Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli : "Usikubali kubomoa nyumba yako Bila Kufidiwa"

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wananchi wa Tanzania kiujumla kutovunja nyumba zao zilizoweka alama X yenye rangi ya kijani bila ya kupatiwa fedha zao za fidia kama inavyopaswa kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Mei 05, 2018 wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Mangula Mkoani Morogoro pindi waliposimamisha msafara wake na kutoa kero zao mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao

"Barabara hii tutaipanua, ila nashukuru Mungu nyumba nyingi hazipo kando kando ya barabara lakini nataka niwatolee ufafanuzi. Kwa mujibu wa sheria upande wa barabara ni mita 22.5 kila upande, mwaka 2007 pakafanywa mabadiliko kwenye barabara kuu na zile za mikoa kufikia mita 30, mabadiliko ya sheria hayo yalipokuwa yakiwekwa kuna baadhi ya nyumba zilikuwa zipo nje ya mita 22.5 kwa hiyo sheria ikawa imewakuta", amesema Rais Magufuli na kuongeza;

"Kuna nyumba zimewekwa alama ya X ya kijani, msibomee. Nyumba yako yenye X ya kijani hutakiwi kubomoa, siku utakayobomoa lazima uwe umepewa hela. Nataka muwaelimishe watanzania wote kuwa ukikuta nyumba yako au ukuta wako umewekwa alama ya X ya kijani na kijani wote mnaifahamu kama kuna mtu hajui rangi ya kijani aende angalie hata nguo za kijani za CCM".

Pamoja na hayo, Rais Magufuli ameendelea kwa kusema "Ukikuta X ya kijani maana yake wewe huna kosa ila hutakiwi kujenga nyumba nyingine katika eneo hilo na ukijenga nyumba nyingine utakuwa umefanya kosa kwasababu sheria imeshapitishwa tangu mwaka 2007. Lakini nyumba yako kama ilikuwepo na ikapigwa X maana yake barabara ikitaka kuja huko lazima ikupe mchuzi".

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amesema atasimama pamoja na wananchi wa watanzania katika kuwapambania masuala ya maendeleo.

Waziri Mkuu Ainyooshea Kidole TRA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuacha kutumia lugha chafu na nguvu katika ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara.

Pia amemwagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kukutana na uongozi wa mamlaka hiyo ili kuieleza umuhimu wa kuzingatia maadili na weledi katika ukusanyaji wa kodi.

Majaliwa ametoa maagizo hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu mbinu zinazotumiwa na TRA kukusanya kodi kwa kuwatoza kodi kubwa isivyo halali wafanyabiasha na wengine kupoteza maisha kwa mshtuko.

Mwakajoka alisema licha ya serikali kutekeleza sera ya viwanda, TRA inatumia mbinu za ovyo kukusanya kodi hali inayowalazimisha baadhi ya wafanyabiashara kuhamishia biashara zao nje ya nchi.

Akijibu swali hilo, Majaliwa alisema aliwahi kutoa maelekezo kwa TRA kutotumia nguvu na kubambikia kodi kubwa na kwamba iwapo wafanyabiashara watakuwa wana malalamiko, inabidi wayafikishe kwenye chombo cha kusikiliza malalamiko kilichopo ndani ya TRA.

“Lakini pia kama inapoonekana ndani ya TRA husikilizwi wizara ya fedha ipo na ndio yenye mamlaka na TRA yenyewe, wafanyabiashara pia wana uhuru mkubwa wa kwenda kwa kiongozi  mkuu wa eneo mkuu wa mkoa kwenye hilo ngazi mkoa au mkuu wa wilaya ngazi ya wilaya ili kulalamikia jamnbo hili na hatimaye mkuu wa mkoa unachukua hatua kujua kwanini kumejitokeza katika jambo hili.

“TRA fanyeni kazi yenu kwa weledi, endeleeni kuwa na mazungumzo na wafanyabiashara na sasa tunaona kila mmoja anaona umuhimu wa kulipa kodi,” amesema Waziri Mkuu.

Mkuchika: Taarifa Za Wastaafu Zihakikiwe Kabla Hawajastaafu

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, amewataka maofisa utumishi wa umma nchini, kuhakikisha wanahakiki taarifa za watumishi wanaotarajia kustaafu miezi sita kabla ya muda wa kustaafu.

Mkuchika amesema hayo jana Mei 5, jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua programu za shahada za utunzaji kumbukumbu na nyaraka pamoja na uhazili katika Chuo cha Taifa cha Utumishi wa Umma.

Alisema wastaafu wamekuwa wakitumia muda mwingi kufuatilia mafao yao baada ya kustaafu kutokana na uzembe wa maofisa utumishi katika halmashauri mbalimbali na baadaye kuwataka wastaafu hao kufuatilia taarifa hizo wenyewe.

“Sasa anamwachia yule mtumishi kuhangaika kwa hiyo unakuta mtumishi ametoka Mtwara, Mwanza anakuja kufuatilia mafao yake wakati ni kazi ambayo anatakiwa aifanye Ofisa Utumishi.

“Utakuta mtumishi mwingine baada ya miaka miwili au mitatu anakufa bado hajalipwa mafao yake kwa sababu karatasi fulani imekosekana,” alisema Waziri Mkuchika.

Daraja la Mto Kilombero labatizwa jina Daraja la Magufuli

$
0
0
Rais John Magufuli amezindua daraja la mto Kilombero ambalo kwa sasa linaitwa daraja la Magufuli.

Akitangaza jina la daraja hilo leo Mei 5 wakati Rais akizindua, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema ametoa jina hilo kutokana na juhudi alizozifanya Rais Magufuli wakati akiwa waziri wa ujenzi.

"Mheshimiwa Rais kwa mamlaka niliyopewa natangaza rasmi daraja hili litaitwa Magufuli, hii ni kutokana na juhudi kubwa uliyoiweka katika kufanikisha ujenzi wa daraja hili," amesema.

Daraja hilo lenye urefu wa zaidi ya mita 300 linaunganisha wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero.

Kambi ya Upinzani waitaka Serikali kuwasikiliza marais wastaafu JK na Mkapa

$
0
0
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wameitaka Serikali kutilia mkazo ushauri uliotolewa na marais wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wa kuwapo kwa mjadala wa kitaifa wa elimu.

Wakizungumza leo Mei 5, 2018 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, wabunge wa upinzani wamesema hali ya elimu ni mbaya na Serikali inaandaa kizazi kijacho kisichoweza kushindana katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema, “Taifa lolote lile ambalo halijui umuhimu au halipendi kuwekeza katika elimu ni Taifa mfu, ukitaka kuua elimu yetu basi usiwekeze katika elimu.”

Mbatia ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa amesema, Taifa hili limebahatika kuwa na marais walimu isipokuwa Mzee Mkapa, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ni Mwalimu, ‘First Lady’ Janeth Magufuli ni mwalimu.

“Leo Tanzania tupo wapi? Na rasilimali kubwa kuliko zote duniani ni rasilimali watu na rasilimali watu tuliyonayo sasa haijitambui na ili ilijitambue lazima iwe na ufahamu.

“Kama Rais Mkapa anaomba mjadala wa elimu na amekuwa akilirudia mara kwa mara. Rais Kikwete amezungumza haya. Rais Mwinyi amesema nchi inaongozwa kama gari bovu. Mwalimu Nyerere alilisema hadi anaingia kaburini,” amesema Mbatia na kuongeza:

“Tuwe na mjadala mpana wa kitaifa, Tanzania ni yetu sote, watoto hawa wanaumia, hivi ukweli watoto wa rais wetu wanasoma katika shule hizi hizi, hebu tumwogope Mwenyezi Mungu.”

Mbatia amesema vitabu vinavyosambazwa sasa shule za msingi ni vibovu na kumtaka Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako kuacha kutoa vitisho kwa watu kuwa watachukuliwa hatua na badala yake, “ajiulize tatizo lipo wapi, nani kalisababisha.”

Naye Waziri kivuli wa elimu, sayansi na teknolojia, Susan Lyimo amesema; “Hakuna nchi yoyote iliyoendelea pasina kuwekeza katika elimu, lakini kinachofanyika sasa, ingawa Serikali haitaki kusikia ila hali ya elimu ni mbaya.”

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya May 6

Serikali Kutumia Bilioni 131.47 Kutekeleleza Miradi Ya Kimkakati

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM,  Dodoma
 Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, Serikali imezindua Mkakati wa kuziwezesha Mamlaka za Serikali za     Mitaa kutekeleza miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea.

 Mkakati huo umezinduliwa Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ambapo amesema kiasi cha shilingi bilioni 131.47 kitatumika kutoa ruzuku ya utekelezaji wa miradi 22 kwa halmashari 17 zilizoko katika mikoa 10 nchini, katika mwaka wa fedha 2018/19.

 Ameitaja mikoa hiyo ambayo Halmashauri zake zimekidhi vigezo vya kunufaika na miradi ya kimkakati katika awamu ya kwanza ya mpango huo kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Morogoro, Mtwara, Pwani, Simiyu na Songwe.

 Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa Halmashuri zinajenga uwezo wa kujitegemea kwa takribani asilimia 80 hadi 100 ifikapo mwaka 2025, badala ya hali ya sasa ambapo halmashauri hizo zinategemea ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa zaidi ya asilimia 88.

Amezitaka halmashuri zitakazopata fedha za miradi hiyo kuhakikisha fedha hizo zinawekezwa kwenye miradi yenye tija, inayokuza ajira kwa wananchi na kuongeza mapato ya halmashauri.

Ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Halmashauri kubuni miradi ya kibiashara kwa ajili ya wananchi wanaowaongoza kwa kutengeneza ajira kwa kutumia rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Alionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watendaji wanaosimamia miradi hiyo ikiwa watatumia fedha hizo kwa malengo tofauti na yaliyokusudiwa na kurejea kauli ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwamba kufuja fedha za Serikali katika kipindi hiki ni sawa na kunywa sumu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, amesema kuwa Serikali inazo fedha za kutosha kufanikisha mkakati huo na kutoa wito kwa viongozi wa Mikoa husika kuchangamkia fursa hiyo kwa kuanisha miradi yenye tija ili ipatiwe fedha.

Alifafanua kuwa tayari Serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 15 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati katika mkoa wa Dar es Salaam katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kwa kujenga Kituo cha Mabasi cha Mbezi Luis, Ujenzi wa Soko la Mburahati katika Manispaa ya Ubungo, Ujenzi wa Soko la Kisasa la Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni na Ujenzi wa Soko la Kisasa la Kisutu, Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa ya Vingunguti katika Manispaa ya Ilala.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- TAMISEMI Selemani Jaffo (Mb) amesema kuwa Ofisi yake itaanza kufuatilia na kupima utendaji kazi wa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini ili kuona kama wanaendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Aliwapongeza Wakurugenzi walioonesha mfano katika kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa kubuni miradi yenye tija na ya kimkakati iliyopewa Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango na kuwataka watendaji wengine waige mfano huo.

Baadhi ya miradi itakaotekelezwa na Halmashauri zilizokidhi vigezo ni pamoja na Ujenzi wa Masoko ya Kisasa, Ujenzi wa Maegesho ya Malori, Ujenzi wa stendi za kisasa, Maghala ya kuhifadhi mazao, Masoko ya Kisasa, Machinjio na Ujenzi wa Viwanda.

Rapa Stamina na mchumba wake wafunga ndoa

$
0
0
Hatimaye rapa Stamina amefunga ndoa  na mchumba wake wa muda mrefu ajulikanaye kwa jina la Veronica jana Mei 05, 2018 mjini Morogoro katika kanisa la Mtakatifu Consolata lilipo maeneo ya SUA mjini humo.

Kwenye harusi hiyo, Wasimamizi walikuwa ni swahiba wake Roma Mkatoliki na Mkewe Nancy .

Mwaka jana rapa Stamina alimvisha pete ya uchumba mchumba wake huyo.

Tazama baadhi ya picha hapa chini za tukio hilo.

Wananchi Wamkataa mganga wa zahanati wakimtuhumu kuiba dawa.

$
0
0
Zahanati ya Kijiji cha Izinga, Kata ya Wampembe wilayani Nkasi mkoani Rukwa, imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wakazi wa kijiji hicho kumkataa mganga wa zahanati hiyo wakimtuhumu kuiba dawa.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, George Fataki alisema wananchi hao wamefikia uamuzi huo baada ya kukamata dawa zikiuzwa katika duka la dawa za binadamu kijijini hapo.

Alisema baada ya wananchi hao kumhoji mmiliki wa duka hilo alieleza kuwa dawa hizo aliuziwa na mganga huyo (jina tunalihifadhi).

Fataki alisema baada ya wananchi hao kupata taarifa hizo walimfuata mganga huyo na walipomhoji alikiri kumuuzia dawa mfanyabiashara huyo baada ya kuona zimekaa muda mrefu bila kutumika na muda wake wa kufikia mwisho wa matumizi ukikaribia.

Alisema Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Hashim Mvogogo alifika kijijini hapo kwa ajili ya shughuli za kikazi na kukuta mgogoro huo.

Kwa mujibu wa Fataki, kaimu mganga huyo alizungumza na wananchi ili wamuache mganga huyo aendelee kutoa huduma katika zahanati hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Misana Kwangula alikiri kuwapo kwa tukio la kufungwa kwa zahanati hiyo na kuongeza kuwa tayari muuguzi huyo alikwisha fikishwa katika mikono ya sheria.

Zari azidi kuumizwa na kifo cha aliyekuwa mume wake, Ivan

$
0
0
Aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady ameonyesha ni kiasi gani anamkumbuka aliyekuwa mume wake, Ivan Ssemwanga ‘Ivan Don’ ambaye ni Marehemu kwa sasa.

Zari ameshare picha ya zamani katika mtandao wa Instagram ikimuonyesha Don akiwa na mwanaye, Pinto ambaye ni mkubwa kwa sasa na kuandika;

"Ni vigumu kuamia ni takribani mwaka mmoja sasa tangu Mungu alipokuita, naona ni kama jana. Hakuna siku inayopita bila kukuombea pamoja na mama yako. Roho zenu ziendelee kupumzika kwa amani.Hakika sisi huja kutoka mbali. Hapa Don anaonekana amembeba Pinto (ambaye ni mkubwa sasa), alianza naye kutoka mbali."

"Can’t believe its almost a year since God called you, it seems like yesterday. No day passes that i don’t pray for you and mom. May your souls continue resting in peace.
We surely come from far. Here Don is seen carrying Pinto ( who is a giant now), started from the botton right? Your missed🌹#RandomPost"

Ivan alifariki May 25, 2017, alijipatia umaarufu mkubwa tangu nchini mwake Uganda hadi Afrika Kusini ambako ameacha utajiri mkubwa uliomfanya kuwa mmoja ya watu matajiri nchini humo kabla ya kufikwa na mauti.

Mtahiniwa Kidato cha Sita Ajinyonga

$
0
0
Siku moja kabla ya kuanza mitihani ya kidato cha sita, mtahiniwa wa Shule ya Sekondari Nyakato, Robert Masaba (21) amekufa ikidaiwa kuwa amejinyonga.

Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) watahiniwa 87,643 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita utakaoanza kesho Mei 7, 2018 hadi Mei 25, 2018.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinadai Masaba amejinyonga usiku wa kuamkia leo Mei 6, 2018 kwenye mwembe akiwa Shule ya Sekondari Kahororo.

Masaba na wenzake walihamishiwa shuleni Kahororo zaidi ya mwaka mmoja uliopita baada ya sekondari ya Nyakato kuathiriwa na tetemeko la ardhi.

Mkuu wa Shule ya Kahororo, Omary Rugambaki amezungumzia tukio hilo akisema polisi wameshafika kwa uchunguzi.

Kidato cha 6 Kuanza Mtihani wa Taifa Kesho

$
0
0
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema watahiniwa 87,643 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita utakaoanza kesho Mei 7, 2018.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema leo Mei 6, 2018 kuwa mtihani utahitimishwa Mei 25, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema kati yao watahiniwa hao, wa shule ni 77,222 na wa kujitegemea ni 10,421.

Dk Msonde amesema mtihani utafanyika sambamba na wa kozi ya ualimu ambao watahiniwa 7,422 wa ngazi ya cheti na stashahada wamesajiliwa kuufanya.

"Maandalizi kwa ajili ya mitihani ya kidato cha sita na ualimu yamekamilika, ikiwamo kusambaza vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mitihani hii," amesema Dk Msonde.

Rais Magufuli: RC atakayeniomba chakula, atakuwa anaomba kufukuzwa kazi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema Mkuu wa mkoa yoyote atakaye omba chakula kwake atakuwa ameomba kufukuzwa kazi.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana, Mey 5, 2018 kwenye ufunguzi wa daraja la Kilombero, ambapo alisema kuwa haiwezekani mvua inyeshe halafu watu wakose chakula.

“Mkuu wa Mkoa atakayeniomba chakula, atakuwa anaomba kufukuzwa kazi, kwa sababu haiwezekani mvua inyeshe hivi, halafu wakose chakula,” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema kuwa “maandiko yanasema asie fanya kazi na asile na asipo kula afe, hakuna chakula cha bure.”

Wema Sepetu baada ya Heaven Sent, ‘kuna project za kutikisa mji’

$
0
0
Baada ya muigizaji Wema Sepetu kuachia filamu yake ya Heaven Sent, 2017 na kushinda tuzo, amefunguka kipi kinafuata kutoka kwake.

Mrembo huyo amesema kwa kushirikiana na timu yake kuna movie wanaandaa ambayo itakuja kubadili tasnia nzima, pia kuna event nyingine kubwa atafanya June mwaka huu.

“Heaven Sent imekuja imeshinda tuzo, so it good thing, tutegemee vitu vikubwa kama nilivyosema hapo awali kuna kitu kitatokea June kwa hiyo tukae mkao wa kula kitu kizuri kinakuja nadhani kitabadilisha tasnia ya filamu as a all, kuna project za kutikisa mji,” Amesema Wema Sepetu.

Usiku wa April 01, 2018 filamu ya Heaven Sent ilimfanya Wema Sepetu kuwa mshindi wa tuzo mbili za Sinema Zetu International Film Festival Awards (SZIFF).

Rais Magufuli Atoa ONYO Kwa Viongozi Wanaowatoza Ushuru wa Mazao Wananchi

$
0
0
Rais Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa serikali kuacha kutoza ushuru kwa wananchi wanaosafirisha bidhaa na mazao ambayo hayajafika uzito wa tani moja,  kwakuwa bunge mwaka 2017 lilipitisha sheria ya kufuta tozo zaidi ya 87 katika sekta ya kilimo.

Rais Magufuli alisema hayo jana Mei 05, 2018, katika sherehe za uzinduzi wa daraja Magufuli lililopo katika mto Kilombero mkoani Morogoro, na kusema kuwa jukumu la serikali ya awamu ya tano ni kutatua kero za wananchi hasa wakulima na kama Rais wa nchi anazijua kero hizo kwasababu amekua kiongozi wa serikali kwa zaidi ya miaka 20.

“Nataka nitoe wito kwa viongozi, ukimuona mtu amebeba magunia 10 ya mpunga maana yake hayajafika tani moja, mpishe wala usimuangalie mwache asafirisha mizigo yake, nataka viongozi wenzangu mnielewe nilizunguka Tanzania nzima kuomba kura kwa ajili ya kuwatetea wananchi, ninafahamu kero za wananchi, wewe kama ni mtoza ushuru nenda ukalime ukajitoze ushuru mwenyewe” alisema Rais Magufuli.

Rais Dkt. Magufuli ameongeza kuwa serikali haiwezi kuwa kikwazo cha maendeleo kwa wananchi na kuongeza kuwa anataka daraja hilo liwanufaishe wananchi wa Morogoro na kuwasihi wakulima kusafirisha bidhaa chini ya tani moja kama wanataka kuepuka kutozwa ushuru.

Daraja la Magufuli lipo katika mto Kilombero, barabara kuu ya Kidatu Ifakara  na lina urefu wa mita 384,  limegharimu shilingi bilioni 61.2 kwa fedha za ndani.

Binti abakwa na kuchomwa moto akiwa hai

$
0
0
Polisi wa India wamesema kwamba , msichana wa miaka 16 nchini humo amechomwa moto  akiwa hai baada ya wazazi wake kulalamika kwa wazee wa kijiji kuwa binti huyo amebakwa.

Inspekta wa Polisi, Shambhu Thakur alipozungumza na gazeti la Hindustan Times amesema kwamba watu 14 wamekamatwa wakihusishwa na mashambulizi hayo katika Jimbo la Mashariki mwa India Jharkhand.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, Polisi huyo amesema wazee wa kijiji waliamuru wanaotuhumiwa  kuhusika na ubakaji huo walipe faini ya Pauni 550 kama adhabu.

Watu hao walikasirishwa na uamuzi huo na kuamua kuwapiga wazazi wa msichana huyo kisha kumchoma moto binti yao.

''Watuhumiwa wawili waliwapiga wazazi kisha wakakimbilia kwenye nyumba yao wakiwa na washirika wao na kumchoma moto msichana,” Ofisa wa Polisi, Ashok Ram alisema.

Polisi wanasema binti alibakwa na wanaume wawili katika eneo lenye msitu karibu na kijiji cha Raja Kendua baada ya kutekwa akiwa peke yake nyumbani kwao baada ya wazazi wake kuelekea kwenye harusi.

Baada ya tukio hilo wazazi walikwenda kupeleka mashtaka kwa wazee wa kijiji kuwashtaki wabakaji.

Mabaraza ya kijiji hayana nguvu kubwa ya kisheria, hata hivyo yana ushawishi mkubwa kwenye sehemu nyingi ya vijiji vya nchini India katika kusuluhisha migogoro kuliko kutumia gharama nyingi kwenye mfumo wa mahakama.

Polisi katika jimbo hilo wamesema wamewakamata watu 14 kati ya 18 ambao watachunguzwa kutokana na madai ya ubakaji na uuaji.

Waziri Mahiga kufanya uzinduzi Israel

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje, Augustine Mahiga atafanya ziara ya kikazi nchini Israel kuanzia kesho Mei 7, 2018 hadi Mei 10, 2018, ziara inayotokana na mwaliko wa Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Atakapowasili nchini humo, Dk Mahiga atafanya mazungumzo na Netanyahu na kushiriki uzinduzi wa ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Israel.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje iliyotolewa leo Mei 6, 2018 imesema Dk Mahiga anakuwa waziri wa kwanza wa Mambo ya Nje kutoka Tanzania kufanya ziara nchini Israel.

Mbali ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili, Waziri Mahiga atatumia ziara hiyo kuishawishi Serikali ya Israel iunge mkono juhudi za Serikali za kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda.

Israel ni moja ya nchi zenye maendeleo makubwa katika sekta za kilimo, viwanda, uhifadhi wa maji, matibabu, ulinzi na usalama, mawasiliano na nishati ya joto ardhi.

“Kupitia ziara hiyo, ajenda ya uchumi wa viwanda ya Tanzania inaweza kupata ushirikiano mkubwa wa Israel kutokana na hatua kubwa ya kimaendeleo iliyofikia,” inasema taarifa ya wizara.

Kabla ya Tanzania kufungua ofisi ya ubalozi Israel, ilikuwa inawakilishwa kupitia ubalozi wa Misri na ubalozi wa Israel nchini Kenya pia unawakilisha Tanzania hadi sasa.

Israel ni moja kati ya nchi sita ambazo Serikali ya Tanzania imefungua balozi mpya. Job Masima aliteuliwa na Rais John Magufuli kuwa balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Israel.

Kitila Mkumbo atii agizo la Rais Magufuli

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo, ametekeleza kwa vitendo agizo alilopewa na Rais Magufuli, la kwenda kijijini Tundu, Wilayani Mikumi kushughulikia kero ya mradi wa maji kijijini hapo.

Mei 4 mwaka huu akiwa kwenye ziara yake Mkoani Morogoro, Rais Magufuli alibaini kero ya Mkandarasi kuchukua fedha kisha kushindwa kukamilisha mradi wa maji katika kijiji cha Tundu Kata ya Kidodi, ambapo moja kwa moja alimpigia simu Prof. Mkumbo na kumtaka kufika kijijini hapo.

Mei 5, Katibu Mkuu huyo wa Wizara hiyo alifika kijijini hapo na kutatua kero hiyo ambapo tayari marekebisho ya mradi huo yameanza. Mradi huo ulielezwa kukamilika lakini ukashindwa kutoa maji kama ilivyokuwa imepangwa.

Pia Prof. Mkumbo ameunda timu maalum ya watalaam watakaopitia upya usanifu wa mradi huo na kuchukua hatua stahiki kwa wahandisi na mtaalam mshauri aliyesanifu mradi huo.

Mbali na hayo pia Katibu ametoa namba maalum kwaajili ya kurahisisha mawasiliano kwa wananchi wenye kero za Maji waweze kuwasiliana naye moja kwa moja ili aweze kushughulika na kero zao.

Rais Magufuli Azindua Stendi ya Mabasi Morogoro...... ataka wamachinga Waruhusiwe kuuza bidhaa zao Ndani ya Stendi Hiyo

$
0
0
Rais John Magufuli ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Morogoro, kuweka utaratibu mzuri ili wamachinga waweze kuuza  bidhaa zao ndani ya stendi ya mabasi ya Msamvu ya mjini Morogoro.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Jumapili Mei 6, 2018 katika uzinduzi wa stendi hiyo, kubainisha kuwa yeye ni Rais wa Watanzania wote.

“Nimekuja kufungua stendi lakini si kufungua stendi ambayo ina ubaguzi. Nimechaguliwa na Watanzania wote. Niwaombe tu mtengeneze mkakati mpya kuwawezesha wamachinga kuruhusiwa kuingia humu na wapewe vitambulisho,” amesema.

Ametoa kauli hiyo baada ya kuuliza iwapo wamachinga wanaruhusiwa kufanya biashara katika stendi hiyo, kujibiwa na mamia ya waliofika kushuhudia uzinduzi huo.

“Fedha isiyojali maskini ni fedha haramu. Wito kwa waziri wa Tamisemi lazima kuwe na eneo la kufanya biashara kwa wamachinga wote katika stendi zitakazojengwa. Fedha zimnufaishe kila mmoja,” ameagiza Rais Magufuli na kuongeza:

“Mnawanyima nafasi wananchi wa hapa maana hawatauza mihogo, machungwa na bidhaa zao kwa wasafiri wanaopita hapa. Ninawaomba manispaa kuangalia jambo hili… lazima tutengeneze utaratibu mzuri utakaowanufaisha watu wote.”

Freeman Mbowe: Imeniuma Sana, Nakosa Maneno ya Kutamka

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa kwa siku kadhaa zilizopita amekuwa katika wakati mgumu na kushindwa kuelewa neno gani anaweza kumpa Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, John Heche kufuatia kifo cha mdogo wake Suguta ambaye alifariki kwa kuchomwa kisu na askari

Mbowe amesema kuwa kifo ambacho kilimpata mdogo wake na Heche kinaumiza sana ndiyo maana kwa siku kadhaa amekosa maneno mazuri ya faraja kumpa kiongozi huyo wa CHADEMA

"Ni siku ya 3 sasa toka ulimpozika mdogo wako, nimefikiria kwa muda mrefu, maneno gani nitumie kukupa pole lakini imeniwia vigumu sana kuyapata maneno hayo kutokana na aina ya kifo kilichokatisha maisha ya kijana mdogo kabisa katika Taifa. 

"Tunafundishwa ya kwamba tushurukuru kwa yote,liwe baya au zuri, sawa tunashukuru lakini kwa kifo cha aina ya mdogo wako kinauma na kuumiza sana, bora mtu akiumwa inakuwa ni rahisi mnasema ni kazi yake Mungu hakuna anayeweza kuipinga na huwa ni kipindi kigumu kuliko wakati mwingine wote wote katika maisha yetu wanadamu pale tunapoondokewa na wapendwa wetu lakini kwa kifo cha aina ya mdogo wako ni maumivu zaidi"

Aidha Mbowe alitumia wakati huo kutoa pole kwa familia ya John Heche kufuatia kifo cha mdogo wake huyo

"Nakupa pole sana Kamanda Heche John katika kipindi hiki kigumu, Mungu akupe nguvu wewe, familia, ndugu, jamaa na marafiki, pole kwa mara nyingine kamanda, apumzike kwa Amani Kamanda Suguta"
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images