Watu wawili wamekufa papo hapo huku wengine 45 wakijeruhiwa baada ya basi la abiria lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na lori katika kijiji cha Vikonje wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa 7.05 mchana wakati basi la Kidia lenye namba za usajili T663 AXL kugonga lori
↧