Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ndalichako wanaosambaza kitabu mitandao Wakamatwe

0
0
Prof. Joyce Ndalichako ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwasaka watu wanaosambaza kitabu mitandaoni  chenye picha ya mwili wa binadamu huku kikiwa kimekosewa  na kuongeza kwamba watu hao wana nia ya kuichafua serikali.

Uamuzi huo umetolewa katika mkutano wa kumi na moja wa Bunge la Jamhuri ya muungano unaoendelea jijini Dodoma unaojadili mapendekezo ya bajeti ya mapato na matumizi ya wizara mbalimbali kwa mwaka 2018/19.

Prof. Ndalichako amesema kuwa kitabu cha kiingereza cha darasa la tatu kinachosambaa mtandaoni kilikuwa na makosa na kilisharekebishwa huku wahusika wakichukuliwa hatua lakini kitabu kinachoonyesha picha sehemu za mwili wa mwanadamu ni kitabu ambacho hakitambuliki na serikali hivyo wanaokisambaza watafutwe na wachukuliwe.

Hata hivyo Waziri Ndalichako ametoa hatua hiyo ikiwa ni baada ya Mbunge wa viti maalum, Martha Mlata, kuomba serikali itoe ufafanuzi kuhusu tukio hilo.

Aidha Katika majadiliano ya bajeti ya wizara ya elimu baadhi ya wabunge wameishauri serikali kufanya maboresho ya mitaala ya kufundishia.

Mbali na hayo serikali imeahidi  kulipa deni la shilingi trilioni 1.2 linalodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii baada ya mpango wa serikali wa kuunganisha mifuko ya jamii utakapokamilika.

Serikali Yataja Sababu za Kuharibika Kwa Barabara Nchini

0
0
Serikali imesema kwamba barabara kuharibika mara kwa mara ni jambo la kawaida na hali hiyo inachangiwa na sababu mbalimbali ambazo hupelekea miundumbinu hiyo kuaribika.

Hayo yamesemwa leo Mei 04 na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Elias Kwandikwa katika kipindi cha maswali na majibu bungeni na kuongeza kuwa barabara hizo huwa na muda maalumu wa kuishi na ndiyo maana serikali hutenga fedha kwa ajili ya marekebisho.

“Ni kweli kuna baadhi ya maeneo baada ya barabara kutengenezwa zinaharibika, ni hali ya kawaida na ndio maana baada ya ujenzi katika kipindi cha maisha ya barabara tunatenga fedha kwa ajili ya kufanya marekebisho” amesema Kwandikwa.

Naibu Waziri amesema kuwa serikali huwa inafanya matengezo makubwa ya barabara kila baada ya miaka 20 tangu kukamilia kwa ujenzi husika kwasababu muda wa maisha ya barabara hiyo unakua umekwisha.

Naibu Waziri Kwandikwa, alikua akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Mariam Msabaha aliyetaka kujua serikali inachukua hatau gani kwa barabara ambazo zinaharibika muda mfupi baada ya ujenzi ya kukamilika.

Rais Magufuli Ampigia Simu Prof. Kitila Mbele ya Wananchi,

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempigia simu Katibu Mkuu wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo mbele ya wananchi wa kijiji cha kidodi , kumtaka kumchukulia hatua mkandarasi aliyepewa mradi wa maji na kutoukamilisha.

Akizungumza kwa sauti kubwa huku wananchi wa Kidodi wakiwa wanasikiliza 'live', Rais Magufuli amesema kwamba mkandarasi huyo alishapewa pesa za mradi milioni 800 lakini maji hayajafika kwa wananchi, hivyo ahakikishe amechukuliwa hatua za kisheria au awepo eneo la mradi kukamilisha.

Awali kabla ya kupiga simu hiyo, Rais Magufuli ametuma salamu kwa mkandarasi huyo kupitia wananchi wa kijiji cha Kidodi, kumtaka azirejeshe fedha alizopewa za mradi pasipo kutekeleza mradi huo muhimu kwa jamii.

“Nafahamu kuna mradi wa maji wa milioni 800 na mkandarasi alipewa, lakini maji hayajafika kwa wananchi, nilidhani mbunge wenu atauliza achukuliwe hatua gani lakini hajauliza, na mkandarasi kama alikula hela atazitapika, naomba mumfikishie huu ujumbe”, amesema Rais Magufuli.

Baada ya simu hiyo Profesa Mkumbo amesema anatarajia kuanza safari mchana huu kwenda kijijini hapo kushughulikia tatizo hilo, na mpaka kesho atakuwa ameshafika eneo la tukio na kutoa suluhu.

Zitto Kabwe avalia njuga Mauaji ya Pwani

0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini, Bw. Zitto Zuberi Kabwe leo bungeni ametoa taarifa kwa Wabunge wenzake pamoja na Mwenyekiti wa Bunge hilo Mussa Azzan Zungu kwamba atatoa hoja binafsi kutaka buge kuunda kamati teule ya kufanya uchunguzi kuhusu mauaji mbalimbali zilizojitokeza katola Mkoa wa Pwani.

Zitto ameyasema hayo kwenye sehemu ya tatu ya hotuba yake juu ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa Mwaka 2018/19.

Katika hotuba yake Zitto amesema kwamba zaidi ya Watanzania 380 wanatajwa ‘kupotezwa’ MKIRU, (Mkuranga, Kibiti na Rufiji)  Bunge lichunguze kama lilivyochunguza Operesheni Tokomeza.

"Naomba kutoa Taarifa kwamba nitatoa hoja binafsi kutaka Bunge lako Tukufu kuunda Kamati Teule kufanya uchunguzi kuhusu kadhia za Mauaji, Kupotea, Kupigwa Risasi, Kuteswa watu wa MKIRU na Kusini kwa ujumla. Ni imani yangu kuwa Wabunge wenzangu mtaunga mkono jambo hili. Zitto Kabwe.

Ameongeza kuwa "Kadhia za namna hii ni nyingi mno, na yeyote kati yetu, akipata wasaa tu wa kwenda MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji) ataelezwa mambo haya kwa undani, makadirio ni kuwa zipo kesi zaidi ya 380 za namna hii za watu kuchukuliwa na kutorudishwa kwa zaidi ya miezi 10 sasa, hizo ni tofauti na zile za watu waliokamatwa, kuteswa na kisha kuachiwa, au wale waliojeruhiwa kwa kupigwa risasi".

"Na si MKIRU tu, bali ukanda wote wa Kusini, wiki mbili zilizopita, Mbunge wa Kilwa Kusini, Mh. Suleiman Bungara ‘Bwege’ (CUF) naye alieleza kadhia za watu 10 wa Jimboni kwake Kilwa, kuchukuliwa Msikitini na Jeshi letu la Polisi, kupigwa risasi, wengine kutokurudishwa mpaka leo, na kuhisiwa kuwa wameuawa, wengine kurudishwa wakiwa na vilema vya kukatwa masikio, kuchomwa ndevu kwa moto".

Rais Magufuli Kataja Sababu Inayomfanya Asiende Nje ya Nchi Mara Kwa Mara

0
0
Rais Dkt. John Magufuli amefunguka sababu inayomfanya asipende kwenda nchi za nje mara kwa mara kwa kudai anahitaji muda wa kutosha kushughulika na matatizo ya wananchi waliomuamini na kumchagua kuwa kiongozi wa nchi.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Mei 04, 2018 wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi barabara ya Kidatu Ifakara mkoani Morogoro yenye urefu wa kilomita 66.9 na kuongeza kuwa viongozi wanaomsaidia ndiyo wanajukumu la kusafiri nje ya nchi na kuhudhuria vikao mbalimbali.

“Kwa sababu mimi ni Rais wa Tanzania, muda wangu mwingi nitatumia kuzunguka kwa wananchi ili nijue shida na vilio vyao, kwa hiyo nazunguka maeneo mengi ya watanzania ili kero zao niweze kuzijibu, na hili ndiyo jukumu langu na ninataka muamini hivyo. Makamu wangu wa Rais atazunguka kweli kwenda nje” amesema Maguful.

Rais Magufuli amesema amepokea mialiko zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani lakini amekua akiwatuma wasaidizi wake ili kumuwakilisha katika nchi hizo.

Barabara hiyo iliyopo eneo la Nyandeo-Kidatu mkoani Morogoro ina urefu wa kilomita 66.9 itajengwa kwa fedha za serikali, Umoja wa Ulaya (EU) pamoja na Shirika la Maendeleo la Uingereza (BFID) na itagharimu kiasi cha shilingi bilioni 104.9.

Rais Magufuli: Bora Kula Sumu Kuliko Fedha za Serikali

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kwamba watu wanaokula fedha za serikali wanajitafutia balaa, kwani ni sawa na wanakunywa sumu.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Morogoro alipokuwa akizundua ujenzi wa babara ya ya Kidatu - Ifakara , na kueleza kwamba wakandarasi hao waliokula hela za miradi wamekunywa sumu, hivyo wajiandae kuhukumiwa au kurudisha fedha hizo.

“Kuna baadhi ya miradi makandarasi wamekula pesa, nataka kuwahakikishia hao wakandarasi wamekula sumu, hela za serikali haziliwi, ni nafuu ukale sumu kuliko kula hela za serikali ya awamu ya tano, Na mimi nataka niwaeleze ukweli kama wapo hapa makandarasi, wamekula sumu tena ile sumu kali, nimeagiza wakandarasi wote waliopewa miradi ya maji, waanze kuishughulikia, au wajiandae kuhukumiwa, au wajiandae kurudisha hizo fedha”, amesema Rais Magufuli.

Sambamba na hilo Rais Magufuli amewataka wakandarasi wa miradi ya barabara ya hiyo mkoani Morogoro kukamilisha miradi hiyo kwa wakati, ili wananchi waweze kuitumia.

Tamko Rasmi la Wizara Ya Elimu Kuhusu Kitabu Kinachosambazwa Mitandaoni

0
0
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeibuka na kukanusha vikali kuwa kitabu kinachosambazwa katika mitandao ya kijamii kinachoelezea viungo vya mwanadamu sio chapisho la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na wala sio miongoni mwa vitabu ambavyo vimesambazwa shuleni.

Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kupitia Wizara ya Elimu Mwasu Sware hii leo Mei 04, 2018 baada ya kusambazwa picha hiyo katika mitandao ya kijamii na kupelekea kuzua mjadala mzito kwa wazazi pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu nchini jambo ambalo wamedai ndiyo sababu pekee ya elimu ya Tanzani kudidimia.

"Kitabu hicho hakina uhusiano wowote wala hakifanani na vitabu ambavyo vimechapishwa hivi karibuni na TET. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawasihi watanzania kupuuza taarifa hizo ambazo siyo za kweli na zina nia ya kupotosha na kuleta usumbufu kwa jamii", amesema Sware.

Soma hapa chini habari kamili kuhusiana na taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Mbunge Aibua Sakata la Vifo vya Mtikila na Chacha wangwe Bungeni

0
0
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Janeth Masaburi amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba kutoa taarifa bungeni juu ya vifo vya wanasiasa Chacha Wangwe aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila.

Wangwe ambaye alikuwa mbunge wa Tarime kwa tiketi ya Chadema alifariki dunia Julai 27 mwaka 2008 katika ajali ya gari iliyotokea Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma,  Mtikila alifariki katika ajali ya gari  Oktoba 4, 2015 Chalinze wilayani Bagamoyo.

Akichangia bajeti ya wizara hiyo  mwaka 2018/19, Masaburi amemtaka pia waziri huyo kutoa taarifa za kifo cha watalii waliomwagiwa tindikali na makanisa yaliyochomwa moto. 

“Tunaomba taarifa, kifo cha Wangwe, Mtikila, watalii waliomwagiwa tindikali na makanisa yaliyochomwa moto Zanzibar,” amesema.

Kuhusu amani amesema Tanzania ipo mahali salama tangu kuasisiwa kwake enzi ya Hayati Mwalimu Nyerere na maraisi wastaafu Ali HassaMwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete.

“Hii nchi yetu sote, humu tupo zaidi ya 300 ila Watanzania wapo milioni 60, kila mtu ana haki hamasa ambazo zinatolewa kwa kutubagua zishindwe kwa jina la yesu.  Bila amani hatuwezi kulima hakuna kwenda shule, kustarehe wala kuzaliana,” amesema.

Amesema watu wasitanie amani kwa kutumia dini kwamba dini fulani inaonewa na kuhoji mbona wapo ndani ya Bunge.

“Tusitanie amani, ninaomba Serikali iongeze bajeti ya kutosha katika vyombo vya ulinzi na usalama pia makazi yao yaboreshwe na kujengwa nchi nzima,”amesema.

Mwigulu Nchemba: Wasioridhishwa na utendaji wa polisi waripoti kwangu

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Dk Mwigulu Nchemba amewataka wasioridhishwa na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kukata rufaa kwake.

Pia, amewataka wanasiasa wanaozungumzia matukio ya kupotea watu kuwa na ushahidi wa kutosha na kama hawana wasiyazungumze kwani yanajenga taswira hasi kwa nchi.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 na kubainisha kuwa si askari wote ni wema na kwamba  wanaokiuka taratibu za kazi hatua zitachukuliwa dhidi yao.

“Damu ya mwanadamu haiwezi kulinganishwa na thamani ya chama chochote au kabila lolote na sisi hatutakubali damu imwagike bure lakini  panapotokea tatizo la kiutendaji la aina hiyo, hilo ni la mtu mmoja,” amesema.

Kuhusu watu wanaopotea amesema, “Kuna mambo mengi ya kimaadili tumeyafanyia msako, kuna watu wamehama majumbani mwao  kwa msako wa dawa za kulevya na wengine tumeambiwa wamevuka mipaka ya nchi yao na ndio hao wanasema wamepotea na ukituuliza yuko wapi na sisi tutasema yupo wapi.”

Amesema kuna ambao wamekimbia baada ya baadhi ya watu waliokamatwa kuwataja kuwa wanatumia silaha.

“Ukijumlisha hao ambao hawapo na kusema wamekufa hiyo siyo sawa kwani kwa sasa Watanzania ambao wanashikiliwa nje ya nchi katika magereza ni zaidi ya 1,000. Ukisema hao watu wameuawa ni makosa,” amesema.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya May 5

Joti Atoa Ufafanuzi Kuhusu Kubomolewa kwa Nyumba Yake.

0
0
Kufuatia  nyumba yake iliyopo Kisarawe kupigwa alama ya X huku akisemekana anatakiwa aibomoe kupisha upanuzi, Komedian maarufu nchini, Lucas Mhavile ‘Joti’ amefungukia tukio hilo ambalo limevuta hisia kwa mashabiki wake na Watanzania wengine waliotaka kujua undani wake.

Joti ameema; “Wanapanua barabara huku kwetu, lakini upanuzi huo wa barabara hauhusiani kabisa na ubomoaji wa nyumba, wengi wanajua nyumba yangu ndiyo inabomolewa, lakini sivyo kinachobomolewa ni ukuta tu.”

Eneo la Kisarawe na Kibada sio eneo la kwanza kwa Dar es Salaam kukukumbwa na adha ya bomoa bomoa, kabla ya hapo maeneo ya Kimara na Kinondoni Dar es Salaam nayo ilipita bomoa bomoa.

Nyumba ya Joti ni miongoni mwa nyumba zaidi ya 100 zilizopigwa X maeneo ya Kisarawe pamoja na Kibada ili kupisha upanuzi wa barabara.

Familia Yaendelea Kupiginia Haki za Tundu Lissu

0
0
Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), imesema haki anazostahili ndugu yao zikiwamo gharama za matibabu, uchunguzi wa waliomshambulia kwa risasi, zitacheleweshwa kwa muda lakini hatimaye ipo siku atazipata.

Msemaji wa familia hiyo, Wakili Alute Mughwai, alisema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake, jijini hapa.Alisema familia haitachoka kudai haki za Lissu na kinachojitokeza ni kucheleweshwa lakini siku moja itapatikana.

Akizungumzia haki ya kupata matibabu, alinukuu kifungu cha 24 cha Sheria ya Utawala wa Bunge, 2008, kinachotoa haki hiyo kwake na mwenza wake pamoja na watoto wanne na kwamba utaratibu mwingine wowote unaokwenda kinyume unakiuka sheria hiyo.

“Mbunge si mtumishi wa serikali, mbunge ana taratibu zake za kupata matibabu… Bunge kama mhimili unaojitegemea hauna taratibu zingine zaidi nje ya sheria hiyo,” alisema.

Aprili 19, mwaka huu, Spika wa Bunge Job Ndugai, aliliambia bunge linaloendelea mjini Dodoma kuwa, familia ya Lissu haijawasilisha Ofisi ya Bunge nyaraka muhimu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais.

Alisema iwapo nyaraka hizo zitapatikana, ofisi yake haitasita kuidhinisha malipo ya matibabu yake.Hata hivyo, Wakili Mughwai alisema utaratibu huo haupo katika sheria ya Bunge.

“Unaposema fuata utaratibu wakati mbunge amepigwa risasi na yupo katika hatari ya kufa unataka kupata nini zaidi? Bunge ambalo ni mhimili unaojitegema limekuwa na utaratibu wa kushughulikia mbunge aliye katika hatari ya kufa baada ya kupigwa rasasi?,” alihoji.

“Huo utaratibu haupo…ni lazima ubuniwe utaratibu wa kuendana na hayo mazingira.”

Alisema tangu kushambuliwa kwa Lissu Septemba 7, mwaka jana mjini Dodoma, familia imekuwa na mawasiliano ya muda mrefu na Ofisi ya Bunge kuhusu matibabu ya Lissu, lakini hata mara moja hawajasema wazi kuhusu utaratibu.

“Kama Bunge wangesema tangu mwanzo katika majadiliano yao kuwa hawawezi kugharimia matibabu yake, tungewaambia ‘thank you’ na kusingekuwapo na vikao vya mjadala,” alisema.

Alisema kwa mfano, Februari 1, mwaka huu, walipokea barua ya Bunge iliyowaarifu kuwa wanawasiliana na Wizara ya Afya kuhusu matibabu ya Lissu na baadaye watawaarifu.

“Ni miezi mitatu sasa, Mei 2 familia imeandika barua Ofisi ya Bunge kuomba mrejesho huo na kujua wamefikia wapi,” alisema. Akizungumzia upelelezi wa tukio hilo, Wakili Mughwai alisema miezi minane sasa imepita na wao bado wanapata kiza kikuu.

“Alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana miezi minane iliyopita na walitakiwa kufanya upelelezi wa kuwatia hatiani watuhumiwa,” alisema huku akisisitiza kuwa wataendelea kudai haki ya ndugu yao bungeni na haki kama mwathirika wa kosa la kijinai.

“Tutaendelea kudai haki hizi hadi zitakapopatikana. Tunajua haki ya mtu inacheleweshwa lakini haitapotea,” alisema.

Akizungumzia hali yake alisema anatarajiwa kufanyiwa operesheni ya 20 ya kurekebisha mifupa katika paja la kulia.

Alisema operesheni iliyopita ilifanyika vizuri na sasa yupo kwa uangalizi wa madaktari kwa siku chache zijazo na baada ya hapo ataendelea na mazoezi ya viungo.

Alisema pamoja na operesheni hiyo atafanyiwa operesheni nyingine ndogo kufuatia kuambukizwa vijidudu na pia kunyoosha mfupa katika paja.

Kuhusu kurudi nchini, alisema hata yeye hajui na kama familia pia haijui.

“Wengi wanatuuliza lini atakuja, jibu letu ni hatujui, na sisi ni watu wa kwanza kutaka arudi nyumbani…hilo ni suala la madaktari wanaomtibu.

“Lissu si mtoto mdogo, anahitaji kutibiwa hayo majeraha na akishapona anatamani kurudi nyumbani,” alisema.

Aikana Kauli ya Spika
Wakili Mughwai alikanusha taarifa ya Spika wa Bunge Ndugai aliyedai kuwa gharama za matibabu ya Lissu yanalipwa na Serikali ya Ujerumani.

“Hiyo habari si ya kweli,” alisema huku akiweka bayana kwamba matibabu ya Lissu, weka na posho za kujikimu vinagharimiwa na wasamaria wema.

“Hii habari imetufedhehesha sana kwa namna moja inatuonyesha sisi familia kuwa ni matapeli.

“Athari ya hii taarifa ni kuwaambia watu waliokuwa wanamchangia gharama za matibabu yake waache,” alisema.

Alisema familia wangekuwa watu wa kwanza kabisa kushukuru kwa kumpata mfadhili huyo mkubwa na wangewaomba wananchi waache kumchangia. Alisema Lissu bado yupo hospitalini na anahitaji msaada.

Wakili Mugwai alitoa namba ya akaunti ya Lissu ya CRDB ambayo ni 01J2043045300 yenye jina la Tundu Antiphas Lissu.

Vitambi Vikubwa vya Polisi Vyamkera Mbunge

0
0
Mbunge  wa Kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amehoji bungeni mjini Dodoma kwa nini baadhi ya askari polisi wana vitambi vikubwa.

Bulembo alitoa hoja hiyo jana alipokuwa ananchangia mjadala wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka ujao wa fedha.

Alihoji sababu za baadhi ya askari kuwa na vitambi vikubwa, akidai vinasababisha washindwe kufanya mazoezi ya kiaskari.

Mbunge huyo pia aliishukia Idara ya Uhamiaji akidai imekuwa ikihangaika na wahamiaji haramu wanaopita kutoka nje huku ikiwalinda walioko ndani ya nchi.

Alisema pamoja na idara hiyo kufanya kazi nzuri, imekuwa ikishughulikia sana wahamiaji na hasa wale wa kutoka Ethiopia.

Bulembo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hadi mwishoni mwa mwaka jana, alisema wakati wakifanya hivyo, wamekuwa wakiwalinda wahamiaji ambao wamo ndani ya nchi na wengine wameishi zaidi ya miaka 20 sasa bila kuwa na vibali maalum.

Alisema hali hiyo ni hatari kwa kuwa wengine wamekuwa wakilindwa na watendaji toka idara hiyo na wanaendesha shughuli zao bila wasiwasi.

“Inashangaza kuna baadhi ya wahindi wapo humu nchini zaidi ya miaka 20 na wanajulikana lakini mnawaacha na badala yake mnawakamata kina Bashe ambao wamezaliwa hapa nchini,” alisema.

Bulembo pia alizungumza kuhusu utendaji wa Kikosi cha Usalama Barabarani akieleza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wabunge kutumia ubunge wao kama kinga dhidi ya kikosi hicho wanapofanya makosa ya barabarani.

Alisema ni vyema kikosi hicho kikafanya kazi yake kama ilivyopangwa na si kuogopa pale kinapowakamata wabunge.

“Kama mbunge kafanya kosa, kamata peleka mahakamani. Ubunge siyo kinga ya kufanya makosa na wala isiwe kuwatishia askari wa barabarani, waacheni wafanye kazi zao,’’ alisema.

Naye Mbunge wa Mkokotoni, Juma Othman Hija (CCM), alisema kumekuwa na uhaba mkubwa wa nyumba za askari katika jimbo lake ambalo pia linakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa vituo vya polisi.

Alisema kutokana na uchakavu huo, askari polisi wakati wa mvua wamekuwa wanalazimika kufanya kazi zao katika chumba cha mahabusu.Alisema hali hiyo ni aibu kwa Jeshi la Polisi kwa kuwa wananchi wengi wanawategemea kufanya kazi ya kuwalinda, lakini linakosa ofisi bora na vitendea kazi.

Alisema jeshi hilo pia linakabiliwa na uhaba wa karatasi akidai kuwa yeye binafsi alikwenda kwenye Kituo cha Polisi cha Kati mjini hapa na alichukuliwa maelezo kwa kutumia karatasi zinazotumika kwa ajili ya shughuli za Bunge.

Ommy Dimpoz- Sijawahi kutoka kimapenzi na Wema Sepetu......ile Ilikuwa ni Kiki Tu

0
0
Mwanamuziki wa Bongo fleva Omari Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi hata siku moja kutoka kimapenzi na Wema Sepetu.

Kipindi cha nyuma ilishawahi kusemekana Kuwa Ommy Dimpoz na Wema Sepetu walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi hasa baada ya picha zao kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Tetesi za Ommy dimpoz na Wema kuwa kwenye mahusiano zilizidi pale ambapo alionekana na Wema Kwenye chumbani wakiwa wamelala ambapo baadae ilikuja kujulikana walikuwa location kwa ajili ya kushoot wimbo wa Wanjera ambao Wema alikuwa ni video queen.

Lakini Kwenye mahojiano na Kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Ommy Dimpoz amethibitisha kuwa zile zilikuwa ni kiki tu kwa ajili ya project zao.

"No, Sijawahi ku-date na msichana yeyote maarufu hapa Bongo, sijawahi.“

Lakini pia Ommy Dimpoz amesisitiza kuwa hajawahi kuwa na Mahusiano na msichana yoyote ambaye ni staa kwa Bongo.

Hivi sasa Ommy Dimpoz anafanya vizuri sana na wimbo wake wa Yanje aliomshirikisha Msanii Seyi Shay kutoka Nigeria.

Familia ya Heche kuweka wakili mauaji ya ndugu yao

0
0
Baada ya maziko ya Suguta Chacha (27) aliyeuawa kwa madai ya kuchomwa kisu akiwa mikononi mwa polisi katika kituo cha Sirari, wilayani Tarime familia yake imesema itaweka wakili kusimamia kesi ya ndugu yao mahakamani.

Suguta ambaye ni ndugu wa mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa kisu na polisi usiku wa kuamkia Aprili 27.

 Heche amesema kwamba ndugu yao alifanyiwa kitendo cha kinyama na kubainisha kuwa wataweka wakili ili mtuhumiwa wa mauaji hayo apate hukumu anayostahili.

“Tunajua yupo wakili wa jamhuri atakayesimamia kesi, lakini nasi tutaweka wetu, tunachotaka ni kwa aliyehusika kupata hukumu anayostahili, familia imeshajipanga kwa ajili ya jambo hilo,” alisema Heche.

Alisema kiuhalisia hakuna fidia yoyote wanayoweza kulipwa ikazidi uhai wa ndugu yao, isipokuwa ni kwa mhusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Tunamshukuru Mungu tumemzika salama, hakuna jambo lolote la kushtua lililojitokeza wakati wa shughuli nzima ya kumuhifadhi ndugu yetu. “Watu walijaa, huzuni na simanzi viliutawala msiba huu ambao unatuumiza sana,” alisema Heche.

Polisi yawafungulia jalada wanaosambaza picha za vitabu mtandaoni

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema jalada la uchunguzi wa watu wanaosambaza vitabu mitandaoni limefunguliwa.

Akizungumza  jana Ijumaa Mei 4, 2018 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Kamanda Sirro amesema wamepokea maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

"Tumepokea maelekezo na tayari tumefungua jalada na tutakapowapata tutawapeleka mahakamani," alisema IGP Sirro.

Kuhusu watu wanaovunja sheria ya mitandao, IGP Sirro amesema wanaendelea kufuatilia na kila atakayekuwa anabainika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Waziri Awataka Trafiki Waache Kuwabambika Kesi Madereva

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amewataka askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kujitafakari kuhusu faini wanazotoza na kuacha kubambikiza kesi kwa madereva.

Akijibu hoja za wabunge walizozitoa wakati wakichangia bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 jana Mei 4, 2018 bungeni mjini Dodoma, Masauni amesema chanzo kikubwa cha ajali barabarani ni pamoja na makosa ya kibinadamu kwa asilimia 76, ubovu wa miundombinu na uchakavu wa magari.

“Bado kuna changamoto za baadhi ya madereva ambao hawafuati sheria. Trafiki acheni tabia za aina hiyo, watu hawajafunga mkanda badala ya kumwelewesha unamtoza faini,”alisema.

“Lazima waangalie uzito wa kosa lenyewe na wafanye kwa mujibu wa sheria. Kama mtu hajafunga mkanda unamtoza faini badala ya kumpa elimu tu. Raia nao wawape ushirikiano askari wetu kwani wanafanaya kazi katika mazingira magumu zaidi.”

Amlisema serikali kwa upande wake inafanya kila juhudi ikiwemo kupata mkopo mkubwa kutoka Benki ya Exim wa Sh500 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Serikali ambapo kila nyumba itajengwa kwa gharama ya Sh25 milioni.

Kuhusu uhamiaji, Masauni amesema Serikali imefanikiwa kufumua mtandao wa watendaji wa idara ya uhamiaji mikoani ambao hawakuwa waaminifu katika utendaji wao wa kazi.

Ameahidi kufanya kila namna ya kuwasaidia wananchi wa mkoa wa Kigoma ambao wamekuwa wakilalamika kuhusu utendaji wa idara hiyo kwa kila wakati kuulizwa kuhusu vitambulisho.

Mbunge Chadema ahoji wabunge Viti Maalum kuzuiwa kufanya mikutano

0
0
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Upendo Peneza amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba kulieleza Bunge sababu za wabunge wa Viti Maalum kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo wanayotokea.

Peneza amesema kama kweli Dk Mwigulu anataka kuwa Rais wa Tanzania siku zijazo, akishindwa kulishughulikia jambo hilo atakuwa amepoteza sifa hiyo kutokana na kuzima ndoto za wanawake na vijana.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani mwaka 2018/19  Peneza alisema polisi wamekuwa wakikandamiza demokrasia,  ikiwamo kuwazuia kufanya mikutano kwenye mikoa yao.

“Kaka yangu, Mwigulu kama ulitegemea kuwa Rais siku moja, wabunge wa viti maalum wapo humu kwa mujibu wa Katiba ambayo inazungumzia uwepo wa wabunge wa viti maalum ambao majina yao yanapendekezwa na vyama vyao,” alisema Peneza.

“Lakini mimi pamoja na wabunge wengine tumekuwa tukizuiwa kufanya mikutano ya hadhara, wabunge tunaambiwa tufanye kazi nyumbani?  Wabunge wa viti maalum tunadhalilishwa, mtuache tufanye kazi.”

Alisema, “Kwa nini tunalipwa fedha, tunahitaji tufanye mikutano kwani tunalipwa, lazima tuwasikilize wananchi na turuhusiwe kufanya mikutano katika maeneo yetu na mwisho tutasema Serikali ya awamu ya tano haitaki wanawake wafanye siasa.”

Alisema kupitia mikutano ya hadhara ndiko ambako wanaibuka wanawake na vijana akiwamo yeye.

Waziri Kabudi Ataja Sababu za masheikh wa Uamsho kuchelewa kufikishwa mahakamani

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema masheikh wa Uamsho kuchelewa kufikishwa mahakamani kunatokana na upelelezi kutokamilika, kwamba Serikali imeomba ushahidi kutoka nje ya nchi.

Akizungumza jana  wakati akijibu hoja  za wabunge zilizoibuka wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2018/19, Kabudi amesema suala hilo halihusu wizara hiyo, kwamba linamhusu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

“DPP ana uwezo wa kufungua mashtaka na kuyafuta na hakuna mtu wa kuingilia . Na kwa sababu hawezi kuingia bungeni nimemwomba anipe majibu kuhusu suala la masheikh wa uamsho.  DPP alikuwa Singida nimemuomba aje aniletee taarifa hapa,”amlisema.

Alisema kuwa suala hilo ni nyeti na adhabu yake ni kubwa, hivyo ndio maana upelelezi umechukua muda mrefu ili kuhakikisha wanapata taarifa za kutosha kabla ya kuwafikisha mahakamani.

Hata hivyo, alisema Serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha suala hilo linafikia mwisho.

“Na hii bahati mbaya sana watu wanaojadiliwa wana hadhi ya masheikh lakini hawakuingizwa kwenye tuhuma za ugaidi kama masheikh, kwa sababu tuhuma lazima tuchunguze kwani wakitiwa hatiani adhabu yake ni kubwa,”alisema.

Alisema uchunguzi huo unafanyika nje ya nchi na ndani ya nchi na kwamba wameomba ushahidi kutoka nje ya nchi kuhusiana na tuhuma hizo.

Mtoto asimama kumuelezea Rais Magufuli shida zao, apewa Milioni 3

0
0
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, mapema leo amemkabidhi mwanafunzi wa kidato cha kwanza Nundoka Msangi, kiasi cha shilingi milioni 3, kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule ya Sekondari Mangula mkoani Morogoro.

Tukio hilo limefanyika wilayani Mikumi mkoani Morogoro, ambapo Rais Magufuli alisimama katika kijiji cha Mangula kwaajili ya kuongea na wananchi waliokuwa wamesimama wakati wa msafara wake akielekea Wilayani Kilombero.

Baada ya kutoa hotuba fupi, Rais Magufuli aliuliza endapo shule ya sekondari katika eneo hilo ina changamoto yoyote, ndipo kijana Nundoka akajitokeza na kusema hawana vyoo na Rais akachangia milioni tatu na kuwataka wanacnhi kushiriki katika ujenzi wa vyoo hivyo.

''Namkabidhi hii pesa kijana Msangi, naomba zitumike vizuri kwenye ujenzi wa vyoo na niwaombe tu wananchi mshiriki vizuri kujenga vyoo hivyo, nitarudi tena kukagua,'' amesema Rais Magufuli wakati akikabidhi fedha hizo.

Magufuli yupo Mkoani Morogoro akiendelea na ziara yake ya siku tatu ambayo inahusisha uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Baadae leo atazindua daraja la Mto Kilombero Mkoani humo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images