. Mwanjelwa.

Mbowe Afunguka Madiwani 46 wa CHADEMA Kuhamia CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (CHADEMA) Mhe, Freeman Mbowe amefunguka na kutoa neno kuhusu madiwani 46 ambao wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema kuwa jambo hilo linafanywa na CCM kwa lengo la kuwakatisha tamaa wana CHADEMA.

Mbowe amesema kuwa wapo watu wanadhani kitendo cha baadhi ya madiwani kuhama CHADEMA na kwenda CCM ni kukiuwa chama hicho na kusema suala hilo haliwezi kutokea kwani madiwani wa CHADEMA nchi nzima wapo zaidi ya 1130 huku madiwani 46 ndiyo waliohama na kwenda CCM na kusema kitendo hicho kinawapa funzo katika maandalizi ya kutafuta viongozi ambao kweli wanaweza kukisimamia chama na si wale wanaotafuta fursa za kutoka kupitia uongozi.

"Kazi kubwa inayofanywa na CCM ni kuwakatisha tamaa na jambo ambalo limefanyika karibuni ambalo linaonekana wana CHADEMA wengi wamerudishwa nyuma basi ni suala la madiwani.

"Madiwani wamenunuliwa jamanii wanaunga mkono juhudi, kuna watu wengine ni mizigo lakini sasa tunafanyaje lakini watu wa CHADEMA wanakata tamaa eti madiwani wanaisha chama kinakufa

"Hiki chama hakifi mzee CHADEMA nchi nzima ina madiwani 1184 madiwani mpaka dakika hii wameondoka ni madiwani 46 kwa hiyo tuna madiwani zaidi ya 1130 wamebaki CHADEMA halafu mtu anasema CHADEMA inakufa una akili wewe?"

Aidha Mbowe amesema kuwa hao viongozi ambao wanahama kutoka CHADEMA na kwenda CCM kwao ni kama funzo kwamba wapo viongozi na watu mbalimbali ambao wapo ndani ya CHADEMA kwa lengo la kutafuta fursa tu na wanapoikosa hiyo fursa na ulaji wanaamua kuondoka.

"Kwetu ni funzo tunapojiandaa kwenda kwenye uchaguzi wa Wenyeviti wa Mtaa, Vijiji, madiwani, wabunge hata nafasi ya Urais tukajiandaa na kina nani wanaoishi ndoto ya CHADEMA lazima safari hii tujiridhishe mapema huyu tukimpa nafasi basi historia yake tunaijua vyema" alisema Mbowe 

Serikali yatolea ufafanuzi zuio la kufanya Mikutano ya Siasa Nchini

$
0
0
Serikali kupitia Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde,imesema kwamba haijaweka zuio kwa vyama vya siasa kufanya siasa, bali kuna sheria ambazo zinapelekea kutokea kwa ahli hiyo.

Akijibu swali Bungeni kwa niaba ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, amesema seikali haijuzia vyama vya siasa kufanya siasa, kwani imevipa uhuru vyama hivyo kufanya shughuli zake za kisiasa, isipokuwa kuna sheria za jeshi la polisi ndizo zinatoa muongozo juu ya ufanyikaji wa mikutano ya siasa na maandamano.

“"Si kweli kwamba serikali inazuia harakati za kisiasa, sheria imetoa uhuru kwa vyama kutafuta wanachama na kufanya mikutano lakini iko subject na sheria nyinginezo, ikiwemo sheria ya Police force na auxiliary service act ambayo pia imeweka masharti katika section namba 44 na 45 ya namna vyama vya siasa vinaweza vikafanya kazi zao hasa katika mikutano na maandamano mbali mbali”, amesema Anthony Mavunde.

Swali lililojibiwa lililoulizwa na Mbunge wa Rombo Joseph Selasini ambalo lilitaka serikali kusimamia sheria ikiwemo inayowaruhusu wanasiasa kufanya siasa.

Kauli ya Jaji Mkuu Kuhusu mlundikano wa kesi Mahakamani

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahimu Juma leo May 7, 2018 amefungua mafunzo elekezi kwa majaji wapya 14 wa Mahakama Kuu nchini yakiwa na lengo la kuwataka wafanye kazi kwa umakini.

Jaji Prof Juma amezindua mafunzo hayo ya wiki 3, katika Kituo cha Mahakama cha Mafunzo ya Uongozi kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Amesema kuwa Majaji wanatakiwa kutambua kadri wananchi wanavyozitambua haki zao, mlundikano wa kesi unaweza kuongezeka lakini hiyo isiwe kigezo cha wao kushindwa kukidhi matarajio ya wananchi ya kusikiliza mashauri yao na kuyatolea maamuzi kwa wakati.

Akizungumzia mlundikano unaosababishwa na upungufu wa majaji, Jaji Prof Juma amewataka majaji kutumia muda wao vizuri na kujitahidi kuamua kesi ambazo zinaweza kutolewa uamuzi mapema na kumalizika.

Rais Magufuli aagiza Bilioni 2 za ujenzi wa mabweni UDSM ziende SUA

$
0
0
Rais John Magufuli ameagiza pesa kiasi cha Tsh. Bilioni 2, za miradi ya maendeleo katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2018/19 zilizokuwa zimepangwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupelekwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), zihamishwe na zipelekwa katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) cha Mjini Morogoro.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo kwa Waziri anayehusika na wizara hiyo, Prof. Joyce Ndalichako, leo Mei 7, 2018 wakati akihutubia Jumuia ya Chuo hicho alipokitembelea na kupata fursa ya kusikiliza kero za wanafunzi, wahadhiri na wafanyakazi wengine wa chuo hicho ambapo alizitolea ufafanuzi na nyingine kuagiza uongozi wa chuo kuzitatua.

“Mimi ninaamini Chuo Kikuu hiki cha SUA kinaweza kikawa chanzo kikubwa cha kubadilisha maisha ya Watanzania wengi, ninakipenda chuo hiki, si kwa sababu ya jina la Sokoine, ni kwa sababu ya jinsi kinavyofanya kazi.

“Ninafahamu kuwa mna changamoto nyingi, Waziri wa Elimu (Prof. Ndalichako) amesema ametenga Shilingi Bilioni 2 kwa ajili ya kuongeza majengo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mimi ninasema hizo bilioni mbili haziendi UDSM, nazihamishia hapa ili zianze kujenga mabweni.

“Tatizo langu mimi ni moja tu, ni usimamizi, nimeenda Chuo cha Mkwawa, Iringa, nilikuwa discouraged, ninapotoa pesa ninafuatilia, mimi siyo ‘kilaza’ kwa kufuatilia, ninafuatilia kila senti, na ninafahamu thamani ya pesa.

“Sipendi nitakapokuja hapa SUA halafu nikute hizo pesa zimetumika vibaya. Niwaambie tu ukweli sitaki kuonekana mnafiki, mzitumie vizuri. Mimi ninataka dhamira ile ya Baba wa Taifa aliyeanzisha chuo hiki cha SUA tuienzi kwa dhati na kwa vitendo katika awamu hii ya tano.

“Serikali inatamani hata kujenga mabweni ya wanafunzi wote elfu tisa hapa SUA, lakini wapo tu watakaotoka na kukaa huko (nje ya chuo), unakuta mwingine labda ameoa au ameolewa, lakini nitajenga tu,” alisema Magufuli.

Jaji Mkuu: “Tunataka hukumu kuanza kutolewa kimtandao”

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma amesema kutokana na ukuaji wa teknolojia hukumu haziwezi kupatikana kwenye makaratasi bali mitandaoni ili Jaji akikosea kitu dunia nzima ijue.

Jaji Prof Ibrahim ameyasema hayo wakati akizindua mafunzo endelevu kwa Majaji wapya 14 walioteuliwa hivi karibuni.

Amesema kuwa kazi ya Ujaji ni kazi ya kipekee kwani kesi zinakuwa ni tofauti hivyo lazima wapate mafunzo.

“Zamani kulikuwa na imani kwamba majaji lazima wajue sheria na hawahitaji mafunzo, lakini ukiangalia dunia ya sasa kuna mambo mengi duniani ikiwemo makosa mapya ya kwenye mitandaoni hivyo elimu endelevu kwa majaji ni lazima,” amesema.

Amesema kuwa ili Jaji aelewe sheria unayoitekeleza lazima ajue chimbuko la sheria anayotekeleza, hivyo lazima kuingia kwenye mfumo wa dijitali.

“Jamii inayotuzunguka imebadilika haiwezekani hukumu zikawa kwenye makaratasi tu bali ni lazima zitolewe na zipatikane haraka kwenye mitandao tena nimewaonya kwamba wakifanya kosa dogo tu dunia nzima itajua,” amesema Prof Jaji Ibrahim.

Bulaya ataka Wabunge, Mawaziri wakatiwe maji

$
0
0
Mbunge wa Bunda Mjini ( CHADEMA ), Ester Bulaya amesema tatizo la maji ni kubwa nchini, akipendekeza mawaziri na wabunge kukatiwa huduma hiyo ili waone adha wanayoipata wananchi.

Mbunge huyo ameyasema hayo leo Mei 7, 2018 alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya mwaka 2018/19, ambapo ameweka wazi kwamba  fedha zinazotengwa huwa hazitolewi.

Mbunge huyo amesema wabunge na mawaziri wakikatiwa maji watahisi uchungu wanaopata wananchi wa kukosa maji safi na salama kwani kuna hospitali zinashindwa kufanya upasuaji kwa kukosa maji, huku wanawake wakipata adha.

Mbunge huyo ameenda mbali na kuongeza kwamba hali ilivyo sasa ni bora mgonjwa akapelekewa ndoo ya maji kuliko chakula.

Mbali na hayo Mbunge huyo ameongeza kwamba hata vijana wanapohamasishwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji kama hakuna maji ni kazi bure.

“Tunaguswa na tatizo la Watanzania, tunaguswa na tatizo la ajira kwa vijana, ambao wanakwenda kuwekeza katika kilimo lakini hakuna maji,” amesema

Mtoto wa Msogange azikataa shule Alizoahidiwa Kusomeshwa na Wafadhili

$
0
0
Mtoto wa video queen maarufu bongo Agnes Masogange ambaye amefariki mwishoni mwa mwezi uliopita,Sania Shaaban, amekataa kusoma shule za bweni ambazo ameahidiwa kusomeshwa na wafadhili, na kutaka kusoma shule za kutwa.

Akizungumza na East Africa Radio, Sania amesema hataki kukaa mbali na shangazi zake ambao ndio wanamlea, na hajazoea shule hizo.

“Napenda kukaa nyumbani kwa sababu nitawamisi shangazi zangu, shangazi zangu wote nawapenda na sijawahi kukaa mbali nao”, amesema Sania.

Kwa upande wa shangazi zake ambo wanamlea Sada na Samia wamesema mtoto huyo hajawahi kukaa mbali na wao, hivyo suala la kwenda kusoma shule za bweni itabidi lifikiriwe kwanza kwa ajili ya usalama wake.

Udart kuhamisha ofisi Jangwani, wafanyakazi wapewa likizo

$
0
0
Mabasi 29 ya mradi wa mabasi yaendayo haraka (Udart) yameharibika kutokana na eneo lake la maegesho kujaa maji yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini hapa.

Maegesho ya mabasi hayo yaliyopo eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam hujaa maji kila inaponyesha mvua kubwa.

Mbali ya mabasi, pia baadhi ya wafanyakazi wamepewa likizo mpaka maegesho mengine ya mabasi hayo yatakapopatikana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 7, 2018 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Udart, Deus Bugaywa amesema kujaa kwa maji eneo hilo kumesababisha shughuli mbalimbali kusimama jambo lililowafanya waanze kutafuta eneo lingine la kufanyia kazi.

Amesema moja ya sababu iliyochangia hali hiyo ni sehemu ya ukuta ya eneo hilo kudondoka na hivyo maji ya Mto Msimbazi kuingia ndani kwa wingi.

Amesema matengenezo ya mabasi hayo yanafanyika eneo la maegesho ya muda katika vituo vyao vya Gerezani, Kivukoni na Kimara wakati wakiendelea kutafuta sehemu nyingine.

Faiza Amwaga Machozi Baada ya Kubeba Mimba Nyingine.

$
0
0
Mwanadada Faiza Ally amejikuta akiingia katika wakati mgumu baada ya kunasa mimba nyingine ya tatu huku mtoto wake wa kiume wa pili akiwa bado na umri wa miezi nane tu huku yeye mwnyewe akiwa anajipa moyo kuwa hawezi kupata mimba kwa sababu alikuwa akitumia vidonge vya kuzuia mimba.

Akitoa taarifa juu ya swala hilo anasema kuwa hakujua kama angeweza kubeba mimba kwa sababu alikuwa anatumia njia ya kuzuia mimba lakini kwa bahati mbaya kaipata mimba huku akiendelea kunywa dawa hizo ambazo zilikwenda na kuharibu mimba hivyo kuanza kuumwa bila kujua anaumwa nini.

Faiza anasema kuwa baada ya hapo alikwenda hospitali ambapo alikwenda na kugundua tatizo kuwa alikuwa na mimba iliyoharibka  kutokana na kutumia vidonge hivyo,alipofika hospitali waligundua tatizo hilo huku wakiona kuwa mimba ilikuwa imeharibika hivyo kuamua kumsafisha ili kumuweka sawa.

Zari- Kuna Foleni Ya Wanaume Wanaonitaka Lakini Mimi Sipo Tayari

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amefunguka na kudai kuna wanaume kibao wamepanga foleni wako tayari kuwa naye lakini yeye mwenyewe ndio hayuko tayari.

Zari alitokwa na povu hilo siku chache zilizopita baada ya kudaiwa amenunua gari lile ili amrushe roho Diamond na hata kudaiwa upweke alionao ndio unamsumbua na hata kudaiwa kuwa amekosa mwanaume wa kumhonga na kuwa naye.

Siku chache zilizopita Zari aliweka wazi kuwa amenunua gari jipya aina ya Range Rover Lakini mara tu baada ya hapo timu za Instagram zilimjia juu na kumsema kuwa ameazima tu gari lile ili amrushe roho Baba watoto wake na kudai hapo alipo ana upweke wa ajabu.

Zari alitumia mtandao wa Snapchat kuandika  ujumbe ambapo aliweka wazi kuwa hana upweke na wala hana shida ya  kuwa na mwanaume kwa sasa maana wapo wengi wanaomtaka:

".Oooh anajinunilisha magari kwa sababu hana raha, Hapana sio kweli Nipo Single kwa sababu nimeamua kuwa hivyo kwa sasa ..foleni ya wanaume wanaotaka kuwa na mimi ni kubwa sana lakini kwa sasa sitaki mtu... nikiwa tayari nitakuwa na Mahusiano lakini kwa sasa ni mimi na watoto wangu tu”.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 8

Mbunge Amtaka Waziri Aombe Radhi

$
0
0
Mbunge wa Monduli (Chadema), Julius Kalanga amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe kuwaomba radhi Watanzania na Bunge kwa kudanganya kuwa fedha za maendeleo zilizotolewa katika bajeti ya mwaka 2017/18 ni asilimia 56 ilhali kamati ya bunge imebaini ni asilimia 22 tu.

Akichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo iliyowasilishwa jana bungeni jijini Dodoma, Kalanga alisema takwimu nyingi za taarifa za hotuba hiyo zinapingana na za Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji.

Alisema waziri huyo ameonesha fedha za miradi ya maendeleo ya maji zimetolewa kwa asilimia 56 ili kulishawishi Bunge lipitishe bajeti hiyo ilihali wilaya nyingi ikiwamo Monduli hazijatengewa bajeti za mradi wowote mwaka huu.

“Waziri anasema ni asilimia 56 wakati kamati inasema 22, tunataka kujua nani ni mkweli? Alihoji Kalanga.

Akiwasilisha bajeti ya Mhandisi Kamwele katika bajeti ya mwaka 2017/18 hadi kufikia Machi mwaka huu wizara ilipokea fedha za maendeleo Sh bilioni 347.5 sawa na asilimia 56.

Polisi yawasaka walinzi wa mahakama Iliyowaka Moto Mbeya

$
0
0
Polisi imesema hadi sasa haijajua chanzo cha kuteketea kwa moja jengo la Mahakama ya Mwanzo Uyole jijini hapa na kwamba, inaendelea kuwasaka walinzi wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu alisema kwamba jengo la mahakama hiyo na mali zote zilizokuwamo ndani, ziliteketea saa tatu usiku wa kuamkia juzi.

‘Tulipata taarifa kwamba mahakama inaungua tuliwataarifu wenzetu wa zimamoto, lakini wote tulikuta jengo limeshateketea na nyaraka zote zikiwamo pikipiki mbili ambazo zilikuwa ni kielelezo katika moja ya kesi,” alisema Taibu na kuongeza:

“Baada ya kukuta hali hiyo tulijiuliza maswali kadhaa imekuaje. Je, mahakama ile ina walinzi, tukaambiwa inao, bahati mbaya walinzi hawakuwapo wakati huo na hatujui walikwenda wapi?”

Alisema hawajajua chanzo cha tukio hilo hivyo jitihada zinaendelea ikiwamo kuwasaka walinzi hao.

Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Moses Mwidete alisema hakuna kilichookolewa kwa kuwa inaonyesha wakati moto huo unazuka hapakuwapo na mtu yeyote, hivyo nyaraka zote muhimu ziliungua.

“Ulinzi upo na ni walinzi wetu (mahakama), lakini hatujui kilichotokea kwa kuwa mlinzi aliyekuwa zamu hatujui alipo hadi muda huu (jana mchana), kila tukipiga simu yake inaita tu haipokelewi na muda mwingine anakata kabisa simu,” alisema Mwidete na kuongeza:

“Tumeomba wenzetu wa polisi na watu wa mitandao watusaidie kupitia utaalamu wao wa kimtandao kumpata.”

Alisema kazi ya kupata ukweli wa chanzo hicho unaendelea na kitengo cha ulinzi na usalama kupitia ofisi ya kamanda wa polisi mkoa na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji.

“Tumewaomba wenzetu wa zimamoto na polisi kutusaidia hili haraka iwezekanavyo.”

Mahakama Yaubana Upande wa Mashitaka Kesi ya vigogo Uthamini wa madini ya almasi

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili vigogo wawili wa uthamini wa madini ya almasi wa Serikali, kwamba kufikia Mei 21, 2018 watoe majibu sahihi kuhusu ulipofikia upelelezi wa kesi hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbrad Mashauri ameeleza hayo jana Jumatatu Mei 7, 2018 muda mfupi baada ya wakili wa Serikali, Saada Mohammed kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba jalada lipo kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Baada ya Saada kueleza hayo, wakili wa utetezi Nickson Ludovick alidai walitegemea upande wa mashtaka wangeiambia mahakama ni lini wataendelea na kesi hiyo kwa sababu walishasema upelelezi umekamilika.

Aliiomba mahakama imwamuru Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kueleza ni lini kesi itaendelea kwa sababu katika kumbukumbu za mahakama zilizopo, zinaonyesha kesi ilishakuwa tayari kwa kuanza kusikilizwa.

Akijibu hoja hiyo, wakili wa Serikali Elia Athanas alidai jalada bado linashughulikiwa katika sehemu ambazo hazipo sawa na hakuna uzembe wowote unaofanywa na ofisi ya DPP.

Baada ya kutolewa kwa hoja hizo, Mashauri aliamuru upande wa mashtaka Mei 21, 2018 kuja na majibu sahihi kuhusu hatua ya upelelezi ilipofikia.

Washtakiwa wanaokabiliwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (Tansort), Archard Kalugendo na mthamini almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu.

Washtakiwa hao wanasota mahabusu kutokana na DPP kuzuia dhamana zao.

Kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh2.4 bilioni.

Mahakama yatishia kuifuta kesi ya Mkurugenzi wa Lucky Vincent

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Arumeru imetishia kuifuta kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Shule ya Lucky Vicent na wenzake kwa sababu ya upande wa mashtaka kuomba kesi hiyo iahirishwe mara kwa mara.

Hayo yamesemwa na Hakimu wa mahakama hiyo, Desderi Kamugisha baada ya wakili wa serikali, Alice Mtenga kuomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine ili waifanyie mabadiliko hati ya mashtaka.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo kwa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Wakili wa utetezi, Method Kimomogolo alikubaliana na hoja za wakili wa serikali, kwamba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Hakimu Kamugisha alikubaliana na ombi la ahirisho la kesi hiyo, huku akiuonya upande wa mashtaka kwamba kama haujajipanga vizuri kuhusu kesi hiyo anaweza kuifuta kwa sababu inaahirishwa mara kwa mara.

Baada ya kusema hayo aliahirisha kesi hiyo hadi leo May 8, 2018 kwa ajili ya kusikilizwa kwa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Download Upya Application Yetu Ya mpekuzi .....Ile Ya Zamani Tutaifuta

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya Mpekuzi Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Maboresho Mapya Yamefanyika ili kukufanya upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

App ya zamani ilikuwa na tatizo kubwa la kuchelewa kufunguka, kuchelewesha habari na muonekano wake haukuwa wa kiwango kinachostahili.

Chakufanya, Ingia PlayStore, Download Upya Application yetu  MPYA. Ukishaipakua hii Mpya, ya zamani ifute tu.

NB: App mpya ina Icon ya Njano

Tumekurahisishia; 

Lori la Mchanga Laparamia Bodaboda.....Watatu Wafariki Dunia

$
0
0
Watu watatu wamefariki dunia papo hapo na wengine takribani 7 kujeruhiwa vibaya  baada ya Lori la mchanga aina ya SCANIA lililodaiwa kupata hitilafu katika mfumo wake wa breki kuwagonga.

Taarifa za ajali hiyo zinasema, ajali imetokea katika maeneo ya Boko Magengeni, jana Mei 7, 2018 ambapo inadaiwa lori hilo liliwaparamia watu waliokuwa pembezoni mwa barabara huku likisaga pikipiki kadhaa ambazo lilizipitia.

Kufuatia tukio hilo, RPC Kinondoni, Jumanne Murilo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema bado wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo hasa cha ajali hiyo.

Mbali na watu hao kupitiwa na roli hilo, zimo bodaboba na gari nyingine za abiria (coaster) ambazo zilipitiwa na lori hilo.

Pia inadaiwa wengine waliojeruhiwa ni wauza mitumba ambao hupanga kando ya barabara huku wengine wengi wakinusurika baada ya kukimbia walipoona ajali.

Credit: GlobalPublisher

Kampuni ya Maxmalipo yatangaza kupunguza wafanyakazi

$
0
0
Kutokana na mabadiliko ya teknolojia kampuni ya Maxcom Africa imetangaza kuajiri wafanyakazi wapya wenye ujuzi unaohitajika.

Kutokana mabadiliko hayo, baadhi ya wafanyakazi waliopo ambao ama nafasi zao zitakufa kutokana na teknolojia mpya inayotumiwa na kampuni hiyo au zitakuwa zinajirudia hivyo kuilazimu kuwapunguza.

Msemaji wa Maxcom Africa, Deogratius Lazari  amesema  kwa sasa kampuni hiyo ina watumishi 451 lakini baada ya Serikali kuanza kutumia mfumo wa kielektroniki kwenye masuala mengi mfano utoaji wa zabuni, ukusanyaji wa mapato na maeneo mengine, baadhi ya majukumu yamepungua huku mengine yakizaliwa.

“Huwezi kurundika wafanyakazi wengi kwenye eneo moja bila kujali tija yao. Tulipunguza baadhi ya wafanyakazi walioonekana ufanisi wao upo chini mwaka jana ila awamu hii ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia,” amesema Lazari.

Amesema yapo maeneo kadhaa ya operesheni za kampuni hiyo ambayo yameimarishwa kiteknolojia kurahisisha majukumu ya menejimenti, wafanyakazi na mawakala zaidi ya 15,000 waliopo nchini kote.

Taarifa ya uwezekano wa kupunguza wafanyakazi wake iliyotolewa na mkurugenzi wa uendeshaji wa kampuni hiyo, Charles Natai inasema utaratibu wa kisheria utazingatiwa kufanikisha mchakato huo kwa wafanyakazi watakaolazimika kupunguzwa. Taarifa ilitolewa Mei 4.

“Jambo hili linatufanya sisi kufanya uamuzi wa kupitia upya mfumo wa uendeshaji wetu na kuboresha miundombinu ya shirika ili kufikia mahitaji yetu ya kibiashara wakati tukiimarisha ufanisi,”  inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Wolper Amtupia Dongo Zito Sarah Wa Harmonize na Kudai ni Mlezi Wa Vijana

$
0
0
Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amemtupia Dongo zito Sarah baada ya habari zake za kumtosa Harmonize na kumchukua Bodyguard wa Diamond, Mwarabu Fighter.

Siku tatu zilizopita stori iliyotrend kupita zote ni ya mpenzi wa Harmonize Sarah kumtosa mpenzi wake na kumchukua Mwarabu Fighter.

Inasemekana Sarah amekufa ameoza kwa Mwarabu kiasi ya kwamba anamuhudumia ipasavyo yaani kampangishia hadi nyumba yaani zile huduma zozote alizokuwa anapata Harmonize zimehamia kwa Mwarabu.

Kama utakumbuka Kuwa Sarah na Wolper ni maadui wakubwa na kisa kikiwa ni penzi la Harmonize na juzi tu wametoka kumgombania Harmonize.

Baada ya tetesi hizo za usaliti kusambaa mitandaoni Sam Misago Tv walimsaka Wolper na kumuuliza nini maoni yake juu ya ishu hii kumuhusu Sarah na Wolper ameishia kumtupia dongo zito Sarah:

"Duh iyo ishu mbona ni exclusive kabisa sijaisikia lakini freshi tu mbona yule demu ni Mlezi wa wana labda kachoka kumlea mwana kaamua kumchukua mwana mwingine freshi tu”.

Bifu la Wolper na Sarah lilianza baada ya Sarah kuanza kuchepuka na Harmonize wakati Wolper yupo Kwenye Mahusiano na Harmonize.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images