Rais wa Marekani, Barack Obama na mtangulizi wake, George W. Bush,
leo wanakutana ana kwa ana kwenye ardhi ya Tanzania watakapoweka mashada
kwenye Ubalozi wa zamani wa Marekani uliolipuliwa mwaka 1998.
Rais
Obama ameweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza mweusi kuchaguliwa kuongoza
Marekani, akipokea wadhifa huo kutoka kwa Rais Bush, ambaye aliiongoza
taifa hilo kuanzia mwaka 2000-2008.
↧