MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora imemhukumu kifungo cha maisha Kashindje Shija (50), baada ya kupatikana na kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitano.
Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Nzega Joseph Ngomero, alisema kuwa, kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, amelazimika kutoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa
↧