Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mwakyembe Azidi Kumfagilia Diamond

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezidi kumfagilia staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kudai kuwa yupo Kwenye listi ya wasanii 10 duniani wenye Sauti nzuri.

Mwakyembe amesema hayo kwenye mahojiano yake na kipindi cha KAA HAPA cha Mrisho Mpoto na kueleza kuwa Diamond kwenye video zake hana haja ya kutumia picha za ajabu ajabu kwani sauti yake ni dhahabu inajiuza.

“Kwenye tasnia yetu ya sanaa  vijana wetu wanaimba  nyimbo nzuri sana, wana vipaji vya hali ya juu. 

"Kinacholeta matatizo hapa ni  picha ambazo haziendani na maadili yetu, kuchanganya na utupu ndani yake hivi vitu kwa kweli wafanye wengine lakini sio hapa. 

"Tuchukulie kijana kama Diamond sauti yeke pekee yake inatosha kabisa kumuuza. Ukisema wasanii 10 duniani tuwe wakweli tuu! wenye sauti nzuri, Diamond huwezi kumtoa pale. 

"Lakini huitaji kuuza ukaongeza na picha za ajabu ajabu wanaofanya hivyo ni wale wenye mapungufu ili kuficha ma’flat flat kwenye nyimbo zao, Diamond yeye haitaji kufanya hivyo”.

Suala hili limekuja baada ya serikali kuingilia kati kazi za wasanii mbali mbali na hata kufungia baadhi ya wasanii kama Roma Mkatoliki na baadae kumfungulia.

Waziri Mwakyembe amesisitiza kuwa serikali haina ugomvi wowote na wasanii bali wapo katika jitihada za kulinda maadili ya nchi yetu.

Nandy Ammwagia Sifa Alikiba

0
0
Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka THT Nandy amekiri kuwa pamoja na mambo mengine yote na maneno yakiwekwa pembeni staa wa Bongo fleva Ali Kiba amemu-insipire sana kwa kinywaji chake.

Nandy amekiri kuwa hatua aliyofikia Ali Kiba ya kuingiza kinywaji chake mtaani ambayo ni Energy drink ni hatua kubwa sana ambayo imempa changamoto hata yeye ya kufanya makubwa zaidi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na The Playlist ya Times, Nandy amekiri kuwa kupitia Kiba ni vizuri wasanii wengi wakajifunza kuwa ni vizuri kuwekeza nje ya muziki.

"Ameni-inspire kwa kinywaji kwa sababu ukiangalia the package ya kinywaji chake jinsi ilivyo ni project fulani ambayo ipo serious”.

Lakini pia Nandy ameongelea uwekezaji wa wasanii wengine kama Diamond Platnumz ambaye ni mmoja kati ya msanii Lakini pia mfanyabiashara.

"Tunaambiwa nje ya kuimba tunatakiwa tuwekeze nje ya muziki wetu na ndicho hiki kaka zetu wanafanya ukimuangalia kama Diamond, Alikiba ni vitu ambavyo wanatuhamasisha”.

Kwa hivi sasa Nandy anafanya vizuri sana ngoma yake ya Ninogeshe inayoshika namba moja kwenye mtandao wa Youtube.

Jamaa Aliyeiba Mahindi Yakang'ang'ania Kichwani Afikishwa Mahakamani

0
0
Mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam, Frank Joseph amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Mlandizi mkoani Pwani akishtakiwa kwa wizi wa mahindi.

Joseph ambaye tukio la kukamatwa kwake liliibua hisia na mijadala mitandaoni ikidaiwa alishindwa kutua mzigo aliodaiwa kuuiba, alisomewa shtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Nabwike Mbaba. 

Mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 124/2018 akidaiwa kuiba mahindi debe moja yenye thamani ya Sh20,000. Baada ya kusomewa shtaka, mshtakiwa huyo alikiri kutenda kosa.

Hakimu Nabwike aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 10 ili kupata maelezo ya mlalamikaji ambaye hakuwepo mahakamani.

Licha ya mahakama kumweleza mshtakiwa kuwa dhamana iko wazi na kumpa sharti la kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh500,000, alishindwa kutimiza sharti hilo hivyo alipelekwa rumande. 

Tangu Mei 3, Joseph alikuwa akishikiliwa na polisi mkoani Pwani akituhumiwa kuiba mahindi kwa mkazi wa Mlandizi.

Tukio la wizi huo lilivuta hisia kwa jamii baada ya mshtakiwa huyo kudaiwa kushindwa kutua mzigo uliokuwa begani hadi alipokimbilia polisi na mwenye mali kupigiwa simu, ambapo alifika na ‘kumsaidia’ kuutua.

Harmonize Amlipua Wolper na Kumuanikia Listi Nzima Ya Wapenzi Wake

0
0
Msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize ameingia Tena Kwenye vita ya maneno na Ex girlfriend wake staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper.

Tangu jana kumekuwa na  taarifa kwenye mitandao ya kijamii zilizomuonyesha Wolper akimrushia Dongo Sarah ambaye ni mpenzi wa Harmonize kwa kumuita Mlezi wa wana baada ya taarifa kusambaa kuwa kamtosa Harmonize na kumchukua Mwarabu Fighter.

Baada ya dongo hilo la Wolper, Harmonize alitokwa na povu zito kwani kwa Kupitia ukurasa wake wa Instagram alimtetea mpenzi wake Sarah na kusema yeye sio Mlezi wa wana ila Wolper ndo Mlezi wa Wana na kuambatanisha na listi kamili ya wanaume wote aliokuwa nao Kwenye Mahusiano

Spika wa Bunge aipa Serikali saa sita kutoa ufafanuzi kuadimika mafuta ya kula

0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameishukia Serikali kuhusu madai ya kupanda kwa bei ya mafuta ya kula akimtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kufikia leo Jumanne Mei 8, 2018 saa 11 jioni kuwasilisha bungeni taarifa ya kinachoendelea kuhusu jambo hilo ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo asubuhi bungeni mjini Dodoma wakati akijibu mwongozo wa mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe aliyehoji kuhusu bei ya mafuta, akidai imepanda na kujibiwa na Mwijage kuwa jambo hilo linashughulikiwa kwa maelezo kuwa kwa sasa umeibuka mvutano.

Tishio la kuadimika kwa mafuta ya kula linatokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuzizuia meli mbili zenye tani 62,000 za mafuta ya kula katika Bandari ya Dar es Salaam tangu mwezi uliopita kushusha mzigo mpaka wamiliki wake watakapolipa kodi husika.

Utata wa kulipa kodi inayodaiwa na TRA, unatokana na madai ya mamlaka hiyo inayosema mafuta yaliyoingizwa ni safi ilhali wamiliki wakieleza ni ghafi.

Leo katika majibu yake, Mwijage baada ya kutoa maelezo marefu amesema alitoa ushauri kwa TRA kwamba wenye mafuta, “nusu ya mzigo ushushwe, tatizo linalokuja tunahukumiwa na historia, nashauri hii kazi unipe mimi, nitakuja saa 11 kukueleza kipi kimetokea.”

Baada ya kauli hiyo ya Mwijage, Spika Ndugai alisimama na kusema: “Nalikubali hili la saa 11 na bahati nzuri nitakuwa hapa. Tunapokuwa bungeni lazima tuseme ukweli yaani iko hivyo.Tukiligeuza Bunge hili kuwa mahali pa kubangazia hivi, mimi niombe saa 11 tupate majibu ya uhakika.”

“Mnatufikisha mahali pagumu sana, kwa mambo madogo mno, hivi tuliosoma kemia hivi kupima mafuta kujua ni ghafi au masafi inachukua muda? Kitu cha dakika kumi na tano watu wanazunguka zunguka. Hamuwamini TBS (Shirika la Viwango Tanzania) au pelekeni Nairobi, Afrika Kusini, Kenya mnapima na kupiga kodi.”

Huku akishangiliwa Ndugai amesema, “…tunaumiza wananchi na hata yakikaa huko yakiingia anayeumia ni mwananchi, sisi tunalumbana tu.”

Awali, baada ya majibu ya  Mwijage, Ndugai alimtaka mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Suleiman Saddiq kulielezea suala hilo na kusema walipokutaka katika semina Jumamosi iliyopita, lilijitokeza ukiwamo mkanganyiko kati ya TBS, TRA na Mkemia Mkuu wa Serikali.

Baada ya Ndugai kueleza msimamo wake kuhusu jambo hilo, Mwijage alinyanyuka alipokuwa ameketi kwenda kuteta na waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama kisha kwa pamoja kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Mwalimu Atiwa Mbaroni kwa Kumtorosha Mwanafunzi wa Kike na Kuishi Naye

0
0
Mwalimu wa Sekondari ya Nyambureti wilayani Serengeti, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumtorosha mwanafunzi wa kidato cha pili kwa zaidi ya siku nne.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Juma Shija alikiri kushikiliwa kwa mwalimu huyo na kwamba alikamatwa Mei 2.

Hata hivyo, mwalimu huyo amekana kuwa na uhusiano na mwanafunzi huyo na kwamba hizo ni hila za baadhi ya watu kutaka kumharibia kazi.

Naye mkuu wa wilaya hiyo, Nurdin Babu alisema mtuhumiwa anadaiwa kumtorosha mwanafunzi huyo wakati wanatoka kwenye michezo ya Umiseta na kukaa naye kwa siku nne.

“Mwalimu hakuonekana kazini kwa siku nne na mwanafunzi halikadhalika, wazazi wakaanza kumtafuta na baada ya kuonekana na kubanwa mtoto alieleza alikuwa kwa mwalimu kwa kuwa ni mpenzi wake,” alisema Babu.

Babu alisema baada ya mtoto kutoboa siri wazazi walikusanyika wakitaka kumshambulia mwalimu huyo hali iliyoufanya uongozi wa wilaya kutuma polisi ili kumnusuru na kumkamata ili aweze kueleza kwa undani.

“Mtoto huyo anadai kuwa walianza uhusiano Oktoba 25, 2017 akiwa kidato cha kwanza na kuwa mke wake akienda masomoni yeye anaendelea naye, kitendo hiki hatuwezi kukivumilia lazima afikishwe mahakamani,” alisema.

Alisema wanaume wakware hawatavumiliwa kwa kuwa wanawaharibia watoto maisha yao.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwa mwaka jana zilikuwapo mimba zaidi ya 25 kwa shule za msingi na sekondari.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Juma Hamsini amemsimamisha kazi mwalimu huyo kutokana na tuhuma hizo za utovu wa nidhamu na kuitaka polisi kuhakikisha inamfikisha mahakmani.

Kenya kuzindua Setillaiti Yake Ijumaa Hii

0
0
Ijumaa Kenya inatarajiwa kuweka historia kwa kuwa na setilaiti ya kwanza kuwahi kutengenezwa nchini humo itayotumwa katika sayari.

Chombo hicho cha kuzunguka sayari kilitengenezwa na wanafunzi na watafiti wa Chuo Kikuu cha Nairobi kwa ushirikiano na shirika la teknolojia za sayari la Japan Space Agency (JAXA).

Naibu makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Peter Mbithi amesema mafanikio hayo ni dhihirisho ya hatua zilizopigwa nchini kuhusu utafiti wa kiteknolojia ambao unaweza kuchangia katika maendeleo yatakayokuza uchumi wa kitaifa.
 
Setilaiti hiyo yenye ukubwa wa sentimita kumi kimchemraba itarushwa kwenye sayari kutoka kituo kilichopo Japan, lakini Wakenya kadhaa watapewa nafasi kushuhudia matukio hayo katika Chuo Kikuu cha Nairobi na yatarushwa moja kwa moja.

“Kutakuwa na tukio Japan, katika sayari na hapa chuoni  kile kitakachofanyika Japan kitashuhudiwa na baadhi ya Wakenya ambao watakuwa huko. Hapa tutakuwa na hafla katika ukumbi ambako matukio yatarushwa  moja kwa moja. Tunasubiri siku hiyo kwa hamu,” amesema Profesa Mbithi.

Wale ambao wangependa kuhudhuria hafla hiyo katika ukumbi wa Chandaria uliopo chuoni hapo, watahitajika kutuma maombi kwenye tovuti ya chuo hicho na watafahamishwa kama wamebahatika kupata nafasi.

Profesa Mbithi ameongeza kuwa setilaiti hiyo itatumiwa kukusanya data kuhusu masuala mbalimbali muhimu kama mabadiliko ya hali ya anga, uhifadhi wa wanyamapori, utabiri wa hali ya hewa miongoni mwa mengine.

Ametoa wito kwa wadau wengine waungane nao ili kuimarisha zaidi utafiti kuhusu masuala ya sayari, kutia nguvu chombo hicho ili kifanikiwe kutimiza malengo yake.

Mkuu wa taasisi ya mafunzo ya uhandisi katika chuo hicho, Profesa Jackson Mbuthia amesema setilaiti hiyo yenye uzani wa kilo 14 itasafirishwa hadi kwenye sayari mwendo wa saa saba mchana Ijumaa.

“Huu ni mwanzo wa safari ambayo itawezesha Kenya kushiriki kwenye sayansi ya sayari. Ni mara yetu ya kwanza kupiga hatua hii lakini tunaamini ni muhimu katika ustawishaji wa sayansi nchini,” amesema.

Wolper Kajibu Mapigo...Kasema ya Wanaume wake Iliyotolewa na Harmonize ni Ndogo sana, Kamuonea

0
0
Mwanadada Wolper amemjibu  msanii wa muziki Harmonize kwa kumwambia kuwa anaona kama ameonewa kutokana na list hiyo aliyoitao yeye kuhusu idadi ya wanaume aliowahi kutembea nao na kusema kuwa mbona kama list hiyo ni ndogo sana.

Wolper anasema kuwa kuna baadhi ya watu Harmonize amewasahau na kwake anaona kama ameonewa kwa sababu hiyo sio idadi kamili ya wanaume aliyowahi kuwa nao kabla ya kwake yeye , lakini pia wolper amemjibu kuwa kuna baadhi ya wanaume ambao amewaweka kimakosa, kwaio kama anataka ni bora amfate mwenywe ili ampe aliowasahau na pia ampe majina ya ukweli.
 
"Mwanaume eeh mwanaume eeh hivi ule wimbo walioimba ni TMK,  Embu tushushe mistari kidogo,  ya ile nyimbo ya wanaume eeh #listndogosanaumenionea #alafukunawengineumekosea #njoodmnikupewaukweli #basiyulewanyumanikajuanimmasaikumbemzungu.


Wabunge Wamkaba Koo Mwijage....Ageuka Mbogo Bugeni

0
0
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Mh. Charlses John Mwijage, amekosa uvumilivu wa kujibu swali la Mbunge wa Mpendae, Salim Hassan Turky (CCM),  kuhusu kwa nini sukari kwa upande wa Tanzania bara imekuwa ikiuzwa bei ghali tofauti na ilivyo Zanzibar.

Akiwa katika maandalizi ya kujibu swali hilo Mh. Mwijage amesema kwamba sababu ya sukari Tanzania bara kuuzwa ghali sana ni kutokana na gharama za uzalishaji bara kuwa juu sana kuliko Zanzibar jibu ambalo lilizua kelele nyingi za Wabunge.

"Mh. Spika nimejitahidi sana kuelezea suala hili lakini muda hautoshi....... Gharama za uzalishaji sukari bara zipo juu kuliko Zanzibar. Nimepewa muda naomba muache niwaeleze....Hili suala siyo rahisi kama mnavyofikiria.... Ndiyo siyo suala rahisi naomba niwaeleze," Mwijage akifafanua huku wabunge wakizidi kupiga kelele.

"I am very good in talking, I can talk....... Mh. Turky ulipopewa kibali na serikali kuingiza sukari ni kwa nini wewe hukuuza rahisi?" Ameongeza Mwijage.

Awali katika swali lake Mh. Turky alitaka kujua kwa nini viwanda vya Tanzania Bara vimekuwa vikishindwa kushusha bei za sukari ilhali Viwanda vya Zanzibar vinauza sukar sh 65000.

Akitolea mfano soko la dunia amesema kwamba "Sukari inauzwa dola 390  ukilipia kodi 25% na VAT 18% sukari inasimama kwa bei ya sh 65000. Watanzania wanalanguliwa kwa kuuziwa sukari 110000 kwa misingi gani"?

Pamoja na hayo Mbunge huyo amesema kwamba "Tulishaomba Cost of Production (Gharama za uzalishaji) hapa bungeni  tangu Naibu Waziri akiwa Malima na hatujaweza kuletewa mpaka leo"

Serikali yafunguka kuhusu raia kupigwa na Polisi

0
0
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema hakuna utaratibu wowote unaoipa mamlaka Jeshi la Polisi kupiga raia au wageni kama baadhi ya askari wanavyowafanyia wananchi bali kuna utaratibu wa kisheria ambao unapaswa kufuatwa pindi raia au mgeni atakuwa amevunja sheria.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 08, 2018 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 24 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Ngara Alex Rafael Gashaza ambapo alitaka kusikia kauli ya serikali juu ya kulipa fidia juu ya wananchi wa Ngara na Tanzania kiujumla pindi wanapokamatwa na Polisi, kupigwa na kisha kuja kubainika kuwa hawana hatia.

"Sio utaratibu wa Jeshi la Polisi kupiga raia au hata wageni, kuna utaratibu ikiwa mgeni au raia amevunja sheria anatakiwa uchukuliwe kwa mujibu wa sheria, itabidi tukae tuchunguze kama kuna ukiukwaji wa sheria tuchukue hatua za kisheria ili sheria ifuate mkondo wake", amesema Mhandisi Masauni.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Masauni amesema pindi hali ya kifedha itaruhusu wanampango wa kukarabati kituo cha Polisi cha Ngara pamoja na nyumba za makazi za maaskari hao.

Spika Ndugai Amtuliza Mwijage....Amtaka Akajipange Upya Aje na Majibu Sahihi

0
0

Spika wa Bunge Job Ndugai amelazimika kuingilia kati mvutano ulioibuka bungeni kuhusu tofauti ya bei ya sukari kati ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa maelezo kuwa majibu yaliyotolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage juu ya jambo hilo hayajajitosheleza.

Kufuatia sakata hilo, Ndugai amesema swali hilo litaulizwa tena wiki ijayo ili Serikali itoe majibu ya kina, “hili ni swali la msingi sana na linapaswa kutolewa majibu mazuri na Serikali.”

Mvutano huo ulitokana na swali la mbunge wa Mpandae (CCM), Salim Hassan Turky aliyehoji tofauti ya bei hizo na kujibiwa na Mwijage, majibu ambayo mbunge huyo hakuridhika nayo.

Katika maelezo yake Mwijage amesema Tanzania Bara haina uhaba wa sukari na kuwatoa hofu watu mbalimbali.

Kuhusu tofauti ya bei kwa pande mbili za muungano, waziri huyo  amesema zaidi ya asilimia 53 ya sukari itumikayo Zanzibar huagizwa kutoka nje kwenye vyanzo ambavyo gharama zake ni nafuu ikilinganishwa na asilimia 29 ya sukari inayoagizwa nje  kwa upande wa bara.

Kufuatia majibu hayo Ndugai amesema swali hilo halikujibiwa vyema. Katika swali la msingi Jaku Hashim Ayoub (BLW) alihoji juu ya tofauti ya bei ya bidhaa hiyo katika pande hizo mbili za muungano na kubainisha kuwa gunia la kilo 50 visiwani Zanzibar linauzwa kwa Sh65,000 huku gunia hilo kwa upande wa Tanzania Bara likiuzwa kwa Sh120,000.

Katika majibu yake ya swali la msingi, Mwijage amesema wametoa maagizo kwa viwanda vinne vya kuzalisha sukari nchini kuongeza ulimaji wa miwa katika mashamba yake.

“Bei ya sukari ina maana kubwa kwa maisha ya Watanzania, haiingii akilini bei ya Tanzania Bara kuwa tofauti na ile ya Zanzibar.

"Kama ni kweli wananchi wa Tanzania bara wanalipa sukari mara mbili ya ya Zanznibar ili tu kulinda wenye viwanda....Haiwezekeni hiyo. Bunge linahitaji majibu ya uhakika. " Amesema Spika Ndugai

Bwege ataka Bombardier zipigwe bei ili Kumaliza Tatizo la Maji Nchini

0
0
Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Suleiman Bungara maarufu Bwege amependekeza kuuzwa kwa ndege mbili za Serikali aina ya Bombardier ili fedha zitakazopatikana zitumike kumaliza changamoto za upatikanaji wa maji nchini, kwa madai kuwa zimedumu kwa miaka 57.

Bwege ametoa kauli hiyo leo Mei 8, 2018 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji mwaka 2018/19.

Huku akizungumza kwa sauti ya kupanda na kushuka, Bwege amemuomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kusimamia upigaji kura wa wabunge, ili kubaini idadi ya wanaounga mkono ununuzi wa ndege hizo na wale wanaotaka fedha kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maji.

“Leo nakuona kama Spika kweli kweli, upo strong (imara) hongera sana,” amesema na kuwataka wabunge kutoshusha lawama kwa waziri wa wizara hiyo, mhandisi Isaack Kamwelwe na Katibu Mkuu wa wizara, Profesa Kitila Mkumbo kwa madai kuwa bila fedha, hawawezi kufanya lolote.

“Serikali inatakiwa kutoa fedha za maendeleo maana mnachokisema si mnachokitenda. Leo mwananchi umuulize ndege na maji nini kizuri, nyinyi wabunge kama kweli tuwaulizeni kununua ndege na kuwapa watu maji bora nini?”

Huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge amesema, “wanaosema inunuliwe ndege na wanaosema tuanze maji wasimame, mkirudi mwaka 2020 (baada ya uchaguzi mkuu) mimi sio Bwege. Mheshimiwa Spika uulize, wanaosema ndege na maji halafu tukawaonyeshe huko, mheshimiwa Spika utaruhusu kweli?  Wabunge tuwaheshimu  mawaziri, sisemi Magufuli mzigo, nasema Serikali ya CCM mzigo.”

Amesema katika jimbo lake amekuwa akiomba mara kwa mara hospitali ya wilaya ipelekewe maji, kwamba akihoji maji anajibiwa ndege kwanza.

“Miaka 57 ya CCM tunaongelea maji? Serikali ya CCM amkeni kama hakuna maji, kama hatupati maji Serikali ya CCM bai bai, maji ni uhai na masheikh wako magereza hakuna maji.”

Amesema kutokana na uhaba huo wa maji ni vyema zikauzwa ndege mbili ili kutatua tatizo la maji, “mheshimiwa Spika kwa kuwa uko vizuri, piga kura anayetaka ndege au maji.”

Mara baada ya kumaliza kuchangia, Spika Ndugai amesema, “hata tukiwalaumu Waziri na Katibu Mkuu tunawaonea. Tukiacha mfuko wa maji, Serikali imetoa asilimia 11, lakini kesho waziri wa fedha, akisimama hapa watueleze. Hivi kama wewe ungekuwa waziri ukisimama hapa utasema nini.”

Kiongozi mbio za mwenge Agoma Kuzindua Mradi wa Milioni 500

0
0
Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Charles Kabeho amegoma kuzindua mradi wa ujenzi wa nyumba tano za watumishi wa halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kwa madai kuwa thamani ya fedha za ujenzi zilizotumika haziendani na nyumba hizo.

Mbali na kukataa kuzindua nyumba hizo zenye thamani ya Sh511milioni, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mradi huo akibainisha kuwa kuna matumizi mabaya ya fedha za umma.

Tukio hilo limetokea leo Jumanne Mei 8, 2018 baada ya kiongozi huyo kutembelea mradi huo wakati mwenge wa Uhuru ukikimbizwa wilayani Kalambo mkoani hapa.

Kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi huo uliyotolewa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kalambo, Simon Kagani alieleza kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa Julai 2016 na kukamilika Aprili 2017 na kugharimu kiasi hicho cha fedha, ambapo Serikali Kuu imechangia Sh496milioni, halmashauri Sh15milioni.

“Siwezi kuzindua mradi huu kwa kuwa nimebaini thamani ya fedha haifanani na nyumba zilizojengwa. Milioni 500 kwa nyumba tano, ina maana kila nyumba ni Sh100milioni, sasa ndugu zangu kuna nyumba ya Sh100milioni hapa?” Amehoji.

Licha ya mkuu wa wilaya hiyo, Julieth Binyura na mwenyekiti wa halmashauri ya Kalambo, Daudi Sichone kutoa ufafanuzi wa ujenzi huo, hawakuweza kumshawishi kiongozi huyo wa mbio za mwenge.

Sugu Kuwasha Moto Baada ya Kutoka Gerezani

0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi “Sugu'' amefunguka na kusema kuwa atawasha moto katika jiji la Mbeya Mjini pindi atakapotoka kutumikia kifungo chake cha miezi mitano jela ambapo sasa kinakwenda ukingoni.

Sugu amesema hayo kupitia kwa Mwenyekiti wa baraza la vijana la Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (BAVICHA) Taifa Patrick Ole Sosopi ambaye mwisho wa wiki iliyopita alipata fursa ya kumtembelea katika gereza la Rwanda.

"Siyo siri ni kwamba tunaamini mwezi huu watatoka wote ila Sugu anasema atawasha moto Mbeya, na kuwatumikia wananchi na kukutumikia chama mahali popote ambako chama kitamfanya aweze kwenda kwa kuwa yeye ni mjumbe wa kamati kuu, hivyo yapo mambo mengi naamini akitoka atayaeleza mwenyewe kwa undani zaidi, pia Masonga ameahidi akitoka atawaeleza wananchi ni jinsi ambavyo tunapaswa kupigania haki zetu na kuwa hatupaswi kuwa waoga nali tunapaswa kufanya harakati kwa njia nzuri na salama na kugusa maisha ya watanzania ambao tunawaongoza na kuwatetea" alisema Sosopi

Mbali na hilo Sosopi alieleza kuwa viongozi hao wametoa shukrani kubwa kwa watanzania pamoja na wanachama wa CHADEMA kwa jinsi ambavyo walikuwa wanakwenda kuwapa faraja kwa kuwaona magereza.

Hata hivyo Sosopi amedai kuwa viongozi hao mwezi huu wanaweza kutoka japo hajasema itakuwa lini na kusema kuwa watu wa magereza wao ndiyo wanajua siku gani na tarehe gani viongozi hao watatoka ndani ya mwezi huu.

"Tuwe na subira siyo kwamba ni siri lakini tuwe na subiri tunatambua kwamba viongozi wetu hawa wamebakisha muda mchache sana watatoka... ni lini nafikiri hatupo tayari kueleza hilo kwani ni mapema zaidi ila tutawaeleza tu tutakapokuwa tunaona kuna sababu ya kuwaeleza ni lini watatoka lakni tunaamini ndani ya mwezi huu watatoka kwa sababu ni wakati muafaka, kama unavyojua sisi si wasemaji wa Magereza kwamba tunajua wanatoka lini, ila tunachojua watatoka ndani ya mwezi huu" alisisitiza Sosopi

Februari 26, 2018 Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi kwa jina maarufu Sugu na mwenzake Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga walihukumiwa kwenda jela kwa miezi mitano kwa kosa la kumkashfu Rais John Pombe Magufuli.

Serikali yamtaka Nape kuandika barua ya maelezo

0
0
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imemtaka Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Nnauye kuandika barua ya maelezo ya matatizo ya jimbo lake kuhusiana na kufungwa kwa vituo vya afya kama ilivyoagizwa hapo awali ili tatizo hilo lisiweze kujirudia.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 08, 2018 na Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Josephat Kandege Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 24 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza la Mbunge Nape Nnauye ambaye aliyeuliza serikali ni kwanini isichukue hatua za dharula kwa zahanati zilizofungwa katika maeneo yote jimboni mwake.

"Tukiwa hapa Bungeni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika alitoa taarifa kwamba kama yupo Mbunge yeyote na wa eneo lolote ambalo tunalazimika kufunga Zahanati au Kituo cha Afya kutokana na ukosefu wa watoa huduma aandika barua na kumpelekea Mkuchika ili tatizo hilo lisiwe kutokea. Naomba kama Mhe. Nape hakuwepo siku hiyo basi atumie fursa hiyo ili hicho anachokisema kisiweze kutokea", amesema Kandege.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri Josephat Kandege amempongeza Mbunge Nape Nnauye kwa jimbo lake kwa kuweza kujengwa vituo vingi vinavyotoa huduma za afya.

Waziri Amkingia Kifua Rais Sakata la Wanafunzi Kupata Mimba

0
0
Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha amemkingia kifua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hakuwahi kukataza waanafunzi waliopata mimba kuzuiwa kuendelea na masomo na badala yake ni kusisitiza kilichoamuliwa tangu 2002.

Ole Nasha amelazimika kufanya jambo hilo leo bungeni wakati alipokuwa akimjibu mbunge wa Suzan  Lymo ambaye alikuwa akitaka majibu ya namna serikali ilivyojipanga kuhusu zile sababu zilizo nje ya uwezo wa wanafunzi kuhimili kubeba mimba zinapatiwa ufumbuzi ikiwa tayari kuna tamko la kuzuia wanafunzi wasiendelee na shule lililotolewa na Rais Magufuli 2017.

Akijibu swali hilo Mh. Ole Nasha amesema kwamba Serikali imefanya marekebisho ya sheria ya elimu sura 363 ambapo imeongeza kipengele cha mtu yoyote ambaye atamuweka ujauzito mwanafunzi atafungwa miaka 30.

Mh. Nasha amesisitiza kuwa "Naomba nimsahihishe Mh. Lymo kwamba katazo lilikuwepo tangu 2012. Rais hajakataza wanafunzi waliopata ujauzito kutokuendelea na masomo. Alichokifanya ni kusisitiza kitu ambacho kilishaamuliwa siku nyingi." - Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha.

Aidha ameongeza kwamba "Serikali imeamua kuchukua uamuzi wa kuwazuia wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni kuendelea na masomo, kwa lengo la kuwalinda, kwani wanaporejea shuleni hunyanyapaliwa na wenzao jambo ambalo huwaathiri kisaikolojia".

"Tunataka kuweka wazi kwamba, hatutegemei wanafunzi wetu katika umri mdogo waendelee kufanya mapenzi wakiwa mashuleni, kwa sababu inawaathiri katika masomo yao. Tumeamua kuchagua hatutaki kuchanganya mapenzi na elimu katika umri huo mdogo." ameongeza

Serikali yaahirisha majibu kuhusu mafuta ya kula Hadi Kesho Jioni

0
0
Licha ya Spika wa Bunge Job Ndugai kuitaka Serikali leo jioni Mei 8, 2018 kutoa majibu kuhusu hali ya upatikanaji wa mafuta ya kula nchini, imesema itatoa maelezo hayo kesho jioni.

Kufuatia hali hiyo Ndugai amesema, “Kesho saa 11 jioni Serikali ikiwa haitakuwa na majibu katika hili nitalifunga kiaina na kuwaacha wananchi.”

Ndugai ametoa kauli hiyo leo jioni baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama kusimama na kutoa kauli ya Serikali kuhusu suala hilo, akiomba jambo hilo kujibiwa kesho.

“Hivi sasa ni saa 12 jioni na kikao cha kupokea matokeo ya uchunguzi wa kisayansi kutoka taasisi husika kinaendelea na kinaongozwa na Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa),” amesema.

“Baada ya kikao hicho kukamilika, ninaomba Bunge lako liridhie taarifa ya Serikali itolewe kesho jioni ili iwe taarifa kamilifu ya kutoa mwelekeo ya kutatua tatizo hilo.”

Asubuhi Ndugai alitaka majibu kuhusu madai ya kuadimika kwa mafuta yatolewe leo jioni baada ya majibu ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhusu suala hilo kutoridhisha.

Tishio la kuadimika kwa mafuta ya kula linatokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuzizuia meli mbili zenye tani 62,000 za mafuta ya kula katika Bandari ya Dar es Salaam tangu mwezi uliopita kushusha mzigo mpaka wamiliki wake watakapolipa kodi husika.

Utata wa kulipa kodi inayodaiwa na TRA, unatokana na madai ya mamlaka hiyo inayosema mafuta yaliyoingizwa ni safi ilhali wamiliki wakieleza ni ghafi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 9

Maagizo aliyoyatoa Waziri Jafo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza feri

0
0
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewapa siku 45 watendaji wa soko la kimataifa la feri kuhakikisha wanarekebisha miundombinu mibovu ambayo imekuwa kero kubwa kwa wafanyabiashara wa maeneo hayo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana na kuona shimo kubwa katika eneo hilo ambalo kwa tathmini ya mafundi wamesema inatakiwa shilingi milioni 36 ili kulikarabati huku makusanyo ya ushuru ya soko hilo yakiwa zaidi ya shilingi milioni 90 kwa mwezi hali iliyompelekea kuwaambia watendaji hao wajitathimini kama wanatosha kuongoza

"Hapa kuna uzembe uliopitiliza na ukiona uzembe kama huu katika vitu ambavyo vya msingi vinavyohusu maisha ya watu, milioni 36 kwa shimo miaka miwili na nusu halijazibwa huu ni uzembe na hii inaonesha hata katika makusanyo yenu ya mapato kuna wizi mkubwa, huwezi kuniambia mmeshindwa kuziba shimo kama hili kwa milioni 36", alisema Jafo.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko hilo wamelalamikia huduma mbovu zilizopo katika soko hilo.

Serikali Yawahamasiha Wananchi kuwekeza Katika Viwanda vya Kusindika Mazao

0
0
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Serikali  imewataka wananchi kushiriki kikamilifu uanzishwaji wa viwanda vidogo vya kusindika vitunguu Saumu  na Mazao mengine ya Biashara katika maeneo yote hapa nchini.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Martha Umbulla, Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa mazao ya Pareto na Vitunguu saumu yanayolimwa katika Wilaya ya Mbulu na maeneo mengine yana thamani kubwa na yanaweza kuchochea na kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya kusindika mazao hayo.

“ Kwa kutambua faida zitokanazo na zao la pareto, Serikali iliamua kuanzisha Bodi ya Pareto kwa lengo la kudhibiti uzalishaji, usindikaji wa biashara ya pareto hapa nchini” Alisisitiza Mhe. Mwijage

Akifafanua amesema kuwa Serikali itaendeleza juhudi za kuhamasisha uwekezaji kwenye viwanda vya kuengua na kuchuja pareto ili kuongeza thamani ya zao hili na kuwanufaisha wananchi katika maeneo yanayolima pareto ikiwemo Wilaya ya Mbulu.

Kwa upande wa zao la Vitunguu saumu Wizara ya Viwanda kupitia karakana za SIDO katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro zinatengeneza  “Blender” ambayo itatumika kusaga zao hili kuwa katika mfumo laini ‘’ Garlic Paste” teknolojia hiyo inapatikana kwa gharama ya shilingi milioni moja na laki nane.

Aidha, SIDO imekuwa ikitoa mafunzo kwa vikundi na watu binafsi juu ya usindikaji wa zao la vitunguu saumu katika mikoa inayolima zao hilo.

Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imekuwa ikihamasisha na imefanikiwa katika kuvutia wawekezaji na wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda hapa nchini.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images