Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 7


Bodi ya mikopo kuanza kupokea maombi mwezi huu

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwataarifu wananchi kuwa inatarajia kuanza kupokea maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi Mei, 2018 baada ya kukamilishwa kwa maboresho makubwa ya mfumo wa uombaji kwa njia ya mtandao.

Maboresho ya mfumo wa maombi
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru amesema katika taarifa yake ya Aprili 17, 2018 kuwa maombi yote yatapokelewa kwa njia ya mtandao (www.olas.heslb.go.tz) ambao umefanyiwa maboresho na Kituo cha Kompyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UCC-UDSM).

Aidha, Bw. Badru amesema dirisha hilo litafunguliwa sambamba na kutangazwa kwa mwongozo wa kina utakaotoa utaratibu wa kuwasilisha maombi, tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi, sifa na vigezo vitakavyotumika katika kuchambua na kutoa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba, 2018.

“Tunawasihi wale wote wanaotarajia kuomba mkopo wa elimu ya juu kusoma kwa makini mwongozo tutakaoutoa kwa vyombo vya habari na tovuti mwanzoni mwa mwezi Mei, 2018 na kuuzingatia,” amesema Bw. Badru.

Bw. Badru amefafanua kuwa wito wa Bodi ya Mikopo umetolewa kutokana na uzoefu wa miaka iliyopita ambapo waombaji wa mikopo waliwasilisha maombi yao bila kuzingatia mwongozo uliotolewa na kusababisha baadhi ya wanafunzi kukosa mikopo.

“Mwaka jana, kwa mfano, zaidi ya waombaji 10,027 kati ya waombaji zaidi ya 61,000 hawakuambatisha nyaraka muhimu kama vyeti vya kuzaliwa au hata vile vya vifo vilivyothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kama tulivyoelekeza,” amesema.

Nyaraka muhimu zinazohitajika
Nyaraka nyingine muhimu ambazo waombaji mikopo wanapaswa kuziandaa ni pamoja na nakala za vyeti vya kitaaluma za kidato cha nne, sita na stashahada ambazo zimethibitishwa na Kamishna wa Viapo yaani Wakili au Hakimu.

Aidha, wanafunzi waombaji wenye ulemavu au wenye wazazi wenye ulemavu wanapaswa kuwa na barua zinazothibitisha ulemavu huo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa, Wilaya au Kituo cha Afya cha Serikali;

Bw. Badru ameongeza kuwa wanafunzi ambao walifadhiliwa katika masomo yao ya Sekondari au Stashahada (Diploma) wawe na barua za uthibitisho wa udhamini huo kutoka katika taasisi zilizogharamia masomo yao.

Maafisa wa HESLB kutoa elimu mikoani
Katika hatua nyingine, Bw. Badru amesema mwaka huu maafisa wa Bodi ya Mikopo watatembelea mikoa mbalimbali ili kukutana na waombaji mikopo kwa lengo la kuwaelimisha kuhusu taratibu sahihi za kuwasilisha maombi yao ya mikopo kwa njia ya mtandao. Ratiba na maeneo itakapofanyia mikutano hiyo itatangazwa mwanzoni mwa mwezi Mei, 2018.

HESLB ilianza kazi rasmi mwaka 2005 ili, pamoja na majukumu mengine, kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa watanzania wahitaji na wenye sifa na kukusanya mikopo iliyoiva ambayo ilitolewa na Serikali tangu mwaka 1994/1995.

Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM
Kwa ufafanuzi: +255 (0) 757 500800

Irani Yasema Marekani itajuta ikijitoa mkataba wa nyuklia.....Ufaransa Yahofia Kuzuka Vita

$
0
0
Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema kwamba endapo Marekani itajiondoa kwenye mkataba wa nyuklia kati ya nchi yake na mataifa yenye nguvu duniani, basi Marekani itajutia maisha yake yote.

"Ikiwa Marekani itaondoka kwenye makubaliano ya nyuklia, mutaona hivi karibuni watakavyojutia kuliko ilivyowahi kuwatokezea kwenye historia," alisema mwanamageuzi Rouhani kwenye hotuba yake ya jana (Jumapili 6 Mei) akiwa kaskazini mwa Iran.

"Trump anapaswa kujua kuwa watu wetu wameunganika, utawala wa Kizayuni (Israel) unapaswa kujuwa kuwa watu wetu wako kitu kimoja," alisema Rouhani.

"Leo, mirengo yote ya kisiasa nchini Iran, ama iwe kulia au kushoto, wahafidhina, wanamageuzi na watu wa mrengo wa kati, wote wameungana," aliongeza.

Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kujiondoa kwenye makubaliano hayo wakati utakapofika muda wa kusainiwa upya tarehe 12 Mei, akiwataka washirika wa Ulaya "kuyarekebisha makosa makubwa yaliyomo" ama sivyo arejeshe upya vikwazo dhidi ya Iran.

Mkataba huo wa nyuklia ulisainiwa mwaka 2015 kati ya Iran na Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Marekani, wakati huo ikiongozwa na Barack Obama.

Chini ya makubaliano hayo, vikwazo vilipunguzwa kwa masharti ya Iran kutokuunda bomu la nyuklia, lakini Iran inasema haioni mafanikio ya ahadi hizo licha ya kutimiza masharti ya mkataba.

Mara kadhaa, Rouhani amekuwa akirejelea msimamo wa nchi yake kupinga kuzuiliwa nchi yake kuunda makombora yasiyo ya kinyuklia, na hilo amelizungumzia pia kwenye hotuba yake ya Jumapili.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa (kushoto) anaamini kuwa Marekani haina sababu ya kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran.

Naye Trump amekuwa akiukosoa mkataba huo, akitaja baadhi ya vifungu ambavyo anasema vinaondoa vikwazo vya nyuklia kuanzia mwaka 2025.

Macron aonya dhidi ya vita
Katika jitihada za kuyaokoa makubaliano hayo, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amependekeza hivi karibuni kwamba mkataba huo utanuliwe kuyashirikisha masuala kama hayo yanayolalamikiwa na Trump, na pia kuondoa kikomo ya muda wa Iran kuruhusiwa kuunda makombora mengine na pia kuangalia dhima ya Iran kwenye eneo la Ghuba na Mashariki ya Kati.

Hatua ya Iran kumuunga mkono Rais Bashara al-Assad, kupitia kundi la Hizbullah la Lebanon, na pia kuwaunga mkono waasi wa Kishia nchini Yemen kumeongeza mzozo kati yake na mataifa ya Magharibi.

Licha ya hayo, jana Rais Macron ameonya kwamba kunaweza kuzuka vita endapo marekani itajiondoa kwenye makubaliano hayo.

"Tunaweza kuibuwa mambo mengine mapya. Kunaweza kukawa na vita," Macron ameliambia gazeti la kila wiki la Ujerumani, Der Spiegel, ingawa ameongeza: "Sidhani kama Donald Trump anataka vita."

Waliojihami kwa silaha wavamia kijiji na kuua Watu 45 Nigeria

$
0
0
Watu 45 wamepoteza maisha katika kijiji kimoja jimbo la Kaduna nchini Nigeria baada ya watu wenye silaha kuvamia kijiji hicho na kuchoma moto nyumba.

Wahanga wa tukio hilo wengi wao wanadaiwa kuwa ni wale wa kundi maalum lililoundwa kwa lengo kulinda mifugo kijijini hapo kufuatia matukio kadhaa ya wizi.

Imeelezwa kuwa watu hao wenye silaha walizingira kijiji cha Gwaska majira ya mchana na kuanza kurusha risasi hovyo huku wakichoma moto nyumba. Kila aliyetaka kutoroka alishambuliwa vikali, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na BBC.

Serikali ya Rais Muhammadu Buhari imeendelea kulaumiwa kwa kile kinachodaiwa kutochukua hatua za kuridhisha kusitisha vitendo hivyo vya kihalifu vinavyochukua maisha ya wananchi wasio na hatia.

Mwezi uliopita, wachimbaji wadogo wa madini 14 waliripotiwa kuuawa na watu wenye silaha katika eneo la Birnin Gwari.

Ali Kiba Aburuzwa Mahakamani

$
0
0
Mfanyabiashara  wa mitumba Hadija Hassan amefungua kesi ya madai ya matunzo ya mtoto dhidi ya msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba maarufu kama King Kiba.

Katika kesi hiyo, Hadija anadai jumla ya Sh. milioni 1.41, ikiwamo Sh. 950,000 za ada na Sh. 460,000 za matumizi ya mtoto wa miaka mitano (jina limehifadhiwa kwa sababu za kisheria na kimaadili).

Hadija ambaye ni mfanyabiashara wa mitumba amefungua kesi ya madai hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akidai matunzo kwa mlalamikiwa ambaye ni mzazi mwenzie -King Kiba.

Kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani hapo, mlalamikaji anadai kuwa Januari, 2013 katika Hospitali ya Mikocheni, jijini Dar es Salaam alizaa mtoto wa kike ambaye baba yake ni mlalamikiwa.

Alidai kupitia hati hiyo kwamba mlalamikiwa anatakiwa kumhudumia mtoto huyo kwa mahitaji yote muhimu ikiwamo chakula, nguo, elimu na matibabu.

"Kutokana na Sheria ya Watoto ya mwaka 2009, mdaiwa anatakiwa kutoa huduma kila mwezi, chakula Sh. 150,000, matunda Sh. 50,000, chakula cha ziada Sh. 50,000, michezo na burudani za watoto Sh. 100,000, nguo Sh. 60,000 na matibabu Sh. 50,000 ambapo jumla ni Sh. 460,000," alidai mlalamikaji kupitia hati hiyo.

Aidha mlalamikiwa anatakiwa kulipa ada ya shule kwa muhula Sh. 950,000, na anadaiwa aliacha kutoa matunzo hayo kwa mtoto tangu Januari, mwaka huu hivyo anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa kutoa matunzo hayo ya Sh. 460,000 kila mwezi na ada.

Pamoja na mambo mengine, mlalamikaji anaomba malipo ya kwanza yatolewe mapema baada ya hukumu, na pia anaiomba mahakama imwamuru King Kiba kumsomesha mtoto, kumnunulia nguo na matibabu ikiwamo kumtafutia bima ya afya.

Pia mlalamikaji anaomba mahakama imwamuru Kiba kulipa gharama za matunzo Sh. 460,000 kuanzia Februari 2017 mpaka siku itakapotolewa hukumu na gharama za kesi ziwe kwa mdaiwa.

Mbali na maombi hayo, Hadija anaomba mahakama itoe amri nyingine yoyote itakayoona inafaa kwa manufaa yake. Kesi imefunguliwa kwa msaada wa Kituo cha Wanawake cha Msaada wa Kisheria (WLAC).

Ali Kiba, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Ali Saleh Kiba amefunguliwa madai hayo ikiwa ni siku chache tangu afunge ndoa iliyopendeza mjini Mombasa Kenya.

Rais Magufuli Aonya Mapigano ya Wakulima na Wafugaji

$
0
0
Rais Magufuli amewataka Wakulima na Wafugaji kuacha vitendo vya kupigana na kwamba katika serikali yake hakuna mtu aliyeko juu zaidi ya mwingine na kusisitiza kwamba watanzania wote ni sawa kwani ndiyo waliyomchagua.

Akizungumza jana na wananchi wa Morogoro akiwa njiani kuelekea Msamvu Raid Magufuli alisema kwamba kamwe vitendo vya kupigana visirudie katika serikali yake na kwamba wale watakaokiuka watashughulikiwa.

Aidha aliongeza kuwa anataka wakulima na wafugaji waishi kwa kuheshimiana kwani yeye anachokihitaji ni amani.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli amewashangaa Wafugaji kuwalisha ng'ombe mazao ya wakulima ilhali kuna majani ya kutosha na wanaposhtakiwa wanaamua kutumia gharama kubwa kuhonga hata kufikia hatua ya kuuza ng'ombe.

"Mimi nimekaa kwa wamasai Monduli, nimechunga mpaka ng'ombe za wamasai nikiwa JKT Makuyuni. Ni watu wazuri tu. Sasa kwanini wamasai wa huku wanachukia mali za wengine wakulima? Nataka niwaaeleze nitalifuatilia hili.

Pamoja na hayo aliongeza "Kama yupo mmoja ambaye analiisha kila siku anajifanya ana mali huyo mimi ndiye ntalala naye mbele mwenyewe".

Israeli: Tupo Tayari Kukaibili Irani Kwa Hali Yoyote Hata kama ni Kwa "Mapambano"

$
0
0
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inawapa Syria silaha zenye ubora zaidi ambazo nitishio kwa Israel ni vyema kuikabili Tehran hivi sasa kuliko hapo baadae.

Netanyaju ameliambia Bunge la nchi hiyo linalokutana Jumapili kuwa “Tunadhamira ya kuzuia vitendo vya uchokozi vya Iran dhidi yetu hata kama hilo litakuwa kwa njia ya mapambano. Ni bora hilo lifanyike hivi sasa kuliko hapo baadae.” Aliongeza: Hatutaki kuongeza mvutano, lakini tuko tayari kwa hali yoyote.”

Israel imerudia mara kadha kuonya kuwa haiwezi kuvumilia uwepo wa kudumu wa majeshi ya Iran katika nchi jirani ya Syria.

Iran ni mshirika muhimu wa Rais wa Syria Bashar Assad, na imekuwa ikitoa misaada muhimu ya kijeshi kwa majeshi ya Assad.

Dk Mengi aitikia wito wa rais kujenga kiwanda cha dawa,Ummy azindua ujenzi

$
0
0
Mwenyekiti  Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi ameingia ubia na Mwekezaji kutoka India kujenga kiwanda cha dawa kitakachogharimu dola za kimarekani milioni 55 sawa na shilingi bilioni 55 za Tanzania.

Ujenzi wa kiwanda hicho kipya kiitwacho  M- pharmaceutical Ltd,  katika eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani umewekewa jiwe la msingi na Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mwishoni mwa wiki.

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda hicho Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alimpongeza Dr Mengi kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais John Magufuli alilolitoa wakati wa uzinduzi wa hospitali mpya kisasa ya Taaluma na Tiba Muhimbili  Mlonganzila.

Novemba mwaka jana akifungua Hospitali hiyo katika hotuba yake Rais John Magufuli aliwataka wafanyabiashara nchini kuanzisha viwanda vya dawa kwa kuwa fedha nyingi zinatumika kuagiza dawa kutoka nje.

Dk Mengi ambaye pia ni Rais wa sekta binafsi alikuwepo katika uzinduzi huo na kusema kwamba yeye na wenzake watalitafakari rasmi suala hilo.

Waziri Ummy Mwalimu pia amemhimiza Dr Mengi na mbia mwenzake kuharakisha ujenzi wake na kumhakikishia kuwa bidhaa zitakazozalishwa zitapata soko kubwa hapa nchini na nchi za ukanda huu, na kunufaika na upendeleo maalum wa  bidhaa zinazozalishwa nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi amesema katika awamu ya kwanza kiwanda hicho kitazalisha chupa milioni 30 kwa mwaka za aina mbalimbali za maji ya dripu zinazotumiwa wakati wa matibabu ya dharura nyakati za ajali, upasuaji, homa kali, na magonjwa ya mlipuko, zinazokidhi vigezo vya kimataifa.

Amesema kipaumbele cha ajira kitatolewa kwa wananchi wa Bagamoyo, na kusisitiza kuwa umuhimu wa Watanzania kujiamini katika kujiletea maendeleo.

Mapema Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Dk Charles Mwijage na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikiro  amewataka viongozi wasiwakwamishe wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika maeneo yao.

Aidha walisema kwamba serikali itashughulikia changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa maji, umeme wa uhakika na gesi asilia katika eneo hilo.

Alisema kwamba taifa linajenga uchumi wa viwanda na ni kazi ya serikali kuwezesha mazingira rafiki kwa ajili ya uwekezaji.

Uwekaji jiwe la msingi ulishuhudiwa na wananchi wa Kerege, Balozi wa Ufaransa Frederic Clavier, balozi wa China Wang Ke, Mbunge wa Bagamoyo Dr Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ramadhan Maneno na  viongozi mbalimbali mbalimbali wa serikali na CCM wa mkoa na wilaya ya Bagamoyo.

Zari Anunua Range Rover Lenye Thamani Ya shilingi Milioni 172

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan amethibitisha kuwa yeye ni Bosslady kweli baada ya kuweka wazi kuwa amenunua gari aina ya Range Rover lenye thamani ya shilingi milioni 171,337,500.

Zari alitangaza mpango wake wa kununua gari hilo wiki chache zilizopita na hatimaye wikiendi hii alilianika gari hilo jipya na kuliweka Kwenye mitandao ya kijamii.

Mara baada ya kuweka gari hilo kuna habari zilizuka kuwa amenunuliwa gari hilo na mpenzi wake taarifa alizozikana na kuweka wazi kuwa amenunua gari lile kwa hela zake mwenyewe.

Lakini pia Zari ameweka wazi mipango yake ya kuanzisha Food franchise kama vile KFC au McDonalds.

Dk. Shein Awaonya Wanaosaka Urais Zanzibar

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amewaonya baadhi ya watu wanaofanya kampeni za kusaka urais wa Zanzibar kabla ya muda wa kufanya hivyo kufika na kusisitiza kuwa yeye bado ni Rais wa Zanzibar.

Amesema kuna baadhi ya viongozi wa chama na serikali tayari wameanza kupanga timu za urais badala ya kushughulika na mambo ya msingi ya kufanya shughuli za chama zitakazofanikisha kuiweka serikali madarakani katika uchaguzi mkuu ujao.

Dk. Shein ametoa onyo hilo jana katika ziara yake ya kutembelea mashina ya chama hicho katika Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

“Nafasi ya urais ndani ya CCM haipatikani kwa kampeni na makundi yasiyo halali bali kwa utaratibu maalumu kupitia vikao vya kikatiba ambavyo vipo kwa mujibu wa Katiba na miongozo na kanuni  mbali mbali za CCM,” amesema.

Dk. Shein pia amebainisha kuwa watu hao wasipoacha tabia hiyo na kuvumilia hadi 2020, atawachukulia hatua kali za kinidhamu zikiwemo kufikishwa katika vikao vya usalama na maadili vya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) ili wahojiwe na kuchunguzwa dhidi ya mwenendo wao  juu ya mwenendo wao usiokuwa na manufaa kwa CCM.

Barua Ya Kumnusuru Malasusa Yasomwa Makanisani

$
0
0
Waumini  wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),  Dayosisi ya Mashariki na Pwani(DMP),  walisomewa barua maalumu kuhusiana na suala  la Askofu wao, Dk. Alex Malasusa.

Kusomwa kwa barua hiyo jana kunatokana na kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani kilichokutana Jumatano iliyopita.

Barua hiyo iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Godfrey Nkini, ilisomwa katika usharika mbalimbali za dayosisi hiyo wakati wa matangazo.

Kwa mujibu wa barua hiyo, washarika wametakiwa kufahamu kwamba Dk. Malasusa ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani na dayosisi itaendelea na umoja na mshikamano na askofu huyo katika kuongoza na kuihubiri injili ya Yesu Kristo.

“Halmashauri kuu inaendelea kulifuatilia jambo hili kwa makini. Washarika mnaombwa kuwa watulivu na kuliombea kanisa.

“Tunaombwa kutunza amani na umoja wa kanisa kama neno la Mungu linavyosema,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo.

Askofu Malasusa, Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini na Kati, Solomon Massangwa na Askofu wa Dayosisi ya Kusini Mashariki, Dk. Lucas Mbedule, wanatuhumiwa kwa usaliti kutokana na uamuzi wao wa kuzuia waraka wa Pasaka ulioandaliwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo usisomwe katika dayosisi wanazoziongoza.

Jumapili iliyopita Askofu Mbedule alilazimika kuomba radhi kutii maagizo ya Baraza la Maaskofu wa KKKT.

Waraka huo ulioandaliwa mwishoni mwa Machi mwaka huu, wiki moja kabla ya maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka, ulichambua masuala ya jamii, uchumi, maisha ya siasa, umuhimu wa katiba mpya na matukio yaliyo kinyume na kile walichokiita tunu na misingi ya taifa.

Licha ya barua hiyo ya kanisa kusomwa baadhi ya waumini walihoji hatua hiyo kutokana na kutosomwa na waraka wa kanisa wa Pasaka na badala yake wamesomewa barua ya kumkingia kifua Askofu Malasusa.

Hatua ya halmashauri kuu ya dayosisi hiyo imeonyesha kumkingia kifua kutokana na barua iliyoandaliwa na chombo hicho na ilisomwa jana.

Kwa mujibu wa nakala ya barua hiyo , Halmashauri Kuu ya Dayosisi hiyo, imesema haikuwa na lengo la kupingana na maazimio ya Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa  KKKT juu ya kusomwa kwa Waraka wa Pasaka.

Barua hiyo imesema maelekezo yote yaliyotolewa yamezingatiwa na imesisitiza kuwa umoja na mshikamano kwa Askofu Dk. Malasusa utaendelea katika kuongoza na kuihubiri Injili ya Yesu Kristo.

Barua hiyo ilieleza kuwa halmashauri hiyo ilikaa kikao Mei 2, mwaka huu na ilijadili na kujiridhisha kuhusu barua aliyoandikiwa Askofu Malasusa kuwa alikiuka mapatano yaliyotolewa na mkutano wa maaskofu wa KKKT.

“Halmashauri Kuu imetafakari kwa kina jambo hili na kujiridhisha kwamba: Haikuwa lengo la DMP kupingana na maazimio ya Mkutano wa Maaskofu daima. Maelekezo yote yaliyotolewa na KKKT Makao Makuu yamezingatiwa.

“Hata hivyo, Halmashauri Kuu imesikitishwa kwa jinsi suala zima lilivyotunzwa hadi kufikia vyombo vya habari na baadhi yao kupotosha ukweli wa suala zima,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.

Kuhusu Askofu Malasusa barua hiyo ilisisitiza: “Washirika mfahamu kwamba Malasusa ni Askofu wa DMP. Halmashauri inatoa pole nyingi kwa Baba Askofu na familia yake kwa usumbufu uliojitokeza. DMP itaendelea na umoja na mshikamano na Askofu Malasusa katika kuongoza na kuhubiri Injili ya Yesu Kristo.”

Pamoja na barua hiyo kutoa pole kwa washirika wote kutokana na kuumizwa kwao na taarifa za kuandikiwa barua Askofu Malasusa za kukiuka mapatano ya Baraza la Maaskofu, ilizodai haikuwa lengo la KKKT Makao Makuu kuwaumiza waumini wake, pia ilieleza inaendelea kulifuatilia jambo hilo kwa makini.

Pia barua hiyo iliwaelekeza washirika hao kuwa watulivu na kuliombea kanisa na kutunza amani na umoja.

Uamuzi wa kumtenga Askofu Malasusa ulifikiwa na kikao cha Baraza la Maaskofu wapatao 25, lililoketi mjini Arusha, chini ya kiongozi wake ambaye ndiye mkuu wa kanisa hilo, Askofu Dk. Fredrick Shoo.

Wafanyabiashara Tunduma Wahamia Zambia

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Gallawa ametoa siku 14 kwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma  a na watendaji wa Mamlaka ya  Mapato Tanzania (TRA) kufanya uchunguzi wa haraka  kubaini  iwapo kuna wafanyabiashara waliohamishia biashara zao  Zambia.

Akizungumza jana katika mkutano na wafanyabiashara mjini Tunduma, Gallawa alisema ameagiza viongozi hao kufanya utafiti kwa haraka kubaini kama wafanyabiashara wa Tanzania wamehamishia biashara zao nchini humo.

Inadaiwa kuwa wafanyabiashara wamehamishia biashara zao Zambia kutokana na vikwazo kutoka TRA vikiwamo utitiri wa kodi tofauti na Zambia.

“Eneo la Tunduma ni dogo kiasi ambacho inatakiwa kuchunguzwa kutambua ni kwa nini wafanyabiashara hao wamehama kwenda kufanya biashara hizo   Zambia.

“Na imani ni kuwa uchunguzi ukishafanyika tutajua ni njia gani ya kuwarudisha na wakaendelea na shughuli zao,” alisema Gallawa.

Alisema   wafanyabiasha wa Tunduma walizoea kufanya biashara bila kulipa kodi  hivyo kuwapo mabadiliko ya sasa inawezekana ikawa ni chanzo cha wao kuhamia   Zambia na kuanzisha biashara zao huko.

Meneja wa TRA Mkoa wa Songwe, Paul Alalaze alisema malalamiko ya wafanyabiasha yamekuwapo kwa muda mrefu yakiwamo ya viwango vya utozwaji wa kodi vikidaiwa kuwa vikubwa tofauti na Zambia.

Alisema kutokana na wafanyabiashara wengi wa Tanzania kuhamia Zambia zinafanyika jitihada za kuwaelimisha  waendelee kufanya shughuli zao  nchini mwao.

“Tunawaelimisha kuwa wanatakiwa warudi kufanyia shughuli zao Tanzania ili kuendelea kujenga uchumi wa nchi yao na si kukimbilia Zambia ambako si kwao kwa sababu  wananufaisha watu wengine,” alisema Alalaze.

Baadhi ya wafanyabiashara walisema  idadi ya wenzano wanaohamishia miradi yao   Zambia inazidi kuongezeka.

Wameitaka Serikali   kufanya uchunguzi   kubaini ukweli wa malalamiko hayo ili kupata ufumbuzi wa kudumu.

Umri Wa Madaktari, Maprofesa Kustaafu Waongezwa

$
0
0
Serikali  imefanya marekebisho ya utumishi wa umma sura 298  kuongeza umri wa kustaafu kazi maprofesa na wahadhiri waandamizi katika vyuo vikuu vya umma.

Wengine watakaohusika ni  madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu katika hospitali za umma nchini.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa   jana ambayo imesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Makwaia Makani.

Taarifa hiyo inasema  umri wa kustaafu kazi kwa madaktari katika hospitali za umma ni miaka 60 badala ya 55 kwa hiari na miaka 65 badala ya 60 kwa mujibu wa sheria.

“Katika kukabiliana na upungufu wa wanataaluma na wataalamu waliopo kwa sasa katika vyuo vikuu vya umma na hospitali za umma nchini.

“Serikali imefanya marekebisho katika sheria ya utumishi wa umma sura 298 kuongeza umri wa kustaafu kazi maprofesa na wahadhiri waandamizi katika vyuo vikuu vya umma na madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu katika hospitali za umma kupitia sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali Namba 1 ya Mwaka 2008.

“Marekebisho yaliyofanywa katika sheria ya utumishi wa umma yameainisha umri wa kustaafu kazi kwa kada tajwa hapo juu kwa miaka 60 badala ya 55 kwa hiari na miaka 65 badala ya 60 kwa mujibu wa sheria. Mabadiliko haya yameanza rasmi Februari 9 mwaka huu,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema madaktari bingwa wote ambao hawakuwa wamefikisha umri wa kustaafu kazi kwa mujibu wa sheria Februari 9 mwaka huu, wataendelea na ajira zao hadi hapo watakapofikisha miaka 65 na kwamba taarifa zao za kustaafu kwa wale waliopata zinafutwa.

Vilevile taarifa hiyo  ilieleza kuwa madaktari bingwa watakaotaka kustaafu kwa hiari watatoa taarifa ya maandishi kwa mkurugenzi mtendaji.

Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha alisema ni kweli tangazo hilo ni la kwao.

Kuanza kwa sheria hiyo kunatokana na kupitishwa  Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba Tano wa Mwaka 2017 ambao utazihusisha sheria tano ikiwamo ya Utumishi wa Umma sura namba 298 ambako kifungu kipya cha 25A kitaongezwa.

Vikao vya kamati za Bunge vimeanza huku miongoni mwa miswada itakayojadiliwa ikiwa ni ule utakaoongeza umri wa kustaafu kwa lazima kutoka miaka 60 hadi 65 kwa maprofesa, wahadhiri waandamizi na madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu wa umma.

Inaelezwa kuwa lengo la kuongezwa kwa sheria hiyo ni kuweka kwenye masharti ya umri wa kustaafu kwa watumishi wa umma ambayo hayapo kwenye sheria ya sasa.

Mfumo huo mpya unalenga kuongeza umri wa kustaafu wa utumishi wa umma kwa ridhaa kwa maprofesa na wahadhiri waandamizi wa vyuo vikuu vya umma na madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu wa hospitali za umma ili uwe 60 kwa wale wanaostaafu kwa hiari badala ya 55 wa sasa.

Pia, mfumo huo unalenga kuongeza umri wa kustaafu kwa lazima uwe miaka 65 badala ya sasa wa miaka 60 ya sasa.

“Marekebisho haya yanalenga kutekeleza uamuzi wa Serikali unaolenga kuongeza umri wa kustaafu kwa maprofesa, wahadhiri waandamizi wa madaktari bingwa wa binadamu kutoka vyuo vikuu vya umma na hospitali za umma,” ilielezwa.

Serikali yatangaza ukaguzi mwingine mpya

$
0
0
Serikali ya awamu ya tano kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imesema itafanya zoezi la ukaguzi nchini nzima katika sehemu za kazi ikiwemo kampuni ya ACACIA ili iweze kuwabaini waajiri ambao hawazingatii vigezo na masharti wanayopaswa kuwafanyia wafanyakazi wao.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 07, 2018 na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 23 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la Mbunge wa viti maalum Jocye B. Sokombi aliyetaka kusikia kauli ya serikali juu ya tatizo la wafanyakazi wa mgodi wa Nyamongo kutolipwa mshahara wala posho pindi wafanyapo kazi zao.

"Mgodi wa dhahabu wa Nyamongo unamilikiwa na kampuni ya ACACIA na kwenye mgodi huo kuna makundi mawili ya wafanyakazi ambapo moja ni wale walioajiriwa na ACACIA na pili wafanyakazi waliajiriwa na makampuni yanayopewa kazi na ACACIA 'sub contractors'. Hivyo kwa wafanyakazi walioajiriwa na ACACIA wao hawalipwi posho bali hulipwa mshahara kwa mwezi", amesema Mavunde.

Pamoja na hayo, Mavunde ameendelea kwa kusema "makampuni mengine huwa wanalipwa mishahara kutokana na aina ya mikataba ya ajira na asili ya kazi anayoifanya mfanyakazi kwa kuzingatia sheria. Ofisi yangu kupitia idara ya kazi itaendelea kufanya kaguzi za kazi katika sehemu za kazi mbalimbali nchini ikiwepo kampuni ya ACACIA kwa lengo la kuwatambua waajiri ambao hawazin gatii matakwa ya sheria za kazi yanayotakiwa".

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri Antony Mavunde amesema idara ya kazi imekuwa na taratibu za kufanya ukaguzi katika makampuni yote kwa lengo la kujua changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwa wafanyakazi.

Kigwangalla ataka Mkataba wa makubaliano

$
0
0
Na Hamza Temba-WMU-Dodoma
..............................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza uandaliwe mkataba wa makubaliano ya awali (MoU) ya utekelezaji wa mradi wa kuendeleza utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous.

Mkataba huo wa makubaliano utahusisha wawekezaji kutoka Jiji la London nchini Uingereza na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA na  utakapokamilika utasainiwa na pande zote mbili.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo juzi ofisini kwake Jijini Dodoma kufuatia maombi yaliyowasilishwa kwake na wawekezaji hao, Eva Sanchez na Nicholas Negre.

Akiwasilisha maombi hayo, Sanchez amesema mradi huo utakuwa wa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA ambao ndio wasimamizi wakuu wa Pori la Akiba Selous utakapoanzishwa mradi huo.

Amesema pamoja na mambo mengine mradi huo wa utalii wa picha pia utasaidia kupiga vita ujangili na kukuza uchumi wa jamii zinazozunguka pori hilo.

Dk. Kigwangalla amewataka wawekezaji hao kuwasilisha andiko la mradi huo, kufanya utafiti wa kina na tathmini ya athari za kimazingira zitakazoweza kujitokeza kutokana na uanzishwaji wa mradi huo.

Amesema kwa sasa Serikali inafanya marekebisho ya Sheria mbalimbali zitakazoiwezesha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA  kutekelezaji majukumu yake ipasavyo ikiwemo uwekezaji wa aina hiyo kwenye sekta ya Utalii wa Picha na Uwindaji wa Kitalii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara amesema mamlaka hiyo itatoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji hao ili kutimiza azma ya Serikali ya kushirikisha wadau, watu binafsi na wawekezaji katika kukuza sekta ya utalii nchini.

Pori la akiba Selous ndio hifadhi kubwa kuliko zote nchini ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba takriban 50,000 katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Mwaka 1982, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Uneso) lilitangaza eneo hilo kuwa moja ya eneo la Urithi wa Dunia na kuanza kuhifadhiwa.

Queen Darlen Amtaka Harmonize Apunguze Uhuni Anamtesa Sarah

$
0
0
Mwanadada pekee kutoka katika kundi la wasafi, Queen Darlen amefunguka na kutoa ushauri kwa msanii mwenzake kutoka katika kundi hilo kwa kumtaka  Harmonize kupunguza tabia ya uhuni kwa sababu anamtesa sana sarah ambae ni mpenzi wake kwa sasa.

Queen Darlen amemtaka Harmonize kuacha kukata  tamaa katika kazi lakini amesmhauri kuwa inabidi apunguze kuwa na wanawake wengi na kutulia na mpenzi aliyenae kwa sasa amabe ni Sarah.

"Apunguze uhuni,atulie mtoto wa watu maskini ya Mungu mzungu yule  anampenda ila yeye mhuni mdogo wangu ,mhuni sana , mdogo wangu maisha ya uhuni sio mazuri anakuwa kama mfalme sulemani. aache hizo.

Hata hivyo kuna tetesi zimekuwa zikisambaa hivi karibuni kuhusu Harmonize kugombana na mpenzi wake huyo wa kizungu huku sababu kubwa ikiwa ni wivu wa mapenzi.

Dogo Janja, Uwoya Wakesha Kusaka Mtoto

$
0
0
Mwanamuziki wa Bongo fleva  Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na mke wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya wanatafuta mtoto.

Uwoya ambaye tayari ana mtoto mmoja Krish aliyezaa na marehemu Ndikumana Kataut amedai yuko katika jitihada za kumtafutia Krish mdogo wake.

Kwenye mahojiano  na Ijumaa Wikienda, kwa nyakati tofauti mastaa  hao walifunguka kuwa, kwa kipindi hiki cha mvua ndiyo muda sahihi wa kusaka mtoto hivyo wanalifanyia kazi suala hilo kwa nguvu zao zote.

"Tupo bize kidogo, tunasaka mtoto maana si unajua watu wanaangalia matunda ya ndoa kwa jicho la tatu hivyo sisi tunaangaika na hilo sasa hivi,” alisema Dogo Janja

Lakini pia Uwoya naye alifunguka na kusema ni haki yake kumpatia mtoto mume wake kama wanandoa lakini hasa hivi sasa anahitaji kumpa mdogo wake Krish kwani ameshakuwa mkubwa.

" Mke lazima amzalie mumewe na mimi na mume wangu sioni tunachosubiri kwa sasa maana Krish ni mkaka mkubwa na anahitaji mdogo wake“.

Irene Uwoya na Dogo janja walifunga ndoa mwaka jana mwishoni.

Wabunge CCM Waibana Serikali kupanda kwa bei ya mafuta ya Kula

$
0
0
Wabunge wa CCM, Juma Nkamia (Chemba) na Hussein Bashe (Nzega Mjini), wameibana Serikali wakitaka ishughulikie kupanda kwa bei ya mafuta na kuondoa kodi ya tende ili kuwapunguzia mzigo wa gharama waislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hayo yamejiri leo Mei 7, 2018 bungeni mjini  Dodoma, wakati Nkamia aliposimama kuomba mwongozo kuhusu  mafuta na Bashe kutaka kuahirishwa kwa shughuli za Bunge kwa dakika 30 ili kujadili suala la kodi ya tende ili iondolewe kama ilivyo kwa nchi jirani.

Nkamia alikuwa wa kwanza kuzungumza akisema, kubainisha kuwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuna taarifa za kuadimika kwa mafuta ya kula, “hali hii inasababisha  mafuta kupanda bei kwa haraka, Serikali inatoa kauli gani ili kuwaondolewa wananchi hofu.”

Kwa upande wake Bashe akitumia kanuni ya 69 ya kuahirisha shughuli za Bunge, amesema, “mwezi wa Ramadhani unakaribia na kama alivyosema Nkamia, bei ya mafuta imepanda, sukari imepanda, lakini nchi zinazotuzunguka zimefuta kodi za tende.”

Akijibu mwongozo huo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema tatizo lililojitokeza ni suala la kodi kwani kwa sasa Taifa lina hifadhi ya mafuta ghafi tani 40,000 na meli zilizopo nje zina tani 50,000.

“Jumla zilizoko nje na ndani  zina tani 90,000. Kinachoweka tatizo ni kodi kwa sheria tulizopitisha Tanzania, tunatoza kodi (meli kutoka nje ya nchi) asilimia 10 kwa mafuta ghafi,” amesema.

“Ila kwa vipimo vinaonyesha si mafuta ghafi ni mafuta masafi hivyo wanataka kutoza asilimia 25 na hapo ndipo kuna tatizo la hadi kufikia leo au kesho tutatoa majibu ya tulipofikia.”

Kuhusu hoja ya tende iliyoulizwa na Bashe, Waziri Mwijage amesema, “ni suala la kwenda kuzungumza na waziri wa fedha, tutalipeleka kuweza kumshawishi ili Bunge na nchi ichume thamani.”

Naye, Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amesema suala la mbegu za pamba kutumika kukamulia mafuta zilipatikana mwaka jana zaidi ya laki moja.

“Suala la mafuta yanayotokana na pamba, kwa uhakika hayakutarajia kuwa mengi, sasa Serikali inachokifanya inaagiza kutoka nje, niseme tu suala la mafuta linafahamika na Serikali inalifanyia kazi na haitapanda bei sana kama mbunge (Nkamia) alivyoonyesha wasiwasi,” amesema Tizeba.

Rais Magufuli Atembelea Chuo cha SUA Morogoro.....Wanafunzi Wafunguka na Kueleza Kero Zao

$
0
0
Wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) wametoa ya moyoni mbele ya Rais John Magufuli kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo chuoni hapo ikiwamo uhaba wa mabweni ya wanafunzi na fedha za mikopo.

Wametoa ya moyoni baada ya kiongozi huyo mkuu wa nchi kutoa nafasi kwa wanafunzi na watumishi wa chuo hicho kueleza mambo mbalimbali wanayokabiliana nayo baada ya kufanya ziara katika chuo hicho kilichopo mjini Morogoro.

Kabla ya Rais kutoa nafasi hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alieleza mafanikio na juhudi zinazoendelea kufanywa na wizara yake ikiwa ni pamoja na kufanikisha utoaji wa mikopo.

Hata hivyo, Emmanuel Gwalaje, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kozi ya wanyama amesema wapo wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo hawajalipwa fedha katika muhula wa kwanza na wanaishi maisha magumu hadi sasa.

Mhadhiri wa chuo hicho, God Swai amesema wanafunzi wanaporwa mitaani na kukabwa kutokana na uhaba wa majengo ya bweni, huku akiomba kujengwa kwa ofisi za wahadhiri chuoni hapo.

Mbali na maombi ya wanafunzi, pia kulikuwa na maombi ya watumishi, huku Amina Juma akiomba Rais Magufuli kuwafikiria watumishi wa darasa la saba waliofukuzwa kazi.

Amesema yeye ni mtumishi chuoni hapo tangu mwaka 1994, aliyeathirika na kuondolewa kwa watumishi wa darasa la saba, akiomba wafikiliwe upya kutokana na hali ngumu ya maisha mtaani.

Utendaji Kazi Chuo Kikuu SUA Wamfurahisha Rais Magufuli.....Awashangaa Wanaosema Elimu ya Tanzania Imeshuka

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema watu ambao wanasema elimu imeshuka nchini wanakosea kwani kuna sehemu ambazo elimu inaonekana ipo vizuri akitolea mfano wa chuo cha kilimo cha Sokoine University of Agriculture (SUA).

Magufuli amesema hayo leo Mei 7, 2018 akiwa katika ziara yake mkoani Morogoro na kusema kuwa watu wasiseme kwa ujumla kushuka kwa elimu ili hali kuna sehemu watu wanafanya vizuri katika elimu, na kudai kuwa wa SUA wameweza kufundisha mpaka Panya na akaelewa hivyo ni wazi kuwa wapo vizuri sana.

"Unajua hata watu ambao wanasema elimu imeshuka sijui kama wamefika hapa kwa sababu wangefika hapa na kumuona Panya anajua bomu liko wapi nadhani asingesema elimu imeshuka, wanamuona Panya amefundishwa mpaka akaelewa eti binadamu ndiyo asielewe, mjue walimu wa hapa wanafundisha mpaka Panya siyo binadamu tu, mpaka anaelewa akinusa hapa kuna kifua kikuu"

Rais Magufuli aliendelea kuzungumzia jambo hilo na kusema kuwa walimu wa SUA na wanafunzi wapo vizuri sana katika masuala ya shule ndiyo maana wanaweza kufanya gunduzi mbalimbali ambazo zinatija na msaada katika maisha ya kila siku.

"Wanafundisha Panya mpaka anatengeneza mapapai mpaka anafanya 'crossbreeding', anafanya papai lianze kuzaa likiwa na miezi mitano badala ya kusubiri miaka mitano halafu linazaa 'production' ya matunda mawili matatu, hizi kazi wamefanya hawa watu yaani hapa kuna vichwa tuache 'generalization' lakini pia lazima tuelewe elimu yetu imetoka wapi, palikuwa na elimu ya UPE aliiacha baba wa taifa kwa sababu hapakuwepo watu wa kwenda kufundisha"

"Nakumbuka baadae likaja suala la kupeleka walimu nafikiri ilikuwa enzi za Mwinyi au Mkapa mtu ukipata 'division zero' kidato cha nne au 'division four' unapelekwa ualimu hayo ndiyo matokeo, tulifanya hivyo kwa sababu ya hali halisi ya wakati huo, tumekuja kwenye awamu iliyopita mimi nimefukuza wanafunzi karibu elfu saba pale UDOM yaani 'four four' wanakwenda kuchukua 'Degree' walipelekwa kwenye awamu ya nne, kwa hiyo ukifuatilia unaweza kujua tumetoka wapi na tunaelekea wapi" alisisitiza Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli amekiri kuwa katika awamu yake ya tano wamekuja na elimu bure na kusema kuwa huenda baadae ikaja kuwa na madhara ila itasaidia kuondoa ujinga kwa watu wengi ambao walikuwa wakikosa elimu hiyo kwa sababu ya kukosa ada ya kulipa shule.

"Na sisi tumekuja tumeingiza elimu ya karo bure wanafunzi wameongezeka walioingia darasa la kwanza wameongezeka mara mbili zaidi wakawa milioni mbili kutoka milioni moja, hivyo inawezekana hii nayo ikaleta madhara baadaye, mtu mwingine angeweza kusema kwamba tungewaacha tu ili wakawe mambumbumbu waweze kutawalika vizuri kwa hiyo tukaaongeza idadi ya wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza"

Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini Mkapa miezi kadhaa iliyopita aliwahi kusikika akisema kuwa kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu elimu ya Tanzania kwa madai kuwa kuna unadhaifu mkubwa na kushukwa kwa kiwango cha elimu ya Tanzania.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images